Ijumaa, 15 Septemba 2017

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE BUT WHAT YOU DO IS... (WEWE SIYO VITU UNAVYOMILIKI BALI KILE UFANYACHO!)

Niliamka katikati ya usiku mnene... na hasa sikuwa nimeamka ila niliamshwa na baridi kali la jiji la Johannesburg kwenye majira ya baridi, baridi ambalo mpaka leo sijui lilipenyaje-penyaje katika wingu zito la nguo nilizovaa, sweta, shuka, na blanketi ambalo niliamini lilitengenezwa ili tu kuithibitishia dunia kuwa baridi si lolote wala si chochote!

Usingizi ulikata kwa sababu ya hilo baridi lakini pia (na hasa) kwa sababu ya wimbo ambao niliacha ukiplay kwa sauti ya chini chini kwenye simu wakati nalala! Nilipoamka ulikuwa unaishiaishia ile replay sauti ikawa inaishiaishia...

Akili yangu ikaanza kufikiri sana kuhusu siyo hasa kilichokuwa kikiimbwa bali mmoja wapo wa waimbaji wa wimbo huo...

Replay ikawa ishaanza tena.. Sauti yake maridadi yenye kuimba kama inatetemeka kwa mbaali ikajaa sana masikioni mwangu na kiukweli hadi moyoni mwangu...
Nikajikuta naanza kusikiliza tena:


"This life don't last forever (hold my hand)"..., wimbo ulianza.

"So tell me what we're waiting for? (hold my hand)

"We better off being together (hold my hand)

"Being miserable alone....

Yes sauti ya Michael Jackson aliyeshirikishwa na Akon ilitetemesha ngoma za masikio yangu kuliko baridi lilivyotetemesha ngozi yangu mpaka nikasahau hata hiyo baridi yenyewe. Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kuwa sauti hiyo ilikuwa ya mtu ambaye alikuwa hayupo duniani tena. And ndo basi tena. Dunia nzima ilikuwa ikimkumbuka Michael Jackson.

Magazeti yaliandika,  Redio zikatangaza, internet ikaenea kumbukumbu zake. Vitu vingi vilisemwa ambavyo baadhi yetu hatukuwahi kuvisikia. Hakika dunia ilijaa huzuni kwa namna yoyote ile ambayo ungetazama simulizi za maisha yake na kazi zake.

Lakini jambo moja ambalo lilikuwa DHAHIRI katika mijadala yote ya kifo chake ni kuwa watu hawakuwa wakiongelea eti alinunuaga nini au alikuwa anamiliki nini na nini au alikuwa anaendesha gari gani nk. Habari zote ziligusa zaidi ALIFANYA NINI. Aliwagusa watu wengi siyo kwa majumba yake au hela zake bali namna alivyowafanya watu wajisikie.

Wimbo uliendelea kuplay nikiwa hata siusikii tena kiukweli nikiwa nawaza tu IMPACT ambayo Michael Jackson aliacha ulimwenguni kiasi kwamba kijana wa kitanzania kama mimi kutoka huko Ukerewe nilikuwa namjua na kuguswa na jinsi alivyofanya kazi yake angali duniani na mpaka kusikitika kuwa hatunaye mtu kama huyo dunia hii tena.

NINI NATAKA KUSEMA:

Mara nyingi sana tumekuwa tukiwaza vitu vya kuwa navyo. Vitu vya kumiliki ili na sisi tuwe WATU KATIKA WATU. Mashindano mengi duniani siyo ya kazi bali ni ya VITU. Siyo kwenye michezo au siasa au kanisani mwenye gari la kawaida anawaza lini naye atapata gari kama la DEWJI. Anasahau kuwa anapaswa kuwaza KAZI GANI afanye itakayowagusa watu wengi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote aliyewahi kutokea duniani. Wengi wetu tunajisahau sana na kuingia katika mtego wa kushindana na watu bila hata kujua kuwa tumeshakuwa OBSESSED na kuwazidi wengine kiasi kwamba tumesahau hatukuumbwa kuja kumzidi mtu. Mashindano yasiyotarajiwa yametupelekea kujikuta tukitengeneza maadui badala ya marafiki. Kwa kutaka sana kuwa AHEAD katika vitu tumejikuta tunacompromise standards zetu za behaviour ama tumejikuta tunakuwa so impatient na process na kutaka tu kutangulia.

Tunasahau kuwa cha muhimu kiukweli siyo nyumba ngapi tutawaachia watoto. Mfalme Suleiman kitu kikubwa zaidi anachokumbukwa nacho ni HEKIMA siyo dhahabu ya OFIRI.  Maana dhahabu zake zote saivi hata sijui ziko wapi. Lakini HEKIMA yake ipo hadi leo!

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE...BUT WHAT YOU DO IS..

Haimaanishi usimiliki. No. Miliki mpaka shetani ajue kuna mtoto wa Mungu hapana chezea! Lakini usisahau kuwa vitu unavyomiliki havitakudefine wewe ni nani hapa duniani. Bill Gates hatambuliwi kwa wingi wa hela zake au majumba anayomiliki ila kwa CONTRIBUTION yake kwa wanadamu wenzake hasa MASIKINI. Ndo maana akala wali maharage Tanga wakati angeweza kuagiza chakula kutoka The Ritz au Ceaser's Palace. Jifunze kwake!

Anamiliki lakini akiondoka duniani hakuna mtu atakuwa anakumbuka viatu vyake au saa ya milionI 100. Ndo maana mara nyingi matajiri wengi huvaa "simple" ili kusaidia wanaowaangalia wasiwa-define kwa vitu wanavyovaa.  Steve Jobs alikuwa anavaa jeans na turtlenecks tu basi. Ili usiangalie sana nje kwake.

Warren Buffet yuko hivyo hivyo. Nk. Na hata matajiri wanaopiga pamba kweli kweli wanajitahidi kufanya vitu vingi kuonyesha kuwa wao ni zaidi ya mavazi yao na magari yao.

Alipofikwa na mkasa mbunge Tundu Lissu gari lake lilionyeshwa kutobolewa na risasi, right? Mi binafsi sijasikia mtu akilihurumia gari na kusema "OH MASIKINI GARI LAKE". Kumbe vitu vyetu havina maana kubwa sana linapokuja suala la kupima "value" yetu. Yani ni hivi unaweza kuwa na ardhi au majumba yenye thamani ya mamilioni lakini thamani yako halisi kwa watu halisi ikawa ni sawa na thamani ya noti ya sh elfu 10 tu. I'm serious.

Kijana mwenzetu #McPilipili amepata ajili na pia hakuna mtu anawaza gari lake. Why? Coz ile Prado is not WHO HE IS. Naamini atakuwa analijua hilo. Albeit now.
Watu wamepost kumtakia heri na kupona siyo eti kuliombea gari. Insurance will take care of that. McPilipili ni WHAT HE DOES. Namna ambavyo amekuwa akifanya watu wajisikie. Na si ana nini.
Unajifunza kitu?

Sasa swali.
Mimi na wewe tukianguka leo hii Mungu akatuita (ni mfano tu usiogope) tutaacha mjadala gani nyuma. Acha watu wachache ambao maybe ulipishana nao kiujumla. Angalia wengi. Majority watafeel vipi.

That's why I write bila kuchoka. Nimeandika article hii kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa usiku ndo nikapumzika. Yes mpaka usiku wa manane maana ninajua kipawa cha kuandika nimepewa nikitumie kuelimisha wengi. Tena haraka. Naamini maandishi yangu siku moja yatasomwa na watu wa mataifa mengi mno. Maandishi yatakayoacha ALAMA maishani mwa watakaoyasoma.

Nilichagua ujasiriamali badala ya sheria kwa kuwa niliona kwangu hii ndo njia nitakayoweza kuufikia ulimwengu wote kwa kazi yangu.

Na wewe unapaswa kuona ni namna gani UNACHOKIFANYA kitakudefine. Usipofushwe na hamu ya gari zuri na nyumba nzuri na viwanja. Hivyo vitakuja tena vingi mno kama ukiamua kuwa BORA ZAIDI katika jambo unalilifanya. Jifunze kuwa bora katika IMPACT YAKO kwa jamii. Hilo ndo la msingi.

Sisi hatumkumbuki na kumfuata Yesu Kristo kwa sababu alikuwa na mali. No.. WHAT HE DID IS WHO HE IS!

Mandela ni Mandela Gandhi ni Gandhi kwa sababu ya  vitu walivyofanya. WHAT THEY DID.

Tarehe 14 October haijafanywa sikukuu nchi hii sababu ya kukumbuka mali za Baba wa Taifa. No. But WHAT HE DID. Sababu WHAT HE DID WAS WHO HE BECAME TO US. Inakumbukwa impact sahihi.
Legacy.

Hata viongozi wa nchi zetu hizi wenye kusemekana kuwa na mali mengi kama hawana IMPACT sahihi katika maisha ya watu basi thamani yao halisi inazidiwa na fundi seremala ambaye yuko kijijini huko hata hajulikani lakini ameishi kwa kutengenezea watu vitu vizuri na wanamthamini kweli kweli. Huyo ana thamani kubwa hata mbele za Mungu kuliko Waziri ambaye ukitaja jina lake watu hata hawalikumbuki na bado yuko hai wala hajafa licha ya kuwa ana majumba ya kifahari na yule seremala analala kwenye mkeka. Ndipo utakapoona seremala anakufa kwa amani (kamaliza kazi) na huyu msomi anakufa kwa pressure na simanzi  (akiwa anajua anadaiwa kazi).

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE... BUT WHAT YOU DO IS.

Mohammad Ali alipoondoka watu walikumbuka alichofanya siyo ati alikuwa analalia kitanda cha aina gani au anaishi nyumba ya ukubwa gani.  Issue ni alifanya nini.


Hujawahi kujiuliza mpaka leo watu wanaongelea BISHANGA na hata hayupo active sana kuigiza kama zamani. Hujaona watu wanaongelea Kanumba na hayupo miaka sasa na wengine wapo wanaigiza lakini bado watu wanaongelea Kanumba.
Impact.
Hawamkumbuki kwa sababu alinunua labda HAMMER au aliporomosha majengo huko Mbweni lakini WHAT HE DID.
Not what he had.

Jifunze.
Usishindane na mtu. Shindania UBORA wako katika like alilokuitia Mungu kufanya. Ukichunguza kazi yako utagundua bado UNAPWAYA sana kwa VIWANGO vya Mungu. Fanyia kazi ubora wa kazi yako. Hiyo ndo watu watakukumbuka nayo. Usiandike kitabu tu ili uuze. No kitaacha ALAMA gani. Siyo kitakufanya ununue gari au kiwanja. Kuna vitabu vingi sana kuhusu mafanikio kifedha lakini THE RICHEST MAN IN BABYLON si mchezo. Kuna vitabu vingi vya kukuhamasisha kufuata ndoto zako bila kuchoka lakini THE ALCHEMIST si mchezo.

Waliovisoma wanaelewa nasema nini.

Mwalimu Mwakasege ni maarufu siyo kwa aina ya magari au majumba. Nina uhakika ana miliki pia kama mwana wa ufalme lakini kinachomtambulisha kwa watu siyo VITU bali KAZI YAKE.

Usikubali utambulishwe na watu kama "yule binti anayevaaga high heels" au "yule jamaa anayeendeshaga NOAH ya silver". Mimi nitafurahi nikitambulishwa kama yule jamaa anayeandikaga kuhusu mambo ya kutunza muda na mambo ya ujasiriamali, nk. Yes WHAT I DO ...not what I have.

Kuna mtu anaitwa MWALIMU MAKWAYA mi sijui hata anapoishi wala anamiliki nini kijana yule lakini najua ANAELIMISHA watu hasa vijana.

What about you?
Watu wanaweza kukutambulisha kwa kazi unayofanya au lazima watumie mavazi yako au nywele zako au gari ndo mtu akujue. Hapo utakuwa unaishi maisha yasiyokuwa na IMPACT kwa a greater majority. Sikia ujue mi siongelei familia yako. No. Sijui umejenga kwenu. That's good hongera sana. But nazungumzia mtu asiyekujua wewe in person amenufaika na nini kwa uwepo wako. Huwa nafurahi nikikutana na post zangu kwenye groups za whatsapp hata kama jina langu wametoa. Huwa nafarijika kuona kumbe nina gusa watu wengi tusiofahamiana. It really makes me happy. Contented.

Josiah Otege, Josinah Leonard , Exuper Njau, Haruni Leonard, Binti Luzutta nawapa challenge: WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE but WHAT YOU DO IS.

Na wewe msomaji wangu naomba ufikiri kama nilivyofikiri mimi usiku ule nilipoamshwa na baridi na kukutana na sauti ya Michael Jackson. Nakuacha na maneno matano ya kwanza kwenye huo wimbo wa Akon na Michael Jackson;

"This life don't last forever..."


Kumbuka hilo uzingatie sana kazi ufanyayo na siyo mali utakazo.


#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
+255 788 366 511

Jumatano, 13 Septemba 2017

WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE! KUJUA WEWE NI MTU AINA GANI TAZAMA SEHEMU UNAZOENDA MARA KWA MARA


Siku kadhaa zilizopita nikiwa nyumbani mchana nilijisahau nikaacha mlango wazi wakati wa gari la taka kupita. Unajua kilichotokea? Nilipoenda kurudishia mlango na kurejea kuketi ghafla nikasikia mlio wa nzi. Akawa anaruka huku na kule. Arrrghh. Instinct yangu ya kwanza kikawaida huwa ni kuchukua dawa ya kuulia wadudu na kuspray. Lakini this time sasa  nipo nyumbani na hiyo dawa hupaswi kuvuta hewa yake maana ni toxic.

What to do?

Nikakumbuka kuwa mpaka muda huo nzi wa watu alikuwa bado anazunguka yani hajapata sehemu ya kusettle. Kwanza nikasmile maana nina mke msafi sana and she knows huwa namwambia.  So nikajua nzi hajasettle maana kaingia kwenye mazingira yasiyo yake.

What to do?

Nikafungua mlango tu wide enough. Kisha nikatoka mlangoni nikaona nzi anazunguka sebuleni kama mara tatu ruti ndefu hivi kisha huyooo akatokea mlangoni kwa spidi ya rocket!
Problem solved.

NATAKA KUSEMA NINI?

Katika vitu ambavyo hatutofautiani kabisa na nzi ni kwamba hata sisi huwa tunakuwa "comfortable" katika mazingira tuliyozoea/jizoesha. Ni vigumu sana ukawa comfortable mahali penye uchafu kama wewe ni msafi. Au penye usafi kama wewe ni mchafu kweli. Utajibana weeee lakini mwisho vitakushinda utaanza tu kuleta "fujo". Utatafuta tu sehemu ya kutokea.

Sasa sikia sikumfukuza nzi alitoka mwenyewe.

Lakini vipi kama ukikuta mzoga kando ya njia halafu kuna nzi wengi (comfort zone yao) halafu ujaribu kuwafukuza (kuwaswaga)? Utakuwa unafanya kazi bure. Wataruka kidogo na kusambaa kisha watarudi tena. Hawawezi kuondoka kabisa. Labda uondoe mzoga. Hao ndo nzi. Nzi mahali pao pa kujidai siyo kwenye usafi. Yani ukiona nzi katulia mahali ambapo wewe unapaona ni pasafi basi ujue kuna tatizo na pua zako au macho yako au vyote. Nzi anajua pa kwenda.

Ndivyo na sisi tulivyo. Ukitaka kujijua wewe ni mtu wa aina gani check where you normally go. Wapi huwa unakwenda mara kwa mara. There's no way ukaenda mara kwa mara sehemu usiyoipenda. Huwezi kuperuzi sana mtandao usioupenda. Kuna mtandao tu ndo comfort zone yakof


Miezi kama mitano iliyopita kuna siku niliingia kwenye daladala. Ghafla nikaona mdada kafungua simu yake. (Umbea huu nao Mungu atusaidie). Basi nimeona akafungua INSTAGRAM.

Akaingia search. Akatype Jina la mtu.......
Akaanza ku-scroll post za za huyo .

Nikawaza tu katika "umbea" wangu huo, dah huyu ameona of all places za kusoma ni hapo. Akawa anaenjoy na kucheka kweli.  Mara anazoom. Basi katika "umbea" huo huo nikamsemesha kidogo:

*Mimi:* Naona unachekicheki news kidogo..?

*Yeye:* Dah yani kakangu huyu (naniliu) ataua watu mwaka huu. Mi lazima nipitie kwake kila siku.

*Mimi:* Aisee huwa namsikia hivi yuko vizuri ee?

*Yeye:* Dah aisee yani hatari mbaya nakwambia. Yani mimi nisipopita kwake nahisi kama naumwa (huku akismile)

*Mimi:* Aisee si mchezo

*Yeye:* Ndo hivyo tunaondoa tu stress.

Mazungumzo hayakudumu sana maana nilimshukuru kiaina nikatoa kitabu nikaanza kuperuzi kidogo na mimi kuondoa hizo stress kivyangu pia.

Ni muda umepita sasa ila tu baada ya kale katukio ka nzi nikakumbuka hiyo siku pia.

Mimi nakutana na vijana wengi sana kupitia mitandao ya kijamii. Hasa kwa ajili ya mambo ya ujasiriamali na naweza kukuhakikisha kuwa asilimia kubwa sana ya vijana hawako COMFORTABLE na mambo ya maana. Mada inayohusu maendeleo yao inaweza kupita na kupata comments 10 tu katika ukurasa wenye followers MILIONI MOJA. Sasa ngoja ije mada ya jambo la ajabu ajabu utaona "MAONI" yatakavyojaa. Sasa ukiona hivyo usijiulize sana we elewa tu THAT'S WHO THEY ARE.

Ukiona vitu vya maana unaona vinakuboa ujue wala hujakosea. Ni kweli kabisa "VINABOA" kwa watu wasio sahihi. Ukiona vitu vya kijinga "HAVIKUBOI" ujue ni kweli kabisa haviboi kwa watu sahihi kwa vitu vitu hivyo pia.
Nzi ataborekaje na harufu you mzoga?

Ukitaka kujua WHO YOU ARE wala usihangike kufanya research kubwa. Angalia tu vitu vichache:

1. Gallery yako ya simu
Ingia now uangalie.  Ina picha za aina gani.
That's who you are.
Ina videos za aina gani?
That's who you are.
Kuna nyimbo za aina gani?
That's who you are.

2. Google Search list yako nini kinaongoza kutafutwa?
That's who you are.

3. YouTube Videos na channels ulizosubscribe nyingi ni zipi?
Ni za mambo ya ndoto zako na mafunzo ya kimaisha au ni muziki na umbea mwingine?
That's who you are.

4. Vipindi vipi vya Redio na TV huwezi kukosa kabisa?
That's WHO YOU ARE.

5. Nini unapenda kusoma bila kukosa.
Ubuyu wa leo leo au hadithi za Shigongo, au Tips za Dewji au Mafundisho ya Strive Masiyiwa?
Wapi upo napo COMFORTABLE?
Wapi unaweza kuahirisha kula kwanza mpaka ujue hicho kitu kilichoandikwa kimeishia wapi?
That's WHO you are.

5. Ukipewa External Hard Disk utaweka nini? Movies au vitabu? Je ni movie gani?
Aina ya movie na series zinazokuattract that's WHO you are.

Nk nk.. check hivyo vitu tu haraka haraka kwa uchache utajijua upo wapi.

Huwa unaenda wapi sana in the physical world lakini pia social media?

Ni muhimu sana kujua who you are mapema katika safari ya mafanikio yako ili uanze kucontrol vitu vinavyokuvuta mapema. Usije ukajikuta ghafla vitu vilivyokuwa vya msingi kwako ghafla vinakuwa vinakuboa halafu hujui kwa nini. Zamani ulikuwa unapenda watu wenye lugha ya staha na heshima na kuwasikiliza kweli kweli lakini siku hizi uko comfortable zaidi kusoma na kusikiliza wasio na staha na wanaotukanana matusi ya nguoni mitandaoni and wala huoni kama ni shida tena. Coz umeshakuwa nzi pia. Nzi mdogodogo.

Huoni shida kuwa kwenye mizoga wa maandishi. In fact unaitafuta na ukikuta haitoi harufu sana unasikitika. Ukikuta maua yananukia hutaki hauko comfortable.  Ulishawahi kuona nzi anaruka kutoa ua moja kwenda jingine kwenye bustani na akatulia na kuenjoy? Hawezi.
Huenda na wewe hutaki habari zenye harufu nzuri.

That's WHO you are now.
That's who you've become.

Na uzuri ni kuwa unaweza kujua kabisa hiyo  WHO YOU ARE ya sasa kama inakupeleka mahali sahihi au la.

Ukitaka ubadili mwelekeo wa maisha yako uwe wenye tija basi angalia WHERE YOU GO ON A DAILY BASIS.

Kama ningekuuliza swali sasa hivi kwamba: Hivi jana ulishinda wapi siku nzima?

Unaweza kusema labda

"Nilishinda kazini"

"Nilishinda nyumbani"

Nk.

Lakini huenda ulishinda WhatsApp. Au Facebook.

Sasa hilo siyo shida.  Ishu ulikuwa wapi na wapi kwenye huo mtandao wa kijamii.

Shaolin Monks hupewa training sana kuhusu eneo la fikra. Na wewe unaweza kujifunza. Kutunza fikra zako zisishikwe na mambo yasiyokuwa na tija kwenye kutimiza ndoto zako. Hold your mind together. Badilisha sehemu UNAZOENDA na utabadilika sana. Kuna watu huwezi kuwaona mpaka ubadili sehemu unazoenda. Yes. Unataka kuonana na Reginald Mengi Samaki Samaki?
Utangoja milele coz Samaki Samaki huenda that's WHO YOU ARE but it's not WHO HE IS.
Umeelewa?

Kwenye Biblia Zakayo alikuwa si mtu mwema machoni pa watu. Lakini WHERE HE WENT changed everything. Alipanda tu kwenye mti ili amwone "MTUMISHI".  Where he went was WHO HE WAS. Mungu anaona sirini. Zakayo pamoja na mabaya yote lakini alikuwa anatafuta pa kwenda ili atoke shimoni. Ni kama alijua hili nalosema hapa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.

Ukiendelea kwenda sehemu zile zile na kuonana na watu walewale na kutazama na kusikiliza vitu vile vile utaendelea kuelekea huko huko unakoelekea. Utaingia kwenye mtego wa kusubiri watu wengine watatue matatizo yako. Utaendelea kuona kuwa Dewji ana bahati na kusahau kuwa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.

Kama wewe ni kijana na unataka kuyafikia mafanikio lazima kwanza u check na hili la WAPI HUWA UNAPENDA KWENDA SANA.

Nakumbuka kuna siku nilikutana na kaka Samuel Sasali Mlimani City na kibongobongo nikamwambia "Kaka hatuonani?". Akaniambia tu "Huenda NJE ZETU (outings) zinatifautiana tu". And rightly so. Of course Sasali huwa ana majibu at all times and ukimuona unajiandaa tu kucheka. But the point is kama sionani naye kanisani na sifanyi naye kazi na WHERE I GO IS not WHO HE IS tutonanaje sasa?

Ni hivyo hivyo kwenye mitandao. Sehemu unazoenda sana ziangalie vema huenda kuna watu mnapishana. Huenda kuna fursa na ideas unapishana nazo na ndo Mungu anazileta lakini wewe hizo sehemu ambako hizo ideas zinapostiwa is not WHERE YOU GO.

Usitafute mchawi gani kakuroga ukawa nzi. Ni wewe mwenyewe. Anza kwenda kwenye maua huenda ukaweza kutengeneza asali.

Ukiona kwenda Serena kula lunch au hata kunywa juice tu haiikuingii akilini ujue that's who you are.

Mpaka ubadilike itabidi ufanye maamuzi ya Kizakayozakayo.

If you want to change your life start by changing WHERE YOU GO.

COZ WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE!


Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa

#ThreeSixteen
#FourteenSix
#TheAloeLawyer

Jumatatu, 21 Agosti 2017

"MY NAME IS CLARISSA" JE WEWE NI BINTI UNAYEWAZA KUTOA UJAUZITO? (Based on a true story)

JE WEWE NI BINTI UNAYEWAZA KUTOA UJAUZITO?
AU WEWE NI KAKA UNAYESHINIKIZA BINTI ATOE UJAUZITO ULIOMPA?Ilikuwa ni siku nzuri ya Jumamosi na jua la Dar es Salaam halikuwa kali sana kipindi hicho. Plus mawingu kidogo yalifanya hali ya hewa kuwa nzuri zaidi. Nilikuwa nimealikwa katika shule mojawapo binafsi hapa jijini kwa ajili ya kusaidia mambo binafsi kwa mwenye shule hiyo. Ilikuwa ni siku ya MAHAFALI ya darasa la saba katika shuke hiyo ya ENGLISH MEDIUM yenye jina kubwa kiasi na yenye watoto kutoka familia zenye uwezo.

Mandhari ilikuwa nzuri mno na yenye kutia hamasa. Magari mazuri mazuri ya wazazi na walezi yakiwa yamepaki vizuri kwa utaratibu. Kila iliyeshuka kwenye gari alionekana kutoka Dar es Salaam ya kwake tofauti na ile wanayoishi wananchi wengine. Watoto wakiwa wamevaa vizuri mno na majoho yao ya graduation na kila aliyeawona bila kujali kama anawafahamu au la alifurahi.

Hakika shule na wazazi walikuwa wamejipanga. Ratiba zote zilienda sawa na graduation ikaenda vema sana kwa utaratibu mzuri na mambo yote yakiendeshwa kwa lugha ya kiingereza. Kila mwalimu, mzazi au mlezi na hata wanafunzi wa madarasa ya chini walionyesha kufurahia kuwa sehemu ya familia moja. Makofi ya hapa na pale  yaliendelea kwa kila jambo lililotangazwa au kufanyika.

Ikafika wakati wa RISALA ya WAHITIMU. Akapanda binti mmoja mzuri sana na kama kawaida akipendeza sana kutokana na mavazi yake ya graduation. Mrefu kidogo. Mwembamba kidogo. (Picha hii chini siyo ya ninayemzungumzia)


"HONOURABLE DEPUTY MINISTER..... MADAM HEADMISTRESS.....,  DISTINGUISHED GUESTS, LADIES AND GENTLEMEN......" alianza risala yake.

"IT'S SUCH A GREAT HONOUR TO STAND BEFORE YOU THIS MORNING ON BEHALF OF MY COLLEAGUES............."


Kila neno lililotoka katika kinywa cha binti huyo lililuwa kama limechongwa na fundi maalumu kinywani mwake. Sauti yake ilikuwa kama sauti ya malaika. Sehemu kubwa ya RISALA yake ALIISEMA na siyo KUISOMA. Wageni, wazazi, wanafunzi wenzake na hata wafanyakazi mbali mbali katika shughuli hiyo walisimama kwa muda kumsikiliza binti huyo.

Minong'ono midogo midogo kati ya wageni na wazazi kuashiria kushangaa kiwango cha binti huyo haikufichika. Ndani ya muda mfupi umati wa watu ulikuwa kimya kusikiliza kwa makini bila mtu yoyote kuwaambia wasilikize kwa makini. Kila mtu alionekana kutikisa kichwa kukubaliana na mambo yule binti aliyekuwa akiyasema katika RISALA yake. Kwa muda huo wote sauti za ndege na vitu vingine zilionekana kama kufa ilisikika sauti ya yule binti ikipasua anga!

Ungeweza kusema huyu binti atakuwa muhubiri mkubwa baadaye, ama kiongozi mkubwa sana. Usingeweza kumwona kama binti wa kawaida.


"WHEN WE CAME HERE ABOUT SEVEN YEARS AGO WE WERE MERE LITTLE BOYS AND GIRLS WITH A DREAM TO MAKE OUR PARENTS PROUD.
BUT NOW WE'RE NOT MERE LITTLE BOYS AND GIRLS. OR ARE WE?" aliuuliza akiwatazama wahitimu wenzake na wao wakijibu kwa pamoja "NOOOO WE ARE NOT" huku umati ukishangilia kwa nguvu sana.


"THIS SCHOOL HAS MADE US USEFUL HUMAN BEINGS...." akaendelea.... "READY TO MAKE NOT ONLY OUR PARENTS PROUD BUT ALSO THE NATION,  OUR BEAUTIFUL NATION, AND THE WORLD PROUD. WE ARE READY TO UNLEASH OUR FULL POTENTIAL TO THE WORLD....."

Makofi zaidi yakafuatia na wazazi kutazamana yumkini wakijiuliza ni mtoto wa nani kati yao. Binti aliongea mambo muhimu kuhusu wazazi, malezi, walimu, elimu, na maisha utafikiri ni mtu mzima mno tena mwenye uzoefu mkubwa wa miaka mingi. Kila alipoongelea wenzake,  au wazazi au hata walimu aliwakazia macho bila kupepesa macho huku akiongea jambo lililowahusu. Yale macho kama ya yule mwanamama Condoleezza Rice au yale ya Michelle Obama akiwa anasisitiza jambo. Binti alionekana kama mzoefu wa kutoa risala au kuongea mbele ya hadhira kubwa. Ungemwona hakika ungevutiwa naye pia.

Kwa mara ya kwanza toka niwe mkubwa nilitamani kurudi utoto pia kama Lady Jaydee na nikagundua bado sijachelewa, kinadharia.


Risala yake ikaisha wakati watu bado wanatamani aendelee. Hakuna aliyewaambia wazazi wasimame lakini ni kama waliambiwa na mtu ndani yao. Wote na wageni wengine na walimu na wanafunzi walisimama na kumshangilia binti yule. STANDING OVATION. Binti akainama na kushukuru. Tena na tena. Na kisha kupeleka risala yake kwa mgeni rasmi.

Mgeni rasmi alishindwa kujizuia na kumpa zawadi ya fedha nzito nzito.

"What's your name?", aliuliza mgeni rasmi.

"My name is CLARISSA...!" Alijibu binti kwa sauti ile ile ya malaika.

"Congratulations Clarissa!"

Binti akashukuru. Umati ukishangilia. Wazazi wakaanza kushika pochi na waleti. Wakaenda kumtuza alipotoka tu jukwaani. Ilibidi walimu wakasaidie kuweka utaratibu maana alizidiwa na fedha.

Sherehe ikaendelea. Kila mara nikawa nikisikia sauti masikioni mwangu ikirudia maneno "MY NAME IS CLARISSA" Hili jina niliwahi kulisikia zamani nadhani, nikawa nikiwaza.

Sherehe ikaendelea.
Ikafikia wakati wa wahitimu kuzawadiwa na shule kwa sababu mbali mbali. Clarissa naye akaitwa mara kadhaa kupokea zawadi. Kila mara akishangiliwa sana! Ndipo watu wakapata kuwaona wazazi wa yule binti.

Lahaula!

Katika watu wote waliokuwepo kuna kijana mmoja alipigwa na butwaa alipowaona wale wazazi wa huyo binti. Kijana huyo ni:

MIMI!


Boy.
Akili yangu ikahama ghafla kutoka kwenye yale mahafali na kurejea miaka 14 nyuma! Nikiwa sekondari. Nikakumbuka mpaka mahali nilipokuwa nimekaa mchana ule miaka 14 nyuma niliposikia sauti ya mmoja wa rafiki zangu wa shuleni akinisemesha:

"Andrew vipi?"

"Safi tu mambo vipi"? Nilimjibu.

"Ah safi tu hivyo hivyo, una muda kidogo"?

Nikafunika daftari langu kisha nikavuta pumzi na kumuuliza:

"Vipi umeachwa"?

Hakunijibu wala hakucheka kama nilivyotarajia. So nikamwambia twende  maeneo ya viwanjani kama ni kitu cha kuongea kwa utulivu. Akakubali.

Tulipofika akaanza kuniambia kuwa jambo analotaka kuniambia linahusu girlfriend wake. Straight forward akaniambia "Ni mjamzito"

Sitasahau nilivyojisikia.
Lakini nikamwambia rafiki yangu maneno haya. "KAMA UMENIITA UNATAFUTA USHAURI WA KUTOA UJAUZITO HUO NAOMBA TUISHIE HAPA HAPA USINIAMBIE CHOCHOTE ZAIDI MAANA  SITAWEZA KUSHIRIKI JAMBO HILO"

Akaniambia: "Ndo maana nimekufata Andrew maana washkaji wote wanasema tukatoe lakini nilitaka na wewe nione utasemaje... ila nimechanganyikiwa kabisa"

Nikawaza mimi ni nani hadi huyu mtu ametaka opinion yangu. Jibu likaja: mimi ni mtu muhimu kwa mtoto aliyetumboni kwa wakati huo.

So nikamuuliza: "Na yeye binti je anasemaje?"

Akasema yeye ameshashauriwa kutoa ujauzito na wenzake wote na hata ndugu zake wa kike!

Kwa kifupi tu nikakaa na rafiki yangu na kwa neema ya Mungu akakubali kuwa hatashauri abortion ifanyike licha ya pressure ya mazingira na wazazi wa pande zote wakija kufahamu. Hasa upande wa binti.

Tukakaa chini tukaandaa mpango wa kuhakikisha ujauzito hautolewi. Tukaenda kwa binti tukamwambia kuna daktari mmoja mtaalamu wa kutoa ujauzito tutampeleka. Siku ilipofika tukamwambia yule daktari amekamatwa na polisi maana alitoa ujauzito wa binti mmoja mwanafunzi akafariki. (Kumbe wapi.) Hapo tunajaribu kumjengea saikolojia ya aogope kuwa kuna kufa.
Visiku vikapitapita.

Binti anazidi kupewa pressure hasa rafiki zake. Wengine walishafanya abortion mara tano. Wanampa uzoefu kuwa mbona ni rahisi tu. Wakawa wanazidi kumwaga siri zao ambazo hata yeye hakuwahi kuzijua kwa kuwatazama tu. Dunia ina siri nyingi..Akaanza kuwa anatusimulia wanavyomshawishi.

Tukaona isiwe tabu. Tukamfata daktari mmoja tukamwambia kuna binti tutamleta kwako anataka kutoa ujauzito lakini akija tunaomba umpimepime kisha umwambie labda mwili wake sijui umekaa vibaya nk. Vyovyote tu afu umwambie utampa dawa kwenye drip. Daktari nahisi aliona vioja lakini akatukubalia tu tukampeleka binti kisha akapimwapimwa na mwisho akawekeza kadrip kadogo kale kumbe kana maji tu. Dah. Sasa sijui niseme Mungu atusamehe. Maana kwa kweli.
Haya binti akaamini ujauzito utatoka after sometime. Kumbe wapi.
Visiku vikaenda.

Hapo tukaanza kuongelea story za watoto watoto. Tukiona wazazi wana watoto wadogo namwambia yule rafiki yangu achekecheke na wale watoto.
Tunamjengea binti saikolojia ya kupenda watoto.

Bila kutarajia ujauzito aliokuwa anaficha umeanza kuwa obvious hakuna cha kuficha tena. Huku sisi tumeanza kuonekana kumjali mno. Huku tunatania mara majina ya watoto yanayovutia mara majina yanayochekesha. Ikafika hatua pressure za rafiki zake na ndugu zikija akiwaza boyfriend wake na pia mimi tunavyomtreat mwishowe akaamua potelea pote sitoi ujauzito tena.
Haikuwa rahisi.
Lakini ilifikia hivyo.

Lakini kilichonisukuma mimi ni kuogopa kuingilia uumbaji wa Mungu. Na kuwaza tu kuwa huwezi kujua huyo mtoto atakuja kuwa nani baadaye!

Miezi kadhaa baadaye katikati ya changamoto nyingi mno zisizosemeka za masomo ndugu na wazazi mtoto alizaliwa.

Wakamwita jina  lake CLARISSA!

Siku zikaenda maisha yakasonga tukaenda njia tofauti tofauti maishani na cha ajabu tukapotezana kwa kweli. Miaka kadhaa baadaye wakaamua kufunga ndoa na kuishi pamoja nk.

Fast Forward miaka 14 toka hiyo story ndo huyo Clarissa aliyekuwa amesimana jukwaani akiwshangaza walimu na wazazi kwa uwezo mkubwa na kipawa kikubwa cha ajabu. Ni Clarissa huyo huyo aliyenifanya nitamani kurudi utoto angalau kinadharia.

Ni Clarissa huyo huyo ambaye nilikuwa na nafasi ya kushauri asije duniani miaka 14 nyuma lakini kwa neema ya Mungu nikawiwa ndani mwangu kuona akija duniani na kuishi na kutimiza alichoumbiwa!

Ni Clarissa huyo huyo ambaye ndugu jamaa na marafiki za wazazi wake hawakutaka aje duniani kwa visingizio vya ni AIBU, huna hela, wazazi wako, masomo yako, utazeeka haraka, nk.

Yote hayo Clarissa alikuwa akiyasikia akiwa tumboni mwa mama yake.

Clarissa ambaye "walio na akili" waliona hakupaswa kuzaliwa lakini akazaliwa.


Nilipigwa na ganzi.

Wazazi wake wameshakuwa na maisha mazuri mno. Clarissa aliyetarajiwa kuleta shida alileta baraka nyingi.

Niliwafata wazazi wake na kuwasalimia.
Walishangaa kuniona pale. Hawakutarajia. Tulikaa sekunde kadhaa bila kujua tuseme nini. Mama wa Clarissa alinitazama machozi yakimlengalenga kwa kumbukumbu ya yaliyotokea. Nilimpongeza sana yeye na rafiki yangu wa shuleni na pia binti yao Clarissa ambaye hakujua kwa nini kati ya wageni wote wazazi wake walionekana kujawa hisia kali wakiongea na mimi. Nilitambulishwa kwake kama "Uncle Andrew" na kuambiwa nilisoma na baba yake.

Nilimshukuru sana Mungu kwa kunipa neema ya kutunza uhai wa kiumbe chake. Nikawaza what if mi ndo ningekuwa nashauri abortion kwa nguvu afu somehow wakaacha kuifanya na kumpata Clarissa halafu ningewaona pale ningekuwa na aibu na fedheha kiasi gani?

So kama wewe ni binti na unawaza kufanya abortion kwa sababu zozote zile kumbuka uanamke wako siyo kwa sababu una jinsia ya kike. Uanamke wako ni pamoja na kuruhusu nature ikutumie wewe kuleta mtoto kwa njia yoyote na wakati wowote ule atakapohitajika kuja huyo mtoto.

Ulishaona kuku anataka kutaga? Akikuta geti au mlango umefungwa atataga hata kwenye bustani. Sasa watu huwa hawalitupi lile yai kisa limetagwa nje. Hulitunza wakijua lina umuhimu wake. Simple logic right? Yes. Nature ikihitaji kuleta mtoto duniani ikakukuta wewe either kwa kupenda au bahati mbaya umepata mbegu za mwanaume katika siku sahihi za kutunga mimba usitake kutupa hilo yai.  Liweke vizuri tu lina kazi yake.

Kama waliotakiwa kubaki duniani ni watu

1. waliozaliwa kwenye ndoa tu
2. ndoa zilizo halali tu
3. mimba zinazoitwa ZILIZOTARAJIWA tu

Hivi hii dunia unadhani ingekuwa na watu wangapi my friend? Fanya research utashangaa. Saaa unadhani Mungu hajui?

Unajua kuna watu wangapi waliofanya vitu vikubwa duniani na walizaliwa wazazi hawajulikani?

Unajua watoto wangapi wameuwa kwa abortion waliotakiwa kuja duniani kufanya mambo makubwa na kutatua matatizo ya dunia hii?

Fikiria mtu kama Alexander Fleming aliyegundua Penicillin angekuwa aborted dunia ingepoteza watu wangapi kwa kukosa penicillin na ampicilin na amoxilin nk.


Ulishawaza Bill Gates angekuwa aborted dunia ingekuwa wapi leo bila Microsoft? Elewa kuwa Mungu yuko ahead of time alijua watu wake wangehitaji hizo software akaamuru mimba itungwe azaliwe Bill Gates.


Sasa wewe ukiabort unaona nini unachokuwa umeinyima dunia? Kisa eti unaona aibu. Kweli? Au unasikia hasira kwa sababu aliyekupa ujauzito ameukana!.

Uanamke wako haupo kwenye watu kukuona hujazaa nje ya ndoa kumbe umeshafanya abortion za kutosha. You're living a lie.

Uanamke wako upo kwenye kukubaliana na hali uliyonayo na kuruhusu nature ilete kiumbe wa kuja kufanya miujiza mingine huku zaidi ya ile aliyofanya Yesu. Yes, Yesu mwenyewe alisema tutafanya makubwa kuliko aliyofanya.
Sasa tutafanyaje kama tunauawa tungali tumboni.

Kina Les Brown na Myles Munroe waliwahi kusema utajiri mkubwa hauko kwenye migodi ya madini kama almasi nk bali uko MAKABURINI ambako watu wamekufa na vipawa hawajavitumia. Nakubaliana nao. Lakini mimi nataka niiambie dunia leo kuwa utajiri mkubwa zaidi wala makaburini haukufika bali uko kwenye vyumba vya siri na kwenye vyoo na kwenye mikasi ya hospitali na mikono ya madaktari ambako watu wakubwa na wenye uwezo mkubwa hawakupewa nafasi ya kufika duniani kabisa kwa sababu walikuwa aborted!Ole wako ukiunyima ulimwengu utajiri uliowekwa tumboni mwako.

Ole wako ukimshawishi mwingine azuie utajiri mkubwa kuja duniani kwa sababu unaogopa aibu kuwa umempa ujauzito binti wakati wewe ni mume wa mtu au ni mchungaji au ni mbunge. Unataka kulinda hadhi ambayo iliondoka ulipofungua zipu na sasa unainyima dunia utajiri kwa sababu ya kulinda eti "heshima". Mungu anakuona! Na dunia ikikosa majibu ya maswali utakuwa responsible.

Ole wako ndugu yangu. Ni nani atakusadia kujibu kesi dhidi ya dunia nzima?

Fikiria wazazi wa Thomas Edison wangemuabort. Tungekuwa na kiburi cha kubonyeza kitufe ukutani halafu balbu inawaka? Unaona THAMANI ya ujauzito wa Thomas Edison?

Unajua kuwa ujauzito unaotaka utolewe huenda ukawa wa THAMANI kuliko thamani ya balbu?

Lakini vipi kama mwanamke kama Oprah angekuwa aborted?


Vipi kuhusu wazazi wa Aliko Dangote? Wangemuabort.

Vipi kama mama wa Dewji angesema sitaki kuzaa sasa hivi?

Mpendao michezo vipi wazazi wa Pele, au Messi au Cristiano Ronaldo wangefanya abortion.Mpaka sasa kuna kina Messi wangapi dunia hii? Jiulize!

Kuna Gandhi wangapi kama yeye.

Mandela wangapi wameshatokea dunia hii?

Vipi kuhusu  wazazi wa mwalimu Nyerere wangemuabort?


Okay labda huko mbali. Tuwe practical kidogo. Huenda umeipenda makala hii. Vipi kama wazazi wangu wangeniabort basi?

Message kama hii iliyoandikwa hivi ungeiona vipi unadhani?
Ungeona zingine tu lakini siyo hii. Believe me.
You see?
Yet mimi nina mambo makubwa sana kuliko hii message.

Kama unawaza kufanya abortion waza tu kuwa sasa unapanga kuinyima dunia kitu CHEMA. Yani unawaza kuinyima dunia vitabu vyenye mambo makubwa na speeches muhimu, muhubiri na mafunzo adimu mno, discoveries na inventions zaidi ya hata quantum physics, entertainments na atristic works zaidi ya Monalisa na vitu vingine vingi ambavyo dunia haijapata kushuhudia!

Ole wako kuinyima dunia utajiri kwa sababu hutaki kuleta mtu duniani ambaye dunia inamtaka aje. Unatupa yai kisa kuku kalitaga bustanini.

Ole wako daktari unayetumia elimu yako kuinyima dunia utajiri mkubwa uliokusudiwa kuisaidia dunia hii na kuitoa katika changamoto ilizo nazo!


Utajiri unabaki kwenye mikasi, na matundu ya vyoo.

Hayo yote nimeyawaza sana. Kama ninavyomuwaza Clarissa na wazazi wake.


Kama umesoma makala hii ukiwa na dilemma ya kutoa ujauzito wako au mtu wako wa karibu au hata wa mbali basi tambua uko karibu na kuinyima dunia utajiri mkubwa. Na dunia itakapolemewa na shida zake na kumlilia aliyeifanya basi atakumbuka jinsi ulivyozuia utajiri na solutions za matatizo mbali mbali kuja mahali pake.

Usikubali kuhusika kuinyima dunia UTAJIRI iliousubiri kwa muda mrefu.

Vumilia tu kama wazazi wa Clarissa!


Yupo afutaye machozi.

Thawabu yako ni kubwa mno ukivumilia. Wakati mbingu zikitambulisha majina ya watu waliofanya vitu vya maana duniani HAKIKA jina lako halitashauliwa.


Asante na Barikiwa sana!


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
WhatsApp +255 788 366 511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com

Ijumaa, 18 Agosti 2017

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED? NI NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA U UCHI?

Wakati nikiwa mtoto mdogo kuna siku nilikuwa naimba wimbo ule wa "NGAPULILA". Niko zangu naimba kwa hisia kweli kweli. Baadhi ya maneno nakumbuka ni haya......

"Rafiki yangu nakuaga mimi oooh,
Nataka kuzamia meli kwenda ng'ambo
Kutafuta maisha eeh, kwani naona maisha ya hapa nyumbani kaka eeh
Yamenishinda
Nakula kwa tabu,
Navaa kwa tabu eeh
Maisha yangu ghetto...
Kulala kwangu ghetto...
Basi naona shida tupu eeh
Shida tupe eeeh

Sina raha maskini mimi ooh
Sina raha hata kidogo,
Ngapulila..."

Wanaoujua watakumbuka lyrics kwa usahihi zaidi. Nachokumbuka ni mama aliposikia nikiimba ALIHUZUNIKA sana. Akaniambia nisiuimbe tena kwa sababu sisi hatuishi GHETTO (tulikuwa tu naishi kijijini lakini nyumba nzuri kwa kweli) na akasema wala sisi siyo MASIKINI (kwa kweli hatukuwa na tatizo la chakula au mavazi yani zile basic needs). Lakini mimi nilikuwa nikiimba huo wimbo nilikuwa naimba kwa hisia kali sababu nilikuwa najiona kuwa ile nyumba tuliyokuwa tukiishi haikuwa ya kitajiri na huenda ndo ghetto yenyewe ya kwenye redio hiyo. (Na kiukweli nilikuja kuelewa vizuri maana ya neno "ghetto" baadaye sana baada ya kuja jijini Daslam na kuzunguka zunguka)­čśŐ

Kumbe sikujua kuwa FIKRA zangu nilikuwa nimesharuhusu watu wengine ikiwemo wanamuziki kuziteka na ku-paint picha fulani ambayo ilikuwa imeshanikaa kichwani na kuanza kuwaza na mimi siku nitoke kijijini nifike huko "NG'AMBO".

Mentor wangu anaita hii kitu "MIND CONTROLLING MIND". Yaani kuruhusu fikra za mtu au kitu kingine kuwa ndo fikra zako na ukaziamini kuliko zile ulizokuwa nazo na ukaanza ku-act accordingly.

Hii ni hatari kuliko HYDROGEN BOMB ambazo North Korea wanatamba kuwa wanazo!

Kupokwa fikra zako ni hatari kwa sababu kiuhalisia na hata kisayansi binadamu ndiye kiumbe pekee chenye uwezo wa KIFIKRA.  Wakakipa hiki kiumbe (binadamu) jina lilalofanania hali hii wakakiita HOMO SAPIENS. Yaani Man (or Animal) Capable of Thought.

Kwa hiyo kuishi kwa FIKRA za wengine ni sawa na kuwa USELESS tu. NA ukishauvaa uhalisia wa kuwa USELESS unaweza kuwa una maisha sahihi kwako lakini ukayaona kana kwamba ni tatizo kubwa kweli kweli kwa sababu si wewe unayewaza bali ni mwingine ndani ya kichwa chako. Na kukubadilisha hadi upate fikra sahihi tena itakuchukua muda mrefu pengine maisha yako yote yaliyobakia.

Nitatumia mfano wa Adamu na Hawa kukuonyesha jinsi gani FIKRA za mtu huvurugwa taratibu taratibu..yani huwa siyo ghafla. Wanaovuruga FIKRA zako huanza taratibu kwa njia na mbinu ambazo si rahisi kuzijua.

Ukipokwa FIKRA itahitaji mtu mwingine akuelekeze na kukuonyesha kuwa tayari FIKRA ulizo nazo ni TATIZO kubwa tayari!

Hii ndiyo maana Mungu alimuuliza Adamu hilo swali maarufu:

"NI NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA U UCHI?"

"WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?"


Swali hilo halikuwa jepesi tu. Wala halikuwa surprise kwa upande wa Mungu? Ila Mungu aliliuliza ili kumsaidia Adam (na mkewe) kujua kuwa FIKRA zao zilikuwa zimeshabadilika na kuwa kitu kingine kabisa.

Why?

Kwa sababu Adam na Eva walikuwa UCHI siku zote toka walipoumbwa lakini hawakuwahi kuona kama ni kitu kibaya. In a way Mungu aliwaumba uchi akijua kuwa endapo wataasi maagizo yake na kuruhusu FIKRA mpya potofu vichwani mwao basi wataanza kuona vitu vya kawaida ambavyo ni vizuri wataanza kuviona ni vibaya including kuwa kwao uchi.

Kumbuka Mungu alipomaliza kuumba aliona kila alichoumba  (ikiwemo kuwaumba wao wakiwa UCHI) ya kwamba NI CHEMA SANA. (Mwanzo 1:31) Fikra sahihi ni kwamba Mungu kuwaumba wakiwa UCHI siyo tu ilikuwa jambo jema bali lililuwa jambo JEMA SANA.

Na kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (likeliness) basi na FIKRA original za mwanadamu ziliona ilikuwa sawa tu kuwa UCHI kama FIKRA za Mungu zilivyoona. Kitabu kinasema walikuwa UCHI lakini HAWAKUONA HAYA (Mwanzo 2:25)
Umenielewa right?
Tuendelee sasa...

ENTER THE DEVIL
Shetani alipoingia alijua ili kubadili maisha ya mwanadamu kama MTAWALA KWA NIABA YA MUNGU ilibidi kuvuruga FIKRA za huyo mwanadamu. Katika kuvizia kwake kwa muda mrefu alipoona fursa ya kutest zali lake alienda STRAIGHT kwenye maneno yatakayovuruga FIKRA.  Na atakuwa alistudy maisha ya hao wapenzi wawili na kugundua nani alikuwa akiongea mwenzake anasikiliza. (Adamu)
Nani alikuwa mgumu kutest zali kwake (Adamu).
Nani alikuwa na sauti inayoweza kufanya mwingine alainike na kusahau kila kitu ndani ya sekunde chache?

Hapa jibu ni HAWA.


Shetani alipoona Hawa akiwa peke yake hakupoteza muda:

"Eti Mungu alisema msile matunda ya miti yote ya bustani?"

First trick hiyo. Kuuliza swali ambalo linaonekana kama la chekechea. Jifunze kuogopa mtu mzima kukuuliza swali la kitoto au la kijinga. Nawaza tu kwamba Hawa wa watu huenda alijicheka kimoyomoyo kwa swali la "kijinga" kama hilo (Matunda yote? Sasa tutaishije na sisi bado "vegans". Si bora tungekuwa walau "vegetarians") Nimewaza tu.

So aliyeuliza na aliyeulizwa wote wanajua hiyo si kweli.

Unaweza kuwaza kwamba lakini Hawa naye si angesema tu "TOKA PEPO".
Wewe mwenyewe mtu akikuleteaga umbea mbona huwa hukemei­čśĽ So siyo rahisi kiasi hicho.

Lakini pia ni kama zinaa. Unaambiwa KIMBIA ukijifanya kuexplain, au kushauri au kukemea utashangaa kitakachotokea.

Tambua pia kuwa HAWA alikuwa tayari VULNERABLE kwa kitendo cha kuwa peke yake bila wasiwasi wa kuwa mbali na mume. Separation.

Kumbuka pia fikra zako zikianza kuvurugwa si rahisi ukajua. So Hawa akajikuta anaendeleza mjadala na shetani... akaanza kuexplain pale akijua anaongea tu na SNAKE.

"Hapana... Ila (Mungu) alisema tusile WALA KUGUSA matunda ya mti ulio katikati ya bustani..." Kama vile haitoshi akavolunteer kuongeza jibu kwamba Mungu alisema wakigusa au kula WATAKUFA.

Shetani akapata dili. Kutoka kwenye swali la kijinga alipata jibu lenye AKILI
Kisha akatumia hilo jibu lenye akili KUVURUGA AKILI za Hawa na hatimaye Adamu.

"HAKYANANI HAMTAKUFA" yani hapo nime-imagine tu huo msisitizo wa shetani.

"HAKIKA HAMTAKUFA"

YOU SHALL NOT SURELY DIE.

Yaani anaongea kama mwenye AUTHORITY.

HAKIKA HAMTAKUFA. Ila ni kwamba..... (akazidi kuvuruga FIKRA za mama yetu zaidi)

"Mungu anajua MKILA:

1. Mtafumbuliwa macho
2. Mtakuwa kama Mungu
3. Mtajua MEMA
4. Na (mtajua) MABAYA pia

Sasa uone jambo moja hapa ambalo shetani hulitumia mpaka leo kuzidi kutumia watu wanaovuruga fikra zetu.

Shetani hakuongelea kabisa suala la KUGUSA matunda. Aliongelea tu KULA.  Lakini maagizo ya Mungu yalikuwa siyo katazo la kula tu bali hata KUGUSA. Mtu anayeBADILI fikra zako hulazimisha fikra zako ziwaze mwisho tu.
Kitendo cha shetani kutoongelea kugusa kilimsahaulisha Hawa hilo kwa muda. Na yumkini alipoamua KUGUSA hakufa. Maana ili ule tunda ulitakiwa kulichuma (kugusa). Kitendo hicho huenda kilimwongezea Hawa nguvu kwenye IMANI MPYA POTOFU ya kuwa kumbe kweli huenda hawatakufa. Baada ya kugusa AKACHUMA.  Kisha AKALA.

Hakufa.

Maagizo ya Mungu yalikuwa in plural. So kama Hawa hajafa logic ya kawaida ni kuwa hata mumewe hatakufa.

So Adamu akapewa.  Akapokea. Yaani naye AKAGUSA. Hakufa.

Then AKALA.

BOOOOM!!!!!!

1. Wakafumbuliwa macho
2. Wakawa kama Mungu (kwa maana tu ya namba 3 na 4 hapa chini)
3. Waliendelea kujua mema
4. Wakajua na MABAYA pia.

Coz Mungu anajua mema na mabaya pia.

TATIZO:
Tatizo ni kwamba kwa kuchagua kumsikiliza shetani FIKRA zao zilibadilika kiasi kwamba yale ambayo mwanzoni waliyaona MEMA sasa yakawa mabaya kweli kweli. Kiasi kwamba kuwa kwao uchi kuliwasumbua kiasi cha kulazimika kuficha uchi wa kila mmoja wao for the first time! Na Mungu alipokuja wakaona AIBU kuonana naye wakiwa vile. Utukufu wa Mungu uliozoeleka ukawa hofu kwao. Zamani waliona mema tu now hata kuonana na Mungu kwa njia na hali ile ile kukawa kubaya."Nimeogopa kwa kuwa nilikuwa UCHI"

Like seriously?  You've been naked all life! So WHO TOLD YOU NOW KWAMBA UKO UCHI?

Kwa maneno mengine NANI AMEKWAMBIA KUWA KUWA KWAKO UCHI NI ISSUE?

Kwa maneno mengine Adamu NANI AMECHAKACHUA FIKRA ZAKO?

NANI AMEKUFANYA UJIDHARAU HADI UJIFICHE?So, my dear reader.....

NANI AMEKUJENGEA INFERIORITY COMPLEX YA KUJIONA HUFAI?

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA WEWE NI MASKINI?

Na ni nani aliyekwambia kuwa NG'OMBE WA MASKINI HAZAI?

Unajua madhara ya kuamini hivyo?

Nani alitwambia SISI ni nchi maskini?

Na ni nani alisema sisi tupo DUNIA YA TATU? Nani alipima DUNIA na alikubaliana na nani kuwa hii sehemu tuliyopo sisi ni ya TATU?
Unajua ndo maana Bill Gates kaja ikawa story kubwa
wakati mimi au Reginald Mengi tukienda Marekani wenyeji wetu tu ndo watajua siyo taifa zima.
Hayo ndo MADHARA ya kuamini tuko dunia ya ngapi sijui.

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

Nani alikwambia kuwa kwa kuwa wewe ni ALBINO huwezi kuolewa? Au huwezi kuwa BALOZI.
Je umepima fikra za mwanasheria na  Balozi Possi?


Nani aliyekupandikiza FIKRA kuwa ili uwe tajiri inabidi umchune binadamu mwenzako ngozi?
Unaona madhara ya kupokwa FIKRA?
Huna malengo, huna mipango, huna mentors,  hujifunzi kwa wenye mafanikio sahihi, hushughulikii kukaa vizuri na akiyekuumba utaacha kuamini kuwa ngozi ya binadamu, au ya kakakuona au meno ya tembo au shamba la bangi ndo vitakupa utajiri?

Nani alikwambia kwa kuwa ulipata ujauzito kwa mazingira mabaya kabisa kwamba unapaswa KUJIUA KULIKO KUENDELEA KUMWONA AU KUMKUMBUKA HUYO MWANAUME?

Nani alikwambia kuwa unapaswa uondoke dunia hii kwa kuwa ulitendewa mabaya? Uliwahi kusikiliza story ya Oprah au Lissa Nichols?


Nani alikwambia kuwa wewe hufai kwa sababu ex boyfriend wako alikuacha?

Nani aliyekuambia ya kuwa wewe ni KILAZA?
Anajua THAMANI ya investment ambayo Mungu aliwekeza ndani yako? Kwa nini unakubali definitions za watu kuhusu wewe ndo ziwe uhalisia wa FIKRA zako?

Nani alikwambia huwezi kufanikiwa bila kusoma ELIMU YA JUU?

Unarisiti ili kuongeza ufahamu au ili kuprove kwa watu kuwa na wewe unaweza kufika Chuo Kikuu? Una prove ili iweje kama siyo INFERIORITY COMPLEX in you imekutafuna for years.

Who told you kuwa usipofika Chuo Kikuu huwezi kutoa mchango muhimu kwa jamii?

Nani aliyekwambia kuwa wewe ni mtupu kichwani, huna future, huna lolote, huna BAHATI. Ilikuwaje kwanza mpaka ukamsikiliza akiongea hadi amalize. Nani alikwambia kuwa huwezi kuanza biashara chini kabisa na ukaja kuwa zaidi ya wote uwaonao juu leo hii?

Nani alikufanya ushindwe kujiamini.
Ngoja nikupe siri. Angalia watu wa ACACIA. Walikula "tunda" kweli kinyume na maagizo. Lakini WALIKUJA. Hawakukimbia.  Mtu mmoja akawaita "WANAUME". And rightly so. They didn't run away. Binafsi nimejifunza kweli kwao. When you've messed up clean your mess!

Ukitaka angalia siku walivyokuja.


In a pack. Like lions.
Confident.
Yaani mtu unamdai afu yuko very confident.
Well suited.
Nigel Chanakira hutumia pia neno "WELL-HEELED" yaani kiatu ambacho soli ni mpya haiko upande.
Kisafiii. Kipyaaaa!

Huyo ni mtu unayemdai anakuja hivyo. Si unaweza kumuogopa bure. No wonder kuna watu fulani walianza kusema "UNAONA WENZETU?". Wakaanza kuaminisha kundi kubwa kuwa "SISI HATUWEZI KUWASHINDA WENZETU SI UNAONA WALIVYOKUJA"

Hayo ndo madhara ya kuamini kuwa tuko inferior kwa "WENZETU". Fikra za kishetani kabisa. Fikra hizi ziliwahi kutetemesha taifa la Israeli wakati wa Musa. Taifa likaambiwa professionals walijiona panzi mbele ya MAJITU.  Hivi professional anayeaminika akijiona panzi mbele ya adui mtu wa kawaida atawaza nini?
 
Hapo ndipo Mungu alipowaza kuwafutilia mbali taifa zima na kuanza na Musa upya (Hesabu 14:11,12). Acha kabisa kupandikiza hofu ndani ya watu. Wanaweza kujawa hofu wakamkosea hadi Mungu kisha akawaadhibu kwa jinsi ambayo hawakuwahi kuona. Kwani Mungu anashindwa nini kuwazungusha jangwani miaka mingi zaidi.  Anashindwa nini kuruhusu lifisadi moja lije kuwa raisi na liirudishe nchi nyuma mpaka kizazi chote hiki kiishe kije kipya.

Umeelewa?

Fikra POTOFU ikipandikizwa ndani ya watu unaweza kuleta madhara ambayo hakuna aliyetarajia.
Na wewe usiruhusu mtu akupandikize fikra eti hutafanikiwa kwa sababu ya SERIKALI au kwa sababu ya Richmond.  Mafanikio YAKO ni WAJIBU WAKO.

Jenga fikra sahihi tu.

Usipoangalia FIKRA zako na kuzichunga utashangaa kumbe siku nyingi mno ushapokwa fikra.  Ndo maana mtu akisema HAKUNA AJIRA unaamini.  Kakwambia nani?
Sikia nikwambie mimi nilipata AJIRA yangu ya kwanza bila experience yoyote na kampuni ilibuni AJIRA hiyo baada ya mimi kwenda interview na kukosa nafasi sababu kuna vigezo sikuwa navyo LAKINI kwa jinsi nilivyojiamini na kujieleza jopo la wa wasaili lilishawishi uongozi utengeneze NAFASI ambayo HAIKUWAHI kuwepo kwenye hiyo kampuni ili tu nisikosekane pale. Sijisifii. Nakupa uhalisia.

AJIRA ZIPO.
Tafuta kama ndicho unachotaka ukikosa ujue siyo kwa kuwa hazipo. Nakupa siri ukienda interview nenda kama ACACIA WALIVYOKUJA!

Nani alikuambia huwezi kuanza biashara yako kwa kuwa huna MTAJI. Unakaa tu kisa "huna mtaji". Nani alikwambia mtaji ni pesa?
Fikra hizo umezitoa wapi. Zimekufanya uwe mpole na mnyonge bure tu.

Nani alikuambia kuwa UKISOMA LAW au ENGINEERING ndo DILI.

Nani amekuambia kuwa HAKUNA HELA MTAANI?
Are you sure hizo fikra hazileti uhalisia huo maishani mwako?
Are you sure fikra hizo haziui creativity yako yako na moyo wa kujituma zaidi?
Niliwahi kusema ukiona wewe huoni hela ila wengine wanaziona ujue tatizo siyo pesa ila ni macho yako.

Nani alikwambia MAISHA NI MAGUMU?
Alikwambia ili iweje?
Unaamini hivyo pia?
Una HAKIKA maisha ya kila mtu ni magumu nchi nzima?

Nani alikwambia Hutakuja kufanikiwa? Why uruhusu fikra zake ziwe ndo fikra zako mpya na unaziamini na kujiona USELESS mpaka fursa za mafanikio unajificha. Ukiitwa kuambiwa kitu cha kukusaidia huendi kwa kuwa umeshajiona HUWEZI.

Nani ALIYEKUAMBIA kuwa huwezi?

Nani aliyekuambia kwa kuwa biashara yako imeyumba basi haitasimama tena kwa hiyo bora ukaajiriwe tu yaishe?
Nani ALIYEKUAMBIA kuwa hutoweza kusimama tena?
Tenda zikitoka unaogopa kujaribu.
Unajificha kwa kuwa "U UCHI"

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

Kubadilisha fikra za Adamu ililazimu sasa ahamishwe mazingira kabisa aende nje ya bustani akajitafutie... ili fikra sahihi zirudi ilibidi asile vilivyopandwa na mwingine bali apande vya kwake upya.
Ili fikra sahihi ziwarejee waIsraeli ilibidi wazunguke jangwani miaka 40.

Nilisema madhara ya kuruhusu FIKRA ZAKO zishikiliwe na wengine ni makubwa kuliko mlipuko wa HYDROGEN BOMB.

Jifunze kujenga FIKRA SAHIHI na utayafikia yale muumba wako aliyokusudia uyafikie kwa WAKATI.

USISEME KAMWE KUWA MIMI SINA HIKI, SINA ELIMU, SINA MTAJI, SINA CONNECTION, SINA MARAFIKI, SINA KIPAJI KAMA CHA FULANI, SINA KWANGU, yote hayo na mengine kama hayo ndo fikra potofu ya "NIKO UCHI".

NANI ALIKWAMBIA KUWA U UCHI?


WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

Barikiwa sana!

#ThreeSixteen

Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511
www.andreamuhozya.blogspot.com

Ijumaa, 28 Julai 2017

UNATAKA KUFANIKIWA? JIFUNZE KUWAAMBIA WATU NENO HILI: "USINITINGISHE TAFADHALI"


"USINITINGISHE TAFADHALI"


Hakika Mungu ni mwema na nina kila sababu ya kumshukuru sana. Wewe pia mshukuru the Mungu.

Leo ninataka kukukumbusha mojawapo ya maneno mengi mno ambayo yatakusaidia kufikia malengo yako. Nalo ni kujifunza kuwaambia watu "WASIKUTINGISHE".

Wakati naanza biashara ninayofanya sasa hivi sikutegemea kupata upinzani mkubwa kiasi hicho kutoka kwa watu wangu wa karibu. Nilidhani kuwa kila mtu ataelewa tu kuwa ni maamuzi sahihi kama nilivyokuwa nikiona mimi. Lakini haikuwa hivyo.

Nilipata upinzani kutoka kila kona.  Kuanzia kwa my love wangu my ubavu wangu. Ndugu zangu. Marafiki.  Nk. Kuchekwa, kukejeliwa, nk. Lakini kanuni moja ambayo imenifanya nisimame na hii biashara mpaka leo ni kwamba nilijifunza jambo fulani utotoni ambalo limekuwa msaada kwangu mpaka sasa.

Wakati tuko shule ya msingi nilipenda sana kuchora na pia kwa sisi wa zamani zamani (eti mmeanza kutuita wahenga) tulikuwa tunafundishwa somo la MWANDIKO!

Bahati mbaya sana kwa sababu ya uhaba wa madawati dawati moja dogo tulikuwa tunakaa wanafunzi watatu hadi wanne.
Kwa hiyo ufanisi wa somo hilo la mwandiko na lile la kuchora (sanaa) ulitegemea sana mtu asikutingishe wala asikuguseguse wala asitingishe dawati!

Kwa sababu nilipenda sana kupata MWANDIKO au mchoro ambao ni PERFECT nilikuwa na-mind sana sana mtu akinitingisha hata kidogo tu.  Kwa hiyo nikikaa tu kidogo nasema "USINITINGISHE". Mbaya zaidi kuna "mamtu" class yalikuwa yamebarikiwa yana mwandiko mzuri hadi raha. Afu na mimi nataka nipate mwandiko wa ukweli afu mtu mara anabadili mkao wake keshakutingisha.  Dah! Ilikuwa inaniumiza kweli. Halafu unakuta mtu haoni kwa nini unahangaikia mwandiko tu ndo unakasirika hivyo!

Mwandiko tu? Kumbe wewe huoni ni mwandiko tu. Unaona SUCCESS, PRESTIGE, REPUTATION, etc.

Leo naona mwandiko wangu si mbaya sana (licha ya kutingishwatingishwa)

Yes.

Kwa hiyo wakati naanza biashara hali ya watu wengi kutokubali ninachofanya niliiona kama "KUNITINGISHA". Na kiukweli sikuwa tayari kuona ninatingishwa wakati nahitaji CONCENTRATION.

Sikumwambia mtu yeyote neno hilo lakini moyoni mwangu na mawazoni mwangu lilijaa. USINITINGISHE TAFADHALI! MSINITINGISHE TAFADHALI!

Nimekuja kuona kuwa watu wote waliofanikiwa katika kitu fulani waliamua kukataa KUTINGISHWA.

Ukiweka huo msimamo hutaeleweka vizuri. Maana wengine hukupinga kwa nia njema. Lakini kama Donald Trump angesikiliza ripoti za CNN na BBC asingefika hapo alipofika. Nakumbuka sana alivyochekwa na anavyochekwa hadi leo. Na kuitwa majina mengi. Kichwani mwake kulijaa na kumeendelea kujaa hilo neno: MSINITINGISHE TAFADHALI

Siyo kwamba hakwami au hakosei. Anakwama mara nyingi kuliko kawaida. Anakosea kweli mambo mengi lakini point ni kwamba hataki KUTINGISHWA wakati anafanya alichokwishaamua kufanya.

Kuna mmoja tunaye nchi hii yeye alisema HAJARIBIWI. Maana yake  USINITINGISHE TAFADHALI.  Na ukimtingisha mtu ALIYEDHAMIRIA kukataa kutingishwa basi utaelewa muda si mrefu.

Watu wote waliofanya kitu na kikawezekana waliweka hiyo attitude: USINITINGISHE TAFADHALI.

Kuna kitabu nilisoma cha kuhusu maisha ya Thomas Edison aliyegundua bulb hii tunayowasha leo.
Aliishi maisha yenye changamoto nyingi na vikwazo vingi. Lakini kichwani mwake ni kama aliiambia tu kila changamoto neno moja: USINITINGISHE TAFADHALI
Maisha ya Bill Gates na Paul Allen ni hivyo hivyo. Jeff Bezos. Jack Ma. Nk.

Yesu aliwahi KUTINGISHWA na mama mzazi kwenye harusi ya Kana huko Galilaya.  Mama anasema: "HAWANA DIVAI". Jibu la Yesu kwa mama mzazi ni kama kumwambia tu "MAMA, USINITINGISHE TAFADHALI ".
Tunasoma pia Yesu akiambiwa na shetani "badilisha mawe yawe bread kama kweli wewe ni mwana wa Mungu" nk. Majibu ya Yesu yote kwa shetani yalikuwa kama kumwambia tu shetani: USINITINGISHE TAFADHALI!

Sijui unaelewa?

Ukitaka kufanikiwa na wewe ni mtu wa kuruhusu kila mtu tu akutingishe hutafanikiwa. You must STAY FOCUSED!

Mafanikio ya aina yoyote yale iwe ni unataka MWANDIKO mzuri au KUFAULU MITIHANI au unataka NDOA IMARA au unataka MAFANIKIO KIBIASHARA au unataka kutimiza ndoto na MAONO yako yanahitaji usiwe mtu wa KUTINGISHWATINGISHWA tu na kila mtu.

Kuna kijana mmoja amemaliza kidato cha sita nimekutana naye hivi juzi tu kupitia hii mitandao. Katika mazungumzo ananiambia anaomba ushauri. Anasema amefaulu mtihani wa Form VI ila kozi aliyotaka kusoma chuo ni PROCUREMENT... lakini watu "wamemtingisha" hadi wakamwambia akasomee mambo ya PLANNING eti ndo DILI. (Sijui wamejuaje) Lakini dogo akakubali lakini kwenda kumwambia "MZEE WAKE" akapinga sana anataka kijana wake akasomee PHARMACY kwamba ndo hatakosa AJIRA mbeleni.
Wamemtingisha dogo mpaka haelewi afanyeje sasa.

Hali hii huwakuta wengi. Unataka kuoa/kuolewa unaambiwa MBONA MAPEMA? Unataka kuanza biashara unaambiwa HEE, HIYO HUTATOKA BORA UFANYE HII. Hahaaaaa! Watingishaji ukiwapa nafasi utatingishika mpaka hutoamini kama ni wewe. Unataka kununua gari unaambiwa SI UJENGE KWANZA? Ukianza kujenga ukakwama wanasema si ungejenga chumba kimoja uhamie hivyo hivyo ndo watu wanaanzaga hivyo. See? Sasa utakuwa REMOTE CONTROLLED na watu hadi lini?

Sikia usichanganye kati ya USHAURI SAHIHI na KUTINGISHWA. Yesu alijua kuwa maneno ya mama yake kwa mama ilikuwa kama USHAURI lakini kwa yeye Yesu ilikuwa kama kuambiwa cha kufanya hasa ukiwa tayari unajua na unasubiri tu wakati muafaka. Mind ya Yesu ilikuwa VERY FOCUSED kwenye huo wakati muafaka aliokuwa akisubiri kiasi kwamba hakutaka KUTINGISHWA kabisaa! "MAMA... SAA YANGU BADO!"

Yaani: USINITINGISHE TAFADHALI

What about you my friend?

Ukishafanya maamuzi fulani kuhusu maisha YAKO unataka mtu mwingine tena aseme nini.

Ngoja nikupe mfano mdogo:

Ukijipanga mstari na watu 10 wa mtaani kwako au familia yako halafu mkawekewa magari 10 tofauti tofauti mbele yenu kila mmoja wenu achague la kwake:

Range Rover,
Jeep Cherokee,
Toyota VX,
Vitz,
Mercedes Benz,
FUSO,
Canter,
Rav 4
BMW
DCM

Wewe utachagua lipi?
Na je unadhani utakalochagua uchaguzi wako ndo sahihi au mbovu kuliko wa wengine? Yani unadhani ukichagua Range mwenzako akachagua FUSO ndo akuone wewe chizi eti kisa kwa nini hukuchagua gari ya kubebea mizigo?? Kwani kila mtu anataka kubeba mizigo?  Kwani hujui kuna watu wana Range na zinawaingizia pesa kuliko wenye FUSO. Na kuna watu wana FUSO wana hela kuliko mwenye Range. Au kama ulichagua Benz afu mwenzako akachagua VX akucheke kwa nini  umechagua gari la chini badala ya kuchukua la juu. Kwani kila mtu anataka gari kubwa dunia hii? Sasa na wewe unaanza kujilaumu eti  ayaa bora ningechagua VX.

Utakuwa hujielewi bado.
Choices zako na decisions zako kama mtu mzima unapaswa kuzisimamia.  Ukikosea si unajifunza tu. Kwani mbona Rais anateua Waziri halafu anagundua baadaye kumbe alikosea au kumbe. Anabadilisha. And life GOES ON.

Jifunze kukataa KUTINGISHWA. Utafika mbali sana sana.


Mimi nimejifunza hilo. Ndo nikaona nikushirikishe na wewe pia. USITINGISHWETINGISHWE


Na wala USINITINGISHE TAFADHALI.


Barikiwa

#ThreeSixteen


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp +255 788 366 511


Jumatatu, 17 Julai 2017

HAKUNA MTU ASIYEWEZA KUFANIKIWA KIUCHUMI #AKIAMUA

HAKUNA MTU ASIYEWEZA KUFANIKIWA KIUCHUMI AKIAMUA


Siku kadhaa zilizopita nilikutana na hawa kina dada wawili mtaani (mitaa ya Sinza) wakiwa wamepumzika baada ya kazi kubwa ya kutembeza mboga za majani mtaani.


Walikuwa wamechoka hakika na walikuwa wamekaa mahali dukani wakiwa wameagiza zao soda baridi kushushia kidogo na labda kulainisha koo kwa sababu ya kazi nzito ya kutembea juani na huku ukiita kwa sauti: "Haya jamani mchicha, mnafu, matembele, mchichaaaaa".

Niliwasalimia na kukatisha safari yangu   ili nikae nao pia ili niendelee kujifunza maisha ningali hapa duniani.

Ama baada ya salamu na maneno mawili matatu ya "Breaking the Ice" nikaanza kureason nao mambo ya biashara na hasa biashara yao.

Mimi:
Hebu niambieni nyinyi changamoto yenu hasa ni nini kwenye hii biashara?

Mmoja wao:
Dah kakangu changamoto ni nyingi mno lakini kubwa ni kwamba watu siku hizi wanaogopa kula mboga za majani si unasikia sijui serikali wanasema mboga zisilimwe sehemu za maji yenye sumu?

Mimi:
Oh poleni nimesikia sikia hivyo pia hasa kuhusu bonde la Msimbazi na Mlalakuwa. Kwani nyie mboga zenu mnatoa huko pia?

Wao:
Hapana sisi tunatoa huko Tegeta! Lakini bado wateja hawaamini wanaogopa tu kwa hiyo kwa kweli ni changamoto.

Mimi:
Sasa kama hali ndo hiyo mnajiandaaje mbeleni mfano serikali ikisema mboga mboga zisiuzwe mtaani ili kuepusha labda magonjwa ya mlipuko nyie mtafanya nini kwa kipindi hicho cha marufuku ya aina hiyo.

Wao:
Eeh kakangu sisi tunaomba tu yasifike huko maana humu ndo tunajipatia kipato chetu na kusaidia mambo ya familia yanaenda. Kwa hiyo serikali isifike huko watusaidie kwa hilo.

(Nikaona nibadili uelekeo wa maswali kidogo...)

Mimi:
Aisee. Kumbe biashara siyo mbaya ee. Safi sana. Kwani kwa mfano kwa kawaida kwa siku mnaweza kutengeneza faida ya shilingi ngapi?

Wao:
Kama siku ikiwa ngumu faida sh 25,000 hivi lakini ikiwa nzuri ni sh 45,000/- mpaka 50,000/- kwa siku!

(Hapo nikawaza upya kabisa. Maana average ya tuseme 35,000/- tu kwa siku 6 wanazofanya kazi ni sh 210,000 kwa wiki. Kwa mwezi ni kama Tshs 840,000/-. Usiwachukulie poa kivile ujue..)

So, Mimi:
Aisee, hongereni sana. Nimeipenda sana bidii yenu. Kumbe mambo siyo mabaya sana. Sasa mna mpango gani na kipato kikubwa sana namna hiyo ambacho mnaingiza kwa sasa? Mnasomesha?

Wao:
Tunashukuru serikali kwa shule za msingi sasa ni bure lakini tuna wa sekondari ndo humu humu tunapata kaka. Tunashukuru Mungu.
(Mmoja wao) mfano mimi mwanangu (akataja jina) anasoma tuition moja na watoto ambao wazazi wao wanafanya kazi kwenye mabenki na hata serikalini.  Kwa kweli Tunashukuru.  Ila ndo hela inaishia huko na matumizi mengine.

Mimi:
Hongera sana. Mnafanya mambo makubwa sana nyie hivi watoto wenu wanajua kwamba nyinyi mnatenda maajabu makubwa namna hii?

Wao:
(Wakacheka kidogo)
Ndiyo wanajua. (Mmoja wao) Wanajua tunavyohangaika mfano mimi mwanangu wa sekondari alirudi nyumbani juzi akaniuliza "Mama nasikia serikali inasema mboga mboga zina sumu, sasa mama wakiwakataza kuuza mi ntapata ada kweli?"

(Alikuwa emotional sana wakati akiongea hivyo so nikaona nikienda huko inaweza kumfanya hata alienda machozi.. si lengo langu for any reason)

Mimi:
Aisee. Sasa mnatamani watoto wenu waje wafanye kazi hii mnayoifanya nyinyi huko mbeleni?

Wao:
Eeh hata! Hii kazi ngumu tunawaambia watie bidii shuleni tu ili wasije wakafanya kazi hii. Migongo inatuuma tukirudi nyumbani, miguu, huku watu mara walalamike mboga zina sumu.

Mimi:
Mna muda gani na hii kazi?

Wao:
Miaka mingi kwa kweli. Zaidi ya tisa.

Mimi:
Wow! Sasa kama hamtaki watoto wenu waje wafanye hiki mnachofanya mmewaandalia akiba yoyote kifedha?

Wao:
Eeh kaka hivi hiyo akiba inatoka wapi hela yenyewe haitoshi ndugu yangu.

Mimi:
Mmesema mnaweza kupata mpaka elfu 45 nk. Sasa hivi unajua ukiweka tu akiba ya sh 5,000/- kila siku unajua kwa siku 10 itakuwa sh 50,000/-? Hiyo ni elfu 50 ambayo ipo tu. Na kwa siku 100 unajua ni sh 500,000/? Na unajua siku 100 ni sawa na miezi mitatu tu na siku 10?

(Nikaona kama "network inasearch kidogo". Nikaendelea kidogo)...

Mimi:
Hivi unajisikiaje dadangu ukiwa na ndugu yako kila baada ya miezi mitatu na siku 10 anakutumia laki 5? Unaweza kufanya mambo mangapi na laki 5?
Lakini mtegemea cha ndugu huwa anafanyaje dada zangu?

Wao:
Anakufa masikini kakangu.. (Kwa huzuni kidogo)

Mimi:
Sasa unaonaje ukajipa mwenyewe hiyo laki 5 kwa kutunza elfu 5 tu kwa siku hiyo elfu 5 ambayo haiathiri sana maisha yako kivile maana unabaki na kati ya elfu 20 hadi 40 kwa siku kwa sababu nyinyi mna uwezo wa kipato cha kila siku. Kati yenu yupo ambaye hawezi kuweka pembeni sh elfu 5?

Wao:
Kwa kweli hakuna..

Mimi:
Sasa TUSAHAU miaka tisa au hata miwili iliyopita. Tuangalie miwili au tisa ijayo. Kwa haraka haraka mwaka ukiisha utakuwa umeweka sh 1,500,000/- ya elfu tano tu ile nyingine unaendelea kutumia.
Baada ya miaka mitano tu una milioni 7,500,000. Fikiria miaka mitano iliyopita hadi sasa kuna milioni 7 na nusu ambayo hukuitunza kutoka kipato chako cha kila siku imepotea.

Mimi:
Ukipata milioni 7 na nusu ukaanza kuwakopesha wauzaji mboga wenzako unajua utakuza kipato chako mara dufu. Kuna Microfinance zilikuwa zinakopesha tu pesa lakini mpaka zimegeuka kuwa benki rasmi sasa (nikawatajia moja). Kumbe hata nyinyi mnaweza na biashara ya mboga unapumzika kabisa miaka mitano tu ijayo. Na mtoto aliyekuwa kidato cha pili hapo atakosa ada ya Chuo? Hata akipata mkopo nusu au robo tu utashindwa kumsaidia mahitaji mengine hapo juu?
Japo ni vizuri umsomeshe tu kwa pesa yako hiyo ya kuweka. Hivi unajua mzazi anayeshangilia mtoto wake kupata mkopo kwa upande mwingine anashangilia mtoto wake kuhitimu akiwa na deni kabla hata hajaanza kuingiza kipato? Watoto wa matajiri wanahitimu bila madeni.  Wa maskini wanahitimu na madeni. Hiyo ndo tofauti mojawapo. Wanaanza maisha wakiwa level tofauti za kiuchumi. Ni vigumu waje kulingana baadaye.

Wao:
Dah kaka yani umetufanya tuone tumepoteza pesa hata kunywa hizi soda jamani. Yani tungeyajua haya zamani mbona tungekuwa mbali mno! Jamani bora hata ulipita na ukatusalimia tumejifunza mengi mno.

Mimi:
Usijali. Hatua zetu tukinuia mema huongozwa na Mungu. So tumshukuru Mungu tu dada zangu.


Wao:
Sasa tunaanzaje?

Mimi:
Kuna wataalamu wa mambo ya uwekaji akiba.  Watu wa mabenki nk. Mkiwakosa niambieni nitawatafutia. Wao wanajua nini ufanye na hiyo sh 5,000 uiweke tu na huwezi kuitoa hadi muda mliokubaliana utimie. Cha msingi siyo hiyo elfu 5 bali ni #NIDHAMU. Hiyo nidhamu watoto wako wakiijifunza wakaibeba na elimu watakayokuwa nayo familia yako na kizazi chako baada yako hawataamini kuwa kuna muuza mboga mboga mitaani ndo chanzo cha wao kufanikiwa.

Cha msingi usijiangalie wewe. Focus kwenye kizazi chako baada yako. Fikiria hali itakuwaje ukiwa mzee na unaona watoto wako na wajukuu zako wamebeba nidhamu nzuri kabisa ya fedha ambayo uliianzisha wewe kwa kuuza mboga mboga na kuweka sh 5,000 tu kwa siku.
Fikiria utakavyokumbuka elfu 5 yako ya kwanza, fikiria inavyoonekana ndogo lakini ilivyobeba utajiri wa vizazi na vizazi.

Wao:
Dah aisee kaka asante Mungu akubariki sana. Yani tunaomba tuje tukae tena tumependa sana mafunzo yako.

Mimi:
Asanteni sana dada zangu aisee.

Mwenye duka (Mangi):
Aisee huwa unatoa semina wapi jamaangu? Maana naona una mambo mazu..! Mazuri aisee.

Mimi:
Nitakuja tuongee zaidi ngoja nawahi mahali maana hata hivyo nilitaka kuwasalimia tu hawa dada zangu.

Kina dada:
Basi tupige hata picha ya ukumbusho maana leo tumepata elimu nzuri sana.(Mangi akawa mpigapicha kwa muda)

Nikawaaga na kuendelea na safari yangu.


Nitawatafuta tena hawa dada zangu nijue wanaendeleaje.....

Usidharau kipato chako....!#ThreeSixteen

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com***The End.****

Jumatatu, 29 Mei 2017

KIPAWA CHAKO NA JINSI YA KUKITUMIA KUTIMIZA MALENGO YAKO KIUCHUMI

:::::::::::::::::::::::::::::::::::

Habari ya leo kijana wa kitanzania. Mungu  ni mwema tuko hai hadi leo.
Naomba muda wako kidogo tuendelee kujifunza kujifunza zaidi pamoja leo.

::::::::::::::::::::::::::::::::::::

Yes...
Mungu aliweka kipawa ndani ya kila mmoja wetu. Ili usife njaa wala usife maskini.

Hata hivyo tunapozungumzia KIPAWA yaani TALENT watu wanachanganya sana mambo, wanaita tu KIPAJI.

Ndo utasikia kuna eti "SHULE ZA VIPAJI MAALUMU" wakati pale wanachomaanisha ni shule za watu waliopata maksi nyingi labda. Wameleta tafsiri mbovu ya hata hivyo "vipaji".

Tafsiri sahihi ya TALENT  ni kitu kinachoitwa KARAMA. Yaani simply ni kitu cha ziada ambacho mtu anacho cha kipekee ambacho mara nyingi wengine hawana. Uwezo fulani alionao mtu wa kufanya jambo muhimu ambao watu wengine hawana. Kila binadamu ana cha kwake.

Hapa tunaweza kupata aina mbali mbali za VIPAWA au UWEZO WA KIPEKEE huo:

Mfano:

1. Kipawa cha Kuongea vizuri
(Orators wazuri wako hapa kama kina Mwalimu Nyerere. Yani akiongea mnapenda hadi uongeaji wake tu yani. Comedians wazuri na na watangazaji kama kina Charles Hilary wako hapa. Yani anavyoongea tu unatamani kipindi chake kisiishe)

2. Kipawa cha Kuandika vizuri
(Ukisoma novel kama Windmills of the Gods ya SIDNEY SHELDON utaelewa maana ya kipawa cha kuandika.
Ana kitu cha kipekee akipewa "pen and paper". Mhe. January Makamba ni mmoja wapo watu miongoni mwetu ambao wana karama hii. Yani akiandika article inakuwa tu ya kipekee from title to conclusion. Huenda ndo maana alikuwa muandaaji wa speeches za Rais Kikwete. Karama. Kipawa. Kipaji)

3. Kipawa cha Uongozi
Unajua watu kama Gandhi?
Yes. Yani anaweza kufanya wananchi wakubali kulala kwenye reli ili kuzuia treni la mkoloni lisipite na wakalala. Anaweza kufanya shule nzima mkagomea chakula. Anaweza pia kufanya msitishe mgomo.  Wafanyabiashara wakubwa wana hii karama.
Hata Yesu alipokuwa duniani alikuwa na hii karama. Yani anaweza kukukuta uko kazini kwako akamwambia tu "FOLLOW ME" na ukaacha kila kitu. Ukamfata.
Hawa ni watu hata kama hatoki familia inayojulikana lakini anakuja kufanya nchi nzima imfate kwa mazuri au yasiyo mazuri.  Napoleon Bonapatre. Unamkumbuka? Margareth Thatcher alikuwa na karama ya uongozi plus ungangari. Na wengine.
Unashangaa hizi nguvu anapata wapi? Nguvu imejificha kwenye karama tu.
Kuna viongozi wa vyama vya siasa hana elimu ndefu kama wengine wala hahangaiki nayo lakini ukimstudy anaweza kufanya watu lukuki wafanye anachotaka.  We unasema ati ana kismati.  What's kismati. Kipawa hicho.. Talent.

4. Kipawa cha Uimbaji.
Wimbo ule ule lakini akiuimba yeye watu wanaweza kushangilia mwanzo hadi mwisho na wakampa na standing ovation wakati wengine hawakupewa yote hayo. Mtu ana sauti nzuri utadhani koo lake lilitengenezwa baada ya mwili wake kuumbwa yani likaumbwa kivyake. Kuna watu kanisani wakiimba huwa najikuta natamani wimbo usifike mwisho. Huwa wananifanya nitamani zaidi mbinguni sema tu sijamaliza kazi kubwa Mungu aliyonipa hapa duniani. Ndo kwanza ninaanza. Lakini mtu anaimba mpaka unahisi ukiitikia utamharibia wimbo vile. Hivyo yani..

Sasa watu wengi wanajua hiki tu ndo kipaji. Au kipaji cha michezo. Basi.

5. Kipawa cha Uchezaji:
Hapa napo ndo wengi wanaishia like I just said.
Lakini kuna vipawa vingi zaidi ya michezo na kuimba kama tulivyoona hapo juu na tutakavyoona hapo chini.

Na hata hapa kwenye michezo kuna kipawa cha kila aina ya mchezo.
(Mfano kuna kipawa kwenye soccer, kwenye football, basketball, racing (ya magari au ya farasi, mitumbwi, pikipiki, baiskeli, nk), riadha, boxing, kung-fu, weight lifting, mieleka, kuogelea, cricket, tennis, kuteleza kwenye barafu au kwenye maji yaani skiing, chess, hockey, golf, gymnastics, na mingine mingi. Kuna tofauti ya Messi na Phelps)
See? Sasa huku kwetu watu wengi wanajua Mbwana Samatta na Hashimu Thabeet basi.

6. Kipawa cha uigizaji
Umesema nani Kanumba? Hujakosea.  Alikuwa na something EXTRA.  Hiyo extra hiyo. Ndo kipawa.
Kuna yule mama mnaijeria yule. MAMA G.

Akiigiza kama Mama Mkwe utamkubali yani utasikia kila anayetazama ile filamu anasema "Huyu mama ana roho mbaya huyu".
Anaigiza hadi unahisi ndivyo alivyo. Hiyo ndo maana ya KITU CHA ZIADA. Kipawa. Mtu hadi anafanana na anachoigiza.

7. Kipawa cha Uchoraji.
Kina Ibra Washokera. Kina Masoud "Kipanya" na wengine. Yani akichora hata kama ni kikatuni tu kikawa hakina maneno utaona tofauti tu. Unakumbuka katuni ya Kingo. Lol. James Gayo huyo. Hazina maneno lakini ujumbe unafika.Kipawa.

Yani nimeona Kingo toka niko mtoto. Ilikuwa inafikirisha sana afu ukiielewa unaona jinsi mchoraji alivyo na kitu cha ziada.

8. Kipawa cha Kufikiri (thinking).
Tofautisha kufikiri na kuwaza. Sizungumzii kuwaza maana kuwaza kila mtu anawaza ila ni wachache wanafikiri. Kuwaza unaweza kuwa huna hela ukajaa mawazo. Mi nazungumzia KUFIKIRI (THINKING).
Kuna watu wana karama hii. Ukimpa a afikirie kitu analeta jibu lenye something EXTRA.
Ulishasikia kitu kinaitwa THINK TANK? Mara nyingi kwenye think tanks kuna watu wenye kitu cha ziada kwenye kufikiria.  Yani ukimpa issue ya mchanga wa dhahabu anaweza kukupa solution ndogo tu na okavango the most effective. Ana karama mwenzako.

9. Kipawa cha Ubunifu (creativity).
Hata wachoraji, watunzi wa vitu nk hii pia wanayo.
But hapa naongelea wabunifu.  Ndo unaona wanabuni magari,
wabunifu wa mitindo ya mavazi, wa matreni, midege ya ajabu, simu hizi na computers nk. Mifumo mbali mbali kama android, MPESA, max malipo, Uber etc. Creativity tu hapo. Sasa mwingine anaweza kukaa miaka nane hajaweza kubuni kitu cha maana. Mwingine mpe nusu saa tu. Inatosha.

10. Kipawa cha Kumbukumbu
(hapa ndo wanafunzi wanofaulu vizuri wapo. Anaweza akasikiliza kidogo tu darasani lakini akakumbuka every detail hata ambavyo mlikuwa mnahisi hakuvisikiliza kwa makini. Na nyie mpaka mmemrekodi mwalimu na notes mmeandika na maswali mmeuliza lakini "pepa" ikija anafaulu yeye zaidi yenu. Ana something EXTRA linapokuja suala la kumbukumbu.
Nk..
Wewe utaomba Roho wa Mungu akukumbushe vitu kwenye mtihani mwenzako hata hajui kuimba labda. Lakini anapata "A" wewe unaondoka na karai.
Kumbuka kipawa alipewa na Mungu. Na wewe una cha kwako labda michezo.  Ndo hivyo.

SASA TUENDELEE..
Nadhani hadi hapo unaweza kuona Michael Jordan alikuwa wapi, na Diamond Platnumz  yuko wapi, Ronaldo na Messi na kina Mbwana Samatta wako wapi, Roger Federer yuko wapi, Tiger Woods yuko wapi, na Les Brown yuko wapi Dan Brown yuko wapi, Jack Chan alikuwa wapi, Kanumba alikuwa wapi, Michael Phelps yuko wapi, Alexander Bell, Mohammad Ali na kina Tyson walikuwa wapi katika hizo hapo juu. Nk.

Yaani Tyson hakujaribu kulazimisha kuimba, Ronaldo hajalazimisha kuchora, Diamond hajalazimisha kuogelea, kina siku nilisema Dan Brown anajiandikia zake vitabu hajalazimisha kuongea kama Les Brown na Les Brown naye hakujaribu kuandika stori za kuvutia kama za Dan Brown na wote wamekuwa mamilionea.


TALENT YAKO NA MAFANIKIO KIUCHUMI
Ni ujinga kumwonea wivu mtu anayefanikiwa kupitia kipawa chake ilhali kila mtu alipewa cha kwake. Muhimu ni wewe kutafuta cha kwako.

Talent ni njia kubwa mno ya kuweza kukupa pesa nyingi na kukufikisha katika utajiri. Leo hii Michael Jackson alishafariki lakini bado analipwa mamilioni, lakini watu lukuki wako hai na hawajui senti tano wataipata wapi...

Lakini anagalia watu kama Michael Jordan na kina Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, na wengineo. Angalia waigizaji kama Tyler Perry na kina Samuel Jackson au Angelina Jolie uone wanavyopata pesa nyingi mno kupitia vipawa vyao.

Siwezi kutaja kila mwenye kipawa hapa maana hatutamaliza. Michezo tu pale juu nimetaja mingi mingi na hiyo ni michezo hatujaongelea vipawa vingine  kama vipawa vya thinking and creativity (ubunifu)  ambao hawa ndo wanabuni mitindo ya mavazi, ya magari, ya ndege na computer na simu na drones nk lakini pia ndo wanabuni solution za migogoro mikubwa ya kati ya mataifa. Hawa nao wanatengeneza pesa nyingi mno. Mfano mtu anayebuni gari la Rolls Royce au Bentley au Ferrari nk hao wanatengeneza pesa nyingi na hawachezi mpira wala hawaimbi R n B au pop!

Tatizo la watu wengi hasa huku kwetu ni kuwaza kuwa vipaji ni mpira na nyimbo na bongo movie basi. Yani kama hajui kuimba wala kucheza wala kuigiza basi. Katoto kakiimba kama Ali Kiba eti ndo kana kipaji.  Kali Kakichora chora ukutani kila siku katakemewa eti kanachafua nyumba.

Lakini point ya msingi hapa ni kuwa kipawa kinaweza kumpa mtu utajiri mkubwa. Kuna wnamichezo wanapesa nyingi mno. Kuna watu wa vipaji wengi wana pesa nyingi. Kuna watu wanalipwa mpaka dola laki 7 kuongea mahali. Yaani kwa saa moja. Imagine! Hiyo ni kama Tshs BILIONI MOJA NA MILIONI 400!!! Kwa saa! Sasa si unaona kipaji kinavyoweza kukufikisha mbali? So usingángáne tu na Bachelor of Law kama niliyosoma mimi. Dan Brown kitabu kimoja tu kinaweza kumpa dola milioni 10. Yaani BILIONI 20! Hivi unaelewa? One BOOK. Sijui INFERNO sijui DIGITAL FORTRESS.

What’s your TALENT? Usidharau nguvu ya kipawa chako. Mungu atakushangaa na ATAKUADHIBU. Trust me. You MUST FIND OUT ni nini Mungu alikupa. Hakuna ambaye aliumbwa bila kupewa kitu EXTRA. Kila mtu anacho. Ndo wenzetu Ulaya wakikijua kwa mtoto wao wala hawahangaiki eti akasome "vidudu" afu aende primary school asome rundo la vitu kisha aende sekondari asome vitu kibao bado high school bado chuoni.  Wakati kumbe yeye mngempeleka kuendeleza kipawa cha kupiga mbezi tu kwenye mabwawa angetangaza nchi na umaskini kwenu ingekuwa bye bye. Lakini mlitaka tu awe daktari. Au mhasibu. Halafu sasa amekuwa what next. Ndo unakuta yeye akiwa kazini anawaza weekend ifike kuna mechi ya bonanza akacheze. Kipawa kilipotezwa.

Usidharau hii. Ukiitumia unaweza kufika bungeni na ikulu mpaka hata UN na wala form four hukumaliza. Wengine wamesoma mpaka maktaba inawajua na ikulu wanapasikia tu.


CONDITIONS ZA KIPAWA CHAKO KUKUFIKISHA KATIKA MAFANIKIO KIUCHUMI

Vipawa pia vina mahitaji yake.

1. Ubora wa team yako.

Moja ni kuwa ili kipawa kikuletee utajiri inahitaji TEAM WORK. Yaani lazima uwe na team ya watu wanaokuhandle wewe na mambo yako yote. Mfano angalia mtu kama Cristiano Ronaldo au Messi. Hafungi magoli bila team work. Yaani anategemea vipaji na creativity ya watu wengine kwenye team ili afike mbali zaidi. Ukimuweka Messi timu kama Mtibwa Sugar hatawika kama anavyowika huko aliko maana huko aliko amezungukwa na professionals na watu wenye creativity na vipawa vya aina ya kwake pia.


Lakini pia Ronaldo au Messi ana kocha wa mazoezi binafsi, ana mshauri wa kisaikolojia anamlipa yeye, ana Manager wake binafsi, mwanasheria wake binafsi, ana mtaalamu wa chakula anayemshauri ale nini asile nini (huyu siyo mpishi ni mtaalamu tu yani nutritionist), ana daktari wake binafsi na wa timu pia yupo. Maana ukitegemea daktari wa timu afu akawa kwa mchezaji mwingine itakuawaje? Ana mtu wa mitindo mfano kinyozi na stylist wa mavazi kabisa,  ana mwalimu wa kufundisha mtoto wake nyumbani, ana designer wa nyumba na wafanyakazi wa nyumbani kama wapishi, watu wa usafi, gardeners, nk.

See? Haya yote watu hawajui wanapomshabikia Ronaldo au Messi au Tiger Woods.

Sasa kama unataka kutumia kipaji kuufikia utajiri inabidi ufundishwe ukweli kama hivi. Usije ukaenda tu Bongo Star Search halafu hujui WHAT IT TAKES kukupelea kwenye mafanikio makubwa kupitia kipaji chako. Inahitaji investement kubwa mno. Na NIDHAMU YA MAZOEZI KUBWA SANA.

Na bahati mbaya sasa investment hii indo inakuwa tena BURDEN kwa mwenye kipaji maana ana watu wengi wa kuwalipa. Inakuwa MZIGO MKUBWA mno. So unashangaa mtu analipwa paundi 365,000 kwa wiki moja tu (yani $468,000/- yaani Tshs BILIONI MOJA) anazipeleka wapi? Unahisi ukizipata wewe utakuwa tajiri. No. Nilishasema hauwi tajiri kwa kupata hela nyingi ila kwa kuwa na MINDSET ya utajiri kwanza. Na kuhakikisha fedha inapita kwenye mfumo wa kuzaa tena.

Unaweza kusema hawa hela zao wanazitumia vibaya..no. Licha ya kununua majumba na magari ya kifahari na kufanya masherehe nk  lakini pia wanalipa watu wengi mno. Kama nilivyoainisha hapo juu. Tena hapo nimeweka vitu general tu.

Kwa hiyo kama una kipaji cha kuongea kama mimi (Public Speaking) unataka kuwa kama kina Les Brown ama una kipaji cha kuandika pia kama mimi (Writing) na unataka kuwa kama kina Dan Brown ama kama kina John Maxwell basi unapaswa kujua kuna TEAM inahitajika. Nani atakuwa mentor wako? Nani atakuwa mtunza fedha wako? Nani atakuwa trainer wako. Mentor na trainer ni watu wawili tofauti. Kina Les Brown walijiandikisha katika madarasa ya DALE CARNEGIE ambaye alikuwa mtaalamu wa kufundisha kitu kinachoitwa Public Speaking.

Sikiliza... Dan Brown mpaka amalize kuandika novel moja anaweza kusafiri nchi 10 kukusanya data na kufanya mikutano na watu maarufu duniani na inamgharimu pesa nyingi na muda mwingi kuandaa manuscript hadi iandikwe.

Nani atakuwa MANAGER WAKO? Wa kuorganise wapi ukaongee na ulipwe shilingi ngapi nk. Usije ukawa wewe ndo kila kitu.  Messi hakuna hakufanya hivyo. Aliandaliwa.  Nani anakusaidia kujiandaa?

Changamoto kubwa ya watu wenye vipawa huku kwetu na hata duniani ni kuwa wanafanya kila kitu wao wenyewe. Kwa hiyo anakuwa hana tofauti tu na mtu aliyejiajiri. Anakuwa kama jongoo miguu mingi lakini spidi kidogo. Kipaji kikididimia naye anaishia hapo.
Lakini ukimtaka Les Brown aje Tanzania  sasa huongei naye yeye unaongea na watu wake. Yeye sasa ni TAASISI.
Hilo ni jambo la kwanza la kuzingatia. Tengeneza team around your talent. Skilled people. Uwalipe.

2. Vipawa vingi vina muda fulani tu.
Yes.
Changamoto ya pili ni timeframe. Hasa kwa wanamichezo. Kwa mchezo kama Soccer kuna muda wake. Umri ukienda mwili unakataa. Unastaafu bila kupenda. Tofauti na uandishi kwamba umri unavyokwenda ndo unazidi kuwa bora zaidi na zaidi.

Mbwana Samatta ana miaka kama mitano au sita tu hivi ya kuhakikisha ameshatimiza ndoto ya kucheza timu kubwa maana vijana wadogo wenye  vipawa vikubwa ni wengi kwenye ulimwengu wa soka kwa hiyo anatakiwa ajitahidi mno. Kwa sasa ana miaka 24. Miaka mitano ijayo mwska 2022 atakuwa na miaka 29. Hapo mwili umeanza kuchoka na wenye vipaji wadogo zaidi watakuwa wameshaibuka wengi. Ni vigumu kukuta bado akicheza timu kubwa mwaka 2025. See? Huo ndo ukweli. Kina Msuva na Kichuya watakuwa wapi?  Ni lazima wafikirie.
Lakini Masudi Kipanya anaweza kuwa bado anachora kipanya chake mpaka hata 2050.
Ni muhimu kujua kipawa chako timeframe yake imekaaje.

3. Vyanzo vingi vya mapato.

Cha tatu ni kuwa lazima uwekeze maeneo mengine usitegemee kipaji chako tu. Katika wanamichezo wote ni Michael Jordan tu ambaye amefikisha utajiri wa dola BILIONI MOJA. Yani ndo yuko kwenye Forbes List ya binadamu  matajiri duniani. Nazungumzia athletes (wanamichezo kama mpira riadha nk) ni yeye tu bilionea. Yani yuko level kama ya Rostam Aziz kwa utajiri
 Sinza mchezo ujue.. lakini hii ni kwa sababu analipwa kwa matangazzo na ana miradi mingine zaidi na zaidi. Kwa hiyo kina Messi siju Ronaldo bado sana kufikia NETWORTH ya dola bilioni moja. Ndo maana unasikia Ronaldo kafungua mradi huu ama ule.

Ndo maana unaona kijana kama Diamond anawekeza kwenye sijui pafyumu, internet, na mambo mengine. Ukisubiri hela za matamasha tu na mechi nk kuna siku kipaji kitaisha makali yake. Kipaji kina life span yake maana hata wewe mwenyewe una life span yako. Angalia watu hapa kwetu kama Mr. Nice. Walipata pesa nyingi lakini hana washauri hana plans hana team ya professionals wa kumshauri cha kufanya matokeo yake SEASON YAKE ilipopita akapotea. Juma Kaseja na Mrisho Ngassa season imepita. Kina Bombi wachekeshaji season imepita. Emanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) amekwenda kwenye kilimo na biashara ya chakula na security na uchimbaji madini. Anatambua kuwa kuna siku Ze Comedy itakuwa hahiwiki tena. Sijui kama inawika tena kwanza.

Swali la kujiuliza je wewe una kipawa gani? Na umeshaanza kukifanyia kazi? Au bado? Una umri gani? Kipawa chako watu waliofanikiwa nacho walitumia MUDA GANI kufikia utajiri? Usiende tu.


GOOD NEWS IS UNAWEZA KUANZA SIFURI

Uzuri ni kwamba hata kama huna shilingi unaweza kuanza hapo ulipo. Mimi nimeanza kuandika 2013 kupitia hii mitandao ya kijamii. Sikuhitaji pesa. Labda bando tu.

Lakini pia nillianza kuandika kitabu changu cha kwanza 2015 ambacho nilikimaliza mwaka huo huo ila toka hapo nakirekebisha na kukipeleka kwa watu wenye mafanikio na upeo zaidi yani kuongeza ideas na kurekebisha na naamini itakuwa ni moja ya best books duniani.
Kiko kwa lugha ya kiingereza. It's a book for the nations.

Lakini pia mwaka jana October nilianza kozi ya Public Speaking na kuongeza uwezo mzuri zaidi wa kiingereza mpaka sasa naendelea nayo na kila siku nafanya mazoezi ya kiingereza na ya kuzungumza kwa sababu pia nina kipawa cha kuongea.
Kwa hiyo najiandaa tu zaidi. Siku nikifika kwenye World Economic Forum kuongea niweze kufikisha ujumbe kwa usahihi na kuwe na hiyo intelligibility.

Point ni kwamba. Nilianza hapo nilipo. Ni watu wanaoniambia kuwa naweza kuandika "vizuri". Mi napokea na kushukuru na kutendea kazi..
Nikienda mahali kuongea ni watu wanaoniambia kuwa naweza kufanya vizuri pia eneo hilo.
Point ninkuwa nimeanza nilipokuwa. Bila kitu. Na wewe unaweza kwa kipawa chako ulichonacho. Haijalishi nani anavuma sasa usiogope. Mentor wangu alisema one day kuwa ukitazama nje mchana kuna kunguru na ndege wengi tu wote wanaruka kuna mpaka mbu na vipepeo.  Vyote vina ruka na hakuna kinachosema "mbona nakosa nafasi ya kurukia". Smart man. So usiwaze kuhusu hilo.  Unaweza pia.

Lakini lazima uzingatie yale mambo matatu niliyoyasema pale juu: yaani team work na timeframe na kuwekeza kwenye vitu vingine.

Na pia lazima uzingatie kwamba ili uweze kukifanya kipawa chako kuwa biashara itahitaji uwe vitu vitatu: yaani bidhaa au huduma, system na team. Hili ni somo linalojitegemea.

Ukitambua kipawa chako unakuwa umetambua kama 50% ya kitu ambacho Mungu alitaka ufanye huku duniani.  Maana kipawa kitalitumikia KUSUDI. Na ukitambua kipawa chako ukaki develop basi hutakufa njaa wala hutakufa maskini. Mungu alimake sure hilo amelifanya kabla hujaja duniani. Usimwangushe!
So ukisema SINA MTAJI Mungu anakuangalia tu. You have something in you.
Vipawa viko vingi. Usilazimishe kipaji cha kuimba huku wewe una cha kuigiza. Usilazimishe cha kuchekesha kumbe una cha kufikiri.
Tambua kipawa chako pasi na shaka. Ujue kabisa mimi niliwekewa hiki.


OK BYE..

Niishie hapo kwa sasa na  naamini utapa mwanga zaidi ili kujua uanzie wapi kama unataka kuitumia njia hii kuufikia utajiri. Ni imani yangu kuwa umejifunza kuhusu njia hii na wewe kama wewe unaweza kuona kama inakufaa au la.

Ila utaona tu kuwa siyo shortcut. Usijaribu kuwa tajiri kwa short cut. It takes time!

Asante sana kwa kuwa hapa na karibu kwa maswali maoni michango zaidi nk.

Much Love!


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp #o788366511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com