Alhamisi, 12 Oktoba 2017

WEWE PIA ULIFUNDISHWA KUTAFUTA THAMANI YA "X"?Mungu ni mwema tunakutana tena. Leo naanza na swali la mathematics kutukumbusha tulikotoka! Hahaaa wale wenzangu HGL na KLF tupo?

::::::::::::::::::::::::::::::::

SWALI:

X + (1⁄2)X + 1 = 100

Tafuta thamani ya X

::::::::::::::::::::::::::::::::

Kuna makundi mawili ya watu hapa. Kuna kundi ambalo swali hilo hapo juu nyuso zitakunjamana kwa kujaribu kufikicha akili. Tutaanza kujiuliza tena nani kachanganya hiyo herufi na hizo namba tena. Kisha tutajiuliza tena sasa hii "X" naanzaje kutafuta thamani yake na kujaribu kukumbuka siku mwalimu anafundisha hivyo vitu alivaa shati gani. Na hivi MAGAZIJUTO inamaanisha nini vile?

Kifupi tutatumia muda mwingi kufikiria kuhusu swali kuliko kutafuta jibu. Na pengine tutapotezea tu.

Lakini kuna baadhi yetu nyuso zitakuwa na tabasamu hata sasa hivi walivyoona hilo swali. Wanakumbuka mbali sana. Watakumbuka walivyokuwa wanafurahi kupata mtihani wenye maswali "marahisi rahisi" kama haya. Kwenye mtihani wa hesabu hao ndo walikuwa wanaweza kukufanya ukapanic kama wamekaa pembeni yako wewe unayejiuliza kwa nini wamechanganya herufi na namba kwenye swali moja.

Na sasa hivi hapa wanaweza kuwa washakokotoa thamani ya X kwenye hilo swali na wameshaipata siku nyiingi wakati sisi wengine tulivoona tu swali tumepata allergy reactions tofauti tofauti.

Huko ndiko tulikotoka. Kwa nia njema kabisa ya watunga mitaala ya kutusaidia kufikirisha bongo zetu vizuri walihakikisha maswali kama hayo ni sehemu ya mafunzo yetu. Tulikaa muda mwingi tukifundishwa vitu vya aina hii.

Lakini sasa wote tupo kapu moja. Ndo maana sasa naomba ujiulize... Ni wapi uliwahi kufundishwa KUTAFUTA THAMANI YAKO MWENYEWE?

Yes, lini uliwahi kufundishwa kuhusu kutafuta thamani yako mwenyewe? Wewe ni nani?Kwa wengi hilo bado.

Na kukosekana kwa fursa hiyo kumefanya watu wengi kuishi kwa kutafuta thamani ya VITU VINGINE (thamani ya X) badala ya kutafuta thamani yao wenyewe.

Tunaishi kwenye dunia ya watu ambao wanachojua ni kutafuta thamani ya X. Hawajui thamani yao wenyewe na hivyo ili kuondoa hali ya kutothaminika wanajifungamanisha na X. Kuna ambao X yao imekuwa ni magari na majumba. Ndo wanachotafuta. Wakikipata wanagundua kuna kitu bado hakiko sawa.


Kuna ambao X yao ni kujua kuongea kiingereza. Kuna ambao X ni kupata elimu ya "juu".


Wakiipata wanagundua kiukweli kwamba hiyo kumbe siyo kila kitu. Lakini wakati wanaitafuta usijaribu kuwaambia kitu kingine. Wana apply MAGAZIJUTO.

Hivi karibuni nikakutana na binti mmoja amejaribu kuapply chuo mwaka jana akakosa. Mwaka huu pia amejaribu akakosa. Akanipigia kuomba ushauri kuwa anasikitika wenzake wanapiga hatua yeye yuko tu pale pale. Nikamuuliza maswali machache na kugundua anafikiri thamani yake ipo kwenye elimu ya "juu".

Lakini uzoefu unaonyesha otherwise.
Mfano. Katika vijana wa kiume wenye thamani katika kuitangaza nchi hii yumo Mbwana Samatta na Diamond Platnumz.Ukijumlisha elimu ya darasani ya hao wote wawili ni ndogo kuliko wengi wetu. Lakini VALUE zetu katika jamii je? Thamani ya mmoja wa hao vijana Mungu aliiweka kwenye KOO na ya mwingine Mungu aliiweka kwenye MIGUU. Kuna watu wana degree nyingi mno nchi hii lakini  thamani ya mchango wao kwa taifa HUENDA haifiki hata nusu ya ile ya Mbwana Samatta tu.

Nikamuuliza binti yule. "Unadhani Mungu alikuumba uje ufanye nini duniani?". Akasema "kwa kweli sijui kakangu". Nikamwambia basi acha kwanza kutafuta THAMANI YA X tafuta kwanza kujua thamani yako Mungu aliiweka wapi.  Akaomba nimpe wiki moja kujitafuta vizuri. Namwonbea Mungu amsaidie kujua wapi thamani yao ipo.

Kuna watu wamesoma hadi chuo kikuu lakini thamani yao imekuwa kuwa MC. Kusherehesha. Basi.
Cha ajabu kuna watu hawana degree lakini thamani yao imekuwa kwenye KUFUNDISHA. Hebu tafakari mtu kama Eric Shigongo mpaka sasa ameshafundisha vijana wangapi?


Lakini kuna watu wana Ph.Ds na kumfundisha mtu kuhusu maisha ya kawaida tu ni shida. Why? Huyu wa PhD huenda thamani yake iko kwenye USHAURI au UTAFITI. Siyo kufundisha.

So unatakiwa ujifunze kuangalia wapi Mungu aliweka TALANTA zako. Na ni ngapi alikupa. Tafuta thamani yako. Achana na kutafuta thamani ya vitu vingine ambavyo unahisi vitakupa furaha lakini mwishoni mwa maisha yako utagundua huna furaha tena na wakati vitu ulivyotafuta unavyo tayari tena vingi. Maisha halisi ni kuishi kwa kutambua thamani yako.

Kutojua thamani kumewafanya mabinti wakatoa rushwa ya ngono kwa kisingizio cha kusaidiwa ajira. Hujajua thamani yako halisi my sister. Kutojua thamani zao kumewafanya mabinti wengine kutamani kuolewa na watu wenye mali na uwezo badala ya kutafuta kuolewa na mtu aliyeumbwa kuja kuwa mume wake.

Kutojua thamani yao kumewafanya vijana wa kiume kutamani kuwa na  girlfriend au mke mwenye shepu nzuri bila kujali ni nini analeta kwenye maisha yake. Wake wengi za matajiri siyo wenye mishepu ya kutisha kama unayoona kwenye TV. Na hata kama ni mwenye hiyo shepu basi kuna kitu cha ziada kichwani. Hili ni gumu kukubalika na ni sababu tulifundishwa kutafuta thamani ya X. Thamani yetu tunafikiri ipo kwenye kufanikiwa kupata thamani ya X. Thamani yetu tunafikiri ipo kwenyei aina ya vitu au watu tulionao.

Kuna watu wanaona kuwa wao ni wa thamani sasa kwa kuwa mume au mke amekuwa WAZIRI. Wanaamini katika thamani ya X. Ulishaona picha ya Michelle Obama na mumewe wakati Obama si "lolote" machoni pa watu? Lakini mwanamke yule alijua ana nini. Akajua kuwa yeye ni FIRST LADY. Alipokuwa akimuona Obama haoni future president anaona MUME WA FIRST LADY MTARAJIWA.
Dada unanielewa?


Sasa wewe mumeo akipewa cheo serikalini unaanza kujitambulisha kama mke wa waziri wa..... Hawa ndo wanawake waliokuwa wanatisha polisi njiani. Eti unajua mi ni nani? Ngoja nimpigie mume wangu sasa. See? Huyu anahisi thamani yake iko katika cheo cha mumewe. Na ndo maana cheo cha mumewe kikikoma anakuwa kama mtu asiye na thamani hata akipita barabarani.

Namheshimu sana dada anaitwa Hoyce Temu. Huyu anajua thamani yake. Amesimama kama yeye. Niliwahi kufanya kazi na kijana anaitwa JACOB MSEKWA yaani huyu jamaa hakuwa na maisha ya kujiweka kama "mtoto wa......". Huyu jamaa alinifundisha kitu kikubwa sana. Alijinasibu kwa utendaji wake wa kazi kiasi kwamba jina la Baba yake halikupewa nafasi kabisa. Alikuwa yeye kama yeye. Lakini ofisi hiyo hiyo kulikuwa na watoto wengine wa "wakubwa" ambao kitu pekee kikubwa kilichowatambulisha ni jina la baba. Walipewa heshima na nidhamu ya woga kwa sababu tu ya nafasi ya mzazi.
So sad.

Pia niliwahi kufanya kazi na dada mmoja anaitwa Madeleine.. huyu ni binti wa  Kimei. Alikuwa akipiga kazi na kujituma pengine kuliko sisi wengine tuliotokea familia "duni". Usingeweza kudhani huyu ni binti wa Kimei kwa hali ya kawaida ya kitanzania. Anajua thamani yake haiko katika jina la  Baba yake. Sitamsahau pia huyu. Lakini wengine unakuta ni mpwa sijui wa mkuu wa kituo cha polisi tu lakini weee mwambie kitu uone.

Na mpaka leo tuna viongozi ambao uongozi wao hauna kitu. Kinachowabeba ni jina alilojenga baba kwa miaka mingi. Basi. Hawakutaka kutafuta thamani yao wao kama wao.
Najua unawajua.

Kutojua thamani zetu ndo kumefanya baadhi yetu kutafuta kwa bidii kuishi Ulaya au Marekani ili tukiongea tusikilizwe. Tusiposikilizwa inatusumbua kweli. Kumbe tunashindwa kujua kuwa thamani yetu haiko kwenye kuishi kwetu Ulaya per se ipo kwenye vitu ambavyo Mungu aliwekeza (invest) ndani yetu. Labda uliwekewa kufundisha kama kina sisi. Labda kuchora kama Masoud Kipanya. Labda kuigiza kama marehemu Kanumba. Au uongozi kama mwalimu Nyerere. Ukiishi thamani yako halisi hata ukifa utasikilizwa. Yani watu wanataka kubadili katiba miaka mingi baada ya kufa kwako lakini bado wanasikiliza kwanza hotuba zako kutafuta ushauri.
Can you imagine?

Usipoishi thamani yako ukafikiri thamani yako ni kuoa mke MKALI au kuolewa na BONGE LA BWANA au ni kupata Masters au kuishi Marekani utashangaa unavyo hivyo lakini bado huthaminiki kivile. Utashangaa Diamond akichepuka inakuwa story hadi BBC wakati wewe hata ufanye nini hakuna anayetaka kujua. Diamond angekuwa mhasibu wa Vodacom leo hii angekuwa na hela nzuri tu lakini hakuna ambaye angetaka kujua sijui kazaa na nani. Sishabikii hayo. No. Nakuonyesha value yako halisi ikikutana na ufahamu sahihi hakika utaongea na nchi itasikia.

So tulitoka huku.....

X + (1⁄2)X + 1 = 100

Tafuta thamani ya X.

Mi nasema sasa huku mtaani acha kutafuta thamani ya X. Tafuta kujua thamani yako. Na kama bado uko shule usiishie tu kutafuta hiyo X ukafurahia umefaulu hesabu. Tafuta thamani yako.

Katika kitu kilichowakwaza ndugu zangu na watu wa karibu ni pale nilipoacha ajira kuanza njia ya ujasiriamali. Nilipoona thamani yangu HALISI haipo kwenye Degree yangu ya sheria au kazi nzuri benki ya kigeni bali nahisi kuna kitu ndani yangu katika kufundisha watu hasa vijana wenzangu. Silipwi chochote lakini furaha ninayopata hapa huwezi kuelewa kirahisi. Najua sasa kuwa nina mchango mkubwa wa mawazo kwa vijana wenzangu kuliko ningekuwa niko zangu mahakamani kuendelea na kazi ya sheria. Sishangai kuwa wapo wasionielewa. Ila tu nawaombea na WAO wagundue thamani zao halisi. Na siyo kutafuta tu thamani zao kupitia X.

Sijui wewe thamani yako iliwekwa kwenye mkono na vidole kama mimi au miguu au mdomo au koo au misuli au kichwani tu huko au kwenye macho. Kuna watu akiona kitu tu anabuni kitu kingine kutokana na alichoona. Kuna mwingine hana macho kama wewe wewe na mimi lakini thamani yake siyo mchezo.

Thamani ya Hellen Keller ilikuwa kwenye kutoona na kutosikia kwake. Akafanikiwa bila macho wala uwezo wa kusikia kuliko mamilioni wenye macho na wenye kusikia vizuri ambao tunataka tu kusikiliza umbea na vitu visivyo na maana.


Niliwahi kusema thamani ya Dan Brown ni kuandika Novel zinazofanya uone maisha upya kabisa na ya Les Brown ni kutoa speech zinazofanya uone maisha upya vile vile. Na wote wamekuwa millionaires.

What about you?

Usifate mkumbo. Yule binti aliyekosa chuo aliniambia kuwa nilimsaidia kutambua kuwa amekuwa kumbe akifata tu mkumbo... na kwamba sasa anahitaji muda wa kukaa na kutafakari juu ya maisha yake.


Point yangu siyo watu wasisome. No. Keller alisoma. Mimi nimesoma nashukuru Mungu.

Point yangu ukasome tena sana tu lakini siyo ili kukamilisha ratiba. Au ili kupata title. Usitafute thamani yako kupitia elimu yako. Thamani yako ni kitu tofauti na elimu ni kitu tofauti.

Thamani yako ni tofauti na mume/mke ni kitu kingine cha kukamilisha hiyo VALUE yako. Sasa usipojua ndo hicho kinachopaswa kukukamilisha tu wewe ndo utakifanya ndo the real thing. Ndo maana unataka a READY-MADE MATERIAL.

Usitafute tu mbinu za kwenda Ulaya hata kama ni kwa kupitia njia za mkato ili na uridhike kuwa na wewe ulishafika Ulaya. Nenda Ulaya ukiwa wewe umeshatambua thamani yako. Hata kama jina lako halijulikani bado but unajitambua. Wanaoenda Ulaya wakiwa wanajitambua hata akirudi anaishi kwa busara siyo labda kujionyesha kama sisi wengine.. Anajua thamani yake haikuwa katika kwenda Ulaya.

Fanya hivi.
Ukiondolewa elimu yako yote, ukanyang'anywa hicho cheo ukaondolewa hizo nyumba na hilo gari utabaki kama NANI?
Hiyo ndo thamani yako.

Ayubu wa kwenye Biblia alijua kuwa THAMANI YAKE HALISI haikuwa kwenye wingi wa mali wala wingi wa wana na mabinti. Thamani yake ilikuwa katika KUMPENDA MUNGU na ndo maana vitu vyote vilipoondoshwa alibaki na simple statement: BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA...... Hata alipougua bado alibaki na thamani yake.


Kifupi alitafuta zaidi thamani yake zaidi kuliko thamani ya X. Na hicho hadi Mungu alijivunia. Mungu hakujivunia wingi wa mali za Ayubu. Lakini sisi tunajivunia wingi wa mali na kuhisi ndo vinatuongezea thamani.

Usijilinganishe na wasio na vitu ukahisi wewe uko juu. Thamani yako iko kwenye CONTRIBUTION  yako kwenye jamii.

Nilipoongea na huyo binti nilimwambia ahakikishe katika maisha yake anakuwa INDISPENSABLE. Yani mtu tegemeo kwenye jamii. Yani watu wakiwa na maswali wanalazimika tu kutafuta majibu kwako watake wasitake. Hapo unakuwa umejenga THAMANI YAKO HALISI. Jamii kukutegemea wewe siyo lazima iwe kwa sababu ya cheo chako au pesa zako. Inawezekana kabisa ukawa huna cheo na watu wakakutegemea. Hapo thamani yako halisi imedhihirika.

Kama cheo  ulichokuwa nacho "kimeEXPIRE" na watu hawakutafuti tena ujue ulipoteza muda kutafuta thamani ya X badala ya kutafuta thamani yako mwenyewe. Hawa ndo ambao ukimuondolea cheo inakuwa ugomvi. Mara mimi nimepigania nchi. Mara mimi hiki. Mara mimi ni muhimu. My friend umuhimu wako huwezi kuitangaza wewe. Wewe ulijisahau ukatafuta thamani ya X ukasahau kutafuta thamani yako. Kuna mawaziri leo hata ukiwashusha vyeo thamani yao kwenye jamii na taifa inajulikana tu. Walijua kutofautisha thamani ya X na thamani yao.

INDISPENSABILITY yako ina maana kuna vitu haviwezi kufanyika bila wewe kushirikishwa kwanza. Siyo kwa sababu ya cheo chako bali by virtue of who you have become. Nakupa mfano wa mwisho. Abraham alikuwa mwenye roho nzuri na ukarimu uliopitiliza kiasi kwamba mpaka alikuwa anaweza kukaribisha wapita njia tu wapate msosi na kupumzika kwake kisha ndo waendelee na safari zao. Yani unakuwa mwema mpaka unaishiwa wa kuwatendea mema unaanza kulazimisha kuwatendea mema wapita njia! Duh. Hii level Mungu mwenyewe akaona hii si mchezo. Huyu mtu siwezi kufanya jambo halafu nimfiche.

Ndo Mungu akamnong'oneza Abrahamu kuhusu mpango wake wa kuiadhibu miji ya Sodoma na Gomora. Tena akaanza kuwaombea watu wa miji hiyo.

See?

Sasa Mungu hakumwambia hizo habari Abrahamu kwa vile Abrahamu alikuwa mtu tajiri. No. Indispensability ya Abrahamu haikuwa kwenye mali bali utu wema wake.

So wewe kama unatafuta mali ili uwe muhimu hapo ni sawa sawa unagongelea msumari kule kwenye ncha.
You're doing it wrong.

Ukitaka kujua angalia watu wanajisikiaje wakisikia majina yafuatayo:


Rugemalila
Bakhressa
Dewji
Rostam


Nani hapa ni INDISPENSABLE?
Yaani ukimtoa huyo lazima umrudishe ili mambo yaende. Na ni nani hata akiondoka watu watamsahau kesho yake tu?

Utakuta watu I'm sure hawatajisikia the same ukiwatajia hayo majina. Kwa nini iwe hivyo wakati hao wote wana pesa?

Issue hapo ni THAMANI ya kila mtu kwenye jamii... Yaani kama ukimnyang'anya pesa zake zote jamii bado itamkubali as a person?
Hiyo ndo thamani yake halisi.

Hapo haijalishi kama ameshatafuta thamani ya X na kuipata. Hapo ni yeye. Thamani yake.

Jichunguze pia.

Are you becoming INDISPENSABLE too au bado unatafuta tu thamani ya X?

Mwisho wa maisha yako utakachowaza sana ni JINA GANI unaacha nyuma. Utaondoka dunia hii ukiacha nini kiishi miaka mingi baada yako? Kwamba ulikuwa na diploma ya ualimu?
Kwani wangapi wanayo?

Ukianza kutafuta thamani yako hutahangaika kujua watu wanakuonaje wala wao wanamiliki nini au wamepiga hatua kiasi gani. Utakuwa more concerned na kujua Mungu aliwekeza nini ndani yako ili uanze kukufanyia kazi mapema ungali na muda bado.

Ajiriwa ndiyo lakini find your real VALUE. Thamani ya Millard Ayo iko wazi. Hakuishia kuajiriwa tu. Alitambua nini Mungu aliweka ndani yake.
Jifunze kwake.

Soma sana tu but find your REAL value.
Tukiondoa elimu yako yote utabaki na nini?

Oa au olewa lakini jua THAMANI yako usije ukaanza kusumbua watu njiani eti, "Unajua mi nani?"

Ukiona mo sijui wewe ni nani ujue hujawa muhimu kwangu. So kaongeze thamani yako nitakujua tu. Au nakosea ndugu zangu? Kwani Max Malipo si unaona mwenyewe thamani yake? Au mpaka akwambie?

That's what I'm talking about.

Achana na thamani ya X saivi hiyo ilikuwa darasani.

Sasa hivi tunabadili swali:


YOU + (1⁄2)YOU + 1 = INDISPENSABILITY

Tafuta thamani ya "YOU".

Ukilipata jibu hapo basi tutakujua sisi wote very soon.


Nakutakia mema!

#FourteenSix

Till next time.


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511
www.andreamuhozya.blogspot.com

Alhamisi, 5 Oktoba 2017

WATOTO WA "WENZETU" HUPATA ELIMU TOFAUTI SANA NA KINA "SISI".

(Sifundishi ubaguzi....)

Wakati wa sakata la ajira za uhamiaji ambako usaili ulifanyikia uwanja wa taifa miaka kama miwili iliyopita kuna vijana wengi sana waliojitokeza.

Baadaye ikaja ya TRA shortly thereafter.  Na mwaka huu tena juzi juzi TRA tena wakaita watu kwa usaili wakajitokeza vijana wengi sana.


Katika hizo instances zote sikuona kijana wa kitanzania mwenye "ngozi nyeupe".

Nikawaza kidogo... Nikajiuliza.

Hivi kuna watanzania vijana wenye asili ya kihindi na kiarabu na hata kipakstani nk hapa nchini?
Nikajijibu kuwa "WAPO".

Nikajiuliza tena kidogo wote wameajiriwa?
Kaakili kangu kakaanza kusearch network kidogo kisha nikajijibu: "HAPANA"

Nikajiuliza tena: Sasa mbona hawaendi kufanya interview kama wenzao sasa?
Nikawa sina jibu. Eti, ulishawahi kujiuliza swali kama hilo?


UMASKINI WA FIKRA NDO KIFUNGO KIREFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA

Sijui kama umewahi kuishi kijiini. Lakini nikuulize tu hivyo hivyo. Hivi ukikuta wanaume 50 wako kwenye tope kwenye shamba kubwa la mpunga na wanakwambia  hawawezi kujikwamua katika tope hilo wanaomba msaada wako utawaza nini? Tufanye hivi liwe ni shamba ambalo wewe una uhakika hilo tope hata mtoto wa shule ya msingi anaweza kutoka.
Utawaza nini?

Kuna kitu hakiko sawa kwenye "bongo" za watu hawa. Si ndiyo?

Fikra zako zikishikiliwa na mtu mwingine utakuwa mfungwa maisha yako yote. Kitu kikubwa  kinachotutofautisha sisi sote siyo eti jinsia au rangi au imani nk. Ni jinsi tunavyotumia UHURU tuliopewa bure wa KUFIKIRI. Sijui wewe utakuwa kundi lipi.

1. Kuna ambao wanautumia uhuru huo KUFIKIRI kweli. Hawa hupiga hatua kidogo kidogo mwisho inakuwa kubwa. Hawa ni wa kuigwa mfano.

2. Kuna ambao wanautumia uhuru huo KUTOFIKIRI tu. Wapo tu hawataki kabisa kufikiri hata kidogo tu. Hapa unakuta wasomi tu wengi. Hawa wanahitaji #MAOMBI nadhani.

3. Kuna wanaoutumia uhuru huo siyo tu KUTOFIKIRI bali KU-DEMAND mtu mwingine afikirie kwa ajili yao.
Sasa hawa wanahitaji #ELIMU lakini nadhani na #VIBOKO  (ikibidi).

Jokes aside... Tuna kundi kubwa la vijana ambao hawataki kufikiri na wanataka mtu mwingine afikirie kwa NIABA yao.
Huu ndo unaitwa MSIBA WA TAIFA.


UNAPOJIFUNZA KWA MTOTO WA FORM ONE

Ngoja nikupe story kidogo.
Hivi karibuni nilisafiri kwa basi. Dar Lux. Basi zuri sana kwa kweli.


Nimekaa pembeni na kijana wa kiume miaka kama 14 hivi mwenye asili ya kiarabu. Nilikuta keshaketi so nikamsabahi na kujitambulisha. "Naitwa Andrea ni mjasiriamali na nafurahi kuwa na wewe safarini mdogo wangu". Akajikuta anasmile na kujitambulisha pia. Well safari imeenda story za hapa na pale but mpaka mwisho wa safari nikajifunza kuwa alikuwa anatoka likizo kurejea shuleni. Katika kuongea naye nikajifunza kuwa baba yake ni mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa.  Na kaka ya huyu kijana yuko nje ya nchi akisomea mambo ya usimamizi wa fedha (za familia)
Dada wa huyo kijana yuko Dubai anafanya kazi katika kampuni moja kubwa kupata uzoefu kwa ajili ya baadaye kusaidia biashara zao. Imagine huyo ni kijana wa Form One.
Yeye huyu kijana yuko kidato cha kwanza hivyo lakini baba yake anamshauri kuhusu kuchagua masomo ya biashara na ameshamwambia kuwa kuna mradi atampa akishamaliza mambo ya masomo yake ili ausimamie na ndo sasa huyo kijana akawa anasema bado anawaza maana anaona jinsi baba yake anavyo"hangaika" kuwaza mambo mengi na ku-manage biashara zake za petrol stations na malori na nyinginezo. Nikawa namtia moyo tu kuwa asiogope changamoto nk.

Lakini huku nikawa najiuliza kimoyomoyo.
Hivi na mimi nilisoma sheria ili nikasolve kesi za ukoo wangu au familia yangu au ili niajiriwe tu ilimradi kwetu waone hela inakuja wamshukuru Mungu kuwa wamepata mtu katika watu?
Niliwaza sana.

Nikawaza hivi sisi tunaposoma degree ya USIMAMIZI WA FEDHA tunakuwa tunataka tukasimamie fedha za nani?
Za familia?
Eti.

Hivi tunaposoma degree ya BIASHARA tunakuwa na lengo la kwenda kuwa  wafanyabiashara au kuajiriwa kwa mfanyabiashara ili yeye ndo AFIKIRIE cha kufanya atwambie sisi nini cha kufanya (Job description) halafu tukishakifanya atupe zawadi (mshahara)?

I mean tunaposomea UALIMU lengo ni kufanyanya nayo nini hiyo elimu.

Uhasibu. Uhandisi.

Kwa nini tuna elimu ya udaktari halafu TUNAGOMA mpaka Ulimboka anapoteza meno na kucha kwa ajili yetu?


Kugoma ni kulazimisha mtu mwingine afikirie cha kufanya. Na asipofanya huna cha kumfanya vile vile. Au naongopa ndugu zangu?

See?

Career guidance katika jamii ya kina sisi #WEUSI ni changamoto kubwa. Tunafanya tu mazoea.  Wengi tumesoma kwa mazoea tu. Mpaka leo ndo tunaendeleza trend hiyi hiyo kwa kizazi kijacho.

Nenda shule yoyote ya msingi leo hapo ulipo uliza watoto wanataka kuwa nani baadaye. Ukiacha wanaotaka kuwa Diamond au Samatta wengi wanakwambia: mwalimu, rubani, mwanasheria, "injinia", mhasibu, daktari, nk. Wachache sana watakwambia kuhusu kuuza nguo au kuuza viwanja au kuuza magari na vitu vya aina hiyo.  Why wazazi #WEUSI wanaona fahari kuwa na daktari au mwanasheria. Ndo maana zikitangazwa nafasi 50 kesho TRA hutoamini "nyomi" utakayoiona. Na hiyo itaendelea hadi Yesu arudi.


WHAT TO DO?

Kujitoa kwenye KIFUNGO cha fikra siyo kitu rahisi lakini ndo njia #pekee ya kuokoa uzao wako ujao. Lazima kuanza kuwaza TOFAUTI na mazoea. Mazoea ndo yametufikisha hapo. Na ni WEWE wa kuanzisha hiyo trend tofauti.

Tuanze kuwaza kama "wenzetu".
Kama wewe ni mzazi anza kitu chako sasa. Hata kama umeajiriwa. Anzisha biashara ambayo una uhakika unaweza kuwa-guide watoto wako wakasome elimu hiyo hiyo wanayosoma wengine ila wakimaliza waje kui APPLY hiyo elimu kwa biashara ya familia. Kama ni kusimamia fedha wasimamie za familia. Siyo tu za Vodacom.

Hivi watoto wa Bakhressa wanafanya kazi Vodacom?

Kuna wakati nilikaa na mtu mmoja hapa jijini ana "hela zake". Akasema mtoto wao wa kwanza wamemjengea Hoteli Zanzibar na mtoto huyo kwa sasa ana miaka kama 14 na anasoma hapa hapa Bongo. Na mtoto anajua. Na mtoto akiwa likizo huwa anaenda ofisini kwa baba yake kujifunza namna ya ku-MANAGE biashara kwa kuona.
Sasa mtoto huyo utamkutaje uwanja wa taifa kufanya interview eti. Au mei mosi amebeba Bango la kuongezwa maslahi?


Kwa sababu ya kushindwa kwetu kufikiri na kutaka SERIKALI ndo ifikirie kwa ajili yetu kuna siku watoto wetu wataambiwa wakafanye interview hata PORINI na wataenda. Tunakuwa kama kondoo tu kupelekwa kokote.

Nimejifunza mengi kwa hawa "wenzetu".
Mtanzania mmoja mwenye asili ya kihindi anamiliki majengo makubwa kama matano  hapa jijini. Miaka 7 iliyopita nilikuta anahangaika na mafundi city centre kwenye ghorofa moja refu huko juu walikuwa wanajenga RESTAURANT moja ya kisasa. Katika kudadisi mbona anapush push hivyo akaniambia hiyo restaurant ilikuwa ni ZAWADI ya birthday ya mtoto wake wa kwanza ambaye alikuwa masomoni Uingereza wakati huo. Na birthday ilikuwa bado wiki moja tu. Hebu fikiria. Sisi birthday tunapeana "baisko" na likeki kuuubwa au eti gari. Thinking yetu iko na shida. Why birthday ya mwanangu nisimpe mradi. Anakuwa anagrow na mradi wake. Of course tunaweza lakini nani yuko tayari aache COMFORT ya ajira kwa ajili ya kuset TREND mpya kwa vizazi vijavyo? Tunalilia NYONGEZA ya mishahara.


Nimesema ukiazimisha mwingine awaze kwa ajili yako akikataa huna cha kumfanya. Si raisi huyo hapo amesema kwa VISION aliyonayo saivi priority ni HUDUMA ZA kijamii. Period. Kwani madktari waliambiwa nini wakati ule? Asiyetaka mshahara uliopo aache kazi.
Unafanya nini sasa.
Waswahili wanasema kila mtu apambane na nini......?

Halafu na wewe unaanza kulaumu raisi mbele ya watoto wako. Eti raisi huyu tutamnyima kura. Wakati hata hukumpa kura yako so in fact hakuna utakachobadili. Unaharibu tu fikra za watoto wako wanaoanza kufikiri kuwa raisi ndo anasababisha wakose ada au wale matembezi wiki nzima.

Ukilazimisha SERIKALI ifikirie kwa ajili ya gharama ya elimu ya juu ya watoto wako watakachofanya hela ambayo zamani walikupa wewe yote saivi wataigawanya ili wapate watoto watano. Wanakwambia  tumedahili wengi zaidi na tumetoa mikopo kwa wengi zaidi.
#Smart.

Utafanya nini?

So kama hatutataka kufikiri tofauti tutaendelea kuishi hivi hivi vizazi na vizazi. Utajiri tunao elimu tunayo tunaenda kuiapply kwenye BIASHARA za "wenzetu". Na watoto wetu tunwafundisha hivyo hivyo.


EMBE! EMBE! EMBE! (Tuendelee)

Wakati niko mdogo kijijini kulikuwa na wahindi wana Pick Up walikuwa wakitoka Nansio wanapita jijini kwetu wanaenda vijiji vya mbali zaidi. Sasa walikuwa wakifika kijijini kwetu wanakuta watoto wa kiume tunawasubiri kuwapa MAEMBE kama zawadi. Embe! Embe! Hata Kiswahili chenyewe tulikuwa hatujui sisi. Embe! Wanachukua MAEMBE hadi wanatosheka wanaondoka. Sisi tupo tu. Na tunajisikia vizuri kweli kuwa wamekubali. Khaaa!
Kuna wakati wakawa wanatupa lift hadi kama kilomita moja hivi wanatwambia turudi. Tunafurahi kweli. Tumepewa lift kwa kugawa "mali" bure. Tulikuta wenzetu wanafanya hivyo so na sisi tukaendelea hivyo hivyo. Hata hatujui kwa nini.

Sasa hiyo inatofauti gani na leo nikapata degree (embe) nikaanza kuwaambia waajiri "Embe"! Embe! Embe!
Halafu wakapokea hiyo degree yako wakakupa kalift kidogo kimaisha (ujira) kisha wanakwambia haya shuka toto jurii.
Hahaaaaa.

It's the same.

Kuna siku nikaenda nao hadi mjini nilikuwa nimeshakuwa rafiki na hao watoto. Nione hawa wanatokaga wapi lakini? Baba yao akawa ananishangaa tu. Lakini nikarudi kijijini kwa miguu. Sasa si ningeshauzwa mimi kama ingekuwa dunia hii ya leo!! Lol.

Lakini naamini unaelewa jinsi tunavyofurahi kupata LIFT badala ya kufikiri ni namna gani TUMILIKI HILO GARI sisi wenyewe na tuwape "weupe" lifti. Nilisema sifundishi ubaguzi. Just kuchokonoa akili zetu ambazo mpaka leo zinawaza kuwa kuajiriwa kwenye ofisi ya WAZUNGU ni "BAHATI".

Sikia.
Watoto wa hao wahindi walikuwa wanafundishwa cha kufanya wakifika kijijini kwetu. Ni kusmile na kutuchekea kidogo. Sisi tunafundishwa na kugombania kugawa Embe! Na kupigana vikumbo nani embe zake zipokelewe.

Utumwa tu wa FIKRA.

Dewji hakuwahi kupanga foleni NBC kuomba kazi. Na wala watoto wake hutawaona njia hiyo. Wala kizazi chake chote.

Au watoto wa Ali Mufuruki wanaenda pia uwanja wa taifa eti interview?
Wapi.


Lakini sisi tumekazana tu kuanzia babu mpaka mjukuu" Embe! Embe! Embe!

Tutaishi kwa lifti na mpaka tutie akili.

#ThreeSixteen
#FourteenSix


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511

Ijumaa, 29 Septemba 2017

MAHALI SAHIHI PA KUANZIA BIASHARA

*MAHALI SAHIHI PA KUANZIA BIASHARA*

Katika maisha mafanikio huwa ni kitu cha watu wachache tu. Iwe kwenye: masomo, michezo, muziki, siasa, biashara, mahusiano nk. Ni wachache tu hufanikiwa. Hii ni kwa sababu mafanikio ni mchakato ambao watu wengi mno hawako tayari kuufata maana inahitaji NIDHAMU ya hali ya juu na BIDII ya kiwango cha juu pia. Na haya si maneno yangu tu bali hata watu waliofika mbali zaidi kama Mohamed Dewji wanasema hivyo.Katika audio niliyokutumia tulipoanza mawasiliano kwa Whatspp...mwishoni kabisa mwa ile video nilieleza kuhusu aina za biashara zinazoweza kukusaidia kufika mbali. Mfano Real Estate, Platform Business, Minerals Oil and Gas nk. Ya mwisho katika mlolongo wa kuzitaja nikasema ni INTELLECTUAL DISTRIBUTION. Na nikasema ndo biashara ambayo nimewashauri watu wengi sana hasa wanaolalamika kuhusu shida ya mitaji kuwa mikubwa kwamba nawashauri kuanza na hii kabla ya kwenda biashara zingine kama Real Estate na zingine nilizotaja. Tatizo watu wemgi hawataki process. Wanataka wafanikiwe kufumba na kufumbua. Lakini naamini wewe unaamini katika process.


So ngoja nitoe ufafanuzi kidogo wa hii biashara kisha utaamua mwenyewe kama unaona inakufaa pia au la. Mimi kazi yangu ni kukufundisha tena kwa kina (in details) bila kuchoka. Lakini maamuzi ya kusema uendelee kujifunza zaidi kwangu hayo ni maamuzi yako. Japo najua ukiamua kuendelea tu kujifunza bila kuchoka utakuja kuelewa vitu vingi sana ambavyo wengi hawaelewi. So sasa ngoja nifafanue zaidi.


I. *INTELLECTUAL DISTRIBUTION NI NINI?*

Hii ni biashara ngeni kwenye masikio ya watu wengi. Hivyo ni biashara ambayo wengi inawapita. Kutokana na kuwa ngeni hii bness imepewa majina mengi mno.

Na kama ilivyo katika biashara nyingine zote hii nayo SIYO RAHISI. Hakuna jambo lenye faida ambalo huwa rahisi rahisi tu.  Ila tu hii biashara haina complications kama biashara zingine.

*Sasa intellectual distribution ni nini?*

Huu ni mfumo au utaratibu wa kufikisha taarifa kuhusu jambo fulani ama huduma ama bidhaa kwa KUAMBIANA AMBIANA. Yani mi nikwambie wewe kitu kisha nikwambie na wewe kawaambie wawili. Na ukiwaambia  unawapa maelekezo pia hivyo hivyo wao kila mmoja aambie watu wawili. Sasa kwa mtindo huu ujumbe ule utafika kwa watu wengi mno. Kama ambavyo tumeambizana kuhusu wapi wanauza simu nzuri au mabegi mazuri au wapi wanapika chakula kitamu sana.


Changamoto kubwa hapa ni kuwa ujumbe unaweza kufika mbali lakini ukawa umeshaongezwa chumvi au umeongezwa maji.


Lakini kama kutakuwa na utaratibu labda ujumbe uwe unapewa ukiwa umeandikwa na pia uwape wengine ukiwa umeandikwa kama ulivyoupokea basi hilo tatizo la kuongezwa chumvi au maji litakuwa halipo. Right?

Kwa sababu ya NGUVU ya habari kutembea kwa njia ya mdomo zaidi basi kuna makampuni yaliamua kuutumia utaratibu huu kwa MAJARIBIO kama njia ya kutangaza bidhaa zao. Yani mfano kampuni FULANI inakupa maelezo kuhusu bidhaa yao. Labda simu. Halafu wanakwambia ilivyo nzuri. Kisha wanakwambia nenda kawaambie watu wawili tu unaowajua. (Hii ndo inaitwa INTELLECTUAL DISTRIBUTION yaani unadistribute intellect). Na wao uwaambie hivyo hivyo. Kampuni zile zikaja kugundua kuwa zile habari zilifika mbali mno. Ambako hata watu hawana TV au hawasikilizi sana redio au kusoma magazeti.


Kampuni hizo zikaamua kuurasimisha mfumo huo. Ila sasa zikasema ukipeleka habari UNALIPWA kama uliyempa habari atakuja kwenye kampuni kununua ile bidhaa uliyomwambia. Kwa hiyo unachosambaza siyo kitu bali TAARIFA. Information. Sasa jiulize hivi huwezi kusambaza taarifa? Hujawahi kumwambia mtu kuhusu jambo fulani linapatikana wapi? I bet ulishawahi. So hapo hukuwa unauza hicho kitu bali ulikuwa unasambaza tu taarifa. Kama ulimwambia mtu kuwa simu nzuri zinapatikawa wapi hukuwa unasambaza simu ya mtu au hakuna aliyekuuliza kama siku hizi unauza simu. Wewe ulikuwa unasambaza tu TAARIFA.

Sasa unayemwambia pia anaweza naye kuwaambia wengine ambao wewe hata hawajui.  Ina maana anatumia muda WAKE kusambaza taarifa. Kwa hiyo sasa mmeanza kuwa wengi mnaosambaza hiyo taarifa. Hicho kitu ndo kinaitwa Intellectual Distribution.

Tuendelee. Usichoke. Jifunze tu.
II. *FAIDA ZA INTELLECTUAL DISTRIBUTION*


Kwa kawaida watu wengi wanatamani kumiliki biashara lakini hawajui basics yani vitu vya muhimu katika biashara ambavyo ni hivi vifuatavyo:


1. Ubora wa bidhaa. Yaani bidhaa yako tukiiweka pamoja na bidhaa ya Mengi zinaweza kushindana kwa ubora?

Usitake kuwa kama Mengi anyhow tu. Lazima ujifunze ukweli wa mambo.


2. Namna gani watu wengi watapata habari kuhusu hizo bidhaa. Utatangaza kwenye TV au utatenga bajeti ya kuweka mabango barabarani na mitaani *nchi nzima* mitaa yote. Au utatumia njia kama waliyotumia Facebook tu hawana Bango wala tangazo na bado Facebook inajulikana zaidi kuliko brand kama Vodafone.

Tarehe 27 June 2017 Facebook walitangaza kuwa wana members (users) bilioni 2 wanaopost na kucomment nk kwa mwezi. Imagine. Lakini ulishawahi kuona tangazo la Facebook kwenye TV eti ili ijulikane kwa watu waje kujiunga?  No. Njia gani inatumika ili watu waijue Facebook?

Simple: *WATU NDO WANAANBIANA*. Hata wewe uliambiwa na mtu. Hiyo ndo inaitwa *RECOMMENDATION BUSINESS* na hii ni rahisi hata wewe unaweza.
Unaweza kufanya anakwambia ana


Ama unaweza kufikisha hizo recommendations zako kupitia njia ya kisasa zaidi ambayo wengi wanaita SOCIAL MEDIA lakini sisi tunasema it's no longer just social media but SOCIAL BUSINESS. Yaani kama bado unadhani vitu kama Facebook na Instagram ni just social media basi unaachwa nyuma. Jifunze haraka. Hizi ni business platforms. So in this regard unaweza kuzitumia kufanya hii recommendation business au Intellectual Distribution.


3. Mfumo gani mwepesi wa kuutumia kuwafikishia bidhaa mahali walipo siyo mpaka waje ulipo. Yaani wanunuzi wako watatoka mahali unapoishi wewe au waweza hata kutoka mabara mengine? Unafanyaje ili kitu chako wateja wengi wawe si majirani zako. Hili watu wengi hawajui wafanyeje. Ulishawahi kujiuliza kwa nini hakuna tajiri mwenye kutumia duka kuuza vitu vyake. Maana duka ni biashara inayohudumia watu wachache tu wanaoweza kufika duka lilipo. Hakuna tajiri mwenye duka.


Watu wengi wameanza biashara huko mtaani bila kuangalia hayo mambo matatu na wameishia njiani. Nadhani unaelewa ilivyo muhimu kuyachukulia serious hayo mambo matatu. Hii ni elimu ya biashara ambayo huwezi kuipata kwenye Degree au Masters ya Biashara.


Sasa sisi tunafundisha biashara siyo kwa nadharia. Bali practical. Na tunakuonyesha biashara ambayo inatumia system inayoweza kumfanya mtu wa kawaida kabisa akaweza kuwa mfanyabiashara mkubwa mno au hata kuwa mwekezaji na hayo mambo matatu yote akawa ameya-cover bila shida. Yaani akawa anajihusisha na biashara ambayo:


1. Ina bidhaa bora sana tayari. Kwa hiyo anaposambaza taarifa hana wasiwasi na ubora wa kitu anachosema.


2. Mfumo mwepesi wa kufikisha taarifa  (njia ya watu kuambiana tu.


3. Njia nyepesi ya watu kupata hizo bidhaa endapo wako mbali na wewe ulipo. Yani kama ambavyo Azam Cola inauzwa mbali kabisa na hapa Dar es Salaam ambapo ndo Bakhressa anaishi.


Na uzuri ni kuwa mtaji wa kuanzia biashara aina hii ni mdogo sana sana ukilinganisha na biashara zingine. Pia hapa mtu atapata mafunzo mengi mno. Hebu fikiria tu ni mambo mangapi umejifunza toka umenifahamu kwa muda huu mfupi. Na hapo hata hujakaa na mimi kwa muda mrefu. Sasa nataka ufikirie ni mambo mangapi utajifunza kama ukiwa katika mikono ya watu aina yangu kila siku kwa miezi sita tu?

Sasa naomba utazame video links nilizokuwekea hapo chini zinaelezea biashara hiyo ninayokwambia ambayo binafsi nimewashauri vijana wengi kuifanya na nimeona wakianza kupiga hatua kuelekea katika mafanikio yao. Of course mimi mwenyewe nafanya na imebadilisha maisha yangu sana! Again kumbuka niliyokufudisha kwenye ile audio kuhusu makundi ya watu. Wenye muda bila hela wenye hela bila muda nk.nk.

And one more important thing ni kuwa *Intellectual Distribution* ni biashara ambayo inakupa kitu kinachoitwa *LEVERAGE* yaani uwezo wa kujigawa wewe ukawa kama vile uko kila mahali. Kwa hiyo unaweza kukuta unapata pesa na muda unao pia. Watu wengi wamekuwa wakii-miss hii concept na hivyo kutoelewa vizuri namna hii biashara ilivyo na manufaa makubwa sana kupitia hiyo LEVERAGE hasa kwa mtu wa kawaida. Yaani uwezo wa wewe kunufaika kupitia muda wa uzalishaji wa watu wengine. Na mfumo unakufavour sababu ni *Recommendation Business*. Again usichoke kujifunza vitu vipya. Mshauri wa Uchumi wa maraisi wawili wa Marekani Profesa Paul Zane Pilzer anasema mafanikio au utajiri upo mikononi mwa wale wanaojifunza vitu vipya HARAKA.


Lakini pia tunawafundisha vijana kuwa itakusaidia kuongeza mkondo mwingine wa kipato tofauti na kipato ulichonacho kwa sasa.

Hii ni muhimu kwa sababu matajiri wote wana njia nyingi za vipato. Forbes wanasema Average Millionaire ana njia saba tofauti za kuingiza pesa. Maskini wana njia hasa moja tu, utakuta hasa mshahara au ana duka afu basi.


Angalia mtu kama Bakhressa ana vyanzo vingapi vya mapato. Au angalia Mengi, huyu ana mahoteli nje ya nchi, mashamba, biashara za madini, media house (TV channels, redio stations na magazeti), ana shares kwenye viwanda vya CocaCola hapa Dar na Moshi, ana viwanda vya kuzalisha bidhaa kama sabuni nk, na vitu vingine viiingi. Huko kote anapata mapato.

What about you?


Fikiria wewe unataka uwe hivyo au mkondo mmoja tu wa kipato unakutosha?


Mtu kama huyu mwenye vyanzo vingi vya mapato huwezi kumlinganisha na mwajiriwa anayesubiri mshahara eti au mtu aliyejiajiri tu ana duka lake mahali fulani pesa zinatoka hapo tu. Kuna tofauti kubwa sana. Na ni muhimu ukaifahamu pia.


Sasa hiyo video link  ninayokutumia inaelezea biashara ambayo unaweza kuifanya popote na biashara hiyo inaweza kukupa *vyanzo vingi vya mapato pia* kwa kutumia huu mfumo wa intellectual distribution yaani recommendation. Nimesema Facebook inatumia recommendation lakini hakuna anayelipwa kwa kurecommend kwa mwenzake. Lakini sisi katika biashara hii utalipwa kwa kurecommend kwa mwingine. Naamini unaweza kufanya hyacinths yote ukiwa nyumbani kwako. Ndiyo dunia mpya ya leo hii si lazima ukakodi duka mahali ulipe kodi wakati unaweza kufanyia kazi nyumbani kwako.Naamini mpaka hapo tuko pamoja.


So kama ulinifatilia kwa umakini toka mwanzo kwenye audio yangu mpaka sasa basi utaelewa mara dufu hizi video. Nimeweka link kwa lugha ya KISWAHILI na nyingine kwa LUGHA ya kiingereza.


1. SWAHILI (testimony)...

Play Video
2. ENGLISH (Official Presentation)...

Play VideoKaribu sana ukishaziangalia hizo video niambie kama upo interested kujifunza zaidi!


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
WhatsApp +255 788 366 511

Jumanne, 26 Septemba 2017

UKITAKA KUPIGA HATUA KIBIASHARA BASI ACHANA NA HELA ZA MAJIRANI ZAKO AU RAFIKI ZAKO AU NDUGU ZAKO


Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba? No lakini vibaiskeli viko kila mahali Buguruni mpaka kigamboni.


Mzee Mengi hauzi maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.

Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na *The Citizen* na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje.

Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake.


Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara.

Tatizo la watu wengi ni kudhani kuwa ukianza kitu chako mfano biashara au ujasiriamali basi ndugu zako na marafiki na majirani ndo wanapaswa kukusapoti. Wasipokusapoti *unanuna* na kuona hawakutakii mema. Unawasema na kulalamika.
Wewe kuna kitu hujajua bado ukikijua kwanza hutataka kuhangaika na makundi hayo ya watu kibiashara.

Kama upo hapo unawaza kuanza biashara na unafikiria kuwauzia jirani zako au ndugu zako basi kajipange upya kwanza. Utakuwa disappointed  na kuanza kulaumu watu bure. Ndiyo maana Mungu alikuumbia ndugu na marafiki wachache kuliko idadi ya watu usiowajua dunia hii.
Ukitaka kupiga hatua kibiashara achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Diamond hauzi karanga kwa ndugu zake au majirani zake. No wateja wa karanga zake ni watu tofauti kabisa.  Majirani wanunue wasinunue no problem.
Wanaoshindana kuview nyimbo zake You Tube au kuzidownload wala wala siyo eti rafiki zake. Ni watu tofauti.

Vijana wengi wanaojifunza kwangu biashara huwa wananiuliza swali: *"SASA BRO NTAMUUZIA NANI MAANA HUKU NINAKOKAA DUH WATU NI WA HALI YA CHINI KWELI KWELI NA HATA RAFIKI ZANGU YANI BORA MIMI"*
Jibu ni moja tu hapa: Ukitaka kupiga hatua katika biashara *achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako*

Anayezalisha tissue papers au toilet papers anauzia rafiki zake? Wanaoanza kutengeneza furniture huwa wanauza kwa ndugu zao? Sasa why wewe unawaza jirani zako ndo wateja.
Unakuta mtu anataka kuanza kufuga kuku anataka majirani zake na wafanyakazi wenzake ndo wale kuku wake! Kwani wanaoshona nguo kwa *Sheria Ngowi* ni ndugu zake au eti jirani zake? No.
Ni watu wengine tofauti kabisa. Maana kwanza jirani ataanza kuleta ujirani kwenye biashara yako changa halafu mtaishia kugombana bila kutarajia.
Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Kakangu alinunua vitu kwangu miaka mitatu na nusu baada ya mimi kuanza biashara. Tena alinunua vitu vingi hadi nikachekelea kwa kweli. But unaona sasa ningesubiri anunue ndo niendelee ningekuwa wapi? See, ukisubiri sapoti ya ndugu unaweza kuipata mwaka keshokutwa.
Sasa si utakufa masikini?

So we anza tu ndugu waje wasije isikukwaze. Kwani mwenye Facebook wewe umejiunga kwa kuwa mna undugu au eti unamsapoti? Kama vipi we acha kujiunga Facebook uone kama atakufa njaa kwa kuwa hutaki kumsapoti.

Kwani hiyo simu uliyonayo unadhani mwenye hiyo kampuni hana ndugu? Angesubiri ndugu zake au rafiki zake wamuuingishe si angeacha biashara kwa kukosa wateja? Maana wewe unatengeneza Tecno wakati ndugu zako wanachotamani ni iPhone hapo si utalaumu watu bure?

Mi nimeona jirani zangu wakija kuuza unga wa lishe. Lakini taste yetu kwenye hivyo vitu ni nyingine. Anasema "niungishe tu hata huu mfuko mmoja tu jirani" Sasa hapo mtu anauza kwa kuhurumiwa. Sasa utafanikiwa kweli? Nilipoanza biashara nilikuwa na list ya rafiki zangu ndugu zangu na majirani. Tena wenye uwezo mzuri. Kila niliyemshirikisha anakwambia tu *"TUPO PAMOJA"*. Hahaaaaaa.
Hawakununua. Nimekwambia hivi kakangu alinunua kwangu miaka mitatu na nusu toka nianze. Baada ya kuona naambiwa tu TUPO PAMOJA ndipo nilipostudy watu waliofanikiwa waliuzia nani vitu vyao. Nikapata jibu. Hebu jiulize.

Kwani anayejenga hoteli anawajengea rafiki zake au majirani? Nani akalale sehemu ambako anajulikana?  Sasa ukitaka ujenge mgahawa au saluni halafu rafiki zako ndo waje utakuwa hujajua kitu bado. Utaifunga tu hiyo saluni.

Cha msingi wewe tengeneza VALUE. Hilo ndo muhimu. Kisha wateja SAHIHI watakuja tena kutoka mbali kweli kweli. Ukiwaza  kufungua biashara huku unawaza mashosti sijui washkaji utaifunga siku si nyingi afu utasema eti wateja hakuna.
Kweli?
Yani katika nchi yenye watu karibu milioni 50 unaweza kukosa wateja kabisa kweli? Ulichokosa siyo wateja ni maarifa.  Knowledge.

Ukitaka kufanikiwa katika biashara hasa mwanzo fanya kama vile huna ndugu wala majirani. Fanya kwa ajili ya watu wasiokujua. Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako. Wakizileta well and good wasipoleta no problem.

Reginald Mengi wakati anaanza kuuza maji ya chupa hakuwa anatafuta marafiki wa kuyanywa hayo maji. Au unadhani ndicho alichofanya? No. Maana unajua marafiki nao huwa ni rahisi kwao kufikiri unawageuza ngazi ya kupandia. Wengi huanza kuona wivu kwa siri kuwa wewe utawazidi kimafanikio sasa kwa nini wakusapoti huku hawataki uwazidi.

Ndo maana nimesema wewe concentrate na VALUE. Dunia ya leo ni dunia ya VALUE. Value yako ikiwa nzuri wateja wako watatoka sehemu ambazo hukuwahi kufikiri kabisa. Kuna siku nimeitwa Oysterbay nyumba ya mtu mmoja mkubwa akihitaji kununua kutoka kwangu. Value. Lakini majirani zangu wala hawana habari. Wana taste nyingine. Value yangu huenda haijawagusa. So sikasiriki.
Achana na hela za majirani. Usizipigie hesabu kabisa. Ndo maana hakuna tajiri anayehangaika na jirani zake.

Umeelewa?

Au niendelee kidogo?😄 Okay... Jifunze kwa ma-MC hawa washereheshaji. Unakuta MC anaishi Kijitonyama lakini sherehe za Kijitonyama watu wanachukua MC wa Magomeni. Sherehe za Masaki watu wanachukua MC wa Mbezi. Wakati Masaki pia kuna ma MC wanaishi. Sherehe iko Mwanza watu wanaita MC kutoka Dar au Arusha. MC huyo huyo majirani zake wanasema *"aah huyu ana bei sana tuchukue fulani afu huyu siku hizi anajiona kweli wakati ni MC wa kawaida tu"*. Unaona sasa? Huyo MC angesubiri kusherehesha kwa majirani angesubiri mpaka azeeke.

Kitabu kinasema Nabii hupata heshima nje ya nyumbani. Ukisubiri watu wanaokuzunguka ndo wawe wateja hujajua vizuri maana ya neno MTEJA.

Huoni Bar iko Sinza lakini wadau wake ni watu wa *Tabataaaa!*
Majirani wanaokunywa pombe wanaoishi jirani na hiyo Bar wanaenda kunywea Kinondoni. Kwani mwenye Samaki Samaki hana majirani? Lakini hapo Samaki Samaki wanaokula na kunywa ni jirani zake? No!

Sasa kwa nini wewe unatengeneza sabuni ya maji unafikiri jirani zako ndo wateja? Wasiponunua unaona eti hawataki kukupa sapoti. Nimesema achana na hela za rafiki zako na jirani zako na ndugu zako. Utafika mbali sana. Yani ndugu watakuja huko mbele ya safari. Au utashangaa hawatakuja tu milele.


Nadhani sasa umeelewa vizuri japo ndo hivyo inauma kusikia lakini ndovile!

Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako!

Ukifanya hivyo ndo utakuwa umeanza kuelewa shughuli hii ya biashara na ujasiriamali ilivyo.


Nakubariki. Nakutakia mema!

#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa

Ijumaa, 15 Septemba 2017

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE BUT WHAT YOU DO IS... (WEWE SIYO VITU UNAVYOMILIKI BALI KILE UFANYACHO!)

Niliamka katikati ya usiku mnene... na hasa sikuwa nimeamka ila niliamshwa na baridi kali la jiji la Johannesburg kwenye majira ya baridi, baridi ambalo mpaka leo sijui lilipenyaje-penyaje katika wingu zito la nguo nilizovaa, sweta, shuka, na blanketi ambalo niliamini lilitengenezwa ili tu kuithibitishia dunia kuwa baridi si lolote wala si chochote!

Usingizi ulikata kwa sababu ya hilo baridi lakini pia (na hasa) kwa sababu ya wimbo ambao niliacha ukiplay kwa sauti ya chini chini kwenye simu wakati nalala! Nilipoamka ulikuwa unaishiaishia ile replay sauti ikawa inaishiaishia...

Akili yangu ikaanza kufikiri sana kuhusu siyo hasa kilichokuwa kikiimbwa bali mmoja wapo wa waimbaji wa wimbo huo...

Replay ikawa ishaanza tena.. Sauti yake maridadi yenye kuimba kama inatetemeka kwa mbaali ikajaa sana masikioni mwangu na kiukweli hadi moyoni mwangu...
Nikajikuta naanza kusikiliza tena:


"This life don't last forever (hold my hand)"..., wimbo ulianza.

"So tell me what we're waiting for? (hold my hand)

"We better off being together (hold my hand)

"Being miserable alone....

Yes sauti ya Michael Jackson aliyeshirikishwa na Akon ilitetemesha ngoma za masikio yangu kuliko baridi lilivyotetemesha ngozi yangu mpaka nikasahau hata hiyo baridi yenyewe. Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kuwa sauti hiyo ilikuwa ya mtu ambaye alikuwa hayupo duniani tena. And ndo basi tena. Dunia nzima ilikuwa ikimkumbuka Michael Jackson.

Magazeti yaliandika,  Redio zikatangaza, internet ikaenea kumbukumbu zake. Vitu vingi vilisemwa ambavyo baadhi yetu hatukuwahi kuvisikia. Hakika dunia ilijaa huzuni kwa namna yoyote ile ambayo ungetazama simulizi za maisha yake na kazi zake.

Lakini jambo moja ambalo lilikuwa DHAHIRI katika mijadala yote ya kifo chake ni kuwa watu hawakuwa wakiongelea eti alinunuaga nini au alikuwa anamiliki nini na nini au alikuwa anaendesha gari gani nk. Habari zote ziligusa zaidi ALIFANYA NINI. Aliwagusa watu wengi siyo kwa majumba yake au hela zake bali namna alivyowafanya watu wajisikie.

Wimbo uliendelea kuplay nikiwa hata siusikii tena kiukweli nikiwa nawaza tu IMPACT ambayo Michael Jackson aliacha ulimwenguni kiasi kwamba kijana wa kitanzania kama mimi kutoka huko Ukerewe nilikuwa namjua na kuguswa na jinsi alivyofanya kazi yake angali duniani na mpaka kusikitika kuwa hatunaye mtu kama huyo dunia hii tena.

NINI NATAKA KUSEMA:

Mara nyingi sana tumekuwa tukiwaza vitu vya kuwa navyo. Vitu vya kumiliki ili na sisi tuwe WATU KATIKA WATU. Mashindano mengi duniani siyo ya kazi bali ni ya VITU. Siyo kwenye michezo au siasa au kanisani mwenye gari la kawaida anawaza lini naye atapata gari kama la DEWJI. Anasahau kuwa anapaswa kuwaza KAZI GANI afanye itakayowagusa watu wengi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote aliyewahi kutokea duniani. Wengi wetu tunajisahau sana na kuingia katika mtego wa kushindana na watu bila hata kujua kuwa tumeshakuwa OBSESSED na kuwazidi wengine kiasi kwamba tumesahau hatukuumbwa kuja kumzidi mtu. Mashindano yasiyotarajiwa yametupelekea kujikuta tukitengeneza maadui badala ya marafiki. Kwa kutaka sana kuwa AHEAD katika vitu tumejikuta tunacompromise standards zetu za behaviour ama tumejikuta tunakuwa so impatient na process na kutaka tu kutangulia.

Tunasahau kuwa cha muhimu kiukweli siyo nyumba ngapi tutawaachia watoto. Mfalme Suleiman kitu kikubwa zaidi anachokumbukwa nacho ni HEKIMA siyo dhahabu ya OFIRI.  Maana dhahabu zake zote saivi hata sijui ziko wapi. Lakini HEKIMA yake ipo hadi leo!

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE...BUT WHAT YOU DO IS..

Haimaanishi usimiliki. No. Miliki mpaka shetani ajue kuna mtoto wa Mungu hapana chezea! Lakini usisahau kuwa vitu unavyomiliki havitakudefine wewe ni nani hapa duniani. Bill Gates hatambuliwi kwa wingi wa hela zake au majumba anayomiliki ila kwa CONTRIBUTION yake kwa wanadamu wenzake hasa MASIKINI. Ndo maana akala wali maharage Tanga wakati angeweza kuagiza chakula kutoka The Ritz au Ceaser's Palace. Jifunze kwake!

Anamiliki lakini akiondoka duniani hakuna mtu atakuwa anakumbuka viatu vyake au saa ya milionI 100. Ndo maana mara nyingi matajiri wengi huvaa "simple" ili kusaidia wanaowaangalia wasiwa-define kwa vitu wanavyovaa.  Steve Jobs alikuwa anavaa jeans na turtlenecks tu basi. Ili usiangalie sana nje kwake.

Warren Buffet yuko hivyo hivyo. Nk. Na hata matajiri wanaopiga pamba kweli kweli wanajitahidi kufanya vitu vingi kuonyesha kuwa wao ni zaidi ya mavazi yao na magari yao.

Alipofikwa na mkasa mbunge Tundu Lissu gari lake lilionyeshwa kutobolewa na risasi, right? Mi binafsi sijasikia mtu akilihurumia gari na kusema "OH MASIKINI GARI LAKE". Kumbe vitu vyetu havina maana kubwa sana linapokuja suala la kupima "value" yetu. Yani ni hivi unaweza kuwa na ardhi au majumba yenye thamani ya mamilioni lakini thamani yako halisi kwa watu halisi ikawa ni sawa na thamani ya noti ya sh elfu 10 tu. I'm serious.

Kijana mwenzetu #McPilipili amepata ajili na pia hakuna mtu anawaza gari lake. Why? Coz ile Prado is not WHO HE IS. Naamini atakuwa analijua hilo. Albeit now.
Watu wamepost kumtakia heri na kupona siyo eti kuliombea gari. Insurance will take care of that. McPilipili ni WHAT HE DOES. Namna ambavyo amekuwa akifanya watu wajisikie. Na si ana nini.
Unajifunza kitu?

Sasa swali.
Mimi na wewe tukianguka leo hii Mungu akatuita (ni mfano tu usiogope) tutaacha mjadala gani nyuma. Acha watu wachache ambao maybe ulipishana nao kiujumla. Angalia wengi. Majority watafeel vipi.

That's why I write bila kuchoka. Nimeandika article hii kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa usiku ndo nikapumzika. Yes mpaka usiku wa manane maana ninajua kipawa cha kuandika nimepewa nikitumie kuelimisha wengi. Tena haraka. Naamini maandishi yangu siku moja yatasomwa na watu wa mataifa mengi mno. Maandishi yatakayoacha ALAMA maishani mwa watakaoyasoma.

Nilichagua ujasiriamali badala ya sheria kwa kuwa niliona kwangu hii ndo njia nitakayoweza kuufikia ulimwengu wote kwa kazi yangu.

Na wewe unapaswa kuona ni namna gani UNACHOKIFANYA kitakudefine. Usipofushwe na hamu ya gari zuri na nyumba nzuri na viwanja. Hivyo vitakuja tena vingi mno kama ukiamua kuwa BORA ZAIDI katika jambo unalilifanya. Jifunze kuwa bora katika IMPACT YAKO kwa jamii. Hilo ndo la msingi.

Sisi hatumkumbuki na kumfuata Yesu Kristo kwa sababu alikuwa na mali. No.. WHAT HE DID IS WHO HE IS!

Mandela ni Mandela Gandhi ni Gandhi kwa sababu ya  vitu walivyofanya. WHAT THEY DID.

Tarehe 14 October haijafanywa sikukuu nchi hii sababu ya kukumbuka mali za Baba wa Taifa. No. But WHAT HE DID. Sababu WHAT HE DID WAS WHO HE BECAME TO US. Inakumbukwa impact sahihi.
Legacy.

Hata viongozi wa nchi zetu hizi wenye kusemekana kuwa na mali mengi kama hawana IMPACT sahihi katika maisha ya watu basi thamani yao halisi inazidiwa na fundi seremala ambaye yuko kijijini huko hata hajulikani lakini ameishi kwa kutengenezea watu vitu vizuri na wanamthamini kweli kweli. Huyo ana thamani kubwa hata mbele za Mungu kuliko Waziri ambaye ukitaja jina lake watu hata hawalikumbuki na bado yuko hai wala hajafa licha ya kuwa ana majumba ya kifahari na yule seremala analala kwenye mkeka. Ndipo utakapoona seremala anakufa kwa amani (kamaliza kazi) na huyu msomi anakufa kwa pressure na simanzi  (akiwa anajua anadaiwa kazi).

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE... BUT WHAT YOU DO IS.

Mohammad Ali alipoondoka watu walikumbuka alichofanya siyo ati alikuwa analalia kitanda cha aina gani au anaishi nyumba ya ukubwa gani.  Issue ni alifanya nini.


Hujawahi kujiuliza mpaka leo watu wanaongelea BISHANGA na hata hayupo active sana kuigiza kama zamani. Hujaona watu wanaongelea Kanumba na hayupo miaka sasa na wengine wapo wanaigiza lakini bado watu wanaongelea Kanumba.
Impact.
Hawamkumbuki kwa sababu alinunua labda HAMMER au aliporomosha majengo huko Mbweni lakini WHAT HE DID.
Not what he had.

Jifunze.
Usishindane na mtu. Shindania UBORA wako katika like alilokuitia Mungu kufanya. Ukichunguza kazi yako utagundua bado UNAPWAYA sana kwa VIWANGO vya Mungu. Fanyia kazi ubora wa kazi yako. Hiyo ndo watu watakukumbuka nayo. Usiandike kitabu tu ili uuze. No kitaacha ALAMA gani. Siyo kitakufanya ununue gari au kiwanja. Kuna vitabu vingi sana kuhusu mafanikio kifedha lakini THE RICHEST MAN IN BABYLON si mchezo. Kuna vitabu vingi vya kukuhamasisha kufuata ndoto zako bila kuchoka lakini THE ALCHEMIST si mchezo.

Waliovisoma wanaelewa nasema nini.

Mwalimu Mwakasege ni maarufu siyo kwa aina ya magari au majumba. Nina uhakika ana miliki pia kama mwana wa ufalme lakini kinachomtambulisha kwa watu siyo VITU bali KAZI YAKE.

Usikubali utambulishwe na watu kama "yule binti anayevaaga high heels" au "yule jamaa anayeendeshaga NOAH ya silver". Mimi nitafurahi nikitambulishwa kama yule jamaa anayeandikaga kuhusu mambo ya kutunza muda na mambo ya ujasiriamali, nk. Yes WHAT I DO ...not what I have.

Kuna mtu anaitwa MWALIMU MAKWAYA mi sijui hata anapoishi wala anamiliki nini kijana yule lakini najua ANAELIMISHA watu hasa vijana.

What about you?
Watu wanaweza kukutambulisha kwa kazi unayofanya au lazima watumie mavazi yako au nywele zako au gari ndo mtu akujue. Hapo utakuwa unaishi maisha yasiyokuwa na IMPACT kwa a greater majority. Sikia ujue mi siongelei familia yako. No. Sijui umejenga kwenu. That's good hongera sana. But nazungumzia mtu asiyekujua wewe in person amenufaika na nini kwa uwepo wako. Huwa nafurahi nikikutana na post zangu kwenye groups za whatsapp hata kama jina langu wametoa. Huwa nafarijika kuona kumbe nina gusa watu wengi tusiofahamiana. It really makes me happy. Contented.

Josiah Otege, Josinah Leonard , Exuper Njau, Haruni Leonard, Binti Luzutta nawapa challenge: WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE but WHAT YOU DO IS.

Na wewe msomaji wangu naomba ufikiri kama nilivyofikiri mimi usiku ule nilipoamshwa na baridi na kukutana na sauti ya Michael Jackson. Nakuacha na maneno matano ya kwanza kwenye huo wimbo wa Akon na Michael Jackson;

"This life don't last forever..."


Kumbuka hilo uzingatie sana kazi ufanyayo na siyo mali utakazo.


#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
+255 788 366 511

Jumatano, 13 Septemba 2017

WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE! KUJUA WEWE NI MTU AINA GANI TAZAMA SEHEMU UNAZOENDA MARA KWA MARA


Siku kadhaa zilizopita nikiwa nyumbani mchana nilijisahau nikaacha mlango wazi wakati wa gari la taka kupita. Unajua kilichotokea? Nilipoenda kurudishia mlango na kurejea kuketi ghafla nikasikia mlio wa nzi. Akawa anaruka huku na kule. Arrrghh. Instinct yangu ya kwanza kikawaida huwa ni kuchukua dawa ya kuulia wadudu na kuspray. Lakini this time sasa  nipo nyumbani na hiyo dawa hupaswi kuvuta hewa yake maana ni toxic.

What to do?

Nikakumbuka kuwa mpaka muda huo nzi wa watu alikuwa bado anazunguka yani hajapata sehemu ya kusettle. Kwanza nikasmile maana nina mke msafi sana and she knows huwa namwambia.  So nikajua nzi hajasettle maana kaingia kwenye mazingira yasiyo yake.

What to do?

Nikafungua mlango tu wide enough. Kisha nikatoka mlangoni nikaona nzi anazunguka sebuleni kama mara tatu ruti ndefu hivi kisha huyooo akatokea mlangoni kwa spidi ya rocket!
Problem solved.

NATAKA KUSEMA NINI?

Katika vitu ambavyo hatutofautiani kabisa na nzi ni kwamba hata sisi huwa tunakuwa "comfortable" katika mazingira tuliyozoea/jizoesha. Ni vigumu sana ukawa comfortable mahali penye uchafu kama wewe ni msafi. Au penye usafi kama wewe ni mchafu kweli. Utajibana weeee lakini mwisho vitakushinda utaanza tu kuleta "fujo". Utatafuta tu sehemu ya kutokea.

Sasa sikia sikumfukuza nzi alitoka mwenyewe.

Lakini vipi kama ukikuta mzoga kando ya njia halafu kuna nzi wengi (comfort zone yao) halafu ujaribu kuwafukuza (kuwaswaga)? Utakuwa unafanya kazi bure. Wataruka kidogo na kusambaa kisha watarudi tena. Hawawezi kuondoka kabisa. Labda uondoe mzoga. Hao ndo nzi. Nzi mahali pao pa kujidai siyo kwenye usafi. Yani ukiona nzi katulia mahali ambapo wewe unapaona ni pasafi basi ujue kuna tatizo na pua zako au macho yako au vyote. Nzi anajua pa kwenda.

Ndivyo na sisi tulivyo. Ukitaka kujijua wewe ni mtu wa aina gani check where you normally go. Wapi huwa unakwenda mara kwa mara. There's no way ukaenda mara kwa mara sehemu usiyoipenda. Huwezi kuperuzi sana mtandao usioupenda. Kuna mtandao tu ndo comfort zone yakof


Miezi kama mitano iliyopita kuna siku niliingia kwenye daladala. Ghafla nikaona mdada kafungua simu yake. (Umbea huu nao Mungu atusaidie). Basi nimeona akafungua INSTAGRAM.

Akaingia search. Akatype Jina la mtu.......
Akaanza ku-scroll post za za huyo .

Nikawaza tu katika "umbea" wangu huo, dah huyu ameona of all places za kusoma ni hapo. Akawa anaenjoy na kucheka kweli.  Mara anazoom. Basi katika "umbea" huo huo nikamsemesha kidogo:

*Mimi:* Naona unachekicheki news kidogo..?

*Yeye:* Dah yani kakangu huyu (naniliu) ataua watu mwaka huu. Mi lazima nipitie kwake kila siku.

*Mimi:* Aisee huwa namsikia hivi yuko vizuri ee?

*Yeye:* Dah aisee yani hatari mbaya nakwambia. Yani mimi nisipopita kwake nahisi kama naumwa (huku akismile)

*Mimi:* Aisee si mchezo

*Yeye:* Ndo hivyo tunaondoa tu stress.

Mazungumzo hayakudumu sana maana nilimshukuru kiaina nikatoa kitabu nikaanza kuperuzi kidogo na mimi kuondoa hizo stress kivyangu pia.

Ni muda umepita sasa ila tu baada ya kale katukio ka nzi nikakumbuka hiyo siku pia.

Mimi nakutana na vijana wengi sana kupitia mitandao ya kijamii. Hasa kwa ajili ya mambo ya ujasiriamali na naweza kukuhakikisha kuwa asilimia kubwa sana ya vijana hawako COMFORTABLE na mambo ya maana. Mada inayohusu maendeleo yao inaweza kupita na kupata comments 10 tu katika ukurasa wenye followers MILIONI MOJA. Sasa ngoja ije mada ya jambo la ajabu ajabu utaona "MAONI" yatakavyojaa. Sasa ukiona hivyo usijiulize sana we elewa tu THAT'S WHO THEY ARE.

Ukiona vitu vya maana unaona vinakuboa ujue wala hujakosea. Ni kweli kabisa "VINABOA" kwa watu wasio sahihi. Ukiona vitu vya kijinga "HAVIKUBOI" ujue ni kweli kabisa haviboi kwa watu sahihi kwa vitu vitu hivyo pia.
Nzi ataborekaje na harufu you mzoga?

Ukitaka kujua WHO YOU ARE wala usihangike kufanya research kubwa. Angalia tu vitu vichache:

1. Gallery yako ya simu
Ingia now uangalie.  Ina picha za aina gani.
That's who you are.
Ina videos za aina gani?
That's who you are.
Kuna nyimbo za aina gani?
That's who you are.

2. Google Search list yako nini kinaongoza kutafutwa?
That's who you are.

3. YouTube Videos na channels ulizosubscribe nyingi ni zipi?
Ni za mambo ya ndoto zako na mafunzo ya kimaisha au ni muziki na umbea mwingine?
That's who you are.

4. Vipindi vipi vya Redio na TV huwezi kukosa kabisa?
That's WHO YOU ARE.

5. Nini unapenda kusoma bila kukosa.
Ubuyu wa leo leo au hadithi za Shigongo, au Tips za Dewji au Mafundisho ya Strive Masiyiwa?
Wapi upo napo COMFORTABLE?
Wapi unaweza kuahirisha kula kwanza mpaka ujue hicho kitu kilichoandikwa kimeishia wapi?
That's WHO you are.

5. Ukipewa External Hard Disk utaweka nini? Movies au vitabu? Je ni movie gani?
Aina ya movie na series zinazokuattract that's WHO you are.

Nk nk.. check hivyo vitu tu haraka haraka kwa uchache utajijua upo wapi.

Huwa unaenda wapi sana in the physical world lakini pia social media?

Ni muhimu sana kujua who you are mapema katika safari ya mafanikio yako ili uanze kucontrol vitu vinavyokuvuta mapema. Usije ukajikuta ghafla vitu vilivyokuwa vya msingi kwako ghafla vinakuwa vinakuboa halafu hujui kwa nini. Zamani ulikuwa unapenda watu wenye lugha ya staha na heshima na kuwasikiliza kweli kweli lakini siku hizi uko comfortable zaidi kusoma na kusikiliza wasio na staha na wanaotukanana matusi ya nguoni mitandaoni and wala huoni kama ni shida tena. Coz umeshakuwa nzi pia. Nzi mdogodogo.

Huoni shida kuwa kwenye mizoga wa maandishi. In fact unaitafuta na ukikuta haitoi harufu sana unasikitika. Ukikuta maua yananukia hutaki hauko comfortable.  Ulishawahi kuona nzi anaruka kutoa ua moja kwenda jingine kwenye bustani na akatulia na kuenjoy? Hawezi.
Huenda na wewe hutaki habari zenye harufu nzuri.

That's WHO you are now.
That's who you've become.

Na uzuri ni kuwa unaweza kujua kabisa hiyo  WHO YOU ARE ya sasa kama inakupeleka mahali sahihi au la.

Ukitaka ubadili mwelekeo wa maisha yako uwe wenye tija basi angalia WHERE YOU GO ON A DAILY BASIS.

Kama ningekuuliza swali sasa hivi kwamba: Hivi jana ulishinda wapi siku nzima?

Unaweza kusema labda

"Nilishinda kazini"

"Nilishinda nyumbani"

Nk.

Lakini huenda ulishinda WhatsApp. Au Facebook.

Sasa hilo siyo shida.  Ishu ulikuwa wapi na wapi kwenye huo mtandao wa kijamii.

Shaolin Monks hupewa training sana kuhusu eneo la fikra. Na wewe unaweza kujifunza. Kutunza fikra zako zisishikwe na mambo yasiyokuwa na tija kwenye kutimiza ndoto zako. Hold your mind together. Badilisha sehemu UNAZOENDA na utabadilika sana. Kuna watu huwezi kuwaona mpaka ubadili sehemu unazoenda. Yes. Unataka kuonana na Reginald Mengi Samaki Samaki?
Utangoja milele coz Samaki Samaki huenda that's WHO YOU ARE but it's not WHO HE IS.
Umeelewa?

Kwenye Biblia Zakayo alikuwa si mtu mwema machoni pa watu. Lakini WHERE HE WENT changed everything. Alipanda tu kwenye mti ili amwone "MTUMISHI".  Where he went was WHO HE WAS. Mungu anaona sirini. Zakayo pamoja na mabaya yote lakini alikuwa anatafuta pa kwenda ili atoke shimoni. Ni kama alijua hili nalosema hapa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.

Ukiendelea kwenda sehemu zile zile na kuonana na watu walewale na kutazama na kusikiliza vitu vile vile utaendelea kuelekea huko huko unakoelekea. Utaingia kwenye mtego wa kusubiri watu wengine watatue matatizo yako. Utaendelea kuona kuwa Dewji ana bahati na kusahau kuwa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.

Kama wewe ni kijana na unataka kuyafikia mafanikio lazima kwanza u check na hili la WAPI HUWA UNAPENDA KWENDA SANA.

Nakumbuka kuna siku nilikutana na kaka Samuel Sasali Mlimani City na kibongobongo nikamwambia "Kaka hatuonani?". Akaniambia tu "Huenda NJE ZETU (outings) zinatifautiana tu". And rightly so. Of course Sasali huwa ana majibu at all times and ukimuona unajiandaa tu kucheka. But the point is kama sionani naye kanisani na sifanyi naye kazi na WHERE I GO IS not WHO HE IS tutonanaje sasa?

Ni hivyo hivyo kwenye mitandao. Sehemu unazoenda sana ziangalie vema huenda kuna watu mnapishana. Huenda kuna fursa na ideas unapishana nazo na ndo Mungu anazileta lakini wewe hizo sehemu ambako hizo ideas zinapostiwa is not WHERE YOU GO.

Usitafute mchawi gani kakuroga ukawa nzi. Ni wewe mwenyewe. Anza kwenda kwenye maua huenda ukaweza kutengeneza asali.

Ukiona kwenda Serena kula lunch au hata kunywa juice tu haiikuingii akilini ujue that's who you are.

Mpaka ubadilike itabidi ufanye maamuzi ya Kizakayozakayo.

If you want to change your life start by changing WHERE YOU GO.

COZ WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE!


Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa

#ThreeSixteen
#FourteenSix
#TheAloeLawyer

Jumatatu, 21 Agosti 2017

"MY NAME IS CLARISSA" JE WEWE NI BINTI UNAYEWAZA KUTOA UJAUZITO? (Based on a true story)

JE WEWE NI BINTI UNAYEWAZA KUTOA UJAUZITO?
AU WEWE NI KAKA UNAYESHINIKIZA BINTI ATOE UJAUZITO ULIOMPA?Ilikuwa ni siku nzuri ya Jumamosi na jua la Dar es Salaam halikuwa kali sana kipindi hicho. Plus mawingu kidogo yalifanya hali ya hewa kuwa nzuri zaidi. Nilikuwa nimealikwa katika shule mojawapo binafsi hapa jijini kwa ajili ya kusaidia mambo binafsi kwa mwenye shule hiyo. Ilikuwa ni siku ya MAHAFALI ya darasa la saba katika shuke hiyo ya ENGLISH MEDIUM yenye jina kubwa kiasi na yenye watoto kutoka familia zenye uwezo.

Mandhari ilikuwa nzuri mno na yenye kutia hamasa. Magari mazuri mazuri ya wazazi na walezi yakiwa yamepaki vizuri kwa utaratibu. Kila iliyeshuka kwenye gari alionekana kutoka Dar es Salaam ya kwake tofauti na ile wanayoishi wananchi wengine. Watoto wakiwa wamevaa vizuri mno na majoho yao ya graduation na kila aliyeawona bila kujali kama anawafahamu au la alifurahi.

Hakika shule na wazazi walikuwa wamejipanga. Ratiba zote zilienda sawa na graduation ikaenda vema sana kwa utaratibu mzuri na mambo yote yakiendeshwa kwa lugha ya kiingereza. Kila mwalimu, mzazi au mlezi na hata wanafunzi wa madarasa ya chini walionyesha kufurahia kuwa sehemu ya familia moja. Makofi ya hapa na pale  yaliendelea kwa kila jambo lililotangazwa au kufanyika.

Ikafika wakati wa RISALA ya WAHITIMU. Akapanda binti mmoja mzuri sana na kama kawaida akipendeza sana kutokana na mavazi yake ya graduation. Mrefu kidogo. Mwembamba kidogo. (Picha hii chini siyo ya ninayemzungumzia)


"HONOURABLE DEPUTY MINISTER..... MADAM HEADMISTRESS.....,  DISTINGUISHED GUESTS, LADIES AND GENTLEMEN......" alianza risala yake.

"IT'S SUCH A GREAT HONOUR TO STAND BEFORE YOU THIS MORNING ON BEHALF OF MY COLLEAGUES............."


Kila neno lililotoka katika kinywa cha binti huyo lililuwa kama limechongwa na fundi maalumu kinywani mwake. Sauti yake ilikuwa kama sauti ya malaika. Sehemu kubwa ya RISALA yake ALIISEMA na siyo KUISOMA. Wageni, wazazi, wanafunzi wenzake na hata wafanyakazi mbali mbali katika shughuli hiyo walisimama kwa muda kumsikiliza binti huyo.

Minong'ono midogo midogo kati ya wageni na wazazi kuashiria kushangaa kiwango cha binti huyo haikufichika. Ndani ya muda mfupi umati wa watu ulikuwa kimya kusikiliza kwa makini bila mtu yoyote kuwaambia wasilikize kwa makini. Kila mtu alionekana kutikisa kichwa kukubaliana na mambo yule binti aliyekuwa akiyasema katika RISALA yake. Kwa muda huo wote sauti za ndege na vitu vingine zilionekana kama kufa ilisikika sauti ya yule binti ikipasua anga!

Ungeweza kusema huyu binti atakuwa muhubiri mkubwa baadaye, ama kiongozi mkubwa sana. Usingeweza kumwona kama binti wa kawaida.


"WHEN WE CAME HERE ABOUT SEVEN YEARS AGO WE WERE MERE LITTLE BOYS AND GIRLS WITH A DREAM TO MAKE OUR PARENTS PROUD.
BUT NOW WE'RE NOT MERE LITTLE BOYS AND GIRLS. OR ARE WE?" aliuuliza akiwatazama wahitimu wenzake na wao wakijibu kwa pamoja "NOOOO WE ARE NOT" huku umati ukishangilia kwa nguvu sana.


"THIS SCHOOL HAS MADE US USEFUL HUMAN BEINGS...." akaendelea.... "READY TO MAKE NOT ONLY OUR PARENTS PROUD BUT ALSO THE NATION,  OUR BEAUTIFUL NATION, AND THE WORLD PROUD. WE ARE READY TO UNLEASH OUR FULL POTENTIAL TO THE WORLD....."

Makofi zaidi yakafuatia na wazazi kutazamana yumkini wakijiuliza ni mtoto wa nani kati yao. Binti aliongea mambo muhimu kuhusu wazazi, malezi, walimu, elimu, na maisha utafikiri ni mtu mzima mno tena mwenye uzoefu mkubwa wa miaka mingi. Kila alipoongelea wenzake,  au wazazi au hata walimu aliwakazia macho bila kupepesa macho huku akiongea jambo lililowahusu. Yale macho kama ya yule mwanamama Condoleezza Rice au yale ya Michelle Obama akiwa anasisitiza jambo. Binti alionekana kama mzoefu wa kutoa risala au kuongea mbele ya hadhira kubwa. Ungemwona hakika ungevutiwa naye pia.

Kwa mara ya kwanza toka niwe mkubwa nilitamani kurudi utoto pia kama Lady Jaydee na nikagundua bado sijachelewa, kinadharia.


Risala yake ikaisha wakati watu bado wanatamani aendelee. Hakuna aliyewaambia wazazi wasimame lakini ni kama waliambiwa na mtu ndani yao. Wote na wageni wengine na walimu na wanafunzi walisimama na kumshangilia binti yule. STANDING OVATION. Binti akainama na kushukuru. Tena na tena. Na kisha kupeleka risala yake kwa mgeni rasmi.

Mgeni rasmi alishindwa kujizuia na kumpa zawadi ya fedha nzito nzito.

"What's your name?", aliuliza mgeni rasmi.

"My name is CLARISSA...!" Alijibu binti kwa sauti ile ile ya malaika.

"Congratulations Clarissa!"

Binti akashukuru. Umati ukishangilia. Wazazi wakaanza kushika pochi na waleti. Wakaenda kumtuza alipotoka tu jukwaani. Ilibidi walimu wakasaidie kuweka utaratibu maana alizidiwa na fedha.

Sherehe ikaendelea. Kila mara nikawa nikisikia sauti masikioni mwangu ikirudia maneno "MY NAME IS CLARISSA" Hili jina niliwahi kulisikia zamani nadhani, nikawa nikiwaza.

Sherehe ikaendelea.
Ikafikia wakati wa wahitimu kuzawadiwa na shule kwa sababu mbali mbali. Clarissa naye akaitwa mara kadhaa kupokea zawadi. Kila mara akishangiliwa sana! Ndipo watu wakapata kuwaona wazazi wa yule binti.

Lahaula!

Katika watu wote waliokuwepo kuna kijana mmoja alipigwa na butwaa alipowaona wale wazazi wa huyo binti. Kijana huyo ni:

MIMI!


Boy.
Akili yangu ikahama ghafla kutoka kwenye yale mahafali na kurejea miaka 14 nyuma! Nikiwa sekondari. Nikakumbuka mpaka mahali nilipokuwa nimekaa mchana ule miaka 14 nyuma niliposikia sauti ya mmoja wa rafiki zangu wa shuleni akinisemesha:

"Andrew vipi?"

"Safi tu mambo vipi"? Nilimjibu.

"Ah safi tu hivyo hivyo, una muda kidogo"?

Nikafunika daftari langu kisha nikavuta pumzi na kumuuliza:

"Vipi umeachwa"?

Hakunijibu wala hakucheka kama nilivyotarajia. So nikamwambia twende  maeneo ya viwanjani kama ni kitu cha kuongea kwa utulivu. Akakubali.

Tulipofika akaanza kuniambia kuwa jambo analotaka kuniambia linahusu girlfriend wake. Straight forward akaniambia "Ni mjamzito"

Sitasahau nilivyojisikia.
Lakini nikamwambia rafiki yangu maneno haya. "KAMA UMENIITA UNATAFUTA USHAURI WA KUTOA UJAUZITO HUO NAOMBA TUISHIE HAPA HAPA USINIAMBIE CHOCHOTE ZAIDI MAANA  SITAWEZA KUSHIRIKI JAMBO HILO"

Akaniambia: "Ndo maana nimekufata Andrew maana washkaji wote wanasema tukatoe lakini nilitaka na wewe nione utasemaje... ila nimechanganyikiwa kabisa"

Nikawaza mimi ni nani hadi huyu mtu ametaka opinion yangu. Jibu likaja: mimi ni mtu muhimu kwa mtoto aliyetumboni kwa wakati huo.

So nikamuuliza: "Na yeye binti je anasemaje?"

Akasema yeye ameshashauriwa kutoa ujauzito na wenzake wote na hata ndugu zake wa kike!

Kwa kifupi tu nikakaa na rafiki yangu na kwa neema ya Mungu akakubali kuwa hatashauri abortion ifanyike licha ya pressure ya mazingira na wazazi wa pande zote wakija kufahamu. Hasa upande wa binti.

Tukakaa chini tukaandaa mpango wa kuhakikisha ujauzito hautolewi. Tukaenda kwa binti tukamwambia kuna daktari mmoja mtaalamu wa kutoa ujauzito tutampeleka. Siku ilipofika tukamwambia yule daktari amekamatwa na polisi maana alitoa ujauzito wa binti mmoja mwanafunzi akafariki. (Kumbe wapi.) Hapo tunajaribu kumjengea saikolojia ya aogope kuwa kuna kufa.
Visiku vikapitapita.

Binti anazidi kupewa pressure hasa rafiki zake. Wengine walishafanya abortion mara tano. Wanampa uzoefu kuwa mbona ni rahisi tu. Wakawa wanazidi kumwaga siri zao ambazo hata yeye hakuwahi kuzijua kwa kuwatazama tu. Dunia ina siri nyingi..Akaanza kuwa anatusimulia wanavyomshawishi.

Tukaona isiwe tabu. Tukamfata daktari mmoja tukamwambia kuna binti tutamleta kwako anataka kutoa ujauzito lakini akija tunaomba umpimepime kisha umwambie labda mwili wake sijui umekaa vibaya nk. Vyovyote tu afu umwambie utampa dawa kwenye drip. Daktari nahisi aliona vioja lakini akatukubalia tu tukampeleka binti kisha akapimwapimwa na mwisho akawekeza kadrip kadogo kale kumbe kana maji tu. Dah. Sasa sijui niseme Mungu atusamehe. Maana kwa kweli.
Haya binti akaamini ujauzito utatoka after sometime. Kumbe wapi.
Visiku vikaenda.

Hapo tukaanza kuongelea story za watoto watoto. Tukiona wazazi wana watoto wadogo namwambia yule rafiki yangu achekecheke na wale watoto.
Tunamjengea binti saikolojia ya kupenda watoto.

Bila kutarajia ujauzito aliokuwa anaficha umeanza kuwa obvious hakuna cha kuficha tena. Huku sisi tumeanza kuonekana kumjali mno. Huku tunatania mara majina ya watoto yanayovutia mara majina yanayochekesha. Ikafika hatua pressure za rafiki zake na ndugu zikija akiwaza boyfriend wake na pia mimi tunavyomtreat mwishowe akaamua potelea pote sitoi ujauzito tena.
Haikuwa rahisi.
Lakini ilifikia hivyo.

Lakini kilichonisukuma mimi ni kuogopa kuingilia uumbaji wa Mungu. Na kuwaza tu kuwa huwezi kujua huyo mtoto atakuja kuwa nani baadaye!

Miezi kadhaa baadaye katikati ya changamoto nyingi mno zisizosemeka za masomo ndugu na wazazi mtoto alizaliwa.

Wakamwita jina  lake CLARISSA!

Siku zikaenda maisha yakasonga tukaenda njia tofauti tofauti maishani na cha ajabu tukapotezana kwa kweli. Miaka kadhaa baadaye wakaamua kufunga ndoa na kuishi pamoja nk.

Fast Forward miaka 14 toka hiyo story ndo huyo Clarissa aliyekuwa amesimana jukwaani akiwshangaza walimu na wazazi kwa uwezo mkubwa na kipawa kikubwa cha ajabu. Ni Clarissa huyo huyo aliyenifanya nitamani kurudi utoto angalau kinadharia.

Ni Clarissa huyo huyo ambaye nilikuwa na nafasi ya kushauri asije duniani miaka 14 nyuma lakini kwa neema ya Mungu nikawiwa ndani mwangu kuona akija duniani na kuishi na kutimiza alichoumbiwa!

Ni Clarissa huyo huyo ambaye ndugu jamaa na marafiki za wazazi wake hawakutaka aje duniani kwa visingizio vya ni AIBU, huna hela, wazazi wako, masomo yako, utazeeka haraka, nk.

Yote hayo Clarissa alikuwa akiyasikia akiwa tumboni mwa mama yake.

Clarissa ambaye "walio na akili" waliona hakupaswa kuzaliwa lakini akazaliwa.


Nilipigwa na ganzi.

Wazazi wake wameshakuwa na maisha mazuri mno. Clarissa aliyetarajiwa kuleta shida alileta baraka nyingi.

Niliwafata wazazi wake na kuwasalimia.
Walishangaa kuniona pale. Hawakutarajia. Tulikaa sekunde kadhaa bila kujua tuseme nini. Mama wa Clarissa alinitazama machozi yakimlengalenga kwa kumbukumbu ya yaliyotokea. Nilimpongeza sana yeye na rafiki yangu wa shuleni na pia binti yao Clarissa ambaye hakujua kwa nini kati ya wageni wote wazazi wake walionekana kujawa hisia kali wakiongea na mimi. Nilitambulishwa kwake kama "Uncle Andrew" na kuambiwa nilisoma na baba yake.

Nilimshukuru sana Mungu kwa kunipa neema ya kutunza uhai wa kiumbe chake. Nikawaza what if mi ndo ningekuwa nashauri abortion kwa nguvu afu somehow wakaacha kuifanya na kumpata Clarissa halafu ningewaona pale ningekuwa na aibu na fedheha kiasi gani?

So kama wewe ni binti na unawaza kufanya abortion kwa sababu zozote zile kumbuka uanamke wako siyo kwa sababu una jinsia ya kike. Uanamke wako ni pamoja na kuruhusu nature ikutumie wewe kuleta mtoto kwa njia yoyote na wakati wowote ule atakapohitajika kuja huyo mtoto.

Ulishaona kuku anataka kutaga? Akikuta geti au mlango umefungwa atataga hata kwenye bustani. Sasa watu huwa hawalitupi lile yai kisa limetagwa nje. Hulitunza wakijua lina umuhimu wake. Simple logic right? Yes. Nature ikihitaji kuleta mtoto duniani ikakukuta wewe either kwa kupenda au bahati mbaya umepata mbegu za mwanaume katika siku sahihi za kutunga mimba usitake kutupa hilo yai.  Liweke vizuri tu lina kazi yake.

Kama waliotakiwa kubaki duniani ni watu

1. waliozaliwa kwenye ndoa tu
2. ndoa zilizo halali tu
3. mimba zinazoitwa ZILIZOTARAJIWA tu

Hivi hii dunia unadhani ingekuwa na watu wangapi my friend? Fanya research utashangaa. Saaa unadhani Mungu hajui?

Unajua kuna watu wangapi waliofanya vitu vikubwa duniani na walizaliwa wazazi hawajulikani?

Unajua watoto wangapi wameuwa kwa abortion waliotakiwa kuja duniani kufanya mambo makubwa na kutatua matatizo ya dunia hii?

Fikiria mtu kama Alexander Fleming aliyegundua Penicillin angekuwa aborted dunia ingepoteza watu wangapi kwa kukosa penicillin na ampicilin na amoxilin nk.


Ulishawaza Bill Gates angekuwa aborted dunia ingekuwa wapi leo bila Microsoft? Elewa kuwa Mungu yuko ahead of time alijua watu wake wangehitaji hizo software akaamuru mimba itungwe azaliwe Bill Gates.


Sasa wewe ukiabort unaona nini unachokuwa umeinyima dunia? Kisa eti unaona aibu. Kweli? Au unasikia hasira kwa sababu aliyekupa ujauzito ameukana!.

Uanamke wako haupo kwenye watu kukuona hujazaa nje ya ndoa kumbe umeshafanya abortion za kutosha. You're living a lie.

Uanamke wako upo kwenye kukubaliana na hali uliyonayo na kuruhusu nature ilete kiumbe wa kuja kufanya miujiza mingine huku zaidi ya ile aliyofanya Yesu. Yes, Yesu mwenyewe alisema tutafanya makubwa kuliko aliyofanya.
Sasa tutafanyaje kama tunauawa tungali tumboni.

Kina Les Brown na Myles Munroe waliwahi kusema utajiri mkubwa hauko kwenye migodi ya madini kama almasi nk bali uko MAKABURINI ambako watu wamekufa na vipawa hawajavitumia. Nakubaliana nao. Lakini mimi nataka niiambie dunia leo kuwa utajiri mkubwa zaidi wala makaburini haukufika bali uko kwenye vyumba vya siri na kwenye vyoo na kwenye mikasi ya hospitali na mikono ya madaktari ambako watu wakubwa na wenye uwezo mkubwa hawakupewa nafasi ya kufika duniani kabisa kwa sababu walikuwa aborted!Ole wako ukiunyima ulimwengu utajiri uliowekwa tumboni mwako.

Ole wako ukimshawishi mwingine azuie utajiri mkubwa kuja duniani kwa sababu unaogopa aibu kuwa umempa ujauzito binti wakati wewe ni mume wa mtu au ni mchungaji au ni mbunge. Unataka kulinda hadhi ambayo iliondoka ulipofungua zipu na sasa unainyima dunia utajiri kwa sababu ya kulinda eti "heshima". Mungu anakuona! Na dunia ikikosa majibu ya maswali utakuwa responsible.

Ole wako ndugu yangu. Ni nani atakusadia kujibu kesi dhidi ya dunia nzima?

Fikiria wazazi wa Thomas Edison wangemuabort. Tungekuwa na kiburi cha kubonyeza kitufe ukutani halafu balbu inawaka? Unaona THAMANI ya ujauzito wa Thomas Edison?

Unajua kuwa ujauzito unaotaka utolewe huenda ukawa wa THAMANI kuliko thamani ya balbu?

Lakini vipi kama mwanamke kama Oprah angekuwa aborted?


Vipi kuhusu wazazi wa Aliko Dangote? Wangemuabort.

Vipi kama mama wa Dewji angesema sitaki kuzaa sasa hivi?

Mpendao michezo vipi wazazi wa Pele, au Messi au Cristiano Ronaldo wangefanya abortion.Mpaka sasa kuna kina Messi wangapi dunia hii? Jiulize!

Kuna Gandhi wangapi kama yeye.

Mandela wangapi wameshatokea dunia hii?

Vipi kuhusu  wazazi wa mwalimu Nyerere wangemuabort?


Okay labda huko mbali. Tuwe practical kidogo. Huenda umeipenda makala hii. Vipi kama wazazi wangu wangeniabort basi?

Message kama hii iliyoandikwa hivi ungeiona vipi unadhani?
Ungeona zingine tu lakini siyo hii. Believe me.
You see?
Yet mimi nina mambo makubwa sana kuliko hii message.

Kama unawaza kufanya abortion waza tu kuwa sasa unapanga kuinyima dunia kitu CHEMA. Yani unawaza kuinyima dunia vitabu vyenye mambo makubwa na speeches muhimu, muhubiri na mafunzo adimu mno, discoveries na inventions zaidi ya hata quantum physics, entertainments na atristic works zaidi ya Monalisa na vitu vingine vingi ambavyo dunia haijapata kushuhudia!

Ole wako kuinyima dunia utajiri kwa sababu hutaki kuleta mtu duniani ambaye dunia inamtaka aje. Unatupa yai kisa kuku kalitaga bustanini.

Ole wako daktari unayetumia elimu yako kuinyima dunia utajiri mkubwa uliokusudiwa kuisaidia dunia hii na kuitoa katika changamoto ilizo nazo!


Utajiri unabaki kwenye mikasi, na matundu ya vyoo.

Hayo yote nimeyawaza sana. Kama ninavyomuwaza Clarissa na wazazi wake.


Kama umesoma makala hii ukiwa na dilemma ya kutoa ujauzito wako au mtu wako wa karibu au hata wa mbali basi tambua uko karibu na kuinyima dunia utajiri mkubwa. Na dunia itakapolemewa na shida zake na kumlilia aliyeifanya basi atakumbuka jinsi ulivyozuia utajiri na solutions za matatizo mbali mbali kuja mahali pake.

Usikubali kuhusika kuinyima dunia UTAJIRI iliousubiri kwa muda mrefu.

Vumilia tu kama wazazi wa Clarissa!


Yupo afutaye machozi.

Thawabu yako ni kubwa mno ukivumilia. Wakati mbingu zikitambulisha majina ya watu waliofanya vitu vya maana duniani HAKIKA jina lako halitashauliwa.


Asante na Barikiwa sana!


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com