Ijumaa, 2 Februari 2018

TABIA TATU ZA MTU ALIYE USINGIZINI (AU JAMII ILIYO USINGIZINI AU TAIFA LILILO USINGIZINI)

MINDSET ni kitu muhimu cha kwanza katika kuleta maendeleo kuliko hata NGUVU KAZI.
Twende taratibu tu utanielewa.

Ulishawahi kujiuliza iliwezekanaje UINGEREZA nchi ndogo kabisa tena ya kisiwa iliyo kwenye baridi huko na yenye watu wachache sana iliwezaje kutawala almost dunia nzima ikiwemo Marekani bila kelele na kwa muda mrefu?
(Juzi kwenye ukurasa wangu wa Facebook niliongelea suala la Israel watu wakaanza kuleta sababu za dini. Ooh imebarikiwa. Oh taifa teule. Lakini mimi nilikuwa naongelea MINDSET. Leo nimeanza na Uingereza)

So back to my example. Tafakari pamoja na mimi. Unadhani Uingereza ilitawala nchi zoote hizo sababu ya kuwa na nguvu kazi kubwa au jeshi kubwa au pesa nyingi au nayo taifa teule lenye mki Mtakatifu? Au leo bado ina influence kubwa kiaasi kwamba Queen Elizabeth akisema leo anakuja kutembea Tanzania huenda ikawa sikukuu unadhani hiyo power ni kwa kuwa yeye mzungu au mwanamke au malkia. Kwani kuna malkia wangapi duniani mbona wengi? Ni sababu ya MINDSET yake na yetu ni tofauti. Yeye anatuona watawaliwa sisi tunamuonaje inategemea na tutakavyobehave aisema chochote kuhusu Tanzania au akisema anakuja kutembea. Na sisi kiongozi wetu akisema anaenda kutembea. Mindset.


Tatizo la mindset ni kubwa ndo maana leo mtu akiwaza utajiri wa watu kama Dewji na Manji na Mengi utasikia anasema eti "Mwenzako karithi huyo" au "Kaanza zamani huyo" na kama ni mchungaji utasikia "Sadaka za waumini hizo". Mindset ya aina hiyo haioni anything beyond sababu nyepesi nyepesi.
Ndo maana nilipoongelea Israel watu wakasema "Imebarikiwa hiyo". Hizo ni akili za kivivu na kishirikina. Hazitaki kuwa responsible.

Unadhani Uingereza walimanage kutawala almost dunia nzima sababu ya ngekewa au eti baraka?

Jibu ni walijenga MINDSET YA TOFAUTI. Mindset ya KUTAWALA. Listen to me Mungu alituumbia mindset ya utawala..so usipoitumia utajikuta umejenga default mode ya KUTAWALIWA TU.

Kuna watu wana MINDSET ya kutawaliwa. Hawawezi KUJITAWALA. By default.

Na kabla hatujafika mbali jiulize wewe binafsi mindset yako ni ya KUTAWALA au KUTAWALIWA? Mtu mwenye mindset ya kutawaliwa hupenda aambiwe cha kufanya. Atafutiwe solution. Asaidiwe kupata majibu ya matatizo yake mwenyewe. Hata akiomba nafasi ya AJIRA mahali hafikirii nje ya anachofanya na akikwama anataka akwamuliwe. Mfano akikwama kifedha anaomba mkopo. Si mbaya but mkopo siyo kuwa ndo solution sahihi ya matatizo ya kiuchumi. Mi zamani nilikuwa teja wa mindset hii. Mpaka nilipoamka usingizini. So naongea nachofahamu.

Watu wengi bado wana mindset ya KUTAWALIWA na kwa sababu hao ni wengi kwenye jamii basi jamii hiyo mwisho huwa na mindset ya KUTAWALIWA na kwa sababu jamii za aina hii ni nyingi katika taifa basi mwisho taifa husika huwa na mindset ya kutawaliwa na mataifa ya aina hii yawapo mengi katika bara fulani basi bara zima kwa ujumla wake litakuwa na mindset ya KUTAWALIWA! Mpaka leo vijana wetu wanatamani kwenda Ulaya hata wakafagie tu. Ukimwambia huku atafute kazi hata ya kufagia hataki. Ila mwambie kuna kazi ya kufagia Ulaya utamkuta Libya akiwa anasubiri boti za kwenda Ulaya. Halafu wakiuzwa kama kuku ndo tunaanza kulaumu kwa nini Marekani haiingilii. With due respect Marekani ndo imewapeleka Libya? Naongea vitu vigumu kidogo so usipanic! Kama unataka kupanic subiri kule chini utapanic tu. So tusilaumu wengine kwa matatizo yetu na mindset zetu. Hata kama US ilidestabilize Libya but what if watu hao wangetesewa Morocco? Au vipi kuhusu wadada wa kazi waliosemekana kutesewa Uarabuni. Tatizo ni mondsetnza KUTAWALIWA.

Ni tatizo la MINDSET hili siyo tatizo la imani wala dini. The problem is watu wameweka mbele imani na dini katika vitu vinavyohitaji AKILI. Mchungaji wangu husema kwamba kuwa na imani siyo mbadala wa kutotumia AKILI na husema kama ni hivyo Mungu asingetupatia akili kama imani ndo mbadala. Najaribu kuwasaidia religous fanatics ambao hawawezi kutazama kitu au kukijadili bila kuingiza imani zao.

Umeshawahi kujiuliza kwa nini North Korea imeendelea kupita sisi hadi ina Nuclear Weapons na hawana dini lukuki kama huku. Wamewezaje kujenga mji mzuri namna hii katikati ya aftermath za vita mbaya iliyowaacha bila chakula na katika kipindi hicho wao wanawekewa vikwazo na sisi tunapewa misaada?
China mpaka dini zinapigwa marufuku kwa kuwa sisi tulionazo dini tumeonekana kusubsitute dini for brain. Nchi kama China zinahofia mambo mengi lakini hilo likiwa mojawapo pia. Dini walizoleta wakoloni walizidilute ili kututawala. Zina mapungufu mpaka tutakapoanza kustudy ndo tutagundua. Nchi za Asia zimetupita katika kudevelop mindset ya KUJITAWALA.

Ndo nakukumbusha ya North Korea kupiga hatua kuliko sisi. Shida hapo ni dini pia? Au nao ni taifa teule? Hawatumii Android wala sijui Microsoft wamedevelop softwares za kwao wenyewe na systems za computers za kwao na maisha yanasonga na ndo wanaongoza kwa ku-hack mitandao duniani. Japo si jambo zuri. Ila nalitumia kama mfano maana wanahack kwa maslahi ya taifa lao. Hata Marekani wanafanya hivyo. Kama utakumbuka mwaka 2014 North Korea ilishutumiwa kuhack mtandao wa Sony na kurelease Movies ikiwemo ya THE INTERVIEW ambayo ilikuwa ikiandaliwa bado iliyokuwa na maudhui yaliyosemekana "kuidhalilisha" North Korea.

Point yangu hapa ni kuwa uwezo wa North Korea katika mambo ya computers ni mkubwa mno kiasi kwamba hata Marekani INAUHOFIA. Soma makala hii fupi ya The New York Times uone mambo ya hawa watu.. https://mobile.nytimes.com/2017/10/15/world/asia/north-korea-hacking-cyber-sony.html?referer=https://www.google.com/

Inawezekanaje North Korea kufikia level za kubishana na Marekani hadharani wakati sisi tunaitwa "sh*thole" countries na tunajichekeshachekesha tu na wengine kufikia hatua ya KUKUBALI hadharani kuwa sisi kweli ni sh*ithole countries. Unaona tatizo la MINDSET ya kutawaliwa?

Mwaka 2017 nilienda kutembea kikijini kwetu Ukerewe na kujifunza upya maisha ya watawala wa zamani. (Babu yangu alikuwa karani wa chief wa Ukerewe na hata nyumbani ni kwenye eneo alilopewa na chief jirani na makazi ya chief). Mojawapo ya vitu nilivyojifunza ni kuwa Chief alikuwa na uwezo wa kukukanya (reprimand) muda wowote tena hadharani au kuchukua mkeo hadharani au kukuadhibu na ULITAKIWA umwambie ASANTE  ili kuonyesha utii. Na wengi walizoea hivyo siyo kwa woga no ilifikia hatua ikawa ndo MINDSET ya kila mtu kusema asante kwa chochote atakachofanya OMUKAMA.

Leo ni miaka mingi imepita machief hawapo lakini "WAPO" bado vichwani mpaka mwa wajukuu ndo maana hata leo ukitembelea nyumbani kwa chief yoyote wa zamani awe Marealle au Mkwawa utapaswa kuingia na kutoka kwa respect. Why? Mindset. Wakoloni walikuja na kuondoka lakini WAPO bado vichwani mwetu. Na wanalijua hilo. In fact walilijua kabla hata hawajaondoka. Wakagundua kumbe kubaki huku hakuna tija bora wabaki vichwani mwetu hata wasipokuwepo tutaendelea kuishi kama vile wapo. Ulishaona ile picha ya farasi amefungwa kwenye kiti?
Wengi mlishaiona. Unakuta mtu anasema tusiguse maslahi ya WAZUNGU kwamba WATATUSHTAKI.

Seriously?

Hii ndo akili ya farasi kwenye kiti. Au ndo ile kuwa jambazi akija kwako akisema lala chini mnaweza kulala hapo mpaka saa nne asubuhi kwa hofu tu kumbe jambazi huenda muda huo keshafika mkoa mwingine. Woga.

Lakini ndivyo watu wengi walivyo. Ndivyo jamii zetu nyingi zilivyo. Ndivyo mataifa yetu mengi ya Afrika yalivyo. Afrika Kusini "wakadanganyishiwa" kupewa Mandela kuwaongoza wazungu wakijua huyu atatawala muda mchache tu lakini hawa watu wana mindset ya kutawaliwa tu. Nenda SA leo uone nani anamiliki uchumi huko mpaka leo? Watu wengi weusi wa Afrika Kusini hawataki kufanya kazi. Wanataka starehe. Unadhani ni bahati mbaya kuwa na maambukuzi ya HIV kuliko nchi zingine?
Wakiona hii watapanic pia.

Tatizo nini? Jibu ni:  USINGIZI.

Na sasa twende kwenye kichwa cha article yangu ya leo.

Kuna TABIA (CHARACTERISTICS) 3 za mtu au jamii au taifa lililoko usingizini.

1. MTU ALIYE USINGIZINI HUWA HAJUI KUWA AMELALA MPAKA AKISHAAMKA

Hii ni tabia ya kwanza.
Hujawahi kuona mtu amelala sebuleni kisha akiamka ndo anashangaa kumbe alikuwa keshalala kwenye kochi. Kisha kuamka ndo anainuka na kwenda kitandani.

Ndivyo watu wengi walivyo. Wako usingizini. Ndivyo jamii nyingi zilivyo. Ziko usingizini na wala hazitambui hilo. Ndivyo mataifa ya Afrika yalivyo yapo usingizini na hayajui.

Mtu aliyeko usingizini na halafu hajui kuwa yupo usingizini unafanyaje ili kumsaidia. Wazungu wanachokifanya wanatumia ile methali yetu ya USIMWAMSHE ALIYELALA ila wao wanaimodify kidogo wanaongeza MUWASHIE NA FENI NA UMFUNIKE NA SHUKA HAPO HAPO SEBULENI.

Ndo wanachofanya. Wanajua nchi zetu zimelala wanachofanya kwanza wanatuwashia feni ili mwili uhisi kaubaridi (mfano wanaiba rasilimali nk) kisha wanatuongezea kashuka (misaada).
Hapo mataifa yetu yananogewa na usingizi.
I pity my continent!

Kuna mahali nilisoma kuwa ukitaka kumtawala mtu mtengenezee problem ambayo hakuwa nayo kabla kisha uje na solution kabla yake. That's what is happening.

Mtu aliyelala huwa hajui kuwa amelala hadi akishaamka. Huyu anahitaji KUAMSHWA ndipo afundishwe njia ya kuendea. Ukimfundisha mtu aliye usingizini utapoteza muda bure. Kuna mawili either tuwasubiri watu wetu hadi watakapoamka wenyewe au tuwaamshe kwa lazima.


2. MTU ALIYE USINGIZINI KUNA VITU VINGI ANAFANYA AMBAVYO ASINGEWEZA KUVIFANYA KAMA ANGEKUWA MACHO.

Ulishaona mtu amelala mpaka mate yanatiririka kwenye kona za midomo. Waliosoma kitabu cha THE BEAUTYFUL ONES ARE NOT YET BORN wanakumbuka yule main character alivyolala kwenye basi kwa style hii.

Ok mtu aliyelala anaweza kukoroma kama mashine ya kusaga lakini akiamka (akiwa macho) mashine inazima. Uliwahi kuota unakimbia au kukimbizwa sijui na nini wengine huota anakimbizwa na nyoka mwingine na mgambo wa manispaa mwingine hata anakimbizwa na vitu vingi labda mchepuko. Anakimbia hadi anaanza kutoka jasho usingizini. Lakini akiamka (akiwa macho) haoni kilichokuwa kinamkimbiza.
Tatizo lilikuwa USINGIZI na wala siyo mgambo wala mchepuko.

Kwa hiyo ukikuta mtu amelala huku anaongea mwenyewe sijui "Hapana... nisamehe.. mgambo jamani..." we utamwelewaje? Si utajua shida siyo kuna mgambo ila ni USINGIZI?

Watu wengi wamelala. Vijana wengi wamelala. Facebook ni sehemu ya biashara leo hii lakini vijana wengi kwao ni kijiwe tu cha kubishania mpira na betting au siasa au dini au kulike picha za makalio au kujadili size ya sehemu za siri za mtu fulani. Hawana tofauti na mtu aliyelala na anatoa mate mdomoni.

Siku wakiamka usingizini hakika hutaona wakibishana tena kama leo.

Kuna watu wamebishana kuhusu Lowassa toka 2015 hadi itafika 2020 bado wanabishana.

Kuna watu wamejadili Manchester toka mwaka 2000 na wachezaji huenda waliokuwepo washatoka wote labda huyu bado anajadili Manchester.

Amejadili Zitto Kabwe toka yuko Chadema hadi leo ana chama chake bado anamjadili kwa kisingizio cha kutoa maoni. Mwenzio ni mwanasiasa na maisha yake mengine yanaendelea.


Tatizo nini hapo?

Jibu ni USINGIZI. Na wanasiasa wanajua. Wakikuona UMELALA sebuleni wanakuwashia feni na kukuletea shuka. Kwa ujinga wako unahisi unasaidiwa kumbe unapotea bila kelele.

Ukiongea leo kuhusu watu walioajiriwa wajifunze kujiajiri hata part time majibu utakayopewa na kejeli nzito nzito ukiwa huna wito na mambo haya ya kuelimisha watu unaacha. Lakini kumbe sisi wengine tumetoka familia za wazazi waliotegemea ajira hadi kustaafu na tumeona yaliyojiri LIVE. Tunajua machungu ya kusubiri pension ya mzazi ndo ilipe ada yako. Ndo maana tunajaribu kuamsha wengine yasiwakute.

Juzi nimekutana na mama mmoja mstaafu anajiuliza afanyeje kujikwamua kifedha maana hali yake inazidi kuwa mbaya watoto wake wako chuo wawili mmoja undergraduate mwingine Masters na yeye ndo amewalipia ada kwa kukusanya pension na kukopakopa huku na kule maana hawakupata mkopo wa serikali. Fikiria maisha ya mzazi kama huyu halafu mtoto wake ukimshauri kuwa huko chuo ajitafutie kipato asimtegemee mzazi wake mzee mstaafu huyo mwanafunzi hatakuelewa kabisa! Why?

Yuko USINGIZINI tena kawashiwa feni na kufunikwa kashuka kazuri.

It's sad kuona vijana wetu wengi wanatumia muda kubishania CHAMPIONS LEAGUE au NDONDO CUP au makalio ya WEMA SEPETU. Na wanamuziki wanatumia advantage ya watu kulala wanakufunika na shuka wanakuimbia ANGALIA SHEPUUUUU na wewe unaitikia "AEEE..."
Yaani unakuta kwenye daladala sauti juu na wanafunzi wanaenda shule na ndo wimbo huo. Hivi hawa kama ndo fikra hizo wanazoimbiwa na kuimba watawaza nini kwenye kipindi cha hesabu sijui unafundisha LOGARITHM. Lakini ukijaribu kuwaambia hizo nyimbo wakae nazo mbali weeee! Utaulizwa wewe BASATA?

Tatizo la usingizi hilo.

Lakini hatuachi kusema kwa kuwa tunajua hawa wamelala sebuleni na wamefunikwa shuka. Sasa wewe unataka kumzimia feni unatarajia areact vipi?

Na hizo reaction mbaya zinatokana na hili la tatu hapa chini:


3. MTU ALIYELALA HUWA HAPENDI KUAMSHWA

Hii ndo tabia ya tatu na ya mwisho (for purposes of this post) ya mtu aliyelala. Wengi tunakumbuka utotoni ilikuwaje tukiamshwa kwenda shule. Weee!! Nani aamke? Hadi uimbiwe nyimbo..maana kuna watoto wanaamshwa kwa raha sana utasikia "Junior please wake up my sweet boy". Lakini kwa kina sisi kama ulikuwa na mama kama wa kwangu mwenzangu kibao kimoja kitafanya siyo tu uamke bali ndani ya dakika10 utakuwa ushamaliza maandalizi yote na uko mlangoni unaelekea shule tena kwa kukimbia.

Umenuna. Kumbe ni kwa faida yako. Lakini kuamka ulikuwa hupendi.

Wengi tunajua kuwa tabia mojawapo ya watu wanaotaka kufanikiwa ni kuamka mapema. Jiulize wewe unapenda kuamka saa 10 alfajiri kila siku?
Jibu ni HAPANA.

Ndivyo watu wengi walivyo. Ndivyo jamii nyingi zilivyo. Ndivyo na mataifa mengi Afrika yalivyo. Hayataki kuamshwa.

Hujasikia wahubiri wakisema ni siku za mwisho tumrudie Mungu? Nani anataka kusikia hizo habari? Nani anaziamini kwanza? Ndo ilivyo katika kila eneo la maisha yetu kielimu kiuchumi, nk.

Watu wetu hawataki KUAMSHWA. Wanataka mambo yawe hivi hivi. Jana nilienda sehemu inaitwa Kimanzichana Mkuranga  huko kuna mashamba mashamba ndani ndani huko. Wakati narudi nikakutana na mama mmoja pale Mbagala akiwa amebeba "dishi" lina mihogo mibichi na karanga na vipande vya nazi..ni wale wanaotembezaga kama huyu hapa kwenye picha
 


Nikasogea karibu naye kidogo kudadisi kidogo..

Mimi:
Habari yako dada naona umebeba "kifurushi". (Ndo jina hilo hapa mjini)

Yeye:
Haaahaa ndiyo nikupe cha 4G? (4G ndo kipande cha kassava na cha nazi na karanga mbichi kwa pamoja. Hahaaa. Mambo hayo)

Mimi:
Asante bana nimekuona nikataka nikuulize kitu maana nimetoka shambani huko Kimanzichana so nikaona huenda siku za usoni naweza kuwa nakuuzia mihogo kwa bei rahisi.

Yeye:
Aah ya Mkuranga hiyo siyo mizuri. Ya Kibiti ndo mizuri.

Mimi:
(Nikapotezea hilo la sehemu)
Kwa hiyo unauzia hapa Mbagala?

Yeye:
Hapana nasimamaga Ubungo pale mataa mitaa hiyo ndo navuka barabara nikapande gari hivyo.

Mimi:
(Huku nikitoa hela hivi ili kuonyesha simpotezei muda) Sasa hapo Ubungo umekuwepo kwa muda gani?

Yeye:
Muda mrefu sana.

Mimi:
Sasa flyover ikikamilika magari yakawa hayasimami yanapitiliza utafanyaje?

Yeye:
Aah yatasimama tu. Yasiposimama basi mipango ya Mungu kakangu. Nikupe vipande vingapi?

Mimi:
(Huku nikiwaza usafi wa hiyo mihogo yenyewe nk.) Nipe kipande kimoja. Sasa dada akitokea mtu wa kukupa mawazo jinsi ya kuboresha hiyo biashara yako na kujiandaa kwa mabadiliko ya barabara nk utapenda kujifunza?

Yeye:
Aah. Mi nshajizoelea hivi hivi. Yakibadilika tutarudi hata kijijini tukalime tu kakamgu mambo mengine ni mipango ya Mungu sa mi ntawambia wasijenge hizo flaiova?

Mimi:
Asante dadangu nakuelewa... kazi njema dada.

Yeye:
(Akivuka barabara) Haya asante kwa heri pia.

Unaona kazi ya kumwamsha mtu ambaye amenogewa na USINGIZI ilivyo? Na keshaongezewa shuka.

Measures nyingi zinazotolewa na serikali kwa watu wa aina hii ni sawa na kuwawashia feni na kuwafunika shuka ili walale vizuri sebuleni either kwa kuhofia kupoteza muda kuamsha mtu asitetaka kuamka au kwa kutaka wazidi kulala ili kusiwe na maswali mengi kwenda serikalini.

In any case hawa wanahitaji KUAMSHWA KWA LAZIMA.

Ndo maana tumepata president ambaye akitaka kukuamsha haijalishi umelala masaa mangapi ila kama umelala sebuleni atakuamsha tu kwa kuzima feni na kuvuta hilo shuka wakati bado umenuna anakumwagia na maji usingizi ukutoke vizuri na wakati unazidi kuchukia anakwambia: "Hivi ulisali kabla ya kulala kweli? Hebu piga magoti kwanza hapo uniombee na mimi baba yako maana hii kazi ya kukuamsha kila siku inahitaji moyo!"

Hahaaaa.

Ni utani lakini naamini unaweza kuelewa jinsi ilivyo ngumu kuamsha mtu aliyelala. Na jibsi anavyochukia kuamshwa. Nimesema aliyelala huwa HAPENDI KUAMSHWA. Usingizi ni mtamu mno. Trust me. Hasa usingizi wa KIFIKRA na KIMAWAZO.

Lakini taifa haliwezi kupiga hatua kwa kuwa na jamii iliyo usingizini.

Walichokifanya wenzetu ni kuhakikisha watu wanaamshwa..Kila mtu apewe mtu wa kuamsha. Marekani haijafika hapo kwa kuchekacheka no. Kasome historia wakati wanajenga taifa lao uone ilikuwaje. Walilazimisha kila mtu kujitambua.

Sisi huku we don't care. Mtu anakula ndizi ganda anatupa hapo hapo kama nyani. Seriously. Zebra cross inawekwa mtu anavuka pembeni yake sehemu yenye hatari. Nenda Mlimani City mpaka wavuka kwa miguu wamewekewa taa ambazo ni wao wanaweza kuzicontrol yani ukitaka kuvuka una uwezo wa kubonyeza taa zikasimamisha magari na ukishavuka unabonyeza tena upande wa pili unabonyeza kuruhusu magari lakini watu wanakimbia katikati ya magari. Akili gani hii. Buguruni waliwekewa daraja kuvuka kuokoa maisha yao lakini mpaka walipowekewa uzio ndo wakaanza kupanda daraja kuvuka barabara.

Bodaboda hawataki kuheshimu sgera za usalama na mamlaka zinawa"potezea" sasa si ndo kuwawashia feni huku? Na wenyewe wanaona raha.

Dereva anapita kwenye kivuko cha waenda kwa miguu afu hakuna anayejali. Fanya hivyo US uone adhabu yake! Mlioenda US tusaidieni adhabu ya kupita taa nyekundu au zebra crossing bila kusimama tafadhali nadhani unaweza kupewa adhabu ambayo huwezi kuisahau maishani.

Sisi mpaka mtoto wa shule agongwe ndo tuweke tuta. No forward thinking watu wamepewa dhamana serikalini lakini they are not leaders. Wanasubiri shida ndo waamke. Tena wakiamka shukuru Mungu. Dereva akiona tochi ndo anapunguza mwendo. Mkitaka muone kuna tatizo kubwa la mindset nchi hii ondoeni tochi wiki moja muone. Watu hawajabadilika FIKRA. Bado wamelala. Akipigwa tochi analalamika eti tochi zimezidi. Hajui ni kwa faida ya wengi na ya kwake.

Matokeo yametoka ndo tunaangalia shule zilizofanya vibaya.

Why now?
Hamkujua zitafanya vibaya kweli? Au mnatuchora tu? Hii ndo shida ya Afrika.

Watu wamelala. Ukikosea ukawapa ubunge unatarajia utapata mawaziri wa aina gani huko mbeleni?

So tatizo linaanzia kwa kila mmoja wetu. Wewe UMEAMKA? Nesi umeamka au uko usingizini. Daktari. Mwalimu. Mkulima umeamka au unasubiri Mungu alete mvua kila mwaka huku miti unachoma mkaa na mingine hupandi. Kwani Mungu ni mganga wa kienyeji? Mungu anatumia systems alizoweka. Ukizi disturb inakula kwako tu.

Askari umeamka ndugu yangu au uko usingizini. Kwa nini mtu apite nje ya ATM akute umelala na bunduki umeweka chini tena mchana eti unasema kuna kaupepo? Hahaaa. Unaijua sehemu inayoitwa DMZ -au Dimilitarised Zone huko Korea? Hebu google uone maaskari hao kama wanaweza hata kupiga kope.

Huku kwetu askari anachat muda wa kazi. I mean WHAT A COUNTRY! Msinipige mawe. Nasema tu. Like seriously?

So wewe umeamka msomaji wangu? Binti umeamka au nikuonyeshe wenzako kama Amina Sanga ambaye ni tunu kubwa ya taifa hili na ingekuwa uwezo wangu ningempatia Ubalozi hata akisomea diplomasia akiwa kazini sawa tu.
  

Si kila siku rais analalamikia balozi zetu nyingi?
Kuna watu huko wamelala. Wanadhani ni 1982 saivi wakati tuna watu walio macho huku kwa nini tusiwatumie?

Kijana wa kiume umeamka? Kama hujaamka basi utaisha kukalamika kila siku kila ukiamshwa na kulaumu serikali haijakupa hela na kutamani kwenda kufagia Ulaya. Shame on you.

Mwajiriwa unapiga umbea tu kazini. Akipita bosi wako akakuhamisha kituo au kukupa adhabu unaanza kusema huyu naye anajipendekeza cheo chenyewe haongezwi.
Hutaki kuamshwa.

Israel ni nchi ya watu walioamshana. Wengi wameamka. Siyo sijui dini. North Korea wameamshana. China wameamshana. Siyo dini hapo.

Afrika imelala na kila tukitaka kuamka feni inaongezwa au tunawashiwa na AC kabisa ili kelele za feni zisije kutuamsha. Lol.

Juzi nikasema inawezekanaje Bara zima la Afrika kukubali nchi moja ya China kutujengea ofisi za Makao Makuu ya AU ati msaada?
Are we even serious? Sijawahi kuona usingizi wa namna hii. Tunadumaza our intellect na wenzetu are taking advantage of that.
Tunataka tu UNAFUU. Watu wanaotuwakilisha humu mjengoni tuna uhakika WAKO MACHO?

Dah........ nimejizuia kuandika kitu kwa kweli. Inasikitisha sana.

That is insulting ourselves. Ndo sasa unakuta nchi zetu za Afrika hizi tunapewa msaada wa kuchimbiwa kisima na serikali ya JAPAN au kujengewa choo cha shule fulani na nchi fulani. Hivi wanatufikiriaje sisi. I mean with all due respect. Hivi Tanzania inaweza kukubaliwa hata kusaidia kujenga chochote Marekani hata kama hela zimetoka kwa wadau binafsi? Unaona sisi tunakubali kwa sababu ya mindset ya KUTAWALIWA.

Mtanzania akitaka kujenga choo cha shule kwa kujitolea mahali fulani anaweza hata kukataliwa na hao shule au halmashauri kisa ataonekana anatafuta umaarufu. Lakini balozi wa nchi fulani atakubaliwa na ITV taarifa tunaweza kuona choo kimejengwa kwa msaada wa nchi fulani.

Seriously?

Shida ni tumelala! That's why hatuoni shida kujengewa choo na kuchimbiwa visima na tuna watu wengi na resouces nyingi kuliko huyo anayetuchimbia.

Wake up Africa!

Serikali haitaweza kutatua tatizo la uchumi kwa kuleta tu viwanda. Haya nawapa mawazo adimu. Myasikilize myaelewe. Tunahitaji PRIVATE sector iwe imara mno. Nafurahi napoona Zantel wamechimba visima TBL wamejenga kitu fulani. Mwakasege amejenga kituo cha polisi. Nk.
Huko ndo kujitambua.

Viongozi wa dini na madhehebu wasiishie kuwekea watu mikono na kutamka baraka kwa watu walioko usingizini. Mnasababisha IMANI nzuri ionekane kama mazingaombwe sasa. Kama nimelala halafu wewe umefumbua macho kabisa na  unaniambia NIPOKEE UTAJIRI kwa kuitikia AMEN basi wewe umelala zaidi yangu. Na kama hujalala basi unajua kuwa UNANIPOTOSHA na unafurahi kuniwashia feni na kunifunika shuka. Injili ya kweli ni ile inayohakikisha NIMEACHA dhambi kwanza kabla ya mengine. Kama hujui wala hutaki kujua kama  nimeachana na dhambi kweli ila kila tukikutana tunaimba na kuruka na unaniambia NIMEBARIKIWA huo usingizi wako hata Yeremia nahisi hakuuona enzi zake. Utanipoteza papa. Kwa kweli hapa don't go deeper papa. No. .

Kama unataka ku go deeper katika hili sasa unashangaa nini China na North Korea wakipiga marufuku imani ya aina hii?

We have to change.

Only the TRUTH has the POWER to change our destiny as a nation and as a continent. Tena siyo ukweli wa kuambiwa na mtu wa nje bali wa kuambizana wenyewe.

Lakini leo akionekana kiongozi kati yetu anayejaribu kuamsha watu usingizini hiyo vita atakayopata ataisoma namba. Shida siyo kutawaliwa shida ni akili za yule farasi aliyefungwa kwenye kiti. Hazitaki kujaribu kuondoka kwenye kifungo cha fikra

Uingereza ilitawaliwa na ROMAN EMPIRE mpaka walipoamka usingizini. Lakini walipoamka wanatutawala hadi leo tunaenda kucheza michezo inayoitwa JUMUIYA YA MADOLA. Ya nini? Mashindano ya nchi zilizowahi kutawaliwa na Uingereza. Hatujajitambua. Eti tunaendeleza umoja. Kweli?

Marekani ilitawaliwa na Uingereza mpaka ilipojitambua kama taifa. Vita iliyozuka si ya kitoto. Kujitambua kuna gharama zake yes. But leo USA is a superpower.

Afrika imetawaliwa na kila mtu na HAIJAJITAMBUA mpaka leo. Hatujioni kama WATAWALA sisi. That's why tupo tu hapa. Hatuna UJASIRI wa kuwa pioneers at anything great.

Waarabu walitoka kwao wakaja hadi Afrika...

Wahindi wakatoka wakaja...

Waingereza wakaja...

Wareno na Wajerumani na Wafaransa wakaona isiwe tabu tugawane hili bara tusigombanie fito. Wakaja nao...

Wachina nao sasa wamekuja...

Sisi tupo tu hapa hapa Afrika tunaogopa hata kutoka nje. Bado tunakariri HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA.

Kweli??

Singapore imefika mbali siyo sababu ya eti ni taifa teule. Walijitambua. Walitawaliwa kama sisi. Nilibahatika kusoma kitabu cha Rais wao wa kwanza FROM THIRD WORLD TO FIRST na kuona safari yao ilivyokuwa ngumu.
Leo hii ukiangalia Singapore utashangaa.  Rwanda imejaribu. Inazidi kujaribu. Na hata mindset ya vijana wa Rwanda imebadilika.  Mwezi uliopita nilikutana na kijana mmoja wa Rwanda yuko UDSM anasomea kozi fulani hivi baada ya kuongea naye kidogo akashangaa eti kuwa mimi ni Mtanzania. Namuuliza kwa nini anashangaa anasema anashangaa kwa sababu wanafunzi watanzania walioko naye Hostel vitu wanavyojadiliana ni vya kitoto hadi haamini kama ni wanafunzi wa CHUO KIKUU ambao ndo picha ya taifa baadaye.

Imagine!

Kwa style ya USINGIZI huu Tanzania kama taifa hatuwezi kuwaza hata siku moja kutuma WAHANDISI wetu Haiti au India wakajenge kitu nao. Safari wanazowaza wao ni waende semina wakale per diem na kupiga picha kwenye majengo mazuri yaliyojengwa na WAHANDISI wa nchi zingine! Wamelala hadi waamshwe kwa lazima. Labda kigezo cha kumaliza course ya UHANDISI kiwe kutengeneza mashine fulani au kama ni Ardhi University lazima mtu abuni jengo la Wizara fulani alete mchoro wa MAANA kwa kila mtu!

Lakini nani anataka hizo shida? Ukifanya hivyo yule mama wa haki za binadamu utasikia anasema nyie serikali kama mmeshindwa KUTULETEA maendeleo msiwatese watoto wetu.
Lol. Nimewaza tu.

Maana walio macho kumbe hawako macho kwa faida ya aliyelala ila wako macho ili waendelee kupata chochote au ili isile kwao. Yani mfano unakuta mtu kapewa nafasi serikalini lakini anafanya kazi ili asitumbuliwe siyo ili alete tija mahali alipo.
Wazungu wanaongeza feni tu taratiibu.

Ndo shida ya USINGIZI HIYO. Tutatawaliwa milele.
Coz hatutaki kuamka. Wenzetu wana THINK TANKS kibao kwa kuzingatia talents na abilities za watu. Sisi huku hata ikianzishwa inazingatia KNOW WHO.

Ndo tatizo la usingizi. In summary:

1. Tumelala na hatujui kama tuko usingizini

2. Siku tukiamka kuna vitu tunavyofanya sasa  hatutafanya tena milele

3. Tatizo ni hatuko tayari kuamka.

Siku nyingine ukisikia kama umelala afu kuna mtu anawasha feni ogopa sana tena amka.

Lakini ukiamshwa basi na wewe amka.


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
WhatsApp: +255 788 366 511