Jumatano, 19 Oktoba 2016

JAMBO LA NANE (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA NANE
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 8.

8. JAMBO LA NANE: MAISHA YAKO YA KIJAMII UMETENGENEZEWA (YOU HAVE A SORT OF AN INBRED SOCIAL LIFE)

Leo nataka nianze kwa kusema kitu fulani.

Kuna siku nilisoma Biblia ikawa inaongelea habari za watu wanaitwa MATOASHI. Mathayo 19:12 pale. Rabbi (mwalimu) mmoja wa Kiyahudi aitwaye Yesu, ajulikanaye pia kama Kristo, akieleza hilo jambo pale. Kwamba duniani kuna #matoashi. Akafafanua kuwa kuna matoashi wa aina tatu:
i.) kuna wa KUZALIWA hivyo,
ii.) kuna matoashi WALIOFANYWA kuwa matoashi na watu wengine
na kuna matoashi WALIOAMUA kuwa matoashi kwa ajili ya Mungu.

Nikapata idea moja kuwa kuna mambo mengine yanakuwa yalivyo katika maisha yetu kwa sababu za our PAST. Historia. Asili yetu nk. Kuna ambayo yanakuwa kwa sababu ya watu wenye control na maisha yetu. Na kuna mambo yanakuwa yalivyo katika maisha yetu kwa sababu ya maamuzi yetu binafsi.

Kwa premise hiyo basi kuna watu wanaajiriwa kwa sababu ndiyo kitu kilicho asili yake. Ndiyo MINDSET yake ilivyojengwa toka utoto ikiwezekana toka akiwa tumbni kwa mama alikuwa akinenewa ajira akipiga teke mama anasema huyu atakuwa polisi huyu au wengine huyu atakuwa mwalimu atufundishie Jamii au huyu atakuwa hiki na kile. Katika formative years zake akiwa mtoto anaona maisha kwa jicho la ajira. Wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, wengi wao au wote wakiwa wameajiriwa kwa namna fulani. Alipoenda shuleni walimu wanaongelea kusoma ili kupata kazi nzuri. Zingine wanamchagulia. Wewe utafaa kuwa meneja wa benki. Wewe mchafu mchafu utakuwa fundi "makenika". Akirudi likizo watu hata majirani wanamwambia "Soma mwanangu, someni mpate kazi mtusaidie sisi wazee wenu hatukusoma" wanampa mifano ya vijana ambao hawakusoma na wapo wapo tu hawana ajira jinsi walivyo hawana mwelekeo. Na wanamwambia kuhusu unaona mtoto wa fulani amesoma amewajengea wazazi wake nyumba nzuri. Soma usichezee elimu. Kama ni wakristo watampa na neno la Biblia "Mshike sana elimu usimwache aende zake" ambalo wengi hasa wanamaanisha FORMAL education.

Huyu mtu hata akija kufika Chuo Kikuu utakuta anachagua kozi ambazo zina AJIRA. Kweli anachagua mwenyewe. Hakuna anayemchagulia. Lakini mindset iliyoko nyuma ya hiyo choice ilijengwa siku nyingi bila yeye kujua. Anafikiri kuwa ana freedom kwa sababu kachagua mwenyewe kusoma LAW. Anachagua kozi ambazo zinaitwa "nzuri". Kozi ambazo "ZINALIPA" (mshahara mzuri). Kama unasoma hapa na ulisoma chuo hebu kuwa mkweli hukuchagua kozi unayoweza kupata AJIRA kirahisi? Kuna binti namfahamu toka akiwa mdogo sasa ni binti kashamaliza chuo ameajiriwa. Ninawajua wazazi wake. Ni wahandisi wabobezi na watoto wao wawili kati ya watatu waliwajengea mazingira ya kuupenda uhandisi na kuona ni kipimo cha kuwa KICHWA DARASANI. First born wao ambaye ndo huyo ninayemwongelea ameshamaliza UDSM COET now ameajiriwa serikalini kama Mhandishi huko Kanda ya Ziwa. Na toka akiwa binti wa shule ya msingi alikuwa akisema anataka kuwa mhandisi kama baba yake. Ukimuuliza kwa nini. Anasema my dad is very bright and we have a good life. Ni kweli walikuwa na maisha fair. Not bad. Middle class family. Chakula kipo. Ada hazichelewi tena English Medium. Toka utoto wanafundishwa hisabati na kiingereza na baba kila siku. Huyu binti alikuwa anasoma novel ngumu ngumu kama COSA NOSTRA akiwa darasa la tano. Fikiria hilo. Hesabu za darasa la saba ameshazikava akiwa STD V. In fact alirushwa kutoka darasa la sita kwenda la saba na mtihani wa taifa akiongoza shuleni kwako akiwa kasoma miaka 6 wenzake 7 yote. Yeye na wadogo zake darasani walikuwa wa kwanza katika madarasa yao wote watatu. Walikuwa level za madarasa tofauti. Na sasa ndoto imetimia kwa huyu wa kwanza. Amekuwa mhandisi ameajiriwa serikalini. Kama baba na mama. Mindset yake toka utoto iko hivyo. Hili ni kundi la kwanza. Yani ndo asili yake. Ndo hapa wanasema mtu anaweza kusoma sana lakini MINDSET yake ikiwa imeshikilia jambo fulani hata ungesema nini. It's a RIGID mind. Imeshakaa hivyo miaka mingi. Hicho ndo anachokiona yeye. Imeshakuwa ASILI yake bila yeye kujua. Haoni option yoyote nyingine. Baba na mama wamekaa serikalini na hawajawa na changamoto ndogo ndogo hizi. So why mtoto aone shida.
Waajiriwa wengi kuajiriwa kwao ni issue ya MINDSET tu. Ni kundi la watu ambao bila kujua wametengenezewa mazingira ya kuwa na vision fulani specific. Toka siku nyingi.

Kundi la pili la waajiriwa ni la wale ambao kuajiriwa ilikuwa siyo saana kwamba aliandaliwa hivyo kifikra ila huyu aliwekewa ulazima fulani wa kuajiriwa. Ametoka familia ya wazazi wanaoitwa HELICOPTER PARENTS.
Mfano kutafutiwa kazi anakuta ipo tayari tayari. "Tushakutafutia kazi mwanetu, keshokutwa unaenda kuanza, usije ukatuangusha huko". Ukitaka kuwaambia kuwa ungependa ufanye mambo binafsi unaulizwa wewe ndo unalipa kodi hapa? Unajua tumegharimika kiasi gani kukusomesha huko Malaysia na kwingineko? Ukitaka kuongea utasikia:  Nyie watoto wa siku hizi hamna ADABU? Mzazi anaongea na wewe unaongea. Sasa aina hii ya mazingira huchomoi. Lazima uende kuajiriwa na usiwaangushe wazazi. Unataka kuachiwa LAANA? Washakwambia wanategemea wewe ndo uje uwe meneja au Mkurugenzi siku moja so usiharibu kazi. Kundi hili la waajiriwa ni kundi la watu ambao wanaishi kwa VISION za wazazi wao. Yule binti mhandisi ana mdogo wake wa kiume anakaribia kumaliza elimu ya juu. Wazazi washaanza kumtafutia kazi. Asije kuhangaika. Internship wanatafuta wazazi. Ajira wanaandaa wazazi.
Wasomi wengi wangetamani maisha yawe hivyo. Straight line life. What a life!

Kundi la tatu ni wale ambao WAMEAMUA wenyewe kuajiriwa. Siyo mindset wala siyo suala la wazazi kutaka na kufunga na kuomba aajiriwe bali yeye kapenda. Mara nyingi hawa wanaajiriwa kwa muda au just for the sake of it. Siku akiona vipi anaondoka kwenye ajira kufanya vitu vingine. Hawa ni wenye vision binafsi. Na anaweza kubakia kwenye ajira maisha yote bila influence ya mtu kwa sababu ndivyo alivyoamua. Ndo vision yake. Kama wale matoashi walioamua wenyewe kuwa mimi nataka niwe TASA nisizae wala kuoa kwa ajili ya Mungu. Vision binafsi. Siyo influence ya mtu wala ya wazazi.

Sasa kama wewe ni mwajiriwa ni muhimu ukajitathmini. Uko kundi gani katika makundi hayo matatu. Mada ninayozungumzia mimi katika Makala zangu hizi ni JINSI ILIVYO NGUMU KWA MWAJIRIWA YEYOTE KUPATA UHURU WA KIPATO. Kwa maana nyingine likija suala la kuingiza kipato mwajiriwa anazaa. Hakuna shida kabisa  Lakini likija suala la uhuru wa kipato mwajiriwa ni TOASHI. Hawezi kuzaa.
Castrated.

Ndo nasema jiulize wewe ni aina gani katika hao watatu.
Umefanywa hivyo toka umezaliwa (uliumbwa na kukua ili uajiriwe)?
Au ulilazimika kuajiriwa kwa sababu ya watu kwenye control na maisha yako?
Au umeamua tu kuwa hutaki kuhangaikia uhuru wa kipato kwa sababu tu "siyo ishu". Au unazopata zinatosha umejenga una magari unaishi vizuri nk watoto wanasoma Intaneshno Skul so inatosha huhitaji kuwa na "tamaa" ya mahela mengi!
Comfort zone.
Which one are you?

Au wewe hujui wewe ni aina gani ya mwajiriwa katika hao. Unatiririka tu. Uko bize from Monday to "THANK GOD IT'S FRIDAAAAAY!!!"


Nimeona niweke hizo categories ili kama umeajiriwa au unataka kuajiriwa ujue WHY? Labda itakusaidia. Na utaelewa zaidi mambo ninayofundisha hapa. Usije kujikuta unakubaliana tu na mimi hata hujui why au unatofautiana na mimi bila kujua why.

Sasa naendelea na sababu ya nane inayozuia mwajiriwa kufikia UHURU WA KIPATO.

Ukiacha sababu saba ambazo nimekwishazisema toka mwanzo.. Maisha ya mwajiriwa yana mambo mengi ambayo si maamuzi yake na mengine ambayo si maamuzi yake.

Mojawapo ya jambo ambalo hana maamuzi nalo ni social life yake. Maisha yake ya kijamii. Asilimia kubwa ya muda wa wajiriwa wengi hutumika katika ESSENTIALLY mazingira yale yale, na watu wale wale, katika working field ile ile, wakizungumzia zaidi mambo yale yale. Kama uliwahi kwenda kutembea gerezani utaelewa kuwa kuna ukuta. Na watu ni wale wale zaidi. Ukiacha wachache wanaokuja kutembelea gereza kusalimia wafungwa, kufundisha dini, kuwatia moyo wafungwa nk.

Ni vizuri ukakumbuka kuwa katika viumbe vyote duniani ni binadamu peke yake ambaye aliumbwa ku-socialize. Maana yake ni kwamba your social life as a human being ina maana kubwa sana katika maisha yako kuliko hata your financial life ambayo ndo ninaiongelea hapa. In a point of fact ni kwamba your financial life inabebwa kwa kwa kiasi kikubwa na your SOCIAL LIFE. Wanasema "YOUR NETWORTH IS EQUAL TO YOUR NETWORK". And vice-versa. Sasa katika setup ya ajira ndo nasema UMESHATENGENEZEWA SOCIETY ya kuishi nayo kila siku bila kupenda kwako.
Unalazimika kukubaliana na hiyo social life. Uwe unawapenda huwapendi ndo hao hao. Wawe ni watu wenye mawazo mazuri kichwani au wawe ni wanaowaza vitu vidogo vidogo ndo hao jamii yako.

Na waajiriwa wengi network yake ni hasa hasa watu wa pale kazini kwake. Watu wa kazini kwake ndo wanajua birthday yake ni lini siyo majirani. Kama umeajiriwa jiulize kati ya labda majirani zako na waajiriwa wenzako nani wanajua zaidi ishu zako? See? Network yako imekuwa ile unayoishi nayo siku nzima. Kuishi kwa kutegemea network ya kazini kwako tu ni sawa na kuishi kwa kudhani kwamba kupata marafiki 5000 Facebook inaonyesha una impact kubwa. Nilisema mwaka jana kuwa Ukurasa Facebook wa Mhe. January Makamba ulikuwa na Likes nyingi kuliko wa Mhe Magufuli. Lakini aliyepitishwa akawa JPM. Impact. Hata sasa Diamond Plutnumz ana watu wengi Fb kuliko Mohamed Dewji. Ni kweli kuwa ana impact zaidi ya MO? Au network ya diamond in life na ya MO vinafanana? Likes za Facebook siyo Network Yako halisi. Hao ni FANS tu. Wanaokubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo tu kwa sababu zao. Network yako halisi ni nje ya mitandao hii. Watu wanajua ndoto zako na wanaweza kukupa mawazo yao wakati wowote. Unaoweza kuwauliza siri za mambo yao mfano mafanikio na wakakupa bila kukuficha.

So network yako ya kazini inaweza kuwa ya watu maarufu mno. Lakini kwa kuwa ni ya kutengenezwa huwezi kufikia Uhuru wa Kipato. Lazima utengeneze MWENYEWE network mpya!

Kuna watu network yake kwa sababu ni ya wafanyakazi wenzake wa BOT anadhani kwa kuwa ni BOT basi atafanikiwa kiuchumi based on that network only. Unapaswa kujenga uwezo wa kufahamiana na kukutana na watu wengi tofauti ujifunze vitu tofauti ambavyo ndo vitakusaidia kufikia malengo ya kuwa huru kifedha. Kuna watu hapa watasema "aaah kwani si hata hapa nakutana na wateja tofauti tofauti". Siongelei wateja. Nimesema hata gerezani kuna wageni wanaenda kila siku. Mi naongelea uwezo wa wewe kwa kuamua kwako kukutana na watu katika mazingira ya nje ya ofisi yako na kushare vitu kuhusu maisha nk wakati ambao unataka kukutana nao ili kujifunza vitu tofauti. Ni vigumu mwajiriwa labda wa Wizarani kunetwork na Waziri. Lakini ni rahisi kwa mtu asiye katika setup ya ajira kunetwork na waziri bila hata woga.

Waajiriwa wengi kwa kuwa ameshasocialize kazini kwake kwa masaa 9 au 10  akili imejaa mafaili na mawazo ya kazi za kesho hana muda wa kusocialize na watu wengine tena anahisi imetosha. Kumbe hajui Uhuru wa kiuchumi unakuja kwa mkusanyiko wa mambo mengi ikiwemo kuwa na watu kwenye network yako ambao either wako level hiyo au wamekaribia au angalau wanaelekea huko.

Wakati nimeajiriwa miaka 7 hivi iliyopita kulikuwa na program niliyokuwa nahudhuria kila Jumatano jioni saa 11 hadi saa mbili usiku yenye lengo la kukutana na watu wengine waajiriwa na wasio waajiriwa kubadilishana mawazo. Bwana Anthony Luvanda anaweza kuikumbuka pale HOLIDAY INN (sasa panaitwa SOUTHERN SUN). Kuna watu waliandaa hiyo program. Tulijengewa mazingira ya kufahamiana na watu wengi tofauti na kujifunza vitu tofauti. Lakini wenzetu wengi walikuwa hawaji kwa sababu "wamechoka" japo ilikuwa bure na chai/maziwa/kahawa/bites za bure kabisa. Siku moja bwana mmoja kutoka Uingereza akasema nchi za Asia watu wanatafuta sehemu kama hizo na wanalipa kiingilio kujifunza na kusocialize. Lakini akasema anashangaa huku ukiweka kiingilio watu waje kusocialize na kujifunza hawatakuja. Na hata ukiweka bure pia hawaji. Hasa waajiriwa.

Hili suala liliniingia sana kichwani. Na naweza kushuhudia kuwa idadi ya watu niliokutana nao kusocialize katika miaka yangu miwili ya ajira ni ndogo kuliko watu niliosocialize nao ndani ya miezi sita tu ya kwanza baada ya kutoka katika ajira. Nikitazama leo mambo ambayo nineshajifunza kwa watu mbali mbali waliofanikiwa maishani tayari ni mengi na makubwa na kuna wakati nawaza nisingekutana au kuwatafuta baadhi yao ningekuwa sijui vitu vingapi.

Siku hizi watu walioajiriwa pamoja wana magroup ya WhatsApp. Wanajadili essentially ishu zile zile. Social life ile ile inaendelea online. Network extension. Not expansion. Don't extend your network.
EXPAND it!

Kama umeajiriwa na ndoto yako siku moja uwe na Uhuru wa Kipato. Usiwe mtumwa wa kipato basi jitathmini kwanza wewe ni aina gani katika yale makundi matatu. Kisha acha kutegemea network ya waajiriwa wenzio. Be bold enough to expand your network. Ujifunze kwa wengine. Mazingira ya kuajiriwa yanakupa uwezo wa kuextend network yako tu. Kama tu simu zenye extension.. Network ni ile ile. To attain financial freedom you must FIRST expand your network.

This is a business school nakupa. Unaweza kuchagua kutilia maanani au kuignore.
It's your choice.

Leo niishie hapa.

Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoandika kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 8 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado zingine 2 tu.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 8 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 9.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis People,

Yes,

Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni