Jumatatu, 29 Mei 2017

KIPAWA CHAKO NA JINSI YA KUKITUMIA KUTIMIZA MALENGO YAKO KIUCHUMI

(MAKALA HII ILIANDIKWA MAY 30 2017)

Na Andrea G. Muhozya 

:::::::::::::::::::::::::::::::::::

Habari ya leo kijana wa kitanzania. Mungu  ni mwema tuko hai hadi leo.
Naomba muda wako kidogo tuendelee kujifunza zaidi pamoja leo.

::::::::::::::::::::::::::::::::::::

Yes...

Mungu aliweka kipawa ndani ya kila mmoja wetu. Ili usife njaa wala usife maskini.

Hata hivyo tunapozungumzia KIPAWA yaani TALENT watu wanachanganya sana mambo, wanaita tu KIPAJI.

Ndo utasikia kuna eti "SHULE ZA VIPAJI MAALUMU" wakati pale wanachomaanisha ni shule za watu waliopata maksi nyingi labda. Wameleta tafsiri mbovu ya hata hivyo "vipaji".

Tafsiri sahihi ya TALENT  ni kitu kinachoitwa KARAMA. Yaani simply ni kitu cha ziada ambacho mtu anacho cha kipekee ambacho mara nyingi wengine hawana. Uwezo fulani alionao mtu wa kufanya jambo muhimu ambao watu wengine hawana. Kila binadamu ana cha kwake.

Hapa tunaweza kupata aina mbali mbali za VIPAWA au UWEZO WA KIPEKEE huo:

Mfano:

1. Kipawa cha Kuongea vizuri
(Orators wazuri wako hapa kama kina Mwalimu Nyerere. Yani akiongea mnapenda hadi uongeaji wake tu yani. Comedians wazuri na watangazaji kama kina Charles Hilary wako hapa. Yani anavyoongea tu unatamani kipindi chake kisiishe)

2. Kipawa cha Kuandika vizuri
(Ukisoma novel kama Windmills of the Gods ya SIDNEY SHELDON utaelewa maana ya kipawa cha kuandika.
Ana kitu cha kipekee akipewa "pen and paper". Mhe. January Makamba ni mmoja wapo watu miongoni mwetu ambao wana karama hii. Yani akiandika article inakuwa tu ya kipekee from title to conclusion. Huenda ndo maana alikuwa muandaaji wa speeches za Rais Kikwete. Karama. Kipawa. Kipaji)

3. Kipawa cha Uongozi
Unajua watu kama Gandhi?
Yes. Yani anaweza kufanya wananchi wakubali kulala kwenye reli ili kuzuia treni la mkoloni lisipite na wakalala. Anaweza kufanya shule nzima mkagomea chakula. Anaweza pia kufanya msitishe mgomo.  Wafanyabiashara wakubwa wana hii karama.
Hata Yesu alipokuwa duniani alikuwa na hii karama. Yani anaweza kukukuta uko kazini kwako akakwambia tu "FOLLOW ME" na ukaacha kila kitu. Ukamfata.
Hawa ni watu hata kama hatoki familia inayojulikana lakini anakuja kufanya nchi nzima imfate kwa mazuri au yasiyo mazuri.  Napoleon Bonapatre. Unamkumbuka? Margareth Thatcher alikuwa na karama ya uongozi plus ungangari. Na wengine.
Unashangaa hizi nguvu anapata wapi? Nguvu imejificha kwenye karama tu.
Kuna viongozi wa vyama vya siasa hana elimu ndefu kama wengine wala hahangaiki nayo lakini ukimstudy anaweza kufanya watu lukuki wafanye anachotaka.  We unasema ati ana kismati.  What's kismati. Kipawa hicho.. Talent.

4. Kipawa cha Uimbaji.
Wimbo ule ule lakini akiuimba yeye watu wanaweza kushangilia mwanzo hadi mwisho na wakampa na standing ovation wakati wengine hawakupewa yote hayo. Mtu ana sauti nzuri utadhani koo lake lilitengenezwa baada ya mwili wake kuumbwa yani likaumbwa kivyake. Kuna watu kanisani wakiimba huwa najikuta natamani wimbo usifike mwisho. Huwa wananifanya nitamani zaidi mbinguni sema tu sijamaliza kazi kubwa Mungu aliyonipa hapa duniani. Ndo kwanza ninaanza. Lakini mtu anaimba mpaka unahisi ukiitikia utamharibia wimbo vile. Hivyo yani..

Sasa watu wengi wanajua hiki tu ndo kipaji. Au kipaji cha michezo. Basi.

5. Kipawa cha Uchezaji:
Hapa napo ndo wengi wanaishia like I just said.
Lakini kuna vipawa vingi zaidi ya michezo na kuimba kama tulivyoona hapo juu na tutakavyoona hapa chini.

Na hata hapa kwenye michezo kuna kipawa cha kila aina ya mchezo.
(Mfano kuna kipawa kwenye soccer, kwenye football, basketball, racing (ya magari au ya farasi, mitumbwi, pikipiki, baiskeli, nk), riadha, boxing, kung-fu, weight lifting, mieleka, kuogelea, cricket, tennis, kuteleza kwenye barafu au kwenye maji yaani skiing, chess, hockey, golf, gymnastics, na mingine mingi. Kuna tofauti ya Messi na Phelps)
See? Sasa huku kwetu watu wengi wanajua Mbwana Samatta na Hashimu Thabeet basi.

6. Kipawa cha uigizaji
Umesema nani Kanumba? Hujakosea.  Alikuwa na something EXTRA.  Hiyo extra hiyo. Ndo kipawa.
Kuna yule mama mnaijeria yule. MAMA G.

Akiigiza kama Mama Mkwe utamkubali yani utasikia kila anayetazama ile filamu anasema "Huyu mama ana roho mbaya huyu".
Anaigiza hadi unahisi ndivyo alivyo. Hiyo ndo maana ya KITU CHA ZIADA. Kipawa. Mtu hadi anafanana na anachoigiza.

7. Kipawa cha Uchoraji.
Kina Ibra Washokera. Kina Masoud "Kipanya" na wengine. Yani akichora hata kama ni kikatuni tu kikawa hakina maneno utaona tofauti tu. Unakumbuka katuni ya Kingo. Lol. James Gayo huyo. Hazina maneno lakini ujumbe unafika.Kipawa.

Yani nimeona Kingo toka niko mtoto. Ilikuwa inafikirisha sana afu ukiielewa unaona jinsi mchoraji alivyo na kitu cha ziada.

8. Kipawa cha Kufikiri (thinking).
Tofautisha kufikiri na kuwaza. Sizungumzii kuwaza maana kuwaza kila mtu anawaza ila ni wachache wanafikiri. Kuwaza unaweza kuwa huna hela ukajaa mawazo. Mi nazungumzia KUFIKIRI (THINKING).
Kuna watu wana karama hii. Ukimpa afikirie kitu analeta jibu lenye something EXTRA.
Ulishasikia kitu kinaitwa THINK TANK? Mara nyingi kwenye think tanks kuna watu wenye kitu cha ziada kwenye kufikiria.  Yani ukimpa issue ya mchanga wa dhahabu anaweza kukupa solution ndogo tu na ikawa ndo the most effective. Ana karama mwenzako.

9. Kipawa cha Ubunifu (creativity).
Hata wachoraji, watunzi wa vitu nk hii pia wanayo.
But hapa naongelea wabunifu.  Ndo unaona wanabuni magari,
wabunifu wa mitindo ya mavazi, wa matreni, midege ya ajabu, simu hizi na computers nk. Mifumo mbali mbali kama android, MPESA, max malipo, Uber etc. Creativity tu hapo. Sasa mwingine anaweza kukaa miaka nane hajaweza kubuni kitu cha maana. Mwingine mpe nusu saa tu. Inatosha.

10. Kipawa cha Kumbukumbu
(hapa ndo wanafunzi wanofaulu vizuri wapo. Anaweza akasikiliza kidogo tu darasani lakini akakumbuka every detail hata ambavyo mlikuwa mnahisi hakuvisikiliza kwa makini. Na nyie mpaka mmemrekodi mwalimu na notes mmeandika na maswali mmeuliza lakini "pepa" ikija anafaulu yeye zaidi yenu. Ana something EXTRA linapokuja suala la kumbukumbu.
Nk..
Wewe utaomba Roho wa Mungu akukumbushe vitu kwenye mtihani mwenzako hata hajui kuomba labda. Lakini anapata "A" wewe unaondoka na karai.
Kumbuka kipawa alipewa na Mungu. Na wewe una cha kwako labda michezo.  Ndo hivyo.

SASA TUENDELEE..
Nadhani hadi hapo unaweza kuona Michael Jordan alikuwa wapi, na Diamond Platnumz  yuko wapi, Ronaldo na Messi na kina Mbwana Samatta wako wapi, Roger Federer yuko wapi, Tiger Woods yuko wapi, na Les Brown yuko wapi Dan Brown yuko wapi, Jack Chan alikuwa wapi, Kanumba alikuwa wapi, Michael Phelps yuko wapi, Alexander Bell, Mohammad Ali na kina Tyson walikuwa wapi katika hizo hapo juu. Nk.

Yaani Tyson hakujaribu kulazimisha kuimba, Ronaldo hajalazimisha kuchora, Diamond hajalazimisha kuogelea. Kuna siku nilisema Dan Brown anajiandikia zake vitabu hajalazimisha kuongea kama Les Brown na Les Brown naye hakujaribu kuandika stori za kuvutia kama za Dan Brown na wote wamekuwa multi-millionaires.


TALENT YAKO NA MAFANIKIO KIUCHUMI

Ni ujinga kumwonea wivu mtu anayefanikiwa kupitia kipawa chake ilhali kila mtu alipewa cha kwake. Muhimu ni wewe kutafuta cha kwako my friend.

Talent ni njia kubwa mno ya kuweza kukupa pesa nyingi na kukufikisha katika utajiri. Leo hii Michael Jackson alishafariki lakini bado analipwa mamilioni, lakini watu lukuki wako hai na hawajui senti tano wataipata wapi...

Lakini angalia watu kama Michael Jordan na kina Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, na wengineo. Angalia waigizaji kama Tyler Perry na kina Samuel Jackson au Angelina Jolie uone wanavyopata pesa nyingi mno kupitia vipawa vyao.

Siwezi kutaja kila mwenye kipawa hapa maana hatutamaliza. Michezo tu pale juu nimetaja mingi mingi na hiyo ni michezo hatujaongelea vipawa vingine  kama vipawa vya thinking and creativity (ubunifu)  ambao hawa ndo wanabuni mitindo ya mavazi, ya magari, ya ndege na computer na simu na drones nk lakini pia ndo wanabuni solution za migogoro mikubwa ya kati ya mataifa. Hawa nao wanatengeneza pesa nyingi mno. Mfano mtu anayebuni gari la Rolls Royce au Bentley au Ferrari nk hao wanatengeneza pesa nyingi na hawachezi mpira wala hawaimbi R n B au pop!

Tatizo la watu wengi hasa huku kwetu ni kuwaza kuwa vipaji ni mpira na nyimbo na bongo movie basi. Yani kama hajui kuimba wala kucheza wala kuigiza basi. Katoto kakiimba kama Ali Kiba eti ndo kana kipaji.  Kali Kakichora chora ukutani kila siku katakemewa eti kanachafua nyumba.

Lakini point ya msingi hapa ni kuwa kipawa kinaweza kumpa mtu utajiri mkubwa. Kuna wanamichezo wanapesa nyingi mno. Kuna watu wa vipaji wengi wana pesa nyingi. Kuna watu wanalipwa mpaka dola laki 7 kuongea mahali. Yaani kwa saa moja. Imagine! Hiyo ni kama Tshs BILIONI MOJA NA MILIONI 400!!! Kwa saa! Sasa si unaona kipawa kinavyoweza kukufikisha mbali? So usingángáne tu na Bachelor of Law kama niliyosoma mimi. Dan Brown kitabu kimoja tu kinaweza kumpa dola milioni 10. Yaani BILIONI 20+! Hivi unaelewa? One BOOK. Sijui INFERNO sijui DIGITAL FORTRESS.

What’s your TALENT? Usidharau nguvu ya kipawa chako. Mungu atakushangaa na ATAKUADHIBU. Trust me. You MUST FIND OUT ni nini Mungu alikupa. Hakuna ambaye aliumbwa bila kupewa kitu EXTRA. Kila mtu anacho. Ndo wenzetu Ulaya wakikijua kwa mtoto wao wala hawahangaiki eti akasome "vidudu" afu aende primary school asome rundo la vitu kisha aende sekondari asome vitu kibao bado high school bado chuoni.  Wakati kumbe yeye mngempeleka kuendeleza kipawa cha kupiga mbizi tu kwenye mabwawa angetangaza nchi na umaskini kwenu ingekuwa bye bye. Lakini mlitaka tu awe daktari. Au mhasibu. Halafu sasa amekuwa what next? Ndo unakuta yeye akiwa kazini anawaza weekend ifike kuna mechi ya bonanza akacheze. Kipawa kilipotezwa.

Usidharau hii. Ukiitumia unaweza kufika bungeni na ikulu mpaka hata UN na wala form four hukumaliza. Wengine wamesoma mpaka maktaba inawajua na ikulu wanapasikia tu.


CONDITIONS ZA KIPAWA CHAKO KUKUFIKISHA KATIKA MAFANIKIO KIUCHUMI

Sasa hapa ndipo shule ilipo. Vipawa pia vina mahitaji yake.

1. Ubora wa team yako.

Moja ni kuwa ili kipawa kikuletee utajiri inahitaji TEAM WORK. Yaani lazima uwe na team ya watu wanaokuhandle wewe na mambo yako yote. Mfano angalia mtu kama Cristiano Ronaldo au Messi. Hafungi magoli bila team work. Yaani anategemea vipaji na creativity ya watu wengine kwenye team ili afike mbali zaidi. Ukimuweka Messi timu kama Mtibwa Sugar (no offense) hatawika kama anavyowika huko aliko maana huko aliko amezungukwa na professionals na watu wenye creativity na vipawa vya aina ya kwake pia.


Lakini pia Ronaldo au Messi ana kocha wa mazoezi binafsi, ana mshauri wa kisaikolojia anamlipa yeye, ana Manager wake binafsi, mwanasheria wake binafsi, ana mtaalamu wa chakula anayemshauri ale nini asile nini (huyu siyo mpishi ni mtaalamu tu yani nutritionist), ana daktari wake binafsi na wa timu pia yupo. Maana ukitegemea daktari wa timu afu akawa kwa mchezaji mwingine itakuawaje? Ana mtu wa mitindo mfano kinyozi na stylist wa mavazi kabisa,  ana mwalimu wa kufundisha mtoto wake nyumbani, ana designer wa nyumba na wafanyakazi wa nyumbani kama wapishi, watu wa usafi, gardeners, nk.

See? Haya yote watu hawajui wanapomshabikia Ronaldo au Messi au Tiger Woods. Au wanapoona analipwa pesa nyingi.

Sasa kama unataka kutumia kipawa kuufikia utajiri inabidi ufundishwe ukweli kama hivi. Usije ukaenda tu Bongo Star Search halafu hujui WHAT IT TAKES kukupelea kwenye mafanikio makubwa kupitia kipawa chako. Inahitaji investement kubwa mno. Na NIDHAMU YA MAZOEZI KUBWA SANA.

Na bahati mbaya sasa investment hii indo inakuwa tena BURDEN kwa mwenye kipawa maana ana watu wengi wa kuwalipa. Inakuwa MZIGO MKUBWA mno. So unashangaa mtu analipwa paundi 365,000 kwa wiki moja tu (yani $468,000/- yaani Tshs BILIONI MOJA) anazipeleka wapi? Unahisi ukizipata wewe utakuwa tajiri. No. Nilishasema hauwi tajiri kwa kupata hela nyingi ila kwa kuwa na MINDSET ya utajiri kwanza. Na kuhakikisha fedha inapita kwenye mfumo wa kuzaa tena.

Unaweza kusema hawa hela zao wanazitumia vibaya..no. Licha ya kununua majumba na magari ya kifahari na kufanya masherehe nk  lakini pia wanalipa watu wengi mno. Kama nilivyoainisha hapo juu. Tena hapo nimeweka vitu general tu. Na bado kodi ni kubwa balaa. 

Kwa hiyo kama una kipawa cha kuongea kama Joel Nanauka (Public Speaking) unataka kuwa kama kina Les Brown ama una kipaji cha kuandika pia kama mimi (Writing) na unataka kuwa kama kina Dan Brown ama kama kina John Maxwell basi unapaswa kujua kuna TEAM inahitajika. Nani atakuwa mentor wako? Nani atakuwa mtunza fedha wako? Nani atakuwa trainer wako. Mentor na trainer ni watu wawili tofauti. Kina Les Brown walijiandikisha katika madarasa ya DALE CARNEGIE ambaye alikuwa mtaalamu wa kufundisha kitu kinachoitwa Public Speaking.

Sikiliza... Dan Brown mpaka amalize kuandika novel moja anaweza kusafiri nchi 10 kukusanya data na kufanya mikutano na watu maarufu duniani na inamgharimu pesa nyingi na muda mwingi kuandaa manuscript hadi iandikwe.

Nani atakuwa MANAGER WAKO? Wa kuorganise wapi ukaongee na ulipwe shilingi ngapi nk. Usije ukawa wewe ndo kila kitu.  Messi hakufanya hivyo. Aliandaliwa.  Nani anakusaidia kujiandaa?

Changamoto kubwa ya watu wenye vipawa huku kwetu na hata duniani ni kuwa wanafanya kila kitu wao wenyewe. Kwa hiyo anakuwa hana tofauti tu na mtu aliyejiajiri. Anakuwa kama jongoo miguu mingi lakini spidi kidogo. Kipaji kikididimia naye anaishia hapo.
Lakini ukimtaka Les Brown aje Tanzania  sasa huongei naye yeye unaongea na watu wake. Yeye sasa ni TAASISI.
Hilo ni jambo la kwanza la kuzingatia. Tengeneza team around your talent. Skilled people. Uwalipe.

2. Vipawa vingi vina muda fulani tu.
Yes.
Changamoto ya pili ni timeframe. Hasa kwa wanamichezo. Kwa mchezo kama Soccer kuna muda wake. Umri ukienda mwili unakataa. Unastaafu bila kupenda. Tofauti na uandishi kwamba umri unavyokwenda ndo unazidi kuwa bora zaidi na zaidi.

Mbwana Samatta ana miaka chini ya 10 hivi ya kuhakikisha ameshatimiza ndoto ya kucheza timu kubwa maana vijana wadogo wenye  vipawa vikubwa ni wengi kwenye ulimwengu wa soka kwa hiyo anatakiwa ajitahidi mno. Kwa sasa ana miaka 24. Miaka mitano ijayo mwaka 2022 atakuwa na miaka 29. Hapo mwili umeanza kuchoka na wenye vipaji wadogo zaidi watakuwa wameshaibuka wengi. Ni vigumu kukuta bado akicheza timu kubwa Ulaya mwaka 2025. See? Huo ndo ukweli. Kina Msuva na Kichuya watakuwa wapi?  Ni lazima wafikirie.
Lakini Masudi Kipanya anaweza kuwa bado anachora kipanya chake mpaka hata 2050.
Ni muhimu kujua kipawa chako timeframe yake imekaaje.

3. Vyanzo vingi vya mapato.

Cha tatu ni kuwa lazima uwekeze maeneo mengine usitegemee kipawa chako tu. Katika wanamichezo wote ni Michael Jordan tu ambaye amefikisha utajiri wa dola BILIONI MOJA. Yani ndo yuko kwenye Forbes List ya binadamu  matajiri duniani. Nazungumzia athletes (wanamichezo kama mpira riadha nk) ni yeye tu bilionea. Yani yuko level kama ya Mo Dewji kwa utajiri. Si mchezo ujue.. lakini hii ni kwa sababu analipwa kwa matangazzo na ana miradi mingine zaidi na zaidi. Kwa hiyo kina Messi siju Ronaldo bado sana kufikia NETWORTH ya dola bilioni moja. Ndo maana unasikia Ronaldo kafungua mradi huu ama ule.

Ndo maana unaona kijana kama Diamond anawekeza kwenye sijui pafyumu, internet, radio stations (added) na mambo mengine. Ukisubiri hela za matamasha tu na mechi nk kuna siku kipawa kitaisha makali yake. Kipawa kina life span yake maana hata wewe mwenyewe una life span yako. Angalia watu hapa kwetu kama Mr. Nice. Walipata pesa nyingi lakini hana washauri hana plans hana team ya professionals wa kumshauri cha kufanya matokeo yake SEASON YAKE ilipopita akapotea. Juma Kaseja na Mrisho Ngassa season imepita. Kina Bombi wachekeshaji season imepita. Emanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) amekwenda kwenye kilimo na biashara ya chakula na security na uchimbaji madini. Anatambua kuwa kuna siku Ze Comedy itakuwa hahiwiki tena. Sijui kama inawika tena kwanza.

Swali la kujiuliza je wewe una kipawa gani? Na umeshaanza kukifanyia kazi? Au bado? Una umri gani? Kipawa chako watu waliofanikiwa nacho walitumia MUDA GANI kufikia utajiri? Usiende tu.


GOOD NEWS IS UNAWEZA KUANZA SIFURI

Uzuri ni kwamba hata kama huna shilingi unaweza kuanza hapo ulipo. Mimi nimeanza kuandika 2013 kupitia hii mitandao ya kijamii. Sikuhitaji pesa. Labda bando tu.

Lakini pia nillianza kuandika kitabu changu cha kwanza 2015 ambacho nilikimaliza mwaka huo huo ila toka hapo nakirekebisha na kukipeleka kwa watu wenye mafanikio na upeo zaidi yani kuongeza ideas na kurekebisha na naamini itakuwa ni moja ya best books duniani.
Kiko kwa lugha ya kiingereza. It's a book for the nations. Nitakipublish miaka ijayo kwa neema ya Mungu kwani ninayafanyia kazi pia yale niliyoyaandika mwenyewe kuthibitisha usahihi wake katika kuleta matokeo.

Lakini pia mwaka jana October 2016 nilianza kozi ya Public Speaking na kuongeza uwezo mzuri zaidi wa kiingereza mpaka sasa naendelea nayo na kila siku nafanya mazoezi ya kiingereza na ya kuzungumza kwa sababu pia nina kipawa cha kuongea.
Kwa hiyo najiandaa tu zaidi. Siku nikifika kwenye World Economic Forum kuongea niweze kufikisha ujumbe kwa usahihi na kuwe na hiyo intelligibility.

Point ni kwamba. Nilianza hapo nilipo. Ni watu wanaoniambia kuwa naweza kuandika "vizuri". Mi napokea na kushukuru na kutendea kazi..
Nikienda mahali kuongea ni watu wanaoniambia kuwa naweza kufanya vizuri pia eneo hilo.
Point ni kuwa nimeanza nilipokuwa. Bila kitu. Na wewe unaweza kwa kipawa chako ulichonacho. Haijalishi nani anavuma sasa usiogope. Mentor wangu alisema one day kuwa ukitazama nje mchana kuna kunguru na ndege wengi tu wote wanaruka kuna mpaka mbu na vipepeo.  Vyote vina ruka na hakuna kinachosema "mbona nakosa nafasi ya kurukia". Smart man. So usiwaze kuhusu hilo.  Unaweza pia.

Lakini lazima uzingatie yale mambo matatu niliyoyasema pale juu: yaani team work na timeframe na kuwekeza kwenye vitu vingine.

Na pia lazima uzingatie kwamba ili uweze kukifanya kipawa chako kuwa biashara itahitaji uwe vitu vitatu: yaani bidhaa au huduma, system na team. Hili ni somo linalojitegemea.

Ukitambua kipawa chako unakuwa umetambua kama 50% ya kitu ambacho Mungu alitaka ufanye huku duniani.  Maana kipawa kitalitumikia KUSUDI. Na ukitambua kipawa chako ukaki develop basi hutakufa njaa wala hutakufa maskini. Mungu ali-make sure hilo amelifanya kabla hujaja duniani. Usimwangushe!

So ukisema SINA MTAJI Mungu anakuangalia tu. You have something in you.

Vipawa viko vingi. Usilazimishe kipawa cha kuimba huku wewe una cha kuigiza. Usilazimishe cha kuchekesha kumbe una cha kufikiri.

Tambua kipawa chako pasi na shaka. Ujue kabisa mimi niliwekewa hiki.


OK BYE..

Niishie hapo kwa sasa na  naamini utapa mwanga zaidi ili kujua uanzie wapi kama unataka kuitumia njia hii kuufikia utajiri. Ni imani yangu kuwa umejifunza kuhusu njia hii na wewe kama wewe unaweza kuona kama inakufaa au la.

Ila utaona tu kuwa siyo shortcut. Usijaribu kuwa tajiri kwa short cut. It takes time!

Asante sana kwa kuwa hapa na karibu kwa maswali maoni michango zaidi nk.

Much Love!


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp #o788366511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
May 30, 2017.

Jumapili, 21 Mei 2017

IN EVERY SITUATION LEARN TO TELL YOURSELF: "OKAY... SO WHAT NEXT?" KATIKA KILA HALI JIFUNZE KUJIAMBIA MANENO HAYA: "NI SAWA... KWA HIYO NINI KINACHOFUATA?"



*******
Asante nyingi kwa Mungu kutupa nafasi hii kujifunza pamoja.
*******


Mara nyingi mno tukikosa vitu tunavyotarajia kupata huwa mioyo yetu inasinyaa.

Hivi ulishawahi kusinyaa moyo? Dah.

Yani mtu unakosa raha. Unajiona hufai na kuona bora wenzako wana bahati. Hii haijalishi kama mtu amekataliwa na boyfriend au girlfriend. Au mwingine hata amekataliwa tu friend request Facebook.  Hahaaaa. Au wamemBLOCK.

Yaani mtu akikublock halafu ukajua kuwa ame-kublock halafu ulikuwa unaona ni mtu muhimu kwako unajisikiaje? Rejected right? Halafu unafanyaje unalia?

Hali huwa ni mbaya zaidi linapofikia suala la mtu amekosa dili. Mfano sisi wajasiriamali yani dili nzuri ghafla ikayeyuka. Aisee. Ukimuuliza Andrea vipi anakujibu "We acha tu"

Au kwa wenzetu "wanaotafuta kazi" pale akikosa AJIRA. Au ameachishwa KAZI. Yaani "hali ya hewa" huwa inakuwa kama imevurugika vibaya sana. Vijana waliokosa AJIRA huwa wengine wanakata tamaa. Mabinti wadogo vishawishi vinakuwa na mvuto zaidi ili aanze kuishi kama "wenzake". Watu wazima kidogo anaweza kukosa mwelekeo na hata kuzorota afya.

Wengi wetu huwa hatuna kawaida ya kutulia na kusahau yaliyopita na kuganga yaliyopo na yajayo! Yani mtu akikosa ajira anakuwa kama kila kitu kimestop!

Kwa wewe uliye kundi hilo naomba niseme na wewe kidogo kabla sijaendelea. BRIAN ACTON na JAN KOUM walianzisha mtandao wa WhatsApp BAADA ya kukosa AJIRA. Mmoja kakosa ajira Facebook mwingine kakosa Twitter.

Lakini walikuja kuuuza huo mtandao wa WhatsApp kwa $22 billion. Yani trilioni 45 za kitanzania. (Mwanzo ilikuwa waiuze kwa $19 bilioni lakini dau likaongezeka) ukisoma hii link utaona hilo http://www.dailymail.co.uk/sciencetech/article-2782370/Facebook-completes-19-billion-acquisition-WhatsApp-European-regulators-green-light.html

Sijui unaelewa kukaa tu na computer na kichwa chako na kuwaza vizuri halafu miaka kadhaa tu baadaye wakawa na utajiri huo?

Na mimi kinachonifurahisha zaidi katika hawa jamaa ni kuwa walimuuzia mtu aliyemnyima mmoja wao kazi. Facebook!

Muhimu ni kuwa hawajalalamikia mtu wala kutaka kujiua.  Walikaa wakaendelea na MENGINE.

Hii tabia ya kuendelea na mengine ni jambo muhimu mno maishani. Ukiwa mtu wa kuangalia PAST tu nini kilipaswa kiweje na kwa nini hakijawa.. na kuanza kusema WHY ME? Utashangaa unakufa kabla hujaishi. Serious. Unafikiri Mungu mjinga? We fanya mengine. Mi siku hizi nina usemi wangu : THE PAST 1 MINUTE IS GONE AND I'M NOT INTERESTED IN IT.
So kama kuna kitu nimefanya au sikufanya basi. Nataka kujua zaidi kuhusu NOW. Kesho nayo mwenye nayo hajanipa bado so NOW ndo pa kuishi. Not the past 1 minute or day or month or year. It's gone. And sitaki kuiwazawaza.

Ndivyo walivyoishi hawa jamaa wa WhatsApp. Yani iko hivi... nakuja kwako kuomba kazi unasema HAKUNA NAFASI. Afu mi na smile najibu tu "OKAY". Then naenda kuanzisha kitu kingine na baadaye wewe uliyesema HAKUNA NAFASI unaanza kunibembeleza nikuuzie nilichobuni halafu mimi nasema kama unakitaka basi utakinunua lakini lazima tufanye wote kazi. Na unakubali. Problem solved. Sasa ukilia na kusubiri watumbuliwe wengine ili wewe uajiriwe na wewe ni jipu.

Ukikosa ULICHOTAKA fanya mengine. Sasa mwingine hapa anauliza "mengine yapi?". SASA si ndo maana juu ya shingo yako kuna kichwa. Au kiliwekwa cha nini.  Kina macho. Pua. Kinywa. Masikio. Nywele. Sasa macho ulipewa ya nini? Ya kutolea machozi? Na kichwa ndani yake kuna UBONGO. Uliwekewa wa nini sasa? Si ungepewa kichwa cha kuku basi.

My point is ukikosa chochote usianze kuwaza milele na milele.

Kwenye kitabu changu nimeandika kuhusu  Steve Jobs jinsi alivyoanzisha kampuni ya Apple. Halafu baadaye corporate politics zikaingia akapigwa chini kutoka kwenye kampuni aliyoanzisha mwenyewe. Inauma mno.

But what did he do? Huyu mimi nikimkumbukaga huwa najifunza sana. Yeye hakulialia milele na milele kama wengi wetu. Alienda kuanzisha kampuni NYINGINE.
Halafu jina la hiyo Kampuni nyingine akaiita "NeXT". Na hapa ndo nimepata title ya makala hii.

Yes. NEXT. So kuna NEXT nyingi mno maishani mwetu. What's your NEXT opportunity? Usililie mlango uliofunga. Kitu kikishatokea songa mbele. Steve Jobs aliifanya hiyo NeXT ikawa nzuri na bora mno kiasi kwamba APPLE waliomtema wakalazimika KUMNUNUA tena. Na sharti lake likawa anawauzia lakini lazima awepo kwenye uongozi wa Apple. Na wakakubali. Ndo kisa cha Jobs kurudi Apple na leo iPhone ni brand kubwa na aghali mno sababu yake.

Sasa kama wewe ni msanii wa muziki umeenda studio wamekukataa usilielie. Kaimbe hata kwenye birthday za watu huko bure. Watu watakuona huko huko. Kwani mwenye studio kabaki na sauti yako na miguu yako? Hapana. Basi angalia your NEXT OPPORTUNITY.

Umeanzisha biashara kila unayemjua ANAAHIDI TU kuwa atakuungisha halafu hawakuungishi wala nini. Unaacha eti. Eti unasema hakuna wateja. Kweli? Nchi hii  ina mamilioni ya watu. Waliokataa kukuungisha hata 50 hawafiki unakataje tamaa? We jiulize tu nani my NEXT customer. Wengine watakuungisha mbeleni. Mi nina mteja wangu mmoja hakununua kwangu miaka mitatu mfululizo lakini kuna siku akaja na sikutumia hata nguvu kumwambia chochote. Leo ni mteja mzuri mno. Three years! Ningeacha baada ya mwaka je? So cha muhimu ni kujiuliza WHAT'S YOUR NEXT.. next opportunity, next relationship, next deal, next student,  next coach or manager, next client, next team, next radio show, next job, next business. Kuna mpaka next husband au wife. Sembuse AJIRA?

Your future iko kwenye "NEXT" zako. Siyo kwenye "LAST". Juzi nikawa naongea na binti mmoja kwenye simu anahitaji ushauri fulani. Lakini kila nikiongea naye huwa anapenda kusema I DID THIS I WAS LIKE THIS nk. Nikamwambia tu I'm not interested in your past coz I'm not going to the past and neither are you. Nikamwambia maneno "DID.. WAS" nk hayaletagi melody nzuri masikioni mwangu so asiwe ananiambia. Aseme zaidi kuhusu SASA. NOW.

Najaribu kuupunguzia ubongo wangu mzigo wa kuwaza kinyumenyume!
Nadhani na wewe unatakiwa usiwaze hivyo.  Fikiria WHAT NEXT. Kisha anza kufanyia kazi.

Maisha lazima yakupe LADHA ZOTE ndugu. Nzuri na ambazo si nzuri. Tamu na zisizo tamu. The key is to take each and move on.

Kuna siku nikiwa mwanafunzi Makongo. Nimetoka shule na njaa balaaa. Nimefika home mchana saa tisane hivi nikakuta maziwa yamebakia kidogo kikombe kimoja tu so nikachemsha halafu nikaweka vijiko vya kutosha vya sukari yani nimekoroga hadi raha angalau ule utamu utasaidia kudanganyishia njaa.. Sasa ile kunywa tu khaaaa! Kumbe nilidhani niliweka sukari kumbe chumvi!! Tena ya kutosha. Aisee yani nilicheka kweli.. njaa ikapata bonge la surprise.
Ndo hivyo. Sometimes unataka sukari life inakupa chumvi...tena ya kutosha. Move on.. Find your NeXT.

Ndivyo maisha yalivyo.

Watu wengi wanaishi kwa mazoea. Kuna mtu aliuza nyumba ili agombee ubunge mwaka juzi 2015. Ukisikia KUJILIPUA ndo kama hivi yani. Akapata hela zake akaingia kwenye mchakato wa uchaguzi. Biashara ikawa "kichaa". Kidogo naye awe kichaa. Maana ubunge hana, nyumba hana, hela nazo hana na marafiki nao hana. Hapo ndo utaelewa kukoroga kitu kwenye maziwa bila kuonja kwanza kama ni sukari kweli. Alipata frustrations za kutosha. Lakini hakujiua. Alianza moja akachechemea taratibu naamini anaendelea na maisha baada ya uchaguzi. Amepata NeXT yake. Ndivyo inavyotakiwa ufanye. Move on. Ukibaki na WHY tu utapata madonda tumboni na mvi za ghafla bila kutarajia na bado utakuwa hujabadilisha kilichotokea! Don't be small minded. Move on.

Awamu hii ya JPM kuna watu wametumbuliwa hadharani. Kuna watu wametuhumiwa na madawa. Kuna watu wamezodolewa na kukashifiwa hadharani. Na katika hao wote kuna makundi mawili. Kuna ambao hawakufunua kinywa chao kabisa. Hata mara moja. Hawa ni Big Minded people.  Na kuna waliowaza "KWA NINI WAMENITAJA". Hawa ni small minded people. Maana watu wameanza kutajwa toka shule ya msingi majina ya wapiga kelele. Au Swahili Speakers. Wakala stiki na zilishapoa. Wengine walitajwa kuwa wamebadili dini ili wawe raisi wa nchi. Hawakupiga mayowe. Sasa wewe wa kwanza kutajwa dunia hii? Yesu alionyesha watakaombetray wawili: Yuda  (atamuuza) na Petro (atamkana). Mmoja alijiua mwingine akalia na kutubu na kukomaa kiutu uzima. Wewe ni Petro au Yuda in that regard? Think for yourself.

Ndo kipindi hiki cha JPM mwingine ana kutu moyoni eti "Kwa nini wamemtumbua baba yangu"? Small minded people. Mwingine ana kutu moyoni eti "Hivi kwa nini girlfriend hajajibu message yangu siku ya tatu leo na naona tiki za blue?" Move on. Don't live in the past.

Wana wa Israeli walikuwa wanawaza kinyumenyume tu. Matango na viungo vya chakula walivyoexperience utumwani. Wakatamani hadi kuzikwa kwenye makaburi kuliko kufa jangwani wakasahau wako huru. Wanachotaka hawakioni wakawa watu wa kupiga "mayowe" tu na kulalamika kila wakati. Nadhani unajua kilichowakuta. So wewe pia kama  ULICHOTAKA hakijawa basi find your "NeXT". Hiyo ndo positive thinking iliyomrudisha Steve Jobs Apple na kuwafanya hao waanzilishi wa WhatsApp kuwa matajiri mno.
Kama hukubali ni sawa pia.

Lakini maisha mazuri na ya utulivu (good and tranquil life) kwa wengi yamekuwa ndoto kwa sababu ya kuwa na WHY zisizoisha. Anabaki anajiuliza hivyo tu. Usibaki na WHY. Swali sahihi ni *WHY NOT?* Yaani: why not nisikose mimi kazi. Nilitaka akose nani ili mi nipate. Kwa nini usitajwe wewe? Kwa nini nisisemwe mimi vyeti vyangu. Nataka nani ndo asemwe. Yes, sometimes WHY is a selfish question. Unajiwazia wewe zaidi. Unaunyima ubongo wako fursa ya kuwa CREATIVE. Unabaki na KUTU moyoni kisa boyfriend kakuacha huli wala hunywi na kujiua unataka. Kisa tu hukujiuliza swali sahihi: Why Not. Kwa nini usiachwe. Kwani wewe umekuwa Mungu? Mungu mwenyewe kuna malaika walimwacha. Sembuse wewe? Kuna watu wametelekezwa na wazazi sembuse boyfriend. Eti anasema inauma wewe hujui tu. No move on. Find your NeXT. Unajuaje labda anayefuata ndo ulikuwa umeumbiwa. Trump alililia wake zake walioondoka? Alifind NeXT. Kumbe huyo ndo First Lady. Ujue kama hujaoa First Lady ikulu huipati hata uweje. Sasa wenye ndoto za kuwa maraisi sijasema umpige chini mkeo unahisi ndo siyo sahihi. Lol. Trump huyo hapo. Ana mind hii ya MOVING ON. Democrats mpaka leo hawaamini walipoteza uchaguzi. Kuna watu wanaamini walishinda uchaguzi. Bado wako na WHY. Why siko IKULU. Move on kwanza.

Ukijifunza kuishi kwenye NEXT utapiga hatua kubwa na kuwashangaza wengi.  FIND YOUR NEXT.
Serengeti Boys yetu imetolewa kwenye michuano. What's NeXT? Au tupo tu hatujui nini tufanye. Watakaa tu au watapewa hata zawadi kuwatia moyo. What NeXT.

Umeomba mkopo benki wamekunyima. What NeXT. Move on. Labda wamekunyima kunde tu.......! Shukuru tu Mungu and tafuta what NeXT.
NeXT ndo kila kitu.


****
By the way ile siku niliyokoroga chumvi ya kutosha kwenye maziwa hadi njaa ikapata surprise  niliangalia mfukoni nikakuta nina sh mia tatu. Enzi hizo. Nikaenda kwa Mangi. Sasa unadhani njaa ilipata dawa au hapana?

Find your NeXT my friend.

Mungu akubariki sana!



Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp #o788366511

Jumamosi, 13 Mei 2017

DUNIA HAITOKUKUMBUKA KWA MAMBO UTAKAYOJISIKIA KUFANYA BALI KWA MAMBO #UTAKAYOSUKUMWA KUYAFANYA


Mungu katuwezesha kukutana tena. Basi Jina lake lizidi kuinuliwa maana kuwa hai ni za zawadi kubwa mno.

Leo nina jambo muhimu kuongea na wewe.


Katika kipindi cha miaka saba ambayo nimeitumia kujifunza na kupractice ujasiriamali na kujifunza kwa watu walioacha ALAMA duniani nimeweza kujifunza mambo mengi. Mojawapo ni kuwa dunia haina muda na mambo unayokuwa COMFORTABLE kuyafanya hata kama utafanikiwa nayo vipi. Ukifa yanaishia hapo na jina lako linabaki kwenye kaburi pale. Born 19.... died 20... hivyo yani.

Dunia inamkumbuka mtu ambaye alitii sauti ya MSUKUMO wa ndani wa kufanya kile alicholetwa hapa duniani kukifanya. Unaweza kuwa effective and successful kwenye jambo fulani hapa duniani lakini kama ukifa na jina lako likafa ni dalili kuwa ulikuwa mbinafsi na ulitaka mafanikio BINAFSI tu wala hukujali kuwa unapaswa uguse watu wengine kabla hujaondoka duniani. Ni vizuri kuangalia sana mambo unayoyafanya kama unayafanya tu kwa kuwa ndicho ULICHOSOMEA au ndicho KIRAHISI KUFANYA au unakifanya kwa kuwa kuna MSUKUMO NDANI YAKO wa kukifanya?

Yaani uligombea ubunge kwa kuwa ULISUKUMWA moyoni au sifa tu au ulitaka kuonyesha watu kuwa wewe ni "kiboko"? Usipoangalia hili jambo utakuwa maarufu kweli kweli lakini siku ukimaliza muda wa ubunge na jina lako linaishia hapo tena ukiwa bado hai. Hivi kila aliyewahi kuwa mbunge mashuhuri au waziri bado anatajwa leo na kukumbukwa?
Ask yourself.

Unafanya biashara kama fashion au una MSUKUMO ndani kuwa ufanye? Kama huna msukumo ndani wa biashara basi utakuwa unaendesha gari kwenye njia ya treni. Kitakachotokea hata wewe mwenyewe hutajua yani. Usifanye biashara ili uwe kama Dewji. Yeye ana msukumo wa kwake. Wewe nawe UNAO?

Umeajiriwa sababu "watoto watakula nini" au umeajiriwa sababu una MSUKUMO kuwa inatakiwa uwepo hapo ulipo ili huduma yako iwanufaishe watu wa Mungu watakaokuja kazini kwako? Usifurahie kuitwa ofisa wa benki au meneja masoko au head mistress nk huku una IGNORE sauti fulani inayokusukuma kutokea ndani kuhusu jambo jingine kabisa. Ukiendelea kuiignore hiyo sauti ipo siku ITANYAMAZA kimya haitazungumza tena kwa kipindi kirefu tu. Lakini ujue utakuwa umeignore kitu ambacho Mungu alikuwa anataka ufanye. Utashangaa umekaa kazini miaka mingi na mpaka unastaafu lakini huna amani moyoni na ukistaafu basi jina linaishia hapo pia. Halafu ile sauti ndo itarudi sasa. How sad.

Unasoma Chuo kwa ajili CV ionekane ina neno "University" au ili ukue-kue kidogo kabla hujaolewa...au unasoma sababu una kitu kinakwambia moyoni kuwa unapaswa kusoma hicho kitu. Au ulichagua kozi kwa kuwa ni nyepesi au kwa sababu "ina AJIRA" au sababu rafiki au anko alisema engineering ndo kozi ya "vichwa" kama wewe. Sasa kichwa gani unaambiwa pa kwenda.

Point ya msingi hapa ni kuwa mahali popote ulipo jitahidi sana kusikiliza sauti ya ndani yako. Siyo maneno ya mzazi tu au mume au mke sijui auntie ambao sauti ya ndani yako hawajui inafananaje. Za ndani kwao zenyewe hawajazisikiliza wataelewaje kuwa huwa kuna sauti ndani ya mtu!? So BE YOU. It's YOUR life. Life is really more than money and fame.

Dunia huyapa heshima kubwa majina ya wale waliofanya vitu vilivyotokana na MSUKUMO fulani ndani yao na siyo waliofanya tu sababu ya fashion au kutaka kujulikana na certainly haiwapi heshima wale waliodharau sauti iliyowaambia ACHA HIKI KAFANYE KILE.

Ni ngumu  kuacha kitu ambacho ni popular machoni pa wengi ili ukafanye kitu ambacho unasukumwa moyoni kufanya hata kama hakieleweki kwa wengine. Lakini ukiweza hilo basi jina lako litakumbukwa miaka mingi hata ukiwa umeondoka.

Ngoja nikupe mifano michache tu ya majina yanayotajwa na kukumbukwa sana na dunia.


1. WILLIAM BOEING

Ilikuwa jioni majira ya saa moja kasoro hivi. Mwangaza wa jua la mwezi wa July uling'arisha anga la magharibi kwa rangi nzuri iliyotulia na jua likaanza kudondoka na kuruhusu giza kuufunika uso wa nchi. Nikiwa futi 30,000 kutoka usawa wa bahari ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kushuhudia jua likizama nikiwa angani mbali kiasi hicho. Kuzama kwa jua (sunset) ni mojawapo ya mambo ninayopendelea sana kuyatazama.

Masikioni mwangu kulikuwa na headphones nikisikiliza muziki wa kusindikizia safari yangu ya kwanza ndani ya ndege aina ya BOEING 737.. Baada ya kutazama jua likiwa limeishia kabisa juu ya mawingu akili ikanirudisha kwenye dirisha la ndege kushoto kwangu lilivyokuwa zuri na lilivyotengenezwa kwa ustadi mkubwa. Na kisha akili yangu ikanileta kwenye ndege yenyewe - BOEING 737.

Muda kidogo baadaye jina la mwanzilishi wa kampuni kubwa ya Boeing likaja kichwani. Huyu ni bwana William Boeing. Nikaanza kutafakari kidogo kuhusu alipoanzia, alichoamua kufanya, ALICHOSUKUMWA kufanya, na dunia inamkumbuka kwa lipi katika hayo.

Akiwa amezaliwa familia "bora" baba yake akiwa mhandisi wa mambo ya madini William alisomeshwa shule za maana mno kwanza Uswizi kisha kwao Marekani kwenye Chuo Kikuu maarufu cha YALE UNIVERSITY. Kama hujui kuhusu Chuo hiki Google tu kidogo uone kusomesha mtu hapo inakuwaje.

Lakini William akakatisha masomo yake YALE UNIVERSITY na AKAAMUA kwenda kufanya biashara ya MBAO!! Dah!.  Kuna watu wana maamuzi magumu. Huwa nasema ni rahisi kuacha VETA ili ukafanye mambo yako. Lakini kuacha YALE UNIVERSITY ukauze MBAO? Hiyo ni level nyingine ya maamuzi. Trust me.

Lakini akafanikiwa sana katika hiyo biashara na kupata fedha nyingi mno. Akajulikana kama muuza mbao maarufu.

 Lakini katika safari zake kibiashara siku moja akatembelea maonyesho ya kibiashara huko Seattle na kuona watu wametengeneza mashine fulani ambayo waliirusha angani IKIWA NA MTU.  Moyo wake ukapiga PAAP! Akapata MSUKUMO mpya kabisa wa kuunda NDEGE yake. Na akaacha kila kitu na hela zake akazielekeza kwenye hilo jambo lililompa msukumo mpya.

Alipitia mengi lakini akafanikiwa. Na leo hii dunia inamkumbuka kwa jambo hilo. Ukitazama leo ndege aina ya BOEING zilivyo leo ni mwendelezo tu wa alichokianzisha. Dunia haikumbuki mbao ngapi aliuza. Ukitaja jina/neno Boeing watu hawalihusishi na mbao bali na kampuni kubwa ambayo imegusa maisha ya watu wengi mno. Na hakuna siku inayoenda leo ambapo hagusi maisha ya watu dunia hii. Na hayupo.

What about you? Think about your end. Forget the comfort. Work on your legacy. Utakumbukwa kwa kipi? Kwamba ulikuwa polisi au mhasibu afu basi? Kuna mapolisi au wahasibu wangapi dunia hii hadi ukumbuke ukumbuke wewe? Gusa maisha ya watu hasa wasikokujua kabisa.


2. FRANCIS SCOTT KEY

Huenda hili likawa jina geni kwako. Huyu alikuwa mwanasheria maarufu tu huko Marekani zamani za kale. Alifanya kazi kubwa mno kama mwanasheria hadi akafikia kuwa DISTRICT ATTORNEY hiki ni cheo cha heshima mno katika kila jimbo la Marekani. Kumbuka Marekani kila jimbo ni nchi. Yeye alikuwa District of Columbia. Yani "jikoni". Hivi Mungu akupe nini?

Lakini kuna jambo lilitokea kati ya mwaka1812 hadi 1815. Nalo ni vita kati ya Marekani na Uingereza. Kuna wamarekani wakakamatwa na Jeshi la Uingereza. Yeye kama mwanasheria akawa amepelekwa kwenda kuNEGOTIATE hao watu waachiliwe. Bahati mbaya naye akashikiliwa. Akakaa kwenye kambi ya adui kwa muda mrefu mno huku akishuhudia nchi yake ikidondoshewa mabomu na hana cha kufanya. Lakini siku moja alfajiri mapema mno mapambazuko yakianza na usiku kucha eneo la Marekani lililokuwa karibu na ile kambi likiwa limeshushiwa "mvua" ya mabomu usiku kucha huyu bwana Francis Scott Key huku akitazama kwa masikitiko eneo la nchi yake lililopigwa mabomu usiku kucha akashangaa kuona bendera ya Marekani ikiwa ipo kwenye mlingoti ikipepea. Kitu hicho kilimpa MSUKUMO wa ajabu mno moyoni. Akapata faraja kubwa kuwa licha ya mabomu yote yale lakini bendera ya nchi yake ilikuwa bado ikipepea vizuri kabisa. Akapata MSUKUMO wa kuandika SHAIRI kuhusu hilo tukio. Kichwa cha hilo shairi ni: THE STAR-SPANGLED BANNER (banner=flag)

Miaka kadhaa baadaye Bunge la Marekani (Congress) likapitisha resolution ya shairi hilo kuwa WIMBO WA TAIFA WA MAREKANI!

Leo hii Francis Scott Key hakumbukwi kwa kesi nyingi alizosimamia kwa kazi aliyosomea bali kwa kitu alichoandika bila kusomea. Popote pale wimbo wa TAIFA wa Marekani unapoimbwa  kila siku anagusa maisha ya watu wengi mno wa nchi yake na nje ya nchi yake wanaoguswa na shairi lake.

Usikute wewe unaweza kuchora picha moja tu au kutunga kitabu kimoja tu na dunia ikakukumbuka kwa hilo ila unang'ang'ana uwe maarufu kama Tundu Lissu.
Think about that.


3. NELSON MANDELA

Mwanamasumbwi na mwanasheria pia msomi kutoka Chuo Kikuu cha FORT HARE na kile cha WITWATERSRAND. Na akiisha kupikwa huko katika vyuo AKAAMUA kufanya kazi kama mwanasheria jijini JOHANNESBURG.

Lakini serikali ya watu wazungu ilipopitisha sheria ya ubaguzi wa rangi Mandela akapata  MSUKUMO mpya ndani yake siyo wa kuwa hakimu au jaji no. Ulikuwa ni msukumo wa kupigania USAWA na kupinga sera za kibaguzi kwa moyo wake wote. Msukumo wa kuwa mwanaharakati.

Alipitia magumu mengi, ndoa yake ya kwanza na bi Evelyn Mase ikafa.
Akaanza kufatiliwa na serikali na kukamatwa mara kwa mara. Mwisho akapewa kesi nzito na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela ambacho alikitumikia katika magereza matatu tofauti ikiwemo la Robben Island.

Miaka 27 baada ya kufungwa akaachiwa. Dunia haikumbuki gloves zake au kesi alizosimamia bali UANAHARAKATI WAKE na KUPIGANIA KWAKE USAWA. Pia dunia inamkumbuka Mandela kama mtu aliyekuwa hana kinyongo na mtu. Mfano licha ya yeye kuachana na mke wake wa kwanza kwa sababu za Evelyn kumtuhumu Mandela kutokuwa mwaminifu na Evelyn kubadili dini na kuolewa na mtu mwingine na nk lakini Evelyn alipokufa Mandela na familia walihudhuria msiba vizuri kwa hisia zote. Lakini pia alipotolewa gerezani alimsamehe mtu aliyeidhinisha Mandela afungwe maisha!!
Dunia inakumbuka hilo.

What about you?


4. ABRAHAM LINCOLN

Mwanasheria mwingine huyu. Tena huyu alikuwa mwanasheria kwa KUJIFUNDISHA mwenyewe na kisha kwenda kufanya BAR EXAM (wanasheria wanajua hii kitu..siku hizi kuna LAW SCHOOL)

So huyu ni kichwa sana acha wewe ambaye umefundishwa na maprofessa wazuri na maktaba unayo na computer na internet na hao waliokufundisha wanakupa mtihani na bado unafeli afu unasema eti profesa kanifelisha! Ungejifundisha mwenyewe nyumbani kama Lincoln afu ndo ukapewe mtihani ungeelewa hata swali linahusu nini kweli? Nataka uone tofauti yako na Abbe! Alikuwa kichwa si mchezo.

Alisimamia kesi kadha wa kadha na kupata ushindi mnono hasa kwa kutumia kipawa chake cha kuongea vizuri.

Hata hivyo dunia leo haimkumbuki kama mwanasheria nguli na kichwa bali kama mojawapo ya maraisi bora kabisa wa Marekani na hasa kwa kuzuia umiliki wa watumwa huko Marekani na kuzuia nchi kusambaratika ilipoingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mgogoro wa umiliki wa watumwa ambao ulizalisha chama cha Republicans mwaka1854. Baada ya Congress kupitisha sheria ya KANSAS-NEBRASKA ACT ambayo ilitaka kila jimbo liamue lenyewe endapo litaruhusu watu wake wamiliki watumwa au la. Majimbo kadhaa yakapinga hiyo sheria yakitaka sheria isiwepo suala la kuchagua kumiliki au kutomiliki. Ndipo Republican Party ilipoanzia hapo na LINCOLN akapata MSUKUMO mkubwa wa kuachana na sheria na kuingia kwenye siasa za uongozi wa juu rasmi akijiunga na chama cha Republican mwaka 1856 na kuwa raisi miaka minne tu baadaye!

Wajasiriamali na watafuta mafanikio wanamkumbuka Lincoln kwa jinsi alivyopambana bila kuchoka kutoka level za chini hadi kufikia kuwa raisi wa Marekani. Sheria ilikuwa tu mahali alipoanzia lakini uongozi wa nchi ukawa ni msukumo wa ndani. Msukumo mkali mno wa ndani uliomvusha kwenye changamoto za vipindi vigumu vya kushindwa uchaguzi kupoteza mke kupata nervous breakdown nk hadi akaja kuwa raisi.

Usidharau msukumo wa ndani. Lincoln angeweza kubaki mahakamani lakini jina    lake lingeishia siku yake ya kufa kama maelfu ya wanasheria wenzake huko ambao hakuna anayewajua wala kuwakumbuka.


5. TAIKICHIRO MORI

Kila mtu anamjua Bill Gates hasa kwa kuwa ni tajiri namba moja duniani. Lakini ni vizuri kupitia historia na kujifunza kwa waliowahi kumtangulia katika nafasi hii.
Taikichiro Mori ni mmoja wapo na alikuwa tajiri namba moja duniani mwaka 1992 utajiri wake ukiwa net worth $13 billion.

Na dunia inamkumbuka hivyo yani licha ya kuwa alikuwa academician mzuri huko Japan na mwenye mafanikio katika eneo hilo.

Alipata mafanikio mazuri katika masomo yake hadi kufikia kuwa mwalimu wa Chuo Kikuu.  Na huko katika kufundisha akafanikiwa hadi kufikia level ya DEAN wa KITIVO CHA BIASHARA katika Chuo kiitwacho YOKOHAMA CITY UNIVERSITY. Ukiwa dean wewe ni mtu mkubwa. Alidumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi alipostaafu mwaka 1959.

Ni baada ya kustaafu ndo alipopata MSUKUMO mpya wa kufanya biashara ya REAL ESTATE. Nadhani hela zake mafao hizo. Lol. Alifanya hiyo biashara kwa miaka mingi na akafanikiwa mno ndo hadi kufikia 1992 akawa tajiri wa kwanza duniani. Dunia inajua alipoanzia lakini inakumbuka na kuheshimu ilichomsukuma kufanya.

Sasa kustaafu ualimu au uhandisi au unesi au chochote siyo mwisho wa maisha. Kama kuna sauti ndani inakwambia kagombee udiwani au kafungue mgahawa tii sauti usifanye mgumu moyo wako. Usiseme miye mzee. Kuna mstaafu mwenzako mzee alitajirika uzeeni. Huyu si mwingine bali.....


6. HARLAND SANDERS (a.k.a Colonel Sanders)



Huyu naye alikuwa mwanasheria lakini sheria ikagoma "kumtoa" baada ya miaka mingi. Akaona afanye vingine kama kuuza insurance covers nayo ikagoma. Akaamua kuuza taa tu sasa. Taa nazo zikampa headache tu. Mpaka anastaafu anapata mafao anayaangalia hivi anaona ujinga kabisa bora akajiue tu.

Lakini kabla ya kujiua akiwa mahali anapanga mipango ya kujiua akapata msukumo mdogo tu ndani kwamba kabla hajajiua aandike kwenye karatasi vitu vyote ambavyo hajawahi kufanya. Akiwa anaandika akakumbuka kuwa yeye alikuwa ni bonge la mpishi. Na kwamba alikuwa ametengeneza formula  (recipe) ya kupika kuku kwa kumchanganya na viungo zaidi ya 10 tofauti tofauti ambavyo ni yeye tu alikuwa anavijua na kuku alikuwa mtamu asikwambie mtu. Khaaa. Akaahirisha kujiua akaenda kuanza kupika kuku ili sasa badala ya kula mwenyewe akawauzie wengine. Lol. Akaanza kuuza kwenye sehemu watu wanakojaza mafuta kwenye gari. Anawaambia huyu kuku ukimla lazima utampenda maana nimeweka recipe ya viungo vingi vizuri vya asili. Kama mchezo akaanza kuingiza vijisenti. Akiwa na umri wa miaka 62 akapata MSUKUMO mwingine wa kuisajili biashara yake kama franchise business akiwa anaiita KENTUCKY FRIED CHICKEN. Kuku wa kukaanga kutoka jimbo la  KENTUCKY. Hiyo ilikuwa mwaka 1952.

Miaka 12 tu baadaye mwaka 1964 biashara ilikuwa imechanganyia akaiuza kwa $2 million. Bilioni kama nne za kitanzania leo. Fikiria mtu mwenye hela aina hiyo mwaka 64!!! Akiwa mzee wa miaka 74.

Kwa hiyo kama umepigika huoni mbele unataka ufe tu mwambie shetani hivi: NAAHIRISHA KUJIUA SITAKUFA BALI NITAISHI NA NITAFANYA KITU HAKIJAWAHI KUTOKEA HATA KAMA NI KUKAANGA DAGAA UPYA.

Ilimradi usikilize sauti ya ndani yako kwa utulivu. Tulia sikiliza. Mungu akiongea utajua tu I tell you. Utashangaa hakuna atakayekufundisha cha kufanya utahangaika huku na kule wewe mwenyewe utajishangaa hutakuwa na muda na critics na wanaokucheka wala hutatafuta kuonewa huruma tena. Utashangaa mifupa yako ina nguvu akili yako imeamka. Huo nao ni kama ubatizo mpya kabisa nakwambia. Na dunia haitataka kujua sijui ulisoma wapi au ulifanya kazi wapi. Dunia itataka kutangaza jina lako kupitia mambo uliyoyafanya kupitia MSUKUMO NDANI YAKO. Kitabu kinasema UTII NI BORA ZAIDI... Ndo maana Sprite wanasema TII KIU YAKO. Sasa mi nasema TII SAUTI YA NDANI YAKO na utashangaa toka hapo hutajitaji alarm ikuamshe utaamka mwenyewe tu.  Kwani jogoo huwa anaamshwa na alarm? Yeye ndo alarm clock. Sasa ukitii sauti ya ndani utashangaa wewe ndo unakuwa ALARM CLOCK.

Usifanye kitu kwa kuogopa watu watakuonaje kama hutafanya. Kuna watu wakiona RANGE ROVER inapita huwa wanasema: DAH MUNGU ALIUMBA VICHWA AISEE. Utukufu unaenda kwa Mungu. Kuna watu wakila KFC huwa wanamtukuza Mungu. Kuna watu wa wakipanda ndege au wakiimba wimbo wa TAIFA au wakilala hoteli nzuri nzuri au wakinunua iPhone huwa wanajisemea dah Mungu aliumba vichwa. Hayo yote na mengine ni zao la watu WALIOTII SAUTI YA NDANI MWAO. Kuna watu wanapaswa waogeee au kusafishia nyumba sabuni yako halafu ile harufu tu mtu anaisikilizia anamtukuza Mungu. Lakini wewe unataka kukata tamaa. Eti huwezi kuuza sabuni.

Kuna mtu mwingine.. Robin Sharma.. aliacha sheria pia baada ya sheria kumpa stress za kutosha akapata MSUKUMO  kuandika kitabu kinaitwa MEGA LIVING ili kusaidia watu jinsi ya kumanage stress. Kisha akaandika THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI

na THE LEADER WHO HAD NO TITLE na akagusa maisha ya mamilioni ya watu na baadaye kukodiwa na mpaka makampuni makubwa duniani kama NIKE, MICROSOFT, PwC, HP ili afundishe viongozi wa hayo makampuni na wafanyakazi wao. Unakuta analipwa hadi dola laki tano kwa saa na anafundisha masaa matano.  So siku hiyo moja anakuwa ameingiza dola milioni moja na nusu.  Yani bilioni tatu za kitanzania kwa siku moja. Hiyo ndo THAMANI anayopewa mtu aliyetii sauti ya muumba wake kutoka ndani.

Ndege huimba kwa msukumo ulio ndani yao. Siyo kwa kuwa ndege wenzake watamwonaje asipoimba. Wewe unafanya vitu ili watu wakuelewe? Yesu hawakumwelewa watakuelewa wewe? Mimi huwa naandika tu sijali atakayeshindwa kuelewa nachosema. Naangalia msukumo ulio ndani ukiniambia andika kuhusu hiki naandika. Hata ikiwa saa saba za usiku.

Ukitazama watu wangapi wanaafiki ndo ufanye kitu wakati moyoni mwako tayari kuna mwafaka ujue hiyo ni dalili ya WOGA na kutotii.  Kumbuka kitabu kinasema UTII NI BORA.
TII SAUTI YA NDANI YAKO


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp #o788367511
All Calls and SMS #o752367511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com