Jumatatu, 21 Agosti 2017

"MY NAME IS CLARISSA" JE WEWE NI BINTI UNAYEWAZA KUTOA UJAUZITO? (Based on a true story)

JE WEWE NI BINTI UNAYEWAZA KUTOA UJAUZITO?
AU WEWE NI KAKA UNAYESHINIKIZA BINTI ATOE UJAUZITO ULIOMPA?



Ilikuwa ni siku nzuri ya Jumamosi na jua la Dar es Salaam halikuwa kali sana kipindi hicho. Plus mawingu kidogo yalifanya hali ya hewa kuwa nzuri zaidi. Nilikuwa nimealikwa katika shule mojawapo binafsi hapa jijini kwa ajili ya kusaidia mambo binafsi kwa mwenye shule hiyo. Ilikuwa ni siku ya MAHAFALI ya darasa la saba katika shuke hiyo ya ENGLISH MEDIUM yenye jina kubwa kiasi na yenye watoto kutoka familia zenye uwezo.

Mandhari ilikuwa nzuri mno na yenye kutia hamasa. Magari mazuri mazuri ya wazazi na walezi yakiwa yamepaki vizuri kwa utaratibu. Kila iliyeshuka kwenye gari alionekana kutoka Dar es Salaam ya kwake tofauti na ile wanayoishi wananchi wengine. Watoto wakiwa wamevaa vizuri mno na majoho yao ya graduation na kila aliyeawona bila kujali kama anawafahamu au la alifurahi.

Hakika shule na wazazi walikuwa wamejipanga. Ratiba zote zilienda sawa na graduation ikaenda vema sana kwa utaratibu mzuri na mambo yote yakiendeshwa kwa lugha ya kiingereza. Kila mwalimu, mzazi au mlezi na hata wanafunzi wa madarasa ya chini walionyesha kufurahia kuwa sehemu ya familia moja. Makofi ya hapa na pale  yaliendelea kwa kila jambo lililotangazwa au kufanyika.

Ikafika wakati wa RISALA ya WAHITIMU. Akapanda binti mmoja mzuri sana na kama kawaida akipendeza sana kutokana na mavazi yake ya graduation. Mrefu kidogo. Mwembamba kidogo. (Picha hii chini siyo ya ninayemzungumzia)


"HONOURABLE DEPUTY MINISTER..... MADAM HEADMISTRESS.....,  DISTINGUISHED GUESTS, LADIES AND GENTLEMEN......" alianza risala yake.

"IT'S SUCH A GREAT HONOUR TO STAND BEFORE YOU THIS MORNING ON BEHALF OF MY COLLEAGUES............."


Kila neno lililotoka katika kinywa cha binti huyo lililuwa kama limechongwa na fundi maalumu kinywani mwake. Sauti yake ilikuwa kama sauti ya malaika. Sehemu kubwa ya RISALA yake ALIISEMA na siyo KUISOMA. Wageni, wazazi, wanafunzi wenzake na hata wafanyakazi mbali mbali katika shughuli hiyo walisimama kwa muda kumsikiliza binti huyo.

Minong'ono midogo midogo kati ya wageni na wazazi kuashiria kushangaa kiwango cha binti huyo haikufichika. Ndani ya muda mfupi umati wa watu ulikuwa kimya kusikiliza kwa makini bila mtu yoyote kuwaambia wasilikize kwa makini. Kila mtu alionekana kutikisa kichwa kukubaliana na mambo yule binti aliyekuwa akiyasema katika RISALA yake. Kwa muda huo wote sauti za ndege na vitu vingine zilionekana kama kufa ilisikika sauti ya yule binti ikipasua anga!

Ungeweza kusema huyu binti atakuwa muhubiri mkubwa baadaye, ama kiongozi mkubwa sana. Usingeweza kumwona kama binti wa kawaida.


"WHEN WE CAME HERE ABOUT SEVEN YEARS AGO WE WERE MERE LITTLE BOYS AND GIRLS WITH A DREAM TO MAKE OUR PARENTS PROUD.
BUT NOW WE'RE NOT MERE LITTLE BOYS AND GIRLS. OR ARE WE?" aliuuliza akiwatazama wahitimu wenzake na wao wakijibu kwa pamoja "NOOOO WE ARE NOT" huku umati ukishangilia kwa nguvu sana.


"THIS SCHOOL HAS MADE US USEFUL HUMAN BEINGS...." akaendelea.... "READY TO MAKE NOT ONLY OUR PARENTS PROUD BUT ALSO THE NATION,  OUR BEAUTIFUL NATION, AND THE WORLD PROUD. WE ARE READY TO UNLEASH OUR FULL POTENTIAL TO THE WORLD....."

Makofi zaidi yakafuatia na wazazi kutazamana yumkini wakijiuliza ni mtoto wa nani kati yao. Binti aliongea mambo muhimu kuhusu wazazi, malezi, walimu, elimu, na maisha utafikiri ni mtu mzima mno tena mwenye uzoefu mkubwa wa miaka mingi. Kila alipoongelea wenzake,  au wazazi au hata walimu aliwakazia macho bila kupepesa macho huku akiongea jambo lililowahusu. Yale macho kama ya yule mwanamama Condoleezza Rice au yale ya Michelle Obama akiwa anasisitiza jambo. Binti alionekana kama mzoefu wa kutoa risala au kuongea mbele ya hadhira kubwa. Ungemwona hakika ungevutiwa naye pia.

Kwa mara ya kwanza toka niwe mkubwa nilitamani kurudi utoto pia kama Lady Jaydee na nikagundua bado sijachelewa, kinadharia.


Risala yake ikaisha wakati watu bado wanatamani aendelee. Hakuna aliyewaambia wazazi wasimame lakini ni kama waliambiwa na mtu ndani yao. Wote na wageni wengine na walimu na wanafunzi walisimama na kumshangilia binti yule. STANDING OVATION. Binti akainama na kushukuru. Tena na tena. Na kisha kupeleka risala yake kwa mgeni rasmi.

Mgeni rasmi alishindwa kujizuia na kumpa zawadi ya fedha nzito nzito.

"What's your name?", aliuliza mgeni rasmi.

"My name is CLARISSA...!" Alijibu binti kwa sauti ile ile ya malaika.

"Congratulations Clarissa!"

Binti akashukuru. Umati ukishangilia. Wazazi wakaanza kushika pochi na waleti. Wakaenda kumtuza alipotoka tu jukwaani. Ilibidi walimu wakasaidie kuweka utaratibu maana alizidiwa na fedha.

Sherehe ikaendelea. Kila mara nikawa nikisikia sauti masikioni mwangu ikirudia maneno "MY NAME IS CLARISSA" Hili jina niliwahi kulisikia zamani nadhani, nikawa nikiwaza.

Sherehe ikaendelea.
Ikafikia wakati wa wahitimu kuzawadiwa na shule kwa sababu mbali mbali. Clarissa naye akaitwa mara kadhaa kupokea zawadi. Kila mara akishangiliwa sana! Ndipo watu wakapata kuwaona wazazi wa yule binti.

Lahaula!

Katika watu wote waliokuwepo kuna kijana mmoja alipigwa na butwaa alipowaona wale wazazi wa huyo binti. Kijana huyo ni:

MIMI!


Boy.
Akili yangu ikahama ghafla kutoka kwenye yale mahafali na kurejea miaka 14 nyuma! Nikiwa sekondari. Nikakumbuka mpaka mahali nilipokuwa nimekaa mchana ule miaka 14 nyuma niliposikia sauti ya mmoja wa rafiki zangu wa shuleni akinisemesha:

"Andrew vipi?"

"Safi tu mambo vipi"? Nilimjibu.

"Ah safi tu hivyo hivyo, una muda kidogo"?

Nikafunika daftari langu kisha nikavuta pumzi na kumuuliza:

"Vipi umeachwa"?

Hakunijibu wala hakucheka kama nilivyotarajia. So nikamwambia twende  maeneo ya viwanjani kama ni kitu cha kuongea kwa utulivu. Akakubali.

Tulipofika akaanza kuniambia kuwa jambo analotaka kuniambia linahusu girlfriend wake. Straight forward akaniambia "Ni mjamzito"

Sitasahau nilivyojisikia.
Lakini nikamwambia rafiki yangu maneno haya. "KAMA UMENIITA UNATAFUTA USHAURI WA KUTOA UJAUZITO HUO NAOMBA TUISHIE HAPA HAPA USINIAMBIE CHOCHOTE ZAIDI MAANA  SITAWEZA KUSHIRIKI JAMBO HILO"

Akaniambia: "Ndo maana nimekufata Andrew maana washkaji wote wanasema tukatoe lakini nilitaka na wewe nione utasemaje... ila nimechanganyikiwa kabisa"

Nikawaza mimi ni nani hadi huyu mtu ametaka opinion yangu. Jibu likaja: mimi ni mtu muhimu kwa mtoto aliyetumboni kwa wakati huo.

So nikamuuliza: "Na yeye binti je anasemaje?"

Akasema yeye ameshashauriwa kutoa ujauzito na wenzake wote na hata ndugu zake wa kike!

Kwa kifupi tu nikakaa na rafiki yangu na kwa neema ya Mungu akakubali kuwa hatashauri abortion ifanyike licha ya pressure ya mazingira na wazazi wa pande zote wakija kufahamu. Hasa upande wa binti.

Tukakaa chini tukaandaa mpango wa kuhakikisha ujauzito hautolewi. Tukaenda kwa binti tukamwambia kuna daktari mmoja mtaalamu wa kutoa ujauzito tutampeleka. Siku ilipofika tukamwambia yule daktari amekamatwa na polisi maana alitoa ujauzito wa binti mmoja mwanafunzi akafariki. (Kumbe wapi.) Hapo tunajaribu kumjengea saikolojia ya aogope kuwa kuna kufa.
Visiku vikapitapita.

Binti anazidi kupewa pressure hasa rafiki zake. Wengine walishafanya abortion mara tano. Wanampa uzoefu kuwa mbona ni rahisi tu. Wakawa wanazidi kumwaga siri zao ambazo hata yeye hakuwahi kuzijua kwa kuwatazama tu. Dunia ina siri nyingi..Akaanza kuwa anatusimulia wanavyomshawishi.

Tukaona isiwe tabu. Tukamfata daktari mmoja tukamwambia kuna binti tutamleta kwako anataka kutoa ujauzito lakini akija tunaomba umpimepime kisha umwambie labda mwili wake sijui umekaa vibaya nk. Vyovyote tu afu umwambie utampa dawa kwenye drip. Daktari nahisi aliona vioja lakini akatukubalia tu tukampeleka binti kisha akapimwapimwa na mwisho akawekeza kadrip kadogo kale kumbe kana maji tu. Dah. Sasa sijui niseme Mungu atusamehe. Maana kwa kweli.
Haya binti akaamini ujauzito utatoka after sometime. Kumbe wapi.
Visiku vikaenda.

Hapo tukaanza kuongelea story za watoto watoto. Tukiona wazazi wana watoto wadogo namwambia yule rafiki yangu achekecheke na wale watoto.
Tunamjengea binti saikolojia ya kupenda watoto.

Bila kutarajia ujauzito aliokuwa anaficha umeanza kuwa obvious hakuna cha kuficha tena. Huku sisi tumeanza kuonekana kumjali mno. Huku tunatania mara majina ya watoto yanayovutia mara majina yanayochekesha. Ikafika hatua pressure za rafiki zake na ndugu zikija akiwaza boyfriend wake na pia mimi tunavyomtreat mwishowe akaamua potelea pote sitoi ujauzito tena.
Haikuwa rahisi.
Lakini ilifikia hivyo.

Lakini kilichonisukuma mimi ni kuogopa kuingilia uumbaji wa Mungu. Na kuwaza tu kuwa huwezi kujua huyo mtoto atakuja kuwa nani baadaye!

Miezi kadhaa baadaye katikati ya changamoto nyingi mno zisizosemeka za masomo ndugu na wazazi mtoto alizaliwa.

Wakamwita jina  lake CLARISSA!

Siku zikaenda maisha yakasonga tukaenda njia tofauti tofauti maishani na cha ajabu tukapotezana kwa kweli. Miaka kadhaa baadaye wakaamua kufunga ndoa na kuishi pamoja nk.

Fast Forward miaka 14 toka hiyo story ndo huyo Clarissa aliyekuwa amesimana jukwaani akiwshangaza walimu na wazazi kwa uwezo mkubwa na kipawa kikubwa cha ajabu. Ni Clarissa huyo huyo aliyenifanya nitamani kurudi utoto angalau kinadharia.

Ni Clarissa huyo huyo ambaye nilikuwa na nafasi ya kushauri asije duniani miaka 14 nyuma lakini kwa neema ya Mungu nikawiwa ndani mwangu kuona akija duniani na kuishi na kutimiza alichoumbiwa!

Ni Clarissa huyo huyo ambaye ndugu jamaa na marafiki za wazazi wake hawakutaka aje duniani kwa visingizio vya ni AIBU, huna hela, wazazi wako, masomo yako, utazeeka haraka, nk.

Yote hayo Clarissa alikuwa akiyasikia akiwa tumboni mwa mama yake.

Clarissa ambaye "walio na akili" waliona hakupaswa kuzaliwa lakini akazaliwa.


Nilipigwa na ganzi.

Wazazi wake wameshakuwa na maisha mazuri mno. Clarissa aliyetarajiwa kuleta shida alileta baraka nyingi.

Niliwafata wazazi wake na kuwasalimia.
Walishangaa kuniona pale. Hawakutarajia. Tulikaa sekunde kadhaa bila kujua tuseme nini. Mama wa Clarissa alinitazama machozi yakimlengalenga kwa kumbukumbu ya yaliyotokea. Nilimpongeza sana yeye na rafiki yangu wa shuleni na pia binti yao Clarissa ambaye hakujua kwa nini kati ya wageni wote wazazi wake walionekana kujawa hisia kali wakiongea na mimi. Nilitambulishwa kwake kama "Uncle Andrew" na kuambiwa nilisoma na baba yake.

Nilimshukuru sana Mungu kwa kunipa neema ya kutunza uhai wa kiumbe chake. Nikawaza what if mi ndo ningekuwa nashauri abortion kwa nguvu afu somehow wakaacha kuifanya na kumpata Clarissa halafu ningewaona pale ningekuwa na aibu na fedheha kiasi gani?

So kama wewe ni binti na unawaza kufanya abortion kwa sababu zozote zile kumbuka uanamke wako siyo kwa sababu una jinsia ya kike. Uanamke wako ni pamoja na kuruhusu nature ikutumie wewe kuleta mtoto kwa njia yoyote na wakati wowote ule atakapohitajika kuja huyo mtoto.

Ulishaona kuku anataka kutaga? Akikuta geti au mlango umefungwa atataga hata kwenye bustani. Sasa watu huwa hawalitupi lile yai kisa limetagwa nje. Hulitunza wakijua lina umuhimu wake. Simple logic right? Yes. Nature ikihitaji kuleta mtoto duniani ikakukuta wewe either kwa kupenda au bahati mbaya umepata mbegu za mwanaume katika siku sahihi za kutunga mimba usitake kutupa hilo yai.  Liweke vizuri tu lina kazi yake.

Kama waliotakiwa kubaki duniani ni watu

1. waliozaliwa kwenye ndoa tu
2. ndoa zilizo halali tu
3. mimba zinazoitwa ZILIZOTARAJIWA tu

Hivi hii dunia unadhani ingekuwa na watu wangapi my friend? Fanya research utashangaa. Saaa unadhani Mungu hajui?

Unajua kuna watu wangapi waliofanya vitu vikubwa duniani na walizaliwa wazazi hawajulikani?

Unajua watoto wangapi wameuwa kwa abortion waliotakiwa kuja duniani kufanya mambo makubwa na kutatua matatizo ya dunia hii?

Fikiria mtu kama Alexander Fleming aliyegundua Penicillin angekuwa aborted dunia ingepoteza watu wangapi kwa kukosa penicillin na ampicilin na amoxilin nk.


Ulishawaza Bill Gates angekuwa aborted dunia ingekuwa wapi leo bila Microsoft? Elewa kuwa Mungu yuko ahead of time alijua watu wake wangehitaji hizo software akaamuru mimba itungwe azaliwe Bill Gates.


Sasa wewe ukiabort unaona nini unachokuwa umeinyima dunia? Kisa eti unaona aibu. Kweli? Au unasikia hasira kwa sababu aliyekupa ujauzito ameukana!.

Uanamke wako haupo kwenye watu kukuona hujazaa nje ya ndoa kumbe umeshafanya abortion za kutosha. You're living a lie.

Uanamke wako upo kwenye kukubaliana na hali uliyonayo na kuruhusu nature ilete kiumbe wa kuja kufanya miujiza mingine huku zaidi ya ile aliyofanya Yesu. Yes, Yesu mwenyewe alisema tutafanya makubwa kuliko aliyofanya.
Sasa tutafanyaje kama tunauawa tungali tumboni.

Kina Les Brown na Myles Munroe waliwahi kusema utajiri mkubwa hauko kwenye migodi ya madini kama almasi nk bali uko MAKABURINI ambako watu wamekufa na vipawa hawajavitumia. Nakubaliana nao. Lakini mimi nataka niiambie dunia leo kuwa utajiri mkubwa zaidi wala makaburini haukufika bali uko kwenye vyumba vya siri na kwenye vyoo na kwenye mikasi ya hospitali na mikono ya madaktari ambako watu wakubwa na wenye uwezo mkubwa hawakupewa nafasi ya kufika duniani kabisa kwa sababu walikuwa aborted!



Ole wako ukiunyima ulimwengu utajiri uliowekwa tumboni mwako.

Ole wako ukimshawishi mwingine azuie utajiri mkubwa kuja duniani kwa sababu unaogopa aibu kuwa umempa ujauzito binti wakati wewe ni mume wa mtu au ni mchungaji au ni mbunge. Unataka kulinda hadhi ambayo iliondoka ulipofungua zipu na sasa unainyima dunia utajiri kwa sababu ya kulinda eti "heshima". Mungu anakuona! Na dunia ikikosa majibu ya maswali utakuwa responsible.

Ole wako ndugu yangu. Ni nani atakusadia kujibu kesi dhidi ya dunia nzima?

Fikiria wazazi wa Thomas Edison wangemuabort. Tungekuwa na kiburi cha kubonyeza kitufe ukutani halafu balbu inawaka? Unaona THAMANI ya ujauzito wa Thomas Edison?

Unajua kuwa ujauzito unaotaka utolewe huenda ukawa wa THAMANI kuliko thamani ya balbu?

Lakini vipi kama mwanamke kama Oprah angekuwa aborted?


Vipi kuhusu wazazi wa Aliko Dangote? Wangemuabort.

Vipi kama mama wa Dewji angesema sitaki kuzaa sasa hivi?

Mpendao michezo vipi wazazi wa Pele, au Messi au Cristiano Ronaldo wangefanya abortion.



Mpaka sasa kuna kina Messi wangapi dunia hii? Jiulize!

Kuna Gandhi wangapi kama yeye.

Mandela wangapi wameshatokea dunia hii?

Vipi kuhusu  wazazi wa mwalimu Nyerere wangemuabort?


Okay labda huko mbali. Tuwe practical kidogo. Huenda umeipenda makala hii. Vipi kama wazazi wangu wangeniabort basi?

Message kama hii iliyoandikwa hivi ungeiona vipi unadhani?
Ungeona zingine tu lakini siyo hii. Believe me.
You see?
Yet mimi nina mambo makubwa sana kuliko hii message.

Kama unawaza kufanya abortion waza tu kuwa sasa unapanga kuinyima dunia kitu CHEMA. Yani unawaza kuinyima dunia vitabu vyenye mambo makubwa na speeches muhimu, muhubiri na mafunzo adimu mno, discoveries na inventions zaidi ya hata quantum physics, entertainments na atristic works zaidi ya Monalisa na vitu vingine vingi ambavyo dunia haijapata kushuhudia!

Ole wako kuinyima dunia utajiri kwa sababu hutaki kuleta mtu duniani ambaye dunia inamtaka aje. Unatupa yai kisa kuku kalitaga bustanini.

Ole wako daktari unayetumia elimu yako kuinyima dunia utajiri mkubwa uliokusudiwa kuisaidia dunia hii na kuitoa katika changamoto ilizo nazo!


Utajiri unabaki kwenye mikasi, na matundu ya vyoo.

Hayo yote nimeyawaza sana. Kama ninavyomuwaza Clarissa na wazazi wake.


Kama umesoma makala hii ukiwa na dilemma ya kutoa ujauzito wako au mtu wako wa karibu au hata wa mbali basi tambua uko karibu na kuinyima dunia utajiri mkubwa. Na dunia itakapolemewa na shida zake na kumlilia aliyeifanya basi atakumbuka jinsi ulivyozuia utajiri na solutions za matatizo mbali mbali kuja mahali pake.

Usikubali kuhusika kuinyima dunia UTAJIRI iliousubiri kwa muda mrefu.

Vumilia tu kama wazazi wa Clarissa!


Yupo afutaye machozi.

Thawabu yako ni kubwa mno ukivumilia. Wakati mbingu zikitambulisha majina ya watu waliofanya vitu vya maana duniani HAKIKA jina lako halitashauliwa.


Asante na Barikiwa sana!


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni