Jumanne, 26 Septemba 2017

UKITAKA KUPIGA HATUA KIBIASHARA BASI ACHANA NA HELA ZA MAJIRANI ZAKO AU RAFIKI ZAKO AU NDUGU ZAKO


Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba? No lakini vibaiskeli viko kila mahali Buguruni mpaka kigamboni.


Mzee Mengi hauzi maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.

Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na *The Citizen* na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje.

Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake.


Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara.

Tatizo la watu wengi ni kudhani kuwa ukianza kitu chako mfano biashara au ujasiriamali basi ndugu zako na marafiki na majirani ndo wanapaswa kukusapoti. Wasipokusapoti *unanuna* na kuona hawakutakii mema. Unawasema na kulalamika.
Wewe kuna kitu hujajua bado ukikijua kwanza hutataka kuhangaika na makundi hayo ya watu kibiashara.

Kama upo hapo unawaza kuanza biashara na unafikiria kuwauzia jirani zako au ndugu zako basi kajipange upya kwanza. Utakuwa disappointed  na kuanza kulaumu watu bure. Ndiyo maana Mungu alikuumbia ndugu na marafiki wachache kuliko idadi ya watu usiowajua dunia hii.
Ukitaka kupiga hatua kibiashara achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Diamond hauzi karanga kwa ndugu zake au majirani zake. No wateja wa karanga zake ni watu tofauti kabisa.  Majirani wanunue wasinunue no problem.
Wanaoshindana kuview nyimbo zake You Tube au kuzidownload wala wala siyo eti rafiki zake. Ni watu tofauti.

Vijana wengi wanaojifunza kwangu biashara huwa wananiuliza swali: *"SASA BRO NTAMUUZIA NANI MAANA HUKU NINAKOKAA DUH WATU NI WA HALI YA CHINI KWELI KWELI NA HATA RAFIKI ZANGU YANI BORA MIMI"*
Jibu ni moja tu hapa: Ukitaka kupiga hatua katika biashara *achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako*

Anayezalisha tissue papers au toilet papers anauzia rafiki zake? Wanaoanza kutengeneza furniture huwa wanauza kwa ndugu zao? Sasa why wewe unawaza jirani zako ndo wateja.
Unakuta mtu anataka kuanza kufuga kuku anataka majirani zake na wafanyakazi wenzake ndo wale kuku wake! Kwani wanaoshona nguo kwa *Sheria Ngowi* ni ndugu zake au eti jirani zake? No.
Ni watu wengine tofauti kabisa. Maana kwanza jirani ataanza kuleta ujirani kwenye biashara yako changa halafu mtaishia kugombana bila kutarajia.
Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Kakangu alinunua vitu kwangu miaka mitatu na nusu baada ya mimi kuanza biashara. Tena alinunua vitu vingi hadi nikachekelea kwa kweli. But unaona sasa ningesubiri anunue ndo niendelee ningekuwa wapi? See, ukisubiri sapoti ya ndugu unaweza kuipata mwaka keshokutwa.
Sasa si utakufa masikini?

So we anza tu ndugu waje wasije isikukwaze. Kwani mwenye Facebook wewe umejiunga kwa kuwa mna undugu au eti unamsapoti? Kama vipi we acha kujiunga Facebook uone kama atakufa njaa kwa kuwa hutaki kumsapoti.

Kwani hiyo simu uliyonayo unadhani mwenye hiyo kampuni hana ndugu? Angesubiri ndugu zake au rafiki zake wamuuingishe si angeacha biashara kwa kukosa wateja? Maana wewe unatengeneza Tecno wakati ndugu zako wanachotamani ni iPhone hapo si utalaumu watu bure?

Mi nimeona jirani zangu wakija kuuza unga wa lishe. Lakini taste yetu kwenye hivyo vitu ni nyingine. Anasema "niungishe tu hata huu mfuko mmoja tu jirani" Sasa hapo mtu anauza kwa kuhurumiwa. Sasa utafanikiwa kweli? Nilipoanza biashara nilikuwa na list ya rafiki zangu ndugu zangu na majirani. Tena wenye uwezo mzuri. Kila niliyemshirikisha anakwambia tu *"TUPO PAMOJA"*. Hahaaaaaa.
Hawakununua. Nimekwambia hivi kakangu alinunua kwangu miaka mitatu na nusu toka nianze. Baada ya kuona naambiwa tu TUPO PAMOJA ndipo nilipostudy watu waliofanikiwa waliuzia nani vitu vyao. Nikapata jibu. Hebu jiulize.

Kwani anayejenga hoteli anawajengea rafiki zake au majirani? Nani akalale sehemu ambako anajulikana?  Sasa ukitaka ujenge mgahawa au saluni halafu rafiki zako ndo waje utakuwa hujajua kitu bado. Utaifunga tu hiyo saluni.

Cha msingi wewe tengeneza VALUE. Hilo ndo muhimu. Kisha wateja SAHIHI watakuja tena kutoka mbali kweli kweli. Ukiwaza  kufungua biashara huku unawaza mashosti sijui washkaji utaifunga siku si nyingi afu utasema eti wateja hakuna.
Kweli?
Yani katika nchi yenye watu karibu milioni 50 unaweza kukosa wateja kabisa kweli? Ulichokosa siyo wateja ni maarifa.  Knowledge.

Ukitaka kufanikiwa katika biashara hasa mwanzo fanya kama vile huna ndugu wala majirani. Fanya kwa ajili ya watu wasiokujua. Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako. Wakizileta well and good wasipoleta no problem.

Reginald Mengi wakati anaanza kuuza maji ya chupa hakuwa anatafuta marafiki wa kuyanywa hayo maji. Au unadhani ndicho alichofanya? No. Maana unajua marafiki nao huwa ni rahisi kwao kufikiri unawageuza ngazi ya kupandia. Wengi huanza kuona wivu kwa siri kuwa wewe utawazidi kimafanikio sasa kwa nini wakusapoti huku hawataki uwazidi.

Ndo maana nimesema wewe concentrate na VALUE. Dunia ya leo ni dunia ya VALUE. Value yako ikiwa nzuri wateja wako watatoka sehemu ambazo hukuwahi kufikiri kabisa. Kuna siku nimeitwa Oysterbay nyumba ya mtu mmoja mkubwa akihitaji kununua kutoka kwangu. Value. Lakini majirani zangu wala hawana habari. Wana taste nyingine. Value yangu huenda haijawagusa. So sikasiriki.
Achana na hela za majirani. Usizipigie hesabu kabisa. Ndo maana hakuna tajiri anayehangaika na jirani zake.

Umeelewa?

Au niendelee kidogo?😄 Okay... Jifunze kwa ma-MC hawa washereheshaji. Unakuta MC anaishi Kijitonyama lakini sherehe za Kijitonyama watu wanachukua MC wa Magomeni. Sherehe za Masaki watu wanachukua MC wa Mbezi. Wakati Masaki pia kuna ma MC wanaishi. Sherehe iko Mwanza watu wanaita MC kutoka Dar au Arusha. MC huyo huyo majirani zake wanasema *"aah huyu ana bei sana tuchukue fulani afu huyu siku hizi anajiona kweli wakati ni MC wa kawaida tu"*. Unaona sasa? Huyo MC angesubiri kusherehesha kwa majirani angesubiri mpaka azeeke.

Kitabu kinasema Nabii hupata heshima nje ya nyumbani. Ukisubiri watu wanaokuzunguka ndo wawe wateja hujajua vizuri maana ya neno MTEJA.

Huoni Bar iko Sinza lakini wadau wake ni watu wa *Tabataaaa!*
Majirani wanaokunywa pombe wanaoishi jirani na hiyo Bar wanaenda kunywea Kinondoni. Kwani mwenye Samaki Samaki hana majirani? Lakini hapo Samaki Samaki wanaokula na kunywa ni jirani zake? No!

Sasa kwa nini wewe unatengeneza sabuni ya maji unafikiri jirani zako ndo wateja? Wasiponunua unaona eti hawataki kukupa sapoti. Nimesema achana na hela za rafiki zako na jirani zako na ndugu zako. Utafika mbali sana. Yani ndugu watakuja huko mbele ya safari. Au utashangaa hawatakuja tu milele.


Nadhani sasa umeelewa vizuri japo ndo hivyo inauma kusikia lakini ndovile!

Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako!

Ukifanya hivyo ndo utakuwa umeanza kuelewa shughuli hii ya biashara na ujasiriamali ilivyo.


Nakubariki. Nakutakia mema!

#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni