Jumamosi, 21 Januari 2017
HOW TO TURN WATER INTO WINE. (JINSI YA KUBADILI MAJI KUWA DIVAI)
Nashukuru Mungu kuweza kuwa nanyi hapa leo tena, ni neema ya Mungu. Hope mpo salama. So leo tujifunze pamoja something very important.
Kwanza nianze kwa kusema kuwa kosa mojawapo katika maisha yako utakalolifanya ni kuishi maisha yako yote hujawahi kusoma Biblia tena kwa USAHIHI siyo kwa ajili ya kuendea mbinguni tu bali kwa ajili ya kujifunza mambo muhimu mbali mbali kuhusu maisha (of course ikiwemo hilo la mbingu). Hii haijalishi unawaza nini kuhusu Biblia au wewe ni dini gani. Nasema hivyo kwa sababu kama utajifunza kitu katika makala yangu hii ya leo basi ujue kuwa unahitaji kuanza kusoma hiki kitabu.
Sasa tuendelee..
Sasa bana.. Kwa miaka mingi toka niko mdogo nimesikia mara nyingi sana kuhusu huu muujiza wa Yesu. Unarekodiwa kuwa muujiza wake wa kwanza in public. Na hata nilikuwaga sielewi. Na wengi hawaielewi lessons mbali mbali zilizo katika story hii inayopatikana John 1:1-11.
Leo naomba tushirikiane kujifunza machache tu ya kukusaidia kuondoka katika hali uliyonayo. Kila mtu ana hali fulani maishani mwake asiyoipenda iwepo either kwake au katika maisha ya watu anaowapenda. Kama huna wewe umeshakamilisha kila unalotaka duniani basi jiandae kurudi kwa muumba wako any time. Sasa kwa makala hii jambo unalotaka ndiyo WINE/DIVAI yako. Ila lazima ubadili maji kuipata.
Unataka kuolewa, kuoa? Watoto? Unataka kufanikiwa kifedha, unataka ajira, unataka nini? Chakula cha kutosha ghalani mwako? Unataka kuwa kiongozi wa nchi au kampuni kubwa? That's your wine.
Unataka kujenga biashara kubwa ya kuigwa mfano? That's your wine.
Unataka kusaidia familia yako iondokane na umaskini kabisa? That's your wine. Unataka kutatua tatizo la michezo Tanzania kutofika mbali? That's your wine? Unataka kumiliki kampuni kubwa ya usafiri wa anga duniani? That's your wine.
Maji ntakwambia ni nini. Be patient...
So baada ya kujifunza upya kuhusu huu muujiza nilijifunza mambo YAFUATAYO ambayo ndo teknolojia yenyewe ya kubadilisha maji kuwa divai:
1. DEALING WITH NEGATIVE PEOPLE
Aisee nilikuwa sijajua hivi vitu na naomba ujue kuwa hakuna kitu kinachokwamisha mafanikio ya watu wengi kama kuruhusu NEGATIVITY kichwani mwako. Huyu mtu anaitwa Yesu alikuwa strict kweli kweli when it comes to that. Hakuwa na maskikhara haijalishi anayeleta negativity ni mama mzazi, mwanafunzi ambaye atakabidhiwa uongozi baadaye, au ndugu wa rafiki yake kipenzi. Kumbuka Simoni Petro alipomkemea Yesu asiongee kuhusu kifo chake Yesu akamkemea back kwa kumwambia "Rudi nyuma yangu shetani". Hakutaka kabisa kuwaza negative. Hata rafiki yake kipenzi alipofariki akaletewa habari alijibu "HAJAFA... AMELALA TU". See? Very positive.
Sasa tuone hapa Kana ya Galilaya. Mama yake Yesu kaalikwa. Na Yesu na wanafunzi wake wamealikwa pia kivyao. Kinywaji kimeisha. Yesu anajua. Na anajua cha kufanya. So hakuhitaji mtu wa kuja kumwambia kuhusu kukosekana kwa DIVAI. Sometimes watu wanaukuja kukuambia habari mbaya kuhusu maisha yako au maisha ya uwapendao huja kwa nia inayoonekana machoni kuwa njema lakini kumbe wanaweza kuwa wanatumika kukuyumbisha kiimani. KUMBUKA. Narudia, KUMBUKA kuwa huhitaji negative statements nyingi ili uishiwe imani au ushindwe kuachieve kitu unachokitaka. Sentensi moja tu inawezekana ikakumaliza wewe na watu wako wote. Eva aliposikia sentensi fulani fupi tu kutoka kwa nyoka (nyoka akiwa ameingiwa na shetani) Eva akala tunda.. Sentensi fupi tu.... "Hakika hamtakufa..." (Mwanzo 3:4). Eva wa watu akaamini kumbe hakuna kufa. Afu kumbe kuna kufanana na Mungu. Akakosesha kizazi kizima cha binadamu. Yesu alikuwa anajua UMUHIMU wackutokaribisha NEGATIVITY kutoka kwa mtu yoyote. Ndo maana mama mzazi alipokuja kuleta habari mbaya. Negative. "Hawana divai". Biblia ya kiingereza inaonyesha alijibu kwa ukali kidogo. "Woman, what have I to do with thee?..." (John 2:4). Halikuwa jibu la kukosa adabu but jibu la kuonyesha strictness. Petro aliitwa shetani katika mambo ya aina hiyo. Lakini huyu ni mama. Ila ni kama aliambiwa " mama niache najua". "Tuna nini mimi nawe?"
That's how you treat negativity. Reject it on the spot. Mtu akikuletea habari za kukwambia nchi ina matatizo, nchi ina njaa, nchi ina ukame, nchi haina ajira, nchi hiki nchi kile. Nchi hii watu hawana hela. Mtaani hali ni ngumu. Afu na wewe ukashabikia.. Ujue you will NEVER get your wine. I'm telling you. Achana na habari za kusikiliza negative people. Kuna watu na pages za kuunfollow na kuna watu wa kublock. They're are simply too negative. Be like Jesus. "Tuna nini mimi na wewe?" ina maanisha pia "What DO I HAVE IN COMMON WITH YOU?". When you're positive you have nothing in common with negativity of any kind.. Mtu akikwambia aisee unajua hali ni ngumu mwambie "Kati yangu na wewe kuna kitu tunafanana?". Ifikie mahali mtu anakuja kukuelezea shida na matatizo akifika kwako anaahirisha. Ukistudy watu wengi walikuwa wanamwambia Yesu matatizo. Mwanangu anaumwa. Rafiki yako amekufa. Hawana divai. Tunaangamia (na dhoruba). Hawakuona kuwa kuwa na Yesu was a solution itself. Watu wanakwambia hakuna ajira
Watu wanakwambia Biashara ni ngumu. Pesa hakuna. Na wewe unasikiliza. You will never accomplish what you want. Lazima ifikie hatua unakataa kusikiliza. Hata kama ni mke/mume au mzazi. Mwambie hamfanani wala hamuwazi the same.. You have nothing in common. Tuna nini mimi nawe. Yesu hakuwahi kuentertain habari kutoka kwa mama toka siku hiyo. Yani alimuunfollow. Yes. Kuna wakati Yesu anahubiri akaambiwa mama na ndugu zako wako nje. Nadhani jibu lake unalikumbuka. Mama na ndugu zangu ni hawa wanaonisikiliza
. Ameshaunfollow.. That's why wakati anakufa akamkabidhi kwa Yohana. Mama tazama mwanao. Biblia ya Kiingereza inasema WOMAN BEHOLD YOU SON
.
Hakutaka kuwa tied na mtu kisa ni mzazi wakati anaweza kumkosesha bila kujua. Unajua wengi Yesu hawamwelewi. Reject negativity completely.
That's step one.
2. IDENTIFY YOU WATER.
Cha pili ni kuwa ukishakataa negativity haitoshi. Wine haiji bila "MAJI" right. So you have to identify your "water". Raw materials. Nini kinapatikana hapo ulipo wewe ambacho kinaweza kukupa what you want. Wengine wenu MAJI yako ni kipawa chako. Wengine maji yako ni idea fulani unayo. Wengine wenu maji yako ni watu wanaokuzunguka majirani nk. Wengi wa vijana wanaohangaika na ajira elimu hiyo hiyo waliyonayo ndo MAJI yenyewe. They have the raw materials. Kila mtu mwenye shida ana some kind of raw materials ya kubadili kuleta DIVAI anayotaka. Find your raw materials. Hii huwezi kujua bila kuwa mtu wa kukaa peke yako kuongea na Mungu na kutafakari neno la Mungu na kutafakari UKUU wa Mungu na kutafakari ambayo Mungu keshakutendea. You must set aside muda wa kutosha ina a day at least 1 hour wa wewe na Mungu wako tu. Utaletewa majibu tu ya kujua what's your WATER. Be sensitive to God's voice wherever you are. Yesu alikuwa katika sensitive mode hiyo wakati mama mzazi analeta habari za hakuna divai. Yesu hakutaka mind yake kuyumbishwa na mtu yoyote hasa kwa vitu ambavyo tayari anajua na anafanyia kazi. Tatizo wewe mind yako haitulii. Unayumbishwa na kila mtu. CCM wakisema hivi unayumbia huko Chadema wakisema hivi unayumbia huko. Hutaki kukaa na kuwaza kama wewe. Ifikie mahali utambue RAW MATERIALS zako on your own.. Usisubiri CCM au UKAWA wakupe solution ya nini unahitaji kutimiza malengo yako.. I'm telling you if you look around kuna MAJI ya kutosha kupata DIVAI ya kutosha. Hivyo ndo Yesu alivyokuwa anawaza. Wakati mama anaona LACK. Yesu aliona PROVIDENCE. Huyu anaona ukame huyu anaona evergreen. Get my point? Ukiona watu wanaongelea UKAME na wewe unaona UKAME ujue kwanza huna imani ndani yako na pili umeshaambukizwa negativity ya kutosha hali yako kiroho na kifikra ni mbaya. Wanaoweza kumwona Mungu ni wanaoweza kuona DIVAI katika vyombo vitupu. And I'm saying lazima uitrain mind yako kukagua mazingira yako ili kuona MAJI. Raw materials. Huwezi kufika hapo kama hujablock baadhi ya watu Facebook na kuunfollow baadhi ya pages na groups. That's why kila unayesikia analalamika. Negativity imejaa vichwani. Wengi wameshindwa kuona anything good anymore. Wanawaza tu HAKUNA hiki, hakuna kile. Hakuna mvua
hakuna ndoa za kweli, hakuna elimu, hakuna ajira, nakutana na vijana wengi wananambia sina mtaji, wengine wanasema hakuna mikono, hakuna dawa hospitali, hakuna hela mtaani, hakuna maua, hakuna wateja. Hawaangalii around. Kumbe kuna maji ya kutosha kujaza mabalasi. Kuna solution hapo hapo ulipo. Block some negative people wanaofanya akili yako isifocus kwenye kuidentify your RAW MATERIALS. Yes. Kataa. Sasa wewe una entertainment eti ooh this is my bae. Your bae? Fine, but you'll NEVER get your wine. Yesu hakufanya kitu cha ajabu. One alikataa negativity. Pili alifocus kwenye raw materials. Umenielewa?
3. TAKE ACTION BY TOTAL FAITH.
Ukishajua MAJI yako ni nini. Just take action.. God is waiting to see you take that step. Sikia. Tragedy kubwa ni kuwa wengi wanaomba Mungu afu wanasubiri majibu. Badala ya kutake action.. Jesus took action.. Akawaambia watumishi "FILL THE WATERPOTS WITH WATER". Ok kujua raw materials tu haitoshi unapaswa kujua wapi ipelekwe. Na njia gani. Haya yote utayajua kama tu wewe ni mtu wa kutuliza kichwa. Acha kuyumbishwa. Tuliza kichwa hicho. Wengine vichwa vyao havitulii hata akilala kichwa kinazungukwa na majinamizi na vikatuni katuni tu. Hawezi kukaa one hour tu aseme natuliza kichwa. Waajiriwa wengi wakipewa likizo badala wakatulie kuwaza wanaenda kushinda kwenye TV au baa au kwenye miradi. Culture ya kutuliza kichwa haiko. Ndo unakuta raw materials ziko na mtu ni positive lakini hawezi kubadili MAJI KUWA DIVAI sababu kichwa hakijatulia. So unapaswa kutuliza kichwa na kutake action kwa imani. Yesu aliwambia JALIZENI MABALASI MAJI. Wakajaza hadi juu. Nice. Kisha Akawaambia TEKENI MKAMPELEKEE MKUU WA MEZA. Yani action after action. Hakuna kusikilizia. Mungu anataka hivyo.
Umekataa negativity
Umetambua raw materials zako
Then take action non stop.
Hapa wengi husita.. Keshajua ana uwezo wa kuongea vizuri badala akaombe kazi kwa imani anasita. Keshajua anaweza kuongea na watu badala akaanze biashara kwa imani anasita. That's why ni wachache wanapata divai. Wachache sana wanabadili MAJI KUWA DIVAI.
Je ungependa kuwa miongoni mwao? Ujumbe wangu kwako ni huu.
Achana na negative people. Mtakutanaga mbinguni. Kama watakuwepo.
Then tambua MAJI yako ni nini?
Then take action.
Write that book.
Compose that song. Hujiulizi huyu kijana anawazaje kichwani?
So take action..
By faithCall that customer
Talk to that potential partner.
Start that business.
Write that speech
Write that proposal
Identify your WATER See the WINE in the water then take action.
That's how to turn water into wine.
Unajua hakuna aliyejua maji yamebadilika saa ngapi exactly kuwa divai except Jesus and God in heaven. Hivyo hivyo watu hawatajua lini exactly ulibadilika kichwani except you. Watu hawatajua lini exactly account yako ilianza kusoma 6 figures except you. Watu hawatajua lini exactly maji yako yamebadilika kuwa DIVAI except you. Be bold. Block all negativity. Permanently. First things first. Ukiweza hilo mengine ni rahisi tu.
Nikikuona unalalamika tena ntajua tu hujajua kuhusu somo la maji na divai. Najua kuwa UMEFUNGA NDOA NA NEGATIVITY na hauko tayari kuandika talaka. Ntakuacha kama ulivyo.
Be bold. Turn your water into WINE. It can be done.
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania.
East Africa
+255788366511
www.andreamuhozya.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni