Ijumaa, 15 Septemba 2017

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE BUT WHAT YOU DO IS... (WEWE SIYO VITU UNAVYOMILIKI BALI KILE UFANYACHO!)

Niliamka katikati ya usiku mnene... na hasa sikuwa nimeamka ila niliamshwa na baridi kali la jiji la Johannesburg kwenye majira ya baridi, baridi ambalo mpaka leo sijui lilipenyaje-penyaje katika wingu zito la nguo nilizovaa, sweta, shuka, na blanketi ambalo niliamini lilitengenezwa ili tu kuithibitishia dunia kuwa baridi si lolote wala si chochote!

Usingizi ulikata kwa sababu ya hilo baridi lakini pia (na hasa) kwa sababu ya wimbo ambao niliacha ukiplay kwa sauti ya chini chini kwenye simu wakati nalala! Nilipoamka ulikuwa unaishiaishia ile replay sauti ikawa inaishiaishia...

Akili yangu ikaanza kufikiri sana kuhusu siyo hasa kilichokuwa kikiimbwa bali mmoja wapo wa waimbaji wa wimbo huo...

Replay ikawa ishaanza tena.. Sauti yake maridadi yenye kuimba kama inatetemeka kwa mbaali ikajaa sana masikioni mwangu na kiukweli hadi moyoni mwangu...
Nikajikuta naanza kusikiliza tena:


"This life don't last forever (hold my hand)"..., wimbo ulianza.

"So tell me what we're waiting for? (hold my hand)

"We better off being together (hold my hand)

"Being miserable alone....

Yes sauti ya Michael Jackson aliyeshirikishwa na Akon ilitetemesha ngoma za masikio yangu kuliko baridi lilivyotetemesha ngozi yangu mpaka nikasahau hata hiyo baridi yenyewe. Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kuwa sauti hiyo ilikuwa ya mtu ambaye alikuwa hayupo duniani tena. And ndo basi tena. Dunia nzima ilikuwa ikimkumbuka Michael Jackson.

Magazeti yaliandika,  Redio zikatangaza, internet ikaenea kumbukumbu zake. Vitu vingi vilisemwa ambavyo baadhi yetu hatukuwahi kuvisikia. Hakika dunia ilijaa huzuni kwa namna yoyote ile ambayo ungetazama simulizi za maisha yake na kazi zake.

Lakini jambo moja ambalo lilikuwa DHAHIRI katika mijadala yote ya kifo chake ni kuwa watu hawakuwa wakiongelea eti alinunuaga nini au alikuwa anamiliki nini na nini au alikuwa anaendesha gari gani nk. Habari zote ziligusa zaidi ALIFANYA NINI. Aliwagusa watu wengi siyo kwa majumba yake au hela zake bali namna alivyowafanya watu wajisikie.

Wimbo uliendelea kuplay nikiwa hata siusikii tena kiukweli nikiwa nawaza tu IMPACT ambayo Michael Jackson aliacha ulimwenguni kiasi kwamba kijana wa kitanzania kama mimi kutoka huko Ukerewe nilikuwa namjua na kuguswa na jinsi alivyofanya kazi yake angali duniani na mpaka kusikitika kuwa hatunaye mtu kama huyo dunia hii tena.

NINI NATAKA KUSEMA:

Mara nyingi sana tumekuwa tukiwaza vitu vya kuwa navyo. Vitu vya kumiliki ili na sisi tuwe WATU KATIKA WATU. Mashindano mengi duniani siyo ya kazi bali ni ya VITU. Siyo kwenye michezo au siasa au kanisani mwenye gari la kawaida anawaza lini naye atapata gari kama la DEWJI. Anasahau kuwa anapaswa kuwaza KAZI GANI afanye itakayowagusa watu wengi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote aliyewahi kutokea duniani. Wengi wetu tunajisahau sana na kuingia katika mtego wa kushindana na watu bila hata kujua kuwa tumeshakuwa OBSESSED na kuwazidi wengine kiasi kwamba tumesahau hatukuumbwa kuja kumzidi mtu. Mashindano yasiyotarajiwa yametupelekea kujikuta tukitengeneza maadui badala ya marafiki. Kwa kutaka sana kuwa AHEAD katika vitu tumejikuta tunacompromise standards zetu za behaviour ama tumejikuta tunakuwa so impatient na process na kutaka tu kutangulia.

Tunasahau kuwa cha muhimu kiukweli siyo nyumba ngapi tutawaachia watoto. Mfalme Suleiman kitu kikubwa zaidi anachokumbukwa nacho ni HEKIMA siyo dhahabu ya OFIRI.  Maana dhahabu zake zote saivi hata sijui ziko wapi. Lakini HEKIMA yake ipo hadi leo!

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE...BUT WHAT YOU DO IS..

Haimaanishi usimiliki. No. Miliki mpaka shetani ajue kuna mtoto wa Mungu hapana chezea! Lakini usisahau kuwa vitu unavyomiliki havitakudefine wewe ni nani hapa duniani. Bill Gates hatambuliwi kwa wingi wa hela zake au majumba anayomiliki ila kwa CONTRIBUTION yake kwa wanadamu wenzake hasa MASIKINI. Ndo maana akala wali maharage Tanga wakati angeweza kuagiza chakula kutoka The Ritz au Ceaser's Palace. Jifunze kwake!

Anamiliki lakini akiondoka duniani hakuna mtu atakuwa anakumbuka viatu vyake au saa ya milionI 100. Ndo maana mara nyingi matajiri wengi huvaa "simple" ili kusaidia wanaowaangalia wasiwa-define kwa vitu wanavyovaa.  Steve Jobs alikuwa anavaa jeans na turtlenecks tu basi. Ili usiangalie sana nje kwake.

Warren Buffet yuko hivyo hivyo. Nk. Na hata matajiri wanaopiga pamba kweli kweli wanajitahidi kufanya vitu vingi kuonyesha kuwa wao ni zaidi ya mavazi yao na magari yao.

Alipofikwa na mkasa mbunge Tundu Lissu gari lake lilionyeshwa kutobolewa na risasi, right? Mi binafsi sijasikia mtu akilihurumia gari na kusema "OH MASIKINI GARI LAKE". Kumbe vitu vyetu havina maana kubwa sana linapokuja suala la kupima "value" yetu. Yani ni hivi unaweza kuwa na ardhi au majumba yenye thamani ya mamilioni lakini thamani yako halisi kwa watu halisi ikawa ni sawa na thamani ya noti ya sh elfu 10 tu. I'm serious.

Kijana mwenzetu #McPilipili amepata ajili na pia hakuna mtu anawaza gari lake. Why? Coz ile Prado is not WHO HE IS. Naamini atakuwa analijua hilo. Albeit now.
Watu wamepost kumtakia heri na kupona siyo eti kuliombea gari. Insurance will take care of that. McPilipili ni WHAT HE DOES. Namna ambavyo amekuwa akifanya watu wajisikie. Na si ana nini.
Unajifunza kitu?

Sasa swali.
Mimi na wewe tukianguka leo hii Mungu akatuita (ni mfano tu usiogope) tutaacha mjadala gani nyuma. Acha watu wachache ambao maybe ulipishana nao kiujumla. Angalia wengi. Majority watafeel vipi.

That's why I write bila kuchoka. Nimeandika article hii kuanzia saa sita usiku hadi saa tisa usiku ndo nikapumzika. Yes mpaka usiku wa manane maana ninajua kipawa cha kuandika nimepewa nikitumie kuelimisha wengi. Tena haraka. Naamini maandishi yangu siku moja yatasomwa na watu wa mataifa mengi mno. Maandishi yatakayoacha ALAMA maishani mwa watakaoyasoma.

Nilichagua ujasiriamali badala ya sheria kwa kuwa niliona kwangu hii ndo njia nitakayoweza kuufikia ulimwengu wote kwa kazi yangu.

Na wewe unapaswa kuona ni namna gani UNACHOKIFANYA kitakudefine. Usipofushwe na hamu ya gari zuri na nyumba nzuri na viwanja. Hivyo vitakuja tena vingi mno kama ukiamua kuwa BORA ZAIDI katika jambo unalilifanya. Jifunze kuwa bora katika IMPACT YAKO kwa jamii. Hilo ndo la msingi.

Sisi hatumkumbuki na kumfuata Yesu Kristo kwa sababu alikuwa na mali. No.. WHAT HE DID IS WHO HE IS!

Mandela ni Mandela Gandhi ni Gandhi kwa sababu ya  vitu walivyofanya. WHAT THEY DID.

Tarehe 14 October haijafanywa sikukuu nchi hii sababu ya kukumbuka mali za Baba wa Taifa. No. But WHAT HE DID. Sababu WHAT HE DID WAS WHO HE BECAME TO US. Inakumbukwa impact sahihi.
Legacy.

Hata viongozi wa nchi zetu hizi wenye kusemekana kuwa na mali mengi kama hawana IMPACT sahihi katika maisha ya watu basi thamani yao halisi inazidiwa na fundi seremala ambaye yuko kijijini huko hata hajulikani lakini ameishi kwa kutengenezea watu vitu vizuri na wanamthamini kweli kweli. Huyo ana thamani kubwa hata mbele za Mungu kuliko Waziri ambaye ukitaja jina lake watu hata hawalikumbuki na bado yuko hai wala hajafa licha ya kuwa ana majumba ya kifahari na yule seremala analala kwenye mkeka. Ndipo utakapoona seremala anakufa kwa amani (kamaliza kazi) na huyu msomi anakufa kwa pressure na simanzi  (akiwa anajua anadaiwa kazi).

WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE... BUT WHAT YOU DO IS.

Mohammad Ali alipoondoka watu walikumbuka alichofanya siyo ati alikuwa analalia kitanda cha aina gani au anaishi nyumba ya ukubwa gani.  Issue ni alifanya nini.


Hujawahi kujiuliza mpaka leo watu wanaongelea BISHANGA na hata hayupo active sana kuigiza kama zamani. Hujaona watu wanaongelea Kanumba na hayupo miaka sasa na wengine wapo wanaigiza lakini bado watu wanaongelea Kanumba.
Impact.
Hawamkumbuki kwa sababu alinunua labda HAMMER au aliporomosha majengo huko Mbweni lakini WHAT HE DID.
Not what he had.

Jifunze.
Usishindane na mtu. Shindania UBORA wako katika like alilokuitia Mungu kufanya. Ukichunguza kazi yako utagundua bado UNAPWAYA sana kwa VIWANGO vya Mungu. Fanyia kazi ubora wa kazi yako. Hiyo ndo watu watakukumbuka nayo. Usiandike kitabu tu ili uuze. No kitaacha ALAMA gani. Siyo kitakufanya ununue gari au kiwanja. Kuna vitabu vingi sana kuhusu mafanikio kifedha lakini THE RICHEST MAN IN BABYLON si mchezo. Kuna vitabu vingi vya kukuhamasisha kufuata ndoto zako bila kuchoka lakini THE ALCHEMIST si mchezo.

Waliovisoma wanaelewa nasema nini.

Mwalimu Mwakasege ni maarufu siyo kwa aina ya magari au majumba. Nina uhakika ana miliki pia kama mwana wa ufalme lakini kinachomtambulisha kwa watu siyo VITU bali KAZI YAKE.

Usikubali utambulishwe na watu kama "yule binti anayevaaga high heels" au "yule jamaa anayeendeshaga NOAH ya silver". Mimi nitafurahi nikitambulishwa kama yule jamaa anayeandikaga kuhusu mambo ya kutunza muda na mambo ya ujasiriamali, nk. Yes WHAT I DO ...not what I have.

Kuna mtu anaitwa MWALIMU MAKWAYA mi sijui hata anapoishi wala anamiliki nini kijana yule lakini najua ANAELIMISHA watu hasa vijana.

What about you?
Watu wanaweza kukutambulisha kwa kazi unayofanya au lazima watumie mavazi yako au nywele zako au gari ndo mtu akujue. Hapo utakuwa unaishi maisha yasiyokuwa na IMPACT kwa a greater majority. Sikia ujue mi siongelei familia yako. No. Sijui umejenga kwenu. That's good hongera sana. But nazungumzia mtu asiyekujua wewe in person amenufaika na nini kwa uwepo wako. Huwa nafurahi nikikutana na post zangu kwenye groups za whatsapp hata kama jina langu wametoa. Huwa nafarijika kuona kumbe nina gusa watu wengi tusiofahamiana. It really makes me happy. Contented.

Josiah Otege, Josinah Leonard , Exuper Njau, Haruni Leonard, Binti Luzutta nawapa challenge: WHAT YOU HAVE IS NOT WHO YOU ARE but WHAT YOU DO IS.

Na wewe msomaji wangu naomba ufikiri kama nilivyofikiri mimi usiku ule nilipoamshwa na baridi na kukutana na sauti ya Michael Jackson. Nakuacha na maneno matano ya kwanza kwenye huo wimbo wa Akon na Michael Jackson;

"This life don't last forever..."


Kumbuka hilo uzingatie sana kazi ufanyayo na siyo mali utakazo.


#FourteenSix


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
+255 788 366 511

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni