Ijumaa, 29 Septemba 2017

MAHALI SAHIHI PA KUANZIA BIASHARA

*MAHALI SAHIHI PA KUANZIA BIASHARA*

Katika maisha mafanikio huwa ni kitu cha watu wachache tu. Iwe kwenye: masomo, michezo, muziki, siasa, biashara, mahusiano nk. Ni wachache tu hufanikiwa. Hii ni kwa sababu mafanikio ni mchakato ambao watu wengi mno hawako tayari kuufata maana inahitaji NIDHAMU ya hali ya juu na BIDII ya kiwango cha juu pia. Na haya si maneno yangu tu bali hata watu waliofika mbali zaidi kama Mohamed Dewji wanasema hivyo.



Kama unasoma makala hii ikiwa tayari nilikutumia audio ya kukukaribisha katika mafunzo haya tulipoanza mazungumzo basi ndani ya ile audio nilieleza kuhusu aina za biashara zinazoweza kukusaidia kufika mbali. Mfano Real Estate, Platform Business, Service Oriented, Minerals Oil and Gas nk. Ya mwisho katika mlolongo wa kuzitaja nikasema ni INTELLECTUAL DISTRIBUTION. Na nikasema ndo biashara ambayo nimewashauri watu wengi sana hasa wanaolalamika kuhusu shida ya mitaji kuwa mikubwa kwamba nawashauri kuanza na hii kabla ya kwenda biashara zingine kama Real Estate na zingine nilizotaja. Tatizo watu wengi hawataki process. Wanataka wafanikiwe kufumba na kufumbua. Lakini naamini wewe unaamini katika process. Lakini hata kama sikukukaribisha kwa audio kilichomo kwenye hiyo audio fupi kilikuwa ndicho hicho yaani aina za biashara na story yangu mimi katika safari ya mafanikio.

Katika dunia ya leo wanaofanikiwa ni watu wanaojifunza njia MPYA za kufanya vitu.



So ngoja nitoe ufafanuzi kidogo wa hii biashara kisha utaamua mwenyewe kama unaona inakufaa pia au la. Mimi kazi yangu ni kukufundisha kwa kina (in details). Lakini maamuzi ya kusema uendelee kujifunza zaidi kwangu ni maamuzi yako. Japo najua ukiamua kuendelea tu kujifunza bila kuchoka utakuja kuelewa vitu vingi sana ambavyo wengi hawaelewi. So sasa ngoja nifafanue zaidi.


I. *INTELLECTUAL DISTRIBUTION NI NINI?*

Hii ni biashara ngeni kwenye masikio ya watu wengi. Hivyo ni biashara ambayo wengi inawapita. Na wengi wakisikia kuhusu hii biashara wanapata "ALLERGY" hasa kwa sababu jina maarufu linalotumika kuitambulisha hii biashara ni NETWORK MARKETING. Kutokana na kuwa ngeni hii biashara imeshindwa kueleweka vizuri kwa wengi na wengi kutoichukulia serious na kukosa fursa nzuri kweli kweli. Naamini wewe utapenda kujifunza vizuri.

Lakini niseme tu kuwa kama ilivyo katika biashara nyingine zote hii nayo SIYO RAHISI RAHISI tu. Hakuna jambo lenye faida ambalo huwa rahisi rahisi tu. Ila tu hii biashara haina complications kama biashara zingine.

*Sasa Intellectual Distribution (ama Network Marketing) ni nini?*

Huu ni mfumo au utaratibu wa kufikisha taarifa kuhusu jambo fulani ama huduma ama bidhaa kwa KUAMBIANA AMBIANA. Yani mimi nikwambie wewe kitu kisha nikwambie na wewe kawaambie wawili. Na ukiwaambia  unawapa maelekezo pia hivyo hivyo wao kila mmoja aambie watu wawili. Sasa kwa mtindo huu ujumbe ule utafika kwa watu wengi mno. Kama ambavyo tumeambizana kuhusu wapi wanauza simu nzuri au mabegi mazuri au wapi wanapika chakula kitamu sana.


Changamoto kubwa hapa ni kuwa ujumbe unaweza kufika mbali lakini ukawa umeshaongezwa chumvi au umeongezwa maji.


Lakini kama kutakuwa na utaratibu labda ujumbe uwe unapewa ukiwa umeandikwa na pia uwape wengine ukiwa umeandikwa kama ulivyoupokea basi hilo tatizo la kuongezwa chumvi au maji litakuwa halipo. Right?

Kwa sababu ya NGUVU ya habari kutembea kwa njia ya mdomo zaidi basi kuna makampuni yaliamua kuutumia utaratibu huu kwa MAJARIBIO kama njia ya kutangaza bidhaa zao. Yani mfano kampuni FULANI inakupa maelezo kuhusu bidhaa yao. Labda simu. Halafu wanakwambia ilivyo nzuri. Kisha wanakwambia nenda kawaambie watu wawili tu unaowajua. (Hii ndo inaitwa INTELLECTUAL DISTRIBUTION yaani unadistribute intellect). Na wao uwaambie hivyo hivyo. Kampuni zile zikaja kugundua kuwa zile habari zilifika mbali mno. Ambako hata watu hawana TV au hawasikilizi sana redio au kusoma magazeti.


Kampuni hizo zikaamua kuurasimisha mfumo huo. Ila sasa zikasema ukipeleka habari UNALIPWA kama uliyempa habari atakuja kwenye kampuni kununua ile bidhaa uliyomwambia. Kwa hiyo unachosambaza siyo kitu bali TAARIFA. Information. Sasa jiulize hivi huwezi kusambaza taarifa? Hujawahi kumwambia mtu kuhusu jambo fulani linapatikana wapi? I bet ulishawahi. So hapo hukuwa unauza hicho kitu bali ulikuwa unasambaza tu taarifa. Kama ulimwambia mtu kuwa simu nzuri zinapatikawa wapi hukuwa unasambaza simu ya mtu au hakuna aliyekuuliza kama siku hizi unauza simu. Wewe ulikuwa unasambaza tu TAARIFA.

Sasa unayemwambia pia anaweza naye kuwaambia wengine ambao wewe hata hawajui.  Ina maana anatumia muda WAKE kusambaza taarifa. Kwa hiyo sasa mmeanza kuwa wengi mnaosambaza hiyo taarifa. Hicho kitu ndo kinaitwa Intellectual Distribution. Au Network Marketing. Yaani MMEFANYA MARKETING ya kitu kwa network ya watu mnaowafahamu au kukutana nao. Ndipo neno NETWORK MARKETING lilipotokea. Naamini tupo pamoja. 

Dunia ya leo haipo tena kwenye MAPINDUZI YA VIWANDA (Industrial Revolution) yaani namna bidhaa zinavyozalishwa kwa wingi (in bulk) na haraka kwa sababu ya uwepo wa mashine na mitambo ya kisasa. Hapana. Huko dunia imeshatoka. Yaani kuzalisha vitu haraka na kwa wingi hilo siyo tatizo tena. Dunia sasa hivi ipo kwenye MAPINDUZI YA USAMBAZAJI (Distribution Revolution) yaani bidhaa zako zikishazalishwa ZITATUMIA njia gani KUSAMBAA kufikia watu wengi zaidi. Yaani TAARIFA kuhusu hivyo vitu vyako zitasambaa haraka au polepole. Hilo ndo litasababisha ufanikiwe kibiashara au la. Ukiwa na duka una vitu hapo dukani labda Sinza halafu taarifa za unachouza zinaishia Sinza tena mtaa ambako duka lako lipo ujue kufanikiwa kwako ni ngumu maana taarifa zimewafikia watu wachache. Maana saivi hatupo kwenye era ya kuzalisha vitu na kurundika ghalani au dukani bali KUSAMBAZA TAARIFA kwenda mbali na wewe ulipo ndo kinaleta mafanikio. Hii ndo elimu mpya lakini wengine wameshaitumia tayari.

Kufanya mambo kwa namna tofauti.



So ndo maana unaona Facebook imeanza miaka michache tu iliyopita lakini mmiliki wake leo ni tajiri mkubwa kabisa duniani.

Fikiria huyu ameanzisha Facebook mwaka 2014 tu wakati huo watu tayari wakiwa ni matajiri leo keshawapita. Hapa ndipo ilipo ELIMU. 

Ni kwamba yeye hahangaiki kuzalisha chochote. Hazalishi habari yoyote tunazalisha sisi wenyewe. Tuna edit wenyewe. Tunapost wenyewe bure.  Yeye amekaa katikati kutusaidia KUSAMBAZA taarifa tu. So taarifa zinasambaa kutoka Mbagala au Upanga au Mbezi Beach kwenye simu yako au yangu na kufika SONGEA au KENYA au CHINA au RUSSIA dakika hiyo hiyo. Usambazaji wa taarifa kwa sasa ndiyo kipindi chake. 
Ndo tunaita DISTRIBUTION REVOLUTION.

So kwa sasa si lazima sana wewe kuwaza uzalishe nini. Acha wengine wazalishe. Wewe angalia je walichozalisha ninaweza kusaidia kusambaza taarifa za hicho kitu na nikatengeneza pesa? Hiyo ndo tunaita INTELLECTUAL DISTRIBUTION ama wengine wanaita RECOMMENDATION BUSINESS. Ama NETWORK MARKETING BUSINESS.

Lakini ukilazimisha tu uwe na duka utakuwa hujaelewa vizuri kipindi gani tupo. Angalia kuna maduka yapo mtaani toka mwaka 1998 hadi sasa lipo mtaa huo huo halijapanuka likawa Supermarket. Aliyeliyelianzisha anakufa wanarithi watoto (kuzazi cha pili) lakini bado halijapanuka kuwa na matawi sehemu tofauti. Why? Kwa sababu tu duka hilo taarifa zake hazifiki mbali ambako ndo kuna wateja wengi zaidi kuliko watu wanaoishi mtaa ule. Na bado Tanroads hawajapita kuvunja ili kupanua barabara. 

Lakini Facebook utamvunjia nini na wakati hana duka? Utamkatia umeme upi. Utamlipisha kodi ipi? See?

Tuendelee. Usichoke. Jifunze tu. Mara nyingi elimu kubwa utaipata kwa kujifunza kusoma vitu virefu. 



II. *FAIDA ZA INTELLECTUAL DISTRIBUTION*


Kwa kawaida watu wengi wanatamani kumiliki biashara lakini hawajui basics yani vitu vya muhimu katika biashara ambavyo ni hivi vifuatavyo:


1. UBORA WA BIDHAA. 
Yaani bidhaa yako tukiiweka pamoja na bidhaa ya GSM zinaweza kushindana kwa ubora?

Usitake kuwa kama Dewji au GSM anyhow tu. Lazima ujifunze ukweli wa mambo.


2. MARKETING STRATEGY
Namna gani watu wengi watapata habari kuhusu hizo bidhaa zako. Utatangaza kwenye TV au utatenga bajeti ya kuweka mabango barabarani na mitaani nchi nzima mitaa yote. Au utatumia njia kama waliyotumia Facebook tu hawana Bango wala tangazo na bado Facebook inajulikana zaidi kuliko brand kama VODAFONE.

Tarehe 27 June 2017 Facebook walitangaza kuwa walikuwa na members (users) bilioni 2 wanaopost na kucomment nk kwa mwezi. Imagine. Lakini ulishawahi kuona tangazo la Facebook kwenye TV eti ili ijulikane kwa watu waje kujiunga?  No. Njia gani inatumika ili watu waijue Facebook?

Simple: *WATU NDO WANAANBIANA*. Hata wewe uliambiwa na mtu. Instagram vile vile. Na sasa THREADS. Hiyo ndo inaitwa *RECOMMENDATION BUSINESS* na hii ni rahisi hata wewe unaweza.

Unaweza kufanya ana kwa ana



Ama unaweza kufikisha hizo recommendations zako kupitia njia ya kisasa zaidi ambayo wengi wanaita SOCIAL MEDIA kama mimi nilivyofanya kukupa taarifa kupitia Social Media. Unaweza kuzitumia kufanya hii recommendation business au Intellectual Distribution.


3. DISTRIBUTION MODEL
Mfumo gani mwepesi wa kuutumia kuwafikishia bidhaa mahali walipo siyo mpaka waje ulipo. Yaani wanunuzi wako watatoka mahali unapoishi wewe au waweza hata kutoka mabara mengine? Unafanyaje ili kitu chako wateja wengi wawe si majirani zako. Hili watu wengi hawajui wafanyeje. Ulishawahi kujiuliza kwa nini hakuna tajiri mwenye kutumia duka mtaani kwake kuuza vitu vyake. Maana duka mtaani ni biashara inayohudumia watu wachache tu wanaoweza kufika duka lilipo. Hakuna tajiri mwenye duka eti anauza unga na sukari vya kupima na viberiti na dawa ya mbu na OMO na wembe. Ingawa akiamua kufungua hayo maduja anaweza kuyaweka kila mtaa. Swali ni kwa nini hawafanyi hivyo eti? Kuna sababu. Na sababu ni kuwa ni watu wachache wataweza kufika duka lilipo hivyo huyo tajiri atalazimika labda afungue duka kila mtaa. Kibiashara inakuwa kipoteza pesa kwani kuset up biashara ya duka inahitaji mtaji mkubwa.

Watu wengi wameanza biashara huko mtaani bila kuangalia hayo mambo matatu na wameishia njiani. Nadhani unaelewa ilivyo muhimu kuyachukulia serious hayo mambo matatu. Hii ni elimu ya biashara ambayo huwezi kuipata kwenye Degree au Masters ya Biashara. Inatokana na practical experience yangu.


Sasa sisi tunafundisha biashara siyo kwa nadharia. Bali practical. Maana hizo za maduka tumefanya pia tena kwa mitaji mikubwa. Tukajifunza na kujua kumbe kuna njia nyingine. Na tunakuonyesha biashara ambayo inatumia system inayoweza kumfanya mtu wa kawaida kabisa akaweza kuwa mfanyabiashara mkubwa mno au hata kuwa mwekezaji na hayo mambo matatu yote akawa ameya-cover bila shida. Yaani akawa anajihusisha na biashara ambayo:


1. Ina bidhaa bora sana tayari. Kwa hiyo anaposambaza taarifa hana wasiwasi na ubora wa kitu anachosema. Kumbuka nimesema dunia ya leo siyo lazima wewe uzalishe kitu. Acha wazalishe wengine wewe angalia ufanyeje ufaidike na uzalishaji wa wengine. Mpaka hapo unakuwa umepunguza ukubwa wa mtaji wa kuanzia.


2. Mfumo mwepesi wa kufikisha taarifa  (njia ya watu kuambiana tu.)


3. Njia nyepesi ya watu kupata hizo bidhaa endapo wako mbali na wewe ulipo. Yani kama ambavyo Azam Cola inauzwa mbali kabisa na hapa Dar es Salaam ambapo ndo Bakhresa anaishi.


Na uzuri ni kuwa mtaji wa kuanzia biashara aina hii yaani hii INTELLECTUAL DISTRIBUTION ni mdogo sana sana ukilinganisha na biashara zingine. Pia hapa mtu atapata mafunzo mengi mno. Hebu fikiria tu ni mambo mangapi umejifunza toka umenifahamu kwa muda huu mfupi. Na hii haijalishi kama utaamua kufanya biashara na sisi au la. Hii elimu itabaki kuwa ya kwako vile vile.

But nataka ni mambo mangapi utajifunza kama ukiwa katika mikono ya watu aina yangu kila siku kwa miezi sita tu? 

Sasa naomba utazame video links nilizokuwekea hapo chini zinaelezea biashara hiyo ninayokwambia ambayo binafsi nimewashauri vijana wengi kuifanya na nimeona wakianza kupiga hatua kuelekea katika mafanikio yao. Of course mimi mwenyewe nafanya na imebadilisha maisha yangu sana! 

Kumbuka jambo hili. Kuna makundi manne ya watu duniani:

1. Wenye muda mwingi ila hawana hela.

2. Wenye hela nyingi ila hawana muda kabisa hawana hata muda na familia ni kazi tu hata makochi yake nyumbani yanakaliwa na housegirl tu.

3. Wasio na muda wala pesa (hawa wanaitwa busy for "nothing". Anahangaika kila siku na kazi ambazo haziwezi kumfanikisha kwa kujidanganya kuwa one day yes. Kumbe hajui ili ufanikiwe kuna vitu inabidi uache. Ikiwezekana hata aina ya vitu unavyofanya inabidi uache uwe tayari kufundishika na kuanza moja toka zero. Wengi hawako tayari. Maskini ni mtu ambaye anafanya kitu hata miaka 10 hapigi hatua ya maana analalamika tu ila hayuko tayari kujifunza vitu vipya au kusikiliza mawazo ya waliokuwa kama yeye zamani ila sasa wamepiga hatua.

4. Na kundi la mwisho ni wale wenye muda mwingi na pesa nyingi ambao hawa ndo watu waliofanikiwa wanaweza nunua chochote popote wakati wowote na wanaweza kwenda popote wakati wowote siyo lazima wasubiri likizo.

 SIJUI WEWE UPO KUNDI LIPI KATIKA HAYO MANNE?

Ji challenge ujijibu kwa DHATI wewe upo kundi lipi katika hayo.

And one more important thing ni kuwa *Intellectual Distribution* ni biashara ambayo inakupa kitu kinachoitwa *LEVERAGE* yaani uwezo wa kujigawa wewe ukawa kama vile uko kila mahali. Kwa hiyo unaweza kukuta unapata pesa na muda unao pia. Watu wengi wamekuwa wakii-miss hii concept na hivyo kutoelewa vizuri namna hii biashara ilivyo na manufaa makubwa sana kupitia hiyo LEVERAGE hasa kwa mtu wa kawaida. 

Yaani uwezo wa wewe kunufaika kupitia muda wa uzalishaji wa watu wengine. Na mfumo unakufavour sababu ni *Recommendation Business*. 

Again usichoke kujifunza vitu vipya. Mshauri wa Uchumi wa maraisi wawili wa Marekani Profesa Paul Zane Pilzer anasema mafanikio au utajiri upo mikononi mwa wale wanaojifunza vitu vipya HARAKA.


Lakini pia tunawafundisha vijana kuwa itakusaidia kuongeza mkondo mwingine wa kipato tofauti na kipato ulichonacho kwa sasa kama unacho kipato tayari ila tu hakitoshi.

Hii ni muhimu kwa sababu matajiri wote wana njia nyingi za vipato. Forbes wanasema Average Millionaire ana njia saba tofauti za kuingiza pesa. Maskini wana njia hasa moja tu, utakuta hasa mshahara au ana duka halafu basi.


Angalia mtu kama Bakhressa ana vyanzo vingapi vya mapato. Hayati mzee Mengi, alikuwa na  mahoteli nje ya nchi, mashamba, biashara za madini, media house (TV channels, redio stations na magazeti), na HISA kwenye viwanda vya CocaCola hapa Dar (Coca-Cola Kwanza) na Moshi (Bonite Bottlers), alikuwa na viwanda vya kuzalisha bidhaa kama sabuni nk, na vitu vingine vingi. Huko kote alikuwa anapata mapato. Ndivyo walivyo matajiri wengi.

Mtu kama huyu mwenye vyanzo vingi vya mapato huwezi kumlinganisha na mwajiriwa anayesubiri mshahara eti au mtu aliyejiajiri tu ana duka lake mahali fulani pesa zinatoka hapo tu. Kuna tofauti kubwa sana. Nayasema haya kwa nia njema kabisa. Na si kuwazodoa watu. Ni kukumbushana tu. 

Sasa hiyo video link  ninayokutumia inaelezea biashara ambayo unaweza kuifanya popote na biashara hiyo inaweza kukupa VYANZO VINGI VYA MAPATO PIA kwa kutumia huu mfumo wa intellectual distribution yaani recommendation. Nimesema Facebook inatumia recommendation lakini hakuna anayelipwa kwa kurecommend kwa mwenzake. 

Lakini sisi katika biashara hii utalipwa kwa kurecommend kwa mwingine. Naamini unaweza kufanya hayo yote ukiwa nyumbani kwako. Ndiyo dunia mpya ya leo hii si lazima ukakodi duka mahali ulipe kodi wakati unaweza kufanyia kazi nyumbani kwako.



Naamini mpaka hapo tuko pamoja.


So kama ulinifatilia kwa umakini toka mwanzo mpaka sasa basi utaelewa mara dufu hizi video. Nimeweka link kwa lugha ya KISWAHILI na nyingine kwa LUGHA ya kiingereza. Utachagua. Ukipenda kufanya nasi karibu sana kuwasiliana nami kwa WhatsApp number +255 788 366 511.

Karibu kutazama video. Video hizi ni za zamani kidogo hivyo mafanikio kwa sasa ni makubwa mno. Nilipost hizi video hapa nilipoolipost makala hii kwa mara ya kwanza mwaka 2017. 

Nachokifanya ni kuedit tu kidogo. Mfano wakati napost mzee Mengi alikuwa hai bado. Lakini hapo juu utsona nimemwita "hayati" maana yake nimesha edit. 

Karibu kutazama video hizi..


1. SWAHILI (testimony)...

Play Video




2. ENGLISH (Official Presentation)...

Play Video



Karibu sana ukishaziangalia hizo video niambie kama upo interested kuanza ili nikueleleze unaanzaje.


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
WhatsApp +255 788 366 511

Jumanne, 26 Septemba 2017

UKITAKA KUPIGA HATUA KIBIASHARA BASI ACHANA NA HELA ZA MAJIRANI ZAKO AU RAFIKI ZAKO AU NDUGU ZAKO


Mzee Bakhressa anaishi Masaki lakini maji ya Uhai au lambalamba na chapati zake hauzii majirani zake. Au ulishaona vile vibaiskeli vya lambalamba za Azam vikizunguka Masaki nyumba kwa nyumba? No lakini vibaiskeli viko kila mahali Buguruni mpaka kigamboni.


Mzee Mengi hauzi maji ya Kilimanjaro kwa ndugu zake au wakwe zake au jirani zake.

Shigongo hauzi magazeti kwa majirani zake maana unaweza kukuta majirani zake wanasoma Daily News na *The Citizen* na wasijue hata sura ya gazeti la Shigongo ipoje.

Dewji hauzi vitu vyake kwa classmate wake wa zamani au jirani zake.


Lakini wote hao niliowataja wamepiga hatua bila kujali jirani au ndugu au classmate zao wa zamani wananunua au la.
Hiyo ndo akili ya kibiashara.

Tatizo la watu wengi ni kudhani kuwa ukianza kitu chako mfano biashara au ujasiriamali basi ndugu zako na marafiki na majirani ndo wanapaswa kukusapoti. Wasipokusapoti *unanuna* na kuona hawakutakii mema. Unawasema na kulalamika.
Wewe kuna kitu hujajua bado ukikijua kwanza hutataka kuhangaika na makundi hayo ya watu kibiashara.

Kama upo hapo unawaza kuanza biashara na unafikiria kuwauzia jirani zako au ndugu zako basi kajipange upya kwanza. Utakuwa disappointed  na kuanza kulaumu watu bure. Ndiyo maana Mungu alikuumbia ndugu na marafiki wachache kuliko idadi ya watu usiowajua dunia hii.
Ukitaka kupiga hatua kibiashara achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Diamond hauzi karanga kwa ndugu zake au majirani zake. No wateja wa karanga zake ni watu tofauti kabisa.  Majirani wanunue wasinunue no problem.
Wanaoshindana kuview nyimbo zake You Tube au kuzidownload wala wala siyo eti rafiki zake. Ni watu tofauti.

Vijana wengi wanaojifunza kwangu biashara huwa wananiuliza swali: *"SASA BRO NTAMUUZIA NANI MAANA HUKU NINAKOKAA DUH WATU NI WA HALI YA CHINI KWELI KWELI NA HATA RAFIKI ZANGU YANI BORA MIMI"*
Jibu ni moja tu hapa: Ukitaka kupiga hatua katika biashara *achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako*

Anayezalisha tissue papers au toilet papers anauzia rafiki zake? Wanaoanza kutengeneza furniture huwa wanauza kwa ndugu zao? Sasa why wewe unawaza jirani zako ndo wateja.
Unakuta mtu anataka kuanza kufuga kuku anataka majirani zake na wafanyakazi wenzake ndo wale kuku wake! Kwani wanaoshona nguo kwa *Sheria Ngowi* ni ndugu zake au eti jirani zake? No.
Ni watu wengine tofauti kabisa. Maana kwanza jirani ataanza kuleta ujirani kwenye biashara yako changa halafu mtaishia kugombana bila kutarajia.
Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako.

Kakangu alinunua vitu kwangu miaka mitatu na nusu baada ya mimi kuanza biashara. Tena alinunua vitu vingi hadi nikachekelea kwa kweli. But unaona sasa ningesubiri anunue ndo niendelee ningekuwa wapi? See, ukisubiri sapoti ya ndugu unaweza kuipata mwaka keshokutwa.
Sasa si utakufa masikini?

So we anza tu ndugu waje wasije isikukwaze. Kwani mwenye Facebook wewe umejiunga kwa kuwa mna undugu au eti unamsapoti? Kama vipi we acha kujiunga Facebook uone kama atakufa njaa kwa kuwa hutaki kumsapoti.

Kwani hiyo simu uliyonayo unadhani mwenye hiyo kampuni hana ndugu? Angesubiri ndugu zake au rafiki zake wamuuingishe si angeacha biashara kwa kukosa wateja? Maana wewe unatengeneza Tecno wakati ndugu zako wanachotamani ni iPhone hapo si utalaumu watu bure?

Mi nimeona jirani zangu wakija kuuza unga wa lishe. Lakini taste yetu kwenye hivyo vitu ni nyingine. Anasema "niungishe tu hata huu mfuko mmoja tu jirani" Sasa hapo mtu anauza kwa kuhurumiwa. Sasa utafanikiwa kweli? Nilipoanza biashara nilikuwa na list ya rafiki zangu ndugu zangu na majirani. Tena wenye uwezo mzuri. Kila niliyemshirikisha anakwambia tu *"TUPO PAMOJA"*. Hahaaaaaa.
Hawakununua. Nimekwambia hivi kakangu alinunua kwangu miaka mitatu na nusu toka nianze. Baada ya kuona naambiwa tu TUPO PAMOJA ndipo nilipostudy watu waliofanikiwa waliuzia nani vitu vyao. Nikapata jibu. Hebu jiulize.

Kwani anayejenga hoteli anawajengea rafiki zake au majirani? Nani akalale sehemu ambako anajulikana?  Sasa ukitaka ujenge mgahawa au saluni halafu rafiki zako ndo waje utakuwa hujajua kitu bado. Utaifunga tu hiyo saluni.

Cha msingi wewe tengeneza VALUE. Hilo ndo muhimu. Kisha wateja SAHIHI watakuja tena kutoka mbali kweli kweli. Ukiwaza  kufungua biashara huku unawaza mashosti sijui washkaji utaifunga siku si nyingi afu utasema eti wateja hakuna.
Kweli?
Yani katika nchi yenye watu karibu milioni 50 unaweza kukosa wateja kabisa kweli? Ulichokosa siyo wateja ni maarifa.  Knowledge.

Ukitaka kufanikiwa katika biashara hasa mwanzo fanya kama vile huna ndugu wala majirani. Fanya kwa ajili ya watu wasiokujua. Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako. Wakizileta well and good wasipoleta no problem.

Reginald Mengi wakati anaanza kuuza maji ya chupa hakuwa anatafuta marafiki wa kuyanywa hayo maji. Au unadhani ndicho alichofanya? No. Maana unajua marafiki nao huwa ni rahisi kwao kufikiri unawageuza ngazi ya kupandia. Wengi huanza kuona wivu kwa siri kuwa wewe utawazidi kimafanikio sasa kwa nini wakusapoti huku hawataki uwazidi.

Ndo maana nimesema wewe concentrate na VALUE. Dunia ya leo ni dunia ya VALUE. Value yako ikiwa nzuri wateja wako watatoka sehemu ambazo hukuwahi kufikiri kabisa. Kuna siku nimeitwa Oysterbay nyumba ya mtu mmoja mkubwa akihitaji kununua kutoka kwangu. Value. Lakini majirani zangu wala hawana habari. Wana taste nyingine. Value yangu huenda haijawagusa. So sikasiriki.
Achana na hela za majirani. Usizipigie hesabu kabisa. Ndo maana hakuna tajiri anayehangaika na jirani zake.

Umeelewa?

Au niendelee kidogo?😄 Okay... Jifunze kwa ma-MC hawa washereheshaji. Unakuta MC anaishi Kijitonyama lakini sherehe za Kijitonyama watu wanachukua MC wa Magomeni. Sherehe za Masaki watu wanachukua MC wa Mbezi. Wakati Masaki pia kuna ma MC wanaishi. Sherehe iko Mwanza watu wanaita MC kutoka Dar au Arusha. MC huyo huyo majirani zake wanasema *"aah huyu ana bei sana tuchukue fulani afu huyu siku hizi anajiona kweli wakati ni MC wa kawaida tu"*. Unaona sasa? Huyo MC angesubiri kusherehesha kwa majirani angesubiri mpaka azeeke.

Kitabu kinasema Nabii hupata heshima nje ya nyumbani. Ukisubiri watu wanaokuzunguka ndo wawe wateja hujajua vizuri maana ya neno MTEJA.

Huoni Bar iko Sinza lakini wadau wake ni watu wa *Tabataaaa!*
Majirani wanaokunywa pombe wanaoishi jirani na hiyo Bar wanaenda kunywea Kinondoni. Kwani mwenye Samaki Samaki hana majirani? Lakini hapo Samaki Samaki wanaokula na kunywa ni jirani zake? No!

Sasa kwa nini wewe unatengeneza sabuni ya maji unafikiri jirani zako ndo wateja? Wasiponunua unaona eti hawataki kukupa sapoti. Nimesema achana na hela za rafiki zako na jirani zako na ndugu zako. Utafika mbali sana. Yani ndugu watakuja huko mbele ya safari. Au utashangaa hawatakuja tu milele.


Nadhani sasa umeelewa vizuri japo ndo hivyo inauma kusikia lakini ndovile!

Achana na hela za majirani zako au rafiki zako au ndugu zako!

Ukifanya hivyo ndo utakuwa umeanza kuelewa shughuli hii ya biashara na ujasiriamali ilivyo.


Nakubariki. Nakutakia mema!

#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa

Ijumaa, 15 Septemba 2017

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE BUT WHAT YOU DO IS... (WEWE SIYO VITU UNAVYOMILIKI BALI KILE UFANYACHO!)

Niliamka katikati ya usiku mnene... na hasa sikuwa nimeamka ila niliamshwa na baridi kali la jiji la Johannesburg kwenye majira ya baridi, baridi ambalo mpaka leo sijui lilipenyaje-penyaje katika wingu zito la nguo nilizovaa, sweta, shuka, na blanketi ambalo niliamini lilitengenezwa ili tu kuithibitishia dunia kuwa baridi si lolote wala si chochote!

Usingizi ulikata kwa sababu ya hilo baridi lakini pia (na hasa) kwa sababu ya wimbo ambao niliacha ukiplay kwa sauti ya chini chini kwenye simu wakati nalala! Nilipoamka ulikuwa unaishiaishia ile replay sauti ikawa inaishiaishia...

Akili yangu ikaanza kufikiri sana kuhusu siyo hasa kilichokuwa kikiimbwa bali mmoja wapo wa waimbaji wa wimbo huo...

Replay ikawa ishaanza tena.. Sauti yake maridadi yenye kuimba kama inatetemeka kwa mbaali ikajaa sana masikioni mwangu na kiukweli hadi moyoni mwangu...
Nikajikuta naanza kusikiliza tena:


"This life don't last forever (hold my hand)"..., wimbo ulianza.

"So tell me what we're waiting for? (hold my hand)

"We better off being together (hold my hand)

"Being miserable alone....

Yes sauti ya Michael Jackson aliyeshirikishwa na Akon ilitetemesha ngoma za masikio yangu kuliko baridi lilivyotetemesha ngozi yangu mpaka nikasahau hata hiyo baridi yenyewe. Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kuwa sauti hiyo ilikuwa ya mtu ambaye alikuwa hayupo duniani tena. And ndo basi tena. Dunia nzima ilikuwa ikimkumbuka Michael Jackson.

Magazeti yaliandika,  Redio zikatangaza, internet ikaenea kumbukumbu zake. Vitu vingi vilisemwa ambavyo baadhi yetu hatukuwahi kuvisikia. Hakika dunia ilijaa huzuni kwa namna yoyote ile ambayo ungetazama simulizi za maisha yake na kazi zake.

Lakini jambo moja ambalo lilikuwa DHAHIRI katika mijadala yote ya kifo chake ni kuwa watu hawakuwa wakiongelea eti alinunuaga nini au alikuwa anamiliki nini na nini au alikuwa anaendesha gari gani nk. Habari zote ziligusa zaidi ALIFANYA NINI. Aliwagusa watu wengi siyo kwa majumba yake au hela zake bali namna alivyowafanya watu wajisikie.

Wimbo uliendelea kuplay nikiwa hata siusikii tena kiukweli nikiwa nawaza tu IMPACT ambayo Michael Jackson aliacha ulimwenguni kiasi kwamba kijana wa kitanzania kama mimi kutoka huko Ukerewe nilikuwa namjua na kuguswa na jinsi alivyofanya kazi yake angali duniani na mpaka kusikitika kuwa hatunaye mtu kama huyo dunia hii tena.

NINI NATAKA KUSEMA:

Mara nyingi sana tumekuwa tukiwaza vitu vya kuwa navyo. Vitu vya kumiliki ili na sisi tuwe WATU KATIKA WATU. Mashindano mengi duniani siyo ya kazi bali ni ya VITU. Siyo kwenye michezo au siasa au kanisani mwenye gari la kawaida anawaza lini naye atapata gari kama la DEWJI. Anasahau kuwa anapaswa kuwaza KAZI GANI afanye itakayowagusa watu wengi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote aliyewahi kutokea duniani. Wengi wetu tunajisahau sana na kuingia katika mtego wa kushindana na watu bila hata kujua kuwa tumeshakuwa OBSESSED na kuwazidi wengine kiasi kwamba tumesahau hatukuumbwa kuja kumzidi mtu. Mashindano yasiyotarajiwa yametupelekea kujikuta tukitengeneza maadui badala ya marafiki. Kwa kutaka sana kuwa AHEAD katika vitu tumejikuta tunacompromise standards zetu za behaviour ama tumejikuta tunakuwa so impatient na process na kutaka tu kutangulia.

Tunasahau kuwa cha muhimu kiukweli siyo nyumba ngapi tutawaachia watoto. Mfalme Suleiman kitu kikubwa zaidi anachokumbukwa nacho ni HEKIMA siyo dhahabu ya OFIRI.  Maana dhahabu zake zote saivi hata sijui ziko wapi. Lakini HEKIMA yake ipo hadi leo!

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE...BUT WHAT YOU DO IS..

Haimaanishi usimiliki. No. Miliki mpaka shetani ajue kuna mtoto wa Mungu hapana chezea! Lakini usisahau kuwa vitu unavyomiliki havitakudefine wewe ni nani hapa duniani. Bill Gates hatambuliwi kwa wingi wa hela zake au majumba anayomiliki ila kwa CONTRIBUTION yake kwa wanadamu wenzake hasa MASIKINI. Ndo maana akala wali maharage Tanga wakati angeweza kuagiza chakula kutoka The Ritz au Ceaser's Palace. Jifunze kwake!

Anamiliki lakini akiondoka duniani hakuna mtu atakuwa anakumbuka viatu vyake au saa ya milionI 100. Ndo maana mara nyingi matajiri wengi huvaa "simple" ili kusaidia wanaowaangalia wasiwa-define kwa vitu wanavyovaa.  Steve Jobs alikuwa anavaa jeans na turtlenecks tu basi. Ili usiangalie sana nje kwake.

Warren Buffet yuko hivyo hivyo. Nk. Na hata matajiri wanaopiga pamba kweli kweli wanajitahidi kufanya vitu vingi kuonyesha kuwa wao ni zaidi ya mavazi yao na magari yao.

Alipofikwa na mkasa mbunge Tundu Lissu gari lake lilionyeshwa kutobolewa na risasi, right? Mi binafsi sijasikia mtu akilihurumia gari na kusema "OH MASIKINI GARI LAKE". Kumbe vitu vyetu havina maana kubwa sana linapokuja suala la kupima "value" yetu. Yani ni hivi unaweza kuwa na ardhi au majumba yenye thamani ya mamilioni lakini thamani yako halisi kwa watu halisi ikawa ni sawa na thamani ya noti ya sh elfu 10 tu. I'm serious.

Kijana mwenzetu #McPilipili amepata ajili na pia hakuna mtu anawaza gari lake. Why? Coz ile Prado is not WHO HE IS. Naamini atakuwa analijua hilo. Albeit now.
Watu wamepost kumtakia heri na kupona siyo eti kuliombea gari. Insurance will take care of that. McPilipili ni WHAT HE DOES. Namna ambavyo amekuwa akifanya watu wajisikie. Na si ana nini.
Unajifunza kitu?

Sasa swali.
Mimi na wewe tukianguka leo hii Mungu akatuita (ni mfano tu usiogope) tutaacha mjadala gani nyuma. Acha watu wachache ambao maybe ulipishana nao kiujumla. Angalia wengi. Majority watafeel vipi.

That's why I write bila kuchoka. Nimeandika article hii kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa usiku ndo nikapumzika. Yes mpaka usiku wa manane maana ninajua kipawa cha kuandika nimepewa nikitumie kuelimisha wengi. Tena haraka. Naamini maandishi yangu siku moja yatasomwa na watu wa mataifa mengi mno. Maandishi yatakayoacha ALAMA maishani mwa watakaoyasoma.

Nilichagua ujasiriamali badala ya sheria kwa kuwa niliona kwangu hii ndo njia nitakayoweza kuufikia ulimwengu wote kwa kazi yangu.

Na wewe unapaswa kuona ni namna gani UNACHOKIFANYA kitakudefine. Usipofushwe na hamu ya gari zuri na nyumba nzuri na viwanja. Hivyo vitakuja tena vingi mno kama ukiamua kuwa BORA ZAIDI katika jambo unalilifanya. Jifunze kuwa bora katika IMPACT YAKO kwa jamii. Hilo ndo la msingi.

Sisi hatumkumbuki na kumfuata Yesu Kristo kwa sababu alikuwa na mali. No.. WHAT HE DID IS WHO HE IS!

Mandela ni Mandela Gandhi ni Gandhi kwa sababu ya  vitu walivyofanya. WHAT THEY DID.

Tarehe 14 October haijafanywa sikukuu nchi hii sababu ya kukumbuka mali za Baba wa Taifa. No. But WHAT HE DID. Sababu WHAT HE DID WAS WHO HE BECAME TO US. Inakumbukwa impact sahihi.
Legacy.

Hata viongozi wa nchi zetu hizi wenye kusemekana kuwa na mali mengi kama hawana IMPACT sahihi katika maisha ya watu basi thamani yao halisi inazidiwa na fundi seremala ambaye yuko kijijini huko hata hajulikani lakini ameishi kwa kutengenezea watu vitu vizuri na wanamthamini kweli kweli. Huyo ana thamani kubwa hata mbele za Mungu kuliko Waziri ambaye ukitaja jina lake watu hata hawalikumbuki na bado yuko hai wala hajafa licha ya kuwa ana majumba ya kifahari na yule seremala analala kwenye mkeka. Ndipo utakapoona seremala anakufa kwa amani (kamaliza kazi) na huyu msomi anakufa kwa pressure na simanzi  (akiwa anajua anadaiwa kazi).

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE... BUT WHAT YOU DO IS.

Mohammad Ali alipoondoka watu walikumbuka alichofanya siyo ati alikuwa analalia kitanda cha aina gani au anaishi nyumba ya ukubwa gani.  Issue ni alifanya nini.


Hujawahi kujiuliza mpaka leo watu wanaongelea BISHANGA na hata hayupo active sana kuigiza kama zamani. Hujaona watu wanaongelea Kanumba na hayupo miaka sasa na wengine wapo wanaigiza lakini bado watu wanaongelea Kanumba.
Impact.
Hawamkumbuki kwa sababu alinunua labda HAMMER au aliporomosha majengo huko Mbweni lakini WHAT HE DID.
Not what he had.

Jifunze.
Usishindane na mtu. Shindania UBORA wako katika like alilokuitia Mungu kufanya. Ukichunguza kazi yako utagundua bado UNAPWAYA sana kwa VIWANGO vya Mungu. Fanyia kazi ubora wa kazi yako. Hiyo ndo watu watakukumbuka nayo. Usiandike kitabu tu ili uuze. No kitaacha ALAMA gani. Siyo kitakufanya ununue gari au kiwanja. Kuna vitabu vingi sana kuhusu mafanikio kifedha lakini THE RICHEST MAN IN BABYLON si mchezo. Kuna vitabu vingi vya kukuhamasisha kufuata ndoto zako bila kuchoka lakini THE ALCHEMIST si mchezo.

Waliovisoma wanaelewa nasema nini.

Mwalimu Mwakasege ni maarufu siyo kwa aina ya magari au majumba. Nina uhakika ana miliki pia kama mwana wa ufalme lakini kinachomtambulisha kwa watu siyo VITU bali KAZI YAKE.

Usikubali utambulishwe na watu kama "yule binti anayevaaga high heels" au "yule jamaa anayeendeshaga NOAH ya silver". Mimi nitafurahi nikitambulishwa kama yule jamaa anayeandikaga kuhusu mambo ya kutunza muda na mambo ya ujasiriamali, nk. Yes WHAT I DO ...not what I have.

Kuna mtu anaitwa MWALIMU MAKWAYA mi sijui hata anapoishi wala anamiliki nini kijana yule lakini najua ANAELIMISHA watu hasa vijana.

What about you?
Watu wanaweza kukutambulisha kwa kazi unayofanya au lazima watumie mavazi yako au nywele zako au gari ndo mtu akujue. Hapo utakuwa unaishi maisha yasiyokuwa na IMPACT kwa a greater majority. Sikia ujue mi siongelei familia yako. No. Sijui umejenga kwenu. That's good hongera sana. But nazungumzia mtu asiyekujua wewe in person amenufaika na nini kwa uwepo wako. Huwa nafurahi nikikutana na post zangu kwenye groups za whatsapp hata kama jina langu wametoa. Huwa nafarijika kuona kumbe nina gusa watu wengi tusiofahamiana. It really makes me happy. Contented.

Josiah Otege, Josinah Leonard , Exuper Njau, Haruni Leonard, Binti Luzutta nawapa challenge: WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE but WHAT YOU DO IS.

Na wewe msomaji wangu naomba ufikiri kama nilivyofikiri mimi usiku ule nilipoamshwa na baridi na kukutana na sauti ya Michael Jackson. Nakuacha na maneno matano ya kwanza kwenye huo wimbo wa Akon na Michael Jackson;

"This life don't last forever..."


Kumbuka hilo uzingatie sana kazi ufanyayo na siyo mali utakazo.


#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
+255 788 366 511

Jumatano, 13 Septemba 2017

WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE! KUJUA WEWE NI MTU AINA GANI TAZAMA SEHEMU UNAZOENDA MARA KWA MARA


Siku kadhaa zilizopita nikiwa nyumbani mchana nilijisahau nikaacha mlango wazi wakati wa gari la taka kupita. Unajua kilichotokea? Nilipoenda kurudishia mlango na kurejea kuketi ghafla nikasikia mlio wa nzi. Akawa anaruka huku na kule. Arrrghh. Instinct yangu ya kwanza kikawaida huwa ni kuchukua dawa ya kuulia wadudu na kuspray. Lakini this time sasa  nipo nyumbani na hiyo dawa hupaswi kuvuta hewa yake maana ni toxic.

What to do?

Nikakumbuka kuwa mpaka muda huo nzi wa watu alikuwa bado anazunguka yani hajapata sehemu ya kusettle. Kwanza nikasmile maana nina mke msafi sana and she knows huwa namwambia.  So nikajua nzi hajasettle maana kaingia kwenye mazingira yasiyo yake.

What to do?

Nikafungua mlango tu wide enough. Kisha nikatoka mlangoni nikaona nzi anazunguka sebuleni kama mara tatu ruti ndefu hivi kisha huyooo akatokea mlangoni kwa spidi ya rocket!
Problem solved.

NATAKA KUSEMA NINI?

Katika vitu ambavyo hatutofautiani kabisa na nzi ni kwamba hata sisi huwa tunakuwa "comfortable" katika mazingira tuliyozoea/jizoesha. Ni vigumu sana ukawa comfortable mahali penye uchafu kama wewe ni msafi. Au penye usafi kama wewe ni mchafu kweli. Utajibana weeee lakini mwisho vitakushinda utaanza tu kuleta "fujo". Utatafuta tu sehemu ya kutokea.

Sasa sikia sikumfukuza nzi alitoka mwenyewe.

Lakini vipi kama ukikuta mzoga kando ya njia halafu kuna nzi wengi (comfort zone yao) halafu ujaribu kuwafukuza (kuwaswaga)? Utakuwa unafanya kazi bure. Wataruka kidogo na kusambaa kisha watarudi tena. Hawawezi kuondoka kabisa. Labda uondoe mzoga. Hao ndo nzi. Nzi mahali pao pa kujidai siyo kwenye usafi. Yani ukiona nzi katulia mahali ambapo wewe unapaona ni pasafi basi ujue kuna tatizo na pua zako au macho yako au vyote. Nzi anajua pa kwenda.

Ndivyo na sisi tulivyo. Ukitaka kujijua wewe ni mtu wa aina gani check where you normally go. Wapi huwa unakwenda mara kwa mara. There's no way ukaenda mara kwa mara sehemu usiyoipenda. Huwezi kuperuzi sana mtandao usioupenda. Kuna mtandao tu ndo comfort zone yakof


Miezi kama mitano iliyopita kuna siku niliingia kwenye daladala. Ghafla nikaona mdada kafungua simu yake. (Umbea huu nao Mungu atusaidie). Basi nimeona akafungua INSTAGRAM.

Akaingia search. Akatype Jina la mtu.......
Akaanza ku-scroll post za za huyo .

Nikawaza tu katika "umbea" wangu huo, dah huyu ameona of all places za kusoma ni hapo. Akawa anaenjoy na kucheka kweli.  Mara anazoom. Basi katika "umbea" huo huo nikamsemesha kidogo:

*Mimi:* Naona unachekicheki news kidogo..?

*Yeye:* Dah yani kakangu huyu (naniliu) ataua watu mwaka huu. Mi lazima nipitie kwake kila siku.

*Mimi:* Aisee huwa namsikia hivi yuko vizuri ee?

*Yeye:* Dah aisee yani hatari mbaya nakwambia. Yani mimi nisipopita kwake nahisi kama naumwa (huku akismile)

*Mimi:* Aisee si mchezo

*Yeye:* Ndo hivyo tunaondoa tu stress.

Mazungumzo hayakudumu sana maana nilimshukuru kiaina nikatoa kitabu nikaanza kuperuzi kidogo na mimi kuondoa hizo stress kivyangu pia.

Ni muda umepita sasa ila tu baada ya kale katukio ka nzi nikakumbuka hiyo siku pia.

Mimi nakutana na vijana wengi sana kupitia mitandao ya kijamii. Hasa kwa ajili ya mambo ya ujasiriamali na naweza kukuhakikisha kuwa asilimia kubwa sana ya vijana hawako COMFORTABLE na mambo ya maana. Mada inayohusu maendeleo yao inaweza kupita na kupata comments 10 tu katika ukurasa wenye followers MILIONI MOJA. Sasa ngoja ije mada ya jambo la ajabu ajabu utaona "MAONI" yatakavyojaa. Sasa ukiona hivyo usijiulize sana we elewa tu THAT'S WHO THEY ARE.

Ukiona vitu vya maana unaona vinakuboa ujue wala hujakosea. Ni kweli kabisa "VINABOA" kwa watu wasio sahihi. Ukiona vitu vya kijinga "HAVIKUBOI" ujue ni kweli kabisa haviboi kwa watu sahihi kwa vitu vitu hivyo pia.
Nzi ataborekaje na harufu you mzoga?

Ukitaka kujua WHO YOU ARE wala usihangike kufanya research kubwa. Angalia tu vitu vichache:

1. Gallery yako ya simu
Ingia now uangalie.  Ina picha za aina gani.
That's who you are.
Ina videos za aina gani?
That's who you are.
Kuna nyimbo za aina gani?
That's who you are.

2. Google Search list yako nini kinaongoza kutafutwa?
That's who you are.

3. YouTube Videos na channels ulizosubscribe nyingi ni zipi?
Ni za mambo ya ndoto zako na mafunzo ya kimaisha au ni muziki na umbea mwingine?
That's who you are.

4. Vipindi vipi vya Redio na TV huwezi kukosa kabisa?
That's WHO YOU ARE.

5. Nini unapenda kusoma bila kukosa.
Ubuyu wa leo leo au hadithi za Shigongo, au Tips za Dewji au Mafundisho ya Strive Masiyiwa?
Wapi upo napo COMFORTABLE?
Wapi unaweza kuahirisha kula kwanza mpaka ujue hicho kitu kilichoandikwa kimeishia wapi?
That's WHO you are.

5. Ukipewa External Hard Disk utaweka nini? Movies au vitabu? Je ni movie gani?
Aina ya movie na series zinazokuattract that's WHO you are.

Nk nk.. check hivyo vitu tu haraka haraka kwa uchache utajijua upo wapi.

Huwa unaenda wapi sana in the physical world lakini pia social media?

Ni muhimu sana kujua who you are mapema katika safari ya mafanikio yako ili uanze kucontrol vitu vinavyokuvuta mapema. Usije ukajikuta ghafla vitu vilivyokuwa vya msingi kwako ghafla vinakuwa vinakuboa halafu hujui kwa nini. Zamani ulikuwa unapenda watu wenye lugha ya staha na heshima na kuwasikiliza kweli kweli lakini siku hizi uko comfortable zaidi kusoma na kusikiliza wasio na staha na wanaotukanana matusi ya nguoni mitandaoni and wala huoni kama ni shida tena. Coz umeshakuwa nzi pia. Nzi mdogodogo.

Huoni shida kuwa kwenye mizoga wa maandishi. In fact unaitafuta na ukikuta haitoi harufu sana unasikitika. Ukikuta maua yananukia hutaki hauko comfortable.  Ulishawahi kuona nzi anaruka kutoa ua moja kwenda jingine kwenye bustani na akatulia na kuenjoy? Hawezi.
Huenda na wewe hutaki habari zenye harufu nzuri.

That's WHO you are now.
That's who you've become.

Na uzuri ni kuwa unaweza kujua kabisa hiyo  WHO YOU ARE ya sasa kama inakupeleka mahali sahihi au la.

Ukitaka ubadili mwelekeo wa maisha yako uwe wenye tija basi angalia WHERE YOU GO ON A DAILY BASIS.

Kama ningekuuliza swali sasa hivi kwamba: Hivi jana ulishinda wapi siku nzima?

Unaweza kusema labda

"Nilishinda kazini"

"Nilishinda nyumbani"

Nk.

Lakini huenda ulishinda WhatsApp. Au Facebook.

Sasa hilo siyo shida.  Ishu ulikuwa wapi na wapi kwenye huo mtandao wa kijamii.

Shaolin Monks hupewa training sana kuhusu eneo la fikra. Na wewe unaweza kujifunza. Kutunza fikra zako zisishikwe na mambo yasiyokuwa na tija kwenye kutimiza ndoto zako. Hold your mind together. Badilisha sehemu UNAZOENDA na utabadilika sana. Kuna watu huwezi kuwaona mpaka ubadili sehemu unazoenda. Yes. Unataka kuonana na Reginald Mengi Samaki Samaki?
Utangoja milele coz Samaki Samaki huenda that's WHO YOU ARE but it's not WHO HE IS.
Umeelewa?

Kwenye Biblia Zakayo alikuwa si mtu mwema machoni pa watu. Lakini WHERE HE WENT changed everything. Alipanda tu kwenye mti ili amwone "MTUMISHI".  Where he went was WHO HE WAS. Mungu anaona sirini. Zakayo pamoja na mabaya yote lakini alikuwa anatafuta pa kwenda ili atoke shimoni. Ni kama alijua hili nalosema hapa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.

Ukiendelea kwenda sehemu zile zile na kuonana na watu walewale na kutazama na kusikiliza vitu vile vile utaendelea kuelekea huko huko unakoelekea. Utaingia kwenye mtego wa kusubiri watu wengine watatue matatizo yako. Utaendelea kuona kuwa Dewji ana bahati na kusahau kuwa WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE.

Kama wewe ni kijana na unataka kuyafikia mafanikio lazima kwanza u check na hili la WAPI HUWA UNAPENDA KWENDA SANA.

Nakumbuka kuna siku nilikutana na kaka Samuel Sasali Mlimani City na kibongobongo nikamwambia "Kaka hatuonani?". Akaniambia tu "Huenda NJE ZETU (outings) zinatifautiana tu". And rightly so. Of course Sasali huwa ana majibu at all times and ukimuona unajiandaa tu kucheka. But the point is kama sionani naye kanisani na sifanyi naye kazi na WHERE I GO IS not WHO HE IS tutonanaje sasa?

Ni hivyo hivyo kwenye mitandao. Sehemu unazoenda sana ziangalie vema huenda kuna watu mnapishana. Huenda kuna fursa na ideas unapishana nazo na ndo Mungu anazileta lakini wewe hizo sehemu ambako hizo ideas zinapostiwa is not WHERE YOU GO.

Usitafute mchawi gani kakuroga ukawa nzi. Ni wewe mwenyewe. Anza kwenda kwenye maua huenda ukaweza kutengeneza asali.

Ukiona kwenda Serena kula lunch au hata kunywa juice tu haiikuingii akilini ujue that's who you are.

Mpaka ubadilike itabidi ufanye maamuzi ya Kizakayozakayo.

If you want to change your life start by changing WHERE YOU GO.

COZ WHERE YOU GO IS WHO YOU ARE!


Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa

#ThreeSixteen
#FourteenSix
#TheAloeLawyer