Jumatano, 13 Septemba 2017
WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE! KUJUA WEWE NI MTU AINA GANI TAZAMA SEHEMU UNAZOENDA MARA KWA MARA
Siku kadhaa zilizopita nikiwa nyumbani mchana nilijisahau nikaacha mlango wazi wakati wa gari la taka kupita. Unajua kilichotokea? Nilipoenda kurudishia mlango na kurejea kuketi ghafla nikasikia mlio wa nzi. Akawa anaruka huku na kule. Arrrghh. Instinct yangu ya kwanza kikawaida huwa ni kuchukua dawa ya kuulia wadudu na kuspray. Lakini this time sasa nipo nyumbani na hiyo dawa hupaswi kuvuta hewa yake maana ni toxic.
What to do?
Nikakumbuka kuwa mpaka muda huo nzi wa watu alikuwa bado anazunguka yani hajapata sehemu ya kusettle. Kwanza nikasmile maana nina mke msafi sana and she knows huwa namwambia. So nikajua nzi hajasettle maana kaingia kwenye mazingira yasiyo yake.
What to do?
Nikafungua mlango tu wide enough. Kisha nikatoka mlangoni nikaona nzi anazunguka sebuleni kama mara tatu ruti ndefu hivi kisha huyooo akatokea mlangoni kwa spidi ya rocket!
Problem solved.
NATAKA KUSEMA NINI?
Katika vitu ambavyo hatutofautiani kabisa na nzi ni kwamba hata sisi huwa tunakuwa "comfortable" katika mazingira tuliyozoea/jizoesha. Ni vigumu sana ukawa comfortable mahali penye uchafu kama wewe ni msafi. Au penye usafi kama wewe ni mchafu kweli. Utajibana weeee lakini mwisho vitakushinda utaanza tu kuleta "fujo". Utatafuta tu sehemu ya kutokea.
Sasa sikia sikumfukuza nzi alitoka mwenyewe.
Lakini vipi kama ukikuta mzoga kando ya njia halafu kuna nzi wengi (comfort zone yao) halafu ujaribu kuwafukuza (kuwaswaga)? Utakuwa unafanya kazi bure. Wataruka kidogo na kusambaa kisha watarudi tena. Hawawezi kuondoka kabisa. Labda uondoe mzoga. Hao ndo nzi. Nzi mahali pao pa kujidai siyo kwenye usafi. Yani ukiona nzi katulia mahali ambapo wewe unapaona ni pasafi basi ujue kuna tatizo na pua zako au macho yako au vyote. Nzi anajua pa kwenda.
Ndivyo na sisi tulivyo. Ukitaka kujijua wewe ni mtu wa aina gani check where you normally go. Wapi huwa unakwenda mara kwa mara. There's no way ukaenda mara kwa mara sehemu usiyoipenda. Huwezi kuperuzi sana mtandao usioupenda. Kuna mtandao tu ndo comfort zone yakof
Miezi kama mitano iliyopita kuna siku niliingia kwenye daladala. Ghafla nikaona mdada kafungua simu yake. (Umbea huu nao Mungu atusaidie). Basi nimeona akafungua INSTAGRAM.
Akaingia search. Akatype Jina la mtu.......
Akaanza ku-scroll post za za huyo .
Nikawaza tu katika "umbea" wangu huo, dah huyu ameona of all places za kusoma ni hapo. Akawa anaenjoy na kucheka kweli. Mara anazoom. Basi katika "umbea" huo huo nikamsemesha kidogo:
*Mimi:* Naona unachekicheki news kidogo..?
*Yeye:* Dah yani kakangu huyu (naniliu) ataua watu mwaka huu. Mi lazima nipitie kwake kila siku.
*Mimi:* Aisee huwa namsikia hivi yuko vizuri ee?
*Yeye:* Dah aisee yani hatari mbaya nakwambia. Yani mimi nisipopita kwake nahisi kama naumwa (huku akismile)
*Mimi:* Aisee si mchezo
*Yeye:* Ndo hivyo tunaondoa tu stress.
Mazungumzo hayakudumu sana maana nilimshukuru kiaina nikatoa kitabu nikaanza kuperuzi kidogo na mimi kuondoa hizo stress kivyangu pia.
Ni muda umepita sasa ila tu baada ya kale katukio ka nzi nikakumbuka hiyo siku pia.
Mimi nakutana na vijana wengi sana kupitia mitandao ya kijamii. Hasa kwa ajili ya mambo ya ujasiriamali na naweza kukuhakikisha kuwa asilimia kubwa sana ya vijana hawako COMFORTABLE na mambo ya maana. Mada inayohusu maendeleo yao inaweza kupita na kupata comments 10 tu katika ukurasa wenye followers MILIONI MOJA. Sasa ngoja ije mada ya jambo la ajabu ajabu utaona "MAONI" yatakavyojaa. Sasa ukiona hivyo usijiulize sana we elewa tu THAT'S WHO THEY ARE.
Ukiona vitu vya maana unaona vinakuboa ujue wala hujakosea. Ni kweli kabisa "VINABOA" kwa watu wasio sahihi. Ukiona vitu vya kijinga "HAVIKUBOI" ujue ni kweli kabisa haviboi kwa watu sahihi kwa vitu vitu hivyo pia.
Nzi ataborekaje na harufu you mzoga?
Ukitaka kujua WHO YOU ARE wala usihangike kufanya research kubwa. Angalia tu vitu vichache:
1. Gallery yako ya simu
Ingia now uangalie. Ina picha za aina gani.
That's who you are.
Ina videos za aina gani?
That's who you are.
Kuna nyimbo za aina gani?
That's who you are.
2. Google Search list yako nini kinaongoza kutafutwa?
That's who you are.
3. YouTube Videos na channels ulizosubscribe nyingi ni zipi?
Ni za mambo ya ndoto zako na mafunzo ya kimaisha au ni muziki na umbea mwingine?
That's who you are.
4. Vipindi vipi vya Redio na TV huwezi kukosa kabisa?
That's WHO YOU ARE.
5. Nini unapenda kusoma bila kukosa.
Ubuyu wa leo leo au hadithi za Shigongo, au Tips za Dewji au Mafundisho ya Strive Masiyiwa?
Wapi upo napo COMFORTABLE?
Wapi unaweza kuahirisha kula kwanza mpaka ujue hicho kitu kilichoandikwa kimeishia wapi?
That's WHO you are.
5. Ukipewa External Hard Disk utaweka nini? Movies au vitabu? Je ni movie gani?
Aina ya movie na series zinazokuattract that's WHO you are.
Nk nk.. check hivyo vitu tu haraka haraka kwa uchache utajijua upo wapi.
Huwa unaenda wapi sana in the physical world lakini pia social media?
Ni muhimu sana kujua who you are mapema katika safari ya mafanikio yako ili uanze kucontrol vitu vinavyokuvuta mapema. Usije ukajikuta ghafla vitu vilivyokuwa vya msingi kwako ghafla vinakuwa vinakuboa halafu hujui kwa nini. Zamani ulikuwa unapenda watu wenye lugha ya staha na heshima na kuwasikiliza kweli kweli lakini siku hizi uko comfortable zaidi kusoma na kusikiliza wasio na staha na wanaotukanana matusi ya nguoni mitandaoni and wala huoni kama ni shida tena. Coz umeshakuwa nzi pia. Nzi mdogodogo.
Huoni shida kuwa kwenye mizoga wa maandishi. In fact unaitafuta na ukikuta haitoi harufu sana unasikitika. Ukikuta maua yananukia hutaki hauko comfortable. Ulishawahi kuona nzi anaruka kutoa ua moja kwenda jingine kwenye bustani na akatulia na kuenjoy? Hawezi.
Huenda na wewe hutaki habari zenye harufu nzuri.
That's WHO you are now.
That's who you've become.
Na uzuri ni kuwa unaweza kujua kabisa hiyo WHO YOU ARE ya sasa kama inakupeleka mahali sahihi au la.
Ukitaka ubadili mwelekeo wa maisha yako uwe wenye tija basi angalia WHERE YOU GO ON A DAILY BASIS.
Kama ningekuuliza swali sasa hivi kwamba: Hivi jana ulishinda wapi siku nzima?
Unaweza kusema labda
"Nilishinda kazini"
"Nilishinda nyumbani"
Nk.
Lakini huenda ulishinda WhatsApp. Au Facebook.
Sasa hilo siyo shida. Ishu ulikuwa wapi na wapi kwenye huo mtandao wa kijamii.
Shaolin Monks hupewa training sana kuhusu eneo la fikra. Na wewe unaweza kujifunza. Kutunza fikra zako zisishikwe na mambo yasiyokuwa na tija kwenye kutimiza ndoto zako. Hold your mind together. Badilisha sehemu UNAZOENDA na utabadilika sana. Kuna watu huwezi kuwaona mpaka ubadili sehemu unazoenda. Yes. Unataka kuonana na Reginald Mengi Samaki Samaki?
Utangoja milele coz Samaki Samaki huenda that's WHO YOU ARE but it's not WHO HE IS.
Umeelewa?
Kwenye Biblia Zakayo alikuwa si mtu mwema machoni pa watu. Lakini WHERE HE WENT changed everything. Alipanda tu kwenye mti ili amwone "MTUMISHI". Where he went was WHO HE WAS. Mungu anaona sirini. Zakayo pamoja na mabaya yote lakini alikuwa anatafuta pa kwenda ili atoke shimoni. Ni kama alijua hili nalosema hapa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.
Ukiendelea kwenda sehemu zile zile na kuonana na watu walewale na kutazama na kusikiliza vitu vile vile utaendelea kuelekea huko huko unakoelekea. Utaingia kwenye mtego wa kusubiri watu wengine watatue matatizo yako. Utaendelea kuona kuwa Dewji ana bahati na kusahau kuwa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.
Kama wewe ni kijana na unataka kuyafikia mafanikio lazima kwanza u check na hili la WAPI HUWA UNAPENDA KWENDA SANA.
Nakumbuka kuna siku nilikutana na kaka Samuel Sasali Mlimani City na kibongobongo nikamwambia "Kaka hatuonani?". Akaniambia tu "Huenda NJE ZETU (outings) zinatifautiana tu". And rightly so. Of course Sasali huwa ana majibu at all times and ukimuona unajiandaa tu kucheka. But the point is kama sionani naye kanisani na sifanyi naye kazi na WHERE I GO IS not WHO HE IS tutonanaje sasa?
Ni hivyo hivyo kwenye mitandao. Sehemu unazoenda sana ziangalie vema huenda kuna watu mnapishana. Huenda kuna fursa na ideas unapishana nazo na ndo Mungu anazileta lakini wewe hizo sehemu ambako hizo ideas zinapostiwa is not WHERE YOU GO.
Usitafute mchawi gani kakuroga ukawa nzi. Ni wewe mwenyewe. Anza kwenda kwenye maua huenda ukaweza kutengeneza asali.
Ukiona kwenda Serena kula lunch au hata kunywa juice tu haiikuingii akilini ujue that's who you are.
Mpaka ubadilike itabidi ufanye maamuzi ya Kizakayozakayo.
If you want to change your life start by changing WHERE YOU GO.
COZ WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE!
Semper Fi,
Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
#ThreeSixteen
#FourteenSix
#TheAloeLawyer
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni