Ijumaa, 23 Septemba 2016

STORY OF AN UNSQUEEZED ORANGE

STORY OF AN UNSQUEEZED ORANGE

So I just asked myself this: what happens when an orange (like the one pictured here) goes #UNSQUEEZED? Well, it becomes useless and will eventually get rotten. And quickly forgotten.

It may have been plucked from the orange tree by the farmer but that wasn't its purpose for being there.

It may have found its way to the market place, like many other lucky oranges, but that wasn't its purpose either: to just end up on the market place.

It may have been picked up by a customer like luckier oranges and eventually get to that kitchen table that most oranges dream of.
But that also wasn't its purpose.

An orange must go through a very painful process that will make it 'bleed' a little: it must first be CUT and then as though that isn't enough, it must be *SQUEEZED.*

So I took a few seconds and looked up the definition of the word SQUEEZE just to check what language experts say. And I got this from Cambridge Dictionary

Squeeze:

"to press something firmly, especially from all sides in order to change its shape, reduce its size or remove liquid from it."

Uh-huh!

And so I thought how many oranges grow on an orange tree in one season? How many grow and get ripe? How many get plucked from the tree? How many reach the market place and how many are damaged or fall by the way side and never get to the market? How many get bought from the market? How many get to the kitchen table? How many are at least cut to find if they are worthy squeezing? And how many are actually SQUEEZED??

Is the number of squeezed oranges the same as the number of oranges that grew from the orange tree? Well, I thought the answer would be no.

This made me feel so sad for all those oranges that grow from orange trees around the world. I grew up in a village so I know how an orange appears on an orange tree. A very beautiful process for those who know it. I felt really sad that some oranges die from the tree while still tiny beautiful things, some die as they grow, some get rotten while on the tree, lucky ones get plucked and get taken to the market place and luckier ones get to the kitchen table and only a few - the luckiest, get cut and squeezed. They fulfill their purpose. But then I thought? Luck? Or they stood their ground and got attractive enough to appeal to the farmer's and customer's sight?

Well, that aside.
So I thought what kind of orange am I?
How far have I gone in the process?
Am I still on the orange tree?
Am I on my way to the market place? And if so, am I still attractive and good shaped enough to appeal to the "buyer's" sight?
Am I on my way to the kitchen?
Or am I actually in the painful cutting-and-squeezing  process?? Coz if I am already there then I should be bold like a grown orange. Bold enough to accept the painful piercing of the knife's edge cutting through me. Oranges bleed silently. I should. I should accept strong hands of life's challenges squeezing me from all sides so that the juice in me, my life purpose, my call, comes to fruition. Oranges never resist the squeezing process. But unfortunately many a times I do. What a strange orange I am!!!

The fact that I have made it to the kitchen table sometimes makes me take it to my pig head. I begin to think of all the poor lads who never made it this far. I feel I'm better than most folks. I forget I remain uncut and still have all the juice in me!! And I think God is a fool? That he formed me to just end on the kitchen table? But that's me. Poor me.

And when a feel a strong hand's touch and sense from afar that I am about to get cut into two here? Oh no. I dread the process. I think of the beautiful shape I have and all that will be gone? I look admiringly at my big size, and someone wants to reduce it? Oh no. I start thinking: maybe I should roll by the kitchen's table and fall down. So that when I'm picked up perhaps I won't be worthy the cut. Poor me. I'm picked when I fall. And sometimes I'm never good enough again. I get trashed into the bin. End of my story.

And in my little mind happy I still am. That I made it to KITCHEN UNIVERSITY.
That I made it to the KITCHEN COMMERCIAL BANK.
That I made it THE UNITED KITCHEN OF AMERICA.

I think of all the lads that never made it this far. I think of how I dodged the cutting process on the kitchen table. I made it this far without a scratch on my skin. And I smile. I forget that I'm in the dust bin. Forgotten. Unused. With life unfulfilled. I forget that I'm way on my way to obscurity. To the abyss of world history. I forget that I wasn't supposed to go to the bin with all the juice in me. I forget that there are many other oranges growing from orange trees and looking forward to cooperate to the end and fulfil their purpose. I forget that I was fooling myself all along. I forget that I led my life comparing my "progress" with that of other oranges whose lives mattered less to me as far as fulfilling my purpose was concerned. Poor me.

But then I made it, so I think. To the #UnitedKitchenofAmerica!! Not many people got the golden chance!...
How uninformed!
How lost a mind I have in my pig head. And I don't know that I'm actually just schooled but yet to be educated. Sadly. So tragic.

But then slowly somehow deep down me I begin to feel something strange. I somewhat feel unfulfilled. I begin to think that even though I made it this far but I am actually poorer than those who died on the orange tree while still tiny beautiful things. I feel like I owe them all and others something. Even though I smile but that's only on the outside. My heart bleeds from the inside. I begin to realize that I'm still full of all the juice in me. What for??? And as I contemplate my fate in the darkness of this bin with the bad smell of pieces of bread and every kind of junk around me, I see a dead orange in here. All-squeezed and empty! And then I ask myself: WHAT ON EARTH WAS I THINKING? "Somebody heeeeelllp?" I start shouting. Nothing. "Heeeeellp!!!" Nothing. Oh no. I hope I get a miracle and get rescued from this bin. I hope I get a chance to fulfill my purpose.

Well now, what about you dear orange?

Are you happy you made it to the United #KING-chen too??? Or that you too were schooled at CAMBRI-chen, or HAVAR-chen University? Happy that you come from a family of oranges that have it all? Happy that you got farther than most of us poor oranges? Happy that you made it farther than the stubborn orange tree that didn't want to release you for so long till someone plucked you off it? You forget that that orange tree fulfilled its purpose although it doesn't know how the market looks like or how Kitchen University or Kitchen Telecom or Kitchen Commercial Bank looks like. Are you happy too? Happy that you made it to the kitchen table, unlike other oranges? Happy that you know way more stuff that most oranges will ever imagine? Well, lucky you. But make sure you don't go uncut and unsqueezed. Or you'll have wasted all your life for nothing. My message to you is: Leave ALL THE JUICE IN YOU behind.
Accept to get cut and squeezed. Don't worry about other oranges. Fulfill your purpose and perhaps that will make a difference.

Note:
If you are still uncut and unsqueezed and you have no idea how on earth to get yourself ready for the preccess. Or if you are in the bin and want to know how to get back and and become any useful again just shout out loud.

Good luck!

Thank you, dear orange.

Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
+255752366511

Jumatano, 21 Septemba 2016

KIPI HUNA KATI YA PESA NA MUDA? PESA? MUDA? VYOTE?

.
KIPI HUNA KATI YA PESA NA MUDA? PESA? MUDA? VYOTE?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUDA MWINGI ILA HAWANA PESA

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo. Akiscroll post za chini akakuta kuna mtu kapost kuhusu UKAWA yumo. Akikuta kuna mtu kapost mtu ana uvimbe mkuuubwa watu wameambiwa wacomment AMEN na yeye huyo anacomment AMEN. Kundi hili ni kundi lenye watu wengi mno. Watu wa aina hii kufanikiwa ni bahati nasibu. Labda kwa bahati tu akutane na post nzuri kama hii na post zingine nzuri huenda ikamsaidia. Otherwise hawa ndo hawaelewi maisha yanaenda wapi maana hawana kitu fulani specific wanachofanya. Wakisikia tu kuna kitu kiko kama dili hivi wanaenda. Wakikuta kumbe kinahitaji bidii na kujituma wanaondoka. Wanataka maisha mazuri yaje tu yenyewe. Hawa huwa na maisha magumu zaidi. Ukimwambia njoo nikuonyeshe njia bora zaidi anakuja. Coz muda anao. Hana shughuli maalumu. Wanahudhuria matamasha na semina nyingi mno lakini hawafanyii kazi chochote. Wamezoea kuishi bila mpangilio maalumu. Ndiyo default life yao. Wanarejea maisha yale Yale ya muda mwingi bila cha kufanya

2. WANA PESA ILA HAWANA MUDA

Hili ni kundi la watu wenye shughuli fulani ya kiuchumi. Labda ameajiriwa au amejiajiri. Wako busy kweli kweli. Na ukweli pesa inaonekana. Hawa huwezi kumwambia njoo tuonane akaja hapo hapo. Huyu lazima apange kwanza ratiba zake. Maana yupo busy. Au lazima aombe ruhusa kazini. Au labda atoroke ndo anaweza kupata muda wa kufanya mambo yake binafsi. Au asubiri weekend ambapo kila ratiba itategemea siku hizo mbili, kama ni ibada, usafi, kutembelea wagonjwa au ndugu kwenda mahali kuona labda kiwanja kinauzwa au kuona ujenzi au mradi wake unaendeleaje nk. Mara nyingi watu wa kundi hili hushindwa kufanya vitu vingi vinavyohusu maendeleo yako binafsi mfano kujisomea, kuhudhuria semina zinazofundisha mambo yanayoweza kuwa na manufaa kwake nk. Sababu ana ratiba iliyobana. Ukiwa na sherehe ukamwomba mchango hashindwi kukuchangia angalau chochote kile lakini muda wa kuja kujumuika na wewe ni vigumu akaupata.
Hili ni kundi ambalo kuna watu wanaitwa MIDDLE CLASS people. Watu wa maisha ya kati. Mambo yako si mabaya sana lakini si kwamba ni mazuri. Wasomi wengi na watafutaji wengi wapo hapa. Na wengi wao huishia kupata changamoto za kiafya ukubwani au uzeeni kama stress na maradhi mbali mbali nk. Sababu ya kutokuwa na muda hata wa kuangalia afya zao, mazoezi, kupumzika vizuri nk kwa kuwa walikuwa busy siku zote. Maisha ya watu hawa middle class mwishoni  huja kuwa magumu kwa kuwa hata kuwa na muda na majirani tu ilikuwa ishu. Kwa kuwa wengi wana magari (mengi ni mkopo. Wengine gari la kazini) na kwa kuwa wanaweza kulipa kodi ya nyumba au hata kupata kakiwanja na Kuanza kujenga huko Malamba Mawili basi wanaridhika. Hawawezi kuota kumiliki nyumba Masaki au kununua kiwanja Upanga. Kama upo kundi hili lazima uanze kutafuta mbinu mbali mbali za kuyakabili maisha vizuri siku za usoni. Waangalie wastaafu ambao walikuwa busy zamani. Saivi utasikia mgongo, miguu, macho nk vinasumbua. Hawa ndo ukimkuta social media wengi wao wako critical kwa kila kitu. Maana haoni kama ana shida yoyote. Lakini siku akiambiwa kazi imeisha hata kama ana PHD utasikia "nimekosa mimi nimekosa sana".
Wakati alipokuwa akipewa mbinu mbadala alikuwa critical. Ukimwambia kitu anakuuliza wewe una nini? Default picture yake ni average life. Not extraordinary life.


3. HAWANA MUDA WALA HAWANA HELA

Ulishasikia mtu anaambiwa "busy for nothing"? Ni kitu kama hicho. Yani mtu unakuta labda ni kibarua tu mahali anatumwa kazi asubuhi mpaka jioni. Labda ameajiriwa kazi ya ulinzi, au gereji, au kwenye mradi wa ujenzi anabeba zege au kupaka rangi. Hashindi njaa ni kweli lakini ukweli hana hela. Wala hatamani kuendelea kuwa hivyo. Kuamka alfajiri kulala saa tano usiku. Hela anayopata inatosha kula kwa mama ntilie tu na nauli. Basi.
 Hawezi kuota hata gari. Hata ya mkopo. Maana hata hakopesheki. Huyu hata muda wa Facebook ni nadra akiingia ni kupitisha macho afu anatoka. Au hata simu ya Facebook hana.


4. WANA MUDA NA WANA PESA

Hapa ndo utakuta wale ambao hana tena shida ya pesa. Pesa iko. Hana tena shida ya muda. Akihitaji kwenda mahali haombi ruhusa wala kuaga mtu labda kumuaga mwenza wake tu. Anaweza kusikia kuna shamba linauzwa mahali na hahitaji kutafuta hela tena ili akalinunue bali anaanza michakato ya kisheria pale pale kununua kama amelipenda. Kuna siku nilienda Morocco Square hapo Kinondoni jirani na Airtel kuna Apartments zinajengwa nikaonana na watu wa NHC waliokuwa wanakagua ujenzi unaendeleaje. Nikawauliza hizo apartments zinauzwaje wakasema kuna za milioni 600 na za milioni 800. Na unatakiwa kulipa cash 10% (yaani aidha milioni 60 au 80 cash) halafu inayobakia unaweza kuimalizia ndani ya miezi 12. Na kuna watanzania kadhaa wamenunua tena kwa hela halali. Hawa wako kundi hili hapa. Hela ipo. Muda upo.
Kuna watu walienda kutembea Marekani kibiashara walipokuwa njiani kurudi wakapita mahalinchi nyingine wakakuta kuna mnada wa nyumba kwenye nchi hiyo. Hawakujiuliza mara mbili wakanunua. Kuna wazee fulani wana mtoto wao alikuwa akisoma Canada. Alipograduate wakamuuliza unataka kuishi wapi akasema huku huku Canada wakamnunulia nyumba Canada. Ukisikia hivyo unaanza kuwaza ni mafisadi. Mawazo yako ninkuwa bila ufisadi watu hawanunui nyumba Canada. Kwa taarifa yako Hawa siyo waajiriwa serikalini wala popote ni wafanya biashara.. Kundi la watu kwenye pesa. Na muda. Wanaweza kuamua kesho wakaenda kutembea visiwa vya Comoros. Watu wanaoishi kundi hili wana discipline kubwa ya maisha. Hawa ni watu wanaopenda kujifunza kila siku. Ukimwambia una idea hakatai kukusikiliza. Coz anaamini kuwa hata mafanikio yake yalitokana na kujifunza vitu vipya.Na watu wengi wanatamani kufika kundi hili. Lakini HAWANA discipline ya kujifunza tabia zinazoweza kukufikisha huko.


Swali muhimu tu la kujiuliza tu ni kuwa je, wewe upo kundi lipi.

Una muda mwingi lakini huna hela? = fukara

Una hela nyingi lakini huna muda? = middle class

Huna muda wala huna hela.. Vijisenti unavyopata vinaishia nauli kula kodi ya nyumba nk? = maskini

Au una muda mwingi na hela siyo shida tena? = tajiri.


Jibu unalo mwenyewe. Hakuna mchawi. Shida siyo Magufuli shida ni wewe kuamua kujifunza how utoke hapo ulipo au uendelee kusubiri Tanzania ya Viwanda.
Sisi tupo katika program ya kusaidiana mawazo tu. Nini unaweza kufanya kufika kundi hilo la nne. Kama unataka kujifunza karibu.

WhatsApp #o788366511 au #o752366511. Mafunzo ni bure ila tu uwe *serious.* So kama unaona unahitaji kujifunza au una ndugu yako rafiki yako mdogo wako nk unayetaka aanze kujifunza mapema mambo muhimu badala ya kupoteza muda mtandaoni mpatie namba hizo.


Semper Fi

Andrea G. Muhozya
Darbes Salaam, Tanzania
East Africa

Jumatatu, 12 Septemba 2016

UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO



Zamani nilikuwa nashangaa kwa nini Bill Gates anasema "kama ulizaliwa maskini hilo si kosa lako ila ukifa maskini hilo ni kosa lako" mpaka nilipogundua #makosa mengi ambayo watu #maskini hufanya. Makosa ya watu maskini ni mengi nitataja machache:

1. KUNA MTI WENYE MZIZI MMOJA?
Ulishawahi kuona mti wowote wenye mzizi mmoja? Hili nilifundishwa jana na mdogo wangu Josinah Leonard. Sasa maskini wengi wameshikilia ajira (au kibarua, au labda ana kakitu anauza) kama njia PEKEE ya kuwaingizia kipato wakati hata mwembe tu au mpapai au mti wowote ule una mizizi mingi tofauti tofauti ya kupata chakula na maji kutoka ardhini.
Ndo maana hakuna tajiri yeyote mwenye mkondo mmoja wa kipato. Wengi wanadhani Bill Gates anamiliki Microsoft tu. Ana vyanzo lukuki vya mapato. Kama wewe una chanzo kimoja cha mapato basi uko mbioni kufa maskini.

2. MAWAZO MGANDO
Kisha nikakumbuka pia maskini wengi wanafanya kosa la kuishi kwa mawazo ya zamani. Yani unakuta akiwaza biashara anawaza duka. Kwani kuna tajiri yoyote mwenye duka au vibanda 1000 vya MPESA? Hujiulizi?. Dunia imebadilika maskini hawabadiliki kichwani. Kampuni kubwa ya TAXI duniani (yani UBER) haimiliki gari hata moja.  Lakini ndo kampuni kubwa ya usafiri wa TAXI duniani.  Anatumia taxi za watu wengine.  Wewe bado unawaza kununua bajaji na boda boda! Things have changed. You must also change.  Kuna mengi ya kueleza hapa ngoja niendelee na mengine. Lakini hapo pia palinifanya nielewe kauli ya Bill Gates.

3. PERSONAL DEVELOPMENT
Maskini wengi hawasomi vitabu. Sikia hakuna tajiri asiyesoma. Bill Gates ana wiki mbili kwa mwaka ambazo yeye huzitumia kusoma vitabu vipya ambavyo hajawahi kusoma maishani
. Hebu jiulize Bill Gates anajifungia kusoma vitabu ili iweje? Wewe ukijifungia ndani ujue unaangalia series. Ukiulizwa umesoma vitabu vingapi mwaka huu hadi sasa January to September... Usikute labda hujasoma kabisa hata kimoja. Lakini message za WhatsApp ulizosoma mwaka mzima huu zinatosha kuchapisha magazeti ya Nipashe ya kujaa kwenye kabati lako la nguo! I mean that's a shame mate. Vitabu hutaki. Ukifa maskini hapo utakataa kuwa si kosa lako? Si unaona sasa kuwa utakubaliana na Bill Gates pia. Listen,  SOMA VITABU. Acha kuishi kwa knowledge ya Mzumbe University sijui UDSM ya miaka mitano au 7 iliyopita sijui bachelor of nini? Soma vitabu huko ndo kuna maarifa. Mtaani hela hazifati Ph.D ya mtu. Kama ni hivyo maprofessor wangekuwa ndo matajiri.  Knowledge ya pesa ina maarifa yake tofauti na Masters of Arts au Ph.D ya mambo ya mazingira. Kama chanzo chako cha taarifa za mafanikio bado ni Tumaini University au ni magroup ya WhatsApp utachelewa sana kujua habari za mafanikio.  Hakuna tajiri asiyefanya personal development. Hata ungekuwa na elimu kubwa kiasi kipi kama hufanyi personal development utabakia kuwa significant katika maeneo mengine lakini si eneo la fedha. Kwa hiyo vitabu ni sehemu ya hiyo personal development. Kuna seminars, nk. Sasa jiulize semina ngapi zinazoongelea mafanikio umehudhuria mwaka huu.?  Ngoja nikwambie kitu usipofanya Personal Development thamani yako itabaki kuwa ile ile ya miaka 7 iliyopita. Jana nilikuwa na kiongozi wangu mmoja katika biashara yetu. And akasema amepata fursa ya kualikwa sehemu kwenda kufanya TRAINING (mafunzo) kwa watu fulani wa "maana".  Jumla ya hao watu ni 165. Jumla ya siku ambazo atatoa hayo mafunzo ni siku 5. Na kila mtu katika hao watu 165 atalipa sh 300,000/- kwa siku. Sasa fanya mahesabu sh laki 3 mara 165 hiyo ni hela yake ya siku halafu zidisha mara siku tano!! Umepiga hiyo hesabu? Sasa wewe unataka tu ukalime vitunguu au matikiti uwe milionea kesho.  Maarifa unayo? Maarifa hujengwa taratibu. Siku nyingine ntaongelea vizuri zaidi kuhusu hiyo personal development.

4. TIME MANAGEMENT
Kosa jingine maskini wanafanya ni kupoteza muda.  Time management mbovu. Hasa vijana. Aisee. Hawana ratiba.  Ratiba pekee waliyonayo baadhi ya vijana ni ratiba ya mechi za premier league anajua ratiba za Manchester hadi mwakani. Lakini ratiba yake ya kila siku kwamba akiamka anaenda wapi hakuna. Hana hata kadiary au ka notebook hata kale ka sh elfu moja.  Angalau awe anaandika vitu muhimu maishani nk.. Nothing. Ana magroup ya WhatsApp ya mpira, ya siasa yani moja linaitwa UKUTA 1 jingine UKUTA MAKAMANDA, UKUTA KANDA YA MAGHARIBI, UKUTA ORIJINO, mtu huyo huyo mmoja bado yuko magroup ya waliosoma pamoja na waliofanya kazi pamoja ambayo yote hayo habari kuanzia asubuhi hadi jioni ni UKUTA uleule. Anacopy message za huku anapeleka huku. Haya.  Mwingine ana magroup HAPA KAZI TU, WATASOMA NAMBA, MAGUFULI JEMBE, CCM KAMPENI, UMOJA WA VIJANA, CCM VYUONI, ukimwona yuko busy utadhani karani wa chama. Wengine  wako kwenye magroup ya NGONO TU maana huku Facebook na instagram kuna watu wanatangaza kutafuta namba ili wakuunge kwenye hayo magroup na unakuta namba 900 au zaidi. Unabaki unashangaa hawa watu muda huo wanaupata wapi? Hapo mtu akishindwa kufanikiwa ni kosa la mzazi? Au la mwenyekiti wa mtaa? Au Naibu Spika? Au la Kubenea? Kweli? Yani Kubenea anahusikaje kukufanya wewe ufanikiwe kiuchumi. Sipatagi connection. Sikia. Linda muda wako kwa WIVU MKALI na ujitenge na kila kitu kinachoiba muda wako. Time is MONEY.


5. KUTOFIKIRIA VIZAZI VIJAVYO
Kosa jingine maskini hufanya ni kutofikiria vizazi vijavyo.  Sasa hii sijui laana? Maana wenzetu hawako hivyo.Mtu hafikirii kuwekeza kwa ajili ya watoto na wajukuu. Muda wako ukiutumia vizuri leo utawafanya watoto wako na wajukuu watumikiwe na mataifa. Lakini kwa style ya wengi wetu hii ya kujifikiria wenyewe ilimradi wewe unamudu kulipa kodi na kula na kuvaa basi watoto Mungu ataleta riziki. Khaaa? Kwa taarifa yako Mungu alisema unapaswa kuacha urithi mpaka kwa wana wa wanao (yani wajukuu). Sasa jiulize hiyo shughuli yako rasmi kwa sasa mwanao anaweza kuja kuiendeleza baada yako. Kwa ajira hiyo ni impossible. Mungu akikuchukua wanaweka tangazo moja kwenye notice board la kifo chako jingine kwenye gazeti la kutafuta mtu wa kujaza nafasi yako. Hiyo ndo reality. Hapo Kubenea hahusiki. Jamani msishangae namtaja sana Mhe. Kubenea ni mbunge wa jimbo langu na namtaja kuwakilisha wabunge wote. Sasa ukianza kuwaza kuhusu vizazi viwili baada yako utajiona jinsi ulivyo nyuma mno. Watu wanajifikiria wenyewe tu.  Ndo maana ni rahisi kuridhika na vihela vidogo. Hutaki kuhangaika ili wajukuu waje wafaidi. Unataka ufaidi wewe kwanza eti unasema "kwa nini nijitese".  Kwani kwa nini Yesu "alijitesa"? Ukiambiwa hivyo unasema" kwani mi Yesu?" shauri yako. Watoto wako au wajukuu watafukua kaburi lako afu watatoa hiyo skeleton waitandike bakora weee afu waizike tena. Omba ujengewe kaburi lako kwa nondo na zege. Wengi wanabaki maskini kwa mawazo ya ubinafsi wa kutowaza watakaokuja after you.

6. KUFIKIRI KUWA KUANZA BIASHARA INAHITAJI UWE NA MTAJI KWANZA
Wengi wamekwama hapa.  Anafikiri kuwa inabidi atafute mtaji kwanza afu ndo atafute cha kufanya. Wakati anautafuta mtaji fursa zinaendelea kumpita.  Akija kuupata anapata matatizo hela tena inatumika kutatua matatizo ya kifamilia.  Anaanza upya tena. Mwisho anaamua kusema basi nahisi "Mungu hapendi". Maskini wengi wana kauli rahisi rahisi tu. "Si wote lazima tuwe matajiri". Anajijumlisha kwenye neno *wote*.  Mtu anayefanikiwa anajua mtaji wa kuanza biashara ni kitu cha mwisho na ni kitu chepesi mno kuliko vingine vyote. Lakini wengi wanawaza mtaji.  See? Kitu cha mwisho na *chepesi* anakifanya kiwe cha kwanza na kigumu.

Sasa hivi naielewa sana kauli hiyo hapo juu ya Bill Gates.  Ukifa maskini hilo ni kosa lako. Anyway.. Kama unataka kujifunza zaidi mambo ya aina hii ama shida yako ni hapo kwenye namba 6 au namba 4 au namba 1 labda unawaza kuwa na vyanzo vingi vya mapato afu hujui unaanzia wapi na unatamani kupata ushauri au una biashara haiendi kokote mwaka wa sita sasa huenda kuna mahali unakosa basi njoo WhatsApp #o788366511 au #o752366511 ujifunze zaidi.

UKIBADILIKA, KILA KITU KITABADILIKA.

Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.

USHAURI WA BURE KWA WANAOWAZA KUFANYA BIASHARA

MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA

Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujajiingiza kwenye biashara. Nimekuwekea baadhi ya mambo hayo hapa chini. Haya ni yale niliyojifunza on the ground ndani ya miaka yangu michache hii ya ujasiriamali toka mwaka 2011 katika biashara mbali mbali nilizofanya. Ukiyazingatia utaona faida yake.

1. HAKIKISHA UNA ELIMU YA BIASHARA
Simaanishi diploma sijui certificate ya chuo au zile notes za Commerce. No.  Hiyo siyo elimu ninayomaanisha. Namaanisha aina ya elimu kwa vitendo kama vile apprenticeship. Yaani kujifunza kwa mtu taratibu uone jinsi biashara inavyofanyika. Kama hilo ni gumu kulingana na mazingira basi hakikisha biashara unayotaka kuifanya au mradi unaotaka kuanzisha una watu wanaofanya kitu hicho hicho walio tayari kukupa elimu kila siku hasa miaka miwili ya kwanza katika jambo hilo. Watu watakaokuwa tayari kukupa siri za mafanikio bila kukuficha. Watu watakaokuwa tayari kukushika mkono kwa dhati mpaka ufikie malengo yako.. Ukijifanya "gangwe", wewe ndo sijui "godzilla" kwa sababu shuleni ulipataga B+ ya Business Law itakula kwako mpaka upate mvi za kope kabla ya muda. Labda kama shida yako ni kufanya show off.  Lakini kama shida yako ni kufanikiwa katika ulimwengu wa biashara unahitaji mtu anayejua hicho kitu vizuri ambaye yuko tayari kukupa information za wapi pa kukanyaga wapi pa kukwepa. Hii ndo elimu nayoiongelea.



2. USIDHARAU MWANZO MDOGO.
Usianze kitu kipya kwa gharama kubwa hususan kwa mara ya kwanza. Ukajikuta unakopa milioni 5, 10, 50, nk ili ukafanye biashara mpya ambayo hata hayupo mtu wa kukuelekeza kwa dhati namna ya kuifanya. Utaishia kupoteza hela za watu na kudaiwa na labda kupata stress au hata heart attack. Na kama utakuwa umeajiriwa bado utaathiri hata ajira yako sababu ya stress. Haya ninayasema kwa experience. Ukipenda chukua huu ushauri kwa umakini sana. Anza kitu chenye mtaji mdogo. Hata Biblia inasema si busara kudharau mwanzo mdogo.  Usitake kuanza alipo Shigongo leo.  Au Dewji. Kubali kuanza kidogo. Halafu ukue taratibu taratibu. Itakupunguzia stress zisizo za lazima. Nilijifunza hilo pia ndani ya miaka hii mitano ya ujasiriamali na biashara.

3. FANYA UTAFITI LAKINI JALI MUDA.
Fanya research kuhusu chochote ambacho unataka kufanya.  Huenda umeshauriwa ufanye biashara fulani. Chochote ambacho mtu atakwambia ukafanye. Google kama ikibidi. Angalia information kuhusu hicho kitu. Tafuta walioifanya WAKAFANIKIWA.  Yaani mfano unataka kuanza ufugaji kwa nini uende kwa walioanza wakashindwa wakati walioifanya wakafanikiwa wapo?  Ukitaka kujiunga na chuo unauliza walio disco au waliofaulu? Fanya utafiti na kusanya zaidi information kutoka kwa waliofanikiwa kuliko waliofeli hiyo biashara. Bottomline is fanya utafiti wa kina.  Ili ujiridhishe. Usisisimke tu.
Na utafiti usifanye miaka nenda rudi. Unataka kufanya biashara au kuumba dunia nyingine? Muda haukungoji. Na kuna vitu ukichelewa kuvifanya katika umri fulani au katika msimu fulani itakugharimu sana. Mfano kama ulikuwa unafanya utafiti wa kufungua Internet Cafe toka mwaka 2002 mpaka leo hivi hata ukiamua kufanya hiyo biashara leo si utakuwa unapoteza muda tu bure? Season yake ilishapita. Maisha hayakusubiri. Fanya utafiti ila jali sana muda.

4. KAMA HUTAKI KUOGA UMEVUA NGUO ZA NINI?
Nimeongelea ufanye utafiki. Sasa kama baada ya utafiti wako utaona moyoni mwako kuwa kuna manufaa ya kuifanya hiyo biashara au kufanya huo mradi basi usijiulize mara mbili. Fanya mara moja. Maana ukianza kujiuliza na wakati umeshafanya research yako vizuri ni dalili tu ya moyo wenye woga woga na wasiwasi ambao kwenye biashara itakuwa kikwazo cha mafanikio. Jifunze kuamini utafiti wako mwenyewe. Watu wengi wamekwama hapa eti. Woga woga tu.  Woga si moja ya kitu cha kuja nacho huku ndugu yangu.  Huku inabidi ujifunze kujiamini. Watu wengi huwa wanakwama hapa. Keshaona kuwa kitu anachotaka kufanya ni sahihi lakini anakuwa bado tu anasitasita. Yupo kama hayupo. Mwisho hela ya mtaji anakula na ule moto aliokuwa nao wa kuanzisha mradi au biashara unazimika anarudi nyuma hatua 50. Mpaka arudishe tena ule moyo wa kuanza tena miaka mingi ijayo na wengine ndo basi tena. Anabaki mtazamaji na mkosoaji wa wengine wakati yeye hata kuanza alishindwa.

5. NANI ANAIFAHAMU VEMA HIYO BIASHARA?
Labda unataka kuanza kilimo tena cha matikiti labda. Je unamfahamu mtu yeyote ambaye anaijua vizuri biashara hiyo nje ndani? Kuanzia mbegu, aina (species) za hayo matikiti, misimu ya mauzo, wadudu shambulizi, nk. Usiombe ushauri kwa mtu asiyejua hiyo biashara kwa namna moja au nyingine. Mfano umeamua kuuza nguo. Unaenda kuomba ushauri kwa muuza magazeti kuhusu biashara. Yeye biashara yake ni leo kwa leo. Yaani leo kama habari UKUTA na kesho habari ikawa kupanda miti basi mambo ya jana  yanakuwa siyo dili tena. Sasa unadhani atakushauri nini? Au unataka kuanza biashara ya kuuza mafuta ya mzeituni (Olive Oil) unaenda kuuliza kwa mama ntilie eti akwambie kama yana soko wakati yeye anapikia mafuta ya kuchakachua. Unadhani atakwambia ukafanye hiyo biashara? So don't ask the wrong people.  Eti unakuta mtu anasema "mimi mama yangu ndo my best friend lazima nikamuulize".  Wakati hana ufahamu nayo. Mbona ulikuwa humuulizi ALGEBRA ulipokuwa shule? Si unaona ee? So..Tafuta mtu anayeijua.

6. UNA NGOZI YA FARU?
Ukitaka ku excel kwenye biashara lazima uwe na ngozi ya faru. Niliwahi kujifunza mahali kuwa Faru ana ngozi ngumu mno. Na kwamba zamani wakati wa zana duni za uwindaji walikuwa wakitumia mishale kwa ngozi ya Faru ilikuwa ikishindwa kupenetrate ile ngozi yake. Na pia kuwa faru anaweza kuwa na ndege mgongoni kwake wanakula wadudu au wanarukaruka pale mgongoni na wala asifeel kama wapo. Inabidi uwe na ngozi ngumu. Kuna watu watakukatisha tamaa, kunachangamoto na mishale mingi itarushwa hakikisha una ngozi ngumu na utashinda hiyo mikikimikiki.

7. NINI TAFSIRI YA MAFANIKIO KWAKO?

Kwa wengi mafanikio ni kupata pesa nyingi. Wengine hata ukimuuliza pesa nyingi kwako ni sh ngapi hana idea. Wengine mafanikio kwao ni magari na majumba wengine mafanikio ni starehe, wengine mafanikio ni kutoa sadaka na kusaidia wengine zaidi wengine mafanikio ni kuajiri watu wengi, wengine mafanikio ni kusomesha watoto international school wengine mafanikio ni kuwa na vitega uchumi wengine mafanikio ni kuwa na akiba kubwa benki nk wengine mafanikio ni kula vizuri na kuwa na afya bora nk. Wewe kwako mafanikio ni nini? Ili ufanikiwe lazima kwanza uwe na definition ya mafanikio yenyewe. La sivyo unaweza kupata kila kitu katika biashara na bado ukawa unahisi hujafanikiwa kabisa. Hii imewasumbua wengi.


Kuomba Mungu ni jambo constant wala sina haja kukwambia. Ni sawa na kuoga. Mpaka uambiwe? Nadhani unanielewa.

So if unapenda kujua zaidi biashara sahihi katika zama hizi karibu kwa WhatsApp #o788366511 au #o752366511 kujifunza.

Semper Fi,

Andrea Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.