Wakati nikiwa mtoto mdogo kuna siku nilikuwa naimba wimbo ule wa "NGAPULILA". Niko zangu naimba kwa hisia kweli kweli. Baadhi ya maneno nakumbuka ni haya......
"Rafiki yangu nakuaga mimi oooh,
Nataka kuzamia meli kwenda ng'ambo
Kutafuta maisha eeh, kwani naona maisha ya hapa nyumbani kaka eeh
Yamenishinda
Nakula kwa tabu,
Navaa kwa tabu eeh
Maisha yangu ghetto...
Kulala kwangu ghetto...
Basi naona shida tupu eeh
Shida tupe eeeh
Sina raha maskini mimi ooh
Sina raha hata kidogo,
Ngapulila..."
Wanaoujua watakumbuka lyrics kwa usahihi zaidi. Nachokumbuka ni mama aliposikia nikiimba ALIHUZUNIKA sana. Akaniambia nisiuimbe tena kwa sababu sisi hatuishi GHETTO (tulikuwa tu naishi kijijini lakini nyumba nzuri kwa kweli) na akasema wala sisi siyo MASIKINI (kwa kweli hatukuwa na tatizo la chakula au mavazi yani zile basic needs). Lakini mimi nilikuwa nikiimba huo wimbo nilikuwa naimba kwa hisia kali sababu nilikuwa najiona kuwa ile nyumba tuliyokuwa tukiishi haikuwa ya kitajiri na huenda ndo ghetto yenyewe ya kwenye redio hiyo. (Na kiukweli nilikuja kuelewa vizuri maana ya neno "ghetto" baadaye sana baada ya kuja jijini Daslam na kuzunguka zunguka)😊
Kumbe sikujua kuwa FIKRA zangu nilikuwa nimesharuhusu watu wengine ikiwemo wanamuziki kuziteka na ku-paint picha fulani ambayo ilikuwa imeshanikaa kichwani na kuanza kuwaza na mimi siku nitoke kijijini nifike huko "NG'AMBO".
Mentor wangu anaita hii kitu "MIND CONTROLLING MIND". Yaani kuruhusu fikra za mtu au kitu kingine kuwa ndo fikra zako na ukaziamini kuliko zile ulizokuwa nazo na ukaanza ku-act accordingly.
Hii ni hatari kuliko HYDROGEN BOMB ambazo North Korea wanatamba kuwa wanazo!
Kupokwa fikra zako ni hatari kwa sababu kiuhalisia na hata kisayansi binadamu ndiye kiumbe pekee chenye uwezo wa KIFIKRA. Wakakipa hiki kiumbe (binadamu) jina lilalofanania hali hii wakakiita HOMO SAPIENS. Yaani Man (or Animal) Capable of Thought.
Kwa hiyo kuishi kwa FIKRA za wengine ni sawa na kuwa USELESS tu. NA ukishauvaa uhalisia wa kuwa USELESS unaweza kuwa una maisha sahihi kwako lakini ukayaona kana kwamba ni tatizo kubwa kweli kweli kwa sababu si wewe unayewaza bali ni mwingine ndani ya kichwa chako. Na kukubadilisha hadi upate fikra sahihi tena itakuchukua muda mrefu pengine maisha yako yote yaliyobakia.
Nitatumia mfano wa Adamu na Hawa kukuonyesha jinsi gani FIKRA za mtu huvurugwa taratibu taratibu..yani huwa siyo ghafla. Wanaovuruga FIKRA zako huanza taratibu kwa njia na mbinu ambazo si rahisi kuzijua.
Ukipokwa FIKRA itahitaji mtu mwingine akuelekeze na kukuonyesha kuwa tayari FIKRA ulizo nazo ni TATIZO kubwa tayari!
Hii ndiyo maana Mungu alimuuliza Adamu hilo swali maarufu:
"NI NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA U UCHI?"
"WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?"
Swali hilo halikuwa jepesi tu. Wala halikuwa surprise kwa upande wa Mungu? Ila Mungu aliliuliza ili kumsaidia Adam (na mkewe) kujua kuwa FIKRA zao zilikuwa zimeshabadilika na kuwa kitu kingine kabisa.
Why?
Kwa sababu Adam na Eva walikuwa UCHI siku zote toka walipoumbwa lakini hawakuwahi kuona kama ni kitu kibaya. In a way Mungu aliwaumba uchi akijua kuwa endapo wataasi maagizo yake na kuruhusu FIKRA mpya potofu vichwani mwao basi wataanza kuona vitu vya kawaida ambavyo ni vizuri wataanza kuviona ni vibaya including kuwa kwao uchi.
Kumbuka Mungu alipomaliza kuumba aliona kila alichoumba (ikiwemo kuwaumba wao wakiwa UCHI) ya kwamba NI CHEMA SANA. (Mwanzo 1:31) Fikra sahihi ni kwamba Mungu kuwaumba wakiwa UCHI siyo tu ilikuwa jambo jema bali lililuwa jambo JEMA SANA.
Na kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (likeliness) basi na FIKRA original za mwanadamu ziliona ilikuwa sawa tu kuwa UCHI kama FIKRA za Mungu zilivyoona. Kitabu kinasema walikuwa UCHI lakini HAWAKUONA HAYA (Mwanzo 2:25)
Umenielewa right?
Tuendelee sasa...
ENTER THE DEVIL
Shetani alipoingia alijua ili kubadili maisha ya mwanadamu kama MTAWALA KWA NIABA YA MUNGU ilibidi kuvuruga FIKRA za huyo mwanadamu. Katika kuvizia kwake kwa muda mrefu alipoona fursa ya kutest zali lake alienda STRAIGHT kwenye maneno yatakayovuruga FIKRA. Na atakuwa alistudy maisha ya hao wapenzi wawili na kugundua nani alikuwa akiongea mwenzake anasikiliza. (Adamu)
Nani alikuwa mgumu kutest zali kwake (Adamu).
Nani alikuwa na sauti inayoweza kufanya mwingine alainike na kusahau kila kitu ndani ya sekunde chache?
Hapa jibu ni HAWA.
Shetani alipoona Hawa akiwa peke yake hakupoteza muda:
"Eti Mungu alisema msile matunda ya miti yote ya bustani?"
First trick hiyo. Kuuliza swali ambalo linaonekana kama la chekechea. Jifunze kuogopa mtu mzima kukuuliza swali la kitoto au la kijinga. Nawaza tu kwamba Hawa wa watu huenda alijicheka kimoyomoyo kwa swali la "kijinga" kama hilo (Matunda yote? Sasa tutaishije na sisi bado "vegans". Si bora tungekuwa walau "vegetarians") Nimewaza tu.
So aliyeuliza na aliyeulizwa wote wanajua hiyo si kweli.
Unaweza kuwaza kwamba lakini Hawa naye si angesema tu "TOKA PEPO".
Wewe mwenyewe mtu akikuleteaga umbea mbona huwa hukemei😕 So siyo rahisi kiasi hicho.
Lakini pia ni kama zinaa. Unaambiwa KIMBIA ukijifanya kuexplain, au kushauri au kukemea utashangaa kitakachotokea.
Tambua pia kuwa HAWA alikuwa tayari VULNERABLE kwa kitendo cha kuwa peke yake bila wasiwasi wa kuwa mbali na mume. Separation.
Kumbuka pia fikra zako zikianza kuvurugwa si rahisi ukajua. So Hawa akajikuta anaendeleza mjadala na shetani... akaanza kuexplain pale akijua anaongea tu na SNAKE.
"Hapana... Ila (Mungu) alisema tusile WALA KUGUSA matunda ya mti ulio katikati ya bustani..." Kama vile haitoshi akavolunteer kuongeza jibu kwamba Mungu alisema wakigusa au kula WATAKUFA.
Shetani akapata dili. Kutoka kwenye swali la kijinga alipata jibu lenye AKILI
Kisha akatumia hilo jibu lenye akili KUVURUGA AKILI za Hawa na hatimaye Adamu.
"HAKYANANI HAMTAKUFA" yani hapo nime-imagine tu huo msisitizo wa shetani.
"HAKIKA HAMTAKUFA"
YOU SHALL NOT SURELY DIE.
Yaani anaongea kama mwenye AUTHORITY.
HAKIKA HAMTAKUFA. Ila ni kwamba..... (akazidi kuvuruga FIKRA za mama yetu zaidi)
"Mungu anajua MKILA:
1. Mtafumbuliwa macho
2. Mtakuwa kama Mungu
3. Mtajua MEMA
4. Na (mtajua) MABAYA pia
Sasa uone jambo moja hapa ambalo shetani hulitumia mpaka leo kuzidi kutumia watu wanaovuruga fikra zetu.
Shetani hakuongelea kabisa suala la KUGUSA matunda. Aliongelea tu KULA. Lakini maagizo ya Mungu yalikuwa siyo katazo la kula tu bali hata KUGUSA. Mtu anayeBADILI fikra zako hulazimisha fikra zako ziwaze mwisho tu.
Kitendo cha shetani kutoongelea kugusa kilimsahaulisha Hawa hilo kwa muda. Na yumkini alipoamua KUGUSA hakufa. Maana ili ule tunda ulitakiwa kulichuma (kugusa). Kitendo hicho huenda kilimwongezea Hawa nguvu kwenye IMANI MPYA POTOFU ya kuwa kumbe kweli huenda hawatakufa. Baada ya kugusa AKACHUMA. Kisha AKALA.
Hakufa.
Maagizo ya Mungu yalikuwa in plural. So kama Hawa hajafa logic ya kawaida ni kuwa hata mumewe hatakufa.
So Adamu akapewa. Akapokea. Yaani naye AKAGUSA. Hakufa.
Then AKALA.
BOOOOM!!!!!!
1. Wakafumbuliwa macho
2. Wakawa kama Mungu (kwa maana tu ya namba 3 na 4 hapa chini)
3. Waliendelea kujua mema
4. Wakajua na MABAYA pia.
Coz Mungu anajua mema na mabaya pia.
TATIZO:
Tatizo ni kwamba kwa kuchagua kumsikiliza shetani FIKRA zao zilibadilika kiasi kwamba yale ambayo mwanzoni waliyaona MEMA sasa yakawa mabaya kweli kweli. Kiasi kwamba kuwa kwao uchi kuliwasumbua kiasi cha kulazimika kuficha uchi wa kila mmoja wao for the first time! Na Mungu alipokuja wakaona AIBU kuonana naye wakiwa vile. Utukufu wa Mungu uliozoeleka ukawa hofu kwao. Zamani waliona mema tu now hata kuonana na Mungu kwa njia na hali ile ile kukawa kubaya.
"Nimeogopa kwa kuwa nilikuwa UCHI"
Like seriously? You've been naked all life! So WHO TOLD YOU NOW KWAMBA UKO UCHI?
Kwa maneno mengine NANI AMEKWAMBIA KUWA KUWA KWAKO UCHI NI ISSUE?
Kwa maneno mengine Adamu NANI AMECHAKACHUA FIKRA ZAKO?
NANI AMEKUFANYA UJIDHARAU HADI UJIFICHE?
So, my dear reader.....
NANI AMEKUJENGEA INFERIORITY COMPLEX YA KUJIONA HUFAI?
WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?
NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA WEWE NI MASKINI?
Na ni nani aliyekwambia kuwa NG'OMBE WA MASKINI HAZAI?
Unajua madhara ya kuamini hivyo?
Nani alitwambia SISI ni nchi maskini?
Na ni nani alisema sisi tupo DUNIA YA TATU? Nani alipima DUNIA na alikubaliana na nani kuwa hii sehemu tuliyopo sisi ni ya TATU?
Unajua ndo maana Bill Gates kaja ikawa story kubwa
wakati mimi au Reginald Mengi tukienda Marekani wenyeji wetu tu ndo watajua siyo taifa zima.
Hayo ndo MADHARA ya kuamini tuko dunia ya ngapi sijui.
WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?
Nani alikwambia kuwa kwa kuwa wewe ni ALBINO huwezi kuolewa? Au huwezi kuwa BALOZI.
Je umepima fikra za mwanasheria na Balozi Possi?
Nani aliyekupandikiza FIKRA kuwa ili uwe tajiri inabidi umchune binadamu mwenzako ngozi?
Unaona madhara ya kupokwa FIKRA?
Huna malengo, huna mipango, huna mentors, hujifunzi kwa wenye mafanikio sahihi, hushughulikii kukaa vizuri na akiyekuumba utaacha kuamini kuwa ngozi ya binadamu, au ya kakakuona au meno ya tembo au shamba la bangi ndo vitakupa utajiri?
Nani alikwambia kwa kuwa ulipata ujauzito kwa mazingira mabaya kabisa kwamba unapaswa KUJIUA KULIKO KUENDELEA KUMWONA AU KUMKUMBUKA HUYO MWANAUME?
Nani alikwambia kuwa unapaswa uondoke dunia hii kwa kuwa ulitendewa mabaya? Uliwahi kusikiliza story ya Oprah au Lissa Nichols?
Nani alikwambia kuwa wewe hufai kwa sababu ex boyfriend wako alikuacha?
Nani aliyekuambia ya kuwa wewe ni KILAZA?
Anajua THAMANI ya investment ambayo Mungu aliwekeza ndani yako? Kwa nini unakubali definitions za watu kuhusu wewe ndo ziwe uhalisia wa FIKRA zako?
Nani alikwambia huwezi kufanikiwa bila kusoma ELIMU YA JUU?
Unarisiti ili kuongeza ufahamu au ili kuprove kwa watu kuwa na wewe unaweza kufika Chuo Kikuu? Una prove ili iweje kama siyo INFERIORITY COMPLEX in you imekutafuna for years.
Who told you kuwa usipofika Chuo Kikuu huwezi kutoa mchango muhimu kwa jamii?
Nani aliyekwambia kuwa wewe ni mtupu kichwani, huna future, huna lolote, huna BAHATI. Ilikuwaje kwanza mpaka ukamsikiliza akiongea hadi amalize. Nani alikwambia kuwa huwezi kuanza biashara chini kabisa na ukaja kuwa zaidi ya wote uwaonao juu leo hii?
Nani alikufanya ushindwe kujiamini.
Ngoja nikupe siri. Angalia watu wa ACACIA. Walikula "tunda" kweli kinyume na maagizo. Lakini WALIKUJA. Hawakukimbia. Mtu mmoja akawaita "WANAUME". And rightly so. They didn't run away. Binafsi nimejifunza kweli kwao. When you've messed up clean your mess!
Ukitaka angalia siku walivyokuja.
In a pack. Like lions.
Confident.
Yaani mtu unamdai afu yuko very confident.
Well suited.
Nigel Chanakira hutumia pia neno "WELL-HEELED" yaani kiatu ambacho soli ni mpya haiko upande.
Kisafiii. Kipyaaaa!
Huyo ni mtu unayemdai anakuja hivyo. Si unaweza kumuogopa bure. No wonder kuna watu fulani walianza kusema "UNAONA WENZETU?". Wakaanza kuaminisha kundi kubwa kuwa "SISI HATUWEZI KUWASHINDA WENZETU SI UNAONA WALIVYOKUJA"
Hayo ndo madhara ya kuamini kuwa tuko inferior kwa "WENZETU". Fikra za kishetani kabisa. Fikra hizi ziliwahi kutetemesha taifa la Israeli wakati wa Musa. Taifa likaambiwa professionals walijiona panzi mbele ya MAJITU. Hivi professional anayeaminika akijiona panzi mbele ya adui mtu wa kawaida atawaza nini?
Hapo ndipo Mungu alipowaza kuwafutilia mbali taifa zima na kuanza na Musa upya (Hesabu 14:11,12). Acha kabisa kupandikiza hofu ndani ya watu. Wanaweza kujawa hofu wakamkosea hadi Mungu kisha akawaadhibu kwa jinsi ambayo hawakuwahi kuona. Kwani Mungu anashindwa nini kuwazungusha jangwani miaka mingi zaidi. Anashindwa nini kuruhusu lifisadi moja lije kuwa raisi na liirudishe nchi nyuma mpaka kizazi chote hiki kiishe kije kipya.
Umeelewa?
Fikra POTOFU ikipandikizwa ndani ya watu unaweza kuleta madhara ambayo hakuna aliyetarajia.
Na wewe usiruhusu mtu akupandikize fikra eti hutafanikiwa kwa sababu ya SERIKALI au kwa sababu ya Richmond. Mafanikio YAKO ni WAJIBU WAKO.
Jenga fikra sahihi tu.
Usipoangalia FIKRA zako na kuzichunga utashangaa kumbe siku nyingi mno ushapokwa fikra. Ndo maana mtu akisema HAKUNA AJIRA unaamini. Kakwambia nani?
Sikia nikwambie mimi nilipata AJIRA yangu ya kwanza bila experience yoyote na kampuni ilibuni AJIRA hiyo baada ya mimi kwenda interview na kukosa nafasi sababu kuna vigezo sikuwa navyo LAKINI kwa jinsi nilivyojiamini na kujieleza jopo la wa wasaili lilishawishi uongozi utengeneze NAFASI ambayo HAIKUWAHI kuwepo kwenye hiyo kampuni ili tu nisikosekane pale. Sijisifii. Nakupa uhalisia.
AJIRA ZIPO.
Tafuta kama ndicho unachotaka ukikosa ujue siyo kwa kuwa hazipo. Nakupa siri ukienda interview nenda kama ACACIA WALIVYOKUJA!
Nani alikuambia huwezi kuanza biashara yako kwa kuwa huna MTAJI. Unakaa tu kisa "huna mtaji". Nani alikwambia mtaji ni pesa?
Fikra hizo umezitoa wapi. Zimekufanya uwe mpole na mnyonge bure tu.
Nani alikuambia kuwa UKISOMA LAW au ENGINEERING ndo DILI.
Nani amekuambia kuwa HAKUNA HELA MTAANI?
Are you sure hizo fikra hazileti uhalisia huo maishani mwako?
Are you sure fikra hizo haziui creativity yako yako na moyo wa kujituma zaidi?
Niliwahi kusema ukiona wewe huoni hela ila wengine wanaziona ujue tatizo siyo pesa ila ni macho yako.
Nani alikwambia MAISHA NI MAGUMU?
Alikwambia ili iweje?
Unaamini hivyo pia?
Una HAKIKA maisha ya kila mtu ni magumu nchi nzima?
Nani alikwambia Hutakuja kufanikiwa? Why uruhusu fikra zake ziwe ndo fikra zako mpya na unaziamini na kujiona USELESS mpaka fursa za mafanikio unajificha. Ukiitwa kuambiwa kitu cha kukusaidia huendi kwa kuwa umeshajiona HUWEZI.
Nani ALIYEKUAMBIA kuwa huwezi?
Nani aliyekuambia kwa kuwa biashara yako imeyumba basi haitasimama tena kwa hiyo bora ukaajiriwe tu yaishe?
Nani ALIYEKUAMBIA kuwa hutoweza kusimama tena?
Tenda zikitoka unaogopa kujaribu.
Unajificha kwa kuwa "U UCHI"
WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?
Kubadilisha fikra za Adamu ililazimu sasa ahamishwe mazingira kabisa aende nje ya bustani akajitafutie... ili fikra sahihi zirudi ilibidi asile vilivyopandwa na mwingine bali apande vya kwake upya.
Ili fikra sahihi ziwarejee waIsraeli ilibidi wazunguke jangwani miaka 40.
Nilisema madhara ya kuruhusu FIKRA ZAKO zishikiliwe na wengine ni makubwa kuliko mlipuko wa HYDROGEN BOMB.
Jifunze kujenga FIKRA SAHIHI na utayafikia yale muumba wako aliyokusudia uyafikie kwa WAKATI.
USISEME KAMWE KUWA MIMI SINA HIKI, SINA ELIMU, SINA MTAJI, SINA CONNECTION, SINA MARAFIKI, SINA KIPAJI KAMA CHA FULANI, SINA KWANGU, yote hayo na mengine kama hayo ndo fikra potofu ya "NIKO UCHI".
NANI ALIKWAMBIA KUWA U UCHI?
WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?
Barikiwa sana!
#ThreeSixteen
Semper Fi,
Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511
www.andreamuhozya.blogspot.com
Ijumaa, 18 Agosti 2017
Ijumaa, 28 Julai 2017
UNATAKA KUFANIKIWA? JIFUNZE KUWAAMBIA WATU NENO HILI: "USINITINGISHE TAFADHALI"
"USINITINGISHE TAFADHALI"
Hakika Mungu ni mwema na nina kila sababu ya kumshukuru sana. Wewe pia mshukuru the Mungu.
Leo ninataka kukukumbusha mojawapo ya maneno mengi mno ambayo yatakusaidia kufikia malengo yako. Nalo ni kujifunza kuwaambia watu "WASIKUTINGISHE".
Wakati naanza biashara ninayofanya sasa hivi sikutegemea kupata upinzani mkubwa kiasi hicho kutoka kwa watu wangu wa karibu. Nilidhani kuwa kila mtu ataelewa tu kuwa ni maamuzi sahihi kama nilivyokuwa nikiona mimi. Lakini haikuwa hivyo.
Nilipata upinzani kutoka kila kona. Kuanzia kwa my love wangu my ubavu wangu. Ndugu zangu. Marafiki. Nk. Kuchekwa, kukejeliwa, nk. Lakini kanuni moja ambayo imenifanya nisimame na hii biashara mpaka leo ni kwamba nilijifunza jambo fulani utotoni ambalo limekuwa msaada kwangu mpaka sasa.
Wakati tuko shule ya msingi nilipenda sana kuchora na pia kwa sisi wa zamani zamani (eti mmeanza kutuita wahenga) tulikuwa tunafundishwa somo la MWANDIKO!
Bahati mbaya sana kwa sababu ya uhaba wa madawati dawati moja dogo tulikuwa tunakaa wanafunzi watatu hadi wanne.
Kwa hiyo ufanisi wa somo hilo la mwandiko na lile la kuchora (sanaa) ulitegemea sana mtu asikutingishe wala asikuguseguse wala asitingishe dawati!
Kwa sababu nilipenda sana kupata MWANDIKO au mchoro ambao ni PERFECT nilikuwa na-mind sana sana mtu akinitingisha hata kidogo tu. Kwa hiyo nikikaa tu kidogo nasema "USINITINGISHE". Mbaya zaidi kuna "mamtu" class yalikuwa yamebarikiwa yana mwandiko mzuri hadi raha. Afu na mimi nataka nipate mwandiko wa ukweli afu mtu mara anabadili mkao wake keshakutingisha. Dah! Ilikuwa inaniumiza kweli. Halafu unakuta mtu haoni kwa nini unahangaikia mwandiko tu ndo unakasirika hivyo!
Mwandiko tu? Kumbe wewe huoni ni mwandiko tu. Unaona SUCCESS, PRESTIGE, REPUTATION, etc.
Leo naona mwandiko wangu si mbaya sana (licha ya kutingishwatingishwa)
Yes.
Kwa hiyo wakati naanza biashara hali ya watu wengi kutokubali ninachofanya niliiona kama "KUNITINGISHA". Na kiukweli sikuwa tayari kuona ninatingishwa wakati nahitaji CONCENTRATION.
Sikumwambia mtu yeyote neno hilo lakini moyoni mwangu na mawazoni mwangu lilijaa. USINITINGISHE TAFADHALI! MSINITINGISHE TAFADHALI!
Nimekuja kuona kuwa watu wote waliofanikiwa katika kitu fulani waliamua kukataa KUTINGISHWA.
Ukiweka huo msimamo hutaeleweka vizuri. Maana wengine hukupinga kwa nia njema. Lakini kama Donald Trump angesikiliza ripoti za CNN na BBC asingefika hapo alipofika. Nakumbuka sana alivyochekwa na anavyochekwa hadi leo. Na kuitwa majina mengi. Kichwani mwake kulijaa na kumeendelea kujaa hilo neno: MSINITINGISHE TAFADHALI
Siyo kwamba hakwami au hakosei. Anakwama mara nyingi kuliko kawaida. Anakosea kweli mambo mengi lakini point ni kwamba hataki KUTINGISHWA wakati anafanya alichokwishaamua kufanya.
Kuna mmoja tunaye nchi hii yeye alisema HAJARIBIWI. Maana yake USINITINGISHE TAFADHALI. Na ukimtingisha mtu ALIYEDHAMIRIA kukataa kutingishwa basi utaelewa muda si mrefu.
Watu wote waliofanya kitu na kikawezekana waliweka hiyo attitude: USINITINGISHE TAFADHALI.
Kuna kitabu nilisoma cha kuhusu maisha ya Thomas Edison aliyegundua bulb hii tunayowasha leo.
Aliishi maisha yenye changamoto nyingi na vikwazo vingi. Lakini kichwani mwake ni kama aliiambia tu kila changamoto neno moja: USINITINGISHE TAFADHALI
Maisha ya Bill Gates na Paul Allen ni hivyo hivyo. Jeff Bezos. Jack Ma. Nk.
Yesu aliwahi KUTINGISHWA na mama mzazi kwenye harusi ya Kana huko Galilaya. Mama anasema: "HAWANA DIVAI". Jibu la Yesu kwa mama mzazi ni kama kumwambia tu "MAMA, USINITINGISHE TAFADHALI ".
Tunasoma pia Yesu akiambiwa na shetani "badilisha mawe yawe bread kama kweli wewe ni mwana wa Mungu" nk. Majibu ya Yesu yote kwa shetani yalikuwa kama kumwambia tu shetani: USINITINGISHE TAFADHALI!
Sijui unaelewa?
Ukitaka kufanikiwa na wewe ni mtu wa kuruhusu kila mtu tu akutingishe hutafanikiwa. You must STAY FOCUSED!
Mafanikio ya aina yoyote yale iwe ni unataka MWANDIKO mzuri au KUFAULU MITIHANI au unataka NDOA IMARA au unataka MAFANIKIO KIBIASHARA au unataka kutimiza ndoto na MAONO yako yanahitaji usiwe mtu wa KUTINGISHWATINGISHWA tu na kila mtu.
Kuna kijana mmoja amemaliza kidato cha sita nimekutana naye hivi juzi tu kupitia hii mitandao. Katika mazungumzo ananiambia anaomba ushauri. Anasema amefaulu mtihani wa Form VI ila kozi aliyotaka kusoma chuo ni PROCUREMENT... lakini watu "wamemtingisha" hadi wakamwambia akasomee mambo ya PLANNING eti ndo DILI. (Sijui wamejuaje) Lakini dogo akakubali lakini kwenda kumwambia "MZEE WAKE" akapinga sana anataka kijana wake akasomee PHARMACY kwamba ndo hatakosa AJIRA mbeleni.
Wamemtingisha dogo mpaka haelewi afanyeje sasa.
Hali hii huwakuta wengi. Unataka kuoa/kuolewa unaambiwa MBONA MAPEMA? Unataka kuanza biashara unaambiwa HEE, HIYO HUTATOKA BORA UFANYE HII. Hahaaaaa! Watingishaji ukiwapa nafasi utatingishika mpaka hutoamini kama ni wewe. Unataka kununua gari unaambiwa SI UJENGE KWANZA? Ukianza kujenga ukakwama wanasema si ungejenga chumba kimoja uhamie hivyo hivyo ndo watu wanaanzaga hivyo. See? Sasa utakuwa REMOTE CONTROLLED na watu hadi lini?
Sikia usichanganye kati ya USHAURI SAHIHI na KUTINGISHWA. Yesu alijua kuwa maneno ya mama yake kwa mama ilikuwa kama USHAURI lakini kwa yeye Yesu ilikuwa kama kuambiwa cha kufanya hasa ukiwa tayari unajua na unasubiri tu wakati muafaka. Mind ya Yesu ilikuwa VERY FOCUSED kwenye huo wakati muafaka aliokuwa akisubiri kiasi kwamba hakutaka KUTINGISHWA kabisaa! "MAMA... SAA YANGU BADO!"
Yaani: USINITINGISHE TAFADHALI
What about you my friend?
Ukishafanya maamuzi fulani kuhusu maisha YAKO unataka mtu mwingine tena aseme nini.
Ngoja nikupe mfano mdogo:
Ukijipanga mstari na watu 10 wa mtaani kwako au familia yako halafu mkawekewa magari 10 tofauti tofauti mbele yenu kila mmoja wenu achague la kwake:
Range Rover,
Jeep Cherokee,
Toyota VX,
Vitz,
Mercedes Benz,
FUSO,
Canter,
Rav 4
BMW
DCM
Wewe utachagua lipi?
Na je unadhani utakalochagua uchaguzi wako ndo sahihi au mbovu kuliko wa wengine? Yani unadhani ukichagua Range mwenzako akachagua FUSO ndo akuone wewe chizi eti kisa kwa nini hukuchagua gari ya kubebea mizigo?? Kwani kila mtu anataka kubeba mizigo? Kwani hujui kuna watu wana Range na zinawaingizia pesa kuliko wenye FUSO. Na kuna watu wana FUSO wana hela kuliko mwenye Range. Au kama ulichagua Benz afu mwenzako akachagua VX akucheke kwa nini umechagua gari la chini badala ya kuchukua la juu. Kwani kila mtu anataka gari kubwa dunia hii? Sasa na wewe unaanza kujilaumu eti ayaa bora ningechagua VX.
Utakuwa hujielewi bado.
Choices zako na decisions zako kama mtu mzima unapaswa kuzisimamia. Ukikosea si unajifunza tu. Kwani mbona Rais anateua Waziri halafu anagundua baadaye kumbe alikosea au kumbe. Anabadilisha. And life GOES ON.
Jifunze kukataa KUTINGISHWA. Utafika mbali sana sana.
Mimi nimejifunza hilo. Ndo nikaona nikushirikishe na wewe pia. USITINGISHWETINGISHWE
Na wala USINITINGISHE TAFADHALI.
Barikiwa
#ThreeSixteen
Semper Fi,
Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp +255 788 366 511
Jumatatu, 17 Julai 2017
HAKUNA MTU ASIYEWEZA KUFANIKIWA KIUCHUMI #AKIAMUA
HAKUNA MTU ASIYEWEZA KUFANIKIWA KIUCHUMI AKIAMUA
Siku kadhaa zilizopita nilikutana na hawa kina dada wawili mtaani (mitaa ya Sinza) wakiwa wamepumzika baada ya kazi kubwa ya kutembeza mboga za majani mtaani.
Walikuwa wamechoka hakika na walikuwa wamekaa mahali dukani wakiwa wameagiza zao soda baridi kushushia kidogo na labda kulainisha koo kwa sababu ya kazi nzito ya kutembea juani na huku ukiita kwa sauti: "Haya jamani mchicha, mnafu, matembele, mchichaaaaa".
Niliwasalimia na kukatisha safari yangu ili nikae nao pia ili niendelee kujifunza maisha ningali hapa duniani.
Ama baada ya salamu na maneno mawili matatu ya "Breaking the Ice" nikaanza kureason nao mambo ya biashara na hasa biashara yao.
Mimi:
Hebu niambieni nyinyi changamoto yenu hasa ni nini kwenye hii biashara?
Mmoja wao:
Dah kakangu changamoto ni nyingi mno lakini kubwa ni kwamba watu siku hizi wanaogopa kula mboga za majani si unasikia sijui serikali wanasema mboga zisilimwe sehemu za maji yenye sumu?
Mimi:
Oh poleni nimesikia sikia hivyo pia hasa kuhusu bonde la Msimbazi na Mlalakuwa. Kwani nyie mboga zenu mnatoa huko pia?
Wao:
Hapana sisi tunatoa huko Tegeta! Lakini bado wateja hawaamini wanaogopa tu kwa hiyo kwa kweli ni changamoto.
Mimi:
Sasa kama hali ndo hiyo mnajiandaaje mbeleni mfano serikali ikisema mboga mboga zisiuzwe mtaani ili kuepusha labda magonjwa ya mlipuko nyie mtafanya nini kwa kipindi hicho cha marufuku ya aina hiyo.
Wao:
Eeh kakangu sisi tunaomba tu yasifike huko maana humu ndo tunajipatia kipato chetu na kusaidia mambo ya familia yanaenda. Kwa hiyo serikali isifike huko watusaidie kwa hilo.
(Nikaona nibadili uelekeo wa maswali kidogo...)
Mimi:
Aisee. Kumbe biashara siyo mbaya ee. Safi sana. Kwani kwa mfano kwa kawaida kwa siku mnaweza kutengeneza faida ya shilingi ngapi?
Wao:
Kama siku ikiwa ngumu faida sh 25,000 hivi lakini ikiwa nzuri ni sh 45,000/- mpaka 50,000/- kwa siku!
(Hapo nikawaza upya kabisa. Maana average ya tuseme 35,000/- tu kwa siku 6 wanazofanya kazi ni sh 210,000 kwa wiki. Kwa mwezi ni kama Tshs 840,000/-. Usiwachukulie poa kivile ujue..)
So, Mimi:
Aisee, hongereni sana. Nimeipenda sana bidii yenu. Kumbe mambo siyo mabaya sana. Sasa mna mpango gani na kipato kikubwa sana namna hiyo ambacho mnaingiza kwa sasa? Mnasomesha?
Wao:
Tunashukuru serikali kwa shule za msingi sasa ni bure lakini tuna wa sekondari ndo humu humu tunapata kaka. Tunashukuru Mungu.
(Mmoja wao) mfano mimi mwanangu (akataja jina) anasoma tuition moja na watoto ambao wazazi wao wanafanya kazi kwenye mabenki na hata serikalini. Kwa kweli Tunashukuru. Ila ndo hela inaishia huko na matumizi mengine.
Mimi:
Hongera sana. Mnafanya mambo makubwa sana nyie hivi watoto wenu wanajua kwamba nyinyi mnatenda maajabu makubwa namna hii?
Wao:
(Wakacheka kidogo)
Ndiyo wanajua. (Mmoja wao) Wanajua tunavyohangaika mfano mimi mwanangu wa sekondari alirudi nyumbani juzi akaniuliza "Mama nasikia serikali inasema mboga mboga zina sumu, sasa mama wakiwakataza kuuza mi ntapata ada kweli?"
(Alikuwa emotional sana wakati akiongea hivyo so nikaona nikienda huko inaweza kumfanya hata alienda machozi.. si lengo langu for any reason)
Mimi:
Aisee. Sasa mnatamani watoto wenu waje wafanye kazi hii mnayoifanya nyinyi huko mbeleni?
Wao:
Eeh hata! Hii kazi ngumu tunawaambia watie bidii shuleni tu ili wasije wakafanya kazi hii. Migongo inatuuma tukirudi nyumbani, miguu, huku watu mara walalamike mboga zina sumu.
Mimi:
Mna muda gani na hii kazi?
Wao:
Miaka mingi kwa kweli. Zaidi ya tisa.
Mimi:
Wow! Sasa kama hamtaki watoto wenu waje wafanye hiki mnachofanya mmewaandalia akiba yoyote kifedha?
Wao:
Eeh kaka hivi hiyo akiba inatoka wapi hela yenyewe haitoshi ndugu yangu.
Mimi:
Mmesema mnaweza kupata mpaka elfu 45 nk. Sasa hivi unajua ukiweka tu akiba ya sh 5,000/- kila siku unajua kwa siku 10 itakuwa sh 50,000/-? Hiyo ni elfu 50 ambayo ipo tu. Na kwa siku 100 unajua ni sh 500,000/? Na unajua siku 100 ni sawa na miezi mitatu tu na siku 10?
(Nikaona kama "network inasearch kidogo". Nikaendelea kidogo)...
Mimi:
Hivi unajisikiaje dadangu ukiwa na ndugu yako kila baada ya miezi mitatu na siku 10 anakutumia laki 5? Unaweza kufanya mambo mangapi na laki 5?
Lakini mtegemea cha ndugu huwa anafanyaje dada zangu?
Wao:
Anakufa masikini kakangu.. (Kwa huzuni kidogo)
Mimi:
Sasa unaonaje ukajipa mwenyewe hiyo laki 5 kwa kutunza elfu 5 tu kwa siku hiyo elfu 5 ambayo haiathiri sana maisha yako kivile maana unabaki na kati ya elfu 20 hadi 40 kwa siku kwa sababu nyinyi mna uwezo wa kipato cha kila siku. Kati yenu yupo ambaye hawezi kuweka pembeni sh elfu 5?
Wao:
Kwa kweli hakuna..
Mimi:
Sasa TUSAHAU miaka tisa au hata miwili iliyopita. Tuangalie miwili au tisa ijayo. Kwa haraka haraka mwaka ukiisha utakuwa umeweka sh 1,500,000/- ya elfu tano tu ile nyingine unaendelea kutumia.
Baada ya miaka mitano tu una milioni 7,500,000. Fikiria miaka mitano iliyopita hadi sasa kuna milioni 7 na nusu ambayo hukuitunza kutoka kipato chako cha kila siku imepotea.
Mimi:
Ukipata milioni 7 na nusu ukaanza kuwakopesha wauzaji mboga wenzako unajua utakuza kipato chako mara dufu. Kuna Microfinance zilikuwa zinakopesha tu pesa lakini mpaka zimegeuka kuwa benki rasmi sasa (nikawatajia moja). Kumbe hata nyinyi mnaweza na biashara ya mboga unapumzika kabisa miaka mitano tu ijayo. Na mtoto aliyekuwa kidato cha pili hapo atakosa ada ya Chuo? Hata akipata mkopo nusu au robo tu utashindwa kumsaidia mahitaji mengine hapo juu?
Japo ni vizuri umsomeshe tu kwa pesa yako hiyo ya kuweka. Hivi unajua mzazi anayeshangilia mtoto wake kupata mkopo kwa upande mwingine anashangilia mtoto wake kuhitimu akiwa na deni kabla hata hajaanza kuingiza kipato? Watoto wa matajiri wanahitimu bila madeni. Wa maskini wanahitimu na madeni. Hiyo ndo tofauti mojawapo. Wanaanza maisha wakiwa level tofauti za kiuchumi. Ni vigumu waje kulingana baadaye.
Wao:
Dah kaka yani umetufanya tuone tumepoteza pesa hata kunywa hizi soda jamani. Yani tungeyajua haya zamani mbona tungekuwa mbali mno! Jamani bora hata ulipita na ukatusalimia tumejifunza mengi mno.
Mimi:
Usijali. Hatua zetu tukinuia mema huongozwa na Mungu. So tumshukuru Mungu tu dada zangu.
Wao:
Sasa tunaanzaje?
Mimi:
Kuna wataalamu wa mambo ya uwekaji akiba. Watu wa mabenki nk. Mkiwakosa niambieni nitawatafutia. Wao wanajua nini ufanye na hiyo sh 5,000 uiweke tu na huwezi kuitoa hadi muda mliokubaliana utimie. Cha msingi siyo hiyo elfu 5 bali ni #NIDHAMU. Hiyo nidhamu watoto wako wakiijifunza wakaibeba na elimu watakayokuwa nayo familia yako na kizazi chako baada yako hawataamini kuwa kuna muuza mboga mboga mitaani ndo chanzo cha wao kufanikiwa.
Cha msingi usijiangalie wewe. Focus kwenye kizazi chako baada yako. Fikiria hali itakuwaje ukiwa mzee na unaona watoto wako na wajukuu zako wamebeba nidhamu nzuri kabisa ya fedha ambayo uliianzisha wewe kwa kuuza mboga mboga na kuweka sh 5,000 tu kwa siku.
Fikiria utakavyokumbuka elfu 5 yako ya kwanza, fikiria inavyoonekana ndogo lakini ilivyobeba utajiri wa vizazi na vizazi.
Wao:
Dah aisee kaka asante Mungu akubariki sana. Yani tunaomba tuje tukae tena tumependa sana mafunzo yako.
Mimi:
Asanteni sana dada zangu aisee.
Mwenye duka (Mangi):
Aisee huwa unatoa semina wapi jamaangu? Maana naona una mambo mazu..! Mazuri aisee.
Mimi:
Nitakuja tuongee zaidi ngoja nawahi mahali maana hata hivyo nilitaka kuwasalimia tu hawa dada zangu.
Kina dada:
Basi tupige hata picha ya ukumbusho maana leo tumepata elimu nzuri sana.
(Mangi akawa mpigapicha kwa muda)
Nikawaaga na kuendelea na safari yangu.
Nitawatafuta tena hawa dada zangu nijue wanaendeleaje.....
Usidharau kipato chako....!
#ThreeSixteen
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
***The End.****

Jumatatu, 29 Mei 2017
KIPAWA CHAKO NA JINSI YA KUKITUMIA KUTIMIZA MALENGO YAKO KIUCHUMI
(MAKALA HII ILIANDIKWA MAY 30 2017)
Mungu aliweka kipawa ndani ya kila mmoja wetu. Ili usife njaa wala usife maskini.
Hata hivyo tunapozungumzia KIPAWA yaani TALENT watu wanachanganya sana mambo, wanaita tu KIPAJI.
Ndo utasikia kuna eti "SHULE ZA VIPAJI MAALUMU" wakati pale wanachomaanisha ni shule za watu waliopata maksi nyingi labda. Wameleta tafsiri mbovu ya hata hivyo "vipaji".
Tafsiri sahihi ya TALENT ni kitu kinachoitwa KARAMA. Yaani simply ni kitu cha ziada ambacho mtu anacho cha kipekee ambacho mara nyingi wengine hawana. Uwezo fulani alionao mtu wa kufanya jambo muhimu ambao watu wengine hawana. Kila binadamu ana cha kwake.
Hapa tunaweza kupata aina mbali mbali za VIPAWA au UWEZO WA KIPEKEE huo:
Mfano:
1. Kipawa cha Kuongea vizuri
(Orators wazuri wako hapa kama kina Mwalimu Nyerere. Yani akiongea mnapenda hadi uongeaji wake tu yani. Comedians wazuri na watangazaji kama kina Charles Hilary wako hapa. Yani anavyoongea tu unatamani kipindi chake kisiishe)
2. Kipawa cha Kuandika vizuri
(Ukisoma novel kama Windmills of the Gods ya SIDNEY SHELDON utaelewa maana ya kipawa cha kuandika.
Ana kitu cha kipekee akipewa "pen and paper". Mhe. January Makamba ni mmoja wapo watu miongoni mwetu ambao wana karama hii. Yani akiandika article inakuwa tu ya kipekee from title to conclusion. Huenda ndo maana alikuwa muandaaji wa speeches za Rais Kikwete. Karama. Kipawa. Kipaji)
3. Kipawa cha Uongozi
Unajua watu kama Gandhi?
Yes. Yani anaweza kufanya wananchi wakubali kulala kwenye reli ili kuzuia treni la mkoloni lisipite na wakalala. Anaweza kufanya shule nzima mkagomea chakula. Anaweza pia kufanya msitishe mgomo. Wafanyabiashara wakubwa wana hii karama.
Hata Yesu alipokuwa duniani alikuwa na hii karama. Yani anaweza kukukuta uko kazini kwako akakwambia tu "FOLLOW ME" na ukaacha kila kitu. Ukamfata.
Hawa ni watu hata kama hatoki familia inayojulikana lakini anakuja kufanya nchi nzima imfate kwa mazuri au yasiyo mazuri. Napoleon Bonapatre. Unamkumbuka? Margareth Thatcher alikuwa na karama ya uongozi plus ungangari. Na wengine.
Unashangaa hizi nguvu anapata wapi? Nguvu imejificha kwenye karama tu.
Kuna viongozi wa vyama vya siasa hana elimu ndefu kama wengine wala hahangaiki nayo lakini ukimstudy anaweza kufanya watu lukuki wafanye anachotaka. We unasema ati ana kismati. What's kismati. Kipawa hicho.. Talent.
4. Kipawa cha Uimbaji.
Wimbo ule ule lakini akiuimba yeye watu wanaweza kushangilia mwanzo hadi mwisho na wakampa na standing ovation wakati wengine hawakupewa yote hayo. Mtu ana sauti nzuri utadhani koo lake lilitengenezwa baada ya mwili wake kuumbwa yani likaumbwa kivyake. Kuna watu kanisani wakiimba huwa najikuta natamani wimbo usifike mwisho. Huwa wananifanya nitamani zaidi mbinguni sema tu sijamaliza kazi kubwa Mungu aliyonipa hapa duniani. Ndo kwanza ninaanza. Lakini mtu anaimba mpaka unahisi ukiitikia utamharibia wimbo vile. Hivyo yani..
Sasa watu wengi wanajua hiki tu ndo kipaji. Au kipaji cha michezo. Basi.
5. Kipawa cha Uchezaji:
Hapa napo ndo wengi wanaishia like I just said.
Lakini kuna vipawa vingi zaidi ya michezo na kuimba kama tulivyoona hapo juu na tutakavyoona hapa chini.
Na hata hapa kwenye michezo kuna kipawa cha kila aina ya mchezo.
(Mfano kuna kipawa kwenye soccer, kwenye football, basketball, racing (ya magari au ya farasi, mitumbwi, pikipiki, baiskeli, nk), riadha, boxing, kung-fu, weight lifting, mieleka, kuogelea, cricket, tennis, kuteleza kwenye barafu au kwenye maji yaani skiing, chess, hockey, golf, gymnastics, na mingine mingi. Kuna tofauti ya Messi na Phelps)
See? Sasa huku kwetu watu wengi wanajua Mbwana Samatta na Hashimu Thabeet basi.
6. Kipawa cha uigizaji
Umesema nani Kanumba? Hujakosea. Alikuwa na something EXTRA. Hiyo extra hiyo. Ndo kipawa.
Kuna yule mama mnaijeria yule. MAMA G.
Akiigiza kama Mama Mkwe utamkubali yani utasikia kila anayetazama ile filamu anasema "Huyu mama ana roho mbaya huyu".
Anaigiza hadi unahisi ndivyo alivyo. Hiyo ndo maana ya KITU CHA ZIADA. Kipawa. Mtu hadi anafanana na anachoigiza.
7. Kipawa cha Uchoraji.
Kina Ibra Washokera. Kina Masoud "Kipanya" na wengine. Yani akichora hata kama ni kikatuni tu kikawa hakina maneno utaona tofauti tu. Unakumbuka katuni ya Kingo. Lol. James Gayo huyo. Hazina maneno lakini ujumbe unafika.Kipawa.
Yani nimeona Kingo toka niko mtoto. Ilikuwa inafikirisha sana afu ukiielewa unaona jinsi mchoraji alivyo na kitu cha ziada.
8. Kipawa cha Kufikiri (thinking).
Tofautisha kufikiri na kuwaza. Sizungumzii kuwaza maana kuwaza kila mtu anawaza ila ni wachache wanafikiri. Kuwaza unaweza kuwa huna hela ukajaa mawazo. Mi nazungumzia KUFIKIRI (THINKING).
Kuna watu wana karama hii. Ukimpa afikirie kitu analeta jibu lenye something EXTRA.
Ulishasikia kitu kinaitwa THINK TANK? Mara nyingi kwenye think tanks kuna watu wenye kitu cha ziada kwenye kufikiria. Yani ukimpa issue ya mchanga wa dhahabu anaweza kukupa solution ndogo tu na ikawa ndo the most effective. Ana karama mwenzako.
9. Kipawa cha Ubunifu (creativity).
Hata wachoraji, watunzi wa vitu nk hii pia wanayo.
But hapa naongelea wabunifu. Ndo unaona wanabuni magari,
wabunifu wa mitindo ya mavazi, wa matreni, midege ya ajabu, simu hizi na computers nk. Mifumo mbali mbali kama android, MPESA, max malipo, Uber etc. Creativity tu hapo. Sasa mwingine anaweza kukaa miaka nane hajaweza kubuni kitu cha maana. Mwingine mpe nusu saa tu. Inatosha.
10. Kipawa cha Kumbukumbu
(hapa ndo wanafunzi wanofaulu vizuri wapo. Anaweza akasikiliza kidogo tu darasani lakini akakumbuka every detail hata ambavyo mlikuwa mnahisi hakuvisikiliza kwa makini. Na nyie mpaka mmemrekodi mwalimu na notes mmeandika na maswali mmeuliza lakini "pepa" ikija anafaulu yeye zaidi yenu. Ana something EXTRA linapokuja suala la kumbukumbu.
Nk..
Wewe utaomba Roho wa Mungu akukumbushe vitu kwenye mtihani mwenzako hata hajui kuomba labda. Lakini anapata "A" wewe unaondoka na karai.
Kumbuka kipawa alipewa na Mungu. Na wewe una cha kwako labda michezo. Ndo hivyo.
SASA TUENDELEE..
Nadhani hadi hapo unaweza kuona Michael Jordan alikuwa wapi, na Diamond Platnumz yuko wapi, Ronaldo na Messi na kina Mbwana Samatta wako wapi, Roger Federer yuko wapi, Tiger Woods yuko wapi, na Les Brown yuko wapi Dan Brown yuko wapi, Jack Chan alikuwa wapi, Kanumba alikuwa wapi, Michael Phelps yuko wapi, Alexander Bell, Mohammad Ali na kina Tyson walikuwa wapi katika hizo hapo juu. Nk.
Yaani Tyson hakujaribu kulazimisha kuimba, Ronaldo hajalazimisha kuchora, Diamond hajalazimisha kuogelea. Kuna siku nilisema Dan Brown anajiandikia zake vitabu hajalazimisha kuongea kama Les Brown na Les Brown naye hakujaribu kuandika stori za kuvutia kama za Dan Brown na wote wamekuwa multi-millionaires.
TALENT YAKO NA MAFANIKIO KIUCHUMI
So ukisema SINA MTAJI Mungu anakuangalia tu. You have something in you.
Vipawa viko vingi. Usilazimishe kipawa cha kuimba huku wewe una cha kuigiza. Usilazimishe cha kuchekesha kumbe una cha kufikiri.
Tambua kipawa chako pasi na shaka. Ujue kabisa mimi niliwekewa hiki.
OK BYE..
Niishie hapo kwa sasa na naamini utapa mwanga zaidi ili kujua uanzie wapi kama unataka kuitumia njia hii kuufikia utajiri. Ni imani yangu kuwa umejifunza kuhusu njia hii na wewe kama wewe unaweza kuona kama inakufaa au la.
Ila utaona tu kuwa siyo shortcut. Usijaribu kuwa tajiri kwa short cut. It takes time!
Asante sana kwa kuwa hapa na karibu kwa maswali maoni michango zaidi nk.
Much Love!
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp #o788366511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
Na Andrea G. Muhozya
:::::::::::::::::::::::::::::::::::
Habari ya leo kijana wa kitanzania. Mungu ni mwema tuko hai hadi leo.
Naomba muda wako kidogo tuendelee kujifunza zaidi pamoja leo.
::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Yes...

Ni ujinga kumwonea wivu mtu anayefanikiwa kupitia kipawa chake ilhali kila mtu alipewa cha kwake. Muhimu ni wewe kutafuta cha kwako my friend.
Talent ni njia kubwa mno ya kuweza kukupa pesa nyingi na kukufikisha katika utajiri. Leo hii Michael Jackson alishafariki lakini bado analipwa mamilioni, lakini watu lukuki wako hai na hawajui senti tano wataipata wapi...
Lakini angalia watu kama Michael Jordan na kina Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, na wengineo. Angalia waigizaji kama Tyler Perry na kina Samuel Jackson au Angelina Jolie uone wanavyopata pesa nyingi mno kupitia vipawa vyao.
Siwezi kutaja kila mwenye kipawa hapa maana hatutamaliza. Michezo tu pale juu nimetaja mingi mingi na hiyo ni michezo hatujaongelea vipawa vingine kama vipawa vya thinking and creativity (ubunifu) ambao hawa ndo wanabuni mitindo ya mavazi, ya magari, ya ndege na computer na simu na drones nk lakini pia ndo wanabuni solution za migogoro mikubwa ya kati ya mataifa. Hawa nao wanatengeneza pesa nyingi mno. Mfano mtu anayebuni gari la Rolls Royce au Bentley au Ferrari nk hao wanatengeneza pesa nyingi na hawachezi mpira wala hawaimbi R n B au pop!
Tatizo la watu wengi hasa huku kwetu ni kuwaza kuwa vipaji ni mpira na nyimbo na bongo movie basi. Yani kama hajui kuimba wala kucheza wala kuigiza basi. Katoto kakiimba kama Ali Kiba eti ndo kana kipaji. Kali Kakichora chora ukutani kila siku katakemewa eti kanachafua nyumba.
Lakini point ya msingi hapa ni kuwa kipawa kinaweza kumpa mtu utajiri mkubwa. Kuna wanamichezo wanapesa nyingi mno. Kuna watu wa vipaji wengi wana pesa nyingi. Kuna watu wanalipwa mpaka dola laki 7 kuongea mahali. Yaani kwa saa moja. Imagine! Hiyo ni kama Tshs BILIONI MOJA NA MILIONI 400!!! Kwa saa! Sasa si unaona kipawa kinavyoweza kukufikisha mbali? So usingángáne tu na Bachelor of Law kama niliyosoma mimi. Dan Brown kitabu kimoja tu kinaweza kumpa dola milioni 10. Yaani BILIONI 20+! Hivi unaelewa? One BOOK. Sijui INFERNO sijui DIGITAL FORTRESS.
What’s your TALENT? Usidharau nguvu ya kipawa chako. Mungu atakushangaa na ATAKUADHIBU. Trust me. You MUST FIND OUT ni nini Mungu alikupa. Hakuna ambaye aliumbwa bila kupewa kitu EXTRA. Kila mtu anacho. Ndo wenzetu Ulaya wakikijua kwa mtoto wao wala hawahangaiki eti akasome "vidudu" afu aende primary school asome rundo la vitu kisha aende sekondari asome vitu kibao bado high school bado chuoni. Wakati kumbe yeye mngempeleka kuendeleza kipawa cha kupiga mbizi tu kwenye mabwawa angetangaza nchi na umaskini kwenu ingekuwa bye bye. Lakini mlitaka tu awe daktari. Au mhasibu. Halafu sasa amekuwa what next? Ndo unakuta yeye akiwa kazini anawaza weekend ifike kuna mechi ya bonanza akacheze. Kipawa kilipotezwa.
Usidharau hii. Ukiitumia unaweza kufika bungeni na ikulu mpaka hata UN na wala form four hukumaliza. Wengine wamesoma mpaka maktaba inawajua na ikulu wanapasikia tu.
CONDITIONS ZA KIPAWA CHAKO KUKUFIKISHA KATIKA MAFANIKIO KIUCHUMI
Sasa hapa ndipo shule ilipo. Vipawa pia vina mahitaji yake.
1. Ubora wa team yako.
Moja ni kuwa ili kipawa kikuletee utajiri inahitaji TEAM WORK. Yaani lazima uwe na team ya watu wanaokuhandle wewe na mambo yako yote. Mfano angalia mtu kama Cristiano Ronaldo au Messi. Hafungi magoli bila team work. Yaani anategemea vipaji na creativity ya watu wengine kwenye team ili afike mbali zaidi. Ukimuweka Messi timu kama Mtibwa Sugar (no offense) hatawika kama anavyowika huko aliko maana huko aliko amezungukwa na professionals na watu wenye creativity na vipawa vya aina ya kwake pia.
Lakini pia Ronaldo au Messi ana kocha wa mazoezi binafsi, ana mshauri wa kisaikolojia anamlipa yeye, ana Manager wake binafsi, mwanasheria wake binafsi, ana mtaalamu wa chakula anayemshauri ale nini asile nini (huyu siyo mpishi ni mtaalamu tu yani nutritionist), ana daktari wake binafsi na wa timu pia yupo. Maana ukitegemea daktari wa timu afu akawa kwa mchezaji mwingine itakuawaje? Ana mtu wa mitindo mfano kinyozi na stylist wa mavazi kabisa, ana mwalimu wa kufundisha mtoto wake nyumbani, ana designer wa nyumba na wafanyakazi wa nyumbani kama wapishi, watu wa usafi, gardeners, nk.
See? Haya yote watu hawajui wanapomshabikia Ronaldo au Messi au Tiger Woods. Au wanapoona analipwa pesa nyingi.
Sasa kama unataka kutumia kipawa kuufikia utajiri inabidi ufundishwe ukweli kama hivi. Usije ukaenda tu Bongo Star Search halafu hujui WHAT IT TAKES kukupelea kwenye mafanikio makubwa kupitia kipawa chako. Inahitaji investement kubwa mno. Na NIDHAMU YA MAZOEZI KUBWA SANA.
Na bahati mbaya sasa investment hii indo inakuwa tena BURDEN kwa mwenye kipawa maana ana watu wengi wa kuwalipa. Inakuwa MZIGO MKUBWA mno. So unashangaa mtu analipwa paundi 365,000 kwa wiki moja tu (yani $468,000/- yaani Tshs BILIONI MOJA) anazipeleka wapi? Unahisi ukizipata wewe utakuwa tajiri. No. Nilishasema hauwi tajiri kwa kupata hela nyingi ila kwa kuwa na MINDSET ya utajiri kwanza. Na kuhakikisha fedha inapita kwenye mfumo wa kuzaa tena.
Unaweza kusema hawa hela zao wanazitumia vibaya..no. Licha ya kununua majumba na magari ya kifahari na kufanya masherehe nk lakini pia wanalipa watu wengi mno. Kama nilivyoainisha hapo juu. Tena hapo nimeweka vitu general tu. Na bado kodi ni kubwa balaa.
Kwa hiyo kama una kipawa cha kuongea kama Joel Nanauka (Public Speaking) unataka kuwa kama kina Les Brown ama una kipaji cha kuandika pia kama mimi (Writing) na unataka kuwa kama kina Dan Brown ama kama kina John Maxwell basi unapaswa kujua kuna TEAM inahitajika. Nani atakuwa mentor wako? Nani atakuwa mtunza fedha wako? Nani atakuwa trainer wako. Mentor na trainer ni watu wawili tofauti. Kina Les Brown walijiandikisha katika madarasa ya DALE CARNEGIE ambaye alikuwa mtaalamu wa kufundisha kitu kinachoitwa Public Speaking.
Sikiliza... Dan Brown mpaka amalize kuandika novel moja anaweza kusafiri nchi 10 kukusanya data na kufanya mikutano na watu maarufu duniani na inamgharimu pesa nyingi na muda mwingi kuandaa manuscript hadi iandikwe.
Nani atakuwa MANAGER WAKO? Wa kuorganise wapi ukaongee na ulipwe shilingi ngapi nk. Usije ukawa wewe ndo kila kitu. Messi hakufanya hivyo. Aliandaliwa. Nani anakusaidia kujiandaa?
Changamoto kubwa ya watu wenye vipawa huku kwetu na hata duniani ni kuwa wanafanya kila kitu wao wenyewe. Kwa hiyo anakuwa hana tofauti tu na mtu aliyejiajiri. Anakuwa kama jongoo miguu mingi lakini spidi kidogo. Kipaji kikididimia naye anaishia hapo.
Lakini ukimtaka Les Brown aje Tanzania sasa huongei naye yeye unaongea na watu wake. Yeye sasa ni TAASISI.
Hilo ni jambo la kwanza la kuzingatia. Tengeneza team around your talent. Skilled people. Uwalipe.
2. Vipawa vingi vina muda fulani tu.
Yes.
Changamoto ya pili ni timeframe. Hasa kwa wanamichezo. Kwa mchezo kama Soccer kuna muda wake. Umri ukienda mwili unakataa. Unastaafu bila kupenda. Tofauti na uandishi kwamba umri unavyokwenda ndo unazidi kuwa bora zaidi na zaidi.
Mbwana Samatta ana miaka chini ya 10 hivi ya kuhakikisha ameshatimiza ndoto ya kucheza timu kubwa maana vijana wadogo wenye vipawa vikubwa ni wengi kwenye ulimwengu wa soka kwa hiyo anatakiwa ajitahidi mno. Kwa sasa ana miaka 24. Miaka mitano ijayo mwaka 2022 atakuwa na miaka 29. Hapo mwili umeanza kuchoka na wenye vipaji wadogo zaidi watakuwa wameshaibuka wengi. Ni vigumu kukuta bado akicheza timu kubwa Ulaya mwaka 2025. See? Huo ndo ukweli. Kina Msuva na Kichuya watakuwa wapi? Ni lazima wafikirie.
Lakini Masudi Kipanya anaweza kuwa bado anachora kipanya chake mpaka hata 2050.
Ni muhimu kujua kipawa chako timeframe yake imekaaje.
3. Vyanzo vingi vya mapato.
Cha tatu ni kuwa lazima uwekeze maeneo mengine usitegemee kipawa chako tu. Katika wanamichezo wote ni Michael Jordan tu ambaye amefikisha utajiri wa dola BILIONI MOJA. Yani ndo yuko kwenye Forbes List ya binadamu matajiri duniani. Nazungumzia athletes (wanamichezo kama mpira riadha nk) ni yeye tu bilionea. Yani yuko level kama ya Mo Dewji kwa utajiri. Si mchezo ujue.. lakini hii ni kwa sababu analipwa kwa matangazzo na ana miradi mingine zaidi na zaidi. Kwa hiyo kina Messi siju Ronaldo bado sana kufikia NETWORTH ya dola bilioni moja. Ndo maana unasikia Ronaldo kafungua mradi huu ama ule.
Ndo maana unaona kijana kama Diamond anawekeza kwenye sijui pafyumu, internet, radio stations (added) na mambo mengine. Ukisubiri hela za matamasha tu na mechi nk kuna siku kipawa kitaisha makali yake. Kipawa kina life span yake maana hata wewe mwenyewe una life span yako. Angalia watu hapa kwetu kama Mr. Nice. Walipata pesa nyingi lakini hana washauri hana plans hana team ya professionals wa kumshauri cha kufanya matokeo yake SEASON YAKE ilipopita akapotea. Juma Kaseja na Mrisho Ngassa season imepita. Kina Bombi wachekeshaji season imepita. Emanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) amekwenda kwenye kilimo na biashara ya chakula na security na uchimbaji madini. Anatambua kuwa kuna siku Ze Comedy itakuwa hahiwiki tena. Sijui kama inawika tena kwanza.
Swali la kujiuliza je wewe una kipawa gani? Na umeshaanza kukifanyia kazi? Au bado? Una umri gani? Kipawa chako watu waliofanikiwa nacho walitumia MUDA GANI kufikia utajiri? Usiende tu.
GOOD NEWS IS UNAWEZA KUANZA SIFURI
Uzuri ni kwamba hata kama huna shilingi unaweza kuanza hapo ulipo. Mimi nimeanza kuandika 2013 kupitia hii mitandao ya kijamii. Sikuhitaji pesa. Labda bando tu.
Lakini pia nillianza kuandika kitabu changu cha kwanza 2015 ambacho nilikimaliza mwaka huo huo ila toka hapo nakirekebisha na kukipeleka kwa watu wenye mafanikio na upeo zaidi yani kuongeza ideas na kurekebisha na naamini itakuwa ni moja ya best books duniani.
Kiko kwa lugha ya kiingereza. It's a book for the nations. Nitakipublish miaka ijayo kwa neema ya Mungu kwani ninayafanyia kazi pia yale niliyoyaandika mwenyewe kuthibitisha usahihi wake katika kuleta matokeo.
Lakini pia mwaka jana October 2016 nilianza kozi ya Public Speaking na kuongeza uwezo mzuri zaidi wa kiingereza mpaka sasa naendelea nayo na kila siku nafanya mazoezi ya kiingereza na ya kuzungumza kwa sababu pia nina kipawa cha kuongea.
Kwa hiyo najiandaa tu zaidi. Siku nikifika kwenye World Economic Forum kuongea niweze kufikisha ujumbe kwa usahihi na kuwe na hiyo intelligibility.
Point ni kwamba. Nilianza hapo nilipo. Ni watu wanaoniambia kuwa naweza kuandika "vizuri". Mi napokea na kushukuru na kutendea kazi..
Nikienda mahali kuongea ni watu wanaoniambia kuwa naweza kufanya vizuri pia eneo hilo.
Point ni kuwa nimeanza nilipokuwa. Bila kitu. Na wewe unaweza kwa kipawa chako ulichonacho. Haijalishi nani anavuma sasa usiogope. Mentor wangu alisema one day kuwa ukitazama nje mchana kuna kunguru na ndege wengi tu wote wanaruka kuna mpaka mbu na vipepeo. Vyote vina ruka na hakuna kinachosema "mbona nakosa nafasi ya kurukia". Smart man. So usiwaze kuhusu hilo. Unaweza pia.
Lakini lazima uzingatie yale mambo matatu niliyoyasema pale juu: yaani team work na timeframe na kuwekeza kwenye vitu vingine.
Na pia lazima uzingatie kwamba ili uweze kukifanya kipawa chako kuwa biashara itahitaji uwe vitu vitatu: yaani bidhaa au huduma, system na team. Hili ni somo linalojitegemea.
Ukitambua kipawa chako unakuwa umetambua kama 50% ya kitu ambacho Mungu alitaka ufanye huku duniani. Maana kipawa kitalitumikia KUSUDI. Na ukitambua kipawa chako ukaki develop basi hutakufa njaa wala hutakufa maskini. Mungu ali-make sure hilo amelifanya kabla hujaja duniani. Usimwangushe!

May 30, 2017.
Jumapili, 21 Mei 2017
IN EVERY SITUATION LEARN TO TELL YOURSELF: "OKAY... SO WHAT NEXT?" KATIKA KILA HALI JIFUNZE KUJIAMBIA MANENO HAYA: "NI SAWA... KWA HIYO NINI KINACHOFUATA?"
*******
Asante nyingi kwa Mungu kutupa nafasi hii kujifunza pamoja.
*******
Mara nyingi mno tukikosa vitu tunavyotarajia kupata huwa mioyo yetu inasinyaa.
Hivi ulishawahi kusinyaa moyo? Dah.
Yani mtu unakosa raha. Unajiona hufai na kuona bora wenzako wana bahati. Hii haijalishi kama mtu amekataliwa na boyfriend au girlfriend. Au mwingine hata amekataliwa tu friend request Facebook. Hahaaaa. Au wamemBLOCK.
Yaani mtu akikublock halafu ukajua kuwa ame-kublock halafu ulikuwa unaona ni mtu muhimu kwako unajisikiaje? Rejected right? Halafu unafanyaje unalia?
Hali huwa ni mbaya zaidi linapofikia suala la mtu amekosa dili. Mfano sisi wajasiriamali yani dili nzuri ghafla ikayeyuka. Aisee. Ukimuuliza Andrea vipi anakujibu "We acha tu"
Au kwa wenzetu "wanaotafuta kazi" pale akikosa AJIRA. Au ameachishwa KAZI. Yaani "hali ya hewa" huwa inakuwa kama imevurugika vibaya sana. Vijana waliokosa AJIRA huwa wengine wanakata tamaa. Mabinti wadogo vishawishi vinakuwa na mvuto zaidi ili aanze kuishi kama "wenzake". Watu wazima kidogo anaweza kukosa mwelekeo na hata kuzorota afya.
Wengi wetu huwa hatuna kawaida ya kutulia na kusahau yaliyopita na kuganga yaliyopo na yajayo! Yani mtu akikosa ajira anakuwa kama kila kitu kimestop!
Kwa wewe uliye kundi hilo naomba niseme na wewe kidogo kabla sijaendelea. BRIAN ACTON na JAN KOUM walianzisha mtandao wa WhatsApp BAADA ya kukosa AJIRA. Mmoja kakosa ajira Facebook mwingine kakosa Twitter.
Lakini walikuja kuuuza huo mtandao wa WhatsApp kwa $22 billion. Yani trilioni 45 za kitanzania. (Mwanzo ilikuwa waiuze kwa $19 bilioni lakini dau likaongezeka) ukisoma hii link utaona hilo http://www.dailymail.co.uk/sciencetech/article-2782370/Facebook-completes-19-billion-acquisition-WhatsApp-European-regulators-green-light.html
Sijui unaelewa kukaa tu na computer na kichwa chako na kuwaza vizuri halafu miaka kadhaa tu baadaye wakawa na utajiri huo?
Na mimi kinachonifurahisha zaidi katika hawa jamaa ni kuwa walimuuzia mtu aliyemnyima mmoja wao kazi. Facebook!
Muhimu ni kuwa hawajalalamikia mtu wala kutaka kujiua. Walikaa wakaendelea na MENGINE.
Hii tabia ya kuendelea na mengine ni jambo muhimu mno maishani. Ukiwa mtu wa kuangalia PAST tu nini kilipaswa kiweje na kwa nini hakijawa.. na kuanza kusema WHY ME? Utashangaa unakufa kabla hujaishi. Serious. Unafikiri Mungu mjinga? We fanya mengine. Mi siku hizi nina usemi wangu : THE PAST 1 MINUTE IS GONE AND I'M NOT INTERESTED IN IT.
So kama kuna kitu nimefanya au sikufanya basi. Nataka kujua zaidi kuhusu NOW. Kesho nayo mwenye nayo hajanipa bado so NOW ndo pa kuishi. Not the past 1 minute or day or month or year. It's gone. And sitaki kuiwazawaza.
Ndivyo walivyoishi hawa jamaa wa WhatsApp. Yani iko hivi... nakuja kwako kuomba kazi unasema HAKUNA NAFASI. Afu mi na smile najibu tu "OKAY". Then naenda kuanzisha kitu kingine na baadaye wewe uliyesema HAKUNA NAFASI unaanza kunibembeleza nikuuzie nilichobuni halafu mimi nasema kama unakitaka basi utakinunua lakini lazima tufanye wote kazi. Na unakubali. Problem solved. Sasa ukilia na kusubiri watumbuliwe wengine ili wewe uajiriwe na wewe ni jipu.
Ukikosa ULICHOTAKA fanya mengine. Sasa mwingine hapa anauliza "mengine yapi?". SASA si ndo maana juu ya shingo yako kuna kichwa. Au kiliwekwa cha nini. Kina macho. Pua. Kinywa. Masikio. Nywele. Sasa macho ulipewa ya nini? Ya kutolea machozi? Na kichwa ndani yake kuna UBONGO. Uliwekewa wa nini sasa? Si ungepewa kichwa cha kuku basi.
My point is ukikosa chochote usianze kuwaza milele na milele.
Kwenye kitabu changu nimeandika kuhusu Steve Jobs jinsi alivyoanzisha kampuni ya Apple. Halafu baadaye corporate politics zikaingia akapigwa chini kutoka kwenye kampuni aliyoanzisha mwenyewe. Inauma mno.
But what did he do? Huyu mimi nikimkumbukaga huwa najifunza sana. Yeye hakulialia milele na milele kama wengi wetu. Alienda kuanzisha kampuni NYINGINE.
Halafu jina la hiyo Kampuni nyingine akaiita "NeXT". Na hapa ndo nimepata title ya makala hii.
Yes. NEXT. So kuna NEXT nyingi mno maishani mwetu. What's your NEXT opportunity? Usililie mlango uliofunga. Kitu kikishatokea songa mbele. Steve Jobs aliifanya hiyo NeXT ikawa nzuri na bora mno kiasi kwamba APPLE waliomtema wakalazimika KUMNUNUA tena. Na sharti lake likawa anawauzia lakini lazima awepo kwenye uongozi wa Apple. Na wakakubali. Ndo kisa cha Jobs kurudi Apple na leo iPhone ni brand kubwa na aghali mno sababu yake.
Sasa kama wewe ni msanii wa muziki umeenda studio wamekukataa usilielie. Kaimbe hata kwenye birthday za watu huko bure. Watu watakuona huko huko. Kwani mwenye studio kabaki na sauti yako na miguu yako? Hapana. Basi angalia your NEXT OPPORTUNITY.
Umeanzisha biashara kila unayemjua ANAAHIDI TU kuwa atakuungisha halafu hawakuungishi wala nini. Unaacha eti. Eti unasema hakuna wateja. Kweli? Nchi hii ina mamilioni ya watu. Waliokataa kukuungisha hata 50 hawafiki unakataje tamaa? We jiulize tu nani my NEXT customer. Wengine watakuungisha mbeleni. Mi nina mteja wangu mmoja hakununua kwangu miaka mitatu mfululizo lakini kuna siku akaja na sikutumia hata nguvu kumwambia chochote. Leo ni mteja mzuri mno. Three years! Ningeacha baada ya mwaka je? So cha muhimu ni kujiuliza WHAT'S YOUR NEXT.. next opportunity, next relationship, next deal, next student, next coach or manager, next client, next team, next radio show, next job, next business. Kuna mpaka next husband au wife. Sembuse AJIRA?
Your future iko kwenye "NEXT" zako. Siyo kwenye "LAST". Juzi nikawa naongea na binti mmoja kwenye simu anahitaji ushauri fulani. Lakini kila nikiongea naye huwa anapenda kusema I DID THIS I WAS LIKE THIS nk. Nikamwambia tu I'm not interested in your past coz I'm not going to the past and neither are you. Nikamwambia maneno "DID.. WAS" nk hayaletagi melody nzuri masikioni mwangu so asiwe ananiambia. Aseme zaidi kuhusu SASA. NOW.
Najaribu kuupunguzia ubongo wangu mzigo wa kuwaza kinyumenyume!
Nadhani na wewe unatakiwa usiwaze hivyo. Fikiria WHAT NEXT. Kisha anza kufanyia kazi.
Maisha lazima yakupe LADHA ZOTE ndugu. Nzuri na ambazo si nzuri. Tamu na zisizo tamu. The key is to take each and move on.
Kuna siku nikiwa mwanafunzi Makongo. Nimetoka shule na njaa balaaa. Nimefika home mchana saa tisane hivi nikakuta maziwa yamebakia kidogo kikombe kimoja tu so nikachemsha halafu nikaweka vijiko vya kutosha vya sukari yani nimekoroga hadi raha angalau ule utamu utasaidia kudanganyishia njaa.. Sasa ile kunywa tu khaaaa! Kumbe nilidhani niliweka sukari kumbe chumvi!! Tena ya kutosha. Aisee yani nilicheka kweli.. njaa ikapata bonge la surprise.
Ndo hivyo. Sometimes unataka sukari life inakupa chumvi...tena ya kutosha. Move on.. Find your NeXT.
Ndivyo maisha yalivyo.
Watu wengi wanaishi kwa mazoea. Kuna mtu aliuza nyumba ili agombee ubunge mwaka juzi 2015. Ukisikia KUJILIPUA ndo kama hivi yani. Akapata hela zake akaingia kwenye mchakato wa uchaguzi. Biashara ikawa "kichaa". Kidogo naye awe kichaa. Maana ubunge hana, nyumba hana, hela nazo hana na marafiki nao hana. Hapo ndo utaelewa kukoroga kitu kwenye maziwa bila kuonja kwanza kama ni sukari kweli. Alipata frustrations za kutosha. Lakini hakujiua. Alianza moja akachechemea taratibu naamini anaendelea na maisha baada ya uchaguzi. Amepata NeXT yake. Ndivyo inavyotakiwa ufanye. Move on. Ukibaki na WHY tu utapata madonda tumboni na mvi za ghafla bila kutarajia na bado utakuwa hujabadilisha kilichotokea! Don't be small minded. Move on.
Awamu hii ya JPM kuna watu wametumbuliwa hadharani. Kuna watu wametuhumiwa na madawa. Kuna watu wamezodolewa na kukashifiwa hadharani. Na katika hao wote kuna makundi mawili. Kuna ambao hawakufunua kinywa chao kabisa. Hata mara moja. Hawa ni Big Minded people. Na kuna waliowaza "KWA NINI WAMENITAJA". Hawa ni small minded people. Maana watu wameanza kutajwa toka shule ya msingi majina ya wapiga kelele. Au Swahili Speakers. Wakala stiki na zilishapoa. Wengine walitajwa kuwa wamebadili dini ili wawe raisi wa nchi. Hawakupiga mayowe. Sasa wewe wa kwanza kutajwa dunia hii? Yesu alionyesha watakaombetray wawili: Yuda (atamuuza) na Petro (atamkana). Mmoja alijiua mwingine akalia na kutubu na kukomaa kiutu uzima. Wewe ni Petro au Yuda in that regard? Think for yourself.
Ndo kipindi hiki cha JPM mwingine ana kutu moyoni eti "Kwa nini wamemtumbua baba yangu"? Small minded people. Mwingine ana kutu moyoni eti "Hivi kwa nini girlfriend hajajibu message yangu siku ya tatu leo na naona tiki za blue?" Move on. Don't live in the past.
Wana wa Israeli walikuwa wanawaza kinyumenyume tu. Matango na viungo vya chakula walivyoexperience utumwani. Wakatamani hadi kuzikwa kwenye makaburi kuliko kufa jangwani wakasahau wako huru. Wanachotaka hawakioni wakawa watu wa kupiga "mayowe" tu na kulalamika kila wakati. Nadhani unajua kilichowakuta. So wewe pia kama ULICHOTAKA hakijawa basi find your "NeXT". Hiyo ndo positive thinking iliyomrudisha Steve Jobs Apple na kuwafanya hao waanzilishi wa WhatsApp kuwa matajiri mno.
Kama hukubali ni sawa pia.
Lakini maisha mazuri na ya utulivu (good and tranquil life) kwa wengi yamekuwa ndoto kwa sababu ya kuwa na WHY zisizoisha. Anabaki anajiuliza hivyo tu. Usibaki na WHY. Swali sahihi ni *WHY NOT?* Yaani: why not nisikose mimi kazi. Nilitaka akose nani ili mi nipate. Kwa nini usitajwe wewe? Kwa nini nisisemwe mimi vyeti vyangu. Nataka nani ndo asemwe. Yes, sometimes WHY is a selfish question. Unajiwazia wewe zaidi. Unaunyima ubongo wako fursa ya kuwa CREATIVE. Unabaki na KUTU moyoni kisa boyfriend kakuacha huli wala hunywi na kujiua unataka. Kisa tu hukujiuliza swali sahihi: Why Not. Kwa nini usiachwe. Kwani wewe umekuwa Mungu? Mungu mwenyewe kuna malaika walimwacha. Sembuse wewe? Kuna watu wametelekezwa na wazazi sembuse boyfriend. Eti anasema inauma wewe hujui tu. No move on. Find your NeXT. Unajuaje labda anayefuata ndo ulikuwa umeumbiwa. Trump alililia wake zake walioondoka? Alifind NeXT. Kumbe huyo ndo First Lady. Ujue kama hujaoa First Lady ikulu huipati hata uweje. Sasa wenye ndoto za kuwa maraisi sijasema umpige chini mkeo unahisi ndo siyo sahihi. Lol. Trump huyo hapo. Ana mind hii ya MOVING ON. Democrats mpaka leo hawaamini walipoteza uchaguzi. Kuna watu wanaamini walishinda uchaguzi. Bado wako na WHY. Why siko IKULU. Move on kwanza.
Ukijifunza kuishi kwenye NEXT utapiga hatua kubwa na kuwashangaza wengi. FIND YOUR NEXT.
Serengeti Boys yetu imetolewa kwenye michuano. What's NeXT? Au tupo tu hatujui nini tufanye. Watakaa tu au watapewa hata zawadi kuwatia moyo. What NeXT.
Umeomba mkopo benki wamekunyima. What NeXT. Move on. Labda wamekunyima kunde tu.......! Shukuru tu Mungu and tafuta what NeXT.
NeXT ndo kila kitu.
****
By the way ile siku niliyokoroga chumvi ya kutosha kwenye maziwa hadi njaa ikapata surprise niliangalia mfukoni nikakuta nina sh mia tatu. Enzi hizo. Nikaenda kwa Mangi. Sasa unadhani njaa ilipata dawa au hapana?
Find your NeXT my friend.
Mungu akubariki sana!
Semper Fi,
Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp #o788366511
Jumamosi, 13 Mei 2017
DUNIA HAITOKUKUMBUKA KWA MAMBO UTAKAYOJISIKIA KUFANYA BALI KWA MAMBO #UTAKAYOSUKUMWA KUYAFANYA
Mungu katuwezesha kukutana tena. Basi Jina lake lizidi kuinuliwa maana kuwa hai ni za zawadi kubwa mno.
Leo nina jambo muhimu kuongea na wewe.
Katika kipindi cha miaka saba ambayo nimeitumia kujifunza na kupractice ujasiriamali na kujifunza kwa watu walioacha ALAMA duniani nimeweza kujifunza mambo mengi. Mojawapo ni kuwa dunia haina muda na mambo unayokuwa COMFORTABLE kuyafanya hata kama utafanikiwa nayo vipi. Ukifa yanaishia hapo na jina lako linabaki kwenye kaburi pale. Born 19.... died 20... hivyo yani.
Dunia inamkumbuka mtu ambaye alitii sauti ya MSUKUMO wa ndani wa kufanya kile alicholetwa hapa duniani kukifanya. Unaweza kuwa effective and successful kwenye jambo fulani hapa duniani lakini kama ukifa na jina lako likafa ni dalili kuwa ulikuwa mbinafsi na ulitaka mafanikio BINAFSI tu wala hukujali kuwa unapaswa uguse watu wengine kabla hujaondoka duniani. Ni vizuri kuangalia sana mambo unayoyafanya kama unayafanya tu kwa kuwa ndicho ULICHOSOMEA au ndicho KIRAHISI KUFANYA au unakifanya kwa kuwa kuna MSUKUMO NDANI YAKO wa kukifanya?
Yaani uligombea ubunge kwa kuwa ULISUKUMWA moyoni au sifa tu au ulitaka kuonyesha watu kuwa wewe ni "kiboko"? Usipoangalia hili jambo utakuwa maarufu kweli kweli lakini siku ukimaliza muda wa ubunge na jina lako linaishia hapo tena ukiwa bado hai. Hivi kila aliyewahi kuwa mbunge mashuhuri au waziri bado anatajwa leo na kukumbukwa?
Ask yourself.
Unafanya biashara kama fashion au una MSUKUMO ndani kuwa ufanye? Kama huna msukumo ndani wa biashara basi utakuwa unaendesha gari kwenye njia ya treni. Kitakachotokea hata wewe mwenyewe hutajua yani. Usifanye biashara ili uwe kama Dewji. Yeye ana msukumo wa kwake. Wewe nawe UNAO?
Umeajiriwa sababu "watoto watakula nini" au umeajiriwa sababu una MSUKUMO kuwa inatakiwa uwepo hapo ulipo ili huduma yako iwanufaishe watu wa Mungu watakaokuja kazini kwako? Usifurahie kuitwa ofisa wa benki au meneja masoko au head mistress nk huku una IGNORE sauti fulani inayokusukuma kutokea ndani kuhusu jambo jingine kabisa. Ukiendelea kuiignore hiyo sauti ipo siku ITANYAMAZA kimya haitazungumza tena kwa kipindi kirefu tu. Lakini ujue utakuwa umeignore kitu ambacho Mungu alikuwa anataka ufanye. Utashangaa umekaa kazini miaka mingi na mpaka unastaafu lakini huna amani moyoni na ukistaafu basi jina linaishia hapo pia. Halafu ile sauti ndo itarudi sasa. How sad.
Unasoma Chuo kwa ajili CV ionekane ina neno "University" au ili ukue-kue kidogo kabla hujaolewa...au unasoma sababu una kitu kinakwambia moyoni kuwa unapaswa kusoma hicho kitu. Au ulichagua kozi kwa kuwa ni nyepesi au kwa sababu "ina AJIRA" au sababu rafiki au anko alisema engineering ndo kozi ya "vichwa" kama wewe. Sasa kichwa gani unaambiwa pa kwenda.
Point ya msingi hapa ni kuwa mahali popote ulipo jitahidi sana kusikiliza sauti ya ndani yako. Siyo maneno ya mzazi tu au mume au mke sijui auntie ambao sauti ya ndani yako hawajui inafananaje. Za ndani kwao zenyewe hawajazisikiliza wataelewaje kuwa huwa kuna sauti ndani ya mtu!? So BE YOU. It's YOUR life. Life is really more than money and fame.
Dunia huyapa heshima kubwa majina ya wale waliofanya vitu vilivyotokana na MSUKUMO fulani ndani yao na siyo waliofanya tu sababu ya fashion au kutaka kujulikana na certainly haiwapi heshima wale waliodharau sauti iliyowaambia ACHA HIKI KAFANYE KILE.
Ni ngumu kuacha kitu ambacho ni popular machoni pa wengi ili ukafanye kitu ambacho unasukumwa moyoni kufanya hata kama hakieleweki kwa wengine. Lakini ukiweza hilo basi jina lako litakumbukwa miaka mingi hata ukiwa umeondoka.
Ngoja nikupe mifano michache tu ya majina yanayotajwa na kukumbukwa sana na dunia.
1. WILLIAM BOEING
Ilikuwa jioni majira ya saa moja kasoro hivi. Mwangaza wa jua la mwezi wa July uling'arisha anga la magharibi kwa rangi nzuri iliyotulia na jua likaanza kudondoka na kuruhusu giza kuufunika uso wa nchi. Nikiwa futi 30,000 kutoka usawa wa bahari ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kushuhudia jua likizama nikiwa angani mbali kiasi hicho. Kuzama kwa jua (sunset) ni mojawapo ya mambo ninayopendelea sana kuyatazama.
Masikioni mwangu kulikuwa na headphones nikisikiliza muziki wa kusindikizia safari yangu ya kwanza ndani ya ndege aina ya BOEING 737.. Baada ya kutazama jua likiwa limeishia kabisa juu ya mawingu akili ikanirudisha kwenye dirisha la ndege kushoto kwangu lilivyokuwa zuri na lilivyotengenezwa kwa ustadi mkubwa. Na kisha akili yangu ikanileta kwenye ndege yenyewe - BOEING 737.
Muda kidogo baadaye jina la mwanzilishi wa kampuni kubwa ya Boeing likaja kichwani. Huyu ni bwana William Boeing. Nikaanza kutafakari kidogo kuhusu alipoanzia, alichoamua kufanya, ALICHOSUKUMWA kufanya, na dunia inamkumbuka kwa lipi katika hayo.
Akiwa amezaliwa familia "bora" baba yake akiwa mhandisi wa mambo ya madini William alisomeshwa shule za maana mno kwanza Uswizi kisha kwao Marekani kwenye Chuo Kikuu maarufu cha YALE UNIVERSITY. Kama hujui kuhusu Chuo hiki Google tu kidogo uone kusomesha mtu hapo inakuwaje.
Lakini William akakatisha masomo yake YALE UNIVERSITY na AKAAMUA kwenda kufanya biashara ya MBAO!! Dah!. Kuna watu wana maamuzi magumu. Huwa nasema ni rahisi kuacha VETA ili ukafanye mambo yako. Lakini kuacha YALE UNIVERSITY ukauze MBAO? Hiyo ni level nyingine ya maamuzi. Trust me.
Lakini akafanikiwa sana katika hiyo biashara na kupata fedha nyingi mno. Akajulikana kama muuza mbao maarufu.
Lakini katika safari zake kibiashara siku moja akatembelea maonyesho ya kibiashara huko Seattle na kuona watu wametengeneza mashine fulani ambayo waliirusha angani IKIWA NA MTU. Moyo wake ukapiga PAAP! Akapata MSUKUMO mpya kabisa wa kuunda NDEGE yake. Na akaacha kila kitu na hela zake akazielekeza kwenye hilo jambo lililompa msukumo mpya.
Alipitia mengi lakini akafanikiwa. Na leo hii dunia inamkumbuka kwa jambo hilo. Ukitazama leo ndege aina ya BOEING zilivyo leo ni mwendelezo tu wa alichokianzisha. Dunia haikumbuki mbao ngapi aliuza. Ukitaja jina/neno Boeing watu hawalihusishi na mbao bali na kampuni kubwa ambayo imegusa maisha ya watu wengi mno. Na hakuna siku inayoenda leo ambapo hagusi maisha ya watu dunia hii. Na hayupo.
What about you? Think about your end. Forget the comfort. Work on your legacy. Utakumbukwa kwa kipi? Kwamba ulikuwa polisi au mhasibu afu basi? Kuna mapolisi au wahasibu wangapi dunia hii hadi ukumbuke ukumbuke wewe? Gusa maisha ya watu hasa wasikokujua kabisa.
2. FRANCIS SCOTT KEY
Huenda hili likawa jina geni kwako. Huyu alikuwa mwanasheria maarufu tu huko Marekani zamani za kale. Alifanya kazi kubwa mno kama mwanasheria hadi akafikia kuwa DISTRICT ATTORNEY hiki ni cheo cha heshima mno katika kila jimbo la Marekani. Kumbuka Marekani kila jimbo ni nchi. Yeye alikuwa District of Columbia. Yani "jikoni". Hivi Mungu akupe nini?
Lakini kuna jambo lilitokea kati ya mwaka1812 hadi 1815. Nalo ni vita kati ya Marekani na Uingereza. Kuna wamarekani wakakamatwa na Jeshi la Uingereza. Yeye kama mwanasheria akawa amepelekwa kwenda kuNEGOTIATE hao watu waachiliwe. Bahati mbaya naye akashikiliwa. Akakaa kwenye kambi ya adui kwa muda mrefu mno huku akishuhudia nchi yake ikidondoshewa mabomu na hana cha kufanya. Lakini siku moja alfajiri mapema mno mapambazuko yakianza na usiku kucha eneo la Marekani lililokuwa karibu na ile kambi likiwa limeshushiwa "mvua" ya mabomu usiku kucha huyu bwana Francis Scott Key huku akitazama kwa masikitiko eneo la nchi yake lililopigwa mabomu usiku kucha akashangaa kuona bendera ya Marekani ikiwa ipo kwenye mlingoti ikipepea. Kitu hicho kilimpa MSUKUMO wa ajabu mno moyoni. Akapata faraja kubwa kuwa licha ya mabomu yote yale lakini bendera ya nchi yake ilikuwa bado ikipepea vizuri kabisa. Akapata MSUKUMO wa kuandika SHAIRI kuhusu hilo tukio. Kichwa cha hilo shairi ni: THE STAR-SPANGLED BANNER (banner=flag)
Miaka kadhaa baadaye Bunge la Marekani (Congress) likapitisha resolution ya shairi hilo kuwa WIMBO WA TAIFA WA MAREKANI!
Leo hii Francis Scott Key hakumbukwi kwa kesi nyingi alizosimamia kwa kazi aliyosomea bali kwa kitu alichoandika bila kusomea. Popote pale wimbo wa TAIFA wa Marekani unapoimbwa kila siku anagusa maisha ya watu wengi mno wa nchi yake na nje ya nchi yake wanaoguswa na shairi lake.
Usikute wewe unaweza kuchora picha moja tu au kutunga kitabu kimoja tu na dunia ikakukumbuka kwa hilo ila unang'ang'ana uwe maarufu kama Tundu Lissu.
Think about that.
3. NELSON MANDELA
Mwanamasumbwi na mwanasheria pia msomi kutoka Chuo Kikuu cha FORT HARE na kile cha WITWATERSRAND. Na akiisha kupikwa huko katika vyuo AKAAMUA kufanya kazi kama mwanasheria jijini JOHANNESBURG.
Lakini serikali ya watu wazungu ilipopitisha sheria ya ubaguzi wa rangi Mandela akapata MSUKUMO mpya ndani yake siyo wa kuwa hakimu au jaji no. Ulikuwa ni msukumo wa kupigania USAWA na kupinga sera za kibaguzi kwa moyo wake wote. Msukumo wa kuwa mwanaharakati.
Alipitia magumu mengi, ndoa yake ya kwanza na bi Evelyn Mase ikafa.
Akaanza kufatiliwa na serikali na kukamatwa mara kwa mara. Mwisho akapewa kesi nzito na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela ambacho alikitumikia katika magereza matatu tofauti ikiwemo la Robben Island.
Miaka 27 baada ya kufungwa akaachiwa. Dunia haikumbuki gloves zake au kesi alizosimamia bali UANAHARAKATI WAKE na KUPIGANIA KWAKE USAWA. Pia dunia inamkumbuka Mandela kama mtu aliyekuwa hana kinyongo na mtu. Mfano licha ya yeye kuachana na mke wake wa kwanza kwa sababu za Evelyn kumtuhumu Mandela kutokuwa mwaminifu na Evelyn kubadili dini na kuolewa na mtu mwingine na nk lakini Evelyn alipokufa Mandela na familia walihudhuria msiba vizuri kwa hisia zote. Lakini pia alipotolewa gerezani alimsamehe mtu aliyeidhinisha Mandela afungwe maisha!!
Dunia inakumbuka hilo.
What about you?
4. ABRAHAM LINCOLN
Mwanasheria mwingine huyu. Tena huyu alikuwa mwanasheria kwa KUJIFUNDISHA mwenyewe na kisha kwenda kufanya BAR EXAM (wanasheria wanajua hii kitu..siku hizi kuna LAW SCHOOL)
So huyu ni kichwa sana acha wewe ambaye umefundishwa na maprofessa wazuri na maktaba unayo na computer na internet na hao waliokufundisha wanakupa mtihani na bado unafeli afu unasema eti profesa kanifelisha! Ungejifundisha mwenyewe nyumbani kama Lincoln afu ndo ukapewe mtihani ungeelewa hata swali linahusu nini kweli? Nataka uone tofauti yako na Abbe! Alikuwa kichwa si mchezo.
Alisimamia kesi kadha wa kadha na kupata ushindi mnono hasa kwa kutumia kipawa chake cha kuongea vizuri.
Hata hivyo dunia leo haimkumbuki kama mwanasheria nguli na kichwa bali kama mojawapo ya maraisi bora kabisa wa Marekani na hasa kwa kuzuia umiliki wa watumwa huko Marekani na kuzuia nchi kusambaratika ilipoingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mgogoro wa umiliki wa watumwa ambao ulizalisha chama cha Republicans mwaka1854. Baada ya Congress kupitisha sheria ya KANSAS-NEBRASKA ACT ambayo ilitaka kila jimbo liamue lenyewe endapo litaruhusu watu wake wamiliki watumwa au la. Majimbo kadhaa yakapinga hiyo sheria yakitaka sheria isiwepo suala la kuchagua kumiliki au kutomiliki. Ndipo Republican Party ilipoanzia hapo na LINCOLN akapata MSUKUMO mkubwa wa kuachana na sheria na kuingia kwenye siasa za uongozi wa juu rasmi akijiunga na chama cha Republican mwaka 1856 na kuwa raisi miaka minne tu baadaye!
Wajasiriamali na watafuta mafanikio wanamkumbuka Lincoln kwa jinsi alivyopambana bila kuchoka kutoka level za chini hadi kufikia kuwa raisi wa Marekani. Sheria ilikuwa tu mahali alipoanzia lakini uongozi wa nchi ukawa ni msukumo wa ndani. Msukumo mkali mno wa ndani uliomvusha kwenye changamoto za vipindi vigumu vya kushindwa uchaguzi kupoteza mke kupata nervous breakdown nk hadi akaja kuwa raisi.
Usidharau msukumo wa ndani. Lincoln angeweza kubaki mahakamani lakini jina lake lingeishia siku yake ya kufa kama maelfu ya wanasheria wenzake huko ambao hakuna anayewajua wala kuwakumbuka.
5. TAIKICHIRO MORI
Kila mtu anamjua Bill Gates hasa kwa kuwa ni tajiri namba moja duniani. Lakini ni vizuri kupitia historia na kujifunza kwa waliowahi kumtangulia katika nafasi hii.
Taikichiro Mori ni mmoja wapo na alikuwa tajiri namba moja duniani mwaka 1992 utajiri wake ukiwa net worth $13 billion.
Na dunia inamkumbuka hivyo yani licha ya kuwa alikuwa academician mzuri huko Japan na mwenye mafanikio katika eneo hilo.
Alipata mafanikio mazuri katika masomo yake hadi kufikia kuwa mwalimu wa Chuo Kikuu. Na huko katika kufundisha akafanikiwa hadi kufikia level ya DEAN wa KITIVO CHA BIASHARA katika Chuo kiitwacho YOKOHAMA CITY UNIVERSITY. Ukiwa dean wewe ni mtu mkubwa. Alidumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi alipostaafu mwaka 1959.
Ni baada ya kustaafu ndo alipopata MSUKUMO mpya wa kufanya biashara ya REAL ESTATE. Nadhani hela zake mafao hizo. Lol. Alifanya hiyo biashara kwa miaka mingi na akafanikiwa mno ndo hadi kufikia 1992 akawa tajiri wa kwanza duniani. Dunia inajua alipoanzia lakini inakumbuka na kuheshimu ilichomsukuma kufanya.
Sasa kustaafu ualimu au uhandisi au unesi au chochote siyo mwisho wa maisha. Kama kuna sauti ndani inakwambia kagombee udiwani au kafungue mgahawa tii sauti usifanye mgumu moyo wako. Usiseme miye mzee. Kuna mstaafu mwenzako mzee alitajirika uzeeni. Huyu si mwingine bali.....
6. HARLAND SANDERS (a.k.a Colonel Sanders)
Huyu naye alikuwa mwanasheria lakini sheria ikagoma "kumtoa" baada ya miaka mingi. Akaona afanye vingine kama kuuza insurance covers nayo ikagoma. Akaamua kuuza taa tu sasa. Taa nazo zikampa headache tu. Mpaka anastaafu anapata mafao anayaangalia hivi anaona ujinga kabisa bora akajiue tu.
Lakini kabla ya kujiua akiwa mahali anapanga mipango ya kujiua akapata msukumo mdogo tu ndani kwamba kabla hajajiua aandike kwenye karatasi vitu vyote ambavyo hajawahi kufanya. Akiwa anaandika akakumbuka kuwa yeye alikuwa ni bonge la mpishi. Na kwamba alikuwa ametengeneza formula (recipe) ya kupika kuku kwa kumchanganya na viungo zaidi ya 10 tofauti tofauti ambavyo ni yeye tu alikuwa anavijua na kuku alikuwa mtamu asikwambie mtu. Khaaa. Akaahirisha kujiua akaenda kuanza kupika kuku ili sasa badala ya kula mwenyewe akawauzie wengine. Lol. Akaanza kuuza kwenye sehemu watu wanakojaza mafuta kwenye gari. Anawaambia huyu kuku ukimla lazima utampenda maana nimeweka recipe ya viungo vingi vizuri vya asili. Kama mchezo akaanza kuingiza vijisenti. Akiwa na umri wa miaka 62 akapata MSUKUMO mwingine wa kuisajili biashara yake kama franchise business akiwa anaiita KENTUCKY FRIED CHICKEN. Kuku wa kukaanga kutoka jimbo la KENTUCKY. Hiyo ilikuwa mwaka 1952.
Miaka 12 tu baadaye mwaka 1964 biashara ilikuwa imechanganyia akaiuza kwa $2 million. Bilioni kama nne za kitanzania leo. Fikiria mtu mwenye hela aina hiyo mwaka 64!!! Akiwa mzee wa miaka 74.
Kwa hiyo kama umepigika huoni mbele unataka ufe tu mwambie shetani hivi: NAAHIRISHA KUJIUA SITAKUFA BALI NITAISHI NA NITAFANYA KITU HAKIJAWAHI KUTOKEA HATA KAMA NI KUKAANGA DAGAA UPYA.
Ilimradi usikilize sauti ya ndani yako kwa utulivu. Tulia sikiliza. Mungu akiongea utajua tu I tell you. Utashangaa hakuna atakayekufundisha cha kufanya utahangaika huku na kule wewe mwenyewe utajishangaa hutakuwa na muda na critics na wanaokucheka wala hutatafuta kuonewa huruma tena. Utashangaa mifupa yako ina nguvu akili yako imeamka. Huo nao ni kama ubatizo mpya kabisa nakwambia. Na dunia haitataka kujua sijui ulisoma wapi au ulifanya kazi wapi. Dunia itataka kutangaza jina lako kupitia mambo uliyoyafanya kupitia MSUKUMO NDANI YAKO. Kitabu kinasema UTII NI BORA ZAIDI... Ndo maana Sprite wanasema TII KIU YAKO. Sasa mi nasema TII SAUTI YA NDANI YAKO na utashangaa toka hapo hutajitaji alarm ikuamshe utaamka mwenyewe tu. Kwani jogoo huwa anaamshwa na alarm? Yeye ndo alarm clock. Sasa ukitii sauti ya ndani utashangaa wewe ndo unakuwa ALARM CLOCK.
Usifanye kitu kwa kuogopa watu watakuonaje kama hutafanya. Kuna watu wakiona RANGE ROVER inapita huwa wanasema: DAH MUNGU ALIUMBA VICHWA AISEE. Utukufu unaenda kwa Mungu. Kuna watu wakila KFC huwa wanamtukuza Mungu. Kuna watu wa wakipanda ndege au wakiimba wimbo wa TAIFA au wakilala hoteli nzuri nzuri au wakinunua iPhone huwa wanajisemea dah Mungu aliumba vichwa. Hayo yote na mengine ni zao la watu WALIOTII SAUTI YA NDANI MWAO. Kuna watu wanapaswa waogeee au kusafishia nyumba sabuni yako halafu ile harufu tu mtu anaisikilizia anamtukuza Mungu. Lakini wewe unataka kukata tamaa. Eti huwezi kuuza sabuni.
Kuna mtu mwingine.. Robin Sharma.. aliacha sheria pia baada ya sheria kumpa stress za kutosha akapata MSUKUMO kuandika kitabu kinaitwa MEGA LIVING ili kusaidia watu jinsi ya kumanage stress. Kisha akaandika THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI
na THE LEADER WHO HAD NO TITLE na akagusa maisha ya mamilioni ya watu na baadaye kukodiwa na mpaka makampuni makubwa duniani kama NIKE, MICROSOFT, PwC, HP ili afundishe viongozi wa hayo makampuni na wafanyakazi wao. Unakuta analipwa hadi dola laki tano kwa saa na anafundisha masaa matano. So siku hiyo moja anakuwa ameingiza dola milioni moja na nusu. Yani bilioni tatu za kitanzania kwa siku moja. Hiyo ndo THAMANI anayopewa mtu aliyetii sauti ya muumba wake kutoka ndani.
Ndege huimba kwa msukumo ulio ndani yao. Siyo kwa kuwa ndege wenzake watamwonaje asipoimba. Wewe unafanya vitu ili watu wakuelewe? Yesu hawakumwelewa watakuelewa wewe? Mimi huwa naandika tu sijali atakayeshindwa kuelewa nachosema. Naangalia msukumo ulio ndani ukiniambia andika kuhusu hiki naandika. Hata ikiwa saa saba za usiku.
Ukitazama watu wangapi wanaafiki ndo ufanye kitu wakati moyoni mwako tayari kuna mwafaka ujue hiyo ni dalili ya WOGA na kutotii. Kumbuka kitabu kinasema UTII NI BORA.
TII SAUTI YA NDANI YAKO
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp #o788367511
All Calls and SMS #o752367511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)