Ijumaa, 18 Agosti 2017

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED? NI NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA U UCHI?

Wakati nikiwa mtoto mdogo kuna siku nilikuwa naimba wimbo ule wa "NGAPULILA". Niko zangu naimba kwa hisia kweli kweli. Baadhi ya maneno nakumbuka ni haya......

"Rafiki yangu nakuaga mimi oooh,
Nataka kuzamia meli kwenda ng'ambo
Kutafuta maisha eeh, kwani naona maisha ya hapa nyumbani kaka eeh
Yamenishinda
Nakula kwa tabu,
Navaa kwa tabu eeh
Maisha yangu ghetto...
Kulala kwangu ghetto...
Basi naona shida tupu eeh
Shida tupe eeeh

Sina raha maskini mimi ooh
Sina raha hata kidogo,
Ngapulila..."

Wanaoujua watakumbuka lyrics kwa usahihi zaidi. Nachokumbuka ni mama aliposikia nikiimba ALIHUZUNIKA sana. Akaniambia nisiuimbe tena kwa sababu sisi hatuishi GHETTO (tulikuwa tu naishi kijijini lakini nyumba nzuri kwa kweli) na akasema wala sisi siyo MASIKINI (kwa kweli hatukuwa na tatizo la chakula au mavazi yani zile basic needs). Lakini mimi nilikuwa nikiimba huo wimbo nilikuwa naimba kwa hisia kali sababu nilikuwa najiona kuwa ile nyumba tuliyokuwa tukiishi haikuwa ya kitajiri na huenda ndo ghetto yenyewe ya kwenye redio hiyo. (Na kiukweli nilikuja kuelewa vizuri maana ya neno "ghetto" baadaye sana baada ya kuja jijini Daslam na kuzunguka zunguka)😊

Kumbe sikujua kuwa FIKRA zangu nilikuwa nimesharuhusu watu wengine ikiwemo wanamuziki kuziteka na ku-paint picha fulani ambayo ilikuwa imeshanikaa kichwani na kuanza kuwaza na mimi siku nitoke kijijini nifike huko "NG'AMBO".

Mentor wangu anaita hii kitu "MIND CONTROLLING MIND". Yaani kuruhusu fikra za mtu au kitu kingine kuwa ndo fikra zako na ukaziamini kuliko zile ulizokuwa nazo na ukaanza ku-act accordingly.

Hii ni hatari kuliko HYDROGEN BOMB ambazo North Korea wanatamba kuwa wanazo!

Kupokwa fikra zako ni hatari kwa sababu kiuhalisia na hata kisayansi binadamu ndiye kiumbe pekee chenye uwezo wa KIFIKRA.  Wakakipa hiki kiumbe (binadamu) jina lilalofanania hali hii wakakiita HOMO SAPIENS. Yaani Man (or Animal) Capable of Thought.

Kwa hiyo kuishi kwa FIKRA za wengine ni sawa na kuwa USELESS tu. NA ukishauvaa uhalisia wa kuwa USELESS unaweza kuwa una maisha sahihi kwako lakini ukayaona kana kwamba ni tatizo kubwa kweli kweli kwa sababu si wewe unayewaza bali ni mwingine ndani ya kichwa chako. Na kukubadilisha hadi upate fikra sahihi tena itakuchukua muda mrefu pengine maisha yako yote yaliyobakia.

Nitatumia mfano wa Adamu na Hawa kukuonyesha jinsi gani FIKRA za mtu huvurugwa taratibu taratibu..yani huwa siyo ghafla. Wanaovuruga FIKRA zako huanza taratibu kwa njia na mbinu ambazo si rahisi kuzijua.

Ukipokwa FIKRA itahitaji mtu mwingine akuelekeze na kukuonyesha kuwa tayari FIKRA ulizo nazo ni TATIZO kubwa tayari!

Hii ndiyo maana Mungu alimuuliza Adamu hilo swali maarufu:

"NI NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA U UCHI?"

"WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?"


Swali hilo halikuwa jepesi tu. Wala halikuwa surprise kwa upande wa Mungu? Ila Mungu aliliuliza ili kumsaidia Adam (na mkewe) kujua kuwa FIKRA zao zilikuwa zimeshabadilika na kuwa kitu kingine kabisa.

Why?

Kwa sababu Adam na Eva walikuwa UCHI siku zote toka walipoumbwa lakini hawakuwahi kuona kama ni kitu kibaya. In a way Mungu aliwaumba uchi akijua kuwa endapo wataasi maagizo yake na kuruhusu FIKRA mpya potofu vichwani mwao basi wataanza kuona vitu vya kawaida ambavyo ni vizuri wataanza kuviona ni vibaya including kuwa kwao uchi.

Kumbuka Mungu alipomaliza kuumba aliona kila alichoumba  (ikiwemo kuwaumba wao wakiwa UCHI) ya kwamba NI CHEMA SANA. (Mwanzo 1:31) Fikra sahihi ni kwamba Mungu kuwaumba wakiwa UCHI siyo tu ilikuwa jambo jema bali lililuwa jambo JEMA SANA.

Na kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (likeliness) basi na FIKRA original za mwanadamu ziliona ilikuwa sawa tu kuwa UCHI kama FIKRA za Mungu zilivyoona. Kitabu kinasema walikuwa UCHI lakini HAWAKUONA HAYA (Mwanzo 2:25)
Umenielewa right?
Tuendelee sasa...

ENTER THE DEVIL
Shetani alipoingia alijua ili kubadili maisha ya mwanadamu kama MTAWALA KWA NIABA YA MUNGU ilibidi kuvuruga FIKRA za huyo mwanadamu. Katika kuvizia kwake kwa muda mrefu alipoona fursa ya kutest zali lake alienda STRAIGHT kwenye maneno yatakayovuruga FIKRA.  Na atakuwa alistudy maisha ya hao wapenzi wawili na kugundua nani alikuwa akiongea mwenzake anasikiliza. (Adamu)
Nani alikuwa mgumu kutest zali kwake (Adamu).
Nani alikuwa na sauti inayoweza kufanya mwingine alainike na kusahau kila kitu ndani ya sekunde chache?

Hapa jibu ni HAWA.


Shetani alipoona Hawa akiwa peke yake hakupoteza muda:

"Eti Mungu alisema msile matunda ya miti yote ya bustani?"

First trick hiyo. Kuuliza swali ambalo linaonekana kama la chekechea. Jifunze kuogopa mtu mzima kukuuliza swali la kitoto au la kijinga. Nawaza tu kwamba Hawa wa watu huenda alijicheka kimoyomoyo kwa swali la "kijinga" kama hilo (Matunda yote? Sasa tutaishije na sisi bado "vegans". Si bora tungekuwa walau "vegetarians") Nimewaza tu.

So aliyeuliza na aliyeulizwa wote wanajua hiyo si kweli.

Unaweza kuwaza kwamba lakini Hawa naye si angesema tu "TOKA PEPO".
Wewe mwenyewe mtu akikuleteaga umbea mbona huwa hukemei😕 So siyo rahisi kiasi hicho.

Lakini pia ni kama zinaa. Unaambiwa KIMBIA ukijifanya kuexplain, au kushauri au kukemea utashangaa kitakachotokea.

Tambua pia kuwa HAWA alikuwa tayari VULNERABLE kwa kitendo cha kuwa peke yake bila wasiwasi wa kuwa mbali na mume. Separation.

Kumbuka pia fikra zako zikianza kuvurugwa si rahisi ukajua. So Hawa akajikuta anaendeleza mjadala na shetani... akaanza kuexplain pale akijua anaongea tu na SNAKE.

"Hapana... Ila (Mungu) alisema tusile WALA KUGUSA matunda ya mti ulio katikati ya bustani..." Kama vile haitoshi akavolunteer kuongeza jibu kwamba Mungu alisema wakigusa au kula WATAKUFA.

Shetani akapata dili. Kutoka kwenye swali la kijinga alipata jibu lenye AKILI
Kisha akatumia hilo jibu lenye akili KUVURUGA AKILI za Hawa na hatimaye Adamu.

"HAKYANANI HAMTAKUFA" yani hapo nime-imagine tu huo msisitizo wa shetani.

"HAKIKA HAMTAKUFA"

YOU SHALL NOT SURELY DIE.

Yaani anaongea kama mwenye AUTHORITY.

HAKIKA HAMTAKUFA. Ila ni kwamba..... (akazidi kuvuruga FIKRA za mama yetu zaidi)

"Mungu anajua MKILA:

1. Mtafumbuliwa macho
2. Mtakuwa kama Mungu
3. Mtajua MEMA
4. Na (mtajua) MABAYA pia

Sasa uone jambo moja hapa ambalo shetani hulitumia mpaka leo kuzidi kutumia watu wanaovuruga fikra zetu.

Shetani hakuongelea kabisa suala la KUGUSA matunda. Aliongelea tu KULA.  Lakini maagizo ya Mungu yalikuwa siyo katazo la kula tu bali hata KUGUSA. Mtu anayeBADILI fikra zako hulazimisha fikra zako ziwaze mwisho tu.
Kitendo cha shetani kutoongelea kugusa kilimsahaulisha Hawa hilo kwa muda. Na yumkini alipoamua KUGUSA hakufa. Maana ili ule tunda ulitakiwa kulichuma (kugusa). Kitendo hicho huenda kilimwongezea Hawa nguvu kwenye IMANI MPYA POTOFU ya kuwa kumbe kweli huenda hawatakufa. Baada ya kugusa AKACHUMA.  Kisha AKALA.

Hakufa.

Maagizo ya Mungu yalikuwa in plural. So kama Hawa hajafa logic ya kawaida ni kuwa hata mumewe hatakufa.

So Adamu akapewa.  Akapokea. Yaani naye AKAGUSA. Hakufa.

Then AKALA.

BOOOOM!!!!!!

1. Wakafumbuliwa macho
2. Wakawa kama Mungu (kwa maana tu ya namba 3 na 4 hapa chini)
3. Waliendelea kujua mema
4. Wakajua na MABAYA pia.

Coz Mungu anajua mema na mabaya pia.

TATIZO:
Tatizo ni kwamba kwa kuchagua kumsikiliza shetani FIKRA zao zilibadilika kiasi kwamba yale ambayo mwanzoni waliyaona MEMA sasa yakawa mabaya kweli kweli. Kiasi kwamba kuwa kwao uchi kuliwasumbua kiasi cha kulazimika kuficha uchi wa kila mmoja wao for the first time! Na Mungu alipokuja wakaona AIBU kuonana naye wakiwa vile. Utukufu wa Mungu uliozoeleka ukawa hofu kwao. Zamani waliona mema tu now hata kuonana na Mungu kwa njia na hali ile ile kukawa kubaya.



"Nimeogopa kwa kuwa nilikuwa UCHI"

Like seriously?  You've been naked all life! So WHO TOLD YOU NOW KWAMBA UKO UCHI?

Kwa maneno mengine NANI AMEKWAMBIA KUWA KUWA KWAKO UCHI NI ISSUE?

Kwa maneno mengine Adamu NANI AMECHAKACHUA FIKRA ZAKO?

NANI AMEKUFANYA UJIDHARAU HADI UJIFICHE?



So, my dear reader.....

NANI AMEKUJENGEA INFERIORITY COMPLEX YA KUJIONA HUFAI?

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

NANI ALIYEKUAMBIA YA KUWA WEWE NI MASKINI?

Na ni nani aliyekwambia kuwa NG'OMBE WA MASKINI HAZAI?

Unajua madhara ya kuamini hivyo?

Nani alitwambia SISI ni nchi maskini?

Na ni nani alisema sisi tupo DUNIA YA TATU? Nani alipima DUNIA na alikubaliana na nani kuwa hii sehemu tuliyopo sisi ni ya TATU?
Unajua ndo maana Bill Gates kaja ikawa story kubwa
wakati mimi au Reginald Mengi tukienda Marekani wenyeji wetu tu ndo watajua siyo taifa zima.
Hayo ndo MADHARA ya kuamini tuko dunia ya ngapi sijui.

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

Nani alikwambia kuwa kwa kuwa wewe ni ALBINO huwezi kuolewa? Au huwezi kuwa BALOZI.
Je umepima fikra za mwanasheria na  Balozi Possi?


Nani aliyekupandikiza FIKRA kuwa ili uwe tajiri inabidi umchune binadamu mwenzako ngozi?
Unaona madhara ya kupokwa FIKRA?
Huna malengo, huna mipango, huna mentors,  hujifunzi kwa wenye mafanikio sahihi, hushughulikii kukaa vizuri na akiyekuumba utaacha kuamini kuwa ngozi ya binadamu, au ya kakakuona au meno ya tembo au shamba la bangi ndo vitakupa utajiri?

Nani alikwambia kwa kuwa ulipata ujauzito kwa mazingira mabaya kabisa kwamba unapaswa KUJIUA KULIKO KUENDELEA KUMWONA AU KUMKUMBUKA HUYO MWANAUME?

Nani alikwambia kuwa unapaswa uondoke dunia hii kwa kuwa ulitendewa mabaya? Uliwahi kusikiliza story ya Oprah au Lissa Nichols?


Nani alikwambia kuwa wewe hufai kwa sababu ex boyfriend wako alikuacha?

Nani aliyekuambia ya kuwa wewe ni KILAZA?
Anajua THAMANI ya investment ambayo Mungu aliwekeza ndani yako? Kwa nini unakubali definitions za watu kuhusu wewe ndo ziwe uhalisia wa FIKRA zako?

Nani alikwambia huwezi kufanikiwa bila kusoma ELIMU YA JUU?

Unarisiti ili kuongeza ufahamu au ili kuprove kwa watu kuwa na wewe unaweza kufika Chuo Kikuu? Una prove ili iweje kama siyo INFERIORITY COMPLEX in you imekutafuna for years.

Who told you kuwa usipofika Chuo Kikuu huwezi kutoa mchango muhimu kwa jamii?

Nani aliyekwambia kuwa wewe ni mtupu kichwani, huna future, huna lolote, huna BAHATI. Ilikuwaje kwanza mpaka ukamsikiliza akiongea hadi amalize. Nani alikwambia kuwa huwezi kuanza biashara chini kabisa na ukaja kuwa zaidi ya wote uwaonao juu leo hii?

Nani alikufanya ushindwe kujiamini.
Ngoja nikupe siri. Angalia watu wa ACACIA. Walikula "tunda" kweli kinyume na maagizo. Lakini WALIKUJA. Hawakukimbia.  Mtu mmoja akawaita "WANAUME". And rightly so. They didn't run away. Binafsi nimejifunza kweli kwao. When you've messed up clean your mess!

Ukitaka angalia siku walivyokuja.


In a pack. Like lions.
Confident.
Yaani mtu unamdai afu yuko very confident.
Well suited.
Nigel Chanakira hutumia pia neno "WELL-HEELED" yaani kiatu ambacho soli ni mpya haiko upande.
Kisafiii. Kipyaaaa!

Huyo ni mtu unayemdai anakuja hivyo. Si unaweza kumuogopa bure. No wonder kuna watu fulani walianza kusema "UNAONA WENZETU?". Wakaanza kuaminisha kundi kubwa kuwa "SISI HATUWEZI KUWASHINDA WENZETU SI UNAONA WALIVYOKUJA"

Hayo ndo madhara ya kuamini kuwa tuko inferior kwa "WENZETU". Fikra za kishetani kabisa. Fikra hizi ziliwahi kutetemesha taifa la Israeli wakati wa Musa. Taifa likaambiwa professionals walijiona panzi mbele ya MAJITU.  Hivi professional anayeaminika akijiona panzi mbele ya adui mtu wa kawaida atawaza nini?
 
Hapo ndipo Mungu alipowaza kuwafutilia mbali taifa zima na kuanza na Musa upya (Hesabu 14:11,12). Acha kabisa kupandikiza hofu ndani ya watu. Wanaweza kujawa hofu wakamkosea hadi Mungu kisha akawaadhibu kwa jinsi ambayo hawakuwahi kuona. Kwani Mungu anashindwa nini kuwazungusha jangwani miaka mingi zaidi.  Anashindwa nini kuruhusu lifisadi moja lije kuwa raisi na liirudishe nchi nyuma mpaka kizazi chote hiki kiishe kije kipya.

Umeelewa?

Fikra POTOFU ikipandikizwa ndani ya watu unaweza kuleta madhara ambayo hakuna aliyetarajia.
Na wewe usiruhusu mtu akupandikize fikra eti hutafanikiwa kwa sababu ya SERIKALI au kwa sababu ya Richmond.  Mafanikio YAKO ni WAJIBU WAKO.

Jenga fikra sahihi tu.

Usipoangalia FIKRA zako na kuzichunga utashangaa kumbe siku nyingi mno ushapokwa fikra.  Ndo maana mtu akisema HAKUNA AJIRA unaamini.  Kakwambia nani?
Sikia nikwambie mimi nilipata AJIRA yangu ya kwanza bila experience yoyote na kampuni ilibuni AJIRA hiyo baada ya mimi kwenda interview na kukosa nafasi sababu kuna vigezo sikuwa navyo LAKINI kwa jinsi nilivyojiamini na kujieleza jopo la wa wasaili lilishawishi uongozi utengeneze NAFASI ambayo HAIKUWAHI kuwepo kwenye hiyo kampuni ili tu nisikosekane pale. Sijisifii. Nakupa uhalisia.

AJIRA ZIPO.
Tafuta kama ndicho unachotaka ukikosa ujue siyo kwa kuwa hazipo. Nakupa siri ukienda interview nenda kama ACACIA WALIVYOKUJA!

Nani alikuambia huwezi kuanza biashara yako kwa kuwa huna MTAJI. Unakaa tu kisa "huna mtaji". Nani alikwambia mtaji ni pesa?
Fikra hizo umezitoa wapi. Zimekufanya uwe mpole na mnyonge bure tu.

Nani alikuambia kuwa UKISOMA LAW au ENGINEERING ndo DILI.

Nani amekuambia kuwa HAKUNA HELA MTAANI?
Are you sure hizo fikra hazileti uhalisia huo maishani mwako?
Are you sure fikra hizo haziui creativity yako yako na moyo wa kujituma zaidi?
Niliwahi kusema ukiona wewe huoni hela ila wengine wanaziona ujue tatizo siyo pesa ila ni macho yako.

Nani alikwambia MAISHA NI MAGUMU?
Alikwambia ili iweje?
Unaamini hivyo pia?
Una HAKIKA maisha ya kila mtu ni magumu nchi nzima?

Nani alikwambia Hutakuja kufanikiwa? Why uruhusu fikra zake ziwe ndo fikra zako mpya na unaziamini na kujiona USELESS mpaka fursa za mafanikio unajificha. Ukiitwa kuambiwa kitu cha kukusaidia huendi kwa kuwa umeshajiona HUWEZI.

Nani ALIYEKUAMBIA kuwa huwezi?

Nani aliyekuambia kwa kuwa biashara yako imeyumba basi haitasimama tena kwa hiyo bora ukaajiriwe tu yaishe?
Nani ALIYEKUAMBIA kuwa hutoweza kusimama tena?
Tenda zikitoka unaogopa kujaribu.
Unajificha kwa kuwa "U UCHI"

WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

Kubadilisha fikra za Adamu ililazimu sasa ahamishwe mazingira kabisa aende nje ya bustani akajitafutie... ili fikra sahihi zirudi ilibidi asile vilivyopandwa na mwingine bali apande vya kwake upya.
Ili fikra sahihi ziwarejee waIsraeli ilibidi wazunguke jangwani miaka 40.

Nilisema madhara ya kuruhusu FIKRA ZAKO zishikiliwe na wengine ni makubwa kuliko mlipuko wa HYDROGEN BOMB.

Jifunze kujenga FIKRA SAHIHI na utayafikia yale muumba wako aliyokusudia uyafikie kwa WAKATI.

USISEME KAMWE KUWA MIMI SINA HIKI, SINA ELIMU, SINA MTAJI, SINA CONNECTION, SINA MARAFIKI, SINA KIPAJI KAMA CHA FULANI, SINA KWANGU, yote hayo na mengine kama hayo ndo fikra potofu ya "NIKO UCHI".

NANI ALIKWAMBIA KUWA U UCHI?


WHO TOLD YOU THAT YOU WERE NAKED?

Barikiwa sana!

#ThreeSixteen

Semper Fi,

Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
#WhatsApp +255 788 366 511
www.andreamuhozya.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni