WANT
SUCCESS? BE A STUDENT OF NATURE TOO.
UNATAKA
MAFANIKIO? KUWA MWANAFUNZI WA ASILI PIA
Kwa muda mrefu nimekuwa mwanafunzi wa mafanikio hasa kutoka
kwa watu mbali mbali ambao ninahisi kwao nina mengi ya kujifunza mambo mbali
mbali. Ninajifunza kwa kusoma kwenye vitabu mbali mbali, kukutana na watu face
to face, pia kwenye Internet hasa YouTube videos, na pia kufuatilia wasemayo
watu mbali mbali (ambao naamini Mungu aliwekeza kitu muhimu ndani yao) kwenye
kurasa zao katika mitandao ya kijamii kama hapa Facebook, LinkedIn, Twitter na Instagram.
Kwa mfano Facebook kina ninapo-login kabla sijasoma chochote
huwa napitia kurasa 10 kwanza kuona
walichoandika zikiwemo za wafuatao:
1.
James Mwanga’mba
2.
Mohamed Dewji
3.
Grant Cardone
4.
Robin Sharma
5.
Strive Masiyiwa
Na zinginezo....
Nimejifunza mengi na ninamshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya
kujifunza kutoka kwao kwa kweli. Kama ni chakula ninapata ladha tofauti tofauti
na virutubisho tofauti tofauti ili afya yangu kuanzia shingoni kwenda juu izidi
kukaa sawa. Najifunza pia kupitia comments mali mbali za watu wanapita katika
kurasa hizo. Mfano juzi Cardone
alipost akiuliza watu waseme MALENGO YAO
MAKUBWA waliyowahi kuyaweka ni yapi and ukipitia comments niliweza kujua
binadamu wenzangu duniani wana malengo yapi makubwa na hivyo kujifunza binadamu
wenzangu wanawaza nini kuhusu maisha haya mafupi ambayo tumekodishwa na Mungu
kwa kitambo.
Nawaombea wote wanaoshirikisha mawazo yao mema Mungu azidi
kuwabariki na kuwawezesha kufanya hivyo ili waweze kuhuisha yale yaliyokufa
ndani ya watu na kuchochea yale yaliyo hai.
Kutokana na kujifunza kwangu kutoka huko kote na kwa uzoefu
wangu wa kuupitia mchakato wa mafanikio nimetambua jambo moja muhimu ambalo
zamani sikuwa nalijua kuhusu mafanikio. Nalo ni hili: UKIWA MWANAFUNZI MZURI WA
ASILI (NATURE) UTAYAFIKIA MAFANIKIO YAKO KWA WAKATI MUAFAKA ZAIDI.
Iwe unaamini katika Mungu au la hiyo haiondoi ukweli kwamba
ASILI (nature) ipo na inaendeshwa na taratibu fulani ambazo hazibadiliki toka
enzi na enzi. Na kwamba taratibu hizo uwe unazijua au huzijui zinaathiri namna
utakavyoishi hapa duniani na yale utakayopata
au yatakayokupata ungali hapa
ulimwenguni. Taratibu ama kanuni hizo zimekuweko toka zamani zilizopita zip
oleo na zitakuwepo zamani zijazo. Mfano kanuni isemayo: unachopanda NDICHO utakachovuna.
Kwa kutazama kwangu maisha yangu binafsi na ya vijana
wenzangu na hata watu wazima katika eno hili la kupata mafanikio nikajifunza
kuwa pamoja na kuwa wengi wetu tunajifunza kwa watu mbali mbali kama nifanyavyo
mimi lakini tumesahau kuzingatia kanuni muhimu wanazofundisha hasa zile
zinazoendesha asili (nature).
Kujaribu kutafuta mafanikio pasipo kuzitii hizi taratibu ama
kanuni muhimu ni kujaribu kuidanganya ASILI kitu ambacho huwa hakina manufaa
kwani hakiwezekani. You can’t cheat
nature. Huwezi kuidanganya asili. Nakualika uendelee kuwa nami hapa chini
ninapojaribu kuzielezea baadhi ya hizo kanuni ili uone kama zinaweza kukusaidia
pia katika mchakato wako wa kuyaendea mafanikio uyatakayo.
1.
KANUNI YA MJUMUIKO (THE LAW OF ASSOCIATION)
Ulishawahi kuona video iitwayo THE CHICKEN AND THE EAGLE?
Unaweza kuitazama hapa https://www.youtube.com/watch?v=dHAfVl-t1Hg
na itakusaidia kuelewa hili nitakaloeleza hapa chini..
Kwa asili ni kwama vitu vinavyofanana vina kawaida ya
kujumuika pamoja, kuenenda pamoja na kufanya mambo yao kwa namna inayofanana. Watu
wa kale waliliona hili wakasema vitu kama: Ndege wafananao huruka pamoja.. kama ndege hawa wawili waitwao Steve Jobs na Bill Gates katika picha yao hii mwaka 1985
Ni
muhimu sana kama candidate wa Mafanikio ukalijua hili na kulizingatia sana. Wengine
wakaitazama hii na kuiweka hivi: Kwa kawaida wewe utakuwa ni wastani wa watu
watano wa karibu unaojumuika nao kila mara. Kwa maana nyingine ni kwamba
ukitaka kujua mafanikio yako yatakuwa kwa kiwango gani angalia mafanikio ya
watu wako wa karibu watano. Mwingine aliyeiona kanuni hii ya asili akasema
ukikaa sana na watu wanne wasio na kipato unajua nini kitatokea? Halafu akajibu
hilo swali kwa kusema: WEWE UTAKUWA WA TANO.
Jambo hili ndo linasabisha uone jinsi inavyokuwa ngumu kwako
kuwa mtu wa karibu wa Dewji “from nowhere” tu. Si kwamba hapendi binadamu
wengine ila anaheshimu kanuni hii. Anatii ASILI inachotaka. Asili inamtaka awe
na watu wa aina fulani karibu ili weweze kumpasha habari sahihi na kumpeleka
mahali sahihi kwa nyakati sahihi ili aweze kuyafikia yale anayoyataka. Kama
hujawa aina hiyo ya mtu ASILI itakataa ukaribu wako na Dewji. Hata ukiwa jirani
yake au mnasali msikiti mmoja au mko gym moja na treadmill anayotumia ndo na
wewe unatumia. Utaishia kusema tu Dewji tuko naye gym moja yule.
Unapoanza kutii kanuni hizi hazitofautishi mpagani au mtu wa
dini au mtu anayeamini kuwa kanuni zenyewe zipo au ni uzushi tu. Ukizifata
utapata matokeo. Ukijumuika sana na wavivu utakuwa kama wao, ukijumuika sana na
wasomaji vitabu utaanza tu kuongea na kuwa kama wao, ukikaa sana na watu
wanosemekana kuwa wako kwenye “system” si muda mrefu utaanza kuwa na tabia na
lugha na haiba ya aina hiyo. Ukijumuika sana na walalamishi utaanza kulalamika
na kulaumu laumu tu kila kitu. Ukijumuika sana na wakosoaji kila kitu utaanza kuwa mkosoaji pia na hata
hutaona kuwa umebadilika.
Kama wewe ni mwanafunzi ukijumuika sana na wanafunzi
wanaonyoa viduku na kuvuta ile kitu kwa siri basi utajikuta umekuwa mmoja wao. Kama
wewe ni mchungaji au mfanyabiashara ukijumuika sana na watu wanaovaa mapetepete sijui ya
bahati na kupiga ramli na kuvuta watu utajikuta na wewe una mapetepete na vitu
vya aina hiyo. Ndege wafananao.....
Ukijumuika na walevi au watumia mihadarati vivyo hivyo kuna
aina fulani ya tabia utaanza kufanana nao. Wewe ni tai lakini utajikuta unaishi na kuenenda kama
kuku. Na hata ukiambiwa kuwa unatakiwa kutoka miongoni mwa kuku unaweza kuona
wanaokwambia ndo hawajui kitu kuhusu wewe. Kumbe shida ni kanunu hii unaiishi
ndivyo sivyo. Ukifollow page za umbea utakuwa mbea
ukifollow za wanaotoa taarifa sahihi kuhusu maisha, mahusiano, biashara, nk
utaanza kuwaza kama wao.
Sasa ukidhani kuwa kufanikiwa ni kuwa na ndoto tu na kuweka
malengo hapo na kufanya kazi kwa bidii ukaignore kanuni hii ukajiendea tu na
kujijumuisha tu na any THOM, DICK AND HARY unaweza kuwa frustrated kwa nini
huoni mafanikio mapema. Angalia basi kila unayeona amefanikiwa kwa definition
yako mwenyewe halafu uone kama katika marafiki zake watano wa KARIBU kuna mtu asiye
na tabia za kimafanikio. Chunguza mwenyewe. Utapata majibu sahihi. Mimi
nililitazama hilo nikajifunza kumbe
nahitaji kuiitii kanuni hii pia KWANZA!
2.
KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA (THE LAW OF SOWING
AND REAPING)
Unaonaje kama ingekuwa ukipanda mahindi unakuwa hujui kitakachoota
ni mchele au minazi au mipapai! Unadhani hiyo level ya uncertainty ingeathiri
vipi maisha yetu?
Lakini kanuni hii ya asili ikawekwa. Na hii inapatikana hasa
ndani ya kanuni nyingine kubwa inayojulikana kama KANUNI YA KISABABISHI NA
MATOKEO (ama the LAW OF CAUSE AND EFFECT) ambayo inasema kuwa hakuna kitu
kinachotokea kwa bahati mbaya tu yani from nowhere ila huwa kuna kisababishi
kwa kila jambo unaloona linatokea. Yaani ukiona ardhi imechipusha mahindi ujue
kuna kilichosababisha. Na hapa ndo kanuni ya kupanda na kuvuna inapoingia.
Anhaa!
Kumbe kilichosababisha ni kuwa kuna kilichopandwa.
Katika vitabu
ninavyokusihi upitie kujiffunza bila kujali imani yako ni Biblia. Mfano ndani
ya kitabu hiki tunapata reference ya kanuni hii. Kitabu cha Wagalatia 6:7 na
kitabu cah Ayubu 4:8. Wagalatia wakaambiwa kuwa Mungu hadhihakiwi bali
apandacho mtu ndicho atakachovuna! Hii ni kauli kali sana. Kali kwa sababu
inalinganisha kutegemea kuvuna usichopanda kumbe ni sawa na KUMDHIHAKI MUNGU. Unataka
kucheat kanuni zake za uumbaji wa mambo. Unataka kumfanya Mungu kama asiyejua
alichoweka in place.
Watu wote waliofanikiwa wanaitumia hii kanuni vlivyo. Kama
ilivyo ukipanda mahindi unavuna mahindi ndivyo ilivyo pia ukipanda mahindi
MENGI utavuna mengi. Kama wewe ni mwanamichezo ukifanya mazoezi mengi utapata
matokeo bora zaidi ya asiyefanya mazoezi kabisa. Michael Phelps ni muogeleaji wa
Marekani anayeongoza kwa medali za dhahabu za Olympic duniani kwa michezo yote
inayochezwa kwenye Olympics.
Mojawapo ya kitu alichowahi kufanya ni kufanya
mazoezi makali kila siku mwaka mzima kwa miaka mitano mfululizo bila kukatisha. Kuna kukimbia, kunyanyua vuma, na kuogelea. na kwa
juma moja anaogelea takribani kilometa 80. Umbali huo ni kama kutoka Dar es
Salaam hadi Zanzibar kwa mtari mnyoofu (https://www.distancecalculator.net/from-dar-es-salaam-to-zanzibar)
Sasa mtu anayepanda hilo unahisi anapaswa avune nini? Akivuna
medali nyingi za dhahabu kwenye Olympics kuliko binadamu yeyote unashangaa?
Tuna waogeleaji ambao wana huo uthubutu? Na je wewe na mimi katika maeneo yetu
ya kuogelea (ndoto zetu) tunapanda bidii kiasi hicho?
Nasema tena ukidhani kufanikiwa ni kuandika malengo tu na
kuyafanyia kazi ukashindwa kujua kumbe kwenye kufanya kazi ukipanda sana mgongo
ukauma jua likakutandika sawasawa na ukachoka kweli kweli ndipo utavuna kwa
kiwango cha “kutisha” basi utatamani mafanikio makubwa ya wengine bure bila
kujua unatakiwa uogelee Dar hadi Zanzibar kwa wiki moja pia. Nilikuwa najiona
ni mwenye bidii katika mambo yangu hadi nilipoanza kujua ratiba za watu
waliofanikiwa katika maeneo ya ndoto zao ndipo nikaona nina kazi kubwa ya
kufanya pia. Nimeona nishee na wewe huenda nawe ukaona unahitaji kukaza kamba
za viatu zaidi.
3.
KANUNI YA NGUVU YA UVUTANO (LAW OF GRAVITATIONAL
PULL)
Hivi Isaac Newton alipokuwa anafikiria kuhusu lile apple
sijui kama alijua ilikuwa ni observation muhimu sana siku ile. Mojawapo ya
nguvu kubwa mno za asili ni nguvu ya uvutano. Dunia hii inategemea mno nguvu
hiyo na kumbe hata kutembea kwako juu ya ardhi ni kwa sababu ya nguvu hiyo.
Yani wewe haujasimama wala kukaa wala kulala ardhini hivi hivi (CAUSE AND
EFFECT) ila kuna nguvu inakuvuta. Ikikata hiyo tutaelea huko angani na kila
kitu kinachojongea juu ya uso wa dunia kitaelea huko angani kuanzia hapo! Ajabu
iliyoje!
Ndipo nikajifunza kuwa ASILI iliweka hilo nalo litufundishe
kitu. Yeyote anayetaka kufanikiwa hana budi kutii kanuni hii ya gravitation.
Siku zote utavutwa pale ambapo nguvu ya kukuvuta ilipo.
Hivi nguvu yako iko wapi? Katika mambo ya mafanikio ama
katika mambo yasiyo ya mafanikio?
Huenda hujanielewa. Labda nitoe mfano. Ukapita Kariakoo
ukakuta kuna TV nje ya duka zinauzwa ila zinaonyesha matukio mbali mbali. Moja
inaonyesha Eric Shigongo anazungumzia jinsi ya kujikwamua kutoka katika hali
ngumu, nyingine inaonyesha Askofu Gwajima yuko LIVE anasema ana siri nzito
anataka kuitoa. Wewe binafsi kiukweli kutoka moyoni wapi utaangalia sana.
Anhaa. Mi sijui. Ila popote utakapoangalia naturally umevutwa kwa sababu huku
ndo kuna nguvu kama sumaku inayoweza kukuvuta zaidi.
Kijana ukiingia mitandaoni ukaanza na page ambayo inakupa
nyepesi nyepesi kwanza mpaka ukasuuzika roho yako hapo ndo ukaanza sasa
kuscroll uone kama kuna kingine cha kukusaidia kupeleka bando ukingoni kabla
haijachacha.. hahaaaaa. Ok. Like seriously, kule ulikoanzia ndo kuna
gravitational pull huko.
Kimsingi basi ni kwamba nguvu inayokuvuta inatosha sana
kukupa majibu ya wapi unaelekea katika safari yako ya mafanaikio au la.
Kumbe siyo tu kuandika malengo na kuyafanyia kazi. Unapaswa
kuwa na watu sahihi wanaokuzunguka na pia kujua upande nini ili uvune nini na
pia kujua nguvu gani iliyo ndani yako na inavutiwa zaidi na vitu gani vilivyo
nje yako. Usipoangalia utapoteza muda mwingi wa maisha yako mafupi ya hapa
duniani kuvutwa na nguvu ya vitu visivyokuwa muhimu.
Mwaka 2010 nilisoma kitabu
cha Robin Sharma niliyemtaja pale juu kiitwacho THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI
ambamo ndani yake anasema ukitaka kufanikiwa lazima ufanye mambo kama roketi
zinavyofanya. Kwambo roketi hutumia nguvu ya ziada na mafuta mengi sana
ku-launch maana zinatakiwa zishindane na nguvu kubwa ya uvutano na ziishinde
ndo ziweze kwenda huko outer space.
Akasema na wewe inabidi upingane na nguvu zinazokuvuta kukurudisha chini ili
uweze kufika kwenye outer space yako. Kwenye mafanikio yako. Sijawahi kusahau.
Kwa hiyo unapaswa kuangalia pia hilo. Pingana na nguvu
zinazokuvuta kukurudisha chini. Una malengo makubwa na ndoto nzuri lakini kuna
nguvu ya marafiki wabaya inakuvuta kukurudisha chini. Usipoishinda utarudi chini tu. Si unaona
ukisimama halafu ukaruka juu. Huwa huendelei kwenda juu huwa unarudi chini tu.
Hata wale rafiki zetu wamasai wanaruka wima wima wale lakini huwa wanarudi
chini. Wanavutwa na nguvu wasiyoweza kuishinda. Kuna watu wanavutwa na
mahusiano yasiyofaa, kuna watu wanavutwa nyuma na kupenda usingizi sana, kuna
watu ni kuchati. Yani hawezi kushinda nguvu ya kuchatichati. Kuna watu ni
habari za siasa na mpira na shilawadu. Yani zisipokuwepo anaweza kuumwa. Lakini
na yeye anataka kufanikiwa kutimiza ndoto zake. Kweli?
Hilo pia nililiona na nikaona kuna vitu vinanivuta kwa nguvu
kweli, lakini ili niwe yule Mungu alliyenikusudia kuwa yanipasa niondoke kwa
nguvu ya roketi pia. Nimeona nishee hili pia kama litakusaidia.
4.
KANUNI YA MVUTO (LAW OF ATTRACTION)
Miaka mingi iliyopita nikiwa mtoto wa shule ya msingi huko kijijini
nilikuwa napenda kuimba nyimbo za bendi nk. Kuna siku mama akanisikia naimba
wimbo wenye maneno yafuatayo: “SINA RAHA MASIKINI MIMI, SINA RAHA HATA KIDOGOO
EEE.. KULALA KWANGU GHETO, MAISHA YANGU GHETTO....” wale wanaoufahamu nadhani
wanaelewa. Mama alisikitika sana akaniomba nisiumbe tena maishani kwa sababu
siyo wimbo mzuri. Lakini nikawa naimba kwa siri. Hahahaaa.. Miaka mingi imepita
sasa na nikitazama mambo ya aina hiyo najifunza kuwa kumbe kweli nguvu ya maneno
ni kubwa sana maana kuna kipindi kweli nilikuja kuishi ghetto na ‘masela’ maisha magumu kweli. Na wakati naishi ghetto hivyo sikuwahi kuwaza
kuwa kuna connection yoyote ya maneno yangu ya zamani na uhalisia huo.
Kimsingi kanuni hii haina tofauti na kanuni ya kupanda na
kuvuna ambayo kama nilivyosema ni mzaliwa wa kwanza wa kanuni ya CAUSE AND
EFFECT.
Yaani sikuishi tu ghetto hivi hivi. Kwa maneno yangu na
kuimba kwangu na hisia nilizokuwa naziweka nikiwa naimba nilikuwa naanzisha
KISABABISHI cha hali ninayoiimba toka utoto. Nilikuwa na-ATTRACT hali hiyo
maishani mwangu. Bila kujua. Nilikuwa najenga negative faith bila kujua.
Vile ulivyo, mambo unayoyamini, mambo unayoyasema ni mbegu. Inaenda
kuATTRACT vitu unavyotamka bila wewe kutaka. Kuna mtu anasema hivi: YANI MIMI
NIKIWA NAENDA KITUO CHA DALADALA HUWA NAKUTA DALADALA INAONDOKA YANI LAZIMA
NIKUTE HIVYO. Huyu anasema kitu anachohisi hakina madhara yoyote. Mwingine
anasema MSHAHARA UKITOKA BANA MI NAJILIA ZANGU RAHA BANA KUJIBANABANA YA NINI
KAMA IPO IPO TU... Haya hizo kauli nyepesi nyepesi zisizotii kanuni za asili.
Unapanda mbegu. Inaenda kuaATTRACT maisha yasiyoleta matunda mazuri maana
hutaki kutii kanuni husika.
Mafanikio si kitu cha ku-PURSUE mafanikio ni kitu unacho
ATTRACT kwa vile unavyozidi kuwa. Mfano kama hujawa mtu ambaye unastahili
kumiliki pesa nyingi huwezi kuziattract. Utakuta unalazimisha tu zije wakati
hujaweza kuwa na urafiki nazo. Haziwezi kujiASSOCIATE na wewe. Ukilazimisha
utaleta matatizo.
Nilimpa mfano kijna mmoja anaishi maeneo ya Kimara hapa Dar es Salaam hivi karibuni nikamuuliza kwamba itatokea nini maji ya mto Ruvu yakiamuriwa na nature yatoke huko yaliko yaje
nyumbani kwenu. Akasema yatabomoa nyumba. Nikamuuliza kwa nini? Akasema sababu
hakuna kitu cha kuya-contain yaingie na kutulia. And yes. Maji yakienda nje ya
utaratibu wake ulioamriwa bila kuwa na nguvu ya kuyazuia huleta uharibifu
usiopimika. Nikamwambia ndivyo na pesa zilivyo. Ukilazimisha milioni 100
zipite mikononi mwako kabla hujawa tayari zitafurikisha maisha yako nay a wengine
pia.
Kwa hiyo badala ya kuweka lengo tu la kupata mahela mengi
weka lengo la kuwa mtu sahihi. Pesa sahihi itakuja. Kama pesa sahihi kwa jinsi
ulivyo sasa ni laki 5 kwa mwezi itakuwa hiyo. Hata ukipata milioni mbili
hutaiweza. Kama pesa sahihi kwako ni milioni 100 kwa mwezi utaipata na wala
hutanyanyua mabega wala kutukana trafiki njiani tena inawezekana hakuna atakayejua.
Benki tu ndo zitajua na watu wachache wa karibu na TRA labda. Lol.
Nikazingatia pia hili. Na lilileta kwangu matokeo mazuri mno
na linazidi kunipatia matokeo mazuri kila siku. Badala ya kukimbizana na
kufanikiwa inabidi mafanikio yanikimbize mimi. Sasa hapa kwenye mafanikio
kukukimbiza siongelei habari za uganga hapa. Maana kuna watu ni mwendo kasi
sana. Huko kwetu zamani kuna jamaa alimpenda binti. Akaenda kwa mganga. Apate
dawa ya kupendwa na yule binti. Sasa mganga akamwambia jama njoo keshokutwa na
yule ndege mwenye rangi rangi nyingi yule. Kule kijijini tulikuwa tukimwita “engolobhya” na pia uje na jogoo mweupe.
Jamaa akamsaka akampata. Mganga akachukua zake jogoo kama kawaida halafu
akamchinja yule ndege akatoa firigisi halafu akaipakazapakaza ile firigisi
kwenye fimbo mbichi. Akaianika ile fimbo eti ikauke. Kisha akampa yule jamaa
akamwambia sasa nenda ukimwona yule binti mpige na hii fimbo atakufata mpaka
utakapoenda. Jamaa akaenda kisimani akategeshea yule binti alipofika tu
kisimani jamaa akaenda taratibu akamtandika binti wa watu bonge moja la stiki
binti akahamaki. Akaanza kumkimbiza yule jamaa hee jamaa ikabidi aanze kukimbia
binti akamkimbiza mpaka kwao. Ikawa kesi kubwa sana sasa jamaa kujieleza hawezi
lakini kumdai mganga hawezi maana mganga alisema atakufata popote
utakapokwenda! Waganga hawana kitu ni akaili tu kidogo.
Sasa kwenye mafanikio usiishi kwa akili za kishirikina kama
hizo. Mi naongelea kanuni. Jiweke katika hali ambayo mafanikio yatakata kona
zoote mpaka yatakuja kwako!
Kwa hiyo malengo ni sawa, bidii ni sawa, kujumuika na watu
sahihi tumesema, kupanda mbegu sahihi ni muhimu, kuvutwa na mambo ya maana ni
muhimu ili usije kuvutwa na yasiyo ya maana na hapa nimesema kujiweka katika
hali amabayo unavuta vitu sahihi kwako. Wewe ndo unavivuta. Ukiwa kiongozi
uongozi utakufata. Ukiwa si kiongozi utagombea kila kitu mpaka siku ya mwisho
hupati. Na ukipata nature itakataa itakutema tu. Utalaumu watu lakini kuna
kanuni haiko sawa. Kuna mtu anagombea ubunge jimbo gumu anapata. Kuna mwingine
udiwani kata nyepesi tu hapati. Huyu hajaattract hiyo position. Kuattract siyo
suala la kutembea unatamka kuwa ntakuwa raisi ntakuwa mbunge. No. Unapaswa kuwa
raisi NDANI YAKO kwanza. Yesu alisemaje OSHA KIKOMBE NDANI KWANZA.....nje
patakuwa safi tu penyewe.
Kuattract mafanikio inabidi uoshe kikombe ndani. Character
sahihi. Hapa nilijifunza the hard way. Na nimekuwa mwanafunzi mwenye kujifunza
mno enoe hili kwa sababu ya unyeti wake. Kuna level fulani ya success huwezi
kuifikia kama kikombe ndani ni kichafu. Hata kama nje ni pasafi kivipi.
Mafanikio yanataka yaingie kwenye kikombe chako. Na huwa yana kawaida ya kunusa
kwanza kikombe chenyewe. Yesu akasema, Safisha kikombe ndani kwanza...
Alijua asili inafanyaje kazi. Uko tayari kujifunza pia? Fanyia
kazi.
Katika biblia kuna mambo kadhaa yaliyowahi kutokea
yanayoweza kutusaidia kuelewa hii kanuni. Mfano kwa habari za kuzaliwa kwa Yesu
kuna mambo kadhaa yaliyotokea na kujipanga sawia ku-indicate kitu kisicho cha
kawaida. Mfano mamajusi na habari ya nyota. Malaika na wachungaji wa mifugo
usiku. Nk.
Kwa habari za kifo cha Yesu kuna habari za pazia la helaku
kuchanika katikati toka juu hadi chini, Kuna jua kuwa giza kwa masaa matatu,
kuna tetemeko kubwa la ardhi. Na kuna AKIDA wa utawala wa RUMI (Roman Centurion)
ambaye alikuwa amesimamia zoezi zima la kuhakikisha mtu anayeitwa Yesu
Mnazareti anakufa kama hukumu ilivyokuwa imetolewa na mamlaka. Tunaambiwa huyu
mtu ALIPOONA hayo yaliyotokea (kwa yale aliyoona mwenyewe) ile alignment ya
mambo ikampa jibu moja tu: “HAKIKA HUYU ALIKUWA MWANA WA MUNGU”.
Interpretation ya NATURAL ALIGNMENT OF THINGS. Mungu
alituwekea alama nyingi mno kuthibitisha kuwa yupo. Na akaweka kanuni nyingi za
kutusaida kutambua mambo yaliyopo na yajayo. Ukiwa mwanafunzi mzuri wa nature
pia utajifunza vitu vikubwa mno katika mambo yanayoonekana ya kawaida.
Confucius aliwahi kusema ukiwa na utayari wa kujifunza unaweza kujifunza hata
kwenye MWAMBA.
Nikiwa mdogo nilikuwa naambiwa ukiona sisimizi wanatoka nje
ya nyumba wanaingia ndani na wamebeba mayai yao ujue siku hiyo ama siku chache
sana mvua itanyesha. Sasa sisimizi wanajuaje ni kitu kingine lakini hapa
naongelea kujifunza kwenye asili. Na kweli mvua ilikuwa inanyesha katika
timeframe hiyo.
Tukiwa tunawinda kuna milio ukisikia ndege wanalia wengi kwa
wakati mmoja unaweza kukuta kuna nyoka mahali hapo. Na ikawa tunaona kweli kuna
nyoka. Mvua ikinyesha ng'ombe wakalia sana usiku ujue mafuriko yanaweza kutokea
na kweli mafuriko yanatokea.
Yapo mengi.
Point yangu hapa ni kuwa kuna haja ya kutazama
ASILI na kujua namna ya kuitafsiri kulingana na hali ilivyo. Kuna mambo Mungu
alitaka tujifunze kwenye ASILI. Kamtazame chungu ewe mvivu! Hiyo ni Mungu
anasema mtu mvivu anatakiwa akajifunze bidii kwa ANTS!!
Kumbuka kufanikiwa nje
ya season yako siyo mafanikio. Kama kuna mzee sasa hivi aliyekuwa na ndoto ya
kuandika kitabu kuhusu jinsi ya kuimarisha chama labda cha AFRO SHIRAZI PARTY
halafu anataka akiandike sasa hivi, dah, ni kweli amefanya lakini ni out of
season. Enzi hizi na Afro Shiraz tofauti.
Njia mojawapo ya kufanikiwa inside of your season yako ni kujifunza
sana kwenye ASILI. Nature has so many answers kuhusu mafanikio yako. Kila
mtu unayekutana naye, kila unachosoma kuna namna ambavyo vinaathiri destiny yako.
Nature haiwezi kudanganya. Yule akida alikuwa anajua
kutasfiri nature’s alignemnet of things. Kuna watu lukuki walikuwa pale lakini
ni yeye tu aliyeona kuwa tafrisi sahihi ya mambo yaliyotokea pale Fuvu la
Kichwa ilikuwa ni ujumbe kuwa huyu mtu alikuwa ni MWANA WA MUNGU.
Kuna wakati ASILI itakuletea mke au mume usijue. Mvua
imenyesha daraja limevunjika mko stranded upande wa pili wa barabara nature
imeleta tukio ili kukukutanisha na mke/mume au business partner mtarajiwa wewe
uko busy unachati na kutuma picha za daraja WhatsApp.
Kwa kuwa tunaishi kipindi cha kutokuwa sensitive na Mungu na
ASILI itokanayo na yeye ndo vitu kama hivyo tunaishia kulaani mvua kwa nini
inanyesha mjini. Internal antennas zetu zimeota kutu siku nyingi. We can't tell a
B from a Bull. Unaota ndoto unapotezea tu unasema kwa kuwa usiku nilikula ugali
ndo maana nikaota niko DUBAI. Tena unajiambia eti DUBAI NA MIMI WAPI NA WAPI?
Hahaaaaa. Antena iko na kutu.
Jua limewaka sana likakupiga ile mbaya kumbe huenda Mungu
anataka ukumbuke ile idea yako ya kuuza jusi za baridi wewe unakazana tu
kulalamika jamani jua litatuua. Na litakuua kweli hata kama siyo leo. Maneno
yana nguvu. Usishangae likakuchagua wewe ndo likupe kansa ya ngozi of all
people. UZIMA NA MAUTI VIKO WAPI.........?
Biblia inasema viko kwenye uwezo wa ulimi wako. See?
Unasafiri kwenda South Africa mmetua tu mkaambiwa kuna fujo
mtaani subirini kidogo. Au mtu wa kukupokea atafika baada ya nusu saa alichelewa
kidogo. Usilaani. Unatakiwa kuwasha antenna. Fast. Nini ASILI inamaanisha.
Nini MUNGU anataka kufanya na wewe. Usikute kuna kitu muhimu cha kufanya au mtu
muhimu wa kuonana naye kabla hujatoka airport.
Mafanikio yamewapita wengi kwa sababu ya kutokuwa sensitive na
mahali walipo. Kuna watu walikaa na John Pombe Magufuli au mama Samia na pengine
hawakuona umuhimu wa kuwa na ukaribu na Magufuli au Samia kwa miaka mingi tu.
Leo hii anatamani angejua enzi hizo. Too late. Out of season.
Unajua kusudi na mambo yalivyojipanga maishani mwako?
Umekosa ajira, unadhalilishwa kwenu, boyfriend kakuacha. Unaweza kuinterpret
hayo mambo tofauti. OPRAH aliyainterpret mambo ya aina hii tofauti. Ndo maana akawa OPRAH. JK ROWLINGS
alitaka kujiua kwa sababu ya kumisintepret mambo lakini alipoaacha kujiua leo
hii ni bilionea ili wewe ujifunze.
Una bidhaa yako unauza hakuna anayekubali kununua....
Colonel Sanders mwanzilishi wa KFC alipopokea pensheni yake
akakata tama ya maisha akainterpret vibaya hiyo hali pia akataka kujiua. Lakini
kabla ya kujiua akasema hebu ngoja nikaandike vitu amabavyo sijawahi kufanya.
Kaandika. Ukawa mwanzo mpya na mawazo ya kujiua yakaishia hapo.Kama unasoma hii
article na ulishawaza kukatisha uhao wako, au wa mtu, hujatafsiri ASILI kwa
usahihi. Asili ikitaka ufe haihitaji uisaidie. Mungu akitaka ufe hahitaji
umsaidie hiyo kazi. ASILI bado inakuhitaji uwepo.
Hilo nalo nikajifunza na kulitazama kwa makini. Nalo
nialifanyia kazi kila mara. Na nina shuhuda za jinsi kuwasha antenna zangu za
ndani kulivyonisaidia sana katika safari yangu ya mafanikio. Ujifunze pia kama
utaona yafaa. ASILI ni mwalimu mzui ukijifunza vema kutafsiri mafunzo yake kwa
usahihi. Kwa hiyo ukijua kwa nini mambo yamejipanga jinsi yalivyojipanga
maishani mwako sasa. Kwa nini umefiwa. Kwa nini umeachwa. Kwa nini umefilisika.
UKIJUA USAHIHI WAKE utapiga hatua haraka sana.
Ninatumaini makala hii imekuwa muhimu kwako. Kama ndivyo nitafurahi kupata maoni yako.
Mungu akubariki na kukufanikisha katika safari yako ya mafanikio.
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp +255788366511
Bro hongera sana kwa kaz unayoifanya.
JibuFutaHakika kwa haya madini uliyotoa yamenifanya niamini katika kufanikiwa.
Asante sana na mungu akubariki.