Jumatano, 15 Februari 2017

KIPI HUNA KATI YA HIVI: NDOTO, MALENGO, MIPANGO, NA NIA YA DHATI? AU HUNA VYOTE?

*KIPI HUNA KATI YA HIVI: NDOTO, MALENGO,  MIPANGO, NA NIA YA DHATI?
AU HUNA VYOTE?*

Karibu kupitia haya pia..

Kila siku iitwapo leo nakutana na kuwasiliana na vijana wenzangu kutoka kila pembe ya nchi hii na wananiambia wanataka kufanikiwa. Katika kuzungumza na kila mtu ninazidi kujifunza vitu vingi. Nimeona nikushirikishe wewe pia huenda vikakusaidia.

So, nimejifunza kuwa kuna vijana wa aina 4.

*KUNDI LA KWANZA*

Hawa hawana ndoto (dreams)❌, wala malengo (goals)❌, wala mipango (plans)❌ za kuwafikisha wanakotaka.

Yes. Wapo wengi tu.
Kwa kifupi hawajui kwa nini hawajafa bado. Seriously ukimuuliza kwa nini bado uko hai atakwambia "ni mipango ya Mungu".  Unaweza kusema hawajajitambua bado. Unaweza kusema hawajielewi. Unaweza kusema hawajui hata kwa nini waliumbwa. Hawa ndo hawajui hata tafsiri ya mafanikio. Wengi wao wanaishi kwa kufuata kinachoitwa "societal norms". Mkumbo tu. Hawa ndo wana muda wa kutosha kujadili kuhusu skendo za wasanii, nchi ina njaa au haina, tuhuma za madawa, Makonda anafaa au hafai. Wewe uko Ukerewe huko tena Ukara, Makonda anakuhusu nini truly?😞😞
Kundi hili lina watu wengi wa kada zote waliosoma na wasiosoma wenye ajira na wasio na ajira na waliojiajiri. Ni kundi kubwa na lina kelele nyingi kwenye social medias. Huyu anaweza kuingia Facebook ku-scroll tu. Kisha mlio wa WhatsApp ukilia huyo. Anaingia kuchek kwenye group kuna nini. Kisha Insta kuangalia nani kapost nini!
Hawa wanaongoza kulaumu serikali na wazazi na kulalamika kukosa sapoti au kukosa mitaji pasi na kujua kuwa tatizo kubwa liko kuanzia shingoni kwake kwenda juu!

Kama upo kundi hili ni dhahiri umaskini ni fungu lako. Hawa hata Mungu wanamfanya mganga wa kienyeji. Wanataka waombewe eti wafanikiwe. Kwa dreams zipi sasa? Kwa goals zipi na plans zipi?
SMH

*KUNDI LA PILI*

Wapo ambao wana ndoto tu peke yake (dreams)✔ ila hawana malengo (goals)❌ wala mipango❌

Hawa angalau wanajua kuna kitu wanapaswa wafanye. Shida unakuta hana malengo. Mfano ana ndoto ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa. Ok sawa. Sasa umejiwekea malengo yapi? Hola. NIL. Nada!!
See? Anaongelea ndoto zake kweli kweli. But hajui aanzie wapi. Mwisho anakata tamaa. Anaanza naye kuongelea madawa ya kulevya mpaka akili yake inaanza kulewa nayo. Afu anaishia hapo.
Hawa huwa nawaambia wakae chini watulie wajiulize kama kweli ndoto wanazosema wanazo ni ndoto kweli au just wishful thinking? Maana ukiwa na ndoto kweli hutatulia. Utakuwa kama mjamzito. Hali yako itakuwa inabadilika tu as time goes on. Nikiona una ndoto halafu maisha yako hayana kuhangaika fulani hivi kusaka njia ya kuitimiza najua hiyo ndoto si yako.
Lazima ukae chini kubuni Goals na Plans za kufikia ndoto yako.
Mfano nina ndoto ya kuwa mtu mwenye maarifa ya mambo mengi. Hiyo ni dream. Goal gani nimeweka? Ok mwaka huu nimeweka lengo (goal)  kusoma vitabu 50 kwa mwaka ili kuongeza maarifa. Kitabu kimoja kila juma. Tunavyoongea tuko juma la saba la mwaka na niko kitabu changu cha saba pia.
Kama upo kundi hili tafuta mtu anaitwa JOEL NANAUKA hapa Facebook. Search hilo jina. Ameandika kitabu kizuri kinaitwa TIMIZA MALENGO YAKO. Kitakusaidia.

*KUNDI LA TATU*

Wapo ambao wana ndoto ✔ na wana malengo✔ ila hawana plans (mipango)❌ ya jinsi ya kutimiza malengo yao.

Hawa wanahitaji usaidizi kidogo.
Nimekupa mfano wa dream yangu na goal ya 50 books. Plan yake je? Hapa iko hivi nimeweka PLAN rahisi tu kuniwezesha kutimiza hiyo goal. Mojawapo ni kuwa kila kitabu nachukua idadi ya kurasa nagawanya kwa (siku) saba. Mfano kitabu nilichomaliza juma lililopita kilikuwa na kurasa kama 420. So nilisoma kurasa 60 kwa siku. Everyday. Cha wiki hii kina kurasa 200. Vingine unakuta kurasa 150. Hivyo hivyo. Nadhani umepata picha.

So ninakutana na vijana wengi wana mpaka malengo. But plans hana. Anataka kuingiza sh milioni 50 mwaka huu ili mwakani afanye kitu kinachompeleka kwenye ndoto zake. Goal nzuri kabisa. Lakini hana plan. Hawa ndo unakuta wanacomment AMEN akikuta Facebook mtu amepost picha ya maburungutu ya pesa. Anaishi kwa superstition.

Lazima uweke plan. Na uifate. Je plan yako ni nini unajiajiri? Au unaajiriwa part time?
Plan.
Plan.

Ukiwaza hivi vitu utapata muda wa kufatilia mambo yasiyoisha ya siasa na wasanii kweli? Unaishi na akili imejaa sura ya Gwajima na Makonda siku nzima. Unajitambua?

Sumbua akili yako. Be serious. Mentor wangu aliniambia "Your mind has to be on a leash at all times! Like a dog on a leash. You must control your mind". #IloveMyMentor.

Kataa kupoteza muda.
Bila hivyo utasema dream zako hadi unaingia kaburini. Ishu ni DISCIPLINE. Nidhamu. Bora ukose kula kuliko kukosa kufata plan yako.

*KUNDI LA NNE*

Wapo ambao wana ndoto✔ wana malengo✔ na mipango mingi✔ tu ila kuyafanyia kazi  wanashindwa❌

Yes. Unaweza kugawanya kurasa za kitabu na usisome vile vile.
Hapo ni ishu ya UDHATI. Napoleon Hill anaiita hii DESIRE na kusema ndiyo chanzo cha mafanikio yoyote. Jim Rohn anaiita hii AMBITION. Kutaka kwa dhati. Nenda You Tube andika Jim Rohn: Power of Ambition usikilize. Kipi bora: bando yako iishe kwa kusikiliza Wema Sepetu sijui anaeleza nini kuhusu Masogange au iishe ukisikiliza na kujifunza vitu vya kukusaidia kufanya lililokuleta hapa duniani. Unakuta mtu yuko Chuoni anasoma lakini mind imejaa ramani ya Central Police Dar. Yani wewe uko UDoM central ya Dar inakuhusu nini lakini? Notes hujamaliza kuandika uko WhatsApp!

It's your choice though.

But hii "EAGER DESIRE", hii ambition ndo Dangote alisema kama huna basi hupaswi kuwa hai. Unasikia maneno hayo?

So kundi hili la watu wasiofanyia kazi mipango yao shida ni HAWANA DHAMIRA YA DHATI kutimiza ndoto zao japo kwa nje wanaonekana kama vile wanaenda kwenye ndoto.

Sasa sijui wewe unajiweka kundi lipi. Najua huwezi kujidanganya mwenyewe. Unajijua ulipo.
Asubuhi ya leo nilikuwa na vijana wanne  mmoja kamaliza kidato cha nne watatu wamemaliza chuo wote wana DREAMS. Hawana goals wala plans! Nimewaelekeza na kuwaomba tuonane kesho Asubuhi tena kila mmoja wao akiwa keshaandika hayo. Watu unaowajadili wana maisha yao. Jaribu kujadili ya kwako.

My friend,

Tafuta kuunganika na watu wanaokupeleka kwenye mafanikio yako. Watu wasiopoteza muda na clip za bungeni kila siku. Mi nataka clip za mambo yanayonipeleka kwenye ndoto zangu. Siyo za madawa ya kulevya. And that's me. Wewe kama unataka za Bunge fine. But if unataka kubadilika utimize na kuishi ndoto zako basi karibu tuzungumze zaidi. I hope nitajifunza kwako na pia utajifunza mawili matatu kwangu.

But truly, UTAWAAMBIA NINI WATOTO WAKO KUHUSU KWA NINI HUKUFANIKIWA MAISHANI with all the time you have?

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa

www.andreamuhozya.blogspot.com

+255788366511