Ijumaa, 14 Oktoba 2016

JAMBO LA NNE (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA NNE
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)


TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 4.


4. JAMBO LA NNE:
MSHAHARA NI PATO LENYE MAKATO MENGI NA KODI KULIKO MAPATO MENGINE YOYOTE (A SALARY IS THE MOST TAXABLE INCOME)


So, how's Nyerere Day my peoplezzz???

I hope iko vizuri. Basi kwangu pia iko vizuri. Hii picha inanikumbusha utotoni. Ilikuwa sebuleni enzi hizo hata sijui Mwalimu Nyerere ndo nani.
Anyway tuachane na picha.


Ila leo nina swali kidogo?
Hivi ni nani aliyebuni mifumo hii ya kodi tuliyo nayo leo?

Aah basi ngoja tu niende straight.

Ni hivi. Ni vigumu kwa mwajiriwa kufikia uhuru wa kipato kwa sababu kitu kinachoitwa mshahara kinaliwa na midomo mingi mno. Mshahara unaliwa na midomo lukuki kabla "mabaki" hayajakufikia wewe. Sijui unanielewa? Unachokipata ni MABAKI ya kitu unachozalisha. Yani kama unazalisha 100% basi ukipata saaaanaaaaaa ni 20%. Otherwise utapata 15% au in most cases 10% ya kitu unachozalisha. Sasa kama unafurahia 10% ya kitu unachozalisha na una elimu ndefu ya kusoma digrii na KUFANYA masters basi kuna shida fulani mahali fulani. Hii ndiyo sababu nyingine kwa nini mwajiriwa yeyote amebanwa. Ulishawahi kuishi "uswazi"? Hahaaa yani uswazi ukimfata mtu ukafikiri hiyo anayopita ni njia inaendelea mbele unashangaa inaishia nyumbani kwake. Khaa! Au chooni kwa mtu. Huamini? We wa kishua ee? Haya ngoja nikupe mfano wa kishuashua basi. We si unajua barabarani kuna alama za barabarani. Kuna njia zingine ukienda unakutana na kibao kinasema: HAKUNA NJIA! Umenielewa sasa? Ndo hivyo na kwa mwajiriwa. Njia ya kuelekea mtaa unaoitwa "UHURU WA KIPATO" ukitokea mtaa wa KUAJIRIWA unakutana na alama ya NO ENTRY. Hapo unageuza tu njia unarudi ulikotoka.
Sijui unanielewa??

Nimetafakari kwa muda na kujifunza mambo haya kwa kina. Ni kwamba watu walio design TAX SYSTEM yani mifumo ya kodi duniani hawakuwa maskini bali "wenye nazo". Sasa unadhani walidesign mfumo wa kodi umnufaishe nani kati ya maskini na tajiri?
Kati ya mwajiriwa na mwajiri?

Ngoja nikupe mfano:
Mwaka jana ulifanyika utafiti nchini Marekani wa jinsi matajiri na maskini wanavyolipa kodi. Ilidhihirika kwamba 20% ya Wamarekani (ambao hawa ni watu wa kipato cha chini) hulipa kodi  10.9% ya mapato yao.
Halafu kundi la watu wa kipato cha kati (yaani Middle Class People) wanalipa 9.4% ya kipato chao kama kodi.
Lakini the top 1% ya Wamarekani (hawa ni matajiri) wanalipa only 5.4% ya mapato yao kama kodi.


Sasa hii iko duniani kote generally. Kwamba mfumo wa kodi uko UPSIDE-DOWN. Aliyetakiwa kulipa kodi kidogo ndo analipa sana. Anayetakiwa kulipa nyingi analipa kidogo. Na hii in a way unakuta ina mantic yake. Yani kwamba asilimia 5.4 ya kodi ya mapato ya Bill Gates ni kiasi gani? Nyingi si ndiyo. Kwa hiyo ili usimvunje moyo wa kuongeza ajira nk bora ukubali hiyo halafu kodi nyingine utawakata wafanyakazi wake kidogo kidogo. Ila hiyo kidogo kidogo ni nyingi mno kwa huyo mwajiriwa. Lakini sasa ufanyeje. Ndo waajiriwa hawana pa kutokea.

Na bahati mbaya kuna misamaha ya kodi kisheria kabisa kwa matajiri na wawekezaji. Hujawahi kusikia? Of course umewahi! Lakini kwa waajiriwa HAINAGA USHEMEJI WANAKATAGA. Nani akusamehe kodi? Thubutu!!

Sasa usipokuwa na maarifa ya hivi vitu utaendelea kudai mshahara uongezeke kumbe hakuna cha maana unachodai. Unaoperate katika mfumo ulio kinyume chako already. Afu unafunga na kuomba Mungu akusaidie uongezwe mshahara. Yani ni sawa na mtoto wa shule kulilia kuwa class monitor au monitress. Hiyo haikufanyi ufaulu mitihani zaidi ya wenzako. Mfumo wa kufaulu ni ule ule. Mama Ndalichako hajuagi huyu alikuwa head boy au head girl. Anachoangalia ni maksi tu. Sasa kulilia kupanda cheo mara ukafanye mastaz ya watu unaisumbua tu kisa unataka kupanda cheo kumbe unajilisha upepo tu.

Tazama mfano huu:

Tarehe 1 mwezi Mei (Mei Mosi) ambayo siku hizi imegeuka na kuwa siku ya WAAJIRIWA badala ya siku ya WAFANYAKAZI. Waajiriwa wameiteka. Hahaaaa. Undava undava.

Anyway. Tarehe 1.5.2016 (mwaka huu) Rais wetu mpendwa Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli alitangaza kuwa MAKATO yanayojulikana kama PAY AS YOU EARN (PAYE) yatashushwa kutoka 11% hadi 9%. Basi ukipenda katafute clip jinsi wafanyakazi, I mean sorry, WAAJIRIWA jinsi walivyoshangilia. Utafikiri sasa unafuu wa maisha umewadia. Yani kama yale maisha bora ya Mhe. JK sasa yamewasili. Lakini je ni kweli?

Tazama hapa kidogo:
Kwa kawaida kwa sasa mshahara chini ya TZS 170,000/- hauna makato. And you can tell why? Sasa huyo si kwamba serikali haitaki kumkata. No. Inataka ila sasa ifanyeje huyu mtu naye aishi. Angalau nauli na hela ya kula asikose.

Lakini kiuhalisia ukichunguza kiundani kwa jicho fulani hivi la mbali utagundua kama makato yake atayabeba mtu mwingine. Sijajuaga ni nani ila huwa nahisi hivyo eti.

Anyway. Tuendelee. Mshahara wa kuanzia TZS 170,000/- hadi 360,000/- ambao ndo ulikuwa ukikatwa PAYE ya 11% ndo Mhe Rais alitangaza kuwa itapungua hadi 9%.

Narudia si kwamba serikali haitaki pesa. Inataka. Lakini kuna mahali kwingine inakuwa inakata kureplace hicho ilichoki-relinguish! Think my friend. It's still LEGAL to think.

Haya mshahara wa kuanzia TZS 360,000/- hadi 540,000/- utakatwa PAYE hiyo mpya lakini hapa kuna Excess Charge ya 20%!!!!! Mayooooooo!
Na mshahara wa TZS 540,000/- na kuendelea una hiyo PAYE na Excess Charge ya 25%!!!!!!

Sijui unaelewa? Sasa umepunguziwa 11% to 9% ya PAYE but mshahara wako una Excess Charge of that magnitude. 
Tuendelee kidogo. Ukiachilia hayo but pia kwa kuwa "huwezi kujitunza uzeeni wewe mwenyewe" basi unalazimishwa kutunziwa pesa zako kama SOCIAL SECURUTY FUNDS.
Makato mengine hayo.
Ulisoma Chuo? Mkopo wa watu umelipa?
Makato mengine hayo.
Makato lukukiii..
Ndo maana siku zile wakabaki wameshika mabango SHEMEJI UNATUACHAJE? Heee! Sasa sijui huyu wa sasa akitoka wataulizaje? Sikia rafiki.. Mfumo wa ajira haunaga USHEMEJI ndugu. 


Kumbuka hakuna maduka ya waajiriwa na wafanyabiashara. Au unadhani siku ukistaafu utakuwa unanunua sukari duka tofauti. Duka la wastaafu.

Sasa ukizingatia makato hayo yote hapo juu na ukija kufikiria kuwa wewe ndo unayezalisha pesa ya umeme, maji, kodi ya jengo ili mwajiri wako amudu vyote hivyo. Na wewe ndo unazalisha FAIDA ya shareholders kama upo kwenye corporate setup. Utaelewa kwa nini wewe ni kama punda fulani hivi ambaye watu husema bora punda afe mzigo ufanyeje.....?
Watu wana maneno!

Sasa Mungu akufanyeje? Akubebe! Jifunze kutumia mfumo mwingine ili ufike mtaa wa  uhuru wa kipato! It's that simple.
Even if it's not easy.

Nadhani unanielewa. Ndiyo maana leo NYERERE DAY 2016 nikakumbuka kumbe wakati Mwalimu anaaga dunia nilikuwa nina mwaka mmoja toka kuja jijini hili la "Darisalama" (kwa sauti ya Paul Makonda). Ni wakuja mimi mwenzenu.. hahaaa. Nikawaza kuwa kumbe wakati Mwalimu anaaga dunia kuna watu walikuwa ndo wamepata ajira zao za kwanza walitoka kibaruani siku ile tukakimbia nao kuelekea Msasani wakati huo mi hata msasani sijui ni wapi wakuja miye. Natiririka tu. Anyway.Ukipiga mahesabu mpaka sasa ni 17 years right? Lakini kumbe kuna watu wakati Mwalimu anaaga dunia walikuwa kwenye ajira kwa miaka 8 tayari au zaidi. Means mpaka hivi leo wana "kajubilei" fulani hivi ka kudumu kwenye mfumo wa AJIRA kwa miaka 25!!! Watu hao ambao wamedumu kwenye ajira tofauti tofauti wakiishi kwa kutegemea ajira kama MAIN SOURCE ya kipato chao mpaka sasa ukiwatizama HAWANA dalili yoyote ya kuwa wanaelekea kufikia ule mtaa wa UHURU wa kipato.

Kama wewe ni mwajiriwa jiulize uko mbali kiasi gani kufikia "kajubilei kako" ka miaka 25 ya ajira. Na ukifika huko utakuwa umesogea kiasi gani kufikia financial freedom. Wengi husema  aah mimi siwezi kuajiriwa miaka 25 wewe. Kuna mtu anasema: Mimi siyo "bw*ge" mimi. Mi ntaajiriwa miaka hii???" Hapo anaonyesha vile vidole vya Chadema. I tell you kuna watu nakutana nao wanasema hivyo. Utashangaa anakata miaka minne, mitano, sita, anahamia kampuni X anakata mwaka mmoja huko ukikutana naye anakwambia "Saivi NAFANYA Masters!" Afu hivi masters huwa "INAFANYWAJE" hata sijui. Akirudi na Masters yake mshahara unapanda kidooogo labda imeongezeka laki mbili hapo juu. Anakutana na EXCESS CHARGE.

Na akitaka kuacha kazi anaambiwa SOCIAL SECURITY FUNDS unaweza ukapata ukifika miaka 55. Anakuwa "MPOULEY".


Anyway.. Leo nisikuchoshe na maneno mengi. Usije kuchelewa kwenda kula batazzzzz...

But bottomline is...
Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa zote kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 4 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Don't read them in isolation.

Na bado zingine 6.
Endelea kuwa na mimi.


But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 4 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA TANO.


Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!


Semper Fidelis,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Alhamisi, 13 Oktoba 2016

JAMBO LA TATU (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA TATU
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)


#TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 3.


3. JAMBO LA TATU:
AJIRA NI AINA MPYA YA UFUGAJI (EMPLOYMENT IS JUST A FORM OF DOMESTICATION)

Duniani hapa kuna watu wanafuga vitu vingi sana. Kuna watu wanafuga nywele, kuna watu wanafuga kucha, kuna watu wanafuga wanyama, nk. Na kuna watu wanafuga WATU.

Sasa katika kundi hili la watu wanaofuga watu si ulishasikia kuwa kuna watu wanafuga sijui majambazi, sijui wanafuga magaidi, sijui wanafuga nini. Point yangu hapa ni kuwa kumbe mtu anaweza kufugwa. Tena kwa RIDHAA yake. Na kwa yeye mwenyewe kutuma maombi ya kufugwa. Na akikubaliwa maombi yake anaweza kutoa hadi sadaka ya shukrani. Sasa kwa nini naeleza mambo haya ni kwa sababu naongelea vitu nilivyoobserve na kujifunza kwa muda mrefu vinavyosababisha watu walioajiriwa hata wakiwa na potential kubwa kiasi gani kichwani lakini anaishia katika maisha duni sana hasa uzeeni. Hawezi kamwe kupata uhuru wa kipato. Shida ni nini licha ya bidii kubwa na kujituma kwingi na elimu ndefu... Anhaa nikajifunza kuwa shida nyingine hapa ni hii ya kutojua kuwa na yeye ni MFUGO. Anafugwa. So wewe unadhani ni kipi kizuri kufuga: kuku au mtu? Anyway. Tuendelee.

Sasa ili ufuge kitu na kifugike lazima ukipe incentive. Kwa kuwa naongelea mifugo nitalazimika kutaja majina au aina za wanyama wanaofugwa. So naamini wasomaji wangu ni watu wazima wenye uwezo wa kuchambua na kuelewa kuwa hiyo ni mifano tu ili kufikisha ujumbe.

Sasa tuendelee. Yes. Ili ufuge kitu na kifugike lazima ukipe #incentive. Hata kama unafuga kucha lazima uzipe incentive ya kuendelea kubakia. Nywele pia. Lazima uzipeleke saluni, uzilishe vizuri, nk, nk. Kama unafuga wanyama kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku, bata, mbwa au paka lazima uwape incentive ili wawe na amani ya kuendelea kuwepo.

Ndivyo na ilivyo katika kufuga mtu.

Bahati mbaya haya mambo watu wengi hawayatilii maanani sana japokuwa yanagusa DESTINY zao. Future zao. Kesho zao. Ndoto zao. Hatma za maisha yao. Uzee wao. Wanachofurahia tu ni zile incentive za muda wanazopata for the time being. Wanasahau kuwa mfugo ni mfugo tu.

So tragic.

Unajua kuku hata afurahi vipi kupewa ulezi na vyote avipendavyo mwisho wake unajulikana. Ngombe wa maziwa hata aletewe majani mazuri kutoka vile viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au kutoka kokote kule kwenye rutuba zaidi ale ashibe afurahi bado destiny yake (as far as kufugwa kwake is concerned) ni KUPRODUCE MAZIWA kwa mfugajimfugaji

Sasa ni #hatari sana kwa huyu ng'ombe kuridhika na kuletewa majani mazuri na maji na kuoshwa na kusafishiwa banda lake akaridhika. Lakini kwa kuwa ni NG'OMBE hilo hatuna shida nalo.

Lakini sasa vipi ikiwa ni binadamu??

Akaridhika pia kuwekewa banda (office cubicle)
, na kuletewa lunch, na maji ya bure bure kwenye dispenser, na kuwekewa dawati, na computer na kuwekewa umeme, nk..? Na akasahau kuwa anapewa vitu hivyo kama incentive tu kidogo ili AKAMULIWE MAZIWA TENA YA KUTOSHA. Tena not once or twice. Ata-produce hayo MAZIWA mpaka siku yakiisha anaambiwa sasa umri wako umeenda unapaswa ukakae na familia uangalie mambo yako na wewe.
Can you imagine that?

Sasa nikuulize, tofauti ya huyu binadamu na yule ng'ombe ni ipi hasa? I mean, with due respect. Lakini waajiriwa wengi hawajioni hivyo. Wanadhani mwajiri wao ana shida na wao. Kumbe shida yake ni MAZIWA. Hawajui kwa nini siku wasipotoa maziwa ya kutosha kwa nini mwajiri anakuwa mkali. Wengi wao wako so brainwashed kiasi kwamba mwajiri akifoka hata kama sababu siyo za msingi wanakosa amani siku nzima. Hata wangekuwa wameshika dini vipi. Mindset.

Sikia my friend. Mindset yako ikikamatwa sawasawa utabadilishana ardhi yako na mtu anakupa kioo. Wazungu hawakututawala physically kwa sababu walikuwa na miili ya kutisha ila ni kwa sababu walijua kucheza na MINDSET tu. Na hata sasa wanatutawala kiuchumi kwa sababu wanajua sana hii kitu mindset. Wanajua kucheza na ufahamu! Africa is still fast asleep. Ndivyo na waajiri walivyo. Wanajua kucheza na mindset. We angalia kiongozi wa juu wa kampuni au shirika kubwa kabisa hapa kwetu ambalo nibla kimataifa tena awe mzungu labla akija kutoka huko Ulaya kulitembelea hilo shirika na akampongeza mwajiriwa yeyote na kumsifia na labda kumpa zawadi ya labda Tsh milioni moja kwa utendaji mzuri. Tena hiyo milioni yenyewe iwe katika dola. Afu mzungu ndiye aombe kupiga picha ya ukumbusho na huyo mbongo. Weee! Huyo mtu anaweza kufia kwenye hilo shirika au hiyo kampuni. Hata angekuwa na ndoto za kuanzisha biashara yake mwenyewe. Hatoki. Why? MINDSET. Hapo mzungu kacheza tu na mindset. Utatoa MAZIWA mengi mno tena hata bila kukamuliwa sana.

Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa kuna sayansi ya kupata nyama nzuri kutoka kwa ng'ombe wakati wa kumchinja. Nilishangaa. Au kupata MAZIWA bora kabla ya kumkamua. Kumbe SIYO suala tu la kumlisha vizuri. Akasema nchi za huko wanachofanya siku ya kumchinja ng'ombe wanamtreat vizuri hajawahi kuona. Yani wanampet pet na kumpa vitu vizuri mno. Yani mwili wake unakuwa very relaxed.  Ng'ombe mpaka anafika machinjioni haoni hata dalili ya kumtia hofu hata kidogo. Amerelax. Mwili uko vizuri. Na akasema ukimtreat ng'ombe vizuri mwili wake huwa unarelease kemikali fulani za muhimu kuifanya nyama yake iwe bora zaidi ukimchinja wakati huo akiwa katika hali ya kurelax! See?

Sasa akanambia ng'ombe akishakuwa amerelax kuna vitu bado vinampet pet huku anaogeshwa mgongoni "anafurahi" akiwa amewekwa sehemu ambayo hawezi kutikisika (yeye hajui)sababu yupo katika mazingira masafi kweli kweli hasikii harufu yoyote ya damu nk hapo ndo inashuswa the SHARPEST BLADE shingoni kwake. Yani hakuna nukta ya ng'ombe kuona kilichotokea. Unaambiwa hapo unapata the best meat.

Alooo! Nikashangaa. Huku kwetu ng'ombe hadi afike machinjioni ameshapigwa stiki kuliko zile alizolamba yule denti.. teh teh.. Ndo unakuta nyama ya ngombe ya leo leo lakini khaa! Kama ya jana. Anyway point hapo ng'ombe kadanganywa. Akadhani anapendwa sana. Kumbe loooh. Siku ya ng'ombe kupendwa sana ndiyo....malizia.

Sasa mazingira hayo hayo ndo huwazunguka waajiriwa wengi. Wanadhani wanapendwa. No. In a point of fact kinapendwa unachoproduce. Acha kuproduce uone. Utapewa majina mabaya hujapata kuona. Au akipatikana "ng'ombe" anayeweza kuzalisha MAZIWA mengi zaidi yako tena kwa muda mfupi utafanyiwa visa hadi utoke mwenyewe. Unabaki kusema "Namwachia Mungu". Unamwachia Mungu? Wakati unaletewa majani kwenye banda hukujua kuwa anayekupa hayo majani ana kitu anataka kwako?


So kwa ujumla wake mazingira hayo ya kufugwa hayawezi kumpa mwajiriwa yeyote uwezo wa kufikia UHURU WA KIPATO.

Angalia watu wote waliofikia uhuru wa kipato. Wanafugwa na mtu yeyote? Jibu ni hapana. Hayupo tajiri yeyote duniani ambaye KAAJIRIWA. Why not? Ni kwa sababu wanajua kuwa kuajiriwa is tantamount to kufugwa. Ni sawa tu na kufugwa. Yes. Unapewa kila kitu unachohitaji ili kumzalishia mtu mwingine anachohitaji yeye. Sasa nani kati yenu atakuwa na financial freedom siku moja? Think about it.

Ukiwaangalia waajiriwa wengi ambao wamegeuza ajira kuwa ndiyo DESTINY yao unaweza kuona kati yao kuna baadhi (ASHAKUM SI MATUSI) wameanza kubehave kama kuku, au bata, kondoo, mbuzi, ng'ombe nk. Afu mwingine kwa sababu anajiona katika mifugo wenzake yeye ndo mwenye mwili mwili mkubwa kama ng'ombe (ana cheo)
 anahisi yeye hawezi kuwa kama kuku. Anasahau kila mtu ana produce cha kwake. Mwingine mayai, mwingine MAZIWA. Na wote mwisho wao hawaujui kamwe.


Hilo ni jambo la kuzingatia sana kama wewe ni mwajiriwa ama wewe ni mwanafunzi unayesoma ili kupata ajira au ni graduate unalilia ajira. That's the future you're crying for. Nakushauri kaa chini angalia nini Mungu aliweka ndani yako kisha mwombe akusaidie jinsi ya kukitimiza. Vijana wengi wamekuwa so BRAINWASHED kuwa wanasoma ili wakaajiriwe. Na hii inaanza mbali. Nani analeta hii brainwashing kama siyo WAFUGAJI? Mind you ukipenda kufugwa ukafikiri umefika kwa sababu unahisi wewe ni jogoo (cheo) wengine ni kuku wa kawaida. Au kwa kuwa wewe banda lako linawaka taa 24/7 na misosi nje nje
wakati wengine wanalala banda lenye giza na msosi wanatafuta mwenyewe mara waliwe na mwewe mara wajifiche ukasahau kuwa wewe ni kuku tu wa kisasa wao wa kienyeji ila nyinyi nyote ni kuku tu basi kuna shida katika fahamu zako. Kwa kuwa wewe umeajiriwa UN mwingine kaajiriwa gereji unahisi uko vizuri eeh. Sawa.

Anyway..
Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa zote kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya tatu zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA.
Na bado zingine saba!
Endelea kuwa na mimi.


But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 3 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM.
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA NNE.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS and Calls: +255752366511
WhatsApp: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com (ndo hii)

Barikiwa!


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumatano, 12 Oktoba 2016

JAMBO LA PILI (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA UWEZO MWAJIRIWA YEYOTE KUTOWEZA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA PILI
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA UWEZO MWAJIRIWA YEYOTE KUTOWEZA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)


TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato). Naamini u mzima na kwenye afya bora.

Ambatana nami tena kidogo hapa...


2. JAMBO LA PILI:
AJIRA HUMPA MTU UZOEFU FINYU (LIMITED EXPERIENCE)

Nimekuwa nikizungumza na waajiriwa wengi (hasa wale ambao ninawaona kuwa wana potential kubwa sana ya kufanya mambo makubwa hapa duniani) na nimekuwa nikiwa-challenge kuhusu kuchukua hatua na kuanza kutendea kazi ndoto zao. Wengi wao huniambia tu "Of course mi nimeajiriwa kupata tu experience (uzoefu) kisha nitaenda kufanya mambo yangu". Na hata wanafunzi wa vyuo ambao nimekuwa nikiongea nao kuhusu kutotegemea ajira tu wamekuwa wakiniambia wanataka kuajiriwa kwanza wapate uzoefu na mtaji (hapa huwa najichekea kimoyomoyo) kisha waende wakafanye mambo yao.

Sasa ukitazama watu wote waliofikia kuwa na UHURU WA KIPATO yani uwezo wa kufanya chochote anachotaka kinachohitaji pesa, wote wana kitu kingine in common. Wana EXPERIENCE ya mambo mengi sana na ukibahatika kukaa nao unaweza kushangaa sana na ndo utafahamu kumbe hawajafanikiwa kwa bahati mbaya.
Lakini mtu ukiwa mwajiriwa hilo ni jambo gumu kuwa nalo (kupata uzoefu mpana). Labda nitoe mifano kidogo.

Ukikaa na mtu aliyefanikiwa sana kifedha unaweza kuanza kujiukiza amejuaje kuhusu mambo ya kitaalamu kama haya huyu mtu? We elewa tu. Imemchukua miaka mingi ya kujaribu vitu tofauti tofauti na kupata huo uzoefu. Tofauti na mtu aliyeajiriwa.

Mfano:
Mtu umeajiriwa MAPOKEZI.
Uzoefu wa kazi ya mapokezi ni pamoja na:
kupokea simu,
kupokea wageni,
kuwaongoza wageni pa kuelekea,
kuwaitia wageni wenyeji wao,
kuchora mistari kwenye daftari la wageni ili waweze kusaini,
kuwapa watu funguo kwenda vyumbani kama ni hotelini,
kupokea barua za field au za watu wanaokuja kuomba kazi kama ni mapokezi kampuni,
na vitu vya aina hiyo.

Now that is a very limited experience kwa mtu anayetaka kufikia uhuru wa kipato. Uhuru wa kipato hauji kwa mtu ambaye kitu ambacho ana uzoefu nacho ni kupokea wageni tu vitu na vya aina hiyo. Yani hajui chochote kuhusu:

~ kutafuta masoko (wateja). Maana yake huyu hajui pesa inakujaje?
~ kutunza fedha na mahesabu
~ kubuni bidhaa mpya au huduma mpya za kuwapa wateja siku zijazo
~  Utatuzi wa migogoro ya wafanyakazi unafanyikaje hajui
~ Hajui IT wanafanyaga nini huko nyuma hana idea angalau kidogo tu ya kawaida ikamsaidie kujua siku akitaka kufanya "mambo yake mwenyewe"
~ Nk.

Kama ni mhasibu wa kampuni au mwanasheria wa kampuni hajui chochote zaidi ya kutunza fedha au kusimamia kesi. See? Very limited.

Sasa basi kwa kuwa kipato chake kinatokana na uzoefu huo finyu ndo maana siyo rahisi kwake kukua zaidi kifedha. Ili kukua kifedha inabidi uwe na ufahamu na UZOEFU MPANA wa mambo yanayohusiana na fedha ikiwemo kupokea wageni kutangaza bidhaa au huduma zako, kutatua migogoro, kutafuta wateja, kutunza fedha, nk, nk.

Sasa simaanishi kuwa wewe ndo uvifanye hivyo vitu kila siku hapana. Namaanisha uwe na uzoefu navyo hata kama uliwahi kufanya kwa mwezi mmoja ukaacha au kwa wiki moja kujifunza tu au kwa mwaka, nk. Kama kweli unataka kufikia uhuru wa kipato badaye kama sasa hivi wewe ni mwajiriwa basi amua hata kujitolea BURE kwa muda wako wa ziada kufanya kazi kwa mtu hata for free ambayo ni tofauti na ile unayoifanyia kule ulikoajiriwa. Fanya tu. This is an INVALUABLE advice I'm giving you right here. Trust me. Utajifunza vitu vingi kudeal na watu wapya katika eneo ambalo siyo COMFORT ZONE yako kazini. Mfano wewe ni IT personnel kazini kwako. Omba kwa mtu binafsi uwe unasaidiana na reception wake kupokea wageni, nk. Ni kama kitu cha kijinga we. But do it. Mwambie just one month. Or one week. Kinachotafutwa ni wewe kupata uzoefu angalau kidogo lakini wa mambo mengi. Of course ukiweza kupata uzoefu huo tofauti kwa muda mrefu zaidi utajua mambo mengi.

Sasa siku ukija kuanzisha biashara yako unakuwa una idea kuhusu wageni, una idea kuhusu fedha, masoko, IT. Hufanyi wewe, umeajiri watu na wala hujui terminologies za Marketing kama wao lakini YOU HAVE AN IDEA WHAT THEY ARE SUPPOSED TO DO. Hakuna tajiri mbumbumbu kwa taarifa yako. Hata kama hajaenda shule. Usifikiri shule ndo kipimo cha ufahamu. Kuna watu wana Masters ya Biashara na wanachokijua ni terminologies tu na Theories lakini kuna mtu anauza mahindi Iringa hata mlango wa darasa la saba hakubahatika kuusogelea ila anafahamu kuhusu mbegu bora, msimu bora, wateja wakoje na jinsi ya kudeal nao, usafirishaji upoje, serikali ikibana hela ufanyeje, pombe za kienyeji zinazotumia mahindi zina effect gani kwenye bei ya mahindi, ufanyeje ili upate masoko ya mbali, ufanyeje mteja anapokuja unampokeaje, unamkaribishaje, ufanyeje ukipeleka hela benki hata kama hujui kuandika wala kuweka sahihi unachoweza ni dole gumba tu ila una milioni 100. See? Sasa wewe kafanye hiyo biashara na Masters yako wakati unachokijua kwa uzoefu wa ajira ni kuandika ripoti yenye terminologies nzuri nzuri na kiingereza chako cha Babbrojohasen sijui ile babra nini. Utashangaa utajikuta unaangukia pua na unalazimika kuanza moja kabisa licha ya elimu uliyonayo kwa kuwa una LIMITED EXPERIENCE. Na ndo maana waajiriwa wengi wanashangaa mtu akiwa anafanya biashara na bado hajawa milionea toka ameanza. Wanamcheka. Hawajui yupo kwenye mchakato wa kupata huo uzoefu. Wao wanataka wakianza biashara iwe level sawa na pale kazini alipoajiriwa. Thubutu. Muulize mwajiri wako. You must gain vast experience first..

Sasa UZOEFU huwa unakuja kidogo kidogo kwa muda mrefu. Ndo maana matajiri wengi utasikia kaanza "ZAMANI". Alianza anauza sijui mihogo. Uzoefu. Alianza anauza maandazi. Uzoefu. Mwingine utasikia alianza anasafirisha mizigo ya watu kwa baiskeli. Uzoefu. Kuna huyu jamaa mmiliki wa Peacock Hotel ambaye anasema alianza kwa kuuza karanga. Uzoefu.!! Joseph Kusaga wakati ameanza si alikuwa anapigisha muziki tu kwenye kumbi za Starehe? Leo hii Clouds Media ni media house ya maana. Na tena wakati anaenda kusajili jina la redio yake watu wakawa wanacheka eti MAWINGU (CLOUDS) FM. Yaani mawingu. Wanamwona wa ajabu.  Uzoefu. Ana uzoefu wa kuchekwa pia.  Waajiriwa wengi wanataka utajiri uje tu ghafla. Anadhani kwa kuwa amefanya kazi benki miaka mingi na yeye ataanzisha benki tu ghafla. Anasahau kuwa hapo malipo sasa ameajiriwa kuhesabu pesa za watu tu na kugonga mihuri. Limited experience. Hajui hizo pesa zinakujaje? Hajui zinapelekwaga wapi? Hata mihuri hajui inatokaga wapi na ni sh ngapi na kwa nini? Anachojua kunyanyua muhuri na kukandamiza kwenye karatasi. Hajui kwa nini wateja wanakuwa wengi au siku zingine wachache. Anafurahi kupewa tips za elfu 20 au hata dola 100 na mapedeshee wanaokuja kuleta hela. Anasahau hana experience kama wao. Anabaki kusema wanauza unga. Yani kila MTU mwenyewe hela nyingi ni Unga au Freemason.. Akili za kichawi kichawi tu kichwani. Na mawazo finyu.

Waajiriwa wengi ni watu VEEERY POTENTIAL kubadilisha hata Uchumi wa nchi au dunia. Lakini shida wamekubali kuishi kwa LIMITED EXPERIENCE.  Na wanamwamini Mungu kuwa IPO siku na wao watakuwa na uhuru wa kipato. Sikia my friend. Biblia inasema hata shetani anaamini Mungu na kutetemeka. But Mungu ni Mungu wa KANUNI. Mtafute MTU anaitwa MGISA MTEBE anaweza kukufafanulia zaidi hili la Mungu wa kanuni ndo utajua kwa nini wapagani wanafanikiwa na kwenye dini zao na Mungu wao wapo macho kodo!


Anyway..
Kama ulisoma makala yangu ya jana iliyoelezea kuwa limiting factor ya kwanza kwa nini mwajiriwa hawezi akafikia Uhuru wa kipato ni kwamba kupata pesa you must show up. Then unganisha ni hii ya pili kuwa you will show up but you end up with limited experience. Utaanza kuona kuwa zote mbili zinafanya kazi against you.
Na bado zingine nane!
Endelea kuwa na mimi.


But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha pili cha kumzuia Mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM.
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA TATU.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS and Calls: +255752366511
WhatsApp: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com (ndo hii)

Barikiwa!


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO

MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO


UTANGULIZI:

Nina siku 10 kuanzia leo ambazo kwa neema ya Mungu nitashare mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia uhuru wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Ninapozungumzia uhuru wa kipato ninachomaanisha ni uwezo wa kufikia hatua pesa ikawa siyo tena kikwazo cha kufanya chochote unachotaka kufanya. Mfano ukihitaji kununua kitu chochote basi pesa isiwe ndo kikwazo. Mfano unahitaji kununua labda gari lolote mfano LANDROVER la make yoyote mfano RANGE ROVER la rangi yoyote mfano RANGE NYEUPE (ranla mwaka wowote mfano toleo la mwaka ujao 2017 basi kikwazo kisiwe ni pesa. Huo ndio uhuru wa kipato. Ni mfano tu. Au unahitaji mwanao asome shule yoyote yenye ada yoyote hata kama ada ni milioni 30 kwa mwaka kikwazo kisiwe pesa. Kama unataka kununua kiwanja au nyumba nchi hii mkoa wowote labda hapa Dar mahali popote labda Masaki au Oyster bay basi kikwazo kisiwe pesa. Hiyo ndiyo Financial Freedom ninayoelezea hapa. Au unataka siku moja umiliki Private Jet. Kikwazo kisiwe pesa.

Ndo nasema kuna mambo 10 yanayomzuia Mwajiriwa kutoweza kufikia UHURU WA KIPATO.


1. JAMBO LA KWANZA:
KUINGIZA KIPATO LAZIMA UWE NA UWEPO KUFANYA KAZI. (YOU MUST SHOW UP PHYSICALLY)


Sasa hili ni jambo la kwanza ambalo waajiriwa wengi huwa hawalitilii maanani. AJIRA ni mfumo mmojawapo wa kutengeneza kipato. Mfumo mwingine ni BIASHARA.

Sasa ajira kama mfumo wa kutengeneza kipato ni mfumo unaohitaji uwepo wako katika eneo lako la kazi ili uweze kutengeneza fedha. Kwa hiyo unalazimika kubadilishana muda wako wa maana (PRODUCTIVE HOURS) kumpa mtu ambaye anahitaji umfanyie jambo fulani kwa kubadilishana na fedha. Sasa kama umeajiriwa naomba nikuulize maswali machache..


SWALI LA KWANZA:
Huoni tatizo katika hilo la wewe kuuza muda wako? Huoni tatizo kuuza kitu ambacho huwezi kukirejesha tena (A NON-RENEWABLE RESOURCE) na wewe kupewa kitu ambacho unaweza kukipata tena (RENEWABLE RESOURCE)? Yes. Muda unaouuza huwezi kuupata tena. Kama umeshauza muda wa masaa 9 kwa siku tano kwa juma kwa muda wa miaka 10 hadi sasa jiulize kama huo muda unaweza kuurejesha tena. Afu unalaumu nchi inauza madini (non renewable resource kama wewe) kwa bei chee kwa njaa ya miaka michache? Are you kidding me?

Hellooo...

Mfano ulianza kazi ukiwa na miaka 30 sasa una miaka 40. Je muda huo wa miaka 30-40 ambapo ndo una nguvu nyingi za mwili na akili iliyoanza kukomaa vizuri na creativity ya hali ya juu na uwezo wa kufanya mambo mengi mapya je unaweza kuurudisha? Jibu ni HAPANA. Muda huo ulishauuza for good! Ni kama almasi za Mwadui. It's gone forever. Miaka kadhaa ijayo ardhi ya mwadui nk itabaki macho kodo!

SWALI LA PILI:
Je fedha ulizotengeneza kwa kipindi chote ulichoajiriwa mfano Tshs milioni 2 hivi ya GROSS SALARY kwa mwezi (hata kama ulianza na mshahara wa 1m or less tufanye tu flat rate ya 2m a month) kwa miaka 10 yani total ya Tshs milioni 240 kwa miaka 10, je hiyo pesa ni impossible kuitengeneza pasipo kuajiriwa? Yani wewe unaona huna uwezo kabisa kabisa wa kuzalisha GROSS income ya Tshs milioni 240 ndani ya miaka 10 kwa njia zingine zozote (halali) bila ajira? Kumbuka hiyo milioni 240 hujapata yote. Kuna ambayo iko NSSF utapewa siku ukifika miaka 55 kama sheria itapitishwa. Is it true kuwa pasipo ajira uliyonayo huwezi kuzalisha pesa ulizowahi kuzalisha toka siku umeajiriwa hadi leo? Au umekuwa brainwashed kuamini kuwa huwezi? Yani kama mwajiri wako ameweza kupata na hana elimu kama ya kwako wala mawazo kama ya kwako wala hajui hata definition ya materminology uliyosoma huko shuleni wala hana kiingereza kama cha kwako cha BabbroJahansen sijui Babbro nini. Wala hana cheti cha Chuo Kikuu wala hata hakumbuki mara ya mwisho darasani alisoma topic gani. Kama huyo kaweza na wewe huwezi basi hiyo ndo tafsiri ya wewe kuwa BRAINWASHED. Na kwa sababu uko brainwashed basi you're not receptive of new ideas. Mindset closed. Na ndo hujui kuwa kitendo cha kupata kipato kwa kulazimika kwenda kufanya kazi kwanza huoni kama ni shida. Hujafahamu kuwa unaweza wewe huyo huyo ukabuni kitu kipya kwa muda wa miezi 6 tu au hata ikikuchukua mwaka au hata miaka mitano na baada ya hapo ukaanza kuingiza kipato 24/7 kama MaxMalipo. Wengine wenu mmeajiriwa mna uwezo wa kuzalisha Tshs milioni 240 kwa mwaka mkiamua. Au hata kwa mwezi mmoja tu. Wengine nyinyi ndo solutiin ya matatizo ya watoto yatima au maji vijijini. Mna miradi mikubwa kichwani but umekaa hapo. Unafurahi kuitwa Meneja Mauzo wa..... Au IT SPECIALIST wa naniliu Tanzania Limited. Nipo hapa kukupa nguvu mpya kuanza safari ya kubuni au kufanya kitu kipya (mfano biashara) ambacho kina POTENTIAL ya siku moja kuja kukupa pesa hata ukiwa umelala is a SIGNIFICANT STEP IN THE RIGHT DIRECTION. Kuliko kuendelea kufanya kitu ambacho hakina hiyo potential kamwe. Kama huniamini mimi fanya hivi:

JIFUNZE KWA MUNGU
Kwa mujibu wa Biblia Mungu aliumba kila kitu kwa SIKU SITA tu. (Mwanzo 2:1) Alichokifanya alivipa tu hivyo vitu uwezo wa ku"REPRODUCE" (Mwanzo 1:28+29).
That's a system ambayo Mungu alitaka tujifunze. Kwamba siyo lazima uumbe kila siku. Unaweza kuumba kwa siku 6 tu na after that ukapumzika (siyo kwa kuwa umechoka no. Bali kwa kuwa umeshaweka SYSTEM ya kukupa results unazotaka. Veeery *SMART.* Isn't it?

Kampuni unaibuni once. Biashara unaianza once. Mradi unauanza once. Hiyo once inaweza kukuchukua six days or even six years etc. But ukishauanza unajenga tu SYSTEM. It is POSSIBLE. Matajiri wanamuiga Mungu. Maskini  sijui wanamuiga nani hata...
Seriously. Maana hata kwenye eneo la #utoaji kuna tofauti sana kati ya makundi haya mawili. Think about it.

So kwa nini usifanye kama Mungu? Create something once and put a system ambayo itakufanya upate kipato 24/7 mpaka siku ukifa wanaendeleza wanao ulipoishia nk. Sasa wewe kila siku unadai unafanya kazi kwa sababu ya Junior. Ooh Junior mwanangu sitaki apate shida. Ok sawa. Sasa hiyo ajira ukifa huyo Junior ndo atapewa kazi yako? Uliona wapi? Umejiandaaje sasa? See. Unatiririka. Sawa. Very good. Endelea tu.

SWALI LA TATU KWAKO:
Tunaendelea. Je hiyo Tshs Milioni 240 uliyoipata ndani ya miaka 10 kwa mfumo wa ajira imeshakupa angalau DALILI yoyote ya kwamba kuna siku utakuwa na Uhuru wa kipato pia? Maybe miaka 10 ijayo tena? Kwamba kwa mfumo huo wa AJIRA utaweza kusomesha mtoto wako shule atakayopenda hata kama ni IST na siyo unayoweza kuafford? Nk. Kuna hiyo dalili? Au unaendelea kutiririka tu kwa sababu "NDO MAISHA BANA". Kweli? Think about it.

Hii ndo shida ya kwanza (first limiting factor) wasiyoiona waajiriwa wengi. Ni wachache mno wanaoona kuwa ni shida. Kwamba pesa haiji hadi uende to a SPECIFIC PLACE ukaperform SPECIFIC DUTIES kwa a SPECIFIC TIME ndipo pesa iingie.

Uliwahi kujiuliza itakuwaje kama utaondoka kwenye mfumo wa kulipwa kwa masaa 9 na ukaweza kulipwa kwa masaa 24? Kama bwana Zuckerberg ambaye analipwa 24/7 awe amelala amesafiri, nk. Kuwaza kuwa ili uingize kipato lazima uende "ofisini" ni traditional thinking ambayo ndo inatafuna jamii hasa vijana wadogo ambao sasa wanasoma ili wakaajiriwe.  Mfumo wa ajira ni an financial dead end.

Usione watu wanahangaika na matikiti na kufuga kuku. Inaweza isimfikishe mbali but ndo hicho nilichosema ni *SIGNIFICANT STEP IN THE RIGHT DIRECTION.* Anajifunza. Huwezi kulingana Nate mawazo huyo. Unajua kitu kipya. Wengine anahitaji tu msaada wa mtaji zaidi au mafunzo muhimu ya kumsaidia. Wewe upo tu kazi yako kucheka. Umesahau *FAINALI UZEENI*. Sikia ndugu. Ukiona mjasiriamali anahangaika usimcheke. Huenda anaumba dunia yake. Na bado yuko "siku ya kwanza" ndo ameumba tu usiku na mchana. Bado huoni kama ksumba cha maana. I tell you wait and see. Salute kwa fighters wote. Keep going. Keep "umbaring" your dunia!💪🏻💪🏻💪🏻

BOTTOMLINE
Bottomline ni kuwa kuingiza kipato kwa mwajiriwa kunategemea yeye KWENDA kufanya kazi. Usikariri. Mungu aliumba Adam, Adam akazaana huko mbeleni. System. Kuzaana ni SYSTEM ya Mungu ya kuumba. Sasa wewe unataka KUUMBA kipato kila siku hadi siku unastaafu? Ukiacha kuumba no kipato. Why? Coz huna system. umesahau kuwa wewe unaoperate kwenye SYSTEM ya mwajiri wako. Ambaye anaweza asije kazini na kipato kikaendelea kuingia kwake. Kaweka system. Wewe ndo ADAM NA HAWA wake. Unareproduce kwa niaba yake.
Amejifunza kwa Mungu.
Wewe umejifunza kwa nani my friend. Mungu huyo huyo?

Hiyo ndiyo kikwazo cha kwanza cha kumzuia Mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM.
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA PILI.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS and Calls: +255752366511
WhatsApp: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com.

Barikiwa!


Semper Fi


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumatano, 5 Oktoba 2016

LIFE BEGINS AT 40.. HOW OLD ARE YOU?

.
*LIFE BEGINS AT 40.... HOW OLD ARE YOU?*

Life Begins at 40..

Huo ni msemo wanao waingereza wakimaanisha maisha yako ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa au toka umefika duniani na toka umeanza kukua nk nk lakini bana maisha #halisi yataanza rasmi siku ukitimiza miaka 40.

Hapo kama bado nauli ya daladala ni ishu, ada, chakula, kodi ya nyumba, nk basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unatumia Facebook kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote.
Nadhani unanielewa sasa hasa wewe ambaye unahisi umri wako bado ni mdogo kwa hiyo bado bado kidogo muda wa kuwa serious na maisha haujafika.
Sikia kijana mwenzangu..TODAY is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.

Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.

Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international school nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!

Hapo ndo unawaza kufuga ng'ombe wa maziwa Kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bizness in Australia. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 300M! Wamejenga mjengo wa ukweli. Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full kutukanwa na makondakta.

Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini mzazi anahitaji support kidogo una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watajua! Halafu unashangaa wenzako wanazidi kuinuliwa. Unaanza kuwaita Freemason.  Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... (Malizia). Wakati wenzako walikuwa wanajenga maisha wewe ulikuwa unashinda Facebook kuongelea UKUTA uwepo au usiwepo.. Harmonize anajua kuomba au hajui. Wema Sepetu atafute mtoto au aache tu. Can you imagine?

Wenzako mkifika miaka 40 watu wa rika lako wana exposure ya uhakika. Wewe at 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe chakula hata virutubisho hakina.  Wenzako at 40 washaacha ajira siku nyingi washatembea dunia na kujifunza maisha kutoka kila mahali. Walishafika kuanzia Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!! Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku Tegeta Posta ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! Unaishi au unaisha?

Acha mawazo mgando. Eti mi nina mshahara mzuri. Mshahara mzuri? Kweli?  Sikia, hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu. Jiandae kusimama mwenyewe. Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini? Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. Don't be afraid. Don't dwell in that comfort zone!! Unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30 ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect. Kisa ulikuwa unafatilia ratiba zote za mechi za mpira na matamasha na mikutano yote ya kisiasa ukasahau muda unaenda. Sasa hivi msimu wa mpira umeanza watu wanatumia muda na pesa kuangalia wanaume wakiwa kazini kwao. Hivi ulishawahi kufikiria lini watu watalipa pesa kukuangalia wewe ukiwa kazini kwako ukiendelea na kazi? Hao unaowafatilia wako ndani ya kazi zao kwa hiyo muda wao unatumikia shughuli zao wakati wewe utatumia muda wako na pesa yako kwenda kuangalia nk. Jenga nidhamu mpya ya kulinda muda wako sasa.

Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime. Kisa? Ulikuwa unatumia muda wote kuangalia vitu vya kuchekesha chekesha na kuongelea mambo ya siasa sijui wasanii sijui msanii gani ana hela nyingi sijui nani kafulia sijui nani ana mimba.. Seriously? Sijui nani hajapendeza kunyoa bora asuke😡😠😠.  Hivi vitu vinaiba muda wako sana ndugu zangu. Mimi mwenyewe nilikuwa hivyo lakini nikastuka mapema sana! Utashangaa umri unaenda bila kupiga hatua. Umri wako ni kila sekunde na kila dakika na kila saa.  Ndo umri huo.  Umri siyo mwaka kwa mwaka. Ni sekunde na dakika. Ndo maana matajiri wanalinda muda wao kwa wivu mkali. Coz TIME IS MONEY.  Utashangaa unapoteza muda afu unafika 40 years ndo unawaza uanzie wapi. Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Hajakupa uuchezee chezee tu. Be careful. Time flies.

Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You? So kama wewe unasema "Mimi bado mdogo.." endelea tu kupoteza muda wako utakumbuka tu siku moja but it might be too late. Endelea tu kupoteza muda na skendo za wasanii. Au unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake. Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira. Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life. Ukifika 40 years uwe very established. Bila hivyo utashangaa kweli. Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya *kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja? Wakati huo wewe unamiliki kigari cha mkopo unakipaki uwanja wa CCM unalipia sh 1000/- tu, mnaita buku. Fikiria vitu kama hivi. Utajua vizuri umuhimu wa kutumia muda wako vizuri.  Ilikuwa January sasa September inabisha hodi. Mwaka unayotumia.  Wewe mwaka huu nini kipya hasa umefanya kimaendeleo. Usiseme nimepata ajira. Ajira haikupeleki popote. Njoo kwetu ujifunze vizuri.

So kama unataka kuhakikisha mambo yanakuwa sawa mapema ungali mdogo ungali na nguvu nyingi bado basi njoo WhatsApp #o788366511 au #o752366511 ukutane na wenzako ambao waliamua kutumia muda vizuri na wakapiga hatua kubwa!
Life begins at 40 my friend.... How Old are you now?


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.

JINSI YA KUZALISHA MUDA ZAIDI ILI KUPATA PESA ZAIDI

SOMO LA LEO:

JINSI YA KUZALISHA MUDA ZAIDI ILI KUPATA FEDHA ZAIDI.

Yes. Unaweza kushangaa mtu anawezaje kuzalisha muda zaidi wakati umefundishwa kuwa muda kila mtu anapewa masaa 24 tu kila siku.
Sasa unaweza kuwa unajiuliza je utazalishaje muda zaidi. Utautoa wapi? Ndo siri za mafanikio hizi sasa ndugu yangu. Zimefichika machoni pa wengi. Mpaka ufanye bidii ya kuzitafuta.

Sasa tunaanza na kipengele hiki cha kucreate muda ambacho  matajiri wengi ndo wanakitumia.

Ni kwamba unaweza kufanya hivyo kwa kununua muda wa wenzako. Yaani kuna mtu ana muda wa masaa 24 kama wewe lakini yeye hana kitu chochote cha kufanya na huo muda ila ana maarifa mengi tu labda kayapata chuo kikuu nk mfano amesomea utunzaji wa kumbukumbu au utunzaji wa fedha. Na yeye hana hizo fedha kwa sasa kwa hiyo elimu yake haimsaidii chochote kama asipopata pa kuitumia. Kwa hiyo wewe tajiri mwenye fedha zinazotakiwa kutunzwa au kusimamiwa unamnunua huyo mtu kwa muda fulani kwa siku. Unampa majukumu (job description) ya kuzisimamia pesa zako kila siku saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni. Anasimamia utajiri wako wa milioni 900 usipotee. Na unamlipa laki 5 kwa mwezi. Hii ndiyo situation ya ajira. Hana cha kufanya na elimu yake anaishi kwa CV. Akiona kwako wewe mshahara mdogo anaenda CRDB anawaambia ana experience ya kufanya kazi kwako wewe Bakhressa. Wao CRDB wanampa ajira awasaidie kusimamia fedha za shareholders (wamiliki) wa benki. Hii ndo ajira. Kwa hiyo basi, ukiweza kununua muda wa masaa tisa tisa ya watu 100 tofauti kwa wakati mmoja it means utakuwa umeongeza muda wako wa uzalishaji  mara nyingi sana. Coz kimahesabu watu 100 wakikufanyia kazi kwa masaa 9 tu kila mmoja kwa siku ina maana utakuwa umepata masaa 900 ya uzalishaji ndani ya masaa 24 ambayo Mungu amekupa. Huyu uliyenunua muda wake yeye amefanya kazi masaa 9 tu kwa siku wewe umefanyiwa kazi ya masaa 900 kwa siku hiyo hiyo moja. Hivi lini atalingana na wewe? Maana itamchukua huyo mtu siku 100 za kufanya kazi kwa masaa 9 kufikisha masaa 900 ya uzalishaji. Lakini ndani ya hizo siku 100 wewe tajiri utakuwa umeshafanyiwa kazi ya jumla ya masaa 90,000! Na itamchukua huyo mtu bila kujali elimu yake siku 10,000/- kufikisha hayo masaa. Yaani takribani miaka 27 ya kufanya kazi kwa mwajiriwa ndiyo inaweza   kumpa utajiri anaozalisha Bakhressa kwa siku 100 tu. Sasa mwambie mwajiriwa mambo kama haya uone. Haelewi kabisaa...! Kisa ni bank teller wa "XYZ Bank". Anafurahia kuvaa uniform za kampuni kubwa. Au ni mhasibu wa "XYZ Clearing and Forwarding" au ni Mwalimu wa "XYZ International School". Unadhani kwa nini tajiri anafungua biashara kila kukicha? Ili anunue muda wa watu wengine weengi zaidi.

Lakini njia hii inakulazimu uwe na mtaji mkubwa ndipo uweze kuajiri watu wengi kiasi hicho. Nadhani utakubaliana na mimi kwa hili.

But kuna namna nyingine ya wewe kuzalisha muda mwingi wa kukuzalishia kipato cha ziada yaani njia ya pili ya kutengeneza hii TIME LEVERAGE yaani kuDUPLICATE muda wako wa uzalishaji zaidi!! Kumbuka ukibakia tu umeajiriwa au kujiajiri mwenyewe unaweza kufanya kazi kuanzia leo mpaka miaka 27 ijayo yaani mwaka 2042 na itakuwa hujawa Dewji au Bakhressa. Hivi utawezaje kumfikia mtu anayeingiza labda milioni 1 na laki 1 hivi kama faida kwa siku moja wakati wewe kwa saa moja unalipwa  tsh 1850/- kwa siku kama elfu 16 hivi yaani laki 5 kwa mwezi! Ndo yaleyale. Faida yake ya siku moja ni mshahara wako wa miezi miwili. Faida yake ya siku kumi ni mshahara wako wa miezi 20 yaani mwaka mmoja na miezi 8! Mwaka mmoja na miezi 8 hizo ni siku takribani 600. Unaongelea yeye kuwa ameshatengeneza Tshs 600,000,000!! Milioni 600 ndani ya mwaka mmoja na miezi 8 tu.  Ambazo wewe utafanya kazi mpaka kustaafu na mwanao atafanya kazi mpaka atastaafu na mjukuu wako pia... Niendelee? Ndani ya huo muda yeye ameshapata faida ya 600 million!

Wanafunzi. Kama wewe ni mwanafunzi na unasoma ujumbe huu take it very serious. Usibweteke na hiyo degree unayosomea ya usimamizi wa fedha za wengine halafu uanze kuishi kwa kusambaza CV yaani bila plan nyingine yoyote maishani mwako. Elimu yote hiyo itakuwa haina manufaa kama ni kwa ajili ya kwenda kumfanyia mtu kazi maisha yako yote. Watoto wako nao waje wakasome elimu kama yako nao wakamfanyie mtu mwingine maisha yao yote. Wajukuu zako hivyo hivyo. Vitukuu... Vilembwe..
Wanafunzi wengi huwa ni wabishi. Wamesoma "elimu ya juu" wengine "wanafanya" masters. Hahaaa. Kuna tofauti ya "kuchukua" degree na "kufanya" masters. Hizi mbwembwe hizi jamani. Haya huyu mtu anawaza kuwa anajua sana vitu vingi. Kumbe anajua tu definition za economics na matajiri hawazijui hizo definition ila wanajua uchumi wenyewe na ndo wanaushikilia. Wanafunzi fungueni macho. Anza kujiandaa mapema. Usitamani tu kuajiriwa kupitia kiasi ndo mpaka baadhi ya dada zetu wanatoa rushwa ya mwili ili aajiriwe tu.

Jifunze haya mambo! Usikae kuchat chat tu na kutumiana vikatuni vya ajabu ajabu. Unachekacheka tu mwaka mzima na miezi 8 ushatumiwa vikatuni kibao mwenzako anatengeneza milioni 600. Unachat chat wenzako wanatengeneza hela. Unataka ukafanye masters ili mshahara upande. Unacheza au?

Anyway...
Kama uko interested kufahamu haya mambo kiundani hususan njia rahisi ya wewe kuzalisha muda zaidi ili kupata kipato zaidi basi wasiliana nas nasi kwa WatsApp  #o752366511.

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Ijumaa, 23 Septemba 2016

STORY OF AN UNSQUEEZED ORANGE

STORY OF AN UNSQUEEZED ORANGE

So I just asked myself this: what happens when an orange (like the one pictured here) goes #UNSQUEEZED? Well, it becomes useless and will eventually get rotten. And quickly forgotten.

It may have been plucked from the orange tree by the farmer but that wasn't its purpose for being there.

It may have found its way to the market place, like many other lucky oranges, but that wasn't its purpose either: to just end up on the market place.

It may have been picked up by a customer like luckier oranges and eventually get to that kitchen table that most oranges dream of.
But that also wasn't its purpose.

An orange must go through a very painful process that will make it 'bleed' a little: it must first be CUT and then as though that isn't enough, it must be *SQUEEZED.*

So I took a few seconds and looked up the definition of the word SQUEEZE just to check what language experts say. And I got this from Cambridge Dictionary

Squeeze:

"to press something firmly, especially from all sides in order to change its shape, reduce its size or remove liquid from it."

Uh-huh!

And so I thought how many oranges grow on an orange tree in one season? How many grow and get ripe? How many get plucked from the tree? How many reach the market place and how many are damaged or fall by the way side and never get to the market? How many get bought from the market? How many get to the kitchen table? How many are at least cut to find if they are worthy squeezing? And how many are actually SQUEEZED??

Is the number of squeezed oranges the same as the number of oranges that grew from the orange tree? Well, I thought the answer would be no.

This made me feel so sad for all those oranges that grow from orange trees around the world. I grew up in a village so I know how an orange appears on an orange tree. A very beautiful process for those who know it. I felt really sad that some oranges die from the tree while still tiny beautiful things, some die as they grow, some get rotten while on the tree, lucky ones get plucked and get taken to the market place and luckier ones get to the kitchen table and only a few - the luckiest, get cut and squeezed. They fulfill their purpose. But then I thought? Luck? Or they stood their ground and got attractive enough to appeal to the farmer's and customer's sight?

Well, that aside.
So I thought what kind of orange am I?
How far have I gone in the process?
Am I still on the orange tree?
Am I on my way to the market place? And if so, am I still attractive and good shaped enough to appeal to the "buyer's" sight?
Am I on my way to the kitchen?
Or am I actually in the painful cutting-and-squeezing  process?? Coz if I am already there then I should be bold like a grown orange. Bold enough to accept the painful piercing of the knife's edge cutting through me. Oranges bleed silently. I should. I should accept strong hands of life's challenges squeezing me from all sides so that the juice in me, my life purpose, my call, comes to fruition. Oranges never resist the squeezing process. But unfortunately many a times I do. What a strange orange I am!!!

The fact that I have made it to the kitchen table sometimes makes me take it to my pig head. I begin to think of all the poor lads who never made it this far. I feel I'm better than most folks. I forget I remain uncut and still have all the juice in me!! And I think God is a fool? That he formed me to just end on the kitchen table? But that's me. Poor me.

And when a feel a strong hand's touch and sense from afar that I am about to get cut into two here? Oh no. I dread the process. I think of the beautiful shape I have and all that will be gone? I look admiringly at my big size, and someone wants to reduce it? Oh no. I start thinking: maybe I should roll by the kitchen's table and fall down. So that when I'm picked up perhaps I won't be worthy the cut. Poor me. I'm picked when I fall. And sometimes I'm never good enough again. I get trashed into the bin. End of my story.

And in my little mind happy I still am. That I made it to KITCHEN UNIVERSITY.
That I made it to the KITCHEN COMMERCIAL BANK.
That I made it THE UNITED KITCHEN OF AMERICA.

I think of all the lads that never made it this far. I think of how I dodged the cutting process on the kitchen table. I made it this far without a scratch on my skin. And I smile. I forget that I'm in the dust bin. Forgotten. Unused. With life unfulfilled. I forget that I'm way on my way to obscurity. To the abyss of world history. I forget that I wasn't supposed to go to the bin with all the juice in me. I forget that there are many other oranges growing from orange trees and looking forward to cooperate to the end and fulfil their purpose. I forget that I was fooling myself all along. I forget that I led my life comparing my "progress" with that of other oranges whose lives mattered less to me as far as fulfilling my purpose was concerned. Poor me.

But then I made it, so I think. To the #UnitedKitchenofAmerica!! Not many people got the golden chance!...
How uninformed!
How lost a mind I have in my pig head. And I don't know that I'm actually just schooled but yet to be educated. Sadly. So tragic.

But then slowly somehow deep down me I begin to feel something strange. I somewhat feel unfulfilled. I begin to think that even though I made it this far but I am actually poorer than those who died on the orange tree while still tiny beautiful things. I feel like I owe them all and others something. Even though I smile but that's only on the outside. My heart bleeds from the inside. I begin to realize that I'm still full of all the juice in me. What for??? And as I contemplate my fate in the darkness of this bin with the bad smell of pieces of bread and every kind of junk around me, I see a dead orange in here. All-squeezed and empty! And then I ask myself: WHAT ON EARTH WAS I THINKING? "Somebody heeeeelllp?" I start shouting. Nothing. "Heeeeellp!!!" Nothing. Oh no. I hope I get a miracle and get rescued from this bin. I hope I get a chance to fulfill my purpose.

Well now, what about you dear orange?

Are you happy you made it to the United #KING-chen too??? Or that you too were schooled at CAMBRI-chen, or HAVAR-chen University? Happy that you come from a family of oranges that have it all? Happy that you got farther than most of us poor oranges? Happy that you made it farther than the stubborn orange tree that didn't want to release you for so long till someone plucked you off it? You forget that that orange tree fulfilled its purpose although it doesn't know how the market looks like or how Kitchen University or Kitchen Telecom or Kitchen Commercial Bank looks like. Are you happy too? Happy that you made it to the kitchen table, unlike other oranges? Happy that you know way more stuff that most oranges will ever imagine? Well, lucky you. But make sure you don't go uncut and unsqueezed. Or you'll have wasted all your life for nothing. My message to you is: Leave ALL THE JUICE IN YOU behind.
Accept to get cut and squeezed. Don't worry about other oranges. Fulfill your purpose and perhaps that will make a difference.

Note:
If you are still uncut and unsqueezed and you have no idea how on earth to get yourself ready for the preccess. Or if you are in the bin and want to know how to get back and and become any useful again just shout out loud.

Good luck!

Thank you, dear orange.

Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
+255752366511