Jumapili, 24 Desemba 2017

ARE YOU EDUCATED OR JUST SCHOOLED? UMEELIMIKA AU UMESOMA TU?



ARE YOU EDUCATED OR JUST SCHOOLED?
UMEELIMIKA AU UMESOMA TU?

Neno ELIMU kwa watu wengi linafungamanishwa sana na neno SHULE. Yaani kwa watu wengi inaonekana mtu aliyekwenda shuleni ndo mwenye elimu. Ndiyo maana utasikia watu wakisema “Aah huyo jamaa kaenda shule huyo usimchezee”, na vitu vya aina hiyo.
Lakini kuihalisia kitu hiki tunachoita ELIMU tunakuwa tukimaanisha tu MFUMO RASMI WA ELIMU ama kwa lugha ya kiingereza FORMAL EDUCATION.

Na KUELIMIKA mtu anaweza kuelimika akiwa hata darasani hajaenda. Tafsiri yetu ya elimu ndo inatufanya tuone kama kwenda darasani ndo kuelimika.

Mfumo huu ambao sisi tumeurithi hasa kutoka kwa wakoloni ni mfumo ambao ulianzishwa ukiwa na malengo yake. Mfano wakati ambapo jamii ya watu waliofanikiwa huko Ulaya ilihitaji watu wa kuwatunzia pesa zao ilibidi taaluma zinazoshughuklikia mambo hayo zianzishwe yaani watu wa kutunza fedha za wengine. Hivyo wakaanza kufundishwa taratibu za ukitaka utunze pesa za mtu vizuri unatakiwa ufanyeje. Na ili kuthibitisha kuwa umeelewa kweli unapewa mitihani na ukifaulu unapewa cheti cha kwenda kumwonyesha mwenye hela zake zinazohitaji kutunzwa anakupokea unaanza kumsaidia mambo ya mahesabu yake.

 Hivyo hivyo wakati watu waliofanikiwa walipohitaji mtu wa kusaidia wafanyakazi wa huyu tajiri waishi vizuri kwa maelewano nk ilibidi watu wanaoitwa leo “Human Resource personnels” waibuke kama taaluma mpya.
Wakati ambapo watu wa kusaidia mitandao ya matajiri iende sawa wameibuka watu wa IT nk kama taaluma mpya.

Kwa hiyo kimsingi mfumo huu wa elimu ulianzishwa kwa ajili ya kumsaidia mtu aliyefanikiwa kiuchumi kuweza kupata watu #sahihi wa kumsaidia mambo yake #kitaalamu. Na siyo hasa kumsaida mtu maskini ili awe tajiri. No. Na nasema NO kwa sababu njia ya mtu kuwa tajiri haihusiani na kusomea uhasibu au IT au sheria nk. Sasa inawezekana kabisa mtu akasomea hivyo vitu na akawa tajiri lakini hatakuwa tajiri kwa sababu amesomea hivyo vitu bali kwa kuwa licha ya kusomea hivyo vitu amejihusisha na mambo mengine sahihi yaliyompelekea kuwa tajiri which means huyo mtu hata asingesomea hivyo vitu angeweza tu kuwa tajiri.

Bahati mbaya sana mfumo rasmi wa elimu (yaani formal education) umeonekana kwa sasa kuwa ndiyo ELIMU YENYEWE. Hiyo nasema ni bahati mbaya kwa sababu inaonekana tumesahau nini hasa MAANA (yaani kazi) ya kitu kinachoitwa ELIMU.

Tukijikita kwenye kujua maana halisi ya ELIMU yaani KAZI ya elimu ni nini tunaweza kuona hasa kuwa watu #wengi tuliopitia mfumo huo rasmi wa vidato na madarasa basi TUMESOMA tu na HATUJAELIMIKA per se. Yaani we are just schooled but not really educated.

Bahati mbaya mtu ukiongea vitu vya namna hii unaonekana eti unaiponda “elimu”. Mi sipondi kitu, Naeleza UKWELI as ninavyouona. Unaweza kupima maneno yangu kwa mizani ukaona kama yako sawa au hayako sawa na ukiona cha kukusaidia chukua. Ukiona hakuna cha maana pia Merry Christmas!
Nimeamua kuandika haya baada ya kuwa nimeongea na vijana wengi mno hasa walioko vyuoni na kugundua kuwa kuna tatizo kubwa mno la kimtazamo (a serious mindset problem) na ni kubwa kiasi kwamba tusipokuwa makini tutajenga jamii based on a LIE. Haina tofauti na hela za wakati wa JK ambapo zilionekana za bwerere na watu kudhani hayo ndo mafanikio YENYEWE wakati UKWELI WA MAMBO ni kuwa kama taifa tulikuwa tunaelekea kule wanyama aina ya DINOSAURS walikoelekea.


KAZI YA ELIMU

Sasa kimsingi kazi ya elimu (yoyote ile) ni kumuwezesha huyo anayeipewa hiyo elimu kuweza kufanya haya mawili:

(a)KUTAMBUA (to identify )
(b) KUKABILI/KUTATUA (to handle)

Sasa ni kutambua na kukabili nini? Jibu ni #kutambua na #kukabiliana na mambo haya matatu:

1.       WAJIBU WAKE
2.       CHANGAMOTO ZAKE
3.       MAFANIKIO YAKE

Hiyo ndo kazi ya elimu na hivyo definition yoyote ya neno EDUCATION  haitakuwa na maana kama hai-address mambo hayo hapo juu. Kwa hiyo kwa kifupi kama elimu uliyonayo haikusaidii kutambua na kukabili WAJIBU wako, CHANGAMOTO zako na MAFANIKIO yako basi hicho unachokiita elimu ni USELESS.

MFANO HAI
Jana nilikutana na binti mmoja anasomea mambo ya UFAMASIA katika chuo kimoja hapa jijini Dar es Salaam. Katika kuongea naye nikamuomba anitajie RESPONDIBILITIES zake angalau 5 hadi 10 kama mwanafunzi. Yaani yeye kama mwanafunzi anawajibu wa kufanya nini na nini. Huwezi kuamini alishindwa. Ina maana hajui huyu mtu kuwa wajibu wake ni nini. Unatarajia huyu mtu uje umpe hata hiyo ajira atajua wajibu huko kweli?

Wengi wanaoitwa WASOMI hawajui wajibu wao kabisa. Ndiyo maana si ajabu kuona amegraduate na anadhani wajibu way yeye kupata ajira ni wa SERIKALI.
Na ukijaribu kumwambia otherwise hamtoelewana kabisa. Yeye anajua akimaliza chuo kuna AJIRA. Yaani huko duniani yeye anajua kuna watu wana WAJIBU wa kumpa yeye ajira. Kuna watu wa kumpa yeye pesa.

Ni kwa sababu ya MINDSET hiyo ndo maana huyu mtu anamaliza chuo kikuu na akitaka kutembeza hata hizo CV anaamini mwenye wajibu wa kumpa nauli ya kusambazia CV zake ni MZAZI au MLEZI. Yaani yeye anadhani kazi yake ni kusoma tu basi. Vingine ni wajibu wa wengine. This is the challenge I’m addressing hapa.

Kuna wasomi wanadhani hawajafanikiwa kwa sababu serikali iliyopo ni ya CCM ...huyo anaamini Chadema wakishika dola tu kila kitu kitakuwa kama Ulaya. Kuna wasomi wanaamini hawajafanikiwa kwa sababu ya wazazi kutowaandalia “mazingira mazuri”. Sijui ndo yakoje mazingira hayo mazuri… kama kijana kutoka Tandale ambaye maneno “PENS DOWN” huenda hakumbuki lini mara ya mwisho ameyasikia na sasa anasambaza karanga zake NCHI NZIMA hadi nchi jirani. Yes Diamond Karanga.


na wewe unazinunua. Hivi huyu aliandaliwa mazingira gani na wazazi. Wewe bado unaendelea kusikia "pens down" mpaka leo na unalaumu wazazi bado?

Wasomi wengi wakiwaza kuanza biashara wanalalamika hawana MTAJI. Mchungaji wangu jana Jumapili akihubiri kanisani akasema hivi:

“Kama unashindwa kuanza biashara kwa sababu umekosa mtaji wa laki tano tu, yaani KAMA UTASHINDWA kuyaendea mafanikio yako kwa sababu ulikosa laki tano basi HUJITAMBUI KABISA!!”

What a powerful statement of fact and naked truth that was!!
Sasa mwambie "msomi" wa leo sentensi kama hiyo uone hizo sababu milioni moja atakazokupa kukupinga.

Msomi wa leo anadhani wajibu wa kupata mtaji ni wa MZAZI WAKE au NDUGU. Yaani haoni jinsi gani yeye kama yeye anawajibika kuupata huo mtaji. Ukimwambia hivyo anasema basi ngoja nitafute AJIRA KWANZA. Akiikosa ajira analaumu system. Hilo ndo tatizo la kusoma bila kuelimika. Maana wasomi walioelimika wapo wengi tu na wamefanikiwa kupiga hatua...







Wasomi wengi leo ndo wanaongoza kuikosoa na hata kuitukana serikali kwenye mitandao ya kijamii kwa nini hawana ajira. Seriously?

Kazi ya elimu ni kukusaidia kuujua WAJIBU WAKO kama msomi. Kama unadhani nauli ya kusambazia CV ni wajibu wa mzazi wako hivi utaacha kudhani mtaji wa biashara yako ni wajibu wake pia?
Sadly hiyo ndo MINDSET ya jamii ya wasomi walio wengi. Who shall deliver us from that mess kama tusipofundishana ukweli?

Nimeeleza pia kuwa kazi ya elimu ni kukuasaidia KUTAMBUA NA KUKABILI changamoto zako. Your challenges. Na ndo hapo unapokuta msomi changamoto yake hajui kama ni yake au hataki kukubakli kuwa ni yake. Mfano changamoto ya nauli niliyoiainisha hapo juu. Kumbuka kuwa walimu wako wana wajibu wa kukufundisha yale waliyofundishwa kukufundisha. Get it? Kwa hiyo wanakufundisha kwa LIMITATIONS za mitaala. Ndo maana kuna mambo yanaitwa EXTRA CURRICULA ndugu yangu. Na ndo maana pia kuna elimu nje ya madarasa yako ya chuo. Mfano elimu ya ujasiriamali.

So ni wajibu WAKO kuitafuta hiyo elimu popote ilipo. Huo siyo wajibu wa lecturer wako. Siyo wajibu wa lecturer wako kukufundisha jinsi ya kutunza pesa zako maishani na kuziwekeza nk. Hayo mambo kasome vitabu vya kina Kiyosaki na kina JIM ROHN ujifundishe mwenyewe.


Kama hutaki au unaona USUMBUFU sawa tu ni mindset yako iko flawed so good luck. But ukifikiri kuwa kazi ya kukufundisha kuhusu mafanikio kifedha ni ya mwalimu wako wa Book Keeping au Commerce basi unapoteza muda wako. Huyo kazi yake ni kukusaidia kujua kuhusu mahesabu ya matajiri ukaajiriwe upate kuishi angalau. Jim Rohn alisema “FORMAL EDUCATION WILL MAKE YOU A LIVING BUT SELF EDUCATION WILL MAKE YOU A FORTUNE” akimaanisha elimu hii ya madarasani na vidato nk inaweza kukutengenezea kipato cha kuishi lakini ukitaka utajiri basi tafuta elimu ya kujifunza kivyako nje ya madarasa.


Hiyo ndo nayosema kuhusu kusoma vitabu na kuhudhuria semina mbali mbali nk. Huo ni wajibu WAKO. Kama ulikuwa hujui nakukumbusha.
Sasa elimu ya miaka 17 darasani toka ulivyoanza chekechea yaani vidudu

hadi chuo kikuu kama haiwezi kutengeneza nauli tu ya kusambazia CV hiyo ni USELESS EDUCATION hata kama ukijisikia vibaya ninaposema hivyo. Elimu ya miaka 17 mfululizo yenye notes na notes ma-counter book na ma-counter book quire 1 mpaka quire 4 kama haiwezi kukusaida kujiajiri hadi uanze kulalamikia SERIKALI ina maana elimu hiyo haijakusaidia kutatua changamoto zako mwenyewe then tunachoweza kusema kuhusu hiyo elimu ni kuwa that "education" is USELESS.

Elimu ambayo ukipata ajira halafu bahati mbaya ukaambiwa cheti chako ni feki licha ya kwamba elimu ndiyo unayo lakini hiki cheti ulichakachua halafu badala ya kusonga mbele unataka kuishtaki serikali na unaanza kulalamika kwenye Jamii Forums kwa nini umefukuzwa kazi ujue elimu hiyo unayodai unayo ni USELESS.

Elimu inapaswa kukufanya kuwa #RESOURCEFUL.

Mojawapo ya vitu ninavyofundisha my business associates kwa sasa ni hiki. Kuwa resourceful. Yaani kuwa na majawabu ya changamoto zako wakati wote. Siyo kulalamika na kulaumu. Kulalamika na kulaumu ni dalili ya kuwa na USELESS EDUCATION. Yes maana kama umefukuzwa kazi kihalali halafu huoni wapi pa kuanzia na unasema umesoma basi hiyo elimu ni USELESS. Yaani siyo USEFUL. Bora ungekaa nyumbani ukachunga ng’ombe ungekuwa mmiliki wa ng’ombe lukuki saivi.

Vijana wengi wa vyuo wako kwenye mitandao ya kijamii wanalalamikia vitu vya ajabu. Mtu yuko chuo cha SAUT Mwanza halafu unakuta ameandika comment ya kulaumu serikali kuhusu EXPANSION JOINTS za hostel za UDSM. Ok naelewa ni kutoa maoni. But huyu huyu mtu hapo alipo ukimuuliza wajibu wake ni upi na changamoto zake atakapomaliza masomo ni zipi na amejiandaa vipi kuzikabili majibu hana kabisa. Halafu anasema ana majibu kuhusu expansion joints. Hapo ana mwaka wa 14 toka aanze kusoma madarasani tangu chekechea. Kesho tena akisikia serikali imepiga mnada ng’ombe analalamika tena. Keshokutwa akisikia sijui mbunge gani kahama chama analalamika tena. Wajibu wake hajui. Hajui hata akigraduate hela ya kupigia picha za kumbukumbu ya graduation itatoka wapi yeye anajua tu hiyo ni changamoto ya watu wengine yeye kazi yake ni kutoa maoni facebook na kutuma vikatuni WhatsApp. Badala muda huo angeutumia kusoma vitu vingine vya kimaisha na kupata maarifa na ujuzi wa KUPAMBANA NA HALI YAKE YA BAADAYE yeye haoni hilo. Mwisho elimu yake yote inakuwa USELESS tu.

Mnawapa wazazi wenu stress zisizo za msingi kwa sababu ya kutotambua wajibu wenu mapema. Unagraduate mzazi au mlezi badala apumzike but ndo anawaza kukupa tena nauli maana boom huna tena. Mzazi au mlezi anawaza kukulisha na kukuvisha na kukulipia umeme maji nk. Bado hata kuomba Mungu upige hatua huombi mzazi ndo apige magoti kukuombea. Hivi hiyo elimu kazi yake nini? That is why nikauliza UMEELIMIKA AU UMESOMA TU? ARE YOU REALLY EDUCATED OR JUST SCHOOLED?

Joho la graduation litakuwa na maana sana kama unaweza kutatua changamoto na kutimiza wajibu wako. Otherwise halina tofauti na dera tu!

Wasomi ambao ni just schooled hata wakienda serikalini au bungeni hawako RESOURCEFUL. Tatizo la jimboni kwake ambalo lingetakiwa akae na wananchi wake na madiwani wakalitatue na ingewezekana kabisa lakini yeye analipeleka Facebook kulalamikia serikali. Huyo elimu yake ni USELESS. Hawa ndo wabunge wasio na MAJIBU bali ni kulaumu na kulalamika from January to DECEMBER halafu January mosi wanaandika HAPPY NEW YEAR. Then wanaanza tena kulalamika!

Laiti kama wasomi wangetambua wajibu wao na kubuni njia za kutatua changamoto zao wenyewe kwanza sidhani kama nchi hii ingekuwa na changamoto zilizopo leo. Maana licha ya kuwa wasomi ni wachache lakini kama wakiwa na impact nzuri basi CHACHU KIDOGO ITACHACHUA DONGE ZIMA.

Binafsi niliona kuwa naweza kuchangia kwa kubadili fikra za vijana hasa walioko vyuoni bado ili waanze kujifunza jinsi ya kuwa RESOURCEFUL wao kwanza. Maana kama atamaliza chuo halafu elimu ya chekechea hadi chuo kikuu haiwezi kumzalishia nauli ya daladala sh 600/- mpaka apewe, sasa huyu ataweza kutatua changamoto za taifa lake kweli?

Hawa ndo wanawaza kuingia duniani kama ABIRIA. Yani anataka abebwe na mfumo. Akute nauli zipo, akute ajira zipo akute mishahara ni minono akitaka kuanza biashara akute mitaji ipo tu hapo inamngoja. Passenger mindset. (Makala inayofuata nitazungumzia hili. Be ready). Kwa kifupi elimu imemfanya asiweze kabisa KUFIKIRIA. And so imekuwa kwake ni useless education.

Elimu ikiwa useless haitakusaidia hata KUTAMBUA na KUHANDLE mafanikio yako. Kuna wasomi wengi walipata nyadhifa kubwa na kwa kuwa wana elimu ambayo huwa haimuandai mtu kujua kama sasa ndo kafanikiwa au la basi wamejikuta wakitolewa kwenye nyadhifa zao bila kutarajia. Ndo unashangaa mtu anatolewa kwenye uwaziri analalamika. Huyo elimu yake imekuwa useless kwake. Na ijapokuwa bado anaweza kuonekana yupo juu kimaisha lakini ni kwamba alishindwa kutambua kuwa sasa amefanikiwa na afanyeje ili mafanikio hayo yadumu – come what may, yaani afanyeje ili awe INDISPENSABLE. Nawafananisha na kijana mwanamuziki aliyetamba sana enzi hizo Mr. Nice ambaye bila shaka wakati ule hakujua kuwa ndo ilikuwa peak yake ya mafanikio na wengine wengi ambao leo wanaweza kuwa wanapitia kipindi kigumu kiuchumi na hawajui kilichotokea ni nini.

Elimu inapaswa ikufanye utambue kuwa sasa hapa ndo kilele cha mafanikio yangu kwa NJIA HII niliyoichagua mimi na ikusaidie kuhandle hiyo success yako.
Kuna wasomi wengi wazuri wamestaafu lakini huwezi kufananisha kiwango cha ELIMU yao na maisha yao ya kustaafu.

So sad, but so true.

Hapo ndo unaona tofauti ya SCHOOLING na REAL EDUCATION. Ngoja nikupe kashule kadogo tena hapa. Ni hivi kuna aina kadhaa za elimu:

1.       LITERACY EDUCATION.
Hapa unaandaliwa kujua kusoma na kuandika na kwa dunia ya leo na kuwa computer literate pia.. na ukishajua hayo unaanza kufundishwa mambo ya msingi kama URAIA, LUGHA, SAYANSI kidogo, HISTORIA nk. Hii hapa kwetu inaanza chekechea hadi High School. Miaka 14. Imagine!!

2.       PROFESSIONAL EDUCATION
Hii sasa ndo wanataka uwe MTAALAMU labda wa sheria, au wa utabibu, au ualimu au uhandisi nk. Hii ndo unapata vyuoni sasa. Miaka mitatu minne hadi mitano (mfano kwa madaktari).

3.       FINANCIAL EDUCATION
Hii ni elimu ya mafanikio kifedha hufundishwi shuleni hii.
Hii ndo unapaswa kutafuta mwenyewe sasa. Kwenye semina sijui Mwakasege anafundisha kuhusu fedha go and listen. Sijui James Mwang’amba anafundisha kuhusu uchumi nenda kajifunze au pata vitabu vyake. Sijui kaja Strive Masiyiwa kutoka Zimbabwe nenda kajifunze. Sasa kama wewe unataka tu matamasha-tamasha halafu vitu kama hivi hutaki basi bado hujatambua WAJIBU wako vizuri.

Sasa imagine ndo hujapata hii elimu ya tatu halafu umeajiriwa hadi ukastaafu… unadhani kitatokea nini hapo? Si ndo una miaka 60 ndo unawaza kuanza mradi wa kufyatua matofali mara mafundi wachakachue ule hasara mara roli lako la mchanga limekamatwa na nyara za serikali kwenye mchanga wako. Kwa sababu ya umri changamoto kama hizo zinakulemea kirahisi. Au ndo unaanza kuwaza kufuga kuku mara wanakufa na huku una mtoto yuko Chuo Kikuu naye hajitambui bado mpaka nauli anakuomba wewe mstaafu. Huku unasikia raisi kwenye TV anasema vyuma vitakaza hadi vitavunjika! Unaiangalia TV hata hujui uifanyeje.

Hiyo ndo hatari ya kufikiri hizo elimu za namba 1 na 2 zimekutosha kwa kuwa unapata mshahara ukasahau kuwa huna elimu namba 3 kwa kiwango kinachotakikana!

SO WHAT NOW?

Well..

Let’s be a bit practical now, shall we?

Kama wewe ni msomi especially kama bado upo masomoni hasa vyuoni basi angalia elimu yako mpaka sasa kama inaweza kukusaidia kupata vitu vifuatavyo bila kuajiriwa:

1.       Kodi ya nyumba angalau miezi sita.
Yaani hapo ulipo chuoni kwa elimu uliyowahi kupata toka chekechea hadi hapo ulipo sasa je unaweza kuitumia hiyo elimu bila kuajiriwa na ukazalisha kodi ya nyumba kwa miezi sita angalau? Kama huwezi basi elimu hiyo ya miaka 14 au zaidi mpaka sasa ni USELESS. Do something fast.

2.       Chakuka angalau cha wiki mbili mbele.
 Je elimu uliyonayo hadi sasa minus ajira inaweza kukufanya ukasurvive kwa upande wa kula kwa angalau wiki mbili mbele? Yani bila boom wala bila kuajiriwa wala bila kupewa hela na mtu. Wewe utumie elimu yako kugenerate income ya chakula. If not it is USELESS

3.       Vocha angalau mwezi mmoja.
Najua mawasiliano ni muhimu. Je elimu yako yaweza kukusaidia pia kutengeneza hela ya vocha kwa mwezi mmoja anagalau?

4.       Transport.
Je elimu uliyo nayo tukakuweka nayo mtaani utaweza kuzalisha nauli angalau nauli ya hata nusu mwezi bila kuomba mzazi?

5.       Mavazi.
Unaweza kuvaa nguo hizo hizo ukitaka but ukitamani kuvaa vizuri elimu uliyonayo unaweza kuigeuza pesa na ikakupa mavazi supposing kwamba ajira hupati wala hakuna wa kukupa?

See… najaribu tu kukusaidia kutambua kuwa hayo mambo ni WAJIBU WAKO. Na wewe kama msomi unapaswa kuwa mfano kwa ambao wanaitwa siyo wasomi. Sasa kama majibu yako hapo juu ni HAPANA kwa maswali yote hayo matano halafu bado unapoteza muda kwenye mitandao ya kijamii kuLIKE picha za Hamisa Mabeto na Zari au kubadili kwa nini watu wanahama vyama basi kuna tatizo kubwa kuanzia kwenye shingo yako kwenda juu!

Huwezi kuwa huna majibu ya maswali hayo hasa wewe msomi ambaye bado upo chuoni na bado hutaki kujifunza mambo EXTRA CURRICULA ya kukusaida kuanza mchakato wa kuwa msomi mwenye elimu USEFUL. Tambua wajibu wako, tambua changamoto zako, tambua mafanikio yako.
Hapo utakuwa UMEELIMIKA hakika.

Mtu aliyesoma tu anaweza kulalamika lakini mtu aliyeelimika anatoa majawabu ya changamoto. Mtu aliyesoma tu ana vitu vingi kichwani ambavyo havimsaidii yeye wala watu wanaomzunguka. Kichwa chake always kikiona changamoto kinajishughulisha na kutafuta nani wa kulaumu. Kichwa cha mtu aliyeelimika (BILA KUJALI KAISHIA DARASA LA PILI AU KAFIKA CHUO KIKUU PIA) kinajishughulisha na kutafuta njia ya kutatua changamoto ya kwake au za watu wengine kabisa. Ndo maana watu wamegundua M-PESA kutatua matatizo ya watu wengine badala ya kulalamikia foleni za benki kila siku. Hiyo ndo namaanisha kuwa #resourceful.

Bottomline: Never complain.

If you are not solving the problem you are not being helpful.


  1. Be EDUCATED, not just SCHOOLED.

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
WhatsAPP +255 788 366 511
Merry Christmas!

Jumanne, 12 Desemba 2017

CONFIDENCE WITHOUT KNOWLEDGE: LEARN FROM SIMON PETER (KUJIAMINI BILA MAARIFA: JIFUNZE KWA SIMON PETRO)


*****
Naongelea biashara na ujasiriamali.
*****

Shalom!

Namshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuwa pamoja tena. Nawapenda sana.

Leo tujifunze pia jambo jingine muhimu katika ulimwengu wa biashara na ujasiriamali.

Katika kusoma Biblia ukikutana na habari za mtu aitwaye Petro aliyekuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu unaweza ukahisi huenda jamaa alikuwa kimbelembele sana.

Kwanza alipenda sana kujibu maswali kabla ya wengine. Ilikuwa ni kama tabia hivi.

Pili alipenda kutoa suggestions bila kuuliza wenzake wala nini. Mfano pale mlimani alipomwambia Yesu: "ukitaka NITAJENGA vibanda vitatu..."
(Mathayo 17:4)

Yaani anasema NITAJENGA wakati pale yuko na wenzake wawili. Kuna watu wanadhani alipanic labda. Lakini kama nilivyosema ukisoma habari zake zote utajua ilikuwa kama tabia yake pia kutaka kuwa tofauti.

Tatu alikuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu papo kwa hapo bila kuuliza mtu. Mfano alivyomkata mtu sikio akijaribu kuzuia Yesu asikamatwe.
(Yohana 18:10)

Nne alikuwa anaweza kutaka afanyiwe kitu cha tofauti na wengine bila kuhofia watawazaje kuhusu yeye.  Mfano kukataa kuoshwa miguu kisha "alipopigwa mkwara" akaona isiwe tabu wala nini ila kama vipi basi aoshwe na kichwani na mikono siyo miguu tu!
(Yohana 13:9)

Kwa kifupi wengine wanaweza kusema labda Petro alikuwa akifanya vitu kwa kukurupuka!

Lakini ukichunguza hayo mambo niliyoyataja na ukachunguza namna alivyokuwa akifanya mambo yake na ukizingatia kazi aliyokuwa akiifanya maishani kabla ya kumfuata Yesu (yaani UVUVI); unaweza kutambua kuwa Petro alikuwa mtu mwenye KUJIAMINI kupita kiasi. Uvuvi si kazi nyepesi. Kukaa macho usiku baharini mara mvua mara mawimbi tena uko kwenye kachombo kadogo lazima uwe ngangari! Kwa hiyo jamaa alikuwa anajiamini sana.


KUJIAMINI KWA PETRO

Na unaweza ukaona kujiamini huko wakati Yesu alipotokea juu ya maji halafu Petro akamwambia Yesu kama ni wewe kweli hebu niamuru na mimi nitembee juu ya maji! Yesu alipompa go-ahead jamaa hakufikiria mara mbili akatoka chomboni na kutembea juu ya maji! Aisee. Usifikiri ilikuwa rahisi. Ilikuwa ni confidence kubwa sana.
(Mathayo 14:29)


Ilikuwa tabia yake kabla hata ya kuongelea imani. Na Yesu alichagua WAVUVI makusudi akijua hawa siku wakielewa somo watapiga kazi bila woga. So Petro kwa confidence ileile akaingia baharini akitembea JUU YA MAJI pia.

Lakini mfano wa pili kusisitiza nature yake ya kujiamini kupita kiasi ilikuwa wakati Yesu alipowatabiria kuwa watamkimbia wote. Petro akasema (natumia maneno yangu hapa:) "AH WAPI..! LABDA HAWA WAOGA WAOGA. SIYO MIMI WEWEE. MIMI!?? MIMI BANA HATA KUFA NA WEWE NITAKUFA NA WEWE HATA WAKIKIMBIA WOTE HAWA! WE HUNIJUI KUMBE?"
(Story nzima pale Marko 14:29-30 uone maneno yake mwenyewe)


TATIZO LA PETRO

Lakini kumbe Petro alikuwa anajiamini YEYE KAMA YEYE. Yaani aliamini uwezo wake wa kuhimili mambo ya siku zote akasahau kuwa sasa alikuwa katika BUSINESS MPYA ambayo ilihitaji maarifa mapya ambayo alikuwa HANA!


MIMI NA WEWE

Hivyo ndivyo watu wengi tulivyo. Tunajiamini bila maarifa sahihi. Matokeo inakuwa ni DISASTER ingawa kwa neema ya Mungu tunasonga mbele.

Mojawapo ya kitu nilichoweka katika kitabu changu kitakachowajia baadaye ni kuwa wakati nilipoacha kazi ili kuanza safari ya kibiashara na ujasiriamali miaka kadhaa iliyopita nilikuwa najiamini kweli kweli!  Yaani ungenikuta wakati ule "ungenipisha njia" tu utake usitake. Nilikuwa najua mi noma. Nilikuwa najiamini kuwa kila kitu kitaenda sawa tu. Ndo maana nilikuwa tayari kushuka chomboni (ajira) na kutembea juu ya maji  (ujasiriamali). Na nikawa nasema yani mimi hata kampuni yangu isipoenda vizuri "Nitakomaa mpaka kieleweke tu maana mi noma."

Lakini kumbe nilikuwa natembea katika ujinga  (IGNORANCE) uleule wa ndugu yetu Petro tu, wa kujiamini bila kuwa na MAARIFA SAHIHI. Miaka miwili tu baada ya kuanzisha kampuni yangu nilikuwa na changamoto nyingi mno tofauti na nilivyokuwa nimetarajia. Nilijikuta ni wakati wa kulipa kodi na pesa hakuna, nilikuwa na wateja kadhaa lakini hawakuwa wakilipa kwa wakati na wengine kutolipa kabisa tofauti na matarajio yangu. Wafanyakazi wanahitaji mishahara inabidi nikope pesa kwa rafiki zangu kulipa baadhi ya mishahara nikitarajia wateja wakilipa nitarejesha. Wateja hawakulipa! Nina madeni. Ninadai watu pia. Nikajikuta ninapata stress ambayo sikuwahi kufikiria ingewahi kuwa hivyo. Hapo nikama nishatembea juu ya maji sasa uhalisia umetokelezea kuwa kumbe sijawa tayari kutembea juu ya maki kama nilivyodhani. Nilipata chest pains ambazo zilinipeleka Muhimbili bila kutarajia kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Hizo ni baadhi tu ya changamoto ambazo naweza kusema kwa sasa. Ziko nyingi.

Hii historia yangu kila mara huwa inanikumbusha ile story ya Petro alivyoanza kutembea juu ya maji kabla hajapata maarifa sahihi kuhusiana na IMANI YAKE. Alianza kuzama maana mashaka yaliibuka.

Hakuwa na maarifa sahihi kwa nini WENGINE (Yesu) waliweza kutembea juu ya maji.


UNATARAJIA KUANZA BIASHARA? JIFUNZE HAPA

Nimekuwa nikikutana na vijana mbali mbali everyday kuongea nao kuhusu biashara na ujasiriamali. Wengi wao hawana tofauti sana na Petro kwa mantiki hiyo niliyoieleza. Kama ilivyokuwa kwangu wakati naanza pia. Vijana wengi wanadhani mafanikio ni kama kutuma 'SMS'. Kwamba unatype tu kidogo kisha unabonyeza SEND afu tayari. Ndo maana wamekuwa WALEVI WA BETTING.

Ukweli ni kwamba mafanikio hasa katika biashara na ujasiriamali yanahitaji kupata MAARIFA sahihi ya kitu unachotaka kufanya. Kujiamini ni kuzuri lakini kudhani kuwa kujiamini kwako ndo kutaleta mpenyo kibiashara bila kuwa na maarifa sahihi ni kachumbari ya disaster! Biblia inasema Watu #wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA! Umeona ee?

So bila msaada sahihi UTAANGAMIA KIBIASHARA. Utasingizia biashara yako imerogwa na shangazi au na mpemba au shetani ameiinukia kumbe shetani yuko zake Brazil huko ni wewe tu huna maarifa sahihi. (Shetani hana uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja...he is not omnipresent).
Maarifa rafiki.
Kuwa mtu wa kufundishika.


Miezi kadhaa iliyopita niliandika makala iliyosema ukitaka kufanikiwa kibiashara epuka pesa za NDUGU, MARAFIKI na MAJIRANI. Na nikaeleza sababu na kutoa mifano. Nashukuru iliwasaidia watu wengi mno kupata maarifa SAHIHI kuhusu eneo la wateja na sasa wanasonga mbele.
Maarifa ni muhimu usijiamini tu ukaishia hapo.


MWONE PETRO TENA

Wakati Yesu anasema wote watamkimbia na Yesu akijua kuwa Petro kwa kujiamini kwake atasema YEYE HATOFANYA HIVYO. Yesu akaona amsaidie Petro maarifa kiduchu ya kumsaidia. Akamwambia Simoni "Shetani amewataka ninyi (ni kama ameomba ruhusa) apate kuwapepeta kama vile ngano lakini ninekuombea wewe ili imani yako isitindike"
(Luka 22:31 na kuendelea)

Lakini kwa kujiamini zaidi ndo hapo Petro akasema hatamwacha Yesu hata baada ya kupata information ambayo alikuwa hana.

Kumbe!

Yesu alitaka kumwonyesha Petro kuwa kujiamini kwako kutakwama tu mahali maana kuna vitu bado hujui. Na kama huamini ngoja uone muda wa jogoo kuwika ukifika kabla hajawika utakuwa umeshanikana mara tatu wewe huyo huyo.

Kumbe shetani alikuwa na ruhusa ya kuwapepeta kina Petro na Petro hajui.

Kumbe Yesu alikuwa ameshamwombea Petro ili asiache njia na Petro hajui.

Ila anajiamini balaa!
Wakati hajui kinachoendelea.


UNAJIFUNZA KITU?

Kuna vijana ukikaa naye anakwambia mimi nataka kufuga kuku. Au kulima mananasi. Au kufanya biashara fulani. Lakini anaishia tu kujiamini sababu labda ana amepata mtaji wa pesa anadhani amemaliza kila kitu.
Au kwa sababu alifaulu Chuo kwenye masomo magumu anahisi hakuna ugumu tena zaidi ya ule.
Anahisi yeye noma.

Mimi nilipoanza nilikuwa nadhani kampuni yangu itasambaa nchi za jirani ndani ya miaka mitano tu. Lakini mpaka mwaka wa pili unafika bado tuna ofisi moja Mbezi Beach na hatuna mawazo ya kwenda hata Morogoro tu hapo. Hahaaaa. Stress za kutosha. Kujiamini bila maarifa ndo huko.

Stress zikianza unaanza kujiona mjinga. Umeajiri watu bila kuwa na KNOWLDEGDE ya kutosha ya mambo. Unazama nao kwenye maji.


BUT WHAT TO DO?

Bila Petro kupata msaada wa kuombewa na Yesu imani yake ingetindika HAKIKA.
Ama bila kuokolewa pale majini alipoanza kuzama story yake ingeishia pale.


WHEN A STUDENT IS READY....THE TEACHER WILL SHOW UP.

Msaada huwa upo tu always. Baada ya kuanza bila maarifa ilifikia hatua nikasema sasa nataka maarifa sahihi. Wachina wana msemo unaosema siku zote mwanafunzi akishakuwa tayari basi mwalimu huwa anatokea. So nilikutana na watu walionisaidia MAARIFA SAHIHI na hayo ndo yamenisaidia kusimama hadi leo.

Kama unataka kujifunza pia hasa kwa mtu unayeanza kufanya biashara njoo tuongee. Hakika hitakuwa bure. Utajifunza mengi ya kukufaa. Leo mimi najiamini kwa sababu ya maarifa siyo kwa kuwa nilifaulu darasani no. Nimejenga imani juu ya KNOWLEDGE SAHIHI. Thats why ninachokifanya sasa kimesimama miaka minne na kimeanza kuzaa MATUNDA mengine sasa.

Usifanye biashara tu kwa kuamini utafanikiwa. Watu wa Mungu wengi wanadhani kwa sababu ya kutoa zaka na kufunga sana ndo unaweza kuwa KICHWA na si mkia katika biashara. Uhalisia ni kwamba wanaoongoza kibiashara (vichwa) katika nchi nyingi wana MAARIFA na SKILLS (UJUZI) ambayo wewe unayefunga tatu kavu kila mwezi hujajishughulisha sana kuyapata. Kanuni inasema ukikosa maarifa #unaangamizwa. Full stop.

Vijana wengi wanaanza biashara kwa "MZUKA" tu. Wako very pumped up. Na wanaweza kutengeneza mpaka pesa za kupiga nazo picha. Wanahisi tayari wamefanikiwa. Lakini sustainable financial success hawaipati. Why? Hawatafuti maarifa sahihi.

Kama ilivyokuwa kwa Petro kufanya mambo kwa kujiamini tu bila maarifa kulimfanya asikitike sana imekuwaje akamkana Yesu tena hata baada ya kupewa warning! Kwamba ilikuwaje KUJIAMINI KOTE kukayeyuka tena mbele ya #kijakazi wa kike?

Inanikumbusha wanaume ambao huwa wanasema wao siku wakioa basi mwanamke hawezi kuwaambia kitu. Watafute baada ya kuoa utashangaa sana walivyo "wapole" mbele ya wake zao. Ishu ni kuwa waliamini CONFIDENCE zao kabla ya kupata maarifa kuhusu mambo ya ndoa yalivyo na dynamics za mahusiano zilivyo.



Biashara na ujasiriamali vinafanana na maisha ya ndoa tu in a way. Kuna dynamics zake. Usione ukadhani. Confidence zako ni nzuri  lakini ukifikiri kuwa ndo unachohitaji ili kudumisha ndoa unaweza kushangaa sana. Na ndivyo na ujasirimali ulivyo. Unahitaji MAARIFA SAHIHI.

Confidence zilimliza Petro na akajifunza.
Usije kupata stress zisizo za lazima katika safari yako ya ujasiriamali na biashara bure kisa hukutaka kujifunza vitu muhimu.

Karibu sana kujifunza kama utakuwa interested. Good luck God bless you always!


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511

Alhamisi, 12 Oktoba 2017

WEWE PIA ULIFUNDISHWA KUTAFUTA THAMANI YA "X"?



Mungu ni mwema tunakutana tena. Leo naanza na swali la mathematics kutukumbusha tulikotoka! Hahaaa wale wenzangu HGL na KLF tupo?

::::::::::::::::::::::::::::::::

SWALI:

X + (1⁄2)X + 1 = 100

Tafuta thamani ya X

::::::::::::::::::::::::::::::::

Kuna makundi mawili ya watu hapa. Kuna kundi ambalo swali hilo hapo juu nyuso zitakunjamana kwa kujaribu kufikicha akili. Tutaanza kujiuliza tena nani kachanganya hiyo herufi na hizo namba tena. Kisha tutajiuliza tena sasa hii "X" naanzaje kutafuta thamani yake na kujaribu kukumbuka siku mwalimu anafundisha hivyo vitu alivaa shati gani. Na hivi MAGAZIJUTO inamaanisha nini vile?

Kifupi tutatumia muda mwingi kufikiria kuhusu swali kuliko kutafuta jibu. Na pengine tutapotezea tu.

Lakini kuna baadhi yetu nyuso zitakuwa na tabasamu hata sasa hivi walivyoona hilo swali. Wanakumbuka mbali sana. Watakumbuka walivyokuwa wanafurahi kupata mtihani wenye maswali "marahisi rahisi" kama haya. Kwenye mtihani wa hesabu hao ndo walikuwa wanaweza kukufanya ukapanic kama wamekaa pembeni yako wewe unayejiuliza kwa nini wamechanganya herufi na namba kwenye swali moja.

Na sasa hivi hapa wanaweza kuwa washakokotoa thamani ya X kwenye hilo swali na wameshaipata siku nyiingi wakati sisi wengine tulivoona tu swali tumepata allergy reactions tofauti tofauti.

Huko ndiko tulikotoka. Kwa nia njema kabisa ya watunga mitaala ya kutusaidia kufikirisha bongo zetu vizuri walihakikisha maswali kama hayo ni sehemu ya mafunzo yetu. Tulikaa muda mwingi tukifundishwa vitu vya aina hii.

Lakini sasa wote tupo kapu moja. Ndo maana sasa naomba ujiulize... Ni wapi uliwahi kufundishwa KUTAFUTA THAMANI YAKO MWENYEWE?

Yes, lini uliwahi kufundishwa kuhusu kutafuta thamani yako mwenyewe? Wewe ni nani?



Kwa wengi hilo bado.

Na kukosekana kwa fursa hiyo kumefanya watu wengi kuishi kwa kutafuta thamani ya VITU VINGINE (thamani ya X) badala ya kutafuta thamani yao wenyewe.

Tunaishi kwenye dunia ya watu ambao wanachojua ni kutafuta thamani ya X. Hawajui thamani yao wenyewe na hivyo ili kuondoa hali ya kutothaminika wanajifungamanisha na X. Kuna ambao X yao imekuwa ni magari na majumba. Ndo wanachotafuta. Wakikipata wanagundua kuna kitu bado hakiko sawa.


Kuna ambao X yao ni kujua kuongea kiingereza. Kuna ambao X ni kupata elimu ya "juu".


Wakiipata wanagundua kiukweli kwamba hiyo kumbe siyo kila kitu. Lakini wakati wanaitafuta usijaribu kuwaambia kitu kingine. Wana apply MAGAZIJUTO.

Hivi karibuni nikakutana na binti mmoja amejaribu kuapply chuo mwaka jana akakosa. Mwaka huu pia amejaribu akakosa. Akanipigia kuomba ushauri kuwa anasikitika wenzake wanapiga hatua yeye yuko tu pale pale. Nikamuuliza maswali machache na kugundua anafikiri thamani yake ipo kwenye elimu ya "juu".

Lakini uzoefu unaonyesha otherwise.
Mfano. Katika vijana wa kiume wenye thamani katika kuitangaza nchi hii yumo Mbwana Samatta na Diamond Platnumz.



Ukijumlisha elimu ya darasani ya hao wote wawili ni ndogo kuliko wengi wetu. Lakini VALUE zetu katika jamii je? Thamani ya mmoja wa hao vijana Mungu aliiweka kwenye KOO na ya mwingine Mungu aliiweka kwenye MIGUU. Kuna watu wana degree nyingi mno nchi hii lakini  thamani ya mchango wao kwa taifa HUENDA haifiki hata nusu ya ile ya Mbwana Samatta tu.

Nikamuuliza binti yule. "Unadhani Mungu alikuumba uje ufanye nini duniani?". Akasema "kwa kweli sijui kakangu". Nikamwambia basi acha kwanza kutafuta THAMANI YA X tafuta kwanza kujua thamani yako Mungu aliiweka wapi.  Akaomba nimpe wiki moja kujitafuta vizuri. Namwonbea Mungu amsaidie kujua wapi thamani yao ipo.

Kuna watu wamesoma hadi chuo kikuu lakini thamani yao imekuwa kuwa MC. Kusherehesha. Basi.
Cha ajabu kuna watu hawana degree lakini thamani yao imekuwa kwenye KUFUNDISHA. Hebu tafakari mtu kama Eric Shigongo mpaka sasa ameshafundisha vijana wangapi?


Lakini kuna watu wana Ph.Ds na kumfundisha mtu kuhusu maisha ya kawaida tu ni shida. Why? Huyu wa PhD huenda thamani yake iko kwenye USHAURI au UTAFITI. Siyo kufundisha.

So unatakiwa ujifunze kuangalia wapi Mungu aliweka TALANTA zako. Na ni ngapi alikupa. Tafuta thamani yako. Achana na kutafuta thamani ya vitu vingine ambavyo unahisi vitakupa furaha lakini mwishoni mwa maisha yako utagundua huna furaha tena na wakati vitu ulivyotafuta unavyo tayari tena vingi. Maisha halisi ni kuishi kwa kutambua thamani yako.

Kutojua thamani kumewafanya mabinti wakatoa rushwa ya ngono kwa kisingizio cha kusaidiwa ajira. Hujajua thamani yako halisi my sister. Kutojua thamani zao kumewafanya mabinti wengine kutamani kuolewa na watu wenye mali na uwezo badala ya kutafuta kuolewa na mtu aliyeumbwa kuja kuwa mume wake.

Kutojua thamani yao kumewafanya vijana wa kiume kutamani kuwa na  girlfriend au mke mwenye shepu nzuri bila kujali ni nini analeta kwenye maisha yake. Wake wengi za matajiri siyo wenye mishepu ya kutisha kama unayoona kwenye TV. Na hata kama ni mwenye hiyo shepu basi kuna kitu cha ziada kichwani. Hili ni gumu kukubalika na ni sababu tulifundishwa kutafuta thamani ya X. Thamani yetu tunafikiri ipo kwenye kufanikiwa kupata thamani ya X. Thamani yetu tunafikiri ipo kwenyei aina ya vitu au watu tulionao.

Kuna watu wanaona kuwa wao ni wa thamani sasa kwa kuwa mume au mke amekuwa WAZIRI. Wanaamini katika thamani ya X. Ulishaona picha ya Michelle Obama na mumewe wakati Obama si "lolote" machoni pa watu? Lakini mwanamke yule alijua ana nini. Akajua kuwa yeye ni FIRST LADY. Alipokuwa akimuona Obama haoni future president anaona MUME WA FIRST LADY MTARAJIWA.
Dada unanielewa?


Sasa wewe mumeo akipewa cheo serikalini unaanza kujitambulisha kama mke wa waziri wa..... Hawa ndo wanawake waliokuwa wanatisha polisi njiani. Eti unajua mi ni nani? Ngoja nimpigie mume wangu sasa. See? Huyu anahisi thamani yake iko katika cheo cha mumewe. Na ndo maana cheo cha mumewe kikikoma anakuwa kama mtu asiye na thamani hata akipita barabarani.

Namheshimu sana dada anaitwa Hoyce Temu. Huyu anajua thamani yake. Amesimama kama yeye. Niliwahi kufanya kazi na kijana anaitwa JACOB MSEKWA yaani huyu jamaa hakuwa na maisha ya kujiweka kama "mtoto wa......". Huyu jamaa alinifundisha kitu kikubwa sana. Alijinasibu kwa utendaji wake wa kazi kiasi kwamba jina la Baba yake halikupewa nafasi kabisa. Alikuwa yeye kama yeye. Lakini ofisi hiyo hiyo kulikuwa na watoto wengine wa "wakubwa" ambao kitu pekee kikubwa kilichowatambulisha ni jina la baba. Walipewa heshima na nidhamu ya woga kwa sababu tu ya nafasi ya mzazi.
So sad.

Pia niliwahi kufanya kazi na dada mmoja anaitwa Madeleine.. huyu ni binti wa  Kimei. Alikuwa akipiga kazi na kujituma pengine kuliko sisi wengine tuliotokea familia "duni". Usingeweza kudhani huyu ni binti wa Kimei kwa hali ya kawaida ya kitanzania. Anajua thamani yake haiko katika jina la  Baba yake. Sitamsahau pia huyu. Lakini wengine unakuta ni mpwa sijui wa mkuu wa kituo cha polisi tu lakini weee mwambie kitu uone.

Na mpaka leo tuna viongozi ambao uongozi wao hauna kitu. Kinachowabeba ni jina alilojenga baba kwa miaka mingi. Basi. Hawakutaka kutafuta thamani yao wao kama wao.
Najua unawajua.

Kutojua thamani zetu ndo kumefanya baadhi yetu kutafuta kwa bidii kuishi Ulaya au Marekani ili tukiongea tusikilizwe. Tusiposikilizwa inatusumbua kweli. Kumbe tunashindwa kujua kuwa thamani yetu haiko kwenye kuishi kwetu Ulaya per se ipo kwenye vitu ambavyo Mungu aliwekeza (invest) ndani yetu. Labda uliwekewa kufundisha kama kina sisi. Labda kuchora kama Masoud Kipanya. Labda kuigiza kama marehemu Kanumba. Au uongozi kama mwalimu Nyerere. Ukiishi thamani yako halisi hata ukifa utasikilizwa. Yani watu wanataka kubadili katiba miaka mingi baada ya kufa kwako lakini bado wanasikiliza kwanza hotuba zako kutafuta ushauri.
Can you imagine?

Usipoishi thamani yako ukafikiri thamani yako ni kuoa mke MKALI au kuolewa na BONGE LA BWANA au ni kupata Masters au kuishi Marekani utashangaa unavyo hivyo lakini bado huthaminiki kivile. Utashangaa Diamond akichepuka inakuwa story hadi BBC wakati wewe hata ufanye nini hakuna anayetaka kujua. Diamond angekuwa mhasibu wa Vodacom leo hii angekuwa na hela nzuri tu lakini hakuna ambaye angetaka kujua sijui kazaa na nani. Sishabikii hayo. No. Nakuonyesha value yako halisi ikikutana na ufahamu sahihi hakika utaongea na nchi itasikia.

So tulitoka huku.....

X + (1⁄2)X + 1 = 100

Tafuta thamani ya X.

Mi nasema sasa huku mtaani acha kutafuta thamani ya X. Tafuta kujua thamani yako. Na kama bado uko shule usiishie tu kutafuta hiyo X ukafurahia umefaulu hesabu. Tafuta thamani yako.

Katika kitu kilichowakwaza ndugu zangu na watu wa karibu ni pale nilipoacha ajira kuanza njia ya ujasiriamali. Nilipoona thamani yangu HALISI haipo kwenye Degree yangu ya sheria au kazi nzuri benki ya kigeni bali nahisi kuna kitu ndani yangu katika kufundisha watu hasa vijana wenzangu. Silipwi chochote lakini furaha ninayopata hapa huwezi kuelewa kirahisi. Najua sasa kuwa nina mchango mkubwa wa mawazo kwa vijana wenzangu kuliko ningekuwa niko zangu mahakamani kuendelea na kazi ya sheria. Sishangai kuwa wapo wasionielewa. Ila tu nawaombea na WAO wagundue thamani zao halisi. Na siyo kutafuta tu thamani zao kupitia X.

Sijui wewe thamani yako iliwekwa kwenye mkono na vidole kama mimi au miguu au mdomo au koo au misuli au kichwani tu huko au kwenye macho. Kuna watu akiona kitu tu anabuni kitu kingine kutokana na alichoona. Kuna mwingine hana macho kama wewe wewe na mimi lakini thamani yake siyo mchezo.

Thamani ya Hellen Keller ilikuwa kwenye kutoona na kutosikia kwake. Akafanikiwa bila macho wala uwezo wa kusikia kuliko mamilioni wenye macho na wenye kusikia vizuri ambao tunataka tu kusikiliza umbea na vitu visivyo na maana.


Niliwahi kusema thamani ya Dan Brown ni kuandika Novel zinazofanya uone maisha upya kabisa na ya Les Brown ni kutoa speech zinazofanya uone maisha upya vile vile. Na wote wamekuwa millionaires.

What about you?

Usifate mkumbo. Yule binti aliyekosa chuo aliniambia kuwa nilimsaidia kutambua kuwa amekuwa kumbe akifata tu mkumbo... na kwamba sasa anahitaji muda wa kukaa na kutafakari juu ya maisha yake.


Point yangu siyo watu wasisome. No. Keller alisoma. Mimi nimesoma nashukuru Mungu.

Point yangu ukasome tena sana tu lakini siyo ili kukamilisha ratiba. Au ili kupata title. Usitafute thamani yako kupitia elimu yako. Thamani yako ni kitu tofauti na elimu ni kitu tofauti.

Thamani yako ni tofauti na mume/mke ni kitu kingine cha kukamilisha hiyo VALUE yako. Sasa usipojua ndo hicho kinachopaswa kukukamilisha tu wewe ndo utakifanya ndo the real thing. Ndo maana unataka a READY-MADE MATERIAL.

Usitafute tu mbinu za kwenda Ulaya hata kama ni kwa kupitia njia za mkato ili na uridhike kuwa na wewe ulishafika Ulaya. Nenda Ulaya ukiwa wewe umeshatambua thamani yako. Hata kama jina lako halijulikani bado but unajitambua. Wanaoenda Ulaya wakiwa wanajitambua hata akirudi anaishi kwa busara siyo labda kujionyesha kama sisi wengine.. Anajua thamani yake haikuwa katika kwenda Ulaya.

Fanya hivi.
Ukiondolewa elimu yako yote, ukanyang'anywa hicho cheo ukaondolewa hizo nyumba na hilo gari utabaki kama NANI?
Hiyo ndo thamani yako.

Ayubu wa kwenye Biblia alijua kuwa THAMANI YAKE HALISI haikuwa kwenye wingi wa mali wala wingi wa wana na mabinti. Thamani yake ilikuwa katika KUMPENDA MUNGU na ndo maana vitu vyote vilipoondoshwa alibaki na simple statement: BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA...... Hata alipougua bado alibaki na thamani yake.


Kifupi alitafuta zaidi thamani yake zaidi kuliko thamani ya X. Na hicho hadi Mungu alijivunia. Mungu hakujivunia wingi wa mali za Ayubu. Lakini sisi tunajivunia wingi wa mali na kuhisi ndo vinatuongezea thamani.

Usijilinganishe na wasio na vitu ukahisi wewe uko juu. Thamani yako iko kwenye CONTRIBUTION  yako kwenye jamii.

Nilipoongea na huyo binti nilimwambia ahakikishe katika maisha yake anakuwa INDISPENSABLE. Yani mtu tegemeo kwenye jamii. Yani watu wakiwa na maswali wanalazimika tu kutafuta majibu kwako watake wasitake. Hapo unakuwa umejenga THAMANI YAKO HALISI. Jamii kukutegemea wewe siyo lazima iwe kwa sababu ya cheo chako au pesa zako. Inawezekana kabisa ukawa huna cheo na watu wakakutegemea. Hapo thamani yako halisi imedhihirika.

Kama cheo  ulichokuwa nacho "kimeEXPIRE" na watu hawakutafuti tena ujue ulipoteza muda kutafuta thamani ya X badala ya kutafuta thamani yako mwenyewe. Hawa ndo ambao ukimuondolea cheo inakuwa ugomvi. Mara mimi nimepigania nchi. Mara mimi hiki. Mara mimi ni muhimu. My friend umuhimu wako huwezi kuitangaza wewe. Wewe ulijisahau ukatafuta thamani ya X ukasahau kutafuta thamani yako. Kuna mawaziri leo hata ukiwashusha vyeo thamani yao kwenye jamii na taifa inajulikana tu. Walijua kutofautisha thamani ya X na thamani yao.

INDISPENSABILITY yako ina maana kuna vitu haviwezi kufanyika bila wewe kushirikishwa kwanza. Siyo kwa sababu ya cheo chako bali by virtue of who you have become. Nakupa mfano wa mwisho. Abraham alikuwa mwenye roho nzuri na ukarimu uliopitiliza kiasi kwamba mpaka alikuwa anaweza kukaribisha wapita njia tu wapate msosi na kupumzika kwake kisha ndo waendelee na safari zao. Yani unakuwa mwema mpaka unaishiwa wa kuwatendea mema unaanza kulazimisha kuwatendea mema wapita njia! Duh. Hii level Mungu mwenyewe akaona hii si mchezo. Huyu mtu siwezi kufanya jambo halafu nimfiche.

Ndo Mungu akamnong'oneza Abrahamu kuhusu mpango wake wa kuiadhibu miji ya Sodoma na Gomora. Tena akaanza kuwaombea watu wa miji hiyo.

See?

Sasa Mungu hakumwambia hizo habari Abrahamu kwa vile Abrahamu alikuwa mtu tajiri. No. Indispensability ya Abrahamu haikuwa kwenye mali bali utu wema wake.

So wewe kama unatafuta mali ili uwe muhimu hapo ni sawa sawa unagongelea msumari kule kwenye ncha.
You're doing it wrong.

Ukitaka kujua angalia watu wanajisikiaje wakisikia majina yafuatayo:


Rugemalila
Bakhressa
Dewji
Rostam


Nani hapa ni INDISPENSABLE?
Yaani ukimtoa huyo lazima umrudishe ili mambo yaende. Na ni nani hata akiondoka watu watamsahau kesho yake tu?

Utakuta watu I'm sure hawatajisikia the same ukiwatajia hayo majina. Kwa nini iwe hivyo wakati hao wote wana pesa?

Issue hapo ni THAMANI ya kila mtu kwenye jamii... Yaani kama ukimnyang'anya pesa zake zote jamii bado itamkubali as a person?
Hiyo ndo thamani yake halisi.

Hapo haijalishi kama ameshatafuta thamani ya X na kuipata. Hapo ni yeye. Thamani yake.

Jichunguze pia.

Are you becoming INDISPENSABLE too au bado unatafuta tu thamani ya X?

Mwisho wa maisha yako utakachowaza sana ni JINA GANI unaacha nyuma. Utaondoka dunia hii ukiacha nini kiishi miaka mingi baada yako? Kwamba ulikuwa na diploma ya ualimu?
Kwani wangapi wanayo?

Ukianza kutafuta thamani yako hutahangaika kujua watu wanakuonaje wala wao wanamiliki nini au wamepiga hatua kiasi gani. Utakuwa more concerned na kujua Mungu aliwekeza nini ndani yako ili uanze kukufanyia kazi mapema ungali na muda bado.

Ajiriwa ndiyo lakini find your real VALUE. Thamani ya Millard Ayo iko wazi. Hakuishia kuajiriwa tu. Alitambua nini Mungu aliweka ndani yake.
Jifunze kwake.

Soma sana tu but find your REAL value.
Tukiondoa elimu yako yote utabaki na nini?

Oa au olewa lakini jua THAMANI yako usije ukaanza kusumbua watu njiani eti, "Unajua mi nani?"

Ukiona mo sijui wewe ni nani ujue hujawa muhimu kwangu. So kaongeze thamani yako nitakujua tu. Au nakosea ndugu zangu? Kwani Max Malipo si unaona mwenyewe thamani yake? Au mpaka akwambie?

That's what I'm talking about.

Achana na thamani ya X saivi hiyo ilikuwa darasani.

Sasa hivi tunabadili swali:


YOU + (1⁄2)YOU + 1 = INDISPENSABILITY

Tafuta thamani ya "YOU".

Ukilipata jibu hapo basi tutakujua sisi wote very soon.


Nakutakia mema!

#FourteenSix

Till next time.


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511
www.andreamuhozya.blogspot.com

Alhamisi, 5 Oktoba 2017

WATOTO WA "WENZETU" HUPATA ELIMU TOFAUTI SANA NA KINA "SISI".

(Sifundishi ubaguzi....)

Wakati wa sakata la ajira za uhamiaji ambako usaili ulifanyikia uwanja wa taifa miaka kama miwili iliyopita kuna vijana wengi sana waliojitokeza.

Baadaye ikaja ya TRA shortly thereafter.  Na mwaka huu tena juzi juzi TRA tena wakaita watu kwa usaili wakajitokeza vijana wengi sana.


Katika hizo instances zote sikuona kijana wa kitanzania mwenye "ngozi nyeupe".

Nikawaza kidogo... Nikajiuliza.

Hivi kuna watanzania vijana wenye asili ya kihindi na kiarabu na hata kipakstani nk hapa nchini?
Nikajijibu kuwa "WAPO".

Nikajiuliza tena kidogo wote wameajiriwa?
Kaakili kangu kakaanza kusearch network kidogo kisha nikajijibu: "HAPANA"

Nikajiuliza tena: Sasa mbona hawaendi kufanya interview kama wenzao sasa?
Nikawa sina jibu. Eti, ulishawahi kujiuliza swali kama hilo?


UMASKINI WA FIKRA NDO KIFUNGO KIREFU ZAIDI KUWAHI KUTOKEA

Sijui kama umewahi kuishi kijiini. Lakini nikuulize tu hivyo hivyo. Hivi ukikuta wanaume 50 wako kwenye tope kwenye shamba kubwa la mpunga na wanakwambia  hawawezi kujikwamua katika tope hilo wanaomba msaada wako utawaza nini? Tufanye hivi liwe ni shamba ambalo wewe una uhakika hilo tope hata mtoto wa shule ya msingi anaweza kutoka.
Utawaza nini?

Kuna kitu hakiko sawa kwenye "bongo" za watu hawa. Si ndiyo?

Fikra zako zikishikiliwa na mtu mwingine utakuwa mfungwa maisha yako yote. Kitu kikubwa  kinachotutofautisha sisi sote siyo eti jinsia au rangi au imani nk. Ni jinsi tunavyotumia UHURU tuliopewa bure wa KUFIKIRI. Sijui wewe utakuwa kundi lipi.

1. Kuna ambao wanautumia uhuru huo KUFIKIRI kweli. Hawa hupiga hatua kidogo kidogo mwisho inakuwa kubwa. Hawa ni wa kuigwa mfano.

2. Kuna ambao wanautumia uhuru huo KUTOFIKIRI tu. Wapo tu hawataki kabisa kufikiri hata kidogo tu. Hapa unakuta wasomi tu wengi. Hawa wanahitaji #MAOMBI nadhani.

3. Kuna wanaoutumia uhuru huo siyo tu KUTOFIKIRI bali KU-DEMAND mtu mwingine afikirie kwa ajili yao.
Sasa hawa wanahitaji #ELIMU lakini nadhani na #VIBOKO  (ikibidi).

Jokes aside... Tuna kundi kubwa la vijana ambao hawataki kufikiri na wanataka mtu mwingine afikirie kwa NIABA yao.
Huu ndo unaitwa MSIBA WA TAIFA.


UNAPOJIFUNZA KWA MTOTO WA FORM ONE

Ngoja nikupe story kidogo.
Hivi karibuni nilisafiri kwa basi. Dar Lux. Basi zuri sana kwa kweli.


Nimekaa pembeni na kijana wa kiume miaka kama 14 hivi mwenye asili ya kiarabu. Nilikuta keshaketi so nikamsabahi na kujitambulisha. "Naitwa Andrea ni mjasiriamali na nafurahi kuwa na wewe safarini mdogo wangu". Akajikuta anasmile na kujitambulisha pia. Well safari imeenda story za hapa na pale but mpaka mwisho wa safari nikajifunza kuwa alikuwa anatoka likizo kurejea shuleni. Katika kuongea naye nikajifunza kuwa baba yake ni mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa.  Na kaka ya huyu kijana yuko nje ya nchi akisomea mambo ya usimamizi wa fedha (za familia)
Dada wa huyo kijana yuko Dubai anafanya kazi katika kampuni moja kubwa kupata uzoefu kwa ajili ya baadaye kusaidia biashara zao. Imagine huyo ni kijana wa Form One.
Yeye huyu kijana yuko kidato cha kwanza hivyo lakini baba yake anamshauri kuhusu kuchagua masomo ya biashara na ameshamwambia kuwa kuna mradi atampa akishamaliza mambo ya masomo yake ili ausimamie na ndo sasa huyo kijana akawa anasema bado anawaza maana anaona jinsi baba yake anavyo"hangaika" kuwaza mambo mengi na ku-manage biashara zake za petrol stations na malori na nyinginezo. Nikawa namtia moyo tu kuwa asiogope changamoto nk.

Lakini huku nikawa najiuliza kimoyomoyo.
Hivi na mimi nilisoma sheria ili nikasolve kesi za ukoo wangu au familia yangu au ili niajiriwe tu ilimradi kwetu waone hela inakuja wamshukuru Mungu kuwa wamepata mtu katika watu?
Niliwaza sana.

Nikawaza hivi sisi tunaposoma degree ya USIMAMIZI WA FEDHA tunakuwa tunataka tukasimamie fedha za nani?
Za familia?
Eti.

Hivi tunaposoma degree ya BIASHARA tunakuwa na lengo la kwenda kuwa  wafanyabiashara au kuajiriwa kwa mfanyabiashara ili yeye ndo AFIKIRIE cha kufanya atwambie sisi nini cha kufanya (Job description) halafu tukishakifanya atupe zawadi (mshahara)?

I mean tunaposomea UALIMU lengo ni kufanyanya nayo nini hiyo elimu.

Uhasibu. Uhandisi.

Kwa nini tuna elimu ya udaktari halafu TUNAGOMA mpaka Ulimboka anapoteza meno na kucha kwa ajili yetu?


Kugoma ni kulazimisha mtu mwingine afikirie cha kufanya. Na asipofanya huna cha kumfanya vile vile. Au naongopa ndugu zangu?

See?

Career guidance katika jamii ya kina sisi #WEUSI ni changamoto kubwa. Tunafanya tu mazoea.  Wengi tumesoma kwa mazoea tu. Mpaka leo ndo tunaendeleza trend hiyi hiyo kwa kizazi kijacho.

Nenda shule yoyote ya msingi leo hapo ulipo uliza watoto wanataka kuwa nani baadaye. Ukiacha wanaotaka kuwa Diamond au Samatta wengi wanakwambia: mwalimu, rubani, mwanasheria, "injinia", mhasibu, daktari, nk. Wachache sana watakwambia kuhusu kuuza nguo au kuuza viwanja au kuuza magari na vitu vya aina hiyo.  Why wazazi #WEUSI wanaona fahari kuwa na daktari au mwanasheria. Ndo maana zikitangazwa nafasi 50 kesho TRA hutoamini "nyomi" utakayoiona. Na hiyo itaendelea hadi Yesu arudi.


WHAT TO DO?

Kujitoa kwenye KIFUNGO cha fikra siyo kitu rahisi lakini ndo njia #pekee ya kuokoa uzao wako ujao. Lazima kuanza kuwaza TOFAUTI na mazoea. Mazoea ndo yametufikisha hapo. Na ni WEWE wa kuanzisha hiyo trend tofauti.

Tuanze kuwaza kama "wenzetu".
Kama wewe ni mzazi anza kitu chako sasa. Hata kama umeajiriwa. Anzisha biashara ambayo una uhakika unaweza kuwa-guide watoto wako wakasome elimu hiyo hiyo wanayosoma wengine ila wakimaliza waje kui APPLY hiyo elimu kwa biashara ya familia. Kama ni kusimamia fedha wasimamie za familia. Siyo tu za Vodacom.

Hivi watoto wa Bakhressa wanafanya kazi Vodacom?

Kuna wakati nilikaa na mtu mmoja hapa jijini ana "hela zake". Akasema mtoto wao wa kwanza wamemjengea Hoteli Zanzibar na mtoto huyo kwa sasa ana miaka kama 14 na anasoma hapa hapa Bongo. Na mtoto anajua. Na mtoto akiwa likizo huwa anaenda ofisini kwa baba yake kujifunza namna ya ku-MANAGE biashara kwa kuona.
Sasa mtoto huyo utamkutaje uwanja wa taifa kufanya interview eti. Au mei mosi amebeba Bango la kuongezwa maslahi?


Kwa sababu ya kushindwa kwetu kufikiri na kutaka SERIKALI ndo ifikirie kwa ajili yetu kuna siku watoto wetu wataambiwa wakafanye interview hata PORINI na wataenda. Tunakuwa kama kondoo tu kupelekwa kokote.

Nimejifunza mengi kwa hawa "wenzetu".
Mtanzania mmoja mwenye asili ya kihindi anamiliki majengo makubwa kama matano  hapa jijini. Miaka 7 iliyopita nilikuta anahangaika na mafundi city centre kwenye ghorofa moja refu huko juu walikuwa wanajenga RESTAURANT moja ya kisasa. Katika kudadisi mbona anapush push hivyo akaniambia hiyo restaurant ilikuwa ni ZAWADI ya birthday ya mtoto wake wa kwanza ambaye alikuwa masomoni Uingereza wakati huo. Na birthday ilikuwa bado wiki moja tu. Hebu fikiria. Sisi birthday tunapeana "baisko" na likeki kuuubwa au eti gari. Thinking yetu iko na shida. Why birthday ya mwanangu nisimpe mradi. Anakuwa anagrow na mradi wake. Of course tunaweza lakini nani yuko tayari aache COMFORT ya ajira kwa ajili ya kuset TREND mpya kwa vizazi vijavyo? Tunalilia NYONGEZA ya mishahara.


Nimesema ukiazimisha mwingine awaze kwa ajili yako akikataa huna cha kumfanya. Si raisi huyo hapo amesema kwa VISION aliyonayo saivi priority ni HUDUMA ZA kijamii. Period. Kwani madktari waliambiwa nini wakati ule? Asiyetaka mshahara uliopo aache kazi.
Unafanya nini sasa.
Waswahili wanasema kila mtu apambane na nini......?

Halafu na wewe unaanza kulaumu raisi mbele ya watoto wako. Eti raisi huyu tutamnyima kura. Wakati hata hukumpa kura yako so in fact hakuna utakachobadili. Unaharibu tu fikra za watoto wako wanaoanza kufikiri kuwa raisi ndo anasababisha wakose ada au wale matembezi wiki nzima.

Ukilazimisha SERIKALI ifikirie kwa ajili ya gharama ya elimu ya juu ya watoto wako watakachofanya hela ambayo zamani walikupa wewe yote saivi wataigawanya ili wapate watoto watano. Wanakwambia  tumedahili wengi zaidi na tumetoa mikopo kwa wengi zaidi.
#Smart.

Utafanya nini?

So kama hatutataka kufikiri tofauti tutaendelea kuishi hivi hivi vizazi na vizazi. Utajiri tunao elimu tunayo tunaenda kuiapply kwenye BIASHARA za "wenzetu". Na watoto wetu tunwafundisha hivyo hivyo.


EMBE! EMBE! EMBE! (Tuendelee)

Wakati niko mdogo kijijini kulikuwa na wahindi wana Pick Up walikuwa wakitoka Nansio wanapita jijini kwetu wanaenda vijiji vya mbali zaidi. Sasa walikuwa wakifika kijijini kwetu wanakuta watoto wa kiume tunawasubiri kuwapa MAEMBE kama zawadi. Embe! Embe! Hata Kiswahili chenyewe tulikuwa hatujui sisi. Embe! Wanachukua MAEMBE hadi wanatosheka wanaondoka. Sisi tupo tu. Na tunajisikia vizuri kweli kuwa wamekubali. Khaaa!
Kuna wakati wakawa wanatupa lift hadi kama kilomita moja hivi wanatwambia turudi. Tunafurahi kweli. Tumepewa lift kwa kugawa "mali" bure. Tulikuta wenzetu wanafanya hivyo so na sisi tukaendelea hivyo hivyo. Hata hatujui kwa nini.

Sasa hiyo inatofauti gani na leo nikapata degree (embe) nikaanza kuwaambia waajiri "Embe"! Embe! Embe!
Halafu wakapokea hiyo degree yako wakakupa kalift kidogo kimaisha (ujira) kisha wanakwambia haya shuka toto jurii.
Hahaaaaa.

It's the same.

Kuna siku nikaenda nao hadi mjini nilikuwa nimeshakuwa rafiki na hao watoto. Nione hawa wanatokaga wapi lakini? Baba yao akawa ananishangaa tu. Lakini nikarudi kijijini kwa miguu. Sasa si ningeshauzwa mimi kama ingekuwa dunia hii ya leo!! Lol.

Lakini naamini unaelewa jinsi tunavyofurahi kupata LIFT badala ya kufikiri ni namna gani TUMILIKI HILO GARI sisi wenyewe na tuwape "weupe" lifti. Nilisema sifundishi ubaguzi. Just kuchokonoa akili zetu ambazo mpaka leo zinawaza kuwa kuajiriwa kwenye ofisi ya WAZUNGU ni "BAHATI".

Sikia.
Watoto wa hao wahindi walikuwa wanafundishwa cha kufanya wakifika kijijini kwetu. Ni kusmile na kutuchekea kidogo. Sisi tunafundishwa na kugombania kugawa Embe! Na kupigana vikumbo nani embe zake zipokelewe.

Utumwa tu wa FIKRA.

Dewji hakuwahi kupanga foleni NBC kuomba kazi. Na wala watoto wake hutawaona njia hiyo. Wala kizazi chake chote.

Au watoto wa Ali Mufuruki wanaenda pia uwanja wa taifa eti interview?
Wapi.


Lakini sisi tumekazana tu kuanzia babu mpaka mjukuu" Embe! Embe! Embe!

Tutaishi kwa lifti na mpaka tutie akili.

#ThreeSixteen
#FourteenSix


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511