(Sifundishi ubaguzi....)
Wakati wa sakata la ajira za uhamiaji ambako usaili ulifanyikia uwanja wa taifa miaka kama miwili iliyopita kuna vijana wengi sana waliojitokeza.
Baadaye ikaja ya TRA shortly thereafter. Na mwaka huu tena juzi juzi TRA tena wakaita watu kwa usaili wakajitokeza vijana wengi sana.
Katika hizo instances zote sikuona kijana wa kitanzania mwenye "ngozi nyeupe".
Nikawaza kidogo... Nikajiuliza.
Hivi kuna watanzania vijana wenye asili ya kihindi na kiarabu na hata kipakstani nk hapa nchini?
Nikajijibu kuwa "WAPO".
Nikajiuliza tena kidogo wote wameajiriwa?
Kaakili kangu kakaanza kusearch network kidogo kisha nikajijibu: "HAPANA"
Nikajiuliza tena: Sasa mbona hawaendi kufanya interview kama wenzao sasa?
Nikawa sina jibu. Eti, ulishawahi kujiuliza swali kama hilo?
UMASKINI WA FIKRA NDO KIFUNGO KIREFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA
Sijui kama umewahi kuishi kijiini. Lakini nikuulize tu hivyo hivyo. Hivi ukikuta wanaume 50 wako kwenye tope kwenye shamba kubwa la mpunga na wanakwambia hawawezi kujikwamua katika tope hilo wanaomba msaada wako utawaza nini? Tufanye hivi liwe ni shamba ambalo wewe una uhakika hilo tope hata mtoto wa shule ya msingi anaweza kutoka.
Utawaza nini?
Kuna kitu hakiko sawa kwenye "bongo" za watu hawa. Si ndiyo?
Fikra zako zikishikiliwa na mtu mwingine utakuwa mfungwa maisha yako yote. Kitu kikubwa kinachotutofautisha sisi sote siyo eti jinsia au rangi au imani nk. Ni jinsi tunavyotumia UHURU tuliopewa bure wa KUFIKIRI. Sijui wewe utakuwa kundi lipi.
1. Kuna ambao wanautumia uhuru huo KUFIKIRI kweli. Hawa hupiga hatua kidogo kidogo mwisho inakuwa kubwa. Hawa ni wa kuigwa mfano.
2. Kuna ambao wanautumia uhuru huo KUTOFIKIRI tu. Wapo tu hawataki kabisa kufikiri hata kidogo tu. Hapa unakuta wasomi tu wengi. Hawa wanahitaji #MAOMBI nadhani.
3. Kuna wanaoutumia uhuru huo siyo tu KUTOFIKIRI bali KU-DEMAND mtu mwingine afikirie kwa ajili yao.
Sasa hawa wanahitaji #ELIMU lakini nadhani na #VIBOKO (ikibidi).
Jokes aside... Tuna kundi kubwa la vijana ambao hawataki kufikiri na wanataka mtu mwingine afikirie kwa NIABA yao.
Huu ndo unaitwa MSIBA WA TAIFA.
UNAPOJIFUNZA KWA MTOTO WA FORM ONE
Ngoja nikupe story kidogo.
Hivi karibuni nilisafiri kwa basi. Dar Lux. Basi zuri sana kwa kweli.
Nimekaa pembeni na kijana wa kiume miaka kama 14 hivi mwenye asili ya kiarabu. Nilikuta keshaketi so nikamsabahi na kujitambulisha. "Naitwa Andrea ni mjasiriamali na nafurahi kuwa na wewe safarini mdogo wangu". Akajikuta anasmile na kujitambulisha pia. Well safari imeenda story za hapa na pale but mpaka mwisho wa safari nikajifunza kuwa alikuwa anatoka likizo kurejea shuleni. Katika kuongea naye nikajifunza kuwa baba yake ni mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa. Na kaka ya huyu kijana yuko nje ya nchi akisomea mambo ya usimamizi wa fedha (za familia)
Dada wa huyo kijana yuko Dubai anafanya kazi katika kampuni moja kubwa kupata uzoefu kwa ajili ya baadaye kusaidia biashara zao. Imagine huyo ni kijana wa Form One.
Yeye huyu kijana yuko kidato cha kwanza hivyo lakini baba yake anamshauri kuhusu kuchagua masomo ya biashara na ameshamwambia kuwa kuna mradi atampa akishamaliza mambo ya masomo yake ili ausimamie na ndo sasa huyo kijana akawa anasema bado anawaza maana anaona jinsi baba yake anavyo"hangaika" kuwaza mambo mengi na ku-manage biashara zake za petrol stations na malori na nyinginezo. Nikawa namtia moyo tu kuwa asiogope changamoto nk.
Lakini huku nikawa najiuliza kimoyomoyo.
Hivi na mimi nilisoma sheria ili nikasolve kesi za ukoo wangu au familia yangu au ili niajiriwe tu ilimradi kwetu waone hela inakuja wamshukuru Mungu kuwa wamepata mtu katika watu?
Niliwaza sana.
Nikawaza hivi sisi tunaposoma degree ya USIMAMIZI WA FEDHA tunakuwa tunataka tukasimamie fedha za nani?
Za familia?
Eti.
Hivi tunaposoma degree ya BIASHARA tunakuwa na lengo la kwenda kuwa wafanyabiashara au kuajiriwa kwa mfanyabiashara ili yeye ndo AFIKIRIE cha kufanya atwambie sisi nini cha kufanya (Job description) halafu tukishakifanya atupe zawadi (mshahara)?
I mean tunaposomea UALIMU lengo ni kufanyanya nayo nini hiyo elimu.
Uhasibu. Uhandisi.
Kwa nini tuna elimu ya udaktari halafu TUNAGOMA mpaka Ulimboka anapoteza meno na kucha kwa ajili yetu?
Kugoma ni kulazimisha mtu mwingine afikirie cha kufanya. Na asipofanya huna cha kumfanya vile vile. Au naongopa ndugu zangu?
See?
Career guidance katika jamii ya kina sisi #WEUSI ni changamoto kubwa. Tunafanya tu mazoea. Wengi tumesoma kwa mazoea tu. Mpaka leo ndo tunaendeleza trend hiyi hiyo kwa kizazi kijacho.
Nenda shule yoyote ya msingi leo hapo ulipo uliza watoto wanataka kuwa nani baadaye. Ukiacha wanaotaka kuwa Diamond au Samatta wengi wanakwambia: mwalimu, rubani, mwanasheria, "injinia", mhasibu, daktari, nk. Wachache sana watakwambia kuhusu kuuza nguo au kuuza viwanja au kuuza magari na vitu vya aina hiyo. Why wazazi #WEUSI wanaona fahari kuwa na daktari au mwanasheria. Ndo maana zikitangazwa nafasi 50 kesho TRA hutoamini "nyomi" utakayoiona. Na hiyo itaendelea hadi Yesu arudi.
WHAT TO DO?
Kujitoa kwenye KIFUNGO cha fikra siyo kitu rahisi lakini ndo njia #pekee ya kuokoa uzao wako ujao. Lazima kuanza kuwaza TOFAUTI na mazoea. Mazoea ndo yametufikisha hapo. Na ni WEWE wa kuanzisha hiyo trend tofauti.
Tuanze kuwaza kama "wenzetu".
Kama wewe ni mzazi anza kitu chako sasa. Hata kama umeajiriwa. Anzisha biashara ambayo una uhakika unaweza kuwa-guide watoto wako wakasome elimu hiyo hiyo wanayosoma wengine ila wakimaliza waje kui APPLY hiyo elimu kwa biashara ya familia. Kama ni kusimamia fedha wasimamie za familia. Siyo tu za Vodacom.
Hivi watoto wa Bakhressa wanafanya kazi Vodacom?
Kuna wakati nilikaa na mtu mmoja hapa jijini ana "hela zake". Akasema mtoto wao wa kwanza wamemjengea Hoteli Zanzibar na mtoto huyo kwa sasa ana miaka kama 14 na anasoma hapa hapa Bongo. Na mtoto anajua. Na mtoto akiwa likizo huwa anaenda ofisini kwa baba yake kujifunza namna ya ku-MANAGE biashara kwa kuona.
Sasa mtoto huyo utamkutaje uwanja wa taifa kufanya interview eti. Au mei mosi amebeba Bango la kuongezwa maslahi?
Kwa sababu ya kushindwa kwetu kufikiri na kutaka SERIKALI ndo ifikirie kwa ajili yetu kuna siku watoto wetu wataambiwa wakafanye interview hata PORINI na wataenda. Tunakuwa kama kondoo tu kupelekwa kokote.
Nimejifunza mengi kwa hawa "wenzetu".
Mtanzania mmoja mwenye asili ya kihindi anamiliki majengo makubwa kama matano hapa jijini. Miaka 7 iliyopita nilikuta anahangaika na mafundi city centre kwenye ghorofa moja refu huko juu walikuwa wanajenga RESTAURANT moja ya kisasa. Katika kudadisi mbona anapush push hivyo akaniambia hiyo restaurant ilikuwa ni ZAWADI ya birthday ya mtoto wake wa kwanza ambaye alikuwa masomoni Uingereza wakati huo. Na birthday ilikuwa bado wiki moja tu. Hebu fikiria. Sisi birthday tunapeana "baisko" na likeki kuuubwa au eti gari. Thinking yetu iko na shida. Why birthday ya mwanangu nisimpe mradi. Anakuwa anagrow na mradi wake. Of course tunaweza lakini nani yuko tayari aache COMFORT ya ajira kwa ajili ya kuset TREND mpya kwa vizazi vijavyo? Tunalilia NYONGEZA ya mishahara.
Nimesema ukiazimisha mwingine awaze kwa ajili yako akikataa huna cha kumfanya. Si raisi huyo hapo amesema kwa VISION aliyonayo saivi priority ni HUDUMA ZA kijamii. Period. Kwani madktari waliambiwa nini wakati ule? Asiyetaka mshahara uliopo aache kazi.
Unafanya nini sasa.
Waswahili wanasema kila mtu apambane na nini......?
Halafu na wewe unaanza kulaumu raisi mbele ya watoto wako. Eti raisi huyu tutamnyima kura. Wakati hata hukumpa kura yako so in fact hakuna utakachobadili. Unaharibu tu fikra za watoto wako wanaoanza kufikiri kuwa raisi ndo anasababisha wakose ada au wale matembezi wiki nzima.
Ukilazimisha SERIKALI ifikirie kwa ajili ya gharama ya elimu ya juu ya watoto wako watakachofanya hela ambayo zamani walikupa wewe yote saivi wataigawanya ili wapate watoto watano. Wanakwambia tumedahili wengi zaidi na tumetoa mikopo kwa wengi zaidi.
#Smart.
Utafanya nini?
So kama hatutataka kufikiri tofauti tutaendelea kuishi hivi hivi vizazi na vizazi. Utajiri tunao elimu tunayo tunaenda kuiapply kwenye BIASHARA za "wenzetu". Na watoto wetu tunwafundisha hivyo hivyo.
EMBE! EMBE! EMBE! (Tuendelee)
Wakati niko mdogo kijijini kulikuwa na wahindi wana Pick Up walikuwa wakitoka Nansio wanapita jijini kwetu wanaenda vijiji vya mbali zaidi. Sasa walikuwa wakifika kijijini kwetu wanakuta watoto wa kiume tunawasubiri kuwapa MAEMBE kama zawadi. Embe! Embe! Hata Kiswahili chenyewe tulikuwa hatujui sisi. Embe! Wanachukua MAEMBE hadi wanatosheka wanaondoka. Sisi tupo tu. Na tunajisikia vizuri kweli kuwa wamekubali. Khaaa!
Kuna wakati wakawa wanatupa lift hadi kama kilomita moja hivi wanatwambia turudi. Tunafurahi kweli. Tumepewa lift kwa kugawa "mali" bure. Tulikuta wenzetu wanafanya hivyo so na sisi tukaendelea hivyo hivyo. Hata hatujui kwa nini.
Sasa hiyo inatofauti gani na leo nikapata degree (embe) nikaanza kuwaambia waajiri "Embe"! Embe! Embe!
Halafu wakapokea hiyo degree yako wakakupa kalift kidogo kimaisha (ujira) kisha wanakwambia haya shuka toto jurii.
Hahaaaaa.
It's the same.
Kuna siku nikaenda nao hadi mjini nilikuwa nimeshakuwa rafiki na hao watoto. Nione hawa wanatokaga wapi lakini? Baba yao akawa ananishangaa tu. Lakini nikarudi kijijini kwa miguu. Sasa si ningeshauzwa mimi kama ingekuwa dunia hii ya leo!! Lol.
Lakini naamini unaelewa jinsi tunavyofurahi kupata LIFT badala ya kufikiri ni namna gani TUMILIKI HILO GARI sisi wenyewe na tuwape "weupe" lifti. Nilisema sifundishi ubaguzi. Just kuchokonoa akili zetu ambazo mpaka leo zinawaza kuwa kuajiriwa kwenye ofisi ya WAZUNGU ni "BAHATI".
Sikia.
Watoto wa hao wahindi walikuwa wanafundishwa cha kufanya wakifika kijijini kwetu. Ni kusmile na kutuchekea kidogo. Sisi tunafundishwa na kugombania kugawa Embe! Na kupigana vikumbo nani embe zake zipokelewe.
Utumwa tu wa FIKRA.
Dewji hakuwahi kupanga foleni NBC kuomba kazi. Na wala watoto wake hutawaona njia hiyo. Wala kizazi chake chote.
Au watoto wa Ali Mufuruki wanaenda pia uwanja wa taifa eti interview?
Wapi.
Lakini sisi tumekazana tu kuanzia babu mpaka mjukuu" Embe! Embe! Embe!
Tutaishi kwa lifti na mpaka tutie akili.
#ThreeSixteen
#FourteenSix
Semper Fi,
Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni