JAMBO LA TISA
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)
TUNAENDELEA:
Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).
Na leo naendelea na sababu ya 9.
9. JAMBO LA TISA: KUPOTEZA UHURU WA MAMBO MENGI (LOSS OF FREEDOM)
Wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikipenda sana maisha ya shuleni. Nilipenda sana kuanza shule mpaka wakalazimika kunipeleka kabla ya wakati lakini shuleni nikarudishwa kwamba mkono sijui ukipita kichwani sijui hauvuki bega. Anyway. Nilianza mwaka uliofuata. Nilipenda vitu vingi. Nilipenda mazingira ya shule, nilipenda sare zangu za shule hasa zile za mara ya kwanza. Aisee! Nilipenda kuhesabu namba (hii nafikiri niliipenda kwa lazima hahaaa maana kulikuwa na stiki za hatari ukichelewa kengele), nilipenda kukimbia mchaka-mchaka na nyimbo zake za Makaburu na za Mandela na nyingine nyingi hasa ule wa "JUA LILE LITELEMKE MAMA!!!". Aisee. Nilipenda gwaride hadi nikawa kiongozi wa gwaride wa shule za msingi kata nzima. Mahaba ya dhati kumoyo. Nilipenda mazingira ya shule. Ramani za Tanzania, Africa, nk za mawe yaliyopakwa chokaa, nilipenda bustani na miti na viwanja vya shule. Nilipenda masomo hasa Kiingereza. Kwa ujumla nilipenda KWENDA shule.
Lakini nyakati za likizo nilizipenda zaidi na kutembelea ndugu, kucheza na rafiki zangu, kwenda kuwinda na kuvua samaki, kwenda kufanya mazoezi ya mambo ya kanisani, kwenda kuangalia mashindano ya mpira kwa watu wazima au jamaa wa Kisukuma wakicheza ngoma zao katika sherehe mbali mbali nk. Nyakati za likizo nilizipenda kwa kweli.
Na baadaye nikapemda kwenda sekondari. Nikaenda. Nikaishi maisha karibia sawa na yale ya shule ya msingi. In terms of ratiba na kanuni na taratibu nyingi. Na nyakati za likizo pia nilipata fursa ya kuishi hasa maisha binafsi yasiyo na kanuni zilizonifunga.
Taratibu taratibu nikaanza kuona kuna kitu fulani moyoni mwangu ambacho kimeanza kupungua kuhusu maisha ya shule. Mfano nikaanza kuona kama maisha ya shule yananiprogram kuanzia mbali ili ifike hatua nione hiyo ndiyo kawaida. Nikaanza kuwaza kuwa hivi siku moja nitaweza kuishi mwaka mzima nikivaa mavazi ninayoyapenda mimi asubuhi hadi jioni January hadi December, na nikienda kula muda ninaosikia hamu ya kula, nikienda kulala muda ninaojisikia kulala iwe SAA moja jioni au saa nane usiku. Niongee na watu kwa lugha ninayopenda na siyo lazima niSPIKI INGILISH! Niweze kwenda kokote ninakotaka kwenda wakati wowote kama nina sababu maalumu bila kuambiwa NIMETOROKA na mtu yeyote wala bila kusubiri idhini ya mtu mwingine. Na nikaona kama kuanzia shule ya msingi nilitengenezwa kuipenda shule siyo kama mimi ndo niliipenda mwenyewe from nowhere. Wanafunzi walionekana bora kuliko watoto waliokuwa wapo tu nyumbani wanalialia na kuongea kikerewe tu mchana hadi usiku na kukaa bila kujua hata kusema neno "SHIKAMOO". Niko sekondari, Seminari, nikaanza kutamani ije siku ambayo nitaendelea na mosomo yangu pasipo kuvaa kitu kinachoitwa sare. Ndiyo ikawa sababu kubwa ya mimi kutaka kusoma Chuo Kikuu badala ya kuendelea na masomo ya Seminari. Sasa sijui ndo wanasema wito uliisha. Hahaaa. But naongelea kilichotokea. Kilichotokea ni kwamba nyakati za likizo nilijihisi huru zaidi kufanya mambo yangu nilizipenda kuliko nyakati za shule ambazo zilikuwa na program ya kufuata kuanzia unapoamka hadi unaporejea kulala. Sisemi system hizo hazina faida. Zina faida nyingi mno. Ila kwa sababu ya series za Makala zangu hizi najaribu kukufanya kuona shida mojawapo ya mindset and mind control iliyotengenezwa na watu waliotengeneza mfumo wa aina ile wa elimu.
Mfumo ule (the Formal Education System) tumeurithi kwa wakoloni ambao waliuanzisha kwa ajili ya kupata watu wa kuwasaidia kazi zao za kiutawala na kazi zinginezo (white collar and a few blue collar jobs). Ni mfumo ambao waliopitishwa huko waliandaliwa kwa kusudi maalumu. Sisi tukaja kuurithi kama ulivyo na makusudi yake kama yalivyo. Na asilimia kubwa ya waajiriwa wamepita katika mfumo huo kwa namna moja ama nyingine.
Na ndiyo maana maisha ya mwajiriwa ni kama maisha ya mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari. Picha hii hapa chini nikikuuliza uniambie ikiwa ni ya WAAJIRIWA ama WANAFUNZI utasema ni kina nani?
I. Mwanafunzi anaishi kwa kengele mwajiriwa anaishi kwa kengele pia bila tu ameipa jina zurizuri. Anaiita ALARM CLOCK.
II. Mwanafunzi ana muda specific wa kwenda na kutoka shuleni. Mwajiriwa pia ana muda specific wa kwenda kazini. Hawezi kwenda au kutoka muda wowote anaotaka yeye.
III. Mwanafunzi ana kazi specific za kufanya. Zinajulikana kabisa na zimeandikwa. Walimu wanajua maana ya SCHEME OF WORK na LESSON PLAN. Mwajiriwa pia ana kazi specific za kufanya zinajulikana na zimeandikwa kabisa. Waajiri na waajiriwa wanajua kitu kinachoitwa JOB DESCRIPTION
III. Mwanafunzi ana mavazi maalumu aendapo shule. Of course kuna shule zina safe. Na zingine hazina sare lakini zina dress code fulani. Na kuna sare za siku ya michezo. Mwajiriwa pia ana mavazi maalumu aendapo kazini. Na hivyo hivyo kuna ajira zina sare na kuna makampuni yana sare unapewa mpaka sare za kuvaa siku ya michezo. Hakuna shida katika hili is that what you're saying? Well, sawa. Inawezekana hakuna shida. Inawezekana nakompliketi maisha tu bila sababu za msingi, au siyo?
IV. Mwanafunzi ana muda maalumu aliopimiwa wa kula. Mwajiriwa pia ana muda uliopimwa wa kula. Hawezi kuamua kula masaa mawili eti alikuwa na mazungumzo na rafiki yake. Watazungumza WhatsApp. Kazi kwanza.
V. Mwanafunzi ana madaraja ya vyeo. Kuna mtu wa komonitor wengine. Class Monitor. Head Prefect. Nk. Hawa ndo CCTV za walimu. Mwajiriwa pia anayo hii. Kuna vyeo. Kuna officer, Manager, Excom, nk. CCTV ya MWAJIRI. Huwezi kuishi wala kuzalisha bila kuwa monitored.
VI. Kuna shule ukiongea kilugha unapewa pembe. Kiswahili ndo habari ya shuleni. Na ukienda sekondari Kiinglish ni lazima. Hata kama hukijui utafundishwa mpaka angalau ujue cha kumjibu mwalimu tu. Waajiriwa pia linapokuja suala la lugha kuna lugha maalumu ya kumhudumia mtu. Ukienda ofisi kadhaa unakuta maneno kwenye vibao tu yanaonyesha lugha gani hapa inaweza kutumika. Kikerewe acha kwenu. Kwanza kinamsaidia nani nchi hii. Hata kama mteja ni mkerewe.
Kuna waajiriwa wamekaririshwa mpaka jinsi ya kuongea na mteja physically kwenye simu. Ulishawahi kupiga simu ile namba 100!? Unasikia wanavyoongea. Piga tena baadaye wanaongea vile vile.
Ulishaenda airport au Railway stesheni usikie wale wanaotangaza matangazo. Ni monotone. Utasikia kale kamlio.. Tii-ntiiii... Afu unasikia sauti nzuriii... "Attention all passengers, the passenger train to Mwanza via Morogoro Dodoma and Shinyanga is on lane number one and will leave in 5 minutes time....! Njoo kesho utasikia hivyo hivyo. Utafikiri ni kitu kimerekodiwa.
Unaambiwa ni kuimprove quality ya service. Hivi ukimpigia Dewji simu na yeye anapokeaga hivyo kwani? Kwa hiyo yeye hana quality nzuri ya huduma kwa kuwa hajapokea kama wale wa namba 100?
Listen my friend. Life is a mind-control game. And employees play in that field very well. Wazungu walituletea dini hawakutuletea mindset education. Ili tubaki na dini tu bila matunda thabiti. Mind is better than religion. Coz Mungu alileta wokovu hakuleta dini. Wazungu walileta formal education wakatunyima SELF EDUCATION. Hii unapaswa kuitafuta mwenyewe. Na hii ndo itakukomboa kifikra.
Sasa kwa mifano niliyoitoa hapo juu hivi kama huna uhuru wa vitu vidogo kama:
~ muda wa kwenda na kutoka katika shughuli yako ya kiuchumi
~ mahali pa kuifanya hiyo shughuli everyday lazima uende hapo huwezi kuamua ukafanyie restaurant au beach hata kama unataka
~ muda wa hata kitu kidogo kama kula
~ mavazi gani uvae.
~ nini ufanye leo katika majukumu yako. Ushapangiwa cha kufanya
~ wakati gani usafiri kwenda utakako kwa sababu zako ni mpaka uruhusiwe
~ kupumzika kwa muda utakao hata kama ni masaa mawili ukakae hapo nje ya ofisini ukiwaza mpango fulani muhimu. Au ukipokea simu moja muhimu sana
Kama huna freedom na vitu vidogo kama hivyo. Unawezaje kupata FINANCIAL FREEDOM katika hiyo setup?
Kumbuka nilishasema kwenye makala zilizotangukia kuwa hata kipato chako hupangi wewe. Nk..
Nikukumbushe tu kwamba AJIRA ni mfumo ambao bado upo upo tu sana huku kwetu. Swali ni je mfumo huu upo kwa ajili YAKO wewe pia uajiriwe?
If YES, then good luck.
If NO, then DO take proper action.
Mi nimemaliza. Na kwa leo naishia hapa.
Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoelezea kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 9 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA linapokuja suala la kufikia uhuru wa kipato. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.
Bado 1 tu.
Endelea kuwa na mimi kidogo tu.
But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 9 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 10 na ya mwisho kwa mfululizo wa makala zangu hizi.
Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com
Barikiwa Sana!
Semper Fidelis,
Yes,
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni