Ijumaa, 28 Julai 2017

UNATAKA KUFANIKIWA? JIFUNZE KUWAAMBIA WATU NENO HILI: "USINITINGISHE TAFADHALI"


"USINITINGISHE TAFADHALI"


Hakika Mungu ni mwema na nina kila sababu ya kumshukuru sana. Wewe pia mshukuru the Mungu.

Leo ninataka kukukumbusha mojawapo ya maneno mengi mno ambayo yatakusaidia kufikia malengo yako. Nalo ni kujifunza kuwaambia watu "WASIKUTINGISHE".

Wakati naanza biashara ninayofanya sasa hivi sikutegemea kupata upinzani mkubwa kiasi hicho kutoka kwa watu wangu wa karibu. Nilidhani kuwa kila mtu ataelewa tu kuwa ni maamuzi sahihi kama nilivyokuwa nikiona mimi. Lakini haikuwa hivyo.

Nilipata upinzani kutoka kila kona.  Kuanzia kwa my love wangu my ubavu wangu. Ndugu zangu. Marafiki.  Nk. Kuchekwa, kukejeliwa, nk. Lakini kanuni moja ambayo imenifanya nisimame na hii biashara mpaka leo ni kwamba nilijifunza jambo fulani utotoni ambalo limekuwa msaada kwangu mpaka sasa.

Wakati tuko shule ya msingi nilipenda sana kuchora na pia kwa sisi wa zamani zamani (eti mmeanza kutuita wahenga) tulikuwa tunafundishwa somo la MWANDIKO!

Bahati mbaya sana kwa sababu ya uhaba wa madawati dawati moja dogo tulikuwa tunakaa wanafunzi watatu hadi wanne.
Kwa hiyo ufanisi wa somo hilo la mwandiko na lile la kuchora (sanaa) ulitegemea sana mtu asikutingishe wala asikuguseguse wala asitingishe dawati!

Kwa sababu nilipenda sana kupata MWANDIKO au mchoro ambao ni PERFECT nilikuwa na-mind sana sana mtu akinitingisha hata kidogo tu.  Kwa hiyo nikikaa tu kidogo nasema "USINITINGISHE". Mbaya zaidi kuna "mamtu" class yalikuwa yamebarikiwa yana mwandiko mzuri hadi raha. Afu na mimi nataka nipate mwandiko wa ukweli afu mtu mara anabadili mkao wake keshakutingisha.  Dah! Ilikuwa inaniumiza kweli. Halafu unakuta mtu haoni kwa nini unahangaikia mwandiko tu ndo unakasirika hivyo!

Mwandiko tu? Kumbe wewe huoni ni mwandiko tu. Unaona SUCCESS, PRESTIGE, REPUTATION, etc.

Leo naona mwandiko wangu si mbaya sana (licha ya kutingishwatingishwa)

Yes.

Kwa hiyo wakati naanza biashara hali ya watu wengi kutokubali ninachofanya niliiona kama "KUNITINGISHA". Na kiukweli sikuwa tayari kuona ninatingishwa wakati nahitaji CONCENTRATION.

Sikumwambia mtu yeyote neno hilo lakini moyoni mwangu na mawazoni mwangu lilijaa. USINITINGISHE TAFADHALI! MSINITINGISHE TAFADHALI!

Nimekuja kuona kuwa watu wote waliofanikiwa katika kitu fulani waliamua kukataa KUTINGISHWA.

Ukiweka huo msimamo hutaeleweka vizuri. Maana wengine hukupinga kwa nia njema. Lakini kama Donald Trump angesikiliza ripoti za CNN na BBC asingefika hapo alipofika. Nakumbuka sana alivyochekwa na anavyochekwa hadi leo. Na kuitwa majina mengi. Kichwani mwake kulijaa na kumeendelea kujaa hilo neno: MSINITINGISHE TAFADHALI

Siyo kwamba hakwami au hakosei. Anakwama mara nyingi kuliko kawaida. Anakosea kweli mambo mengi lakini point ni kwamba hataki KUTINGISHWA wakati anafanya alichokwishaamua kufanya.

Kuna mmoja tunaye nchi hii yeye alisema HAJARIBIWI. Maana yake  USINITINGISHE TAFADHALI.  Na ukimtingisha mtu ALIYEDHAMIRIA kukataa kutingishwa basi utaelewa muda si mrefu.

Watu wote waliofanya kitu na kikawezekana waliweka hiyo attitude: USINITINGISHE TAFADHALI.

Kuna kitabu nilisoma cha kuhusu maisha ya Thomas Edison aliyegundua bulb hii tunayowasha leo.
Aliishi maisha yenye changamoto nyingi na vikwazo vingi. Lakini kichwani mwake ni kama aliiambia tu kila changamoto neno moja: USINITINGISHE TAFADHALI
Maisha ya Bill Gates na Paul Allen ni hivyo hivyo. Jeff Bezos. Jack Ma. Nk.

Yesu aliwahi KUTINGISHWA na mama mzazi kwenye harusi ya Kana huko Galilaya.  Mama anasema: "HAWANA DIVAI". Jibu la Yesu kwa mama mzazi ni kama kumwambia tu "MAMA, USINITINGISHE TAFADHALI ".
Tunasoma pia Yesu akiambiwa na shetani "badilisha mawe yawe bread kama kweli wewe ni mwana wa Mungu" nk. Majibu ya Yesu yote kwa shetani yalikuwa kama kumwambia tu shetani: USINITINGISHE TAFADHALI!

Sijui unaelewa?

Ukitaka kufanikiwa na wewe ni mtu wa kuruhusu kila mtu tu akutingishe hutafanikiwa. You must STAY FOCUSED!

Mafanikio ya aina yoyote yale iwe ni unataka MWANDIKO mzuri au KUFAULU MITIHANI au unataka NDOA IMARA au unataka MAFANIKIO KIBIASHARA au unataka kutimiza ndoto na MAONO yako yanahitaji usiwe mtu wa KUTINGISHWATINGISHWA tu na kila mtu.

Kuna kijana mmoja amemaliza kidato cha sita nimekutana naye hivi juzi tu kupitia hii mitandao. Katika mazungumzo ananiambia anaomba ushauri. Anasema amefaulu mtihani wa Form VI ila kozi aliyotaka kusoma chuo ni PROCUREMENT... lakini watu "wamemtingisha" hadi wakamwambia akasomee mambo ya PLANNING eti ndo DILI. (Sijui wamejuaje) Lakini dogo akakubali lakini kwenda kumwambia "MZEE WAKE" akapinga sana anataka kijana wake akasomee PHARMACY kwamba ndo hatakosa AJIRA mbeleni.
Wamemtingisha dogo mpaka haelewi afanyeje sasa.

Hali hii huwakuta wengi. Unataka kuoa/kuolewa unaambiwa MBONA MAPEMA? Unataka kuanza biashara unaambiwa HEE, HIYO HUTATOKA BORA UFANYE HII. Hahaaaaa! Watingishaji ukiwapa nafasi utatingishika mpaka hutoamini kama ni wewe. Unataka kununua gari unaambiwa SI UJENGE KWANZA? Ukianza kujenga ukakwama wanasema si ungejenga chumba kimoja uhamie hivyo hivyo ndo watu wanaanzaga hivyo. See? Sasa utakuwa REMOTE CONTROLLED na watu hadi lini?

Sikia usichanganye kati ya USHAURI SAHIHI na KUTINGISHWA. Yesu alijua kuwa maneno ya mama yake kwa mama ilikuwa kama USHAURI lakini kwa yeye Yesu ilikuwa kama kuambiwa cha kufanya hasa ukiwa tayari unajua na unasubiri tu wakati muafaka. Mind ya Yesu ilikuwa VERY FOCUSED kwenye huo wakati muafaka aliokuwa akisubiri kiasi kwamba hakutaka KUTINGISHWA kabisaa! "MAMA... SAA YANGU BADO!"

Yaani: USINITINGISHE TAFADHALI

What about you my friend?

Ukishafanya maamuzi fulani kuhusu maisha YAKO unataka mtu mwingine tena aseme nini.

Ngoja nikupe mfano mdogo:

Ukijipanga mstari na watu 10 wa mtaani kwako au familia yako halafu mkawekewa magari 10 tofauti tofauti mbele yenu kila mmoja wenu achague la kwake:

Range Rover,
Jeep Cherokee,
Toyota VX,
Vitz,
Mercedes Benz,
FUSO,
Canter,
Rav 4
BMW
DCM

Wewe utachagua lipi?
Na je unadhani utakalochagua uchaguzi wako ndo sahihi au mbovu kuliko wa wengine? Yani unadhani ukichagua Range mwenzako akachagua FUSO ndo akuone wewe chizi eti kisa kwa nini hukuchagua gari ya kubebea mizigo?? Kwani kila mtu anataka kubeba mizigo?  Kwani hujui kuna watu wana Range na zinawaingizia pesa kuliko wenye FUSO. Na kuna watu wana FUSO wana hela kuliko mwenye Range. Au kama ulichagua Benz afu mwenzako akachagua VX akucheke kwa nini  umechagua gari la chini badala ya kuchukua la juu. Kwani kila mtu anataka gari kubwa dunia hii? Sasa na wewe unaanza kujilaumu eti  ayaa bora ningechagua VX.

Utakuwa hujielewi bado.
Choices zako na decisions zako kama mtu mzima unapaswa kuzisimamia.  Ukikosea si unajifunza tu. Kwani mbona Rais anateua Waziri halafu anagundua baadaye kumbe alikosea au kumbe. Anabadilisha. And life GOES ON.

Jifunze kukataa KUTINGISHWA. Utafika mbali sana sana.


Mimi nimejifunza hilo. Ndo nikaona nikushirikishe na wewe pia. USITINGISHWETINGISHWE


Na wala USINITINGISHE TAFADHALI.


Barikiwa

#ThreeSixteen


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa
www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp +255 788 366 511


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni