Alhamisi, 27 Oktoba 2016

IT TAKES "A LITTLE EXTRA" TO MAKE A DREAM COME TRUE


Katika zawadi kadhaa nilizowahi kupata maishani mwangu ambazo zilibadilisha maisha yangu moja wapo ni kadi ya kunitakia mafanikio mema katika mitihani yangu ya kumaliza kidato cha sita.

Kadi hiyo niliipata kutoka kwa walezi wangu Mr & Mrs Senga Kabipi aka baba na mama Laurent Kabipi. Nikiwa nimepitia mabonde na milima hadi kufikia kipindi cha mimi pia kuikabili NECTA ya Form VI, kadi hiyo ilikuja  katika kipindi muafaka sana ambacho nilikuwa nikihitaji binadamu yeyote wa kunitia moyo na kuniambia nitafanikiwa. Ninakumbuka daima nilivyotiwa nguvu na kitendo tu cha kupewa ile kadi. It was so powerful!

Hata hivyo ni maneno yaliyoandikwa kwenye hiyo kadi ambayo yalinifanya niikumbuke zaidi ile kadi hadi leo. Yalisema hivi:

Dear Andrea,

It takes A LITTLE EXTRA..

A LITTLE EXTRA COURAGE

A LITTLE EXTRA HOPE

A LITTLE EXTRA BELIEF

A LITTLE EXTRA PUSH

A LITTLE EXTRA STEP

It takes A LITTLE EXTRA EFFORT...

....TO MAKE A DREAM COME TRUE.

Wishing you all the best in your exams,

Yours,

Mr & Mrs Kabipi.

That was it. So baada ya kufurahi nikaanza kujiuliza kuhusu ujumbe huo. Nikawaza kweli eti. Huu ujumbe mbona unanipa mawazo tena. Bado siku mbili kufanya NECTA. Nimeshasongoka miaka miwili mizima nimejiandaa nimeshajiamini kuingia kwenye NYAMBIZI la Makongo High School. Afu naambiwa #EXTRA tena? Lakini moyoni nikasema Mungu huenda ameniletea ujumbe muhimu mno kunisaidia si tu kwa mitihani yangu bali hata maishani. Nikaazimia kufanya hiyo extra. Walimu walisema usisome hadi siku ya pepa mi nikasema nitafanya EXTRA. Sitaenda kwenye mtihani wowote bila kufanya EXTRA. Nilifanikiwa kufanya vema mitihani yangu na nilishukuru kwa zile EXTRA nilizofanya kipindi chote cha wakati wa NECTA.

Ni miaka mingi imepita now na nimekuja kugundua kumbe ndoto nyingi hufia mlangoni. Maono mengi hufia karibu na kuzaliwa. Mafanikio ya watu wengi hushindwa kuwafikia kwa sababu tu ya kutofanya kitu EXTRA. Just some little extra stuff. Angalia watu wote waliofanikiwa duniani katika kila eneo. Iwe ni siasa, michezo, dini, biashara nk. Wote kuna kitu kidogo tu EXTRA wanafanya. Kuna wakati nilisikia kuwa Cristiano Ronaldo alikuwa wakimaliza mazoezi kocha akiwaruhusu kuondoka yeye anabaki anaanza kufanya mazoezi kidogo EXTRA. Huenda ikawa penalties au free kicks etc. Kidogo tu. Afu ndo anaondoka. A little EXTRA. Sets him apart.

Angalia wanamuziki waliofanikiwa. Siyo kipaji tu. Vipaji viko lukuki. Lakini nani yuko tayari kufanya that little EXTRA. Akae studio kwa muda extra kidogo. Akienda gym kwa ajili ya mazoezi ya pumzi basi azidishe muda kidogo tu EXTRA. Akifanya mazoezi ya vocals afanye kwa muda kidogo tu EXTRA. Nitajie ni nani na utakuta ni ambaye tayari ni jina kubwa kabisa!

Angalia watu wengi wanaopanda vyeo makazini kihalali. Wamefanya kitu kidogo EXTRA. Huwezi kufanya EXTRA halafu Mungu akakuacha. Never. Uwe mpagani uwe mnini kanuni za mafanikio si za dini ni tabia inayobidi kujengwa.

Angalia wafanya biashara waliofanikiwa lazima utakuta kuna hicho kitu EXTRA katika maisha yao. Anaamka mapema kidogo au kulala late kidogo. Siyo late akiwa anatuma katuni katuni WhatsApp no. Labda anasoma kitu fulani EXTRA. Au anasaidia wengine a little EXTRA. Kuna kitu EXTRA Dewji amefanya, siyo suala la kurithi. Wamerithi wangapi?

Angalia watu wanaokuwa wahubiri wa kimataifa. Utakuta kuna kitu anafanya EXTRA. One more EXTRA foreign language. Maombi kidogo EXTRA. Kufunga kidogo EXTRA. Kusoma NENO kidogo EXTRA. Nk. Hata Mtume Paulo ana nyaraka nyingi kuliko mitume wengine kwa sababu ya hiyo EXTRA.

So swali la kujiuliza kwa wewe unayetaka kufanikiwa maishani ni hili: NI KITU GANI EXTRA UNAFANYA AMBACHO WENGINE HAWAFANYI? Kama huna any little EXTRA basi utakuwa wa kawaida. Just ordinary. Just any Thom, Dick and Harry. Afu kila siku unajiambia  "MUNGU ALINIUMBA KUWA EXTRAORDINARY" Ni kweli kabisa. Lakini Mentor wangu mmoja alisema  tofauti kati ya ORDINARY na EXTRAORDINARY ni hiyo EXTRA tu. Ukiondoa EXTRA katika EXTRAORDINARY unabaki na ORDINARY. Sasa kama unakiri uliumbwa kuwa EXTRAORDINARY halafu huna kitu EXTRA unachofanya daily basi mtajuana na muumba wako ambaye bado amekupa uhai hadi sasa.

Azimia leo kufanya hizo EXTRA ndogo ndogo. You will definitely become EXTRAORDINARY.

Don't forget,

IT TAKES "A LITTLE EXTRA" TO MAKE A DREAM COME TRUE.

Barikiwa sana.

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
#o752366511
Tanzania,
East Africa.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

USIENDELEZE TATIZO KUWA SEHEMU YA SULUHISHO.

Habari za wakati huu..

Watu #wengi mno wamekulia katika maisha duni ya #kimaskini.  Wamezaliwa familia duni, kusomeshwa kwa tabu au kushindwa kwenda shule au kuishia "njiani". Kukosa mavazi, kukosa malazi, kukosa chakula, kifupi kukosa basic needs. Bill Gates anasema kama wewe pia umezaliwa katika familia maskini hilo siyo kosa lako. Ila ukifa maskini hilo ni kosa lako. Unasikia maneno hayo? So shida siyo utokako rafiki. Shida ni uendako. Where are you going?

Shida ni maamuzi yako hapo ulipo. Je, umechukua uamuzi wa kuendeleza mlolongo wa umaskini ama umedhamiria kukata huo mzizi wa umaskini na uanzishe mkondo wa mafanikio kuanzia kwako kwenda kwenye uzao wako ujao mbele yako? That's the issue.

Tatizo haliko kwa wazazi wako diwani wako au mbunge wako au Naibu Spika au Meya wa Manispaa tatizo lipo kwenye fikra zako na maamuzi yako.  Umeamua nini? Kulalamika au kuchukua hatua. Kusoma message kama hizi za kukupa tumaini jipya na mawazo mbadala au kushabikia comments za watu wanaotukanana na kudhalilishana kila siku mitandaoni? Yote hayo ni maamuzi.

Umeamua kujiendeleza kwa kujisomea vitabu vya namna ya kufanikiwa kama kina #Shigongo walivyofanya au umeamua kusoma link za blog za umbea na vitu vinavyoua uwezo wako wa kuwaza vema? Umeamua kusikiliza clip za kina Jim Rohn au Darren Hardy huko YouTube au wewe ni nyimbo za Justin Bieber au za Ali Kiba na Diamond? Yote ni maamuzi.

Umeamua kuandika malengo yako ya mwaka huu na ya miaka mitano ijayo kwenye notebook yako ili uwe na ramani binafsi ya maisha yako au wewe unajiendea tu kulingana na matukio ya kila siku kwenye mitandao. Yaani ukiamka tu hata huna malengo unaanzia Facebook kuona kuna habari gani mpya, kisha uende WhatsApp kujua kuna video gani imetumwa ya kuchekesha. Bila kujua kidogo kidogo umri unaenda kidogo kidogo unaendelea kuulea na kuukomaza umaskini ulioukuta katika familia.

Magroup ya WhatsApp yamegeuka kuwa source ya taarifa kichwani mwako badala ya kupata taarifa kwenye vitabu vya kukusaidia kujikwamua katika maisha na hata kuikwamua familia yako au badala ya kuangalia videos za watu wanaokuonyesha njia ya kupitia wewe unataka video za watu wanaokata viuno tu au clip za bungeni basi. Halafu ukimaliza kupoteza muda wa masaa sita mtandaoni kesho unalaumu serikali kwa kutokukukwamua kiuchumi. Are you serious?? Muda unaoutumia kusoma vitu visivyokuwa na tija na kufatilia mijadala mireefu iliyokupeleka mbele kimafanikio muda huo ungeutumia kujifunza vitu muhimu ungeweza kupiga hatua haraka na kuwa msaada kwa wenzako wengi ambao hawana mwelekeo bado. Lakini kwa kuwa umeshailevya akili yako na vitu visivyokupeleka popote nayo inakukumbusha kila siku kuendelea kuilisha vitu hivyo hivyo.

Uko addicted na vitu vya kuchekesha chekesha tu eti unajifariji kuwa unacheka uongeze siku. Nani alikudanganya siku zinaongezwa kwa kucheka? Unazidi kujaza kichwa chako vitu ambavyo siyo serious wakati tatizo ulilonalo la kuuondoa umaskini ni tatizo serious.  Yaani adui yuko serious kajipanga kukumaliza afu  wewe unamwendea kwa kuchekacheka. Muda unayoyoma na wewe unazidi kuendeleza gurudumu la umaskini ulioukuta nyumbani kwenu.. Kutunza muda wako kwa WIVU ndiyo uamuzi wa kwanza mkubwa unaopaswa kuuchukua ili upige hatua kuelekea mafanikio.

Watu wengi ni #wabobezi wa kupoteza muda.  ðŸ•£ðŸ•£Mungu aliumba 24hours tu kwa kila mtu. Jinsi unavyopoteza muda wako ndivyo unavyopoteza fursa muhimu mno.  Mfano. Kuna wakati utafika hutakuwa na nguvu ulizonazo leo za kufanya kazi nk. Utajutia sana muda wako wa sasa. Usiambatane na mtu anayepoteza muda wake kwani kama wake anaupoteza hataona shida kupoteza wa kwako. Muda unaenda sana rafiki.

Hushangai mtu anafikia kupata mtoto halafu hana pampers.🚼🚼 Yaani utadhani mtoto kashtukiza kuja. Ama utadhani wamekuja wote mzazi na mtoto duniani siku moja. Huoni ajabu? Hiyo ni kwa sababu hakujua kuwa pampers zilitakiwa kuandaliwa zamani.  Wakati alipokuwa anaupoteza muda. Linda muda wako.  Utajitenga na umaskini taratibu taratibu. Umaskini hauna kawaida ya kuwapata watu wanaotumia muda wao vema kwa manufaa. Nzi hufuata uchafu si vinginevyo. Umaskini vile vile hufuata watu wasiojua thamani ya muda. Umaskini ni kama ugonjwa wa kipindupindu. Ili uwe maskini lazima kuna kanuni za mafanikio uzivunje. Kipindupindu pia ni kanuni za afya tu umevunja. Usikubali kuendeleza umaskini kuutoa kwa wazazi na kuwarithisha watoto wako huo ugonjwa.  Hebu chukia. Kama unavyochukia kipindupindu (kama unakichukia that is, maana watu wengine hata hawajielewi kabisa). Umaskini si kitu cha kukumbatia. Ni ugonjwa unaochangia kuharibu misingi mingi ya kiroho, kifamilia na taifa kwa ujumla. Amua kuutimua maishani mwako. Na ndo nasema njia ya kwanza ni kujifunza kutumia muda wako vizuri. Tembelea www.andreamuhozya.blogspot.com kujifunza zaidi.

Njia nyingine ni kujifunza kuangalia fursa mbali mbali zinazokuzunguka. Unajua linapokuja suala la fursa watu wengi wanahitaji kufundishwa jinsi ya kujua kitu fulani ni fursa na kitu fulani ni fursa ya sasa na kingine ni fursa ya miaka ijayo. Si kila mtu anajua. Usipoangalia fursa zilizopo na zijazo utalaumu serikali mpaka siku unakufa. Ili kuuzimisha moto wa umaskini unaotafuna jamii yako na familia yako inabidi ujifunze kutambua na kutumia fursa zilizopo mbele yako na uzifanyie kazi.

Umaskini hauna kawaida ya kuogopa mshahara wako. Utapata mishahara kila mwezi kwa miaka 20 - 40 hadi ustaafu na umaskini utakuwa bado ni sehemu ya maisha yako.  Why? Kwa sababu mshahara ni ujira kidogo tu wa kumwezesha mfanyakazi asije kazini uchi wala asije kwa miguu wala asije kazini akiwa na njaa. Basi.  Mshahara si njia ya kuuondoa umaskini. Ndiyo maana watu wengi walioajiriwa bado ni maskini. Umaskini hauogopi mshahara
. Ni ugonjwa mbaya na mgumu dozi ya mshahara haisaidii.  Ni sawa na kutaka kumaliza malaria sugu kwa panadol. Lazima utafute FURSA za kukusaidia kujikwamua hapo ulipo.  Fursa zipo nyingi mno. Ni lazima ujue pia fursa ipi inafaa katika mazingira yako. Usije ukawa kama mimi kabla sijajua vema mambo haya nilikuwa nauza vitu mahali ambapo hakuna wateja wa vitu vya aina ile. Usicheke.  Sikuwa na maarifa. Now ninayo ndo nakumegea na wewe. So ni hivi:

~ Tumia muda wako kutafuta fursa zilizopo.

~ Tumia muda wako kuzielewa hizo fursa vizuri.

~ Tumia muda wako vizuri kuzitofautisha hizo fursa.

~ Na tumia muda wako kufanyia kazi fursa uliyoamua kuituma kuutokomeza umaskini kutoka kwenye familia yako.

Kwa matumizi hayo ya muda sioni kama utahitaji Bunge liwe LIVE kwanza au sioni kama utakuwa na muda wa kulalamikia serikali kuhusu umaskini wako na familia yako. Ifike mahali ukubali kuwa jukumu la kujikwamua kutoka katika umaskini ni LA KWAKO mwenyewe.  Siku ukijivika hilo jukumu ndo siku utakayokuwa umeanza kuwa mtu mzima kiukweli ukweli. Mtu yeyote ambaye anataka au kutamani kukwamuliwa kutoka umaskini bado hajakuwa vizuri.  Simaanishi kuwa usiombe msaada.  La hasha. Kila mtu huhitaji msaada. ILA kuna watu wanataka mtu mwingine aje awasaidie kuishi maisha yao hapa duniani afu wajikute wamefanikiwa.  That's never going to happen. Wake up! Tumia muda tafuta fursa.  Ziko nyingi. Nenda semina mbali mbali ujifunze.

Kama unawaza kujikwamua kimaisha ila hujui wapi uanzie au unatatanishwa na fursa unazoziona au una hofu ya kujaribu basi wasiliana nasi kwa WhatsApp #o788366511 #o752366511 tushauriane.  Usikubali kurithi umaskini na kuwarithisha watoto wako.


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumapili, 23 Oktoba 2016

AKILI YAKO ISIPOKAA SAWA MAFANIKIO HUTAYAONA


Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikichunguza maisha ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa. Lengo langu hasa ni kufikia mafanikio makubwa na kuwasaidia wengine wanaotaka kufanikiwa pia.

Nimejifunza vitu vingi kutoka kwa watu waliofanikiwa ambao niliweza kuonana nao ana kwa ana. Na hata wale ambao bado sijaweza kupata fursa ya kuwaona nimekwisha jifunza tayari mambo muhimu kutoka kwao.

Leo nataka niongee kitu ambacho watu wengi wanaotaka kufanikiwa hawajakijua bado. Na hivyo wanakwama kupiga hatua kimafanikio na mwisho wanajikuta wanakata tamaa ya kutafuta mafanikio tena.

Hiki kitu kinaitwa MINDSET. Yaani MTAZAMO. Yani ni kweli sikatai kabisa kuwa kufanikiwa kunahitaji vitu kadhaa muhimu. Najua na wewe unavijua na hata nikisema tuvitaje kwa pamoja unajua.
Vitu kama:

~ kufanya kazi kwa bidii sana (kujituma),
~ kuishi kwa kuweka malengo,
~ kuwa na hamasa yani kitu kinachokuhamasisha  au kukusukuma kufanya kazi malengo yako (motivation),
~ pia kuwa na coach, na mentor na role model wako ni muhimu sana kwa ajili ya inspiration
~ na vitu vya aina hiyo

Lakini nimekuja kufahamu kuwa kuna jambo la msingi sana ambalo ndo nataka nikushirikishe hapa ambalo usipolijua utahangaika sana kufikia mafanikio. Jambo hilo ni kwamba ili vitu vyote tulivyotaja hapo juu ili vizae matunda sahihi na kukuletea mafanikio inabidi uwe na kitu kimoja kwanza: AKILI ILIYOKAA SAWA au unaweza kuita MTAZAMO SAHIHI (THE RIGHT MINDSET)

Mazingira ambayo tumezaliwa na kutokea au kukulia yana nafasi kubwa sana ya kutujenga kimtazamo. Yani MTAZAMO wako kuhusu mafanikio jinsi ulivyo unachangiwa sana na mahali ulipokulia, watu waliokulea (wazazi, shule, kabisa/msikiti etc) toka ukiwa mdogo. Pia jamii iliyokuwa inakuzunguka ukiwa mdogo.
Halafu na watu wanaokuzunguka sasa.
Hao woote wanachangia sana kukufanya kujenga MTAZAMO ulionao kuhusu maisha na kuhusu mafanikio.

Kuna watu kutokana na mazingira niliyoyaeleza hapo juu wamejenga mtazamo kuwa hawawezi kufanikiwa kimaisha mpaka uwe mjini au uwe na degree au utoke familia bora au uende Ulaya au Marekani hata akizama baharini.
Hata kama ni kwenda kuosha vyombo. Yani bora akaoshe vyombo Dubai kuliko kuuza mitumba au kuanzisha mradi mdogo Tanzania. Wengine wameshajiona kama wanyama vichwani mwao bila kujua. Mwingine anajiona mbwa. Yani wewe unaongea naye unamwona ni binadamu kumbe mwenzio MTAZAMO wake anajiona kama mbwa. Hujawahi sikia mtu anasema "bora ningezaliwa MBWA Marekani?" Huyo mtazamo wake ni kuwa mbwa walioko Marekani wana mafanikio kuliko yeye. Kama na wewe huo ni mtazamo wako unapaswa kutubu mbele za Mungu haraka mno yani usijisumbue kutafuta mafanikio wakati ushamfanya Mungu ni mjinga kwa kukuumba binadamu. Tubu kwanza. Unaweza ukawa na bidii na ndoto kubwa na malengo lakini mtazamo wa kwamba mpaka uende Marekani ndo ufanikiwe siyo mtazamo sahihi kukufikisha katika mafanikio.

Kuna ambao mtazamo wao ni kuwa akioa binti aliyesoma au kama ni binti ana mtazamo akiolewa na mtu mwenye uwezo mzuri kifedha hapo yeye pia atafanikiwa. Hawa wa hivi hata umfundishe biashara vipi. Hata umhamasishe vipi kuwa anaweza bado yeye ànawaza kupata mjamaa mwenye nazo. Na hawa baadhi yao wanajikuta wanachezewa tu na kushushwa thamani wakidhani wamepata mtu sahihi kumbe wamekosea mno sababu ya kuwa na mtazamo huo. Anaweza akawa na bidii ya kazi lakini mtazamo huo siyo mtazamo sahihi ili ufikie mafanikio.

Kuna wenye mtazamo kuwa kwa kuwa UKAWA haikuchukua dola hawawezi kufanikiwa. Na kuna wanaodhani kwa kuwa CCM imekamata dola ndo watafanikiwa. Sikia kufanikiwa ni suala binafsi. Kuna watu wamefanikiwa Tanzania na kuna watu Marekani ni hohe hahe. Kuna watu wanaipenda UKAWA/CCM ambao hata siyo wanasiasa kabisa wamefanikiwa na kuna wanaoiopenda UKAWA/CCM ambao ni hohehahe. Tofauti siyo chama kipi anapenda. Tofauti ni kichwani kwako kuna mtazamo UPI kuhusu mafanikio. Hufanikiwi kwa sababu ya chama unachoshabikiaunachoshabikia

Kuna watu wana mtazamo kuwa ili ufanikiwe labda uwe na sapoti ya watu wa karibu. Utasikia mtu anasema "Sisi wabongo hatupendani ndo maana hatufanikiwi" kashajenga hiyo. Kuwa hawezi kufanikiwa kwa kuwa hawapendani. Au "yani mi nina ndugu wana uwezo ila hata kukupa sapoti yani utadhani hawanijui". Anadhani ndugu wakimpa sapoti ndo atafanikiwa. Ni kweli wote waliofanikiwa wanapendwa, au walipewa sapoti na ndugu? Ukijua story za waliofanikiwa utashangaa mno. Huo siyo mtazamo sahihi.

Wengine wanafikiri kufanikiwa ni bahati. Hawa ndo wanawaza kuvaa pete za bahati. Au kuangalia nyota zinasemaje kwenye gazeti. Kuna watu wamesoma nyota toka darasa la saba mpaka sasa wana miaka 40 maisha yameshaanza rasmi na bado mafanikio hayasomeki. Huo siyo mtazamo sahihi. Watu hawafanikiwi kwa sababu birthday yako mvua imenyesha na jua likawaka. Huo ni ushirikina. Na hata ukifanikiwa mafanikio yako yatakutesa mpaka either uyakatae ufe maskini au uteseke na kuishi na majoka ndani ya nyumba sijui kulala na majini makaburini sijui kuua wazazi au watoto na kuishi kwa moyo ulio na majuto mno na uchungu usiosemeka maisha yako yote hata kama kwa nje unatoa tabasamu na kuwaambia vijana wasikate tamaa watatoka kumbe wewe una joka chumbani.
Huo siyo mtazamo sahihi.

Kuna mitazamo mingi mno ambayo si sahihi. Na nimeanza kusaidia kutoa elimu kidogo kidogo kwa vijana wenzangu kupitia kwenye blog yangu www.andreamuhozya.blogspot.com kuhusu mambo mbali mbali lakini pia kwa njia ya WhatsApp.

Kama wewe pia unataka kufanikiwa na umefanya vitu mbali mbali kwa bidii lakini bado hujaona mwelekeo njoo tuongee kuhusu mambo ya mtazamo. Ni muhimu kuliko unavyoweza kufikiria. Usije ukapoteza muda mwingi mno kufanya kitu ambacho ungeweza kuwa umeshafanikiwa ila kuna mahali una mindset isiyo sahihi. Au usijepoteza muda kufanya kitu kisicho na faida bila kujua kwa sababu ya kufata mkumbo tu. Afu mwisho unajikuta mtu mzima na majukumu makubwa mengi hela huna unaanza kupata pressure miaka 40 tu. Njoo tushauriane mambo muhimu.

Usiijaze mind yako na picha chafu za kwenye mitandao na vitu vya kuchekeshachekesha tu huko WhatsApp. Mafanikio yanahitaji akili iliyo SAFI. Lazima uwe na the RIGHT MIND. Ilishe akili yako vitu muhimu vya kuifanya itafakari siyo ilale tu na kukaa bila kukua. Mfano makundi mengi ya WhatsApp yamekuwa na vitu vya kitoto kitoto tu. Na watu ndo wanafurahi. Picha za ajabu ajabu na habari za umbea na entertainment tu haziifanyi akili yako ndo ikue. Unahitaji vitu tofauti. Unahitaji MTAZAMO mpya. Kama kweli upo serious na mafanikio yako. Muda haukusubiri. October inayoyoma. Mwaka unaisha.. Umefanikiwa malengo mangapi so far? Be yourself. Kuwa wewe. Angalia maisha yako!

Karibu tuzungumze WhatsApp #o788-366511 au #o752366511


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumamosi, 22 Oktoba 2016

WHAT KIND OF YOUNG PERSON ARE YOU?

WHAT KIND OF YOUNG PERSON ARE YOU?

There are things that are so easy to do in life and anybody can do these things. Especially young people.

It's easy to TALK
Yes it's easy to talk, talk, talk, talk and keep talking after keeping talking. Most young people are now involved in talking. Just talking. Talking about what they want in life. Talking about how they want it. Why they want it. When they want it. But that's all they do. TALK. They don't do anything about it.

It's easy to PROCRASTINATE.
I call procrastination the food of a lazy mind. It's most people mind's *default mode.*
And so most people do so, especially young people. (Especially here in Africa more than elsewhere.) Well, young people the world over generally somehow  think they still have all the time in the world to go about it LATER. They put it all off. It's not a convenient time, they think. They are looking for that perfect, perfect time. When they're grown up. The perfect, perfect moment to do it. When they have the money or a college degree. Now they're still having a little fun to lighten up their youthful selves a little, so they think. Their philosophy about life is founded on a lie that they not only believe but also protect: Have Fun While You're Still Young. Okay little brother, alright lil sister. Have fun. But remember TIME flies while you're having fun. So that's the generation of young people we have. Putting off everything. Or here in Africa they're waiting for a share of that AID MONEY promised by the government when it gets AID MONEY promised by the *donor!* If you're one of these wake up from that slumber! Learn from those who've woken up and done something.


It's easy to JUDGE.
So most people do that. Young people also do so. When they see someone successful their verdict is: inherited. Or: stolen. Or: swindled. Or: luck. And so on and so forth. They still want to be successful, yet most of them have no idea how to go about it.

It's easy to WATCH.
U-huh! Yes it is. And so most people do so. Young people love this the most. Yes they love watching TV series or watch their favourite athletes in action because it's easy to watch. Yes, it's easier to watch than to put in the work and sweat and discipline yourself until you become someone's favourite actor or athlete!
They love to put their headphones on and shut the whole world out and listen to their favourite songs and feel so good. Yes that's easier than putting in the work to nourish your talent and find a role model and get yourself a mentor and a coach who will subject you to a disciplined routine to ensure that you one day get paid for doing what you love doing. Look at how many people you'll find on a football pitch on early Monday morning drenched in sweat. Then look how many you'll find on Sunday afternoon - especially on a derby!

It's easy to do SMALL TALK.
So most people do so. And young people love it.
Talking nonsense and filling their minds with irrelevant and unhelpful things that intoxicate their minds and unknowingly impair their ability to have a sound judgement. Avoiding all serious subjects and deep, thought-provoking conversations. And then they expect to live a life that has a meaningful impact and to leave a meaningful legacy when they're gone.
To change this world!


We live in a world where the generation of young people we do have has lost its sense of purpose. Young people who don't know why on earth they're here for? A typical youngster of today thinks success is having a beautiful profile picture of Facebook and a 100k followers on Instagram or going out with the opposite number often. A typical youngster of today has half of their brain filled with filth, irrelevant information and negativity and thinks that you can actually MICROWAVE success!

So which young person are you?

Are you one that has spent this almost gone year just #talking and #procrastinating and #judging and #watching and indulding is #petty talk and #wishful thinking, or are you a young person that has spent this year taking steps to live with distinction and to make both your presence and your contribution felt and appreciated?

Will your family, or community or nation or continent or world at large ever get to benefit from the gifts and talents that God Almighty invested in you? Or did He create you to come here and just have all the fun you could have and then die, never having lived at all? Yes, never having lived at all, for I consider life as a service to others, and success as serving other people to the fullest and to the best of your ability - what the late Caribbean Pastor used to call DYING EMPTY!

What kind of young person are you? One that has spent 2016 striving to become well informed and knowledgeable of the things that you need to know in order to make a worthwhile contribution? Or one that has spent almost an entire year now going from music concert to another, downloading all the music songs you could download and watching them things: bad things, dirty things, and  thinking about #BAE 24/7? And yet having the audacity to say you want a good life? Who's going to give you that? You want to become successful? Good. But don't you know that what you've been doing is detrimental and amounts to sabotaging your own cause?

How many books have you read so far this year?
Books that added something to your knowledge bank account.
Or will you enter 2017 with the knowledge you acquired 5 years ago and expect to live to make a difference?  Coz I'm not talking about just existing! I'm talking about LIVING! And leaving a legacy. I'm talking about you becoming a leader and not a follower. Haven't you heard that "LEADERS ARE READERS"?

Listen to me, I once heard a story of one of the richest people of our time. He once visited this country's beautiful national parks and game reserves and spent all of his time there reading books and barely watching any of the elephants, gazelles, lions or flamingos! That man is Bill Gates!
"Why would he do that" you might ask. I will tell you why! It's because he knows the VALUE of spending time getting informed. Adding onto one's knowledge bank account. Lemme tell you something: Reading is one of the strongest and most valuable currencies in the KNOWLEDGE ECONOMY. You can quote me!
Will you emulate him?
Or would you rather die than read! Or write!
Don't you know your ideas can change our world?


What kind of young person are you? One that is the problem with this continent of Africa or one that's the solution to the many problems and challenges we do have including education, poverty, health related challenges and others? Are you one to ask other people to give you a job or one to give other people the job they need? What kind are you? I'm talking to you! Are you one to make your brothers and sisters step up and do something to change our continent or are you one who thinks that Africa's challenges will be resolved by some #muzungu with a briefcase of AID MONEY!  Surviving on life support!

What are you doing to mend the broken lives and alleviate the challenges due to poverty and backwardness of the people in your own nation?
Or are you still having a little more fun first? What difference has such entertainment and fun done into your life so far? And into the lives of those around you?
Are you hearing me?

What kind of young person are you?
One that Africa will be proud to have ever had or one that Africa's history won't consider to have ever walked this continent? Listen to me my friend. Your nation, your people, our people our continent is looking and yearning for serious young people. For young men and women that will be the envy of the world!
The problem with somevof you young people is you think you are a happenstance! You think you're an accident! Don't you know that you have a purpose? Haven't you heard that even while you were still in your mother's womb the creator knew you and had set you apart for a purpose? Find that purpose! It isn't about how or where or when you were born. It only matters that you were born.

So better get serious already, or our history will forget all about you like that ant you stepped on the first day you went to school so many years ago? Remember that #ant? Of course YOU DON'T. And that's how you'll be forgotten, if you don't take your life as seriously as you should.

What kind of young person are you?
And what kind should you have been?
What kind must you be to steer your nation and our continent to a better future. To our own African dream of progress, unity and excellence!
What's your contribution going to be?


Step up my brother! You're not here to get a degree on Six Packs Acquisition. Do something!
Step up my sister! You're not here to look sexy and flash a well-curved figure to lustful eyes and get LIKED but to contribute something to better our situation. Be one of those sisters of ours who've done that!
Step up and do your part.
Do everything you can do.
A noble human soul once said: ALL YOU CAN DO IS ALL YOU CAN DO, BUT ALL YOU CAN DO IS ENOUGH.
That man was Art Williams.
Don't you underestimate the power of All You Can Do!

So, are you going to do something?
Or are you going to just talk about doing something?
What kind of young person are you?

I dare you today!
I dare you to get yourself on active mode!
ACTIVATE THE CODES! Are you hearing what I'm telling you?
Put in the work!
Sweat if you will!
Give it your all!
Bring in the PASSION!
It's a noble thing you're doing.
And the sons and daughters of Africa will be proud you made a difference!
Coz that's the kind of young person you ought to be!
One whose life will make a difference!
Don't die with that greatness in you.
Don't deny us a chance to benefit from your contribution!
Step up and make a difference! Hold the pen and rewrite Africa's history with your name in it!
I promise you your story will be told to future generations and your name will live in their hearts forevermore.

Step up and make it happen!



Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa!

+255788366511(WhatsApp only)
www.andreamuhozya.blogspot.com

Ijumaa, 21 Oktoba 2016

JAMBO LA KUMI NA LA MWISHO (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA KUMI NA LA MWISHO
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 10 na ya mwisho.

10. JAMBO LA 10: WAAJIRIWA WENGI HUISHIA KUWA WAOGA (MOST EMPLOYEES END UP BEING COWARDS)


SO WE ARRIVE.... Siku kumi za kujifunza pamoja.

Leo tutajifunza jambo la mwisho

Zamani nilikuwa nikijiuliza kwa nini wale watu ambao walikuwa na USHAWISHI (influence) sana shuleni ama vyuoni kwa nini wakiajiriwa ni vigumu sana kuwasikia tena. Mtu ambaye alikuwa akiitisha mgomo vijana wenzake Chuo kizima au shule nzima watu wanagoma mpaka wakati mwingine wanasababisha taifa zima kujadili hilo suala lakini akiingia kwenye ajira si rahisi kumsikia tena.
Wala kukuta akipewa cheo kikubwa labda.

Nikaja kugundua kuwa setup ya mfumo wa ajira ilivyo japokuwa inafanana na mfumo wa shule kwa maana ya ratiba lakini kuna tofauti kubwa ya PRINCIPAL au HEADMASTER na mtu anayeitwa BOSS aisee. Yani Principal wa chuo anaweza kuwa hata na elimu ndefu na umaarufu mkubwa nchi nzima lakini haogopwi kama mtu anayeitwa BOSS hata kama boss mwenyewe hata shule hakwenda ila ndo boss. Hapana chezea AJIRA.


Ni watu wachache sana... EXTREMELY FEW PEOPLE... ambao wako katika ajira na wana ujasiri katika mambo wanayoyaamini. Wengi wanapoajiriwa wanajifunza kuwa waoga. Bosi akiingia ofisini wengine hata mazungumzo yanakatayanakata
. Au mwajiriwa akiitwa ofisini kwa bosi yani automatically anajiset kuappear "vizuri" wakati alikuwa tu okay. Wengi hiyo inakuwa si kwa sababu eti heshima bali WOGA tu. Yani bosi akiingia ofisini ni shida...

~ wengine wanaweza kutetemeka hata kama kwa nje kajikaza. Anavibrate ndani kwa ndani. We jiulize kama wewe ni Mwalimu hivi Mama Ndalichako akitinga hapo shuleni bila taarifa hali itakuwaje. Woga. Kwani mmeua MTU nyie?

~ wengine hata anaweza kushindwa kuongea vizuri. Angalia Waziri akitembelea mahali hasa kwa idara zilizo chini yake.

~ wengine anaweza kutamani atoke katika mazingira hayo.

Confidence inaanza kuondoka taratibu.
Mwishowe wanahitimu katika UOGA.
Wanakuwa waoga wa vitu vingi.

~ Waoga wa kuomba kuongezewa maslahi.
~ Waoga wa kuondoka kazini kutafuta maslahi kwingine hata kama ni ajira nyingine
~ Waoga kabisa wa kujaribu kutafuta maisha katika mifumo mingine ya fedha nje ya mfumo wa ajira kama ujasiriamali au biashara. Yani aneshakuwa ADDICTED to kuishi kwa mfumo wa ajira tu.
~ Waoga wa kutoharibu kazi kwa sababu ya kuogopa itakuwaje akiambiwa kazi imeisha.


Mtu huyu anaanza kupoteza vitu muhimu:

1. Kwanza anapoteza UJASIRI.. Self confidence and hata self esteem.

2. Pili anapoteza HONESTY....hawezi kusema ukweli hadharani. Ila bosi akiondoka ndo unamsikia eti.."To be honest....." Hahaaaa

3. Mwisho anapoteza INDEPENDENCE OF THINKING.
Yaani hata angekuwa na mawazo au opinion tofauti vipi atasikilizia kwanza wenzake wanawazaje. Wanatakaje. Anaanza kuwa victim wa GROUP THINKING. Anasahau Mungu alituumba individually. Anasahau kuwa kuna vitu vya kukubaliana na wengine lakini when it comes to matters of PRINCIPLES zako unatakiwa usimame imara unshakable ukisimamia principles zako. Bosi akisema unaobey.


Kama wewe ni mwajiriwa jiulize hujawahi kucompromise principles zako kwa sababu ya kulinda "KIBARUA" chako? Kwamba unaamini hiki si sahihi hata aje nani na ukasimama imara kulinda msimamo wako! Come what may! Je ndivyo ulivyo katika ajira yako? Kwamba you can tell your boss to their face kuwa jambo fulani si sahihi hata kama itakuwaje ilimradi si sahihi?
Thubutu!

Ndo hii sasa kwamba kwa sababu kuna BOSS. MASTER. Hapo unajikuta unaCOMPROMISE kwa sababu mfumo huo umempa control yeye ya kudetermine mambo mengi juu yako. Unaogopa KUHARIBU kazi. Unaanza kujiuliza:

~ Watoto watakula nini?
~ Kodi ntalipaje?
~ Mkopo ntaumaliziaje?

Is that the mind of a free person?

Na wenzako "wanaokutakia mema" wanakuita kando wanakwambia "Aah, we huyu bosi mwache kama alivyo. We unadhani sisi hatuoni kuwa anakosea? We potezea tu atajiona mjinga"
Unapotezea.
Una compromise.

Hatimaye unakuwa miongoni mwao. Unakuwa muoga kabisa. Hata kama ulikuwa wewe ndo unaendesha migomo vyuoni.
End of your story.
Coz MAFAHALI WAWILI HAWAFANYI NINI.....?


And so..ndo hivyo...

Na kwa kuwa mada yangu katika hizi makala ilikuwa ni kuhusu uhuru wa kipato...then sababu hii ya mwajiriwa husika kuwa mwoga, na kuishi kwa hofu inamnyima uwezo wa kufikia FINANCIAL FREEDOM. Why? Kwa sababu uhuru wowote ule huwa mtu hapewi, huwa anautafuta na kuupata. Hata uhuru wa kisiasa w kifikra na hata huu wa kipato. No one will give it to you. Unapaswa kujifunza UKWELI kuhusu mfumo ambao wewe upo. Je mfumo uliopo wewe kuna mtu yeyote ambaye unaweza kuwa na access naye ambaye ametumia huo mfumo wa ajira akafikia uhuru wa kipato? Kwamba hahitaji tena kwenda kazini ili kuingiza pesa labda aende tu sababu working is a mark of NOBILITY? Je yupo unayemjua ambaye alimake FORTUNE kupitia ajira ili walau ukajifunze kwake? Jipe jibu.
Na kama yupo je wewe na yeye mpo katika footing sawa? Tafuta kujua ukweli.


TRUTH shall set you FREE.


And so I rest my case, for now. Nimezungumza mawazo yangu kwa siku 10 sasa. Naamini nimetimiza wajibu wa kutoishi na mawazo muhimu bila kuwashirikisha wengine ambao huenda yanaweza kuwasaidia.

Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoelezea kuanzia ile ya kwanza hadi hii mwisho zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA linapokuja suala la kufikia uhuru wa kipato. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Na mpaka hapo nimefikia mwisho wa mfululizo wa makala hizi.

Asante sana kwa kuwa nami tangu mwanzo mpaka leo.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!


Semper Fi great people,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

JAMBO LA TISA (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA TISA
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 9.

9. JAMBO LA TISA: KUPOTEZA UHURU WA MAMBO MENGI (LOSS OF FREEDOM)

Wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikipenda sana maisha ya shuleni. Nilipenda sana kuanza  shule mpaka wakalazimika kunipeleka kabla ya wakati lakini shuleni nikarudishwa kwamba mkono sijui ukipita kichwani sijui hauvuki bega. Anyway. Nilianza mwaka uliofuata. Nilipenda vitu vingi. Nilipenda mazingira ya shule, nilipenda sare zangu za shule hasa zile za mara ya kwanza. Aisee! Nilipenda kuhesabu namba (hii nafikiri niliipenda kwa lazima hahaaa maana kulikuwa na stiki za hatari ukichelewa kengele), nilipenda kukimbia mchaka-mchaka na nyimbo zake za Makaburu na za Mandela na nyingine nyingi hasa ule wa "JUA LILE LITELEMKE MAMA!!!". Aisee. Nilipenda gwaride hadi nikawa kiongozi wa gwaride wa shule za msingi kata nzima. Mahaba ya dhati kumoyo. Nilipenda mazingira ya shule. Ramani za Tanzania, Africa, nk za mawe yaliyopakwa chokaa, nilipenda bustani na miti na viwanja vya shule. Nilipenda masomo hasa Kiingereza. Kwa ujumla nilipenda KWENDA shule.

Lakini nyakati za likizo nilizipenda zaidi na kutembelea ndugu, kucheza na rafiki zangu, kwenda kuwinda na kuvua samaki, kwenda kufanya mazoezi ya mambo ya kanisani, kwenda kuangalia mashindano ya mpira kwa watu wazima au jamaa wa Kisukuma wakicheza ngoma zao katika sherehe mbali mbali nk. Nyakati za likizo nilizipenda kwa kweli.

Na baadaye nikapemda kwenda sekondari. Nikaenda. Nikaishi maisha karibia sawa na yale ya shule ya msingi. In terms of ratiba na kanuni na taratibu nyingi. Na nyakati za likizo pia nilipata fursa ya kuishi hasa maisha binafsi yasiyo na kanuni zilizonifunga.

Taratibu taratibu nikaanza kuona kuna kitu fulani moyoni mwangu ambacho kimeanza kupungua kuhusu maisha ya shule. Mfano nikaanza kuona kama maisha ya shule yananiprogram kuanzia mbali ili ifike hatua nione hiyo ndiyo kawaida. Nikaanza kuwaza kuwa hivi siku moja nitaweza kuishi mwaka mzima nikivaa mavazi ninayoyapenda mimi asubuhi hadi jioni January hadi December, na nikienda kula muda ninaosikia hamu ya kula, nikienda kulala muda ninaojisikia kulala iwe SAA moja jioni au saa nane usiku. Niongee na watu kwa lugha ninayopenda na siyo lazima niSPIKI INGILISH! Niweze kwenda kokote ninakotaka kwenda wakati wowote kama nina sababu maalumu  bila kuambiwa NIMETOROKA na mtu yeyote wala bila kusubiri idhini ya mtu mwingine. Na nikaona kama kuanzia shule ya msingi nilitengenezwa kuipenda shule siyo kama mimi ndo niliipenda mwenyewe from nowhere. Wanafunzi walionekana bora kuliko watoto waliokuwa wapo tu nyumbani wanalialia na kuongea kikerewe tu mchana hadi usiku na kukaa bila kujua hata kusema neno "SHIKAMOO". Niko sekondari, Seminari, nikaanza kutamani ije siku ambayo nitaendelea na mosomo yangu pasipo kuvaa kitu kinachoitwa sare. Ndiyo ikawa sababu kubwa ya mimi kutaka kusoma Chuo Kikuu badala ya kuendelea na masomo ya Seminari. Sasa sijui ndo wanasema wito uliisha. Hahaaa. But naongelea kilichotokea.  Kilichotokea ni kwamba nyakati za likizo nilijihisi huru zaidi kufanya mambo yangu nilizipenda kuliko nyakati za shule ambazo zilikuwa na program ya kufuata kuanzia unapoamka hadi unaporejea kulala. Sisemi system hizo hazina faida. Zina faida nyingi mno. Ila kwa sababu ya series za Makala zangu hizi najaribu kukufanya kuona shida mojawapo ya mindset and mind control iliyotengenezwa na watu waliotengeneza mfumo wa aina ile wa elimu.

Mfumo ule (the Formal Education System) tumeurithi kwa wakoloni ambao waliuanzisha kwa ajili ya kupata watu wa kuwasaidia kazi zao za kiutawala na kazi zinginezo (white collar and a few blue collar jobs). Ni mfumo ambao waliopitishwa huko waliandaliwa kwa kusudi maalumu. Sisi tukaja kuurithi kama ulivyo na makusudi yake kama yalivyo. Na asilimia kubwa ya waajiriwa wamepita katika mfumo huo kwa namna moja ama nyingine.

Na ndiyo maana maisha ya mwajiriwa ni kama maisha ya mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari. Picha hii hapa chini nikikuuliza uniambie ikiwa ni ya WAAJIRIWA ama WANAFUNZI utasema ni kina nani?


I. Mwanafunzi anaishi kwa kengele mwajiriwa anaishi kwa kengele pia bila tu ameipa jina zurizuri. Anaiita ALARM CLOCK.


II. Mwanafunzi ana muda specific wa kwenda na kutoka shuleni. Mwajiriwa pia ana muda specific wa kwenda kazini. Hawezi kwenda  au kutoka muda wowote anaotaka yeye.


III. Mwanafunzi ana kazi specific za kufanya. Zinajulikana kabisa na zimeandikwa. Walimu wanajua maana ya SCHEME OF WORK na LESSON PLAN. Mwajiriwa pia ana kazi specific za kufanya zinajulikana na zimeandikwa kabisa. Waajiri na waajiriwa wanajua kitu kinachoitwa JOB DESCRIPTION


III. Mwanafunzi ana mavazi maalumu aendapo shule. Of course kuna shule zina safe. Na zingine hazina sare lakini zina dress code fulani. Na kuna sare za siku ya michezo. Mwajiriwa pia ana mavazi maalumu aendapo kazini. Na hivyo hivyo kuna ajira zina sare na kuna makampuni yana sare unapewa mpaka sare za kuvaa siku ya michezo. Hakuna shida katika hili is that what you're saying? Well, sawa. Inawezekana hakuna shida. Inawezekana nakompliketi maisha tu bila sababu za msingi, au siyo?


IV. Mwanafunzi ana muda maalumu aliopimiwa wa kula. Mwajiriwa pia ana muda uliopimwa wa kula. Hawezi kuamua kula masaa mawili eti alikuwa na mazungumzo na rafiki yake. Watazungumza WhatsApp. Kazi kwanza.


V. Mwanafunzi ana madaraja ya vyeo. Kuna mtu wa komonitor wengine. Class Monitor. Head Prefect. Nk. Hawa ndo CCTV za walimu. Mwajiriwa pia anayo hii. Kuna vyeo. Kuna officer, Manager, Excom, nk. CCTV ya MWAJIRI. Huwezi kuishi wala kuzalisha bila kuwa monitored.


VI. Kuna shule ukiongea kilugha unapewa pembe. Kiswahili ndo habari ya shuleni. Na ukienda sekondari Kiinglish ni lazima. Hata kama hukijui utafundishwa mpaka angalau ujue cha kumjibu mwalimu tu. Waajiriwa pia linapokuja suala la lugha kuna lugha maalumu ya kumhudumia mtu. Ukienda ofisi kadhaa unakuta maneno kwenye vibao tu yanaonyesha lugha gani hapa inaweza kutumika. Kikerewe acha kwenu. Kwanza kinamsaidia nani nchi hii. Hata kama mteja ni mkerewe.
Kuna waajiriwa wamekaririshwa mpaka jinsi ya kuongea na mteja physically kwenye simu. Ulishawahi kupiga simu ile namba 100!? Unasikia wanavyoongea. Piga tena baadaye wanaongea vile vile.
Ulishaenda airport au Railway stesheni usikie wale wanaotangaza matangazo. Ni monotone. Utasikia kale kamlio.. Tii-ntiiii... Afu unasikia sauti nzuriii... "Attention all passengers, the passenger train to Mwanza via Morogoro Dodoma and Shinyanga is on lane number one and will leave in 5 minutes time....! Njoo kesho utasikia hivyo hivyo. Utafikiri ni kitu kimerekodiwa.


Unaambiwa ni kuimprove quality ya service. Hivi ukimpigia Dewji simu na yeye anapokeaga hivyo kwani? Kwa hiyo yeye hana quality nzuri ya huduma kwa kuwa hajapokea kama wale wa namba 100?

Listen my friend. Life is a mind-control game. And employees play in that field very well. Wazungu walituletea dini hawakutuletea mindset education. Ili tubaki na dini tu bila matunda thabiti. Mind is better than religion. Coz Mungu alileta wokovu hakuleta dini. Wazungu walileta formal education wakatunyima SELF EDUCATION. Hii unapaswa kuitafuta mwenyewe. Na hii ndo itakukomboa kifikra.

Sasa kwa mifano niliyoitoa hapo juu hivi kama huna uhuru wa vitu vidogo kama:

~ muda wa kwenda na kutoka katika shughuli yako ya kiuchumi
~ mahali pa kuifanya hiyo shughuli everyday lazima uende hapo huwezi kuamua ukafanyie restaurant au beach hata kama unataka

~ muda wa hata kitu kidogo kama kula
~ mavazi gani uvae.
~ nini ufanye leo katika majukumu yako. Ushapangiwa cha kufanya
~ wakati gani usafiri kwenda utakako kwa sababu zako ni mpaka uruhusiwe
~ kupumzika kwa muda utakao hata kama ni masaa mawili ukakae hapo nje ya ofisini ukiwaza mpango fulani muhimu. Au ukipokea simu moja muhimu sana

Kama huna freedom na vitu vidogo kama hivyo. Unawezaje kupata FINANCIAL FREEDOM katika hiyo setup?
Kumbuka nilishasema kwenye makala zilizotangukia kuwa hata kipato chako hupangi wewe. Nk..

Nikukumbushe tu kwamba AJIRA ni mfumo ambao bado upo upo tu sana huku kwetu. Swali ni je mfumo huu upo kwa ajili YAKO wewe pia uajiriwe?

If YES, then good luck.
If NO, then DO take proper action.

Mi nimemaliza. Na kwa leo naishia hapa.

Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoelezea kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 9 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA linapokuja suala la kufikia uhuru wa kipato. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado 1 tu.
Endelea kuwa na mimi kidogo tu.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 9 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 10 na ya mwisho kwa mfululizo wa makala zangu hizi.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis,

Yes,

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa

Jumatano, 19 Oktoba 2016

JAMBO LA NANE (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA NANE
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 8.

8. JAMBO LA NANE: MAISHA YAKO YA KIJAMII UMETENGENEZEWA (YOU HAVE A SORT OF AN INBRED SOCIAL LIFE)

Leo nataka nianze kwa kusema kitu fulani.

Kuna siku nilisoma Biblia ikawa inaongelea habari za watu wanaitwa MATOASHI. Mathayo 19:12 pale. Rabbi (mwalimu) mmoja wa Kiyahudi aitwaye Yesu, ajulikanaye pia kama Kristo, akieleza hilo jambo pale. Kwamba duniani kuna #matoashi. Akafafanua kuwa kuna matoashi wa aina tatu:
i.) kuna wa KUZALIWA hivyo,
ii.) kuna matoashi WALIOFANYWA kuwa matoashi na watu wengine
na kuna matoashi WALIOAMUA kuwa matoashi kwa ajili ya Mungu.

Nikapata idea moja kuwa kuna mambo mengine yanakuwa yalivyo katika maisha yetu kwa sababu za our PAST. Historia. Asili yetu nk. Kuna ambayo yanakuwa kwa sababu ya watu wenye control na maisha yetu. Na kuna mambo yanakuwa yalivyo katika maisha yetu kwa sababu ya maamuzi yetu binafsi.

Kwa premise hiyo basi kuna watu wanaajiriwa kwa sababu ndiyo kitu kilicho asili yake. Ndiyo MINDSET yake ilivyojengwa toka utoto ikiwezekana toka akiwa tumbni kwa mama alikuwa akinenewa ajira akipiga teke mama anasema huyu atakuwa polisi huyu au wengine huyu atakuwa mwalimu atufundishie Jamii au huyu atakuwa hiki na kile. Katika formative years zake akiwa mtoto anaona maisha kwa jicho la ajira. Wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, wengi wao au wote wakiwa wameajiriwa kwa namna fulani. Alipoenda shuleni walimu wanaongelea kusoma ili kupata kazi nzuri. Zingine wanamchagulia. Wewe utafaa kuwa meneja wa benki. Wewe mchafu mchafu utakuwa fundi "makenika". Akirudi likizo watu hata majirani wanamwambia "Soma mwanangu, someni mpate kazi mtusaidie sisi wazee wenu hatukusoma" wanampa mifano ya vijana ambao hawakusoma na wapo wapo tu hawana ajira jinsi walivyo hawana mwelekeo. Na wanamwambia kuhusu unaona mtoto wa fulani amesoma amewajengea wazazi wake nyumba nzuri. Soma usichezee elimu. Kama ni wakristo watampa na neno la Biblia "Mshike sana elimu usimwache aende zake" ambalo wengi hasa wanamaanisha FORMAL education.

Huyu mtu hata akija kufika Chuo Kikuu utakuta anachagua kozi ambazo zina AJIRA. Kweli anachagua mwenyewe. Hakuna anayemchagulia. Lakini mindset iliyoko nyuma ya hiyo choice ilijengwa siku nyingi bila yeye kujua. Anafikiri kuwa ana freedom kwa sababu kachagua mwenyewe kusoma LAW. Anachagua kozi ambazo zinaitwa "nzuri". Kozi ambazo "ZINALIPA" (mshahara mzuri). Kama unasoma hapa na ulisoma chuo hebu kuwa mkweli hukuchagua kozi unayoweza kupata AJIRA kirahisi? Kuna binti namfahamu toka akiwa mdogo sasa ni binti kashamaliza chuo ameajiriwa. Ninawajua wazazi wake. Ni wahandisi wabobezi na watoto wao wawili kati ya watatu waliwajengea mazingira ya kuupenda uhandisi na kuona ni kipimo cha kuwa KICHWA DARASANI. First born wao ambaye ndo huyo ninayemwongelea ameshamaliza UDSM COET now ameajiriwa serikalini kama Mhandishi huko Kanda ya Ziwa. Na toka akiwa binti wa shule ya msingi alikuwa akisema anataka kuwa mhandisi kama baba yake. Ukimuuliza kwa nini. Anasema my dad is very bright and we have a good life. Ni kweli walikuwa na maisha fair. Not bad. Middle class family. Chakula kipo. Ada hazichelewi tena English Medium. Toka utoto wanafundishwa hisabati na kiingereza na baba kila siku. Huyu binti alikuwa anasoma novel ngumu ngumu kama COSA NOSTRA akiwa darasa la tano. Fikiria hilo. Hesabu za darasa la saba ameshazikava akiwa STD V. In fact alirushwa kutoka darasa la sita kwenda la saba na mtihani wa taifa akiongoza shuleni kwako akiwa kasoma miaka 6 wenzake 7 yote. Yeye na wadogo zake darasani walikuwa wa kwanza katika madarasa yao wote watatu. Walikuwa level za madarasa tofauti. Na sasa ndoto imetimia kwa huyu wa kwanza. Amekuwa mhandisi ameajiriwa serikalini. Kama baba na mama. Mindset yake toka utoto iko hivyo. Hili ni kundi la kwanza. Yani ndo asili yake. Ndo hapa wanasema mtu anaweza kusoma sana lakini MINDSET yake ikiwa imeshikilia jambo fulani hata ungesema nini. It's a RIGID mind. Imeshakaa hivyo miaka mingi. Hicho ndo anachokiona yeye. Imeshakuwa ASILI yake bila yeye kujua. Haoni option yoyote nyingine. Baba na mama wamekaa serikalini na hawajawa na changamoto ndogo ndogo hizi. So why mtoto aone shida.
Waajiriwa wengi kuajiriwa kwao ni issue ya MINDSET tu. Ni kundi la watu ambao bila kujua wametengenezewa mazingira ya kuwa na vision fulani specific. Toka siku nyingi.

Kundi la pili la waajiriwa ni la wale ambao kuajiriwa ilikuwa siyo saana kwamba aliandaliwa hivyo kifikra ila huyu aliwekewa ulazima fulani wa kuajiriwa. Ametoka familia ya wazazi wanaoitwa HELICOPTER PARENTS.
Mfano kutafutiwa kazi anakuta ipo tayari tayari. "Tushakutafutia kazi mwanetu, keshokutwa unaenda kuanza, usije ukatuangusha huko". Ukitaka kuwaambia kuwa ungependa ufanye mambo binafsi unaulizwa wewe ndo unalipa kodi hapa? Unajua tumegharimika kiasi gani kukusomesha huko Malaysia na kwingineko? Ukitaka kuongea utasikia:  Nyie watoto wa siku hizi hamna ADABU? Mzazi anaongea na wewe unaongea. Sasa aina hii ya mazingira huchomoi. Lazima uende kuajiriwa na usiwaangushe wazazi. Unataka kuachiwa LAANA? Washakwambia wanategemea wewe ndo uje uwe meneja au Mkurugenzi siku moja so usiharibu kazi. Kundi hili la waajiriwa ni kundi la watu ambao wanaishi kwa VISION za wazazi wao. Yule binti mhandisi ana mdogo wake wa kiume anakaribia kumaliza elimu ya juu. Wazazi washaanza kumtafutia kazi. Asije kuhangaika. Internship wanatafuta wazazi. Ajira wanaandaa wazazi.
Wasomi wengi wangetamani maisha yawe hivyo. Straight line life. What a life!

Kundi la tatu ni wale ambao WAMEAMUA wenyewe kuajiriwa. Siyo mindset wala siyo suala la wazazi kutaka na kufunga na kuomba aajiriwe bali yeye kapenda. Mara nyingi hawa wanaajiriwa kwa muda au just for the sake of it. Siku akiona vipi anaondoka kwenye ajira kufanya vitu vingine. Hawa ni wenye vision binafsi. Na anaweza kubakia kwenye ajira maisha yote bila influence ya mtu kwa sababu ndivyo alivyoamua. Ndo vision yake. Kama wale matoashi walioamua wenyewe kuwa mimi nataka niwe TASA nisizae wala kuoa kwa ajili ya Mungu. Vision binafsi. Siyo influence ya mtu wala ya wazazi.

Sasa kama wewe ni mwajiriwa ni muhimu ukajitathmini. Uko kundi gani katika makundi hayo matatu. Mada ninayozungumzia mimi katika Makala zangu hizi ni JINSI ILIVYO NGUMU KWA MWAJIRIWA YEYOTE KUPATA UHURU WA KIPATO. Kwa maana nyingine likija suala la kuingiza kipato mwajiriwa anazaa. Hakuna shida kabisa  Lakini likija suala la uhuru wa kipato mwajiriwa ni TOASHI. Hawezi kuzaa.
Castrated.

Ndo nasema jiulize wewe ni aina gani katika hao watatu.
Umefanywa hivyo toka umezaliwa (uliumbwa na kukua ili uajiriwe)?
Au ulilazimika kuajiriwa kwa sababu ya watu kwenye control na maisha yako?
Au umeamua tu kuwa hutaki kuhangaikia uhuru wa kipato kwa sababu tu "siyo ishu". Au unazopata zinatosha umejenga una magari unaishi vizuri nk watoto wanasoma Intaneshno Skul so inatosha huhitaji kuwa na "tamaa" ya mahela mengi!
Comfort zone.
Which one are you?

Au wewe hujui wewe ni aina gani ya mwajiriwa katika hao. Unatiririka tu. Uko bize from Monday to "THANK GOD IT'S FRIDAAAAAY!!!"


Nimeona niweke hizo categories ili kama umeajiriwa au unataka kuajiriwa ujue WHY? Labda itakusaidia. Na utaelewa zaidi mambo ninayofundisha hapa. Usije kujikuta unakubaliana tu na mimi hata hujui why au unatofautiana na mimi bila kujua why.

Sasa naendelea na sababu ya nane inayozuia mwajiriwa kufikia UHURU WA KIPATO.

Ukiacha sababu saba ambazo nimekwishazisema toka mwanzo.. Maisha ya mwajiriwa yana mambo mengi ambayo si maamuzi yake na mengine ambayo si maamuzi yake.

Mojawapo ya jambo ambalo hana maamuzi nalo ni social life yake. Maisha yake ya kijamii. Asilimia kubwa ya muda wa wajiriwa wengi hutumika katika ESSENTIALLY mazingira yale yale, na watu wale wale, katika working field ile ile, wakizungumzia zaidi mambo yale yale. Kama uliwahi kwenda kutembea gerezani utaelewa kuwa kuna ukuta. Na watu ni wale wale zaidi. Ukiacha wachache wanaokuja kutembelea gereza kusalimia wafungwa, kufundisha dini, kuwatia moyo wafungwa nk.

Ni vizuri ukakumbuka kuwa katika viumbe vyote duniani ni binadamu peke yake ambaye aliumbwa ku-socialize. Maana yake ni kwamba your social life as a human being ina maana kubwa sana katika maisha yako kuliko hata your financial life ambayo ndo ninaiongelea hapa. In a point of fact ni kwamba your financial life inabebwa kwa kwa kiasi kikubwa na your SOCIAL LIFE. Wanasema "YOUR NETWORTH IS EQUAL TO YOUR NETWORK". And vice-versa. Sasa katika setup ya ajira ndo nasema UMESHATENGENEZEWA SOCIETY ya kuishi nayo kila siku bila kupenda kwako.
Unalazimika kukubaliana na hiyo social life. Uwe unawapenda huwapendi ndo hao hao. Wawe ni watu wenye mawazo mazuri kichwani au wawe ni wanaowaza vitu vidogo vidogo ndo hao jamii yako.

Na waajiriwa wengi network yake ni hasa hasa watu wa pale kazini kwake. Watu wa kazini kwake ndo wanajua birthday yake ni lini siyo majirani. Kama umeajiriwa jiulize kati ya labda majirani zako na waajiriwa wenzako nani wanajua zaidi ishu zako? See? Network yako imekuwa ile unayoishi nayo siku nzima. Kuishi kwa kutegemea network ya kazini kwako tu ni sawa na kuishi kwa kudhani kwamba kupata marafiki 5000 Facebook inaonyesha una impact kubwa. Nilisema mwaka jana kuwa Ukurasa Facebook wa Mhe. January Makamba ulikuwa na Likes nyingi kuliko wa Mhe Magufuli. Lakini aliyepitishwa akawa JPM. Impact. Hata sasa Diamond Plutnumz ana watu wengi Fb kuliko Mohamed Dewji. Ni kweli kuwa ana impact zaidi ya MO? Au network ya diamond in life na ya MO vinafanana? Likes za Facebook siyo Network Yako halisi. Hao ni FANS tu. Wanaokubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo tu kwa sababu zao. Network yako halisi ni nje ya mitandao hii. Watu wanajua ndoto zako na wanaweza kukupa mawazo yao wakati wowote. Unaoweza kuwauliza siri za mambo yao mfano mafanikio na wakakupa bila kukuficha.

So network yako ya kazini inaweza kuwa ya watu maarufu mno. Lakini kwa kuwa ni ya kutengenezwa huwezi kufikia Uhuru wa Kipato. Lazima utengeneze MWENYEWE network mpya!

Kuna watu network yake kwa sababu ni ya wafanyakazi wenzake wa BOT anadhani kwa kuwa ni BOT basi atafanikiwa kiuchumi based on that network only. Unapaswa kujenga uwezo wa kufahamiana na kukutana na watu wengi tofauti ujifunze vitu tofauti ambavyo ndo vitakusaidia kufikia malengo ya kuwa huru kifedha. Kuna watu hapa watasema "aaah kwani si hata hapa nakutana na wateja tofauti tofauti". Siongelei wateja. Nimesema hata gerezani kuna wageni wanaenda kila siku. Mi naongelea uwezo wa wewe kwa kuamua kwako kukutana na watu katika mazingira ya nje ya ofisi yako na kushare vitu kuhusu maisha nk wakati ambao unataka kukutana nao ili kujifunza vitu tofauti. Ni vigumu mwajiriwa labda wa Wizarani kunetwork na Waziri. Lakini ni rahisi kwa mtu asiye katika setup ya ajira kunetwork na waziri bila hata woga.

Waajiriwa wengi kwa kuwa ameshasocialize kazini kwake kwa masaa 9 au 10  akili imejaa mafaili na mawazo ya kazi za kesho hana muda wa kusocialize na watu wengine tena anahisi imetosha. Kumbe hajui Uhuru wa kiuchumi unakuja kwa mkusanyiko wa mambo mengi ikiwemo kuwa na watu kwenye network yako ambao either wako level hiyo au wamekaribia au angalau wanaelekea huko.

Wakati nimeajiriwa miaka 7 hivi iliyopita kulikuwa na program niliyokuwa nahudhuria kila Jumatano jioni saa 11 hadi saa mbili usiku yenye lengo la kukutana na watu wengine waajiriwa na wasio waajiriwa kubadilishana mawazo. Bwana Anthony Luvanda anaweza kuikumbuka pale HOLIDAY INN (sasa panaitwa SOUTHERN SUN). Kuna watu waliandaa hiyo program. Tulijengewa mazingira ya kufahamiana na watu wengi tofauti na kujifunza vitu tofauti. Lakini wenzetu wengi walikuwa hawaji kwa sababu "wamechoka" japo ilikuwa bure na chai/maziwa/kahawa/bites za bure kabisa. Siku moja bwana mmoja kutoka Uingereza akasema nchi za Asia watu wanatafuta sehemu kama hizo na wanalipa kiingilio kujifunza na kusocialize. Lakini akasema anashangaa huku ukiweka kiingilio watu waje kusocialize na kujifunza hawatakuja. Na hata ukiweka bure pia hawaji. Hasa waajiriwa.

Hili suala liliniingia sana kichwani. Na naweza kushuhudia kuwa idadi ya watu niliokutana nao kusocialize katika miaka yangu miwili ya ajira ni ndogo kuliko watu niliosocialize nao ndani ya miezi sita tu ya kwanza baada ya kutoka katika ajira. Nikitazama leo mambo ambayo nineshajifunza kwa watu mbali mbali waliofanikiwa maishani tayari ni mengi na makubwa na kuna wakati nawaza nisingekutana au kuwatafuta baadhi yao ningekuwa sijui vitu vingapi.

Siku hizi watu walioajiriwa pamoja wana magroup ya WhatsApp. Wanajadili essentially ishu zile zile. Social life ile ile inaendelea online. Network extension. Not expansion. Don't extend your network.
EXPAND it!

Kama umeajiriwa na ndoto yako siku moja uwe na Uhuru wa Kipato. Usiwe mtumwa wa kipato basi jitathmini kwanza wewe ni aina gani katika yale makundi matatu. Kisha acha kutegemea network ya waajiriwa wenzio. Be bold enough to expand your network. Ujifunze kwa wengine. Mazingira ya kuajiriwa yanakupa uwezo wa kuextend network yako tu. Kama tu simu zenye extension.. Network ni ile ile. To attain financial freedom you must FIRST expand your network.

This is a business school nakupa. Unaweza kuchagua kutilia maanani au kuignore.
It's your choice.

Leo niishie hapa.

Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoandika kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 8 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado zingine 2 tu.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 8 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 9.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis People,

Yes,

Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa

Jumatatu, 17 Oktoba 2016

JAMBO LA SABA (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA SABA
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 7.

7. JAMBO LA SABA: ONGEZEKO LA KIPATO CHAKO NI HADI UOMBE AU MWAJIRI APENDE.. (BEING UNDER A MASTER a.k.a. BOSS)

Nianze leo kwa kusema kama umeajiriwa na unasoma hii makala yangu ya leo na huna NDOTO ya kufikia kuwa na uhuru wa kipato nakushauri usitilie maanani sana wala mawazo haya usiyajali sana maana huenda utaona hayaingii akilini. Na kiukweli nakushauri hata usiendelee zaidi kusoma. Lakini kama unatamani kufikia level siku moja uwe huna changamoto ya fedha tena then nakuomba tuendelee pamoja.

So.....

Changamoto nyingine niliyoiona katika kujifunza kwangu inayomkwamisha mwajiriwa yeyote kufikia uhuru wa kipato ni kwamba hana uwezo wa kuongeza kipato chake wakati wowote anaotaka bali hilo jambo linategemea aidha AOMBE kuongezewa kipato (au hata kubembeleza kwa baadhi ya waajiriwa) AMA hata kama hajaomba basi itokee MWAJIRI wake (au bosi) apende au kuamua kukuongezea kipato.

Sasa siko hapa kumsifia mtu aliyejiajiri lakini katika hili mtu aliyejiajiri anaweza kuamua kesho wapate pesa zaidi. Yes. Akaamua tu kuwa kesho ataanza kazi zake SAA 11 alfajiri. Na atakunywa chai tu na atafunga kazi zake saa nne usiku. Huyu yuko likely kuongeza kipato hiyo kesho. Na akiamua keshokutwa pia kiongezeke hilo hasa liko mikononi mwake.
Lakini kwa mtu aliyeajiriwa kuongeza kipato (mshahara) ni MCHAKATO ambao yeye hana control nao kivile. Yes. Maana unaweza kuwa umeajiriwa ukafanya kazi alfajiri hadi usiku afu kumbe bosi wako akahisi unataka uchukue cheo chake. Atakupiga vita hadi basi. Inaweza shida isiwe bosi wewe ukapiga kazi kweli kweli lakini nyinyi kama ofisi in general hamjazalisha kwa kiwango MWAJIRI alichotaka. Na inawezekana mmezalisha alichotaka ila hamuwezi kumlazimisha awapandishe mishahara wakati anawalipa kwa viwango halali vya serikali. Kwa hiyo unaweza kukaa na kipato FLAT (mfano milioni 1 kwa mwezi) kwa miaka miwili mfululizo au hata mitano. Unapiga kazi kubwa lakini kipato kipo FLAT sababu kuongezeka mshahara ni mchakato usio na control nao.

Kuna ambao ajira zao zina vigezo vya kuongezeka mshahara. Mfano ukienda kuongeza elimu ndo kipato kinaongezeka.  So haijalishi sana umefanya kazi vipi bila elimu. Sasa hapo kuna nyakati inategenea pia huyo mwanadamu atakayekuwa anakufundisha huko chuoni ukitofautiana naye unaweza uka"DISCO" na hilo ongezeko la mshahara likaota mbawa. Na ndo maana waajiriwa wengi wanaosoma sijui kufanya hizo Masters za kupandisha mishahara hata hawasomi kuongeza weledi bali lengo ni mshahara upande. Unakuwa mtumwa wa elimu. Sasa unataka kuongeza kipato kwa wrong formula. Formula sahihi ya kuongeza kipato ni either kuongeza significance ya huduma unayotoa au kuongeza idadi ya matatizo unayotatua. That's why kuna watu hawajasoma kivile na wanaongezeka kipato kila wakati. Lakini sasa kwa sababu mfumo uliopo ni AJIRA basi the right formula doesn't necessarily apply. Ukiwa BANK TELLER ukaongeza ubora wa huduma unayoitoa utaishia kuwa EMPLOYEE OF THE MONTH (which is encouraging by the way) lakini huwezi kuongezeka kipato kwa sababu umepiga kazi kama punda kwa mwezi mzima. No. Mshahara wako kama ni laki tano ndiyo utaikuta kwenye ATM hapo nje. Si ndo ulisaini mwenyewe kwenye contract.

Which brings us to another issue. Kwamba thamani yako kifedha kama MWAJIRIWA (your monetary value as an employee) haiko kwenye ubora wa kazi zako bali kwenye what you NEGOTIATED from the start. Sasa shida ni kuwa kwa waajiriwa wengi unapoomba kazi hauko katika position strong ya negotiation. Unakuta mtu anataka tu kazi. Haangalii WORTH yake. Anaogopa akiikosa hiyo atakaa nyumbani mpaka lini. Watu wengi wanapenda kuishi kwa KUPIGA SHIDA SINDANO YA GANZI. Immediate relief. Short-term comfort. Not long term financial growth. Haangalii kama kuna possibility ya kipato chake anachoanza nacho kukua baadaye.
Worse, haangalii kama endapo kitakua kitakua kwa kuzingatia thamani halisi ya contribution yake kama individual. Ganzi ikiisha inakuwa shida mara mbili. Hilo limekuwa kaburi la kuchimba mwenyewe kwa waajiriwa walio wengi.
Sasa anakaa hapo. Anashangaa sukari inapanda hana njia zaidi ya kulalamika mpaka ishuke. Why? Kwa sababu kipato chake hakipandi kutokana na mfumuko wa bei. Lakini mfanyabiashara wa mahindi au magari mafuta yakipanda anaongeza bei ya mahindi. Anayekuja kulalamika ni mwajiriwa ambaye hana uwezo wa kuongeza kipato kesho yake hata afanyeje kazi. Na bado anataka kufanikiwa kiuchumi. Wanashangaa siku zinaenda. Mwisho anamaliza miaka 20 kwenye mfumo wa ajira. Ana Ph.D ya kuajiriwa unadhani utamshauri kuanza biashara akuelewe. Anaogopa. Ukizingatia wiki iliyopita nilisema anakuwa na LIMITED EXPERIENCE. Akichungulia upande wa wafanyabiashara wanaoanza anaona wengi WANASTRUGGLE. Anaogopa kugive up laki nane ya kila mwezi afu aje kustruggle kuanzisha sijui mradi sijui biashara. Anaona wengine wameanza biashara wakafeli wakapoteza mitaji wameanza moja tena. Anataka akija kuanza hela yake isipotee! Anafanya ANALYSIS kwanza. Miaka inaenda. Utumwa unaendelea kumtumikia mtu aliyemwajiri. Mwisho anakuwa sugu wa shida za kimaisha. Inakuwa sehemu ya maisha.
End of the story.

Kwa kuwa naongelea route ya kufikia FINANCIAL FREEDOM kiujumla hili jambo  la mwajiriwa kutokuwa na maamuzi kuhusu lini kipato chake kipande na kwa kiwango gani linafanya kazi kumzuia mwajiriwa kufikia uhuru wa kipato. Na hata kikipanda hakiko REAL-WORTH-BASED. Hivi kama unalipwa mshahara wa milioni 2 per month do you really think thats your worth? Mpaka mtu akupe milioni mbiki ujue unachozalisha ni maybe 10 times. Kwa hiyo basi huwezi kufikia uhuru wa kipato endapo ili kuongeza kipato chako lazima uwe in good terms na MWAJIRI au mwalimu wa Masters ili usije kukosa Masters. Waajiri wengi wametumia hiyo power waliyonayo ya kudetermine nani apate ongezeko la kipato na wakati gani, kuwanyonya na kuwakamua waajiriwa kadri iwezekanavyo na wengine hata kufikia hatua mbaya ya kuomba rushwa ya ngono ili kuboresha maslahi ya mwajiriwa husika. What a tragedy!! Usione hayakukuti kuna watu wanasimulia mambo.

Sometimes utafanya wewe kazi halafu atapanda cheo na kipato BOSI wako. Ndo wakubwa wanamwona yeye. Your worth watajifanya hawaioni. Au utaambiwa fungu hakuna. Subiri bajeti ijayo ipite. Subiri kwanza tuone hii hali. Unaambiwa ngoja tuone huyu Magufuli (Rais JPM) tuone kwanza mwelekeo. Mwelekeo gani mnanyonya tu waajiriwa!!?

Haya mambo hunitatiza sana. Sijui wewe mwajiriwa.

Kama wewe unasoma hapa na una uwezo wa kusema mwezi ujao nataka mshahara wangu uwe mara mbili ya huu wa mwezi huu na hilo likawezekana basi hongera sana. Lakini naamini unasoma makala yangu hii ukiwa Sayari ya #Jupiter.
Siyo duniani..

Kwa kuwa muda leo umenitupa mkono na nilikuahidi kuwa nitaandika kitu leo naomba niishie hapa. Ni karibu SAA 12 na nusa sasa jioni. Naamini utapata kitu hata katika haya machache.

Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoandika kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 7 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado zingine 3 tu.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 7 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 8.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis People,

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumapili, 16 Oktoba 2016

JAMBO LA SITA (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA SITA
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 6.

6. JAMBO LA SITA: KUWA CHINI YA  "BWANA"... (BEING UNDER A MASTER a.k.a. BOSS)

Miaka mingi iliyopita kulikuwa na mfumo rasmi na halali kisheria wa uchumi (uzalishaji mali) ulioitwa UTUMWA (SLAVERY). Mfumo huo uliruhusu MTU kumiliki watu ambao waliitwa watumwa. Na yeye kuitwa " bwana" au kwa kiingereza SLAVE MASTER. Kwa hiyo neno master ni neno zito kuliko wengi tunavyoweza kulichukulia.

Miaka mingi baada ya mfumo huo kukawa na mfumo wa UKABAILA (FEUDALISM) ambapo watumwa waligeuzwa kuwa watumishi hasa mashambani kwa ajili ya kusustain mfumo huo mpya wa uchumi. Na biashara ya watumwa (SLAVE TRADE) ikashamiri ili wamiliki wa mashamba makubwa Ulaya na Marekani wapate nguvu kazi rahisi (cheap labour) ya kutumika kuzalisha mali mashambani na kutumika majumbani nk.

Baada ya muda kwa sababu ya mafanikio katika sayansi na teknolojia basi zikaja zama za viwanda. Na hapa ndo ikatokea changamoto kati ya watu waliokuwa wakimiliki watumwa na wale waliokuwa wakimiliki viwanda. Wamiliki wa viwanda pia walihitaji watu. Lakini siyo watu tu. No walihitaji watu ambao wako "HURU". Sasa ni hiyo concept ya "uhuru" ambayo nitaiongelea hapa leo. Kwa hiyo wenye viwanda wakaingia vita na wamiliki wa watumwa. Kampeni za kuzuia biashara ya watumwa zikaanzishwa. Si kwa sababu watumwa walikuwa wanapendwa sana no. Ni kwa sababu kulikuwa na mfumo mpya unaowahitaji. Mpaka kina Sultan Seyyid Said nk wakajikuta katika hiyo vita. Huko nchini Marekani kukatokea vita kati ya wanazi wa Democrats ambao ndo walikuwa wakimiliki watumwa na wale wa Republicans ambao walikuwa hasa na viwanda sasa. Miaka minne iliyompa ABRAHAM LINCOLN jina lisilosahaulika Marekani kwa kushinda hiyo vita na kukomesha utumwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa ujumla viwanda duniani vilihitaji labourers. Na wakapatikana. Wakaanza kwenda wenyewe kuajiriwa viwandani. Na mahali kwingine. Leo hii mfumo ume evolve watu hawafanyi kazi viwandani tu bali sekta mbali mbali. Mashuleni, mashambani, mahospitalini, huduma za usafiri, huduma za ushauri (consultations, mfano sheria, kodi, mahesabu, nk), mahotelini, etc. Watu leo wameajiriwa kila eneo la uzalishaji mali.

Katika uhusiano wa zamani wa utumwa mtumwa alikuwa chini ya "BWANA" yaani Master. Katika kutafuta njia ya kuleta mahusiano mapya kati ya wafanyakazi waliotoka utumwani na waajiri wao wapya likabuniwa neno jipya linaitwa BOSS ili watu wasiendelee kujifeel kama bado wapo chini ya MASTER. Kimsingi neno "boss" limetolewa katika neno la kidachi (Dutch) linaloitwa BAAS ambalo cha ajabu linamaanisha MASTER/BWANA. Kwa hiyo neno boss ni neno MASTER tu ila limepakwa rangi rangi mpaka uzikwangue rangi ndo utajua.

Kimsingi basi mahusiano yaliyopo kati ya mwajiriwa na mwajiri au mwakilishi wa mwajiri ni yale yale tu kati ya mtumwa na bwana wake. Kilichobadilika ni uhusiano umepakwa rangi.

Juzi nilisema kuwa kuna kitu kinaitwa MINDSET. Na nikasema MINDSET yako ikikamatwa utabadikishana ardhi yako na mtu afu yeye anakupa kioo. Mindset.

Kilichofanyika ni kucheza na mindset tu ya mtumwa yule yule. Yani kumuuliza: kati ya kuwa mtumwa na kulala kwenye mabanda na kushinda mashambani unavuna pamba kwa mijeledi huna haki hata ya kuzaana.. Kati ya hayo maisha na kuishi huru ukilipwa vijisenti kutokana na nguvu zako na vikakusaidia kununua chakula UNACHOTAKA, na kununua vijinguo unavyotaka na kulala unakotaka na hata kijiuhuru cha kwenda mahali mahali kula bata jioni na wenzako mkijipongeza kumaliza siku na kupeana michapo ya hapa na pale NI YAPI WEWE UNACHAGUA???

Unadhani mtumwa angechagua nini? Yani hapo hata iweje anachagua "B". Kabla hata hujamaliza kumuuliza. Na ni kweli. It's good. But that's the problem with most of us. We just settle for anything good. Basi. Kumbe huyo anayekuuliza amecreate tu mazingira ya win-WIN situation. Hapo nimeandika win ya herufi ndogo na WIN ya hefuri kubwa. Kumbe unakuwa una illusion ya kuwa uko huru lakini ni utumwa ule ule tu ile umekuwa upgraded. Ukitaka mtu asiache kutumia simu unafanyaje. Upgrade it. Kila siku simu zinavitu vipya. Na vina mafufaa. Lakini ndo win WIN.

Na kwa kuwa topic yangu ni kuhusu kwa nini MWAJIRIWA hawezi kufikia uhuru wa kipato ndo maana hii win WIN situation naiongelea. Kwamba mwajiriwa ni a modern day slave. Bado ana MASTER. Ambaye anamwambia what to do.

I. Unapoajiriwa unapewa Job Description.. Kazi yako ni kuvuna pamba kila siku asubuhi mpaka jioni ujira wako ni huu. Unakubali unakataa?
Wachache hukataa. Mtumwa hakuwa na choice. Waajiriwa pia HAWANA choice. Yani mfano ukichoka si unaweza kupumzika. Mwajiriwa hata akichoka kupumzika siyo choice kazi lazima ziishe. Bora punda afanyeje...........? Unakumbuka?

II. Waajiriwa wamefungwa pingu pia.
Wajiriwa wamekuwa watumwa wa kipato in the sense kwamba hawezi kuacha kwenda hata kama hajisikii vizuri. Kazi zake anafanya nani? Pamba yake atavuna nani? Hela itakuwaje asipoenda? So anahisi yuko huru kwa sababu anaenda mwenyewe kumbe hajui kuwa kuna INVICIBLE CHAINS tu. Au somewhat loose chains. Hazionekani kwa macho tu lakini zipo. Kwani nchi zetu sisi hizi ziko huru? Si ni bendera tu. Bado uchumi wa nchi zetu uko mikononi mwa wengine. Mpaka leo nchi za Africa Magaribi zinalipa kodi kwa ufaransa kwa miundombinu ambayo ufaransa ilijenga wakati wa ukoloni. Colonial tax.
Kataa kulipa uone.
Hahaaaa
Ndo hivyo. Invincible chains.
Tragic.
Waajiriwa wengi wamekuwa watumwa kiasi kwamba akihisi kesho kazi hana anaweza kuugua ghafla. Kama umeajiriwa jiulize kama kesho ukifika ofisini ukaambiwa hakuna kazi tena.. From nowhere. Utapiga kamluzi kuzuri au utapiga "yeleuwiiii" moja ya hatari au kupigwa bumbuwazi hapo. Enchained.
That's how it is.
Bosi yupo kuhakikisha hutambui uwepo wa hiyo minyororo.

III. Your MASTER (boss) is a-l-w-a-y-s righhhht!!!!!
Waajiriwa wengi wanajua hii situation. Hutakiwi kutofautiana na boss wako sana. Au Mara kwa Mara. Atamwaga ugali na mboga na kuzima jiko.
So kama vipi kama unaona mawazo ya bosi siyo sawa we potezea tu maisha yasonge. Usawa wenyewe huu wa kusomeshana namba. We tulia mwache "anajua anachokifanya."
Waajiriwa wengi wako hivyo. Mawazo yao mazuri hawathubutu kuyaweka wazi kama yanakinzana na mtazamo wa MASTER! or Mistress! Hii imeua creativity ya waajiriwa wengi na wameamua kufia ajirani bila kujua wanainyima dunia mambo mazuri mno. Ackton na Koum wangeajiriwaga Facebook kama walivyotaka huenda Leo hii kusingekuwa na WhatsApp. Sometimes losing your job usiichukulie negative. Ukaamua kutafuta nyingine. Think. Why kuna shida katika ajira yako. Why ideas zako watu wanasema nzuri na wewe unajua fika but bosi wako hazikubali. Think. Unaweza kuwa unainyima dunia jambo kubwa mno kwa kung'ang'ana tu kubaki ajirani. Boss tu ndo yuko sahihi.
Umekuwa mtumwa wa fikra zake yeye.
Za kwako ziko kichwani kwa ajili ya nini sasa. Mapambo au?
Simaanishi umchukie bosi ila ndo ujue.

IV. Watumwa walikuwa wakipewa adhabu zinazoshabihiana na za waajiriwa. Reprimand. Kufokewa. Kupunguziwa "share" (kukatwa mshahara), nk. Katika ulimwengu wa Biashara hakuna mtu wa kukupa adhabu. Huhitaji adhabu. Adhabu ni kwa watoto. Ukiacha penal system. Mtu mzima unahitaji ushauri not reprimand ambayo ipo zaidi kudiscourage makosa wakati makosa ni sehemu ya kujifunza. Unadhani Dewji hakosei? Kwani Bhakressa akivunja printer bahati mbaya anakatwa mshahara? Vunja wewe sasa utasikia Mara gross negligence Mara sijui nini. Utadhani umevunja glass ya bi mkubwa enzi za utoto. Ndo utaelewa maana ya kuwa na boss.
Ukizidisha makosa utakatwa "mguu" kama #KuntaKinte wa ile movie ya #ROOTS. Kipato kikatike.

V. Watumwa walikuwa wakipewa incentives mbali mbali kuwahamasisha kuzalisha zaidi. Chakula zaidi. Sherehe mbili tatu. Siku yao maalumu kupumzika. Nk.  Ndivyo ilivyo kwa waajiriwa pia. Mei Mosi. Family Day. Nk. Afu waajiriwa wanependa sikukuu kweli. Labda ili kuescape kidogo kutumwatumwa. Wapumzike kidogo watembee waone hata bichi.
Sijawahi kusikia siku ya WAWEKEZAJI.
Anyway..
Bosi wako yupo kusimamia vitu kama hivyo viwepo na kumonitor effectiveness yake.

VI. Lengo halisi la slave masters lilikuwa kumsqueeze mtumwa mpaka jasho lake la mwisho kwa "malipo" kiduchu. Lengo la WAAJIRI wa leo ni lile lile. Kazi ya bosi ni kuhakikisha hilo linatimia kikamilifu.

Kuna researcher mmoja wa Harvard Business School aliandika makala kwenye mtandao wa FORBES inaitwa: "The Messy Link Between Slave Owners And Modern Management". Kaisome, google hiyo title utapata.

Sasa katika #mazingira hayo ya uwepo wa MASTER-SLAVE relationship uhuru wa kipato hauwezi kupatikana. Nimesema huu ni essentially mfumo ule ule tu ila umepakwa rangi. Kama magari ya baadhi ya yadi za kitaa. Unakuta gari lina mvuto kwa nje kumbe. Nunua tu baada ya muda utaanza kuelewa kwa nini walikubali kukupunguzia bei...

Again, bottomline is Uhuru wa kipato kwa mfumo wa ajira ni myth. Ndo maana wastaafu wengi wana suffer. Hawakujua walikuwa wakitumika katika win-WIN situation.

Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoandika kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 6 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado zingine 4.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 6 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 7.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis my People,

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Jumamosi, 15 Oktoba 2016

JAMBO LA TANO (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA TANO
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 5.

5. JAMBO LA TANO: HAKUJAWAHI KUWA NA  AJIRA SALAMA... (THERE'S NEVER BEEN THE SO-CALLED "JOB SECURITY", AND NEVER WILL THERE BE ANY)

Leo sianzi na swali. Naanza na ASSIGNMENT hahaaa. Usiseme hee shule tena? Usijali. Ni fupi tu.

(Assignment):
Kama wewe ni mwajiriwa mahali popote naomba chukua kalamu la karatasi. Kisha andika sababu 10 ambazo unadhani zinakupa UHAKIKA wa kumaliza huu mwaka ukiwa kwenye hiyo ajira. Huu mwaka tu. I'm serious. Write them down. Labda..

1. Mchapakazi
2. Mwaminifu na Mwadilifu
3. Una elimu kubwa zaidi
3. Bosi ni Ndugu Yako, (au mchepuko), nk
4. Una kipaji kimoja unique sana so lazima waendelee kukuajiri.
5.
6.
7.
8.
9.
10.

Andika usiache. Halafu ukimaliza kuziandika utagundua hakuna hata moja ambayo inakupa UHAKIKA kuwa ajira yako iko SECURE(salama).
None!

Huenda hukubaliani na mimi kwa sababu unazoziamini sana. Lakini ngoja nikupe sababu chache kwa nini JOB SECURITY IS A MYTH. Ni kitu kisichokuwa halisi.

(I). HUNA CONTROL NA MAWAZO YA BOSI WAKO.

Na katika ubinadamu kuna mengi. Anaweza asikupende tu. Kaamka na hasira zake akakuanzishia visa tu. Au kama ana mamlaka ya kukufuta akakufutilia mbali asubuhi. Unabisha? Kuna watu walifukuzwa kazi katika mazingira yasiyoeleweka. Yani bosi wako anawaambia wamiliki wa kampuni: MNANITAKA MIMI AU HUYU? Wamiliki wanaamua kukusacrifice wewe hata kama hawajaelewa? Unadhani haliwezi kutokea kwako?
Au unafuta katika Jina la Yesu. Basi sawa. Endelea kufuta bila maarifa. Unajua hata ukiwa unachora picha na penseli inabidi uwe una maarifa ya kuchora. Usitegemee kufuta tu. Ufutio utaisha na picha haiko. "Watu wangu wanangamizwa kwa kukosa maarifa" ~ hilo ni NENO la BWANA. Sasa wewe endelea kufanya Yesu kuwa "ufutio" wako utauona mwisho wake.

(II). HUNA CONTROL YA MAPATO YA SEHEMU YAKO YA KAZI

Inawezekana sasa hivi mnapata pesa pesa kidogo hivyo siyo shida kukulipa wewe huo mshahara. Ikitokea competition ya maana sokoni kampuni yenu ikakosa kuona faida cha kwanza wanaangalia wapi pa kupunguza MATUMIZI. Unaweza ukajikuta huna ajira na hutaamini. Naamini ushajipanga pa kuanzia.
Hapa ndipo ninaposhauri ukasome kitabu muhimu sana cha mtu anaitwa Dr. Spencer Johnson kiitwacho WHO MOVED MY CHEESE?
Utaelewa. Usije ukadhani ajira ni yako. Ajira ni ya mwajiri tu. Wewe umekodishwa kwa muda tu. Anytime mwenye nayo anaichukua. Afu na wewe utaanza kuuliza WHO MOVED MY CHEESE? Kweli? "Your" cheese?

Unaikumbuka UCHUMI Supermarket? Ilikuwa imeajiri watu wengi siyo. Ikafunga ofisi zake. Halafu inakuwaje sasa.
What about ada za hao watoto wako. Au ndo elimu bure! Kuna kitu cha BURE kweli dunia hii? It's not free. There's no free lunch wazungu wanasema. You'll somehow pay for it in a different way.
Think. It's still LEGAL to think.

Halafu mwingine akiona unaongelea sijui Uchumi Supermarket yeye anaona haimhusu. Anajisemea Kwanza Mimi Mwalimu. Ajira UHAKIKA. Unafikiri kutumbuliwa ni kwa Wakurugenzi tu na wakuu wa mikoa? Umesahau methali ya MWENZAKO AKINYOLEWA.....

(III). HUNA CONTROL NA UWEPO WA MWAJIRI AU BOSI MPYA

Kumetokea mara kadhaa makampuni kwa sababu kadha wa kadha yameuzwa au kuingia ubia. MERGERS AND ACQUISITIONS. Huwezi kuzuia. Hapo unajikuta chini ya bosi mpya au mwajiri (kampuni) mpya.

Kuna kampuni inaitwa Yahoo! Sijui kama kuna kijana wa mtandaoni asiyeijua. Ilikuwa MAARUFU. Wakitengeneza pesa nyingi. Wakiajiri watu wengi. Siku moja BILL GATES (MICROSOFT) akaamua kuwa itakuwa dili nzuri akiwanunua. Kwa sababu uwezo anao akawanunua. Yani unanua kampuni na wafanyakazi wake wote. What happened later? Unajua? Kama hujui ni kwamba baada ya kununua Yahoo! MICROSOFT wakaona wana mzigo mkubwa sana wa waajiriwa. Wakaamua kupunguza waajiriwa 800!!!! Wengi kati yao wakiwa waliokuja kutoka Yahoo!. Hapo unalipwa stahiki zako unaenda. Sasa security ipo wapi? Hivi kama Bill Gates anapunguza watu 800 hujiulizi.

Juzi juzi hapa kwetu kuna kampuni maarufu ya Africa Barrick Gold (ABG) maarufu kama Barrick ambayo iliuza baadhi ya hisa zake kwa ACACIA na hivyo kuipa ACACIA uwezo wa kufanya baadhi ya maamuzi kuhusu ajira. Watu wamepoteza ajira katika mazingira hayo.

Sasa nini kinaweza zuia Vodacom au Tigo au Twiga Cement au ITV au TCC (Sigara) au CRDB wasifikie huko. Soma alama za Nyakati. NBC iliuza baadhi ya hisa zake kwa ABSA Bank ya South Africa na ABSA hisa zao nyingi zinamilikiwa na BARCLAYS BANK ya Uingereza. Sasa hapo nani mmiliki wa NBC? Afu wewe hutaki kusoma THE WRITING ON THE WALL.
Stanbic Bank ilikuja Tanzania kwa kununua MERIDIAN BIAO kuna watu wakipoteza kazi enzi hizo.
Unajua mwenye hisa nyingi Fastjet ni nani?
TBL je?
Vodacom je?
Unajua nani mwenye hisa nyingi?
Unajua maamuzi yake anafikiria nini kichwani?

See. So, ajira ni a sort of gambling. Kamari. Hujui hata keshokutwa tu kama ajira yako itakuwa salama.

Sasa Uhuru wa kipato hapo hauwezi kuja kamwe.

Unakumbuka transition ya kutoka SHOPRITE kwenda NAKUMATT? Siku hizi naona kuna wakenya mle wameajiriwa kwa kazi ya kuoka mikate. Sijui kama wote waliokuwa Shoprite wamepata nafasi Nakumatt.

Wakati nakuja jijini kulikuwa na hoteli maarufu sana SHERATON, baadaye mmiliki akabadilika akaitwa MOVENPICK, baadaye akaja mwingine ROYAL PALM, saivi yupo mwingine SERENA. Hivi kinachomzuia Serena kuajiri mtu mpya kwenye nafasi yako ni kipi? Ask yourself.

(IV). HUWEZI KUJUA MAAMUZI YA SERIKALI KUHUSU SEHEMU YAKO YA KAZI AU AJIRA YAKO

Kuna mtu alijua kuna uhakiki wa vyeti ungekuja?
We unajua baadaye watahakiki nini?

Serikali inaweza kulipiga marufuku shirika unalofanyia kazi kwa madai ya kujihusisha na labda USHOGA. Hapo ajira yako vipi?
Sijui magazeti na redio vikifungiwaga kwa muda usiojulikana huwa ajira zinakuwaje? Wanaendelea kulipwa mshahara bila kuzalisha?
Serikali inaweza kuja na maamuzi ya kurasimisha jambo au kuharamisha jambo ambalo likaathiri ajira yako moja kwa moja.
Au kuanzisha sheria ya kuajiri watu waliopita JKT kwanza na waliopo kazini waende JKT pia ndo waendelee na ajira. Utakataa?
Au huamini kuwa hilo linaweza kutokea?
Kwani mjadala wa FAO LA KUJITOA uliwahi kufikiria kuwa utakuwepo?
Nini kinazuia serikali kufuta ajira za shirika fulani na kuajiri upya? Sasa hapo undugu wako na bosi ndo utajua. Kama rais anaweza kumtaja mke wa Waziri kung'ang'ania ajira itakuwa wewe na huyo bosi ambaye ni ndugu yako?
Unategemea undugu?
Serikali ikifanya maamuzi ya kubadilisha wakuu wote wa idara zote nyeti ukapata bosi mpya?
Unategemea nini
Kipaji?
Uadilifu?
Hujui kuna watu hata uadilifu wako hawana time nao. Hawakutaki tu wewe. Licha ya uadilifu.

(V). HUNA CONTROL NA TEKNOLOJIA KUREPLACE AJIRA YAKO

Unafahamu kitu kinaitwa teknolojia. Basi welcome to the future.

Kuna watu walikuwa wameajiriwa kwenye call box miaka ya nyuma. Kuna makondakta wanapoteza kazi kwa mfumo wa mwendo kasi. Tunakoenda dunia hii ni treni za umeme madereva mpo? Ulaya sasa  kuna electric cars.
Watoto wanaosomea urubani kuna ndege hazina rubani now.
Kuna DRONES now..
Nani kati yetu aliwaza miaka 20 iliyopota kuhusu drones.
ThreeD videos?
Sasa hivi teknolojia imefikia unaweza kupima damu yako au mapigo ya moyo kwa kutumia Application kwenye simu yako!
Sisi huku bado watu wanafanya kazi ya kuajiriwa kujaza mafuta kwenye magari Petrol Station.
Teknolojia imeshaondoa hizo vitu nchi za wenzetu. It's a matter of time huku  kwetu yatafika.
Nchi za wenzetu kuna mahali hotelini ukienda restaurant ni self-service hakuna hata mhudumu wa eti akupakulie. No, unapakua mwenyewe ukimaliza kula vyombo unaweka kwenye conveyer belt vinapelekwa kwenda kuoshwa na machine.
Sasa wale mnasomea kuajiriwa kwenye Restaurant Mahotelini...
Subiri uone siku tukiwa na angalau umeme wa uhakika ndo mambo mengi yataibuka hujawahi kuona. Ajira nyingi miaka 20 ijayo hazitakuwepo. Technology is taking over baby! Sasa unasemaje una uhakika na ajira yako wakati teknolojia ikibisha hodi tu ajira yako inakuwa past tense.


Kazi nyingi za kufanywa na binadamu zinaenda kuwa replaced na computer. Unadhani komputer haiwezi nini sasa hivi?

~ Kupika?
~ Kuendesha gari?
~ Kupanga mafaili?
~ Kupiga muhuri?
~ Kutegua mabomu?
~ Kufagia na kufuta vioo?
~ Kushona nguo?
~ Kupokea wageni?
~ Kufanya interview?
~ Kuendesha ndege?
~ Kuongoza magari barabarani?
~ Kupakua mizigo bandarini?
~ Kufanya utafiti wa wapi kuna madini na wapi kuna udongo wenye rutuba?
~ Kuandaa risala?
~ Kutambua mhalifu?
~ Kujua kitu anachowaza mtu?
~ Kufanya auditing?
~ Kuandaa ripoti?
~ Kutoa tahadhari (prediction) kuhusu hali ya hewa au ujio wa Tsunami?
~ Kutangaza mpira?
~ Au kumoderate mdahalo?
~ Kupokea simu?
Kwani unapopiga simu na kuambiwa sijui bonyeza nyota.. Unadhani ni MTU yule? Si automation tu. Na majibu unayapata.


Kuna mtu akisoma baadhi ya vitu hapo juu anashangaa anasema aah wapi?
Huamini kuwa one day computer itafanya virtually everything? Basi hujaijua computer ninayozungumzia hapo juu. Tunaongelea computer mbili tofauti kama huamini kuwa in future mtu anaweza kuingia benki na kusiwe na mhudumu hata mmoja wala hata mlinzi!!! Welcome to the microchip world bruh!
Nahmean?
Sasa hivi watu wanatengeneza BURGER maabara. Hahaaaa. Watu wana gari isiyo na Dereva.
Anyway.

Fanya hivi ingia FACEBOOK kaangalie page inaitwa #FUTURISM. Usiache. Utapata picha dunia inaelekea wapi..

Sasa..
Ukitoka kwenye hiyo page ujiulize ajira ngapi zitapotea kwa computer kufanya vitu vyote hivyo kwa UFASAHA bila kukosea hata kidogo au kwa advancement hiyo ya teknolojia?
Uliwahi kuwaza mwaka 1999 wakati wa Floppy Disks kuwa kuna siku tutakuwa na kichip kidogo kinaitwa memory card chenye uwezo wa kutunza kumbukumbu za sheria zooote za nchi na regulations zake na ka-chip kenyewe kako kama ukucha tu.!!

Sasa piga mahesabu miaka 20 ijayo.

That's the future we are facing.  But most of us are so enstranged to the reality we do face. Total strangers to reality.
Teknolojia itaondoa walioajiriwa shambani, kiwandani mpaka sokoni. Sasa wataenda wapi? Ndo ujue Mungu alichoweka ni KAZI si AJIRA. Coz ajira ikiwa haipo still things can go. With technology.

Sasa ukikaa katika ajira mpaka siku uambiwe hatukuhitaji kwa sababu tumeleta hii mashine inaweza kufanya kazi zako kwa usahihi sijui utaendelea kufuta kwa Jina la Yesu? Maarifa.
Afu vijana wanasoma BANKING AND FINANCE wakaajiriwe kama Bank Tellers wakati sasa hivi kuna ATM za mpaka kuweka hela benki dunia hii.
Bill Gates ana mradi wa Tsh Trilioni 150 wa kuangamiza mbu duniani ili kuondoa Malaria kabisa. Sasa kama umeajiriwa shirika la kudeal na malaria hiyo ndo future yako.

Sasa basi kwa mazingira hayo ya kutokuwa na control ya source yako ya income (ajira) sahau kuhusu financial freedom. It just can't happen in that setup. Kupata uhuru wa kipato unapaswa kuwa na uwezo wa kucontrol source yako ya income.

Anyway.
Hayo ni baadhi ya mambo machache tu yenye lengo la kukupa picha ya hali halisi kuhusu AJIRA. Kwamba ajira haina usalama wowote kama unavyodhani. Kama wewe pia umeajiriwa kwa kigezo cha ajira kuwa na job security.

Lakini katika pita pita zangu huku na kule nimekuwa nikikutana na waajiriwa wakisema:
"Mwenzako nina ajira angalau nina UHAKIKA wa kuingiza kitu". Kama swala ni UHAKIKA wa kuingiza kipato basi utakuwa hujajua vizuri kitu kuhusu ajira. Ieleweke kwamba siko hapa kukwambia acha kazi. That's your business. Mimi nipo kukwambia kwa nini ajira siyo mfumo sahihi wa kukupeleka kwenye uhuru wa kipato. So kama financial freedom si ndoto yako wala usihofu sana kuhusu haya unayoyasoma hapa. Wewe ambaye unajisemea saivi kuwa cha msingi mkono uende kinywani. Wewe unayedhani uliumbwa ili kupeleka mkono kinywani. Wewe usijali sana kuhusu unayoyasoma hapa. Endelea kuwa na uhakika wa kupeleka mkono kinywani.

But bottomline is...
Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa zote kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 5 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Na bado zingine 5. Dah siku kweli hazigandi.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 5 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA SITA.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis my People,

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.