Ahadi ni deni.
Niliahidi kuwa makala yangu inayofuata itazungumzia suala la Traveller's mindset Vs. Passenger's mindset so nashukuru Mungu nimetimiza ahadi licha ya mambo kuwa mengi na hii ikiwa makala yangu ya kwanza ya mwaka huu mzuri wa 2018 toka Yesu aje dunia hii.
Tuendelee...
::::::::::::::::::::::::::::::: :::::::::: :::::::::::::::::::::::::::::::::
Mwanzo!
September 2017.
Ni Jumamosi.
Alarm ya simu yangu inaita kwa nguvu mida ya saa 10 na robo alfajiri. Naamka papo kwa hapo ili mlio usivuruge usingizi wa mke wangu maana alikuwa amefanya kazi kubwa jana yake kuniandalia vitu muhimu kwa safari yangu ya simu hii.
Ninazima alarm nashukuru Mungu kwa kuniamsha salama (ningekuwa nimekufa nisingesikia alarm au siyo?)
Nikakimbia bafuni chap chap kujimwagia maji ili kuondoa kabisa uchovu na usingizi. Well mwezi huo bado asubuhi kulikuwa na kibaridi sana hata hapa Dar es Salaam. Nilimaliza kujisafi na kuelekea chumba kingine ambapo nilikuwa nimeweka begi langu ili pia maandalizi yangu ya mwisho yasiondoe usingizi wa mke wangu.
Begi la size ya kati hivi lilikuwa tayari nguo kadhaa za kutosha kubadili huko niendako, mashuka mawili, taulo, viatu na sandals, begi lilijaa hadi likafunga kwa shida kidogo. Begi la mgongoni (backpack) lilikuwa na notebook, na vitabu viwili, biblia laptop na scarf nzito ya kufunga shingoni ikitokea hali ya baridi. Maji ya kunywa dawa chache muhimu mswaki nk.
Nikamuaga mke wangu nikampigia bajaj fasta huyo Ubungo.. Safari ya Mwanza ikawa imeiva. Kaubaridi ka alfajiri kalinifanya nivae shati na kuweka na koti juu yake.
Safari ikaanzia Shekilango na ilikuwa nzuri tu licha ya kuonekana kama kulikuwa na hitilafu kiaina kwenye gari (kwa mtu anayejua gia zinavyopaswa kuingia kwenye gari) lakini ilikuwa salama na kiyoyozi kizuri kikipuliza na kuubembeleza mwili.
Lakini baada ya kukaribia tu Chalinze basi likaharibika kabisa tatizo tukiwa tunadhani ni dogo kumbe gear box..!
"What the.....????"
Sauti kadhaa zikasikika.
Well wa kulalamika walikuwepo wa kupiga simu walikuwepo wa kupiga selfie pia walikuwepo. Wa kununa kimya kimya walikuwepo.
Wa kulaumu kiwanda lilichotengeneza basi nao walikuwepo. Wa kulaumu dereva walikuwepo wwa kulaumu mmiliki walikuwepo wa kulaumu SUMATRA walikuwepo. Wa kulaumu serikali walikuwepo. Na wa kujilaumu kwa nini hawakusafiri jana yake pia walikuwepo.
Wa kuchukulia poa pia walikuwepo.
Tatizo lililodhaniwa na wengi kuwa litachukua muda mfupi likachukua nusu saa lisaa mara masaa. Kutoka saa mbili hadi saa sita kasoro ndipo tulipoondoka kwa basi la kukodishiwa.
Lakini katika kipindi hicho cha masaa takribani matatu nilijifunza jambo muhimu mno ambalo ndilo hasa chimbuko la makala yangu hii. Nilijifunza kumbe kuna tofauti kubwa kati ya MSAFIRI na ABIRIA tuwapo safarini.
Nianzie lilipoharibika basi....
Kwa kuwa sasa basi liliharibika na likazimwa engine AC pia ilizima. Kwa hiyo hali ya hewa ndani ya basi haikuwa rafiki sana. Wengi walifungua madirisha.
Binafsi niliamua kutoka nje ambako tayari kulikuwa na watu kadhaa wamekaa pembeni wengine kwenye miti nk. Lengo langu nitafute sehemu ya peke yangu nisome kitabu angalau kuliko kupoteza muda kulalamika tu kama everybody else. Muda ni mali au siyo?
Nimevaa cadet na shati na koti. Pembeni ya barabara kama mita 10 hivi kulikuwa na gogo kuna kijana mmoja tuliyekuwa naye kwenye basi wa miaka kama thelasini hivi nilivyomuona amevaa pensi na yeboyebo (zile wanavaa sana wachina) na tshirt na amevaa miwani ya jua amelala kwenye gogo moja kubwa lilikuwe mahali pale kama mtu anayeota jua. Amekaa kama vile alikuwa pale toka jana yake usiku.
Nilipomuana nikaona ni mtu tofauti sana na watu wengine wote waliokuwepo hasa kwa alivyovaa.
Nilisogea nikamsabahi akatoa miwani yake ya jua na kuining'iniza kichwani ili tuonane. Well tukateta mawili matatu (mi hupenda sana kusikia kutoka kwa watu wengine naamini ndo njia bora ya kujifunza)
So nikamuuliza:
"Unaelekea wapi kiongozi?"
Yeye: "Mwanza"
Mimi: (huku nikimuangalia juu hadi chini) Anhaa Okay mimi pia naelekea Mwanza. Unafanya kazi Mwanza?
Yeye: No naenda kutembea tu.
Mimi: Oh safi sana. Napenda kusafiri sana pia. Naelekea Mwanza pia japo naenda kibiashara na kumsalimia mama.
Yeye: Wewe huonekani kama MSAFIRI. Unaonekana kama ABIRIA tu.
(Dah jibu lake lilinifanya niwaze huyu jamaa amenionaje kwanza. Kwanza nimevaa vizuri kuliko yeye au hajioni? Na ina maana kusafiri kote huku nchi hii bado kaniona mshamba au??🤔)
Wakati naandaa cha kusema akaendelea. Na hapa ndo shule ilipo.
Yeye: Ndo maana sasa hivi kuna joto lakini umevaa vest na shati na koti na "moka" wakati siyo mazingira yake.
(Nilitamani nijiangalie juu hadi chini. Nikajikausha. Kiukweli jua lilikuwa linazidi kuwa kali na joto kuzidi kuongezeka. Lakini nilikuwa bado nimevaa koti. Well nikaona siyo tabu. Nikatoa koti nikaweka mkononi. Akacheka kidogo.
Yeye: Watu wengi unaowaona hapa nje wanalalamika ni kwa sababu ni ABIRIA. They are not TRAVELLERS. Maana wangekuwa wasafiri wangeweza kuwa na uzoefu nini kinaweza kutokea safarini na kikitokea ukiwa karibu na makazi ya watu ubehave vipi na ikiwa porini pia uta survive vipi au kwa ujumla tu ufanyeje kama huna solution.
Mimi: Aisee. That's very interesting. I guess sijawahi kuwaza haya mambo licha ya kusafiri kwa muda mrefu.
Yeye: No bro wewe hujasafiri kwa muda mrefu ila umekuwa ABIRIA kwa muda mrefu.
(Ulishawahi kumtazama mtu kwa jicho fulani hivi? Ilikuwa kidogo nimwangalie kwa hasira lakini desire ya kujifunza ilikuwa kubwa. Nikajikausha.
Ila dah. Yaani hilo neno liliingia akilini mwangu kwa nguvu utafikiri analigongelea kwa nyundo)
Yeye: Mtu akiwa abiria concern yake ni kufika anakoenda. Hapo katikati hata kitokee nini yeye anawaza KUFIKA TU wakati kumbe chenye maana ni ile SAFARI na siyo destination.
Dah! Yaani I was TRANSFIXED. Sikuwa naamini masikio yangu. Nikamuangalia tena nikakosa cha kumuuliza wala kumsemesha. Kuna nyakati akili yako huwa inajua kuwa sasa hapa niko DARASANI sitakiwi kujitingisha. Hii ni shule adimu. So niliamua kumpa attention yangu yote.
Akakaa vizuri kwenye gogo lile akaendelea....
Yeye: Kwa mfano hii safari yetu imesimama hapa. Lakini watu wengi wanalalamika badala ya kushukuru Mungu kuwa wamepewa chance ya kuinteract ambayo wasingeipata kama basi lisingeharibika. Hapa ndipo kuna connection muhimu za baadhi yao. Hapa ndo kuna muda wa kutafakari mambo muhimu kwa baadhi yao lakini wengi wanalalamika tu. Why? Kwa sababu ni ABIRIA siyo WASAFIRI.
(Wow! Nikasema huyu kijana naona yuko vizuri sana kichwani)
Akaendelea...
Yeye: Eneo hili tulilopo sasa hivi huu ni ukanda wa wanyama kupita kutoka Mikumi kuelekea mpaka Saadani. Kila baada ya miaka kadhaa huwa wanyama wanapita maeneo haya haya na kwenda mbuga zingine. Na zamani kabla ya barabara hizi na kabla ya watu kujenga makazi eneo hili lilikuwa na wanyama wengi wakipita.
::::::::::::::::::::::::::::::::
Kwa kifupi alinieleza kuhusu wanyama ambayo nilikuwa sijui. Alinieleza mambo mengi kuhusu safari na wasafiri na kuhusu abiria na siku nyingi sana zimepita baada ya safari ile lakini mambo niliyojifunza hayajapita kabisa.
Alinifanya nikajifunze upya kuhusu tofauti ya msafiri na ABIRIA na nimekuandalia tofauti chache kati yao kama ifuatavyo:
1. ABIRIA ANATAMANI KUFIKA TU MSAFIRI ANATAMANI HATA SAFARI ISIISHE JAPO ANAJIKUTA INAISHA TU AFANYEJE
Anachotaka ABIRIA ni KUFIKA tu. Mengine yote ni usumbufu kwake na upotezaji wa muda. MSAFIRI pia anataka kufika lakini awe ameifurahia safari yake hapo katikati.
Ujiangalie pia katika maisha. Je wewe unatamani tu KUFIKA? Unatamani tu kumaliza shule, au kupata degree. Au kuoa/kuolewa. Au kufanikiwa. Ila mchakato hapo katikati unaona usumbufu. Binafsi ninakutana na watu wengi katika kufundisha kwangu ujasiriamali lakini wengi wanataka tu kupata pesa basi. Process hawataki. Usije kwenye ulimwengu wa biashara kama ABIRIA. No. Be a traveller. Mchakato ndo muhimu. Siyo mamilioni utakayopata.
So wewe je ni MSAFIRI au ABIRIA?
Unatamani chuo kiishe tu upate degree au pia unaenjoy hayo maisha yako ya chuoni?
Unatamani tu upate ajira au unaenjoy interviews unatamani hata isingeisha? Ndo utajijua wewe ni abiria au msafiri. Ukienda ibadani unatamani iishe uondoke au ikiisha unasema dah imeishajeishaje hii kitu.
Kwa ABIRIA kuchelewa kufika ni usumbufu au mkosi lakini kwa msafiri kuchelewa kufika ni sehemu ya safari. Wasikilize watu waliochelewa kufika Moshi wakati wa Christmas utajua nachosema kulingana na wanavyosimulia.
Ndivyo ilivyo.
Mtu anaanza biashara akichelewa kufanikiwa anaacha. Huyo ni ABIRIA. Msafiri ataona hiyo ni sehemu ya kuyafikia mafanikio yake.
Wewe una mindset ipi?
2. ABIRIA HUBEBA KILA KITU LAKINI MSAFIRI HUBEBA VICHACHE TU VYA MAANA
Again. Ukikumbuka story yangu niliposafiri nilibeba mpaka mashuka taulo nk. Seriously??? Lol.
Ndivyo ilivyo kwa wengi wetu. Tumekuwa ABIRIA for a long time maishani. Abiria atabeba mabegi mawili, simu mbili, chaja, powerbank, nguo kibao, laptop, viatu tofauti tofauti, pesa taslimu tena nyingi, na nyingine nyingi kwenye MPESA, kadi za benki, nk.
Ndugu yangu unaenda Mwanza au sayari ya Mars?? Ulishaona movie ya *Coming To America* jinsi Eddie Murphy na msaidizi wake walivyotua Marekani na rundo la mabegi meeengi na kwanza yote yalipotea (stolen).
Lakini msafiri hubeba vitu muhimu tu. Tena vichache. Camera. Nguo chache mno. Taulo la nini wakati anaweza kupata huko aendako na asipopata poa tu atakauka tu hata iweje. See?
Hawa watu watatumia fedha kiwango tofauti sana.
Sasa katika maisha tuna a lot of baggages tumejifunza nyumbani, shuleni na kwenye jamii. Ukiishi maisha yako umebeba hizo baggage zooote kama kina Eddie Murphy utaingia gharama nyingi sana na stress zisizo na msingi kwa sababu you are moving with things you don't need. Watu wengi wamejaza vitu unnecessary vichwani mwao. Sasa lazima tu uchelewe kufika unakotaka kimaisha maana unarudishwa nyuma na mzigo mkuubwa wa vitu ambavyo havihitajiki katika safari ya mafanikio yako.
Mwaka jana 2017 July niliandika makala fupi kuwa ukimwambia Bakhressa kuwa MIHOGO ni biashara kubwa atakuita boardroom muongee vizuri. Wakati ukimwambia mtu msomi na elimu zake atakwambia hiyo achana nayo. Kwa sababu msomi amebeba mawazo ya vitabuni yooote kama yalivyo. Bakhressa hana hiyo mizigo so ukimpa idea kichwa inaichuja haraka kuliko msomi ambaye yeye anataka idea yako ieandane kwanza na definitions alizosoma kitabuni.
Be a traveller!! Acha kubeba "mataulo na mashuka na maviatu na mahela" nk. Namaanisha acha kutembea na mawazo yasiyokusaidia sana. Unayo tu. Vitu vingi tulivyojifunza maishani havitusaidii zaidi ya kuwa mzigo tu kwetu. Jiulize mambo uliyojifunza toka chekechea hadi labda degree mangapi unayahitaji ili kutimiza kusudi la kuishi kwako? Be a traveller. Ndiyo maana vitu alivyofanya Yesu viliandikwa vichache vya MUHIMU.
3. IKITOKEA SHIDA CHA KWANZA KWA ABIRIA NI KULALAMIKA CHA KWANZA KWA MSAFIRI NI KUJIFUNZA NI NINI KIMETOKEA (KWA USAHIHI WAKE) NA YEYE ANAWEZAJE KUWA SEHEMU YA SULUHISHO IF POSSIBLE
Katika maisha ndivyo ilivyo pia. Ikitokea shida katika ndoa mwanandoa ambaye ni abiria tu ataanza kwa kulalamika. Lakini ambaye ndoa kwake ni safari ataanza kwa kujiuliza WHAT HAPPENED, WHY EXACTLY and WHAT TO DO.
Katika masomo hivyo hivyo. Ukifeli ukalalamikia Waziri au NACTE au lecturer, wewe ni abiria. Jiulize why umefeli kiukweliukweli. Then tafuta solution ya *kiukweliukweli.*
Biashara ikiwa ngumu jiulize why kwako imekuwa NGUMU. What exactly is the reason. Then how can you fix it.
Umekosa mkopo chuo cha kwanza ni nini kulalamika? Au kufikiria why exactly umekosa kwanza. Hao waliokunyima mkopo ni kama basi lililoharibika njiani. Tuna assume hutabaki hapo milele. But sasa while uko hapo unajifunza nini? TRAVELLERS NEVER COMPLAIN.. IF YOU DO YOU ARE NOT A TRAVELLER.
4. ABIRIA HUJIPIGA PICHA YEYE LAKINI MSAFIRI HUPIGA PICHA MATUKIO.
Wengi wetu tumekuzwa kama abiria. Ni jukumu lako kujifunza kuwa msafiri badala ya kulalamikia ulivyokuzwa.
Kwa kifupi abiria akiwa hata kwenye ndege angani atajipiga picha kwenye ndege. Lakini msafiri atapiga picha za matukio. Msafiri anaamini zaidi kuwa kumbukumbu nzuri zaidi ni matukio na siyo sura yake. Mfano abiria atapiga selfie akiwa kwenye basi au ndege
lakini muda huo huo jua linachomoza au kuzama lina mwanga fulani mzuri abiria haoni kabisa hilo tukio ila msafiri hawezi kumiss hilo tukio.
Akienda mbuga za wanyama abiria utamjua tu hata alivyovaa hafanani kama yuko mbugani. Lakini hata picha abiria atajipiga picha nyingi za yeye akiwa mbugani kuliko alichokikuta mbugani.
Katika maisha ni hivyo hivyo. Unapitia moments nyingi hapo shuleni au nyumbani au kazini au katika biashara yako. Weka rekodi ya matukio muhimu siyo kingine.
Abiria hata notebook hana lakini msafiri ana JOURNAL.
Unakutana na watu wengi kila siku. Je kichwani mwako inabaki kumbukumbu ya sura za watu au tukio lililotokea. Kumbuka kinachokufundisha ni tukio siyo sura ya mtu.
Weka rekodi za matukio muhimu. Ni tukio gani muhimu katika biashara yako. Usipige picha tu uko ofisini unakunywa chai. Piga matukio muhimu pia kama lift imekwama, nk. Utajifunza katika hayo kuliko chai ambayo mchana tu ushaisahau.
Ulishawahi kuona mtu akienda nje ya nchi. Picha nyingi anapiga kwenye vitu common. Huyo ni abiria. Msafiri ni mtu ambaye mindset yake ni katika vitu vipya. Hata akipiga picha katika sehemu common ataipiga kitofauti sana na huenda sura yake isiwepo.
Abiria hupenda kupiga picha na watu maarufu. Lakini msafiri hupenda #kukutana na watu maarufu hata wasipopiga picha. Ukikutana na Dewji muhimu ni nini kwako: Picha ya ukumbusho au kitu ulichojifunza kwake?
Watu wengi wamepoteza fursa muhimu kwa sababu ya kung'ang'ana kupata selfie na Mengi badala ya kukaa pembeni umuulize kitu ambacho jibu lake litafungua njia yako even wider.
Kupiga picha na Bill Gates ni nzuri lakini je ndicho unachohitaji ili ufanikiwe kimaisha? Yeye alifanikiwa kwa kupiga picha na watu maarufu kwani?
Abiria anachotaka ni akifika awe na sura yake kwenye picha zaidi ya 20 alizopiga. Msafiri anataka akifika ana picha 20 pia lakini ni za matukio muhimu yaliyojiri safarini.
Be a traveller.
5. ABIRIA HATAKI KITU KIPYA.... LAKINI MSAFIRI ANAKITAMANI
Hili ndo limewashinda wengi wanaojaribu kufanikiwa wakiwa na mindset ya ABIRIA.
Abiria akikuta kuna njia mpya tofauti na aliyoizoea anaona usumbufu. Msafiri ndo hufungua macho ili aone mambo mapya. Na ajifunze.
Ukiwa abiria hata serikali ikianzisha utaratibu fulani wewe unataka mambo yawe kama yalivyokuwa siku zote. Hauko open-minded kujifunza mambo kwanza uyaelewe. Kanisani wakiweka utaratibu mpya unaona usumbufu hata nyumbani mzazi akiweka utaratibu mpya unaona usumbufu. Kina Ben Carson walizoea wakitoka shule ni kucheza, kuangalia TV na kula afu ndo homework. Mama yao akabadilisha gia. Akasema kuanzia sasa ni homework kwanza kisha kucheza, kisha ndo TV tena TV ni mara mbili tu kwa wiki. Tena mtaangalia vipindi nitakavyochagua mimi viwili tu wiki nzima. Weeeee! Mbona ilikuwa shughuli. Lakini fast forward miaka mingi sana baadaye sasa hivi Ben Carson ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miji huko Marekani!!
Hajawa waziri kwa kuachwa kuangalia TV bali kwa kunyimwa huo uhuru. Kwa kulazimishwa kuwa MSAFIRI badala ya kuachwa kuwa ABIRIA tu kama wengine.
Nimejifunza kuwa watu wanaofanikiwa ni watu wenye kupenda kujifunza vitu vipya. Siyo lazima wavifanye no. Ila wanajifunza tu. Lakini wakiona vinaanufaa wanajaribu na mwisho wanafanikiwa sana. Yani ukija na idea mpya anakwambia njoo tuongee nikusikilize. Kisha ataamua baada ya kukusikiliza.
Lakini mtu mwenye mindset ya kiabiria abiria atakwambia NO usije. Niko busy. Sina muda. Nk. Anabaki na level ya ufahamu aliyonayo. Anajua barabara ya zamani tu. Basi likichepuka kupita njia mpya anasinzia. Waulize madereva taxi wa zamani jinsi ambavyo walikataa kujifunza kuhusu vitu kama UBER na TAXIFY na kuviona kama usumbufu na uone sasa hivi walivyoanza kuelewa dunia inakoelekea.
Usiwe ABIRIA. Utakosa vingi maishani. Kijana mwenzetu Diamond angekuwa na akili za kiabiria (passenger mindset) asingekubali kujaribisha perfume wala karanga.
Kwanza angesema "Niko busy saivi hiyo idea ngoja kwanza nimalize album hii inayokuja". But unadhani wasanii wengine waliomtangulia kupata pesa unadhani hawakupewa ideas kama hizo? Walipewa. But labda walizidharau.
Wakawa na mindset za passenger tu. Leo wamepotea.
"Professa Jay" alipopewa idea ya kuingia siasa akaona ajaribu. Huyo hapo anasema mwenyewe anaongoza binadamu na wanyama.
Anyway point ni kuwa alikuwa na mindset ya TRAVELLER. Wanamuziki waliobaki na mindset za kipassenger huenda wakaja kupotea kabisa.
Mtazame P. DIDDY. Traveller huyo siyo passenger. Anaskiliza idea mpya. And look wapi yupo sasa.
Kama unataka kufanikiwa na idea mpya hutaki hata kusikiliza tu ujue UNAJIDANGANYA. Usiamini maneno yangu. Fanya utafiti wako kuhusu wote waliofanikiwa uone kama walijataa kusikia idea mpya na ngeni.
So lazima ujifunze hilo pia. Usikariri barabara. Kuwa tayari ku explore new arenas. Hilo nalo ni tofauti kubwa kati ya MSAFIRI na ABIRIA.
Wewe ni yupi kati ya hao?
:::::::::::::::::::::::::::::::::::
Yako mambo mengi mno niliyojifunza kuhusu tofauti ya mtu ambaye ameishi kama ABIRIA na yule anayeishi kama MSAFIRI.
Nimeshea na wewe hayo machache niliyoona yanaweza kukufaa pia.
Toka nisafiri na huyo kijana aitwaye MATHIAS SAGUTI (instagram @mathias_cyclist_official_page)
Namshukuru Mungu kila siku kunikutanisha na watu walionifanya kuzidi kujua vitu vipya vya manufaa.
Nakuombea wewe pia ya kwamba maandishi haya yasikuache jinsi yalivyokukuta.
Nikushukuru kusoma mpaka hapa. Kama umejifunza chochote cha kukufaa nitafurahi kusikia kwenye comment section.
Barikiwa sana!
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255788366511
*MWISHO*
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::