Jumamosi, 14 Januari 2017

UNATAKA MAFANIKIO, SAWA LAKINI UNALIMA MAHINDI AU MINAZI?



Kwa neema ya Mungu wa mbingu na nchi nimepata wasaa wa kushare na nyinyi tena jambo muhimu.

Nimebarikiwa kukutana na watu wengi mno hasa vijana kila siku na kubadilishana mawili matatu kuhusu mafanikio. Na nimejifunza kuwa watu wengi hawafikii mafanikio wanayoyataka sababu wanataka KULIMA MAHINDI.

Wanataka kuvuna haraka haraka so hawataki KULIMA MINAZI.

Kila anayetafuta mafanikio ni MKULIMA.  But kuna watu wamechagua kulima mahindi na wachache wamechagua kulima MINAZI. Nadhani kwa kuangalia mazao niliyoyataja unaweza kuona tofauti kubwa ipo zaidi katika inachukua muda gani kuja kuvuna. Mahindi ni fasta tu.....lakini minazi! Weeee.....  Inabidi uvute pumzi kweli kweli.

So nimejifunza kuwa ukitegemea kilimo cha mahindi utavuna haraka lakini ukishavuna itabidi ulime tena. Au siyo? So hiyo ndo inakuwa life. Ila minazi utasubiri sana.  But ukianza kuvuna hulimi tena. Ujue Mungu bana ana vitu amazing sana ukitafakari. Sasa the best way for you in life ni kulima minazi. I believe hadi hapa umeshaelewa kuwa majina ya mazao nimeyataja tu kama kiwakilishi cha njia utayotumia kufikia mafanikio yako.  Kubali kuinvest a lot of time. Kama umewahi kuangalia video ya CHINESE BAMBOO utakuwa unanielewa vema.  But kama hujaitazama nakushauri stop kwanza kusoma huku chini kisha uingie hapa https://youtu.be/2nFDmrLGgYM uitazame ni fupi tu. Kisha utakuja uendelee. Tutaenda sawa mno.

Now...
Watu wengi hawataki kuinvest muda kwa kuwa wanataka wafanikiwe WAO. Kuna a selfish motive ndani ya kutaka kwao mafanikio. Na hata akificha if he/she sticks around long enough itadhihirika tu kwa kukosa kwake subira. Kufanya jambo linaloleta matokeo baada ya muda mrefu mno ni jambo ambalo wengi hawataki. Na kwa kuwa sasa tunaishi katika ulimwengu wenye Instagram na kufesibuka kwa sana mtu akiona picha za wenzake wanavaa vizuri vizuri anatamani kuwa kama wao haraka haraka. So kama wameajiriwa anatamani kuajiriwa fasta. Ndo maana waajiriwa wengi wana magari (of course ya mikopo) sababu kubwa ni hii "comparison fever".  Nimeielezea kwa kina sana in my upcoming book. Lakini kama unataka mafanikio ya kudumu hupaswi kamwe kujilinganisha na mtu.  Unapaswa kuangalia PLAN ZAKO (kama unazo that is) na kuzifanyia kazi.  Unachoweza kufanya ni kuangalia waliofanikiwa walipita wapi kisha ujifunze kwao na kuboresha. Lakini usitake kuwa Bakhressa leo kwa miaka mitano.
It takes time. Bhakhressa hajaanza "kulima"  mwaka juzi.
Long time kitambo.
It took him time.
Being Dewji took time.
Being Mengi took time.
Being Dangote took a very long time, and many a sleepless night.
Being Warren Buffet took time.
Being a really successful YOU takes time. A long time. Ni kama kulima Chinese Bamboo. Si umeshaicheki hiyo video? Kama bado hebu icheki.  Seriously.

Winning an election especially for the first time as a party takes a long time.

Talking of which najifunza mengi kwa vyama vya upinzani hapa kwetu Tanzania. Jinsi ambavyo, kwa mawazo yangu madogo, ninavyoona wanahangaika kulima mahindi badala ya kulima minazi ambayo ndo itawafikisha mbali.

Mfano:

Niweke WAZI hapa kuwa suala la upinzani kuchukua dola ni jambo jema mno kwa ustawi wa taifa letu kwa ajili ya kuencompass mawazo mbadala ambayo mengi huonekana kama hayafanyiwi kazi na chama tawala.  Huo ni mtazamo wangu na siyo sababu nataka kufurahisha mtu. Ni jambo jema,  but I like to say siyo lazima ENDAPO mawazo yao yatafanyiwa kazi na taifa likaendelea vizuri. And that can become a bigger problem kwa upinzani kama CCM ikiboresha say hata 70% tu ya issues.

HOWEVER shida ya vyama vya upinzani ninayoiona mimi ni kuwa mpaka sasa hawataki kulima minazi wanataka mahindi.  Bila kujua kuwa mkulima wa mahindi akivuna lazima alime tena msimu ujao bali mkulima wa minazi akilima mara moja tu kinachobaki ni kuvuna. Mfano Sasa hivi ukitazama upinzani wanawaza 2020 washinde uraisi.  Mahindi. Wakishindwa "tumeibiwa kura". Hawaonagi wapi wamekosea.  Haya,  ikiisha hiyo watawaza 2025. Which mpaka sasa ni ngumu kwao. Coz kama wataendelea kupresent Mhe Lowassa, au Mhe Sumaye as wagombea wao basi wawe na uhakika wa kushindwa kama CCM itamweka tu hata Nape au Makonda. (I believe ccm ina a surprise package for 2025 yuko anapikwa kupokea mikoba ya Magufuli) See? That's the difference.

Upinzani wana nani anapikwa now? Wanapaswa wapike mtu au watu for a long time. Minazi. Hivi mfano wangepika mtu kama Mnyika for say, 30 years toka alipokuwa 25 years old mpaka afike 55 years old akiwa anaandaliwa tu kuwa raisi every single day for 30 years wangeshindwa kuiondoa CCM kama wana hiyo GOAL? See,  strategies hizo hazionekani that's why wanatafuta mtu ambaye ni maarufu tayari (ready made product) kama Lowassa ambaye kajijenga kivyake or rather and worse kajengwa na ccm hiyo hiyo. Ccm ina akili sijawahi ona. Imeinvest kwa lots of youth muda mrefu. Wapinzani hawataki kuinvest for the long haul. Wanawaza 2020 eti.  Na 2025.  Ukiwauliza nani anagombea in 2040 usikute hata idea hiyo haijafikiriwa. Sasa kama plan za miaka 25 tu mbele hakuna mnatamani nchi ili muipeleke wapi? They've already failed in 2025. I assure you. Trump alijiandaa for a long time and hakuna aliyejua kuwa atashinda nomination ya GOP.  That's why kina Obama na Clinton waliishia kumkejeli na kudharau wakati yeye kisha study kuhusu ELECTORAL COLLAGE for many years kimya kimya.
Kuishinda ccm unahitaji surprise package ya hatari ambayo wapiga wakiiona wanasema wow, huyu sasa ndo tulikuwa tunataka. Inahitaji kulima minazi. Waangalie mbali aisee. Tatizo watu wanataka now now. Kilimo cha mahindi.

That's why hawana key ideas wanazosimama nazo bila kutetereka.  Utasikia ufisadi.  Saivi kimya.  Maksi zinaondoka.  Saivi unasemwa udikteta na uonevu mara raisi anajifanya mtakatifu mara serikali imekula rambi rambi mara serikali imenyima watu msosi wakati wana njaa. Mara ruzuku za CUF.  Yani HAKUNA central idea ya kusimama nayo hata katiba ni kama inapotezewa sababu ya siasa za matukio. Kwa nini wasiseme okay kuna tetemeko but issue central ni katiba hatuhami mpaka ije. Au Okay raisi kaja na style tofauti ya uongozi but tunasimama na katiba. Hakuna central issue. But wanakuwa wa matukio sababu wanataka wewe RELEVANT bado kama CCM.  Ndo unasikia ukuta, ukiisha inakuja kata funua,  maneno yenyewe ya mtaani kabisa.  Kata funua ndo nini kwa watu serious wanataka nchi. Wameshindwa kuja na phrase inayoeleweka kweli? Eti kata funua.  Hata nayo haiwi communicated kwa wapiga kura ieleweke inamaanisha nini? How can God give you authority ya kuongoza watu wake?

Kama upinzani ambao by the way una maanisha chadema, kama wanataka kushika dola wajipange  for a really long time.  Wakubali kilimo cha minazi. Otherwise basi maneno ya "Profesa" Jay kwenye wimbo wake Bongo Dar es Salaam yanawahusu: "..mtangoja milele na "mtakufa" bila kelele kama walivyokufa wafuasi wa kibwetere".  Mhe Haule anapaswa awakumbushe maneno hayo.

Watu wengi hawana tofauti kimwenendo na hilo nililolieleza. Wana-approach success kwa kutaka wafanikiwe WAO. Na hivyo wanakosa wao na kuwakosesha hata watoto wao. Ni kweli inawezekana utafanikiwa wewe.  Lakini angalia zaidi after wewe yatadumu.  Nyerere aliona hilo.  CCM yake imeyumba kweli kweli lakini bado ipo ipo sana. Uongo?

Thomas Edison na invention ya light bulb, kina Henry Ford, Ferdinand Porsche kina Lamborghini kina William Deloitte walifanikiwa kwa kuchagua kulima minazi. Siyo mahindi. Njaa ya msimu kama haiui basi haina shida. Wanasema   WHAT DOESN'T KILL YOU MAKES YOU STRONGER. Manji amekuta utajiri wa babu, wewe kwa nini usiweke FOUNDATION ya wajukuu zako kufanikiwa.  Hutaki. Afu unasema babu yangu hivi kwa nini hakuwahi viwanja Masaki? Kwani umeambiwa vimeisha? Si ukanunue sasa wewe ili wewe uwe babu mzuri kama unavyosema? Shida unataka kulima mahindi. Short term relevance. Yani uwe kwenye chati kila siku. Long term and meaningful success inahitaji uonekenane kama haupo. Kwani mwaka 2000 ulikuwa unamjua Dangote?

Mafanikio yasiyodumu baada yako hata mbinguni huendi.  Yani kazi yako IKIFA baada ya wewe kufa imekula kwako.  MATUNDA yako lazima yadumu.  Alisema "mpate kuzaa matunda na matunda yenu yadumu/yakae".  Sasa matunda ya kudumu yanachukua muda.  Kama kulima minazi.  Wajukuu watakuta minazi. Mahindi hawakuti.  That's the differen.  Kama unafanya kitu ambacho eti "kinakuweka mjini".  Yani shida yako ni kikuweke mjini tu basi unalima mahindi.. Watoto na wajukuu wataishi kwa kutegemea mvua na chakula cha msaada. Why subject them to such a sorry life wakati ungeweza kufanya kitu cha kudumu for them.
Ungeweza kujenga biashara imara lakini ukasingizia eti ooh siyo kila mtu lazima awe na miradi.  Watoto na wajukuu zako wataishi kwa kusubiri ajira. Na maroboti yanakuja, drones zishafika, Google kitu kinaitwa ARTIFICIAL INTELLIGENCE (au Al kwa kifupi) ujifunze jinsi ajira zitakavyopotea huko tuendako.
Ungeweza kufanyia kazi kipawa chako ukakifanyia kazi na kujinoa kwa muda mrefu ili siku ukiingia sokoni uweke alama but hutaki.
Ungeweza kuja kufungua kampuni kubwa baadaye ili utatue hilo tatizo la ajira linalokukera lakini wewe unataka uajiriwe WEWE. Ili uvae vizuri ukope gari ukale Samaki Samaki afu basi.  Ukifa na degree yako inakuwa imeishia hapo. Hakuna kinachodumu.  Mungu akikuuliza huko ulikotoka uliacha nini jibu huna. Kisa ulipenda kulima mahindi ukaona minazi usumbufu. Eti ntaushije. Eti siwezi kujitesa maisha yenyewe mafupi. Ngoja ukifa hujaacha kazi ya maana hapa ndo utayakuta huko maisha marefu kweli kweli.

Usiwe blinded na RELEVANCE ya muda mfupi.  Matajiri wengi walipita vipindi vya kuchekwa na kukosa hata pesa at times.
Kutothaminiwa na ndugu au jamii nk.  Kwa kuwa tu walionekana hawavuni haraka haraka kama wengine. Kumbe mwenzao amelima minazi. Au Chinese Bamboo.
Wengi wakilima wakaona inakawia huishia njiani na kwenda kulima mahindi tena. Afu basi. Wanakuwa relevant now. Lakini jina lako hata wajukuu watakuwa hawalijui.  Ukichunguza kwa nini watoto leo wanajiita Don Ronaldo sijui Boss Lady.  Pamoja na mambo mengine but pia ni kwa sababu kwenye surname yake huyo mtu hakuna Dewji wala Mengi wala Mufuruki. Si rahisi mtoto wa Dewji kujiita sijui Don Van Persie au Sijui Undertaker hahaaaa.  Issue ni surname sometimes. So usije shangaa watoto wako na wajukuu hata jina lako wametupa kando tena hata hujafa. Surname haina mvuto. Kila uliona minazi inakukawiza kula bata.


Chagua vizuri.

Usiangalie leo tu my friend.


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
+255788366511
www.andreamuhozya.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni