Jumatatu, 12 Septemba 2016
UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO
Zamani nilikuwa nashangaa kwa nini Bill Gates anasema "kama ulizaliwa maskini hilo si kosa lako ila ukifa maskini hilo ni kosa lako" mpaka nilipogundua #makosa mengi ambayo watu #maskini hufanya. Makosa ya watu maskini ni mengi nitataja machache:
1. KUNA MTI WENYE MZIZI MMOJA?
Ulishawahi kuona mti wowote wenye mzizi mmoja? Hili nilifundishwa jana na mdogo wangu Josinah Leonard. Sasa maskini wengi wameshikilia ajira (au kibarua, au labda ana kakitu anauza) kama njia PEKEE ya kuwaingizia kipato wakati hata mwembe tu au mpapai au mti wowote ule una mizizi mingi tofauti tofauti ya kupata chakula na maji kutoka ardhini.
Ndo maana hakuna tajiri yeyote mwenye mkondo mmoja wa kipato. Wengi wanadhani Bill Gates anamiliki Microsoft tu. Ana vyanzo lukuki vya mapato. Kama wewe una chanzo kimoja cha mapato basi uko mbioni kufa maskini.
2. MAWAZO MGANDO
Kisha nikakumbuka pia maskini wengi wanafanya kosa la kuishi kwa mawazo ya zamani. Yani unakuta akiwaza biashara anawaza duka. Kwani kuna tajiri yoyote mwenye duka au vibanda 1000 vya MPESA? Hujiulizi?. Dunia imebadilika maskini hawabadiliki kichwani. Kampuni kubwa ya TAXI duniani (yani UBER) haimiliki gari hata moja. Lakini ndo kampuni kubwa ya usafiri wa TAXI duniani. Anatumia taxi za watu wengine. Wewe bado unawaza kununua bajaji na boda boda! Things have changed. You must also change. Kuna mengi ya kueleza hapa ngoja niendelee na mengine. Lakini hapo pia palinifanya nielewe kauli ya Bill Gates.
3. PERSONAL DEVELOPMENT
Maskini wengi hawasomi vitabu. Sikia hakuna tajiri asiyesoma. Bill Gates ana wiki mbili kwa mwaka ambazo yeye huzitumia kusoma vitabu vipya ambavyo hajawahi kusoma maishani
. Hebu jiulize Bill Gates anajifungia kusoma vitabu ili iweje? Wewe ukijifungia ndani ujue unaangalia series. Ukiulizwa umesoma vitabu vingapi mwaka huu hadi sasa January to September... Usikute labda hujasoma kabisa hata kimoja. Lakini message za WhatsApp ulizosoma mwaka mzima huu zinatosha kuchapisha magazeti ya Nipashe ya kujaa kwenye kabati lako la nguo! I mean that's a shame mate. Vitabu hutaki. Ukifa maskini hapo utakataa kuwa si kosa lako? Si unaona sasa kuwa utakubaliana na Bill Gates pia. Listen, SOMA VITABU. Acha kuishi kwa knowledge ya Mzumbe University sijui UDSM ya miaka mitano au 7 iliyopita sijui bachelor of nini? Soma vitabu huko ndo kuna maarifa. Mtaani hela hazifati Ph.D ya mtu. Kama ni hivyo maprofessor wangekuwa ndo matajiri. Knowledge ya pesa ina maarifa yake tofauti na Masters of Arts au Ph.D ya mambo ya mazingira. Kama chanzo chako cha taarifa za mafanikio bado ni Tumaini University au ni magroup ya WhatsApp utachelewa sana kujua habari za mafanikio. Hakuna tajiri asiyefanya personal development. Hata ungekuwa na elimu kubwa kiasi kipi kama hufanyi personal development utabakia kuwa significant katika maeneo mengine lakini si eneo la fedha. Kwa hiyo vitabu ni sehemu ya hiyo personal development. Kuna seminars, nk. Sasa jiulize semina ngapi zinazoongelea mafanikio umehudhuria mwaka huu.? Ngoja nikwambie kitu usipofanya Personal Development thamani yako itabaki kuwa ile ile ya miaka 7 iliyopita. Jana nilikuwa na kiongozi wangu mmoja katika biashara yetu. And akasema amepata fursa ya kualikwa sehemu kwenda kufanya TRAINING (mafunzo) kwa watu fulani wa "maana". Jumla ya hao watu ni 165. Jumla ya siku ambazo atatoa hayo mafunzo ni siku 5. Na kila mtu katika hao watu 165 atalipa sh 300,000/- kwa siku. Sasa fanya mahesabu sh laki 3 mara 165 hiyo ni hela yake ya siku halafu zidisha mara siku tano!! Umepiga hiyo hesabu? Sasa wewe unataka tu ukalime vitunguu au matikiti uwe milionea kesho. Maarifa unayo? Maarifa hujengwa taratibu. Siku nyingine ntaongelea vizuri zaidi kuhusu hiyo personal development.
4. TIME MANAGEMENT
Kosa jingine maskini wanafanya ni kupoteza muda. Time management mbovu. Hasa vijana. Aisee. Hawana ratiba. Ratiba pekee waliyonayo baadhi ya vijana ni ratiba ya mechi za premier league anajua ratiba za Manchester hadi mwakani. Lakini ratiba yake ya kila siku kwamba akiamka anaenda wapi hakuna. Hana hata kadiary au ka notebook hata kale ka sh elfu moja. Angalau awe anaandika vitu muhimu maishani nk.. Nothing. Ana magroup ya WhatsApp ya mpira, ya siasa yani moja linaitwa UKUTA 1 jingine UKUTA MAKAMANDA, UKUTA KANDA YA MAGHARIBI, UKUTA ORIJINO, mtu huyo huyo mmoja bado yuko magroup ya waliosoma pamoja na waliofanya kazi pamoja ambayo yote hayo habari kuanzia asubuhi hadi jioni ni UKUTA uleule. Anacopy message za huku anapeleka huku. Haya. Mwingine ana magroup HAPA KAZI TU, WATASOMA NAMBA, MAGUFULI JEMBE, CCM KAMPENI, UMOJA WA VIJANA, CCM VYUONI, ukimwona yuko busy utadhani karani wa chama. Wengine wako kwenye magroup ya NGONO TU maana huku Facebook na instagram kuna watu wanatangaza kutafuta namba ili wakuunge kwenye hayo magroup na unakuta namba 900 au zaidi. Unabaki unashangaa hawa watu muda huo wanaupata wapi? Hapo mtu akishindwa kufanikiwa ni kosa la mzazi? Au la mwenyekiti wa mtaa? Au Naibu Spika? Au la Kubenea? Kweli? Yani Kubenea anahusikaje kukufanya wewe ufanikiwe kiuchumi. Sipatagi connection. Sikia. Linda muda wako kwa WIVU MKALI na ujitenge na kila kitu kinachoiba muda wako. Time is MONEY.
5. KUTOFIKIRIA VIZAZI VIJAVYO
Kosa jingine maskini hufanya ni kutofikiria vizazi vijavyo. Sasa hii sijui laana? Maana wenzetu hawako hivyo.Mtu hafikirii kuwekeza kwa ajili ya watoto na wajukuu. Muda wako ukiutumia vizuri leo utawafanya watoto wako na wajukuu watumikiwe na mataifa. Lakini kwa style ya wengi wetu hii ya kujifikiria wenyewe ilimradi wewe unamudu kulipa kodi na kula na kuvaa basi watoto Mungu ataleta riziki. Khaaa? Kwa taarifa yako Mungu alisema unapaswa kuacha urithi mpaka kwa wana wa wanao (yani wajukuu). Sasa jiulize hiyo shughuli yako rasmi kwa sasa mwanao anaweza kuja kuiendeleza baada yako. Kwa ajira hiyo ni impossible. Mungu akikuchukua wanaweka tangazo moja kwenye notice board la kifo chako jingine kwenye gazeti la kutafuta mtu wa kujaza nafasi yako. Hiyo ndo reality. Hapo Kubenea hahusiki. Jamani msishangae namtaja sana Mhe. Kubenea ni mbunge wa jimbo langu na namtaja kuwakilisha wabunge wote. Sasa ukianza kuwaza kuhusu vizazi viwili baada yako utajiona jinsi ulivyo nyuma mno. Watu wanajifikiria wenyewe tu. Ndo maana ni rahisi kuridhika na vihela vidogo. Hutaki kuhangaika ili wajukuu waje wafaidi. Unataka ufaidi wewe kwanza eti unasema "kwa nini nijitese". Kwani kwa nini Yesu "alijitesa"? Ukiambiwa hivyo unasema" kwani mi Yesu?" shauri yako. Watoto wako au wajukuu watafukua kaburi lako afu watatoa hiyo skeleton waitandike bakora weee afu waizike tena. Omba ujengewe kaburi lako kwa nondo na zege. Wengi wanabaki maskini kwa mawazo ya ubinafsi wa kutowaza watakaokuja after you.
6. KUFIKIRI KUWA KUANZA BIASHARA INAHITAJI UWE NA MTAJI KWANZA
Wengi wamekwama hapa. Anafikiri kuwa inabidi atafute mtaji kwanza afu ndo atafute cha kufanya. Wakati anautafuta mtaji fursa zinaendelea kumpita. Akija kuupata anapata matatizo hela tena inatumika kutatua matatizo ya kifamilia. Anaanza upya tena. Mwisho anaamua kusema basi nahisi "Mungu hapendi". Maskini wengi wana kauli rahisi rahisi tu. "Si wote lazima tuwe matajiri". Anajijumlisha kwenye neno *wote*. Mtu anayefanikiwa anajua mtaji wa kuanza biashara ni kitu cha mwisho na ni kitu chepesi mno kuliko vingine vyote. Lakini wengi wanawaza mtaji. See? Kitu cha mwisho na *chepesi* anakifanya kiwe cha kwanza na kigumu.
Sasa hivi naielewa sana kauli hiyo hapo juu ya Bill Gates. Ukifa maskini hilo ni kosa lako. Anyway.. Kama unataka kujifunza zaidi mambo ya aina hii ama shida yako ni hapo kwenye namba 6 au namba 4 au namba 1 labda unawaza kuwa na vyanzo vingi vya mapato afu hujui unaanzia wapi na unatamani kupata ushauri au una biashara haiendi kokote mwaka wa sita sasa huenda kuna mahali unakosa basi njoo WhatsApp #o788366511 au #o752366511 ujifunze zaidi.
UKIBADILIKA, KILA KITU KITABADILIKA.
Semper Fi,
Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni