Jumatatu, 12 Septemba 2016

USHAURI WA BURE KWA WANAOWAZA KUFANYA BIASHARA

MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNATAKA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA BIASHARA

Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujajiingiza kwenye biashara. Nimekuwekea baadhi ya mambo hayo hapa chini. Haya ni yale niliyojifunza on the ground ndani ya miaka yangu michache hii ya ujasiriamali toka mwaka 2011 katika biashara mbali mbali nilizofanya. Ukiyazingatia utaona faida yake.

1. HAKIKISHA UNA ELIMU YA BIASHARA
Simaanishi diploma sijui certificate ya chuo au zile notes za Commerce. No.  Hiyo siyo elimu ninayomaanisha. Namaanisha aina ya elimu kwa vitendo kama vile apprenticeship. Yaani kujifunza kwa mtu taratibu uone jinsi biashara inavyofanyika. Kama hilo ni gumu kulingana na mazingira basi hakikisha biashara unayotaka kuifanya au mradi unaotaka kuanzisha una watu wanaofanya kitu hicho hicho walio tayari kukupa elimu kila siku hasa miaka miwili ya kwanza katika jambo hilo. Watu watakaokuwa tayari kukupa siri za mafanikio bila kukuficha. Watu watakaokuwa tayari kukushika mkono kwa dhati mpaka ufikie malengo yako.. Ukijifanya "gangwe", wewe ndo sijui "godzilla" kwa sababu shuleni ulipataga B+ ya Business Law itakula kwako mpaka upate mvi za kope kabla ya muda. Labda kama shida yako ni kufanya show off.  Lakini kama shida yako ni kufanikiwa katika ulimwengu wa biashara unahitaji mtu anayejua hicho kitu vizuri ambaye yuko tayari kukupa information za wapi pa kukanyaga wapi pa kukwepa. Hii ndo elimu nayoiongelea.2. USIDHARAU MWANZO MDOGO.
Usianze kitu kipya kwa gharama kubwa hususan kwa mara ya kwanza. Ukajikuta unakopa milioni 5, 10, 50, nk ili ukafanye biashara mpya ambayo hata hayupo mtu wa kukuelekeza kwa dhati namna ya kuifanya. Utaishia kupoteza hela za watu na kudaiwa na labda kupata stress au hata heart attack. Na kama utakuwa umeajiriwa bado utaathiri hata ajira yako sababu ya stress. Haya ninayasema kwa experience. Ukipenda chukua huu ushauri kwa umakini sana. Anza kitu chenye mtaji mdogo. Hata Biblia inasema si busara kudharau mwanzo mdogo.  Usitake kuanza alipo Shigongo leo.  Au Dewji. Kubali kuanza kidogo. Halafu ukue taratibu taratibu. Itakupunguzia stress zisizo za lazima. Nilijifunza hilo pia ndani ya miaka hii mitano ya ujasiriamali na biashara.

3. FANYA UTAFITI LAKINI JALI MUDA.
Fanya research kuhusu chochote ambacho unataka kufanya.  Huenda umeshauriwa ufanye biashara fulani. Chochote ambacho mtu atakwambia ukafanye. Google kama ikibidi. Angalia information kuhusu hicho kitu. Tafuta walioifanya WAKAFANIKIWA.  Yaani mfano unataka kuanza ufugaji kwa nini uende kwa walioanza wakashindwa wakati walioifanya wakafanikiwa wapo?  Ukitaka kujiunga na chuo unauliza walio disco au waliofaulu? Fanya utafiti na kusanya zaidi information kutoka kwa waliofanikiwa kuliko waliofeli hiyo biashara. Bottomline is fanya utafiti wa kina.  Ili ujiridhishe. Usisisimke tu.
Na utafiti usifanye miaka nenda rudi. Unataka kufanya biashara au kuumba dunia nyingine? Muda haukungoji. Na kuna vitu ukichelewa kuvifanya katika umri fulani au katika msimu fulani itakugharimu sana. Mfano kama ulikuwa unafanya utafiti wa kufungua Internet Cafe toka mwaka 2002 mpaka leo hivi hata ukiamua kufanya hiyo biashara leo si utakuwa unapoteza muda tu bure? Season yake ilishapita. Maisha hayakusubiri. Fanya utafiti ila jali sana muda.

4. KAMA HUTAKI KUOGA UMEVUA NGUO ZA NINI?
Nimeongelea ufanye utafiki. Sasa kama baada ya utafiti wako utaona moyoni mwako kuwa kuna manufaa ya kuifanya hiyo biashara au kufanya huo mradi basi usijiulize mara mbili. Fanya mara moja. Maana ukianza kujiuliza na wakati umeshafanya research yako vizuri ni dalili tu ya moyo wenye woga woga na wasiwasi ambao kwenye biashara itakuwa kikwazo cha mafanikio. Jifunze kuamini utafiti wako mwenyewe. Watu wengi wamekwama hapa eti. Woga woga tu.  Woga si moja ya kitu cha kuja nacho huku ndugu yangu.  Huku inabidi ujifunze kujiamini. Watu wengi huwa wanakwama hapa. Keshaona kuwa kitu anachotaka kufanya ni sahihi lakini anakuwa bado tu anasitasita. Yupo kama hayupo. Mwisho hela ya mtaji anakula na ule moto aliokuwa nao wa kuanzisha mradi au biashara unazimika anarudi nyuma hatua 50. Mpaka arudishe tena ule moyo wa kuanza tena miaka mingi ijayo na wengine ndo basi tena. Anabaki mtazamaji na mkosoaji wa wengine wakati yeye hata kuanza alishindwa.

5. NANI ANAIFAHAMU VEMA HIYO BIASHARA?
Labda unataka kuanza kilimo tena cha matikiti labda. Je unamfahamu mtu yeyote ambaye anaijua vizuri biashara hiyo nje ndani? Kuanzia mbegu, aina (species) za hayo matikiti, misimu ya mauzo, wadudu shambulizi, nk. Usiombe ushauri kwa mtu asiyejua hiyo biashara kwa namna moja au nyingine. Mfano umeamua kuuza nguo. Unaenda kuomba ushauri kwa muuza magazeti kuhusu biashara. Yeye biashara yake ni leo kwa leo. Yaani leo kama habari UKUTA na kesho habari ikawa kupanda miti basi mambo ya jana  yanakuwa siyo dili tena. Sasa unadhani atakushauri nini? Au unataka kuanza biashara ya kuuza mafuta ya mzeituni (Olive Oil) unaenda kuuliza kwa mama ntilie eti akwambie kama yana soko wakati yeye anapikia mafuta ya kuchakachua. Unadhani atakwambia ukafanye hiyo biashara? So don't ask the wrong people.  Eti unakuta mtu anasema "mimi mama yangu ndo my best friend lazima nikamuulize".  Wakati hana ufahamu nayo. Mbona ulikuwa humuulizi ALGEBRA ulipokuwa shule? Si unaona ee? So..Tafuta mtu anayeijua.

6. UNA NGOZI YA FARU?
Ukitaka ku excel kwenye biashara lazima uwe na ngozi ya faru. Niliwahi kujifunza mahali kuwa Faru ana ngozi ngumu mno. Na kwamba zamani wakati wa zana duni za uwindaji walikuwa wakitumia mishale kwa ngozi ya Faru ilikuwa ikishindwa kupenetrate ile ngozi yake. Na pia kuwa faru anaweza kuwa na ndege mgongoni kwake wanakula wadudu au wanarukaruka pale mgongoni na wala asifeel kama wapo. Inabidi uwe na ngozi ngumu. Kuna watu watakukatisha tamaa, kunachangamoto na mishale mingi itarushwa hakikisha una ngozi ngumu na utashinda hiyo mikikimikiki.

7. NINI TAFSIRI YA MAFANIKIO KWAKO?

Kwa wengi mafanikio ni kupata pesa nyingi. Wengine hata ukimuuliza pesa nyingi kwako ni sh ngapi hana idea. Wengine mafanikio kwao ni magari na majumba wengine mafanikio ni starehe, wengine mafanikio ni kutoa sadaka na kusaidia wengine zaidi wengine mafanikio ni kuajiri watu wengi, wengine mafanikio ni kusomesha watoto international school wengine mafanikio ni kuwa na vitega uchumi wengine mafanikio ni kuwa na akiba kubwa benki nk wengine mafanikio ni kula vizuri na kuwa na afya bora nk. Wewe kwako mafanikio ni nini? Ili ufanikiwe lazima kwanza uwe na definition ya mafanikio yenyewe. La sivyo unaweza kupata kila kitu katika biashara na bado ukawa unahisi hujafanikiwa kabisa. Hii imewasumbua wengi.


Kuomba Mungu ni jambo constant wala sina haja kukwambia. Ni sawa na kuoga. Mpaka uambiwe? Nadhani unanielewa.

So if unapenda kujua zaidi biashara sahihi katika zama hizi karibu kwa WhatsApp #o788366511 au #o752366511 kujifunza.

Semper Fi,

Andrea Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni