Jumatatu, 24 Aprili 2017

WANT SUCCESS? BE A STUDENT OF NATURE TOO. (UNATAKA MAFANIKIO? KUWA MWANAFUNZI WA ASILI PIA)



WANT SUCCESS? BE A STUDENT OF NATURE TOO.

UNATAKA MAFANIKIO? KUWA MWANAFUNZI WA ASILI PIA


Kwa muda mrefu nimekuwa mwanafunzi wa mafanikio hasa kutoka kwa watu mbali mbali ambao ninahisi kwao nina mengi ya kujifunza mambo mbali mbali. Ninajifunza kwa kusoma kwenye vitabu mbali mbali, kukutana na watu face to face, pia kwenye Internet hasa YouTube videos, na pia kufuatilia wasemayo watu mbali mbali (ambao naamini Mungu aliwekeza kitu muhimu ndani yao) kwenye kurasa zao katika mitandao ya kijamii kama hapa Facebook, LinkedIn, Twitter na Instagram.  
Kwa mfano Facebook kina ninapo-login kabla sijasoma chochote huwa napitia kurasa 10 kwanza kuona walichoandika zikiwemo za wafuatao:
1.       James Mwanga’mba
2.       Mohamed Dewji
3.       Grant Cardone
4.       Robin Sharma
5.       Strive Masiyiwa
Na zinginezo....

Nimejifunza mengi na ninamshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya kujifunza kutoka kwao kwa kweli. Kama ni chakula ninapata ladha tofauti tofauti na virutubisho tofauti tofauti ili afya yangu kuanzia shingoni kwenda juu izidi kukaa sawa. Najifunza pia kupitia comments mali mbali za watu wanapita katika kurasa hizo. Mfano juzi Cardone alipost akiuliza watu waseme MALENGO YAO MAKUBWA waliyowahi kuyaweka ni yapi and ukipitia comments niliweza kujua binadamu wenzangu duniani wana malengo yapi makubwa na hivyo kujifunza binadamu wenzangu wanawaza nini kuhusu maisha haya mafupi ambayo tumekodishwa na Mungu kwa kitambo.

Nawaombea wote wanaoshirikisha mawazo yao mema Mungu azidi kuwabariki na kuwawezesha kufanya hivyo ili waweze kuhuisha yale yaliyokufa ndani ya watu na kuchochea yale yaliyo hai.
Kutokana na kujifunza kwangu kutoka huko kote na kwa uzoefu wangu wa kuupitia mchakato wa mafanikio nimetambua jambo moja muhimu ambalo zamani sikuwa nalijua kuhusu mafanikio. Nalo ni hili: UKIWA MWANAFUNZI MZURI WA ASILI (NATURE) UTAYAFIKIA MAFANIKIO YAKO KWA WAKATI MUAFAKA ZAIDI.

Iwe unaamini katika Mungu au la hiyo haiondoi ukweli kwamba ASILI (nature) ipo na inaendeshwa na taratibu fulani ambazo hazibadiliki toka enzi na enzi. Na kwamba taratibu hizo uwe unazijua au huzijui zinaathiri namna utakavyoishi hapa duniani na yale utakayopata au yatakayokupata ungali hapa ulimwenguni. Taratibu ama kanuni hizo zimekuweko toka zamani zilizopita zip oleo na zitakuwepo zamani zijazo. Mfano kanuni isemayo: unachopanda NDICHO utakachovuna.


Kwa kutazama kwangu maisha yangu binafsi na ya vijana wenzangu na hata watu wazima katika eno hili la kupata mafanikio nikajifunza kuwa pamoja na kuwa wengi wetu tunajifunza kwa watu mbali mbali kama nifanyavyo mimi lakini tumesahau kuzingatia kanuni muhimu wanazofundisha hasa zile zinazoendesha asili (nature).

Kujaribu kutafuta mafanikio pasipo kuzitii hizi taratibu ama kanuni muhimu ni kujaribu kuidanganya ASILI kitu ambacho huwa hakina manufaa kwani hakiwezekani. You can’t cheat nature. Huwezi kuidanganya asili. Nakualika uendelee kuwa nami hapa chini ninapojaribu kuzielezea baadhi ya hizo kanuni ili uone kama zinaweza kukusaidia pia katika mchakato wako wa kuyaendea mafanikio uyatakayo.


1.       KANUNI YA MJUMUIKO (THE LAW OF ASSOCIATION)
Ulishawahi kuona video iitwayo THE CHICKEN AND THE EAGLE? Unaweza kuitazama hapa https://www.youtube.com/watch?v=dHAfVl-t1Hg na itakusaidia kuelewa hili nitakaloeleza hapa chini..
Kwa asili ni kwama vitu vinavyofanana vina kawaida ya kujumuika pamoja, kuenenda pamoja na kufanya mambo yao kwa namna inayofanana. Watu wa kale waliliona hili wakasema vitu kama: Ndege wafananao huruka pamoja.. kama ndege hawa wawili waitwao Steve Jobs na Bill Gates katika picha yao hii mwaka 1985 

Ni muhimu sana kama candidate wa Mafanikio ukalijua hili na kulizingatia sana. Wengine wakaitazama hii na kuiweka hivi: Kwa kawaida wewe utakuwa ni wastani wa watu watano wa karibu unaojumuika nao kila mara. Kwa maana nyingine ni kwamba ukitaka kujua mafanikio yako yatakuwa kwa kiwango gani angalia mafanikio ya watu wako wa karibu watano. Mwingine aliyeiona kanuni hii ya asili akasema ukikaa sana na watu wanne wasio na kipato unajua nini kitatokea? Halafu akajibu hilo swali kwa kusema: WEWE UTAKUWA WA TANO.

Jambo hili ndo linasabisha uone jinsi inavyokuwa ngumu kwako kuwa mtu wa karibu wa Dewji “from nowhere” tu. Si kwamba hapendi binadamu wengine ila anaheshimu kanuni hii. Anatii ASILI inachotaka. Asili inamtaka awe na watu wa aina fulani karibu ili weweze kumpasha habari sahihi na kumpeleka mahali sahihi kwa nyakati sahihi ili aweze kuyafikia yale anayoyataka. Kama hujawa aina hiyo ya mtu ASILI itakataa ukaribu wako na Dewji. Hata ukiwa jirani yake au mnasali msikiti mmoja au mko gym moja na treadmill anayotumia ndo na wewe unatumia. Utaishia kusema tu Dewji tuko naye gym moja yule. 

Unapoanza kutii kanuni hizi hazitofautishi mpagani au mtu wa dini au mtu anayeamini kuwa kanuni zenyewe zipo au ni uzushi tu. Ukizifata utapata matokeo. Ukijumuika sana na wavivu utakuwa kama wao, ukijumuika sana na wasomaji vitabu utaanza tu kuongea na kuwa kama wao, ukikaa sana na watu wanosemekana kuwa wako kwenye “system” si muda mrefu utaanza kuwa na tabia na lugha na haiba ya aina hiyo. Ukijumuika sana na walalamishi utaanza kulalamika na kulaumu laumu tu kila kitu. Ukijumuika sana na wakosoaji  kila kitu utaanza kuwa mkosoaji pia na hata hutaona kuwa umebadilika. 

Kama wewe ni mwanafunzi ukijumuika sana na wanafunzi wanaonyoa viduku na kuvuta ile kitu kwa siri basi utajikuta umekuwa mmoja wao. Kama wewe ni mchungaji au mfanyabiashara ukijumuika sana na watu wanaovaa mapetepete sijui ya bahati na kupiga ramli na kuvuta watu utajikuta na wewe una mapetepete na vitu vya aina hiyo. Ndege wafananao..... 

Ukijumuika na walevi au watumia mihadarati vivyo hivyo kuna aina fulani ya tabia utaanza kufanana nao. Wewe ni tai lakini utajikuta unaishi na kuenenda kama kuku. Na hata ukiambiwa kuwa unatakiwa kutoka miongoni mwa kuku unaweza kuona wanaokwambia ndo hawajui kitu kuhusu wewe. Kumbe shida ni kanunu hii unaiishi ndivyo sivyo. Ukifollow page za umbea utakuwa mbea ukifollow za wanaotoa taarifa sahihi kuhusu maisha, mahusiano, biashara, nk utaanza kuwaza kama wao.

Sasa ukidhani kuwa kufanikiwa ni kuwa na ndoto tu na kuweka malengo hapo na kufanya kazi kwa bidii ukaignore kanuni hii ukajiendea tu na kujijumuisha tu na any THOM, DICK AND HARY unaweza kuwa frustrated kwa nini huoni mafanikio mapema. Angalia basi kila unayeona amefanikiwa kwa definition yako mwenyewe halafu uone kama katika marafiki zake watano wa KARIBU kuna mtu asiye na tabia za kimafanikio. Chunguza mwenyewe. Utapata majibu sahihi. Mimi nililitazama hilo  nikajifunza kumbe nahitaji kuiitii kanuni hii pia KWANZA!


2.       KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA (THE LAW OF SOWING AND REAPING)
Unaonaje kama ingekuwa ukipanda mahindi unakuwa hujui kitakachoota ni mchele au minazi au mipapai! Unadhani hiyo level ya uncertainty ingeathiri vipi maisha yetu? 

Lakini kanuni hii ya asili ikawekwa. Na hii inapatikana hasa ndani ya kanuni nyingine kubwa inayojulikana kama KANUNI YA KISABABISHI NA MATOKEO (ama the LAW OF CAUSE AND EFFECT) ambayo inasema kuwa hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya tu yani from nowhere ila huwa kuna kisababishi kwa kila jambo unaloona linatokea. Yaani ukiona ardhi imechipusha mahindi ujue kuna kilichosababisha. Na hapa ndo kanuni ya kupanda na kuvuna inapoingia. 

Anhaa! Kumbe kilichosababisha ni kuwa kuna kilichopandwa. 

Katika vitabu ninavyokusihi upitie kujiffunza bila kujali imani yako ni Biblia. Mfano ndani ya kitabu hiki tunapata reference ya kanuni hii. Kitabu cha Wagalatia 6:7 na kitabu cah Ayubu 4:8. Wagalatia wakaambiwa kuwa Mungu hadhihakiwi bali apandacho mtu ndicho atakachovuna! Hii ni kauli kali sana. Kali kwa sababu inalinganisha kutegemea kuvuna usichopanda kumbe ni sawa na KUMDHIHAKI MUNGU. Unataka kucheat kanuni zake za uumbaji wa mambo. Unataka kumfanya Mungu kama asiyejua alichoweka in place. 

Watu wote waliofanikiwa wanaitumia hii kanuni vlivyo. Kama ilivyo ukipanda mahindi unavuna mahindi ndivyo ilivyo pia ukipanda mahindi MENGI utavuna mengi. Kama wewe ni mwanamichezo ukifanya mazoezi mengi utapata matokeo bora zaidi ya asiyefanya mazoezi kabisa. Michael Phelps ni muogeleaji wa Marekani anayeongoza kwa medali za dhahabu za Olympic duniani kwa michezo yote inayochezwa kwenye Olympics

Mojawapo ya kitu alichowahi kufanya ni kufanya mazoezi makali kila siku mwaka mzima kwa miaka mitano mfululizo bila kukatisha. Kuna kukimbia, kunyanyua vuma, na kuogelea. na kwa juma moja anaogelea takribani kilometa 80. Umbali huo ni kama kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar kwa mtari mnyoofu (https://www.distancecalculator.net/from-dar-es-salaam-to-zanzibar

Sasa mtu anayepanda hilo unahisi anapaswa avune nini? Akivuna medali nyingi za dhahabu kwenye Olympics kuliko binadamu yeyote unashangaa? Tuna waogeleaji ambao wana huo uthubutu? Na je wewe na mimi katika maeneo yetu ya kuogelea (ndoto zetu) tunapanda bidii kiasi hicho?

Nasema tena ukidhani kufanikiwa ni kuandika malengo tu na kuyafanyia kazi ukashindwa kujua kumbe kwenye kufanya kazi ukipanda sana mgongo ukauma jua likakutandika sawasawa na ukachoka kweli kweli ndipo utavuna kwa kiwango cha “kutisha” basi utatamani mafanikio makubwa ya wengine bure bila kujua unatakiwa uogelee Dar hadi Zanzibar kwa wiki moja pia. Nilikuwa najiona ni mwenye bidii katika mambo yangu hadi nilipoanza kujua ratiba za watu waliofanikiwa katika maeneo ya ndoto zao ndipo nikaona nina kazi kubwa ya kufanya pia. Nimeona nishee na wewe huenda nawe ukaona unahitaji kukaza kamba za viatu zaidi.


3.       KANUNI YA NGUVU YA UVUTANO (LAW OF GRAVITATIONAL PULL)
Hivi Isaac Newton alipokuwa anafikiria kuhusu lile apple sijui kama alijua ilikuwa ni observation muhimu sana siku ile. Mojawapo ya nguvu kubwa mno za asili ni nguvu ya uvutano. Dunia hii inategemea mno nguvu hiyo na kumbe hata kutembea kwako juu ya ardhi ni kwa sababu ya nguvu hiyo. Yani wewe haujasimama wala kukaa wala kulala ardhini hivi hivi (CAUSE AND EFFECT) ila kuna nguvu inakuvuta. Ikikata hiyo tutaelea huko angani na kila kitu kinachojongea juu ya uso wa dunia kitaelea huko angani kuanzia hapo! Ajabu iliyoje! 

Ndipo nikajifunza kuwa ASILI iliweka hilo nalo litufundishe kitu. Yeyote anayetaka kufanikiwa hana budi kutii kanuni hii ya gravitation. Siku zote utavutwa pale ambapo nguvu ya kukuvuta ilipo.
Hivi nguvu yako iko wapi? Katika mambo ya mafanikio ama katika mambo yasiyo ya mafanikio?

Huenda hujanielewa. Labda nitoe mfano. Ukapita Kariakoo ukakuta kuna TV nje ya duka zinauzwa ila zinaonyesha matukio mbali mbali. Moja inaonyesha Eric Shigongo anazungumzia jinsi ya kujikwamua kutoka katika hali ngumu, nyingine inaonyesha Askofu Gwajima yuko LIVE anasema ana siri nzito anataka kuitoa. Wewe binafsi kiukweli kutoka moyoni wapi utaangalia sana. Anhaa. Mi sijui. Ila popote utakapoangalia naturally umevutwa kwa sababu huku ndo kuna nguvu kama sumaku inayoweza kukuvuta zaidi.

Kijana ukiingia mitandaoni ukaanza na page ambayo inakupa nyepesi nyepesi kwanza mpaka ukasuuzika roho yako hapo ndo ukaanza sasa kuscroll uone kama kuna kingine cha kukusaidia kupeleka bando ukingoni kabla haijachacha.. hahaaaaa. Ok. Like seriously, kule ulikoanzia ndo kuna gravitational pull huko. 

Kimsingi basi ni kwamba nguvu inayokuvuta inatosha sana kukupa majibu ya wapi unaelekea katika safari yako ya mafanaikio au la.
Kumbe siyo tu kuandika malengo na kuyafanyia kazi. Unapaswa kuwa na watu sahihi wanaokuzunguka na pia kujua upande nini ili uvune nini na pia kujua nguvu gani iliyo ndani yako na inavutiwa zaidi na vitu gani vilivyo nje yako. Usipoangalia utapoteza muda mwingi wa maisha yako mafupi ya hapa duniani kuvutwa na nguvu ya vitu visivyokuwa muhimu. 

Mwaka 2010 nilisoma kitabu cha Robin Sharma niliyemtaja pale juu kiitwacho THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI ambamo ndani yake anasema ukitaka kufanikiwa lazima ufanye mambo kama roketi zinavyofanya. Kwambo roketi hutumia nguvu ya ziada na mafuta mengi sana ku-launch maana zinatakiwa zishindane na nguvu kubwa ya uvutano na ziishinde ndo ziweze kwenda huko  outer space. Akasema na wewe inabidi upingane na nguvu zinazokuvuta kukurudisha chini ili uweze kufika kwenye outer space yako. Kwenye mafanikio yako. Sijawahi kusahau.

Kwa hiyo unapaswa kuangalia pia hilo. Pingana na nguvu zinazokuvuta kukurudisha chini. Una malengo makubwa na ndoto nzuri lakini kuna nguvu ya marafiki wabaya inakuvuta kukurudisha chini.  Usipoishinda utarudi chini tu. Si unaona ukisimama halafu ukaruka juu. Huwa huendelei kwenda juu huwa unarudi chini tu. Hata wale rafiki zetu wamasai wanaruka wima wima wale lakini huwa wanarudi chini. Wanavutwa na nguvu wasiyoweza kuishinda. Kuna watu wanavutwa na mahusiano yasiyofaa, kuna watu wanavutwa nyuma na kupenda usingizi sana, kuna watu ni kuchati. Yani hawezi kushinda nguvu ya kuchatichati. Kuna watu ni habari za siasa na mpira na shilawadu. Yani zisipokuwepo anaweza kuumwa. Lakini na yeye anataka kufanikiwa kutimiza ndoto zake. Kweli?

Hilo pia nililiona na nikaona kuna vitu vinanivuta kwa nguvu kweli, lakini ili niwe yule Mungu alliyenikusudia kuwa yanipasa niondoke kwa nguvu ya roketi pia. Nimeona nishee hili pia kama litakusaidia. 


4.       KANUNI YA MVUTO (LAW OF ATTRACTION)
Miaka mingi iliyopita nikiwa mtoto wa shule ya msingi huko kijijini nilikuwa napenda kuimba nyimbo za bendi nk. Kuna siku mama akanisikia naimba wimbo wenye maneno yafuatayo: “SINA RAHA MASIKINI MIMI, SINA RAHA HATA KIDOGOO EEE.. KULALA KWANGU GHETO, MAISHA YANGU GHETTO....” wale wanaoufahamu nadhani wanaelewa. Mama alisikitika sana akaniomba nisiumbe tena maishani kwa sababu siyo wimbo mzuri. Lakini nikawa naimba kwa siri. Hahahaaa.. Miaka mingi imepita sasa na nikitazama mambo ya aina hiyo najifunza kuwa kumbe kweli nguvu ya maneno ni kubwa sana maana kuna kipindi kweli nilikuja kuishi ghetto na ‘masela’ maisha magumu kweli.  Na wakati naishi ghetto hivyo sikuwahi kuwaza kuwa kuna connection yoyote ya maneno yangu ya zamani na uhalisia huo.

Kimsingi kanuni hii haina tofauti na kanuni ya kupanda na kuvuna ambayo kama nilivyosema ni mzaliwa wa kwanza wa kanuni ya CAUSE AND EFFECT. 

Yaani sikuishi tu ghetto hivi hivi. Kwa maneno yangu na kuimba kwangu na hisia nilizokuwa naziweka nikiwa naimba nilikuwa naanzisha KISABABISHI cha hali ninayoiimba toka utoto. Nilikuwa na-ATTRACT hali hiyo maishani mwangu. Bila kujua. Nilikuwa najenga negative faith bila kujua.

Vile ulivyo, mambo unayoyamini, mambo unayoyasema ni mbegu. Inaenda kuATTRACT vitu unavyotamka bila wewe kutaka. Kuna mtu anasema hivi: YANI MIMI NIKIWA NAENDA KITUO CHA DALADALA HUWA NAKUTA DALADALA INAONDOKA YANI LAZIMA NIKUTE HIVYO. Huyu anasema kitu anachohisi hakina madhara yoyote. Mwingine anasema MSHAHARA UKITOKA BANA MI NAJILIA ZANGU RAHA BANA KUJIBANABANA YA NINI KAMA IPO IPO TU... Haya hizo kauli nyepesi nyepesi zisizotii kanuni za asili. Unapanda mbegu. Inaenda kuaATTRACT maisha yasiyoleta matunda mazuri maana hutaki kutii kanuni husika.

Mafanikio si kitu cha ku-PURSUE mafanikio ni kitu unacho ATTRACT kwa vile unavyozidi kuwa. Mfano kama hujawa mtu ambaye unastahili kumiliki pesa nyingi huwezi kuziattract. Utakuta unalazimisha tu zije wakati hujaweza kuwa na urafiki nazo. Haziwezi kujiASSOCIATE na wewe. Ukilazimisha utaleta matatizo.

Nilimpa mfano kijna mmoja anaishi maeneo ya Kimara hapa Dar es Salaam hivi karibuni nikamuuliza kwamba itatokea nini maji ya mto Ruvu yakiamuriwa na nature yatoke huko yaliko yaje nyumbani kwenu. Akasema yatabomoa nyumba. Nikamuuliza kwa nini? Akasema sababu hakuna kitu cha kuya-contain yaingie na kutulia. And yes. Maji yakienda nje ya utaratibu wake ulioamriwa bila kuwa na nguvu ya kuyazuia huleta uharibifu usiopimika. Nikamwambia ndivyo na pesa zilivyo. Ukilazimisha milioni 100 zipite mikononi mwako kabla hujawa tayari zitafurikisha maisha yako nay a wengine pia.

Kwa hiyo badala ya kuweka lengo tu la kupata mahela mengi weka lengo la kuwa mtu sahihi. Pesa sahihi itakuja. Kama pesa sahihi kwa jinsi ulivyo sasa ni laki 5 kwa mwezi itakuwa hiyo. Hata ukipata milioni mbili hutaiweza. Kama pesa sahihi kwako ni milioni 100 kwa mwezi utaipata na wala hutanyanyua mabega wala kutukana trafiki njiani tena inawezekana hakuna atakayejua. Benki tu ndo zitajua na watu wachache wa karibu na TRA labda. Lol.

Nikazingatia pia hili. Na lilileta kwangu matokeo mazuri mno na linazidi kunipatia matokeo mazuri kila siku. Badala ya kukimbizana na kufanikiwa inabidi mafanikio yanikimbize mimi. Sasa hapa kwenye mafanikio kukukimbiza siongelei habari za uganga hapa. Maana kuna watu ni mwendo kasi sana. Huko kwetu zamani kuna jamaa alimpenda binti. Akaenda kwa mganga. Apate dawa ya kupendwa na yule binti. Sasa mganga akamwambia jama njoo keshokutwa na yule ndege mwenye rangi rangi nyingi yule. Kule kijijini tulikuwa tukimwita “engolobhya” na pia uje na jogoo mweupe. Jamaa akamsaka akampata. Mganga akachukua zake jogoo kama kawaida halafu akamchinja yule ndege akatoa firigisi halafu akaipakazapakaza ile firigisi kwenye fimbo mbichi. Akaianika ile fimbo eti ikauke. Kisha akampa yule jamaa akamwambia sasa nenda ukimwona yule binti mpige na hii fimbo atakufata mpaka utakapoenda. Jamaa akaenda kisimani akategeshea yule binti alipofika tu kisimani jamaa akaenda taratibu akamtandika binti wa watu bonge moja la stiki binti akahamaki. Akaanza kumkimbiza yule jamaa hee jamaa ikabidi aanze kukimbia binti akamkimbiza mpaka kwao. Ikawa kesi kubwa sana sasa jamaa kujieleza hawezi lakini kumdai mganga hawezi maana mganga alisema atakufata popote utakapokwenda! Waganga hawana kitu ni akaili tu kidogo.

Sasa kwenye mafanikio usiishi kwa akili za kishirikina kama hizo. Mi naongelea kanuni. Jiweke katika hali ambayo mafanikio yatakata kona zoote mpaka yatakuja kwako! 

Kwa hiyo malengo ni sawa, bidii ni sawa, kujumuika na watu sahihi tumesema, kupanda mbegu sahihi ni muhimu, kuvutwa na mambo ya maana ni muhimu ili usije kuvutwa na yasiyo ya maana na hapa nimesema kujiweka katika hali amabayo unavuta vitu sahihi kwako. Wewe ndo unavivuta. Ukiwa kiongozi uongozi utakufata. Ukiwa si kiongozi utagombea kila kitu mpaka siku ya mwisho hupati. Na ukipata nature itakataa itakutema tu. Utalaumu watu lakini kuna kanuni haiko sawa. Kuna mtu anagombea ubunge jimbo gumu anapata. Kuna mwingine udiwani kata nyepesi tu hapati. Huyu hajaattract hiyo position. Kuattract siyo suala la kutembea unatamka kuwa ntakuwa raisi ntakuwa mbunge. No. Unapaswa kuwa raisi NDANI YAKO kwanza. Yesu alisemaje OSHA KIKOMBE NDANI KWANZA.....nje patakuwa safi tu penyewe. 

Kuattract mafanikio inabidi uoshe kikombe ndani. Character sahihi. Hapa nilijifunza the hard way. Na nimekuwa mwanafunzi mwenye kujifunza mno enoe hili kwa sababu ya unyeti wake. Kuna level fulani ya success huwezi kuifikia kama kikombe ndani ni kichafu. Hata kama nje ni pasafi kivipi. Mafanikio yanataka yaingie kwenye kikombe chako. Na huwa yana kawaida ya kunusa kwanza kikombe chenyewe. Yesu akasema, Safisha kikombe ndani kwanza...

Alijua asili inafanyaje kazi. Uko tayari kujifunza pia? Fanyia kazi. 


KANUNI YA TAFSIRI YA MPANGILIO WA MAMBO (LAW INTEPRETING THE ALIGNMENT OF THINGS)
Katika biblia kuna mambo kadhaa yaliyowahi kutokea yanayoweza kutusaidia kuelewa hii kanuni. Mfano kwa habari za kuzaliwa kwa Yesu kuna mambo kadhaa yaliyotokea na kujipanga sawia ku-indicate kitu kisicho cha kawaida. Mfano mamajusi na habari ya nyota. Malaika na wachungaji wa mifugo usiku. Nk.

Kwa habari za kifo cha Yesu kuna habari za pazia la helaku kuchanika katikati toka juu hadi chini, Kuna jua kuwa giza kwa masaa matatu, kuna tetemeko kubwa la ardhi. Na kuna AKIDA wa utawala wa RUMI (Roman Centurion) ambaye alikuwa amesimamia zoezi zima la kuhakikisha mtu anayeitwa Yesu Mnazareti anakufa kama hukumu ilivyokuwa imetolewa na mamlaka. Tunaambiwa huyu mtu ALIPOONA hayo yaliyotokea (kwa yale aliyoona mwenyewe) ile alignment ya mambo ikampa jibu moja tu: “HAKIKA HUYU ALIKUWA MWANA WA MUNGU”.

Interpretation ya NATURAL ALIGNMENT OF THINGS. Mungu alituwekea alama nyingi mno kuthibitisha kuwa yupo. Na akaweka kanuni nyingi za kutusaida kutambua mambo yaliyopo na yajayo. Ukiwa mwanafunzi mzuri wa nature pia utajifunza vitu vikubwa mno katika mambo yanayoonekana ya kawaida. Confucius aliwahi kusema ukiwa na utayari wa kujifunza unaweza kujifunza hata kwenye MWAMBA. 

Nikiwa mdogo nilikuwa naambiwa ukiona sisimizi wanatoka nje ya nyumba wanaingia ndani na wamebeba mayai yao ujue siku hiyo ama siku chache sana mvua itanyesha. Sasa sisimizi wanajuaje ni kitu kingine lakini hapa naongelea kujifunza kwenye asili. Na kweli mvua ilikuwa inanyesha katika timeframe hiyo.

Tukiwa tunawinda kuna milio ukisikia ndege wanalia wengi kwa wakati mmoja unaweza kukuta kuna nyoka mahali hapo. Na ikawa tunaona kweli kuna nyoka. Mvua ikinyesha ng'ombe wakalia sana usiku ujue mafuriko yanaweza kutokea na kweli mafuriko yanatokea.
Yapo mengi. 

Point yangu hapa ni kuwa kuna haja ya kutazama ASILI na kujua namna ya kuitafsiri kulingana na hali ilivyo. Kuna mambo Mungu alitaka tujifunze kwenye ASILI. Kamtazame chungu ewe mvivu! Hiyo ni Mungu anasema mtu mvivu anatakiwa akajifunze bidii kwa ANTS!! 

Kumbuka kufanikiwa nje ya season yako siyo mafanikio. Kama kuna mzee sasa hivi aliyekuwa na ndoto ya kuandika kitabu kuhusu jinsi ya kuimarisha chama labda cha AFRO SHIRAZI PARTY halafu anataka akiandike sasa hivi, dah, ni kweli amefanya lakini ni out of season. Enzi hizi na Afro Shiraz tofauti. 

Njia mojawapo ya kufanikiwa inside of your season yako ni kujifunza sana kwenye ASILI. Nature has so many answers kuhusu mafanikio yako. Kila mtu unayekutana naye, kila unachosoma kuna namna ambavyo vinaathiri destiny yako.
Nature haiwezi kudanganya. Yule akida alikuwa anajua kutasfiri nature’s alignemnet of things. Kuna watu lukuki walikuwa pale lakini ni yeye tu aliyeona kuwa tafrisi sahihi ya mambo yaliyotokea pale Fuvu la Kichwa ilikuwa ni ujumbe kuwa huyu mtu alikuwa ni MWANA WA MUNGU.

Kuna wakati ASILI itakuletea mke au mume usijue. Mvua imenyesha daraja limevunjika mko stranded upande wa pili wa barabara nature imeleta tukio ili kukukutanisha na mke/mume au business partner mtarajiwa wewe uko busy unachati na kutuma picha za daraja WhatsApp. 

Kwa kuwa tunaishi kipindi cha kutokuwa sensitive na Mungu na ASILI itokanayo na  yeye ndo vitu kama hivyo tunaishia kulaani mvua kwa nini inanyesha mjini. Internal antennas zetu zimeota kutu siku nyingi. We can't tell a B from a Bull. Unaota ndoto unapotezea tu unasema kwa kuwa usiku nilikula ugali ndo maana nikaota niko DUBAI. Tena unajiambia eti DUBAI NA MIMI WAPI NA WAPI? Hahaaaaa. Antena iko na kutu. 

Jua limewaka sana likakupiga ile mbaya kumbe huenda Mungu anataka ukumbuke ile idea yako ya kuuza jusi za baridi wewe unakazana tu kulalamika jamani jua litatuua. Na litakuua kweli hata kama siyo leo. Maneno yana nguvu. Usishangae likakuchagua wewe ndo likupe kansa ya ngozi of all people. UZIMA NA MAUTI VIKO WAPI.........?  Biblia inasema viko kwenye uwezo wa ulimi wako. See?

Unasafiri kwenda South Africa mmetua tu mkaambiwa kuna fujo mtaani subirini kidogo. Au mtu wa kukupokea atafika baada ya nusu saa alichelewa kidogo. Usilaani. Unatakiwa kuwasha antenna. Fast. Nini ASILI inamaanisha. Nini MUNGU anataka kufanya na wewe. Usikute kuna kitu muhimu cha kufanya au mtu muhimu wa kuonana naye kabla hujatoka airport. 

Mafanikio yamewapita wengi kwa sababu ya kutokuwa sensitive na mahali walipo. Kuna watu walikaa na John Pombe Magufuli au mama Samia na pengine hawakuona umuhimu wa kuwa na ukaribu na Magufuli au Samia kwa miaka mingi tu. Leo hii anatamani angejua enzi hizo. Too late. Out of season.


Unajua kusudi na mambo yalivyojipanga maishani mwako? Umekosa ajira, unadhalilishwa kwenu, boyfriend kakuacha. Unaweza kuinterpret hayo mambo tofauti. OPRAH aliyainterpret  mambo ya aina hii tofauti. Ndo maana akawa OPRAH. JK ROWLINGS alitaka kujiua kwa sababu ya kumisintepret mambo lakini alipoaacha kujiua leo hii ni bilionea ili wewe ujifunze.
Una bidhaa yako unauza hakuna anayekubali kununua....

Colonel Sanders mwanzilishi wa KFC alipopokea pensheni yake akakata tama ya maisha akainterpret vibaya hiyo hali pia akataka kujiua. Lakini kabla ya kujiua akasema hebu ngoja nikaandike vitu amabavyo sijawahi kufanya. Kaandika. Ukawa mwanzo mpya na mawazo ya kujiua yakaishia hapo.Kama unasoma hii article na ulishawaza kukatisha uhao wako, au wa mtu, hujatafsiri ASILI kwa usahihi. Asili ikitaka ufe haihitaji uisaidie. Mungu akitaka ufe hahitaji umsaidie hiyo kazi. ASILI bado inakuhitaji uwepo.

Hilo nalo nikajifunza na kulitazama kwa makini. Nalo nialifanyia kazi kila mara. Na nina shuhuda za jinsi kuwasha antenna zangu za ndani kulivyonisaidia sana katika safari yangu ya mafanikio. Ujifunze pia kama utaona yafaa. ASILI ni mwalimu mzui ukijifunza vema kutafsiri mafunzo yake kwa usahihi. Kwa hiyo ukijua kwa nini mambo yamejipanga jinsi yalivyojipanga maishani mwako sasa. Kwa nini umefiwa. Kwa nini umeachwa. Kwa nini umefilisika. UKIJUA USAHIHI WAKE utapiga hatua haraka sana.


Ninatumaini makala hii imekuwa muhimu kwako. Kama ndivyo nitafurahi kupata maoni yako. 

Mungu akubariki na kukufanikisha katika safari yako ya mafanikio.


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp +255788366511