Jumamosi, 25 Juni 2016

KUTIMIZA NDOTO ZAKO INAKUPASA KUONA MBALI ZAIDI YA WANAOKUZUNGUKA

KUTIMIZA NDOTO ZAKO INAKUPASA KUONA MBALI ZAIDI YA WANAOKUZUNGUKA



Naitwa Andrea Muhozya na nina ndoto kubwa za kutimiza maishani. Nimeokoka, nampenda Yesu. Ni Mtanzania kwa kuzaliwa, mwenyeji wa Ukerewe, mkoani Mwanza. Kwa sasa ninaishi Dar es Salaam.  Nina taaluma ya sheria (holder wa LL.B) ambayo niliipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 2008.  Lakini kwa sasa najishughulisha na biashara hususan biashara ya mtandao (Network Marketing) kupitia kampuni ya Forever Living Products yenye makao makuu nchini Marekani lakini ikiwa imesambaa nchi zaidi ya 150 duniani

Kampuni hii pia ipo hapa Tanzania.

Safari yangu ya maisha ambayo ndo kwanza imekucha imeanza mbali kama ilivyo kwa watu wengi wenye ndoto maishani na imejaa kona kona (Waingereza wanaita TWISTS & TURNS).

Nikiwa kama mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya kawaida sana ya watoto watatu tulikuzwa na mzazi mmoja ambaye ni mama (single-parent family) na maisha hayakuwa mepesi sana kutokana na hali halisi ya kuwa mzazi alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kijijini akiwa mwaminifu kazini na hatukuwa na miradi ya biashara ya kusaidia kuongeza kipato hivyo mshahara wake ndiyo ulikuwa kila kitu kwetu na hata kwa ndugu zetu wengine. Sikujua sana mzigo aliokuwa akiubeba mama mpaka aliposhindwa kunilipia ada nikiwa kidato cha pili nikiwa Seminari ya Makoko mjini Musoma, ambapo nilipata ufadhili wa walimu wangu kuanzia hapo na mtu mwingine ambao walinisomesha hadi namaliza kidato cha sita. Mungu awabariki siku zote. Nikiwa Seminari mzazi wangu akitamani nisomee upadre mimi nikawa na ndoto ya kuwa mwanasheria. A twist in the tale.  Kama yule Obi Okonkwo wa kitabu NO LONGER AT EASE cha Chinua Achebe alivyoamua kusoma Lugha wakati ametumwa kusomea sheria. Wakati mwingine inabidi uangalie ndani ya moyo wako Mungu ameweka nini. Usije ukapishana nacho.

Nilipoingia Chuo Kikuu nikaamua kusoma sheria nikiwa na ndoto ya kuja kuingia kwenye siasa za kimataifa kwa ajili ya mambo ya haki za binadamu,  watoto na mazingira lakini baada ya kumaliza chuo nikaona kuwa moyoni mwangu siasa haukuwa mwelekeo wa kutimiza ndoto zangu za maisha na za kusaidia wengine.
Another twist, another turn.

Baada ya Chuo Kikuu kama ilivyo kwa wanafunzi wengi huwaza ajira kama njia ya kutimiza ndoto zao. So nikaingia kwenye mfumo wa ajira kupitia benki ya Stanbic Tanzania. Nilidumu katika ajira hiyo kwa miaka miwili tu kuanzia 18 July 2008 hadi 18 July 2010 nilipositisha ajira yangu (resign) wakati ndo imeanza kunoga ili nikaangalie njia nyingine ya kutimiza ndoto zangu baada ya kuona kuwa mfumo wa ajira usingenifikisha mahali nilipokuwa nataka kufika maishani. Kumbuka ninatoka familia ya mzazi aliyeajiriwa hadi kustaafu na nilikuwa nikiwaza pia nikisubiri hadi kustaafu itakuwaje. Japo ajira yangu ilikuwa nzuri niliamua kufumba macho na kuzitazama ndoto zangu kubwa mbele yangu.
Another twist another turn.

Kwa kuwa sikuwa na UZOEFU wa biashara wa uhakika hapo kabla niliamua kuanza chini kabisa ambapo si wengi walinielewa. Na hapa ndipo ningependa usikilize kitu.  Usifikiri lazima ueleweke na kila mtu ndipo uwe sahihi. Mimi nilijua sitaeleweka but nilijua nilikuwa nafanya nini.  Nilienda kuanza na biashara ndogo ambayo kwa akili ya mtu wa kawaida kuona msomi wa Chuo Kikuu unaacha kazi Benki tena Makao Makuu halafu unaenda kuuza Popcorn (bisi)  stendi ya Mwenge nadhani hata wewe unaweza ukahisi mawazo ya watu yalivyosumbuka kunitafsiri. Kila mtu alisema chake.  Wengine huyu kadata, amerogwa, mpelelezi, hajielewi, nk. Kwa kuwa nilijua nilichokuwa nafanya niliamua kuifanya. Nilijua mpaka SIDO ni wapi,  mahindi yanatoka wapi, mafuta gani yanafaa, nilifika mpaka Century Cinemax Mlimani City kujua wao wanapata wapi mahindi na mashine na mafuta gani na sukari gani wanatumia ndo nikajua kwa nini wanauza bei wanayouza. Tembea ujifunze. So watu hawakunielewa lakini mimi ni mtu nayependa sana kujifunza📄.  Biashara ya Popcorn ilinifanya nijue wale vijana pale Mwenge wanatengeneza mpaka Tsh elfu 70 kwa siku moja. Hebu piga mara siku saba za wiki afu mara wiki nne za mwezi afu unaona mtu mwenye mshahara wa laki nne anavyomdharau muuza bisi bila kujua tofauti kati yao.  Story short, nilijifunza vitu vingi sana na baada ya kuwa nimejifunza vingi nikaamua kuanza biashara nyingine pale pale Mwenge. Nilikuwa nshajua wapi watu wanapita kwa wingi nk. Wapi kodi ni ndogo wapi kodi kubwa pale stendi.  Nani dalali nani dalali wa dalali. Nk.  Nikaingia kufanya biashara ya kuuza vitabu. Nilifanya kwa miaka miwili bila mafanikio hadi nikafunga duka baadaye. Lakini kabla sijafunga duka nilikuwa nimeshaiupgrade na kuanza biashara nyingine ya kampuni ya Ulinzi. Nikawa na ofisi Mbezi Beach mimi na wenzangu wachache. Miaka miwili baadaye biashara hiyo ilikuwa umetupatia wakati mgumu  na mimi personally iliniingiza kwenye madeni mengi hasa na marafiki zangu wa karibu kitu ambacho niliona kinaathiri mahusiano yangu nk. Kumbuka huko kote sikuwa na mtu ananiita kunifundisha cha kufanya ni wachache sana ambao walikuwa na utayari wa kunipa tips za mafanikio.  Kikubwa tu ni kuwa kila biashara ilinipa experience tofauti tofauti lakini matokeo yanayofanana. Kwamba sikuona ikinipeleka kutimiza ndoto zangu.

Wakati nawaza nifanye nini kusonga mbele... Ndoto bado ninazo. Njia mbali mbali bado hazinisogezi walau kupiga hatua... Basi hapo ndipo nikashirikishwa mfumo wa Biashara ya Mtandao na rafiki yangu Edwin Simon Ndege na nikauelewa vizuri na kuamua kuanza kufanya rasmi biashara hii ya Mtandao kupitia kampuni hii ya Forever Living Products Jumamosi ya October 23, 2013, saa moja jioni. Na namshukuru sana Mungu kunikutanisha na Edwin maana alinionyesha wanasema THE THING ITSELF. Yaani alibonyeza reli 😀😀.

Niliona ni biashara ambayo ingenipatia ndoto zangu zote.  Kifupi niliona *vitu 10* ambavyo ningevipata katika biashara hii. Ngoja ni vitaje halafu uone kwa nini sikuiachia hii fursa ukizingatia hisitoria ya biashara nilizotangulia kufanya:

1. Kuja kuwa mmiliki wa biashara KUBWA
2. Kipato cha ziada
3. Uhuru wa kipato
4. Afya bora (kampuni hii inajihusisha na bidhaa za afya na urembo)
5. Uhuru wa muda
6. SAFARI za kimataifa. Napenda kusafiri sana.
7. Kupanuka kifikra maana mafunzo ni mengi kwa waliotangulia.  Nilipenda sana hii.  Maana siku ya Kwanza tu nilijifunza kwa watu zaidi ya sita!  Napenda kujifunza unakumbuka ee?
8. Kusaidia watu wengine.
9. Kustaafu kwa wakati nitakaotaka siyo sababu ya umri. Tamu sana hii
10. Kuacha urithi. Biashara hii inarithishwa kwa vizazi viwili mfululizo baada yangu.

Mimi sijui wengine huona nini wanapoonyeshwa hii fursa! Labda wanaona kitu kimoja. Mimi niliona hayo kumi mbele yangu. Hebu fikiria! Ningewezaje kukataa aina hiyo ya future.

NINI KIMETOKEA TANGU HAPO
Mengi yametokea na sijajutia kuianza hii biashara. Afya yangu imeboreka mara 100. Mfano tu kutokana na bidhaa nzuri za hii kampuni sijaumwa malaria tena toka nimeanza hii biashara. Afya ni muhimu sana. Kuna watu wanapata pesa lakini kila siku hospitali. Hili ni jambo kubwa sana ukizingatia mimi nilikuwa napatikana na malaria kila baada ya miezi minne hivi hapo kabla. What a business. Kumbe nilikuwa na weak immunity.

Pia nimekuwa mtu mwenye mtazamo *mkubwa* mno na ndoto zangu zimepanuka zaidi.  Mfano zamani nilikuwa na ndoto ya kumiliki gari zuri (lolote).  Sasa hivi naona PORSCHE MACAN.  Hiyo ndo tofauti.  Nawaza kumiliki boti, private jet nk.

Treni hapana. Hahahaaaaa

Mafanikio ya kifedha je?
Wengi huniuliza swali hili. Kama nilivyosema kwanza kabisa nimefanikiwa sana kubadili mtazamo wangu kuhusu maisha na kuhusu mafanikio. Unajua watu wengi hudhani kuwa kufanikiwa lazima uwe na uwezo wa kuonyesha pesa nyingi mkononi au benki. Ndiyo maana wengine wanapiga picha na noti za elfu kumi nyingi nyumbani kwao. Hujawahi kuona watu kama hao? Hata wanamuziki wanaofanya hivyo kwenye nyimbo zao.

Lakini sasa hivi mtazamo wangu umebadilika sana! Nimetambua na nazidi kutambua kuwa mafanikio yangu kifedha ni matokeo ya kuwasaidia watu wengine kufanikiwa kwanza.  Yaani Bakhressa anafanikiwa sana sababu ni matokeo ya yeye kuwasaidia watu wengine KWANZA. Mfano anawapa watu chakula, ajira (yaani mshahara), kodi kwa serikali nk, nk. Kwa kuwa anafanya hayo kwanza ndiyo anapata mafanikio kama malipo ya kuwasaidia wengine kufanikiwa.. Huo ndiyo mtazamo wangu mpya. Ndiyo maana niko tayari kusaidia kila mtu katika biashara yangu. Kadri nitakavyosaidia wengi kwa moyo wote bila kuchoka wala kulalamikia wingi wa watu ndivyo nitakavyofanikiwa zaidi kifedha.

Hivyo mafanikio makubwa niliyonayo ni FIKRA ZANGU KWANZA. Sasa hivi mimi ni mtu mwenye kuona mbali na kuwaza makubwa zaidi ya hapo zamani. Biashara hii imenipanua sana fikra kwa sababu ya mafunzo kuwa mengi. Hivyo ninajua mafanikio makubwa ya kifedha yapo njiani.

Hata hivyo siyo kwamba sipati fedha. Ninapata. Kwa kuwa biashara hii haina mshahara kipato changu kinategemea MIMI mwenyewe nimefanya kazi kiasi gani. Kwa mfano je ni kweli nimemtafuta wateja? Je ni kweli nimewashirikisha watu wapya fursa hii ili iwasaidie pia? Kumbuka kama sisaidii wengine siwezi pia kufanikiwa. Kwa hiyo kuna miezi nasaidia watu na kuongea na wateja na ninatengeneza laki 6 hadi laki 8 kwa mwezi kwa cheo changu cha Supervisor. Najua wengi huwa hawastushwi na fedha ndogo kama hizi.Wala hawaoni mbali zaidi (beyond) ya kipato cha aina hii. Hata hivyo hicho kipato ni bonus tu ya kujenga team hakihusiani na bidhaa ninazouza kwa wateja wangu. Nina nyakati nauza bidhaa za thamani hiyo ama zaidi kwa mwezi. Still bado siyo pesa ya kumshtua mtu. Na lengo langu siyo kushtua watu ni kubadili maisha yangu na kuwasaidia wengine kuishi ndoto zao. Ndiyo maana naona beyond kipato hicho. Kwa sababu kuna watu walio mbele yangu wenye vipato mara 40 ya hicho.  Na namshukuru Mungu sana kwa hilo maana ninajua KUMBE INAWEZEKANA.

Lakini lazima nipige kazi. Sasa vipi nikikaa nyumbani bila kushirikisha watu biashara? Anhaaa. Nikifanya hivyo ukweli sitopata pesa kwa kuwa hata Biblia inasema ASIYEFANYA KAZI NA ASILE. Na kama nilivyosema mfumo huu siyo kama ajira. Mfumo huu unahitaji nidhamu kubwa na kujifunza kila siku kwa waliofanikiwa na kujituma kwa dhati bila kusukumwa sukumwa. Kwa kuwa nimeshatambua kuwa napaswa kusaidia watu wengi mno nimeamua kufanya hivyo kwa nguvu zangu zote kusaidia kila aliye tayari kusaidiwa. Nashukuru kuona naweza kushika mkono wengine pia.

Lengo langu ni kwamba ndani ya mwaka mmoja toka sasa niwe nimeongeza kipato changu mara 10 ya hiki ninachopata kwa sasa. Kwa kuwa mindset yangu imepanuka najua nitafikia lengo hilo. Je, kwa mfano mwezi kama huu mwakani nikiwa na kipato mara 10 ya hicho nilichokutajia itakuwa ni kidogo? Na pia ndani ya kipindi hicho nataka kuwasaidia watu watano kupata kipato mara 10 ya wanachopata sasa. Na mwakani ninataka kusafiri miji mikubwa ya nchi saba tofauti kupitia hii kampuni. Miji hiyo ni Dubai, Johannesburg, Barcelona, Monte Carlo, Rome, London na New York. Miji mitatu katika hiyo (Barcelona, Monte Carlo na Rome) nitaizuru kupitia Merikebu ya Kifahari (Cruise Ship). Hebu pata picha!!
Furaha iliyoje! Ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu lakini sasa inaelekea kutimia kupitia mpango wa hii kampuni kuwezesha kila mtu kutimiza ndoto zake. Utapata wapi biashara ya aina hii dunia ya leo? Nitafurahia kipato changu na kuwa na muda wa kuibariki familia yangu kufurahi pamoja katika safari hizo. Vipi kama siku moja ukiweza kusafiri pia katika Cruise Ship? Si watu wengi hupata hiyo fursa duniani, ndiyo maana naichukulia biashara hii kama zawadi kutoka kwa Mungu hasa nikiangalia itakavyowafaa watoto na wajukuu zangu baada yangu.

Nazidi kujifunza kila siku. Sitaacha kujifunza. Najua nitatimiza ndoto zangu zote kupitia kujifunza.


SWALI FUPI: Je, unahisi ni biashara yenye kutimiza ndoto zako pia? Kumbuka kama una ndoto na unataka kuzitimiza kuwa tayari kutoeleweka na wengi na hata kupitia majaribu mbalimbali. Usisubiri kueleweka na kila mtu. Ndiyo ujumbe uliopo katika picha hii ifuatayo..
Huko nje kuna watu wengi wasioijua hii biashara vizuri. Njoo kwetu ujifunze kwa usahihi na kuielewa fursa hii na pamoja tutawasaidia watanzania wengi sana kujikwamua kiuchumi na kuishi maisha ya ndoto zao.
Karibu sana utajifunza mengi mno ambayo wengi hawayajui kuhusu biashara hii. Kujifunza zaidi WhatsApp #o788366511 au #o752366511.

Semper Fi.

AGM
Dar es Salaam, Tanzania
East A