.
🚴 WITO KWA NDUGU ZANGU WA MIKOANI 📚📖
Ni siku #nyingine tena. Na leo niongee kitu kingine tena. Huenda umeshasoma message zangu nyingi hasa LIFE BEGINS AT 40 (uhalisia wa maisha huanza ukifika umri wa miaka 40) ya kwanza na ya pili ambazo zimesomwa na watu weengi zaidi toka nianze kuandika. Usisome tu ukaishia kuwaforwadia wengine halafu ukaachia hapo. Fanyia kazi.
Okay.. Nimekuwa nikisafiri nchi hii huku na kule kwa shughuli binafsi na pia biashara. Okay safari za ndani ya nchi zinakufanya ujue nchi yetu hii ikoje kama vile safari za nje zinavyofanya ujue nchi zingine maisha yakoje.
Safari nyingi huwa nasafiri kwa njia ya mabasi. Nimekuwa nikijifunza mengi sana kutoka kwa watanzania wasafiri wenzangu. Na mojawapo ya vitu nilivyojifunza ni kuwa UKITAKA KUJUA MTU ANAWAZA NINI ANGALIA VITU ANAVYONUNUA.
Ukiwa stendi ya Ubungo kuna wachuuzi wa vitu mbalimbali mle ndani wanapita yalipopaki mabasi madirishani na wengine huingia ndani ya mabasi. Wengi wanauza maji, mikate, juisi, matunda, magazeti, vitabu, leso, simu, flash, power bank, miwani, nk. Sasa ukiwa pale unaweza kuona mtu ananunua kila kitu kwenda nacho huko mkoani lakini siyo KITABU.
Sasa huwa najiuliza. Hivi nyie ndugu zetu kutoka huko kwetu mikoani mkija Dar huwa mnaona tu nguo na juisi na mikate vitabu hamuoniiiiii au????? Mtasema labda vya kidhungu.. Mbona vya kiswahili vipo viiingi tu..!!
Mbinu za Kupata Kazi
Mbinu za Kufanikiwa katika Maisha
Mbinu za Kufanikiwa Katika Biashara.
Mbinu za Kuanzisha Biashara.
Siri za Kutoka Umaskini Hadi Mafanikio
Mbinu za Kupata Mtaji
Mbinu za Kupata Masoko..
Nk nk
Hivi hamjaona tu..? Yaani kila siku mnanunua tu magazeti kuona nini kipya leo toka enzi na enziiii na enzi.. Vichwa vya habari vya magazeti havitabadili maisha yako. Ulishasoma habari ngapi:
MKAPA ANG'AKA..
KIGOGO TANESCO AFUMANIWA..
MWINYI APIGWA KIBAO..
ULIMBOKA SIRI NZITO..
DR BILALI AIBUKA..
JK NJE TENA..
BUNGENI HAPATOSHI..
TAIFA STARS HOI..
KIKWETE ABADILI MAWAZIRI..
MADAKTARI WASALIMU AMRI..
PINDA AMWAGA MACHOZI BUNGENI..
MANGU IGP MPYA..
GWAJIMA HALI MBAYA..
LOWASSA TISHIO CCM..
SELELI AHAMIA CHADEMA..
nk nk!
Nunueni vitabu aisee. Mna uwezo wa kuibadili nchi hii na kubadilisha taswira ya maisha huko bila kuhitaji watoto waje wajenge huko. Mtajenga wenyewe na hawa wanaokatalia mjini mtaona wanakuja tu. Vitabu vina maarifa mengi sana na huenda ukawa hujajua hilo bado.
~ Vitabu ni vitamu kuliko juisi ya Azam.
~ Vitabu vinakata kiu kuliko maji ya Uhai
~ Vitabu vinatoa habari muhimu sana kuliko ITV
~ Vitabu vinaleta matokeo mazuri sana kuliko Simba 5 Yanga 0
~ Vitabu vinajenga msingi imara zaidi kuliko Twiga Cement
~ Vitabu vitakufikisha mbali zaidi ya basi la Shabiby
Sijui niseme nini zaidi ili twende sawa?
Utajiri mkubwa uko huko mikoani lakini sababu ya kukosa maarifa utajiri huo utafaidiwa na watu wa Kinondoni na siyo Simiyu au Njombe. Someni vitabu. Vitabu vitawafanya mpate maarifa ya kumiliki uchumi na utajiri ambao Mungu aliuweka kwenye mipaka yenu. Sasa nyie mpo mpo tu halafu mmekaa na ardhi ipo tu mnalishia ng'ombe miaka nenda rudi mpaka inamomonyoka mnahamia ardhi nyingine ugomvi kila siku na wakulima. Ufugaji wa kisasa upo hamjui kwa sababu upo kwenye vitabu. Mna uwezo wa kumilikishwa ardhi mkaitumia kufanikiwa ila maarifa hayo hayapatikani kwenye front page ya Nipashe. Someni vitabu. Mtaishia kuchoma moto mashamba ya wawekezaji au kuvamia migodi na bado maisha yenu hayatabadilika. Mtaishia kuchagua viongozi wakawawakilishe bungeni halafu nyie mkae mnywe viroba na kusikiliza bunge redioni na kusubiri maisha bora. Ndo maana na wao wamelifanya bunge kama sehemu ya kubadilishia maisha yao. Mtabadili wabunge, mtabadili vyama, mtabadili mpaka nguo badala ya kuvaa kijani mvae nyekundu na blue lakini nasema hivi kama hamna maarifa nyinyi wenyewe mtakaa kweli kweli.
Sikia, kipato chako hakiongezwi na mwajiri wako au serikali. Ni wewe mwenyewe. Lakini kama unachonunua wewe ni vocha, juisi na magazeti aisee daah utakaa sana. Mwanamama mmoja maarufu wa Ujerumani Helen Keller ambaye alizaliwa kipofu aliwahi kusema: KITU KIBAYA ZAIDI YA KUZALIWA KIPOFU NI KUZALIWA NA MACHO YANAYOONA HALAFU UKAKOSA UWEZO WA KUONA MBELENI (SIGHT without VISION). Sasa uwezo wa kuona mbeleni unakuja kwa maarifa.
Hata Biblia inasema WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA. Unaona mambo hayo? Ukombozi wako uko mikononi mwako mwenyewe. Ukombozi wa familia yako si kazi ya bosi wako.
Mafanikio ya kizazi chako si kazi ya Serikali. Kama hutaki kukubali endelea kumsubiri Magufuli aje akufanye wewe uanze kutumia jiko la umeme au gesi badala ya mkaa. Utashangaa nyumba yako iko karibu na bomba la gesi lakini unapikia kuni. Halafu unalaumu serikali. Soma vitabu upate maarifa. Utashangaa namna utakavyopata MTAZAMO tofauti sana kuhusu maisha. Kila kitu chako kitabadilika. Hutolaumu mtu wala serikali.
Sasa nyie kujisomea bado..haya basi hata kuwasikiliza watu waliojisomea hamtaki. Au uongo? Nyie mnataka kusikikiza politiki tu. Akija #Slaa, au #Magufuli au #Zito Kabwe haooo mnajaa. Akija #EricShigongo au James Mwang'amba hata hamwendi. Sijui hata kama mnawajua.
Halafu na nyinyi wasomi mlioko mikoani hivi mmeenda kugonga mihuri tu na kusaini mafaili jamani. Hebu watu waone mkiiathiri jamii kwa kuambukiza watu hamu ya kutafuta maarifa. Sasa wewe mwalimu wa Sekondari au afisa wa serikali au meneja wa benki mtu akija kwako kumejaa CD za bongo movie na magazeti ya Udaku. Umenunua bodaboda kuna kijana anaendesha anakuletea posho jioni unaona maisha yameishia hapo. Hebu waonyesheni mfano watanzania huko mliko. Someni vitabu. Na wataanza kuiga mfano na wengi mtajikuta mnapata maarifa sahihi. Huko huko Simiyu, Namanga, Mtera, Kasulu, Dumila, Shirati, Bihalamuro, nk mtafanikiwa kweli na kuwafanya watu wakutafute wewe kujifunza mafanikio. Haijalishi elimu yako. Amua tu kuanza kusoma vitabu. Sasa nyie stendi za huko kwenu mnauza vitunguu tu na nyanya na vikapu na mahindi ya kuchemsha hakuna mwenye wazo la kuuza vitabu? Haya Sasa hata mkija huku mnataka bado mnunue mahindi na juisi na karanga halafu basi. Hebu badilisheni hilo mtaona mabadiliko makubwa sana. Kumbuka tu wapo watakaokucheka lakini ipo siku watakuita uwafundishe kuhusu mafanikio!
Tena utaitwa mpaka huko mjini. Mnaweza kufanikiwa huko huko mkajenga hoteli zenye hadhi kubwa na utalii ukafika huko mkaingiza kipato zaidi. Huko huko mkajenga Shule zenye hadhi.. Huko huko maendeleo yakawafata. Makampuni yatawafata. Watalii watawafata. Siyo kila siku watalii wanaishia Arusha tu Ruaha na sehemu kama hizo. Maarifa ni muhimu sana. Soma vitabu. Anza leo. Hakika mtakubali haya maneno siku moja.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu vitabu vya kukusaidia, ama kuhusu wazo la biashara, ama mambo ya elimu ya mafanikio kwa ujumla WatsApp #o752366511.
Semper Fi
Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
Zingatia na fanyia kazi
JibuFutaDah, zaid kilicho nipanua zaid akil(haya maneno ya huyu mama Hellen keller) ni yana maan kubw san ukijarib kuyafikiria kiundan zaid. Sight without vision.
JibuFuta