Jumatano, 21 Septemba 2016

KIPI HUNA KATI YA PESA NA MUDA? PESA? MUDA? VYOTE?

.
KIPI HUNA KATI YA PESA NA MUDA? PESA? MUDA? VYOTE?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUDA MWINGI ILA HAWANA PESA

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo. Akiscroll post za chini akakuta kuna mtu kapost kuhusu UKAWA yumo. Akikuta kuna mtu kapost mtu ana uvimbe mkuuubwa watu wameambiwa wacomment AMEN na yeye huyo anacomment AMEN. Kundi hili ni kundi lenye watu wengi mno. Watu wa aina hii kufanikiwa ni bahati nasibu. Labda kwa bahati tu akutane na post nzuri kama hii na post zingine nzuri huenda ikamsaidia. Otherwise hawa ndo hawaelewi maisha yanaenda wapi maana hawana kitu fulani specific wanachofanya. Wakisikia tu kuna kitu kiko kama dili hivi wanaenda. Wakikuta kumbe kinahitaji bidii na kujituma wanaondoka. Wanataka maisha mazuri yaje tu yenyewe. Hawa huwa na maisha magumu zaidi. Ukimwambia njoo nikuonyeshe njia bora zaidi anakuja. Coz muda anao. Hana shughuli maalumu. Wanahudhuria matamasha na semina nyingi mno lakini hawafanyii kazi chochote. Wamezoea kuishi bila mpangilio maalumu. Ndiyo default life yao. Wanarejea maisha yale Yale ya muda mwingi bila cha kufanya

2. WANA PESA ILA HAWANA MUDA

Hili ni kundi la watu wenye shughuli fulani ya kiuchumi. Labda ameajiriwa au amejiajiri. Wako busy kweli kweli. Na ukweli pesa inaonekana. Hawa huwezi kumwambia njoo tuonane akaja hapo hapo. Huyu lazima apange kwanza ratiba zake. Maana yupo busy. Au lazima aombe ruhusa kazini. Au labda atoroke ndo anaweza kupata muda wa kufanya mambo yake binafsi. Au asubiri weekend ambapo kila ratiba itategemea siku hizo mbili, kama ni ibada, usafi, kutembelea wagonjwa au ndugu kwenda mahali kuona labda kiwanja kinauzwa au kuona ujenzi au mradi wake unaendeleaje nk. Mara nyingi watu wa kundi hili hushindwa kufanya vitu vingi vinavyohusu maendeleo yako binafsi mfano kujisomea, kuhudhuria semina zinazofundisha mambo yanayoweza kuwa na manufaa kwake nk. Sababu ana ratiba iliyobana. Ukiwa na sherehe ukamwomba mchango hashindwi kukuchangia angalau chochote kile lakini muda wa kuja kujumuika na wewe ni vigumu akaupata.
Hili ni kundi ambalo kuna watu wanaitwa MIDDLE CLASS people. Watu wa maisha ya kati. Mambo yako si mabaya sana lakini si kwamba ni mazuri. Wasomi wengi na watafutaji wengi wapo hapa. Na wengi wao huishia kupata changamoto za kiafya ukubwani au uzeeni kama stress na maradhi mbali mbali nk. Sababu ya kutokuwa na muda hata wa kuangalia afya zao, mazoezi, kupumzika vizuri nk kwa kuwa walikuwa busy siku zote. Maisha ya watu hawa middle class mwishoni  huja kuwa magumu kwa kuwa hata kuwa na muda na majirani tu ilikuwa ishu. Kwa kuwa wengi wana magari (mengi ni mkopo. Wengine gari la kazini) na kwa kuwa wanaweza kulipa kodi ya nyumba au hata kupata kakiwanja na Kuanza kujenga huko Malamba Mawili basi wanaridhika. Hawawezi kuota kumiliki nyumba Masaki au kununua kiwanja Upanga. Kama upo kundi hili lazima uanze kutafuta mbinu mbali mbali za kuyakabili maisha vizuri siku za usoni. Waangalie wastaafu ambao walikuwa busy zamani. Saivi utasikia mgongo, miguu, macho nk vinasumbua. Hawa ndo ukimkuta social media wengi wao wako critical kwa kila kitu. Maana haoni kama ana shida yoyote. Lakini siku akiambiwa kazi imeisha hata kama ana PHD utasikia "nimekosa mimi nimekosa sana".
Wakati alipokuwa akipewa mbinu mbadala alikuwa critical. Ukimwambia kitu anakuuliza wewe una nini? Default picture yake ni average life. Not extraordinary life.


3. HAWANA MUDA WALA HAWANA HELA

Ulishasikia mtu anaambiwa "busy for nothing"? Ni kitu kama hicho. Yani mtu unakuta labda ni kibarua tu mahali anatumwa kazi asubuhi mpaka jioni. Labda ameajiriwa kazi ya ulinzi, au gereji, au kwenye mradi wa ujenzi anabeba zege au kupaka rangi. Hashindi njaa ni kweli lakini ukweli hana hela. Wala hatamani kuendelea kuwa hivyo. Kuamka alfajiri kulala saa tano usiku. Hela anayopata inatosha kula kwa mama ntilie tu na nauli. Basi.
 Hawezi kuota hata gari. Hata ya mkopo. Maana hata hakopesheki. Huyu hata muda wa Facebook ni nadra akiingia ni kupitisha macho afu anatoka. Au hata simu ya Facebook hana.


4. WANA MUDA NA WANA PESA

Hapa ndo utakuta wale ambao hana tena shida ya pesa. Pesa iko. Hana tena shida ya muda. Akihitaji kwenda mahali haombi ruhusa wala kuaga mtu labda kumuaga mwenza wake tu. Anaweza kusikia kuna shamba linauzwa mahali na hahitaji kutafuta hela tena ili akalinunue bali anaanza michakato ya kisheria pale pale kununua kama amelipenda. Kuna siku nilienda Morocco Square hapo Kinondoni jirani na Airtel kuna Apartments zinajengwa nikaonana na watu wa NHC waliokuwa wanakagua ujenzi unaendeleaje. Nikawauliza hizo apartments zinauzwaje wakasema kuna za milioni 600 na za milioni 800. Na unatakiwa kulipa cash 10% (yaani aidha milioni 60 au 80 cash) halafu inayobakia unaweza kuimalizia ndani ya miezi 12. Na kuna watanzania kadhaa wamenunua tena kwa hela halali. Hawa wako kundi hili hapa. Hela ipo. Muda upo.
Kuna watu walienda kutembea Marekani kibiashara walipokuwa njiani kurudi wakapita mahalinchi nyingine wakakuta kuna mnada wa nyumba kwenye nchi hiyo. Hawakujiuliza mara mbili wakanunua. Kuna wazee fulani wana mtoto wao alikuwa akisoma Canada. Alipograduate wakamuuliza unataka kuishi wapi akasema huku huku Canada wakamnunulia nyumba Canada. Ukisikia hivyo unaanza kuwaza ni mafisadi. Mawazo yako ninkuwa bila ufisadi watu hawanunui nyumba Canada. Kwa taarifa yako Hawa siyo waajiriwa serikalini wala popote ni wafanya biashara.. Kundi la watu kwenye pesa. Na muda. Wanaweza kuamua kesho wakaenda kutembea visiwa vya Comoros. Watu wanaoishi kundi hili wana discipline kubwa ya maisha. Hawa ni watu wanaopenda kujifunza kila siku. Ukimwambia una idea hakatai kukusikiliza. Coz anaamini kuwa hata mafanikio yake yalitokana na kujifunza vitu vipya.Na watu wengi wanatamani kufika kundi hili. Lakini HAWANA discipline ya kujifunza tabia zinazoweza kukufikisha huko.


Swali muhimu tu la kujiuliza tu ni kuwa je, wewe upo kundi lipi.

Una muda mwingi lakini huna hela? = fukara

Una hela nyingi lakini huna muda? = middle class

Huna muda wala huna hela.. Vijisenti unavyopata vinaishia nauli kula kodi ya nyumba nk? = maskini

Au una muda mwingi na hela siyo shida tena? = tajiri.


Jibu unalo mwenyewe. Hakuna mchawi. Shida siyo Magufuli shida ni wewe kuamua kujifunza how utoke hapo ulipo au uendelee kusubiri Tanzania ya Viwanda.
Sisi tupo katika program ya kusaidiana mawazo tu. Nini unaweza kufanya kufika kundi hilo la nne. Kama unataka kujifunza karibu.

WhatsApp #o788366511 au #o752366511. Mafunzo ni bure ila tu uwe *serious.* So kama unaona unahitaji kujifunza au una ndugu yako rafiki yako mdogo wako nk unayetaka aanze kujifunza mapema mambo muhimu badala ya kupoteza muda mtandaoni mpatie namba hizo.


Semper Fi

Andrea G. Muhozya
Darbes Salaam, Tanzania
East Africa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni