Alhamisi, 17 Novemba 2016

DO YOU BELONG TO THE "SOFT GENERATION"? THEN FORGET ABOUT SUCCESS. (KAMA U KATI YA WATU WA KIZAZI LAINI-LAINI BASI SAHAU KUHUSU MAFANIKIO)


Toka kuumbwa kwa dunia kumekuweko watu waliofanikiwa na watu wasiofanikiwa. Kumekuweko kizazi cha watu wachache jasiri na wenye uthubutu wa kweli na kizazi cha watu wengi laini-laini ambao kwao mambo yanapaswa yatokee tu kama wanavyotaka bila wao kuyaleta. Kumekuwako kizazi cha watu wachache waliotaka kujua ukweli hasa wa mambo upoje licha ya "uhalisia" unaohubiriwa, na kumekuweko kizazi cha watu wanaosema "hali iko hivi" (yani uhalisia uko hivi) na hauwezi kubadilika mpaka mtu au watu fulani waibadili. Kumekuwako watu wanaosema "Wazazi wangu wange....basi ningefanikiwa. Au Serikali iki...... nitafanikiwa. Bosi wangu akiniongeza mshahara....nitafanikiwa. Nikipata mkopo nitafanikiwa kufanya hivi na vile. Nikilipwa na wateja wangu mapema nitafanikisha hili. Au anasema: Mimi  ningeshaanzisha saluni yangu lakini... Ama: Aisee ninataka kuwa mwanamuziki mkubwa lakini....

See? Kizazi chenye "ifs-and-buts". Kizazi chenye litania ya sababu kwa nini mafanikio ni magumu kwao. Hii ndo soft generation ninayoiongelea.

Kama umebahatika kusikia ndoto za watu wengi hapa duniani unaweza kushangaa jinsi watu walivyo na ndoto kubwa ambazo zinaweza kumaliza matatizo mengi tuliyonayo. Na yumkini wewe pia una "mandoto" ya kufa mtu. Yani ukiangalia ndoto zako daah unajisemea aisee "one day ntakuwa balaa". But jiulize swali moja tu: DO YOU BELONG TO THE SOFT GENERATION?
Kama ndivyo then sahau kufanikiwa!

Success is not for soft people. Are you hearing me?
Mafanikio hayakuumbiwa watu soft-soft. Mafanikio siyo kitu kinachokuja kama upepo tu from nowhere. Mafanikio ni kitu unachopaswa #kukitafuta na kukiendea na mpaka ukipate you've got to be #TOUGH first.

Usifikiri ni swala la kuomba Mungu tu. Unaweza kupiga magoti kuomba mpaka magoti yapate "sigda" na usifanikiwe kama wewe upo katika kundi la soft generation. Nimestudy watu waliofanikiwa na bado naendelea kuwastudy wengi zaidi and naweza kukwambia wote niliowastudy hadi sasa ni watu TOUGH. Imara. Wasiolialia wala kulalamikia hali ya maisha wala kuongelea "uhalisia". Watu kama Jack Ma, watu kama Nelson Mandela, watu kama Mohamed Dewji watu kama Jim Rohn watu kama Margareth Thatcher watu kama Abraham Lincoln watu kama Aliko Dangote. Hawa ni watu tough! Angalia toka enzi na enzi, hivi baba yetu wa imani mzee Abraham alikuwa soft soft? Musa je? Mtu anaweza kufunga siku 40 usiku na mchana na akarudia tena hilo zoezi mara ya pili akiwa ni mtu soft soft? Wewe ukifunga siku mbili unaanza kusikilizia tumbo na kichwa. Coz you're soft. Hivi Christopher Columbus alikuwa soft soft? Hivi kweli mwalimu Nyerere alikuwa soft soft? TOUGH people.
Watu wanaofanikiwa huwa hawana kawaida ya kuishi kwenye eti uhalisia. And let me tell you my friend. "Uhalisia" ni kitu BINAFSI. Unaweza kuwa katika watu wanaosema maisha ni magumu but kwako uhalisia ukawa tofauti. Unaweza kuwa kati ya watu wenye furaha na amani na ukawa anxious and perplexed. Na unaweza kuwa kati ya watu wasio na furaha na wanaolalamika na ukawa positive and happy. But you've got to be a tough person first. Lazima uachane na tabia za kitotototo za kulialia. Usifikiri Mungu anabadilisha formula zake kwa sababu ya kulalamika kwako wiki nzima afu weekend unaenda kumwimbia nyimbo za slow motion. In fact ukizidi kulalamika Mungu anafika mahali anachukia na anaweza kukufuta kabisa. Maana your mind inakuwa imeanza kupoteza uwezo iliyoumbiwa wa kuwa creative na kuwa positive. Kumbuka kuna KIZAZI cha taifa fulani Mungu aliwahi kuzuia kisifikie kilele cha mafanikio kabisa sababu ya kulalamika. Kawatoa utumwani wanalalamika. Kawavusha bahari ile kuwa test kidogo tu wanalalamika. Kawajaribu tena kuona kama wanamwamini zaidi wanazidi kulalamika tu. Kakaa kimya na kiongozi wao mwezi mmoja na siku 10 tu wakaanza mchakato wa kupata "mungu" mpya! Khaa. Kwa kuwa Mungu  HANAGA kawaida ya kushindana na wanadamu akazuia tu hawa hawaingii Canaan aisee never bora waingie watoto wao kuliko hawa. Kulalamika. Hiyo ndo effect ya complaining and whining. Na kukasirikakasirika tu usipopata unachotaka - Being crybabies!
Yani usipopata unachotaka badala ya kuwa creative unatafuta wa kulaumu huku umekasirika. Mungu ataku-mind sana yani.

Tuna wimbi kubwa la soft generation people siku za leo.  #Whiners and #crybabies! Watu wanaolialia tu. Ooh nimeomba nauli sijapewa sasa mi ntaendaje shule. Oh nilitaka kuja ila mvua ikanyesha sasa ningefanyaje? Khaaa!
You are such a soft person my friend! Oh  "Nimeapply kazi sijaitwa yani serikali hii imezuia ajira sijui tutaishije nchi hii mi nachukia sana".
You're a Crybaby! Mtaishije wewe na nani kwanza?

Ooh, "Tumemaliza JKT hakuna ajira mtupe ajira tusije kuwa majambazi kwa nini hamtupi ajira".

Crybabies! Huko JKT mlienda kujifunza kuandika CV za kazi kwani?

Ooh ninataka kujiajiri lakini sina mtaji serikali yenyewe haijaleta viwanda walitudanganya tu!
Crybaby wewe!

Juzi niliongelea hilo la mtaji kwa mfano. Kwamba ukihitaji mtaji inabidi uwe na a very consuming idea kwanza kichwani. Naamini uliisoma hiyo makala. If not utapoteza muda kutafuta mtaji na hutaupata. Kuna formula za kufanikiwa. Usijiendee tu. Unakuwa tu mtu wa kulialia tu.
Halafu unasubiri pia uje ufanikiwe! Kweli?

Oh mi natamani kuwa mbunge lakini huko mpaka umjue MTU.
Are you serious? You simply don't really know what you want.
Soft generation!

Oh mi ninataka sana kusaidia yatima lakini sina uwezo! Usitudanganye unataka kusaidia yatima wewe. Kwa nini usiende kuwasaidia kupiga deki? Who told you kuwa msaada ni hela tu? Why usijitolee kwenda kuwafundisha tuition au kuwafundisha muziki au kucheza nao tu, kwani huo si ni msaada wa kisaikolojia mzuri zaidi kuliko kwenda kuwapelekea biskuti na peremende na kupiga nao picha ili ukapost Instagram!?

Kawaombe kupiga deki weekend uone kama watakataa. Hapo unaanza kujihurumia na kuhesabu gharama. Coz you are so sooooft. Yani kila kitu ooh mimi, unajua, yani hii hali, yani uchumi.. Soft generation.

Wengine huwa wananambia unajua kaka wewe hujui tu. Listen, najua sana. What I'm trying to tell you here is usipoacha kuwa "a whiner na crybaby" basi utafika mwisho wa maisha yako unalalamika tu na kukasirika huna kitu cha maana umefanya duniani hapa. Ukiambiwa jisomee vitabu ooh unajua mimi, muda, nachoka sana, narudi usiku sana.
Soooft generation!
Unajihurumia.
You don't want to sacrifice.
Mentor wangu alisema juzi kuwa kama huwezi kusacrifice #USINGIZI au #CHAKULA hivyo vitu viwili basi mafanikio kwako ni ndoto hata mafanikio ya kiroho. Smart man. #ILoveMyMentor.

Na ndo maana kuna vitabu lukuki vimeandikwa kukwambia cha kufanya ili ufanikiwe katika nyakati zinazoitwa ngumu. Lakini wewe unaweza kukesha kusubiri matokeo ya TRUMP na HRC kuliko kusoma kitabu cha namna gani ufanikiwe kutimiza ndoto zako. Eti ooh siyo hobby yangu. Kwa hiyo kukesha unakodolea macho CNN ndo hobby yako? Hobby? Na mafanikio yatakujibu hivyohivyo wewe siyo hobby ya yenyewe! Hivi unawezaje kukesha ukisubiri pambano la MAYWEATHER afu ukashindwa kukesha ukiandaa mipango yako halafu ukataka ufanikiwe?
God is not a fool my friend.
Afu unatoka unaenda kulaumu mbunge wako!  Wakati hutaki kujifunza unataka vitu vinavyofurahisha akili tu. Ndo maana magroup mengi ya WhatsApp hayakujengi lakini unapenda kukaa humo. Vitu unavyofeed mind yako kutoka kwenye hayo magroup vinaua safari yako ya mafanikio but hutaki kuviacha. Ajabu ukiambiwa kuna group la kusaka mafanikio unasema "na mimi jamani niungeni". Coz ni kweli unatamani kufanikiwa. Lakini ukiwekwa kwenye hilo group afu ukaambiwa jamani eeh humu kwenye group kila siku jioni lazima kila mtu aseme amejifunza nini kwenye kitabu anachosoma kwa sasa, heee group linageuka kuwa chungu. Halafu unataka mafanikio! No my brother, no my sister, mafanikio hayatakuja kwako kamwe!
Coz you are too soooft. Ukiambiwa kuna semina ya bure kujifunza ujasiriamali unasema ooh muda sina, ooh muda mbaya muda huo ndo nakuwa natoka kazini. Lakini ukiambiwa kuna Fiesta usiku wa manane na kuna kiingilio elfu 20 siku hiyo hata kazini unatoroka mapema ili uwahi kukaa (I MEAN KUSIMAMA) mbele karibu na jukwaa na kupigwa na umande mpaka asubuhi huku ukichekacheka watu wanaokata viuno na kuitikia imoooooooooo!! Afu unashangaa hela huna. Huo muda ungekuwa umekaa unajifunza mambo muhimu ungefika mbali. Wengine nyie ni mabilionea wakubwa wa baadaye lakini you are too soft! Unataka vitu vya kudumaza mind yako tu. Mungu atakupaje mafanikio?
You are not ready!
You're too soooft! Watu niliokutajia pale juu ni tough people. Check baadhi yao hapa wanasemaje.


Quit being soft.
Kama unataka kufanikiwa lazima uwe TOUGH kwanza kabla hujaanza safari ya mafanikio. Why? Sababu utakumbana na challenges njiani, utakutana na watu wa kukukatisha tamaa wengi mno. Utafika mahali inahitaji upersist lakini kwa sababu you belong to this SOFT GENERATION utaachia njiani..
Coz you're too soft.
Success is not for soft people or crybabies! Unalialia tu. Utafika uzeeni una Ph.D ya kulialia. Crybaby! Utapoteza nafasi ya kuwasaidia wengine kufanikiwa kwa sababu ulichagua kuwa MLALAMISHI na CRYBABY. Ukasahau you have to toughen up in order to get the things you want in life. Unaishi kwa "group thinking". Kwa kuwa wengine wanalalamika basi unadhani na wewe uliumbwa kulalamika kama wao! Unaanza kuwa mbobezi wa kujihurumia na kuomba huruma za wengine. Ndo maana unashangaa mtu anakuja Facebook kila siku status zake mara "This flu is killing me". Mvua ikinyesha tu ooh "jamani hii mvua si ikanyeshe Mtera?" Khaa! Mungu anakuangaliaaa..anakuacha tu. Jua likiwaka sawasawa unaona status eti "Arrrgh hili joto litatuua". Khaa. Si uweke mabarafu kwenye kwapa!? Crybaby!

Haya mara kaandika: Jamani "Baba Jesca" punguza kidogo hali imekuwa ngumu mno! Huoni mazuri coz your mind imekuwa tuned kulalamika.
Ndo hapo unashangaa mzee ndo anaongeza kaspidi gavana kidogo anabinya kidogo zaidi anakaza zaidi. Hahaaaaaa. Hapo ndo utajua kama ile mikia ya pweza hivi ni mikia au miguu, au mikono?

Sasa wewe endelea kusubiri raisi mwingine. 2020. Au 2025 ndo uanze kufanikiwa. Utashangaa anakuja wa type hii hii yani. Hapo unashangaa na kujiuliza hawa wenzangu waliofanikiwa wamefanyaje?

Wamefanyaje?

I'll tell you wamefanyaje:
Walichagua kutokulalamika na kuwa creative...
Walichagua kutotegemea serikali na kujitegemea wenyewe...
Walichagua kujifunza mapema...
Walichagua semina za mafanikio badala ya fiesta...
Walichagua kuahirisha "entertainment" kwanza...
Walichagua kusacrifice muda wao wa kuenjoy na kupumzika wakaamua kupigana kufa na kupona no matter what wakati wewe ulipokuwa unatukana serikali kwenye mitandao...
Walichagua kujitafutia njia za kutengeneza kipato wakiwa chuo wakati wewe ukichagua kutegemea siasa na kusubiri mkopo na ajira...
Walichagua kuonekana wajinga wakati wewe ukila bata...
Walichagua kuomba Mungu kila wakati mpaka usiku wa manane wakati wewe ukisubiri kuombewa na kuonewa huruma na kuwekewa mikono na nabii naniliu...

Walichagua kuanza kidogo chini wakati wewe ukisubiri ukafanye Masters kwanza...
Walichagua kuamini katika kujibidiisha na kujituma ili kubadilisha maisha yao na vizazi vyao wakati wewe ukiridhika na comfort zone...

Hapo ndo utajua kama utakula mijadala uliyokuwa unapoteza nayo muda sijui Wema Sepetu sijui Boss Lady. Hapo ndo unabaki unakasirikia waliokupita kimafanikio. Unawachukia bila sababu. Unabaki kushabikia siasa na Simba na Yanga. Ikikodishwa unalalamika, coz ndo unachoweza zaidi, hahaa hapo muda umeisha uzee umekukuta.
Hapo ndo utajua Fiesta imoo au haimo!

So achana na group thinking.
Itakupoteza. And by the way kama kweli hali imekuwa ngumu kwako like you say basi nikushauri tafuta kakitabu kanaitwa TOUGH TIMES NEVER LAST BUT TOUGH PEOPLE DO.
Utaelewa nachosema. You've got to be TOUGHER than your situation.

Muda unaotumia Facebook, Instagram na Snapchat au WhatsApp ungeutumia vizuri mbona ungesaidia watu wengi mno! Hivi unadhani Mungu atakusahau wakati anaona unatumia muda wako vizuri kujifunza mambo muhimu? Lakini vijana wengi ninawaona humu kwenye mitandao wakikuta mada kama hizi wengine wanatukana wengine much know, wengine wanaignore tu wanataka kila post iwe inaongelea vitu soft soft tu. Tunazalisha taifa la walalamishi na crybabies! Watoto wadogo wanajifunza kwa kuona. Wasomi wengi vyuo vikuu ni walalamishi na crybabies. Shame! Ndo maana unashangaa mtu anamaliza chuo akitaka kwenda kusambaza CV anaomba nauli kwa wazazi. Yani kama elimu ya Chuo Kikuu inashindwa kukuzalishia nauli wewe itamsaidia nani sasa? Utasikia eti. Ah sasa bro sijapata kazi si unajua tena. Ulalamishi tu. Si ukafundishe hata tuition? It's a shame! Wasomi ndo wanaenda kuwa watendaji. Wabunge. Unashangaa analalamika tu.
Why?
Soft generation.

I'm telling you utakuwa mbunge au waziri na utaondoka hukumbukwi. Coz you did not touch lives. You were not successful. Coz ulikuwa whiner and such a sorry crybaby maisha yote. Ndo unashangaa mtu mzima anaachishwa kazi anaanza kulia hadharani. Eti ntaishije? It's a shame. And that's a representation of what our society is beginning to look like!

You need to be TOUGH.
Tough for the dreams you have.
Tough for your children.
Tough for others.
Tough for your nation.
Tough for the world.
Tough for God!
Tough for YOURSELF.
Mungu hakukuumba uje ulie toka unazaliwa mpaka unakufa. Mungu alikupa uwezo wa ku-withstand every tough situation. Lakini umechagua kulialia. Yani umekuwa mtu wa: Ooh yani sijui nianzie wapi? Khaa! Yani utadhani mwili wako umekufa ganzi kuanzia shingoni kwenda juu!


Stop being too soft.
Kama uko kwenye soft generation bonyeza kitufe cha EXIT haraka sana. Toka humo.
Learn to be tough and to fight for what you want. Siyo kulalamika. Ain't nothing gonna change because you whine or complain. Achana na kutukana serikali haikusaidii.
That's being a CRYBABY! Success is never for crybabies. I told you that already.
Achana na kufollow page za watu wanaolalamika na kukasirika every day. Haikusaidii kusikiliza crybabies.

Amua kusema kuanzia leo sitaki kulalamika. Wala kusikiliza malalamiko.
But I will fight for my dreams.
I will fight for my success.
I will soldier on and toughen up mpaka nifanikiwe.
Coz I have the DNA of God.
The DNA of success.

Amua kwamba kuanzia leo nikikosa kitu nachotaka sitakasirika wala kulalamika bali nitakuwa mbunifu na kuwaza upya ili nikipate hicho nilichotaka. Anza kujifunza tabia ya kuwa tough minded. Jifunze hata kwa machinga. Akitembeza vitambaa watu 10 mfululizo kawaonyesha na wote hawanunui hakati tamaa na kurudi nyumbani baada ya lisaa. Anajua atauza tu.

Success is not for soft people.
And never for crybabies.
TOUGHEN UP MY FRIEND!

If you belong to the soft generation then you can as well kiss your success goodbye and forget about being successful. Be it at school, or in business or your relationship; be it in politics, sports or whatever endeavour - success is for tough people.

Amua kuwa imara! No matter what.
Uninstall the software of whining and complaining. Weka mpya ya kuwa imara na kung'ang'ana.

THEN AND ONLY THEN WILL YOU BECOME SUCCESSFUL!

Badilika!

Barikiwa!

Kwa mawasiliano zaidi au maswali, ushauri, appointments contact me via:

WhatsApp only: +255788366511
Sms + Calls: +255752366511

Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni