Jumanne, 12 Desemba 2017

CONFIDENCE WITHOUT KNOWLEDGE: LEARN FROM SIMON PETER (KUJIAMINI BILA MAARIFA: JIFUNZE KWA SIMON PETRO)


*****
Naongelea biashara na ujasiriamali.
*****

Shalom!

Namshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuwa pamoja tena. Nawapenda sana.

Leo tujifunze pia jambo jingine muhimu katika ulimwengu wa biashara na ujasiriamali.

Katika kusoma Biblia ukikutana na habari za mtu aitwaye Petro aliyekuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu unaweza ukahisi huenda jamaa alikuwa kimbelembele sana.

Kwanza alipenda sana kujibu maswali kabla ya wengine. Ilikuwa ni kama tabia hivi.

Pili alipenda kutoa suggestions bila kuuliza wenzake wala nini. Mfano pale mlimani alipomwambia Yesu: "ukitaka NITAJENGA vibanda vitatu..."
(Mathayo 17:4)

Yaani anasema NITAJENGA wakati pale yuko na wenzake wawili. Kuna watu wanadhani alipanic labda. Lakini kama nilivyosema ukisoma habari zake zote utajua ilikuwa kama tabia yake pia kutaka kuwa tofauti.

Tatu alikuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu papo kwa hapo bila kuuliza mtu. Mfano alivyomkata mtu sikio akijaribu kuzuia Yesu asikamatwe.
(Yohana 18:10)

Nne alikuwa anaweza kutaka afanyiwe kitu cha tofauti na wengine bila kuhofia watawazaje kuhusu yeye.  Mfano kukataa kuoshwa miguu kisha "alipopigwa mkwara" akaona isiwe tabu wala nini ila kama vipi basi aoshwe na kichwani na mikono siyo miguu tu!
(Yohana 13:9)

Kwa kifupi wengine wanaweza kusema labda Petro alikuwa akifanya vitu kwa kukurupuka!

Lakini ukichunguza hayo mambo niliyoyataja na ukachunguza namna alivyokuwa akifanya mambo yake na ukizingatia kazi aliyokuwa akiifanya maishani kabla ya kumfuata Yesu (yaani UVUVI); unaweza kutambua kuwa Petro alikuwa mtu mwenye KUJIAMINI kupita kiasi. Uvuvi si kazi nyepesi. Kukaa macho usiku baharini mara mvua mara mawimbi tena uko kwenye kachombo kadogo lazima uwe ngangari! Kwa hiyo jamaa alikuwa anajiamini sana.


KUJIAMINI KWA PETRO

Na unaweza ukaona kujiamini huko wakati Yesu alipotokea juu ya maji halafu Petro akamwambia Yesu kama ni wewe kweli hebu niamuru na mimi nitembee juu ya maji! Yesu alipompa go-ahead jamaa hakufikiria mara mbili akatoka chomboni na kutembea juu ya maji! Aisee. Usifikiri ilikuwa rahisi. Ilikuwa ni confidence kubwa sana.
(Mathayo 14:29)


Ilikuwa tabia yake kabla hata ya kuongelea imani. Na Yesu alichagua WAVUVI makusudi akijua hawa siku wakielewa somo watapiga kazi bila woga. So Petro kwa confidence ileile akaingia baharini akitembea JUU YA MAJI pia.

Lakini mfano wa pili kusisitiza nature yake ya kujiamini kupita kiasi ilikuwa wakati Yesu alipowatabiria kuwa watamkimbia wote. Petro akasema (natumia maneno yangu hapa:) "AH WAPI..! LABDA HAWA WAOGA WAOGA. SIYO MIMI WEWEE. MIMI!?? MIMI BANA HATA KUFA NA WEWE NITAKUFA NA WEWE HATA WAKIKIMBIA WOTE HAWA! WE HUNIJUI KUMBE?"
(Story nzima pale Marko 14:29-30 uone maneno yake mwenyewe)


TATIZO LA PETRO

Lakini kumbe Petro alikuwa anajiamini YEYE KAMA YEYE. Yaani aliamini uwezo wake wa kuhimili mambo ya siku zote akasahau kuwa sasa alikuwa katika BUSINESS MPYA ambayo ilihitaji maarifa mapya ambayo alikuwa HANA!


MIMI NA WEWE

Hivyo ndivyo watu wengi tulivyo. Tunajiamini bila maarifa sahihi. Matokeo inakuwa ni DISASTER ingawa kwa neema ya Mungu tunasonga mbele.

Mojawapo ya kitu nilichoweka katika kitabu changu kitakachowajia baadaye ni kuwa wakati nilipoacha kazi ili kuanza safari ya kibiashara na ujasiriamali miaka kadhaa iliyopita nilikuwa najiamini kweli kweli!  Yaani ungenikuta wakati ule "ungenipisha njia" tu utake usitake. Nilikuwa najua mi noma. Nilikuwa najiamini kuwa kila kitu kitaenda sawa tu. Ndo maana nilikuwa tayari kushuka chomboni (ajira) na kutembea juu ya maji  (ujasiriamali). Na nikawa nasema yani mimi hata kampuni yangu isipoenda vizuri "Nitakomaa mpaka kieleweke tu maana mi noma."

Lakini kumbe nilikuwa natembea katika ujinga  (IGNORANCE) uleule wa ndugu yetu Petro tu, wa kujiamini bila kuwa na MAARIFA SAHIHI. Miaka miwili tu baada ya kuanzisha kampuni yangu nilikuwa na changamoto nyingi mno tofauti na nilivyokuwa nimetarajia. Nilijikuta ni wakati wa kulipa kodi na pesa hakuna, nilikuwa na wateja kadhaa lakini hawakuwa wakilipa kwa wakati na wengine kutolipa kabisa tofauti na matarajio yangu. Wafanyakazi wanahitaji mishahara inabidi nikope pesa kwa rafiki zangu kulipa baadhi ya mishahara nikitarajia wateja wakilipa nitarejesha. Wateja hawakulipa! Nina madeni. Ninadai watu pia. Nikajikuta ninapata stress ambayo sikuwahi kufikiria ingewahi kuwa hivyo. Hapo nikama nishatembea juu ya maji sasa uhalisia umetokelezea kuwa kumbe sijawa tayari kutembea juu ya maki kama nilivyodhani. Nilipata chest pains ambazo zilinipeleka Muhimbili bila kutarajia kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Hizo ni baadhi tu ya changamoto ambazo naweza kusema kwa sasa. Ziko nyingi.

Hii historia yangu kila mara huwa inanikumbusha ile story ya Petro alivyoanza kutembea juu ya maji kabla hajapata maarifa sahihi kuhusiana na IMANI YAKE. Alianza kuzama maana mashaka yaliibuka.

Hakuwa na maarifa sahihi kwa nini WENGINE (Yesu) waliweza kutembea juu ya maji.


UNATARAJIA KUANZA BIASHARA? JIFUNZE HAPA

Nimekuwa nikikutana na vijana mbali mbali everyday kuongea nao kuhusu biashara na ujasiriamali. Wengi wao hawana tofauti sana na Petro kwa mantiki hiyo niliyoieleza. Kama ilivyokuwa kwangu wakati naanza pia. Vijana wengi wanadhani mafanikio ni kama kutuma 'SMS'. Kwamba unatype tu kidogo kisha unabonyeza SEND afu tayari. Ndo maana wamekuwa WALEVI WA BETTING.

Ukweli ni kwamba mafanikio hasa katika biashara na ujasiriamali yanahitaji kupata MAARIFA sahihi ya kitu unachotaka kufanya. Kujiamini ni kuzuri lakini kudhani kuwa kujiamini kwako ndo kutaleta mpenyo kibiashara bila kuwa na maarifa sahihi ni kachumbari ya disaster! Biblia inasema Watu #wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA! Umeona ee?

So bila msaada sahihi UTAANGAMIA KIBIASHARA. Utasingizia biashara yako imerogwa na shangazi au na mpemba au shetani ameiinukia kumbe shetani yuko zake Brazil huko ni wewe tu huna maarifa sahihi. (Shetani hana uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja...he is not omnipresent).
Maarifa rafiki.
Kuwa mtu wa kufundishika.


Miezi kadhaa iliyopita niliandika makala iliyosema ukitaka kufanikiwa kibiashara epuka pesa za NDUGU, MARAFIKI na MAJIRANI. Na nikaeleza sababu na kutoa mifano. Nashukuru iliwasaidia watu wengi mno kupata maarifa SAHIHI kuhusu eneo la wateja na sasa wanasonga mbele.
Maarifa ni muhimu usijiamini tu ukaishia hapo.


MWONE PETRO TENA

Wakati Yesu anasema wote watamkimbia na Yesu akijua kuwa Petro kwa kujiamini kwake atasema YEYE HATOFANYA HIVYO. Yesu akaona amsaidie Petro maarifa kiduchu ya kumsaidia. Akamwambia Simoni "Shetani amewataka ninyi (ni kama ameomba ruhusa) apate kuwapepeta kama vile ngano lakini ninekuombea wewe ili imani yako isitindike"
(Luka 22:31 na kuendelea)

Lakini kwa kujiamini zaidi ndo hapo Petro akasema hatamwacha Yesu hata baada ya kupata information ambayo alikuwa hana.

Kumbe!

Yesu alitaka kumwonyesha Petro kuwa kujiamini kwako kutakwama tu mahali maana kuna vitu bado hujui. Na kama huamini ngoja uone muda wa jogoo kuwika ukifika kabla hajawika utakuwa umeshanikana mara tatu wewe huyo huyo.

Kumbe shetani alikuwa na ruhusa ya kuwapepeta kina Petro na Petro hajui.

Kumbe Yesu alikuwa ameshamwombea Petro ili asiache njia na Petro hajui.

Ila anajiamini balaa!
Wakati hajui kinachoendelea.


UNAJIFUNZA KITU?

Kuna vijana ukikaa naye anakwambia mimi nataka kufuga kuku. Au kulima mananasi. Au kufanya biashara fulani. Lakini anaishia tu kujiamini sababu labda ana amepata mtaji wa pesa anadhani amemaliza kila kitu.
Au kwa sababu alifaulu Chuo kwenye masomo magumu anahisi hakuna ugumu tena zaidi ya ule.
Anahisi yeye noma.

Mimi nilipoanza nilikuwa nadhani kampuni yangu itasambaa nchi za jirani ndani ya miaka mitano tu. Lakini mpaka mwaka wa pili unafika bado tuna ofisi moja Mbezi Beach na hatuna mawazo ya kwenda hata Morogoro tu hapo. Hahaaaa. Stress za kutosha. Kujiamini bila maarifa ndo huko.

Stress zikianza unaanza kujiona mjinga. Umeajiri watu bila kuwa na KNOWLDEGDE ya kutosha ya mambo. Unazama nao kwenye maji.


BUT WHAT TO DO?

Bila Petro kupata msaada wa kuombewa na Yesu imani yake ingetindika HAKIKA.
Ama bila kuokolewa pale majini alipoanza kuzama story yake ingeishia pale.


WHEN A STUDENT IS READY....THE TEACHER WILL SHOW UP.

Msaada huwa upo tu always. Baada ya kuanza bila maarifa ilifikia hatua nikasema sasa nataka maarifa sahihi. Wachina wana msemo unaosema siku zote mwanafunzi akishakuwa tayari basi mwalimu huwa anatokea. So nilikutana na watu walionisaidia MAARIFA SAHIHI na hayo ndo yamenisaidia kusimama hadi leo.

Kama unataka kujifunza pia hasa kwa mtu unayeanza kufanya biashara njoo tuongee. Hakika hitakuwa bure. Utajifunza mengi ya kukufaa. Leo mimi najiamini kwa sababu ya maarifa siyo kwa kuwa nilifaulu darasani no. Nimejenga imani juu ya KNOWLEDGE SAHIHI. Thats why ninachokifanya sasa kimesimama miaka minne na kimeanza kuzaa MATUNDA mengine sasa.

Usifanye biashara tu kwa kuamini utafanikiwa. Watu wa Mungu wengi wanadhani kwa sababu ya kutoa zaka na kufunga sana ndo unaweza kuwa KICHWA na si mkia katika biashara. Uhalisia ni kwamba wanaoongoza kibiashara (vichwa) katika nchi nyingi wana MAARIFA na SKILLS (UJUZI) ambayo wewe unayefunga tatu kavu kila mwezi hujajishughulisha sana kuyapata. Kanuni inasema ukikosa maarifa #unaangamizwa. Full stop.

Vijana wengi wanaanza biashara kwa "MZUKA" tu. Wako very pumped up. Na wanaweza kutengeneza mpaka pesa za kupiga nazo picha. Wanahisi tayari wamefanikiwa. Lakini sustainable financial success hawaipati. Why? Hawatafuti maarifa sahihi.

Kama ilivyokuwa kwa Petro kufanya mambo kwa kujiamini tu bila maarifa kulimfanya asikitike sana imekuwaje akamkana Yesu tena hata baada ya kupewa warning! Kwamba ilikuwaje KUJIAMINI KOTE kukayeyuka tena mbele ya #kijakazi wa kike?

Inanikumbusha wanaume ambao huwa wanasema wao siku wakioa basi mwanamke hawezi kuwaambia kitu. Watafute baada ya kuoa utashangaa sana walivyo "wapole" mbele ya wake zao. Ishu ni kuwa waliamini CONFIDENCE zao kabla ya kupata maarifa kuhusu mambo ya ndoa yalivyo na dynamics za mahusiano zilivyo.



Biashara na ujasiriamali vinafanana na maisha ya ndoa tu in a way. Kuna dynamics zake. Usione ukadhani. Confidence zako ni nzuri  lakini ukifikiri kuwa ndo unachohitaji ili kudumisha ndoa unaweza kushangaa sana. Na ndivyo na ujasirimali ulivyo. Unahitaji MAARIFA SAHIHI.

Confidence zilimliza Petro na akajifunza.
Usije kupata stress zisizo za lazima katika safari yako ya ujasiriamali na biashara bure kisa hukutaka kujifunza vitu muhimu.

Karibu sana kujifunza kama utakuwa interested. Good luck God bless you always!


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni