Jumanne, 17 Novemba 2015

MAISHA YAKO NI KITABU

YOUR LIFE IS A BOOK.
MAISHA YAKO NI KITABU..

Kuandika kitabu changu cha kwanza kumenifanya nijifunze mambo mengi sana ya kimaisha ambayo sikuwahi kujifunza au hasa kuyatilia maanani..

Mojawapo ni kwamba maisha yetu ni kitabu.

Yes, maisha yako ni kitabu.
Na ni wewe unayekiandika. Sasa naongea  kwa live experience. Kazi ya kuandika ni kazi kubwa inayohitaji siyo tu uweke akili yako hapo bali na moyo wako wote hapo. Kuna wakati unaweza kusema sijui niishie hapa? Lakini unaamua kusema hapana nitaifanya kazi hii na kulipa gharama ya kutafuta maarifa kwa kusoma vitabu, Ku interview watu, kuangalia videos mbalimbali kuhusu nachoandikia, kuwauliza wazee kuhusu mambo ya zamani, kujifunza kuhusu Ulimwengu unakoenda kupiga magoti kumwomba Mungu na kukaa mezani muda wa kutosha kuandika na kupanga na kupangua mambo.. Kifupi mpaka kitabu kikamilike kazi kubwa imefanyika!

Sasa katika maisha yako unaandika kitabu pia. Bahati mbaya sana kila mtu ana size ya kitabu chake. Yaani siku za maisha yake.  Kuna wenye kurasa nyingi Halafu hawajajitambua so kurasa nyingine wanazipita bila kuandika chochote, kuna wenye kurasa chache lakini wamejitambua. Ni kama Ulimwengu wa vitabu. Kuna vitabu kidogo tu kama THE RICHEST MAN IN BABYLON (Mtu Tajiri Zaidi Wa Babeli) lakini vina nondo za kufufuka mtu. Na kuna vitabu vikuubwa namna hii.. (Hahaaa kama unaona mikono yangu) lakini huenda manufaa yake yakawa kiduchu kabisa.

Je, maisha yako umeshajua ni kitabu kikubwa au kidogo? Chembamba au kipana?
Usikute upo kurasa za mwisho mwisho tena za kakitabu kadogo halafu unaishi kama mtu ambaye yuko kurasa za katikati za kitabu kikubwa chenye kurasa nyiingi sana. Ndiyo maana yule nabii wa kale alioongelea kuomba Mungu atufundishe kuhesabu SIKU a.k.a kurasa za maisha yetu. Ni hatari sana kufa bila kumaliza kusudi halafu watu wanadhani kila kifo ni premature kumbe muda wako umeisha na spika wa bunge kakwambia ukae! Whether point zako zimeisha au ulikuwa hujamaliza "muda umeisha muheshimiwa tuwape nafasi wengine pia tafadhali kaa chini au microphone yako itazimwa!" Sasa wewe badala ya kupanga point mapema ungali na muda wa kuandika kitabu chako upo tu unashukuru Mungu kwa kukuumba kila siku ukiamka na kulala asante Mungu kwa Zawadi ya uhai. Sawa basi ongea point basi twende mbele. What are you doing na huo uhai sasa?

Ajabu ukiona wengine wanaandika vitabu vyao unashangaa. Write your book. Na kuna kazi kubwa. Wengine wameishia kwenye introduction tu mwaka wa 10 sasa hivi hawajafanya kitu. Mungu kakupa ndoto kichwani hutaki kuifata. Kwa sababu unaona hauko comfortable. Nani alikwambia uliumbwa uje kuwa comfortable? Write your book.  Usiishi maisha ya mtu mwingine. Ishi maisha YAKO. Hey, unaandika kitabu CHA KWAKO ati.

Je kitabu chako ni kikubwa? Au kidogo? Lazima ujue. Maandalizi ya kuandika kitabu cha kurasa 40 na kitabu cha kurasa labda 200 ni vere vere vere tofauti. Yawezekana maisha yako yanapaswa yawe majibu kwa mtu au watu walioko Lima, Perth, Seoul au Quebec lakini wewe unahangaika ku IMPRESS watu wa Sinza kwa Remmy! Uaikute maisha yako yanapaswa kusaidia hata nchi nzima hii au bara lote au hata dunia. Lakini wewe unahangaika kushindana na watu usiowajua Instagram. Uliza Mungu kama hujajua ukubwa au udogo wa kitabu chako mapema.  Usije ukaja kuuliza ukaambiwa una kurasa chache tu zimebaki sasa sijui utaandika conclusion ya nini .

Write your book. Na usione wivu wowote kitabu cha mwingine kikiwa labda kikubwa. Kazi ya kukiandika pia anayo kubwa zaidi kuliko wewe. Andika cha kwako.
Usiishi bila kuwa na positive impact yoyote. Acha alama nzuri katika uso wa dunia ukijua kuwa ukifa tu wewe na Mungu mnaanza kupitia ukurasa mmoja mmoja.

Wanasema waingereza YOU LIVE ONLY ONCE, BUT IF YOU DO IT RIGHT ONCE IS ENOUGH.

Maisha yako ni kitabu.
Kiandike vizuri

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni