Ijumaa, 23 Machi 2018

USIPOFANIKIWA KIUCHUMI KIPINDI KAMA CHA JPM BASI UTAJILAUMU SANA MBELENI!

[....Kwa wanafunzi wa mafanikio tu....]

USIPOFANIKIWA KIUCHUMI KIPINDI KIGUMU KAMA CHA JPM BASI UTAJILAUMU MBELENI!

Wiki takribani tatu ziliopita niko zangu mitaa ya Mlimani City mle ndani maeneo ya duka la vitabu pale nikakutana na rafiki yangu mjasiriamali anayejua maana ya kushikilia ndoto na maono kaka Prosper Mwakitalima. Kuonana kwetu ilikuwa bahati kwa kila mmoja wetu maana tulishapanga kuonana ili kubadilishana mawazo mara kwa mara lakini majukumu yakawa yanatubana lakini nahisi Mungu akaaamua atukutanishe tu kwa lazima, lol.

So salamu za hapa na pale na kutaniana kidogo then tukabadilishana mawazo kidogo na licha ya muda kuwa mfupi lakini conversation yetu ikaanza kuwa deep kidogo kadri tulivyozidi kuzungumza. Prosper ni mtu ambaye ukibarikiwa kuwa naye karibu hakika utagundua kuwa nchi hii imebahatika kuwa na vichwa adimu sana na very soon dunia italitambua jambo hilo.
Huwezi kuelewa ninachosema kama huna kawaida ya kukutana na watu wenye vichwa vilivyotulizana.

Tarehe 28 February niliandika Makala kuhusu umuhimu wa kuwa na AKILI ILIYOTULIA (possessing a quiet mind) kama unataka kufanikiwa. Pro ni mmoja wa watu wenye akili inayoweza kutulia katikati ya kelele. Mafanikio yake kwa kiasi kikubwa mno yanatokana na hilo.

So back to mimi na Prosper katika mambo niliyomuuliza ni anaonaje hali ya uchumi wa nchi kwa sasa. Prosper aliniangalia kwa  jicho kavu sana na bonge la smile na kusema very unapologetically, na namnukuu: “KAKA, USIPOFANIKIWA KIUCHUMI KIPINDI HIKI CHA JPM BASI HUENDA USIFANIKIWE KABISA TENA!”

Wow! What a powerful statement! Ni watu wachache mno nchi hii wanaoweka kuwa na guts tu za kukwambia kauli kama hiyo kipindi hiki.

Well mimi na Pro tulizidi kupeana tips mbali mbali za jinsi ya kufanikiwa fursa mbali mbali za kuwekeza, namna ya kuanza biashara haraka na kwa nini vijana wengi hawapigi hatua hata ndogo tu kuelekea mafanikio kiuchumi. Then tukaagana na kuahidiana kukutana tena kwa ajili ya "kikombe cha kahawa". Kaka Prosper, bado nakumbuka bro. Mbingu zinajua we have to meet again and again.

So kama nilivyosema ni wiki takribani tatu zimepita na nimetafakari sana kauli ile na kufikiria ni vijana wangapi wanaona na kusema kitu cha aina hiyo katikati ya makelele yanayoendelea hivi sasa katika taifa letu kuhusu uchumi kuwa mgumu. Nimefikiria na kuona jinsi gani vijana wengi wasivyoona kabisa kipindi hiki kama kipindi cha kufanikiwa kiuchumi bali wanachoona ni hali ngumu na kudorora kwa uchumi. Well Makala hii haikulazimishi kuona ninachoona mimi ama anachoona Prosper ama mtu mwingine. Ndiyo maana juu kabisa nimesema hii ni Makala kwa “Wanafunzi wa Mafanikio” na siyo kwa ajili ya any Tom, Dick and Harry. So una uhuru wa kuona unachokiona.

Lakini kwa wewe ambaye ni mwanafunzi wa mafanikio basi nakualika upitie machache hapa chini na kuzidi kujifunza mambo yanayoweza kubadili maisha yako hasa katika kipindi hiki kinachoitwa KIGUMU.

Hebu naomba tuanzie hapa.
Hivi unafahamu kitu kinachoitwa RIPOTI YA UTAJIRI DUNIANI ambayo hutolewa kila mwaka? Kama ndiyo mara ya kwanza unasikia kuhusu kitu hiki basi tambua kuwa ulikuwa umechelewa sana kujua jambo muhimu mno la kukusadia kuyaendea mafanikio yako. Mwalimu wangu wa mafanikio (my mentor) aliniambia kama nataka kufanikiwa basi nistop kusikiliza ripoti za vifo vingapi vimetokea, ajali ngapi zimetokea, na mambo mengine ya aina hiyo na badala yake nianze kujaza kichwani mwangu taarifa za mambo ya mafanikio na ripoti zinazozungumzia mambo ya mafanikio zaidi. Na namshukuru sana. Jambo hilo limenibadili share sana!

Sasa hii Ripoti ya Utajiri wa dunia ya kila mwaka hutolewa na Kampuni (firm) muhimu sana duniani iitwayo KNIGHT FRANK. Yafuatayo ni mambo machache kuhusu hali ya uchumi wa dunia kutokana na ripoti za kampuni hii kutoka mwaka 2012 hadi mwaka huu 2018 na projection zake hadi mwaka 2022. Na ninavyoandika Makala hii pembeni yangu kuna hiyo Wealth Report ya mwaka huu 2018 nimetoka kuipitia tena kwa mara nyingine.

Sasa ni hivi…

Kwa mujibu wa Kampuni hiyo ya Knight Frank, mwaka 2017 na 2018 utajiri wa mataifa ya Amerika, Asia na Ulaya Magharibi unashuka katika miaka hii miwili (japokuwa bado wako juu mno zaidi yetu licha ya kushuka kwao lakini wameshuka) na utajiri wa Mashariki ya Kati umebaki jinsi ulivyokuwa bali utajiri wa Urusi na bara la Afrika unakua kutoka 54% hadi 69% kwa nchi ya Russia na kutoka 57% hadi 76% kwa bara letu la Afrika. Sasa nikuulize. Wewe mwaka jana na mwaka huu ulikuwa unaona Afrika kama sehemu ambayo matajiri wanaongezeka?

Habari ndiyo hiyo. Sasa mpaka hapo bado una mawazo ya kukimbia Afrika ukaajiriwe Ulaya??
Think again.

Kwa upande wa Tanzania sasa, Ripoti ya mwaka 2012 ilionyesha kuwa Tanzania ilikuwa na mabilionea 160 tu. Yaani watu wanaoitwa dollar millionaires. Nataka ujifunze kitu muhimu hapa na uone kwa nini narudia sana kukukumbusha umuhimu wa kuwa na akili iliyotulia katikati ya kelele nyingi zinazoendelea. Soma kwa umakini sana nachosema hapa. Nimesema mwaka 2012 kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huo ya Utajiri wa Tanzania kulikuwa na mabilionea 160 tu. Kumbuka kipindi hicho ndo Rais Kikwete ana miaka 7 madarakani na ndicho kipindi wanachosema watu kuwa hali ilikuwa nzuri.

Miaka mitatu baadaye wakati utawala wa Rais Kikwete unaondoka yaani mwaka 2015 mabilionea 30 zaidi walikuwa wameongezeka Tanzania na kufikia idadi ya mabilionea 190.

So wakati JPM anaingia madarakani kulikuwa na mabilionea takribani 190 hivi. Sasa mwaka mmoja tu baadaye yaani 2016 Tanzania ilikuwa na mabilionea 210. Ni kama mabilionea wapya 20 ndani ya mwaka mmoja tu wa utawala wa JPM. Je wewe ulikuwa unahisi unaongezeka kiuchumi au hapana.

Nadhani ukisoma ripoti kama hizi kama akili yako haijatulia unaweza kuona ni propaganda za kisiasa. How come mabilionea waongezeke wengi hivyo katika kipindi ambacho uchumi tunaambiwa unashuka kwa kasi?

Lakini kama umeshtuliwa na idadi hiyo ya mabilionea wapya wa mwaka 2016 basi jiandae kushtuka zaidi. Maana Wealth Report ya mwaka jana 2017 inaonyesha kuwa mwaka jana pekee mabilionea wapya waliozalishwa Tanzania walikuwa 40 ndani ya mwaka mmoja tu wa 2017!!! Yaani ni wengi mno ndani ya mwaka jana tu kuliko miaka miaka minne ya utawala wa Rais Kikwete ambapo wewe unasema ati hali ilikuwa nzuri.

Again how come watu wote hao 40 kuwa mabilionea wapya kwa mwaka ambao tunaambiwa hali ilikuwa mbaya na uchumi unakaribia kufa? Hapo ndo maneno ya rafiki yangu Prosper yanapo-make sense. Na point yangu hapa ni kwamba ukiendelea kulalamika na kulaumu na kusubiri mambo yabadilike utendelea kushangaa ripoti za aina hii kila mwaka.

Projection zinaonyesha kuwa kufikia mwaka 2022 yani miaka minne tu ijayo basi idadi ya mabilionea Tanzania itakuwa watu 460 kutoka 250+ wa sasa. Kwa maana hiyo kuna watu kama 200 siyo mabilionea sasa hivi lakini ndani ya miaka minne ijayo watakuwa mabilionea. Bado unasikiliza story za uchumi unakufa? Ngoja nikupe mfano. Hoteli ya Landmark Ubungo ilibadilisha operation ikawa Hostel na watu wakasema unaona uchumi unakufa? Lakini baadaye kidogo ikarudina kuwa hoteli tena na hakuna aliyesema kuwa swali uchumi unakua. Swali ni je huyu mwenye hoteli ni mjinga?  No. Ni kawaida kubadili biashara. Huku sikia mwenye mabasi ya Sumry  aliuza yote na sasa yuko serious kwenye kilimo? Jifunze kufanya utafiti binafsi. Inakufanya uone vitu visivyoonekana.

Sasa watu 200 kuwa mabilionea wapya ndani ya miaka minne ijayo. Na wewe si angalau uwe milionea wakati huo?

Lakini tatizo unapenda kulisha akili yako habari za umbea na maandamano na kusahau kuwa una nafasi ya kutuliza akili na kusaidia jamii yako kwa kufanikiwa ndani ya miaka tajwa hii na ukaweza kutoa ajira na kusaidia wasiojiweza. Habari unazopenda kufatilia ni nani katoa wimbo gani na kwa nini hajamshirikisha nani. Kweli?
Eti nani kahamia chama fulani na je amehama au amenunuliwa? Again nazungumza na mwanafunzi wa mafanikio. Hayo mambo ya umbea na maisha ya watu hayapaswi kuwa sehemu ya fikra zako na muda wako hata kidogo. Unapaswa kutumia muda wako kusoma vitabu na kupata taarifa sahihi kuhusu mambo ya mafanikio yako. Hizo habari zingine zinachelewesha mno juhudi zako za mafanikio. Najua si rahisi kuziacha lakini jitenge nazo na utaanza kuona utakavyopiga hatua haraka na kuanza kuona fursa  nyingi mno za mafanikio zilizokuzunguka mpaka utajiuliza kama ulikuwa kipofu zamani au?

Nikasoma ripoti moja hivi karibuni iliyosema mauzo ya hisa katika soko la hisa na Dar es Salaam yani Da es Salaam Stock Exchange (DSE) yalipanda kutoka hisa laki 7 hadi hisa milioni 3 ndani ya wiki moja kutokea tarehe 9 Machi hadi tarehe 16 Machi na kusababisha mauzo yatoke Tsh milioni 518 hadi Bilioni 5 ndani ya wiki hii moja. So wakati wewe unasubiri kujua hatma ya maandamano kama yapo au hayapo unahangaika kutafuta nani anasapoti na nani anapinga wenzako wanahangaika kusubiri hisa zao kama zinapanda bei wauze wapige pesa wakawekeze kwenye miradi mbali mbali. Halafu ukisikia mabilionea wanaongezeka unapanic na kubisha.

Jiulize ulikuwa unajua habari hizo za soko la hisa kufanya vizuri hivyo? Kipindi taarifa hizo zinatolewa kipindi hicho hicho kuna taarifa za polisi wamemkamata nani sijui msanii gani analalamika sijui uchawi umetokea wapi watu sijui wakawaje. Sasa wewe nawe unakuta upo na hizo habari. No huwezi fanikiwa.

My friend wewe ni mwanafunzi wa mafanikio. Zingatia kuwa una muda mchache sana wa kuishi hapa duniani na uutumie tu kwa mambo ya msingi yanayohusiana na hatma ya maisha yako. Na kama una mpango wa kufanikiwa basi huna luxury ya kufatilia umbea hata kidogo. Narudia, kama una mpango wa kufanikiwa kiuchumi basi huna luxury ya kufatilia umbea hata kidogo. Don’t fool yourself na kutaka kufurahisha ubongo wakati mafanikio hayawezi kuja bila kuusumbua ubongo. Haiwezekani kichwa cha Bakhresa kinasumbuka kuwaza azalishe nini zaidi na auze nini au abuni biashara gani mpya halafu wewe cha kwako kinawaza nani kakamatwa au nani kaachiwa au nani anataka kuandamana au nani anapinga maandamano halafu unataka na wewe uwe kama Bakhresa. Jambo hilo linawezekanaje?
Hebu kuwa serious.

Gazeti la THE GUARDIAN la Jumapili ya tarehe 11 mwezi huu Machi liliandika tena FRONT PAGE habari za ripoti hii ya Utajiri ya Knight Frank ya mwaka huu 2018 hasa kwa Tanzania. Lakini ni watanzania wangapi wenye kujua kusoma kiingereza wanaopenda kufatilia habari kama hizi. Wewe unayesema hujui kiingereza haya haya hapa nimekuewekea kwa Kiswahili sasa usijesema hukuwa na hizo taarifa.

Kwa mujibu wa gazeti hilo (The Guardian Jumapili 11 Machi) likinukuu ripoti kwa sehemu na pia kutoa observation yake lilisema kuwa Matajiri wakubwa Tanzania hawafiki 20. Yaani watu wenye utajiri wa $50 milioni na zaidi (Bilioni 110 na kuendelea), Hawafiki 20 nchi hii na kwamba idadi yao itaendelea kuwa ndogo hivyo hivo kwa miaka mitano ijayo. Miongoni mwa waliotajwa katika kundi hili ni:

Mohamed Dewji
Said Salim Bakhresa
Rostam Aziz
Reginald Mengi
Ally Awadh (Lake Oil Group)
Shekhar Kanabar (Synarge Group)
Shubash Patel (Motisun Group)
Ghakib Said Mohamed (GSM Group)
Fida Hussein Rashid (Africarriers Group)
Salim Turky (Turky’s Group of Companies)
Yogesh Manek (MAC Group)
Abdulaziz Abood (Abood Group)
Haroon Zakaria (Murzah Oils)

(Watoto wa UFALME mpo?)

Ewe mwanafunzi wa mafanikio kiuchumi ulikuwa unajua majina mangapi katika haya?

Unadhani watu hawa wanapitisha taarifa gani katika vichwa vyao kila siku?
Nataka kukupa challenge kidogo. Unadhani taarifa ulizonazo wewe kichwani ndizo hizo hizo walizo nazo wao pia?
So ukianza kufikira hivi vitu hutapata kamwe muda wa kupoteza kujadili mambo yasiyo na tija katika safari yako ya mafanikio kiuchumi. Nimejaribu kwa siku kadhaa kuandika makala hii toka nionane na kaka Prosper lakini nimekuwa natingwa na shughuli mbali mbali lakini ikabidi sasa nisimamishe shughuli zingine nikuandikie wewe rafiki yangu haya mambo upate mwanga zaidi katika safari yako ya mafanikio kiuchumi. Hivi ninavyoandika hapa ni saa saba za usiku. Nakuandikia hadi usiku hivi kwa kuwa nakupenda na nakutakia mafanikio makubwa kiuchumi kuliko mtu yeyote maana yumkini ukawa wewe ndiyo jibu la ajira ya vijana wengi mno nchi hii. Kwa nini tumsubiri Dangote atoke Nigeria kuja kutupa ajira wakati tunaweza kukuandaa wewe na ukapunguza mno tatizo la ajira nchi hii.

So kama itanilazimu kukuandikia makala saa saba za usiku ili zikusaidie nitafanya hivyo mpaka mwisho wa uhai wangu. Ila sasa usiniangushe! Taarifa hizi uzitumie vizuri.

Turudi kwenye mada. Je ulikuwa unamjua huyo Yogesh Manek?

Slim Turky?

Shekhar Kanabar?

Take it as a challenge. Nakuandikia vitu adimu sana. Tumia vizuri taarifa hizi uone chochote cha kujifunza jifunze andika kwenye notebook yako ili uwe unajikumbusha mara kwa mara.

Kulingana na ripoti nyingine ya Utajiri kutoka kampuni ya Credit Suisse inasema utajiri wa dunia nzima kwa sasa ni thamani ya $280 trilioni. Na 0.7% tu ya watu duniani inacontrol asilimia 46% ya utajiri huu wakati 70% ya watu wanaofanya kazi duniani inacontrol 2.7% tu ya utajiri huo. So unaweza kuona ni wapi unatakiwa kusimama ili uweze kuleta tofauti duniani. Kwenye KUAJIRIWA ama kwenye KUAJIRI wengine.

Hakuna kipindi ambacho fursa za kufanikiwa kiuchumi zimeongezeka na kuwa wazi mno kama kipindi hiki ch JPM. Kwa sababu ya uwajibikaji kubadilika kidogo basi fursa ambazo zamani usingeweza kuzisikia hata kidogo mpaka umjue mtu sasa hivi unaweza kuwa na access nazo kirahisi kabisa na kuzifanyia kazi kama wengine.

Hivi unajua sasa hivi ukiwa na pesa kidogo mno unaweza kuuziwa ardhi kwa bei rahisi kuliko wakati wa JK? Kwa kifupi huu ndo wakati wa kumiliki ardhi kirahisi zaidi na kihalali kuliko kipindi kingine chochote.

Taifa letu kwa sasa ni kama limemka usingizini na ndo maana unaona walioamka nalo wanazidi kuongezeka kiuchumi. Tambua kuwa hakuna mtu atakayeleta pesa nyumbani kwako wewe ukiwa Instagram unalike picha za Wema Sepetu. Lazima kwanza uachane na mambo ya kijinga kisha uamke usingizini tatu uache kusikiliza taarifa mbaya uanze kusikiliza taarifa nzuri.

Unajua kila kitu kikizidi unakuwa addicted nacho. Au hata kama hujawa totally addicted unakuwa kwenye dependence level. Yani huwezi kufunction vizuri bila hicho kitu. Unajua kuna mtu asipovuta sigara akili haichangamki. Dependency level. Na kuna mtu asipopata umbea wa Instagram naye akili haikai sawa wakati kuna mwenzako asipoona post za Strive Masiyiwa yeye ndo akili haikai sawa anaweza kuanza kurudia za nyuma tu kama Masiyiwa hajaandika kitu kipya.

So wewe ungependa uwe addicted na habari mbaya na za umbea na watu wanaodhalilishana au habari nzuri na za mafanikio?
It's your choice!
Lakini kama kweli wewe ni mwanafunzi wa mafanikio basi hapo choice iko very clear.

Kila mwaka kuna ripoti zinazokwambia biashara ngapi zinafungwa watu wangapi hawana ajira wanafunzi wangapi wamekosa mkopo, miradi mingapi inayofungwa nk. Na ingawaje ripoti hizo zinatolewa tambua kuwa kuna ripoti zingine zinatolewa pia kuhusu biashara zinazokuja juu, vijana wanaopiga hatua kimafanikio, matajiri wanaoongezeka, miradi inayofunguliwa na jinsi inavyoweza kushiriki katika miradi hiyo.

Ukichagua kujaza taarifa za kundi la kwanza la ripoti basi very soon utaanza kuamini kuwa mafanikio kiuchumi hayawezekani kipindi hiki. Na utaanza kupenda habari negative negative na ripoti tu za vifo na ajali na magonjwa na matusi ya Instagram.

Lakini ukijaza kichwa chako na taarifa za kundi la pili la taarifa but soon utaanza kujiona kama mtu anayefanikiwa katikati ya watu wanaolalamila usiku na mchana.

Kumbuka wewe ni mwanafunzi wa mafanikio. Hupaswi kamwe kuonekana wala kusikika ukilalamika.  Ondoka kundi hilo la wanaolalamila haraka. Ingia kundi la wanaochukua hatua. Yes. Take Action. Hilo ndiyo kundi la waliobarikiwa siyo suala la dini hapa. Hilo ndo kundi la watu ambao Mungu anasubiri waombe halafu awaonyeshe mwanga zaidi. Hilo ndiyo kundi la wanaoleta mabadiliko ya kweli. Hilo ndiyo kundi la watu ambao wakiamka asubuhi mbingu zinajua na dunia inatambua.

Ningependa wewe uwe miongoni mwa watu hao wanaoleta mabadiliko chanya. Lakini kama hutapenda kuacha taarifa zisizo na tija kwako hakika hutafanikiwa kipindi hiki chenye fursa nyingi mno za wazi kwa wale wenye UTHUBUTU wa kujaribu. Na kama kakangu Prosper alivyosema basi kama hufanikiwi katika kipindi cha namna hii ambacho ukitaka kununua ardhi mwenye nayo anakubembeleza badala ya kuringa kama enzi za JK basi huenda usije kufanikiwa tena.

Na kama itakuwa hivyo hakika utajilaumu sana.

Acha wengine walalamike na kupiga umbea. Wewe choose bo be different.
Miaka minne ijayo waweza kuwa miongoni mwa mabilionea wapya waliosemwa na Knight Frank.

Tukutane katika makala nyingine ya mafanikio Mungu akitupa neema tena.


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp +255 788 366 511