Jumamosi, 13 Mei 2017

DUNIA HAITOKUKUMBUKA KWA MAMBO UTAKAYOJISIKIA KUFANYA BALI KWA MAMBO #UTAKAYOSUKUMWA KUYAFANYA


Mungu katuwezesha kukutana tena. Basi Jina lake lizidi kuinuliwa maana kuwa hai ni za zawadi kubwa mno.

Leo nina jambo muhimu kuongea na wewe.


Katika kipindi cha miaka saba ambayo nimeitumia kujifunza na kupractice ujasiriamali na kujifunza kwa watu walioacha ALAMA duniani nimeweza kujifunza mambo mengi. Mojawapo ni kuwa dunia haina muda na mambo unayokuwa COMFORTABLE kuyafanya hata kama utafanikiwa nayo vipi. Ukifa yanaishia hapo na jina lako linabaki kwenye kaburi pale. Born 19.... died 20... hivyo yani.

Dunia inamkumbuka mtu ambaye alitii sauti ya MSUKUMO wa ndani wa kufanya kile alicholetwa hapa duniani kukifanya. Unaweza kuwa effective and successful kwenye jambo fulani hapa duniani lakini kama ukifa na jina lako likafa ni dalili kuwa ulikuwa mbinafsi na ulitaka mafanikio BINAFSI tu wala hukujali kuwa unapaswa uguse watu wengine kabla hujaondoka duniani. Ni vizuri kuangalia sana mambo unayoyafanya kama unayafanya tu kwa kuwa ndicho ULICHOSOMEA au ndicho KIRAHISI KUFANYA au unakifanya kwa kuwa kuna MSUKUMO NDANI YAKO wa kukifanya?

Yaani uligombea ubunge kwa kuwa ULISUKUMWA moyoni au sifa tu au ulitaka kuonyesha watu kuwa wewe ni "kiboko"? Usipoangalia hili jambo utakuwa maarufu kweli kweli lakini siku ukimaliza muda wa ubunge na jina lako linaishia hapo tena ukiwa bado hai. Hivi kila aliyewahi kuwa mbunge mashuhuri au waziri bado anatajwa leo na kukumbukwa?
Ask yourself.

Unafanya biashara kama fashion au una MSUKUMO ndani kuwa ufanye? Kama huna msukumo ndani wa biashara basi utakuwa unaendesha gari kwenye njia ya treni. Kitakachotokea hata wewe mwenyewe hutajua yani. Usifanye biashara ili uwe kama Dewji. Yeye ana msukumo wa kwake. Wewe nawe UNAO?

Umeajiriwa sababu "watoto watakula nini" au umeajiriwa sababu una MSUKUMO kuwa inatakiwa uwepo hapo ulipo ili huduma yako iwanufaishe watu wa Mungu watakaokuja kazini kwako? Usifurahie kuitwa ofisa wa benki au meneja masoko au head mistress nk huku una IGNORE sauti fulani inayokusukuma kutokea ndani kuhusu jambo jingine kabisa. Ukiendelea kuiignore hiyo sauti ipo siku ITANYAMAZA kimya haitazungumza tena kwa kipindi kirefu tu. Lakini ujue utakuwa umeignore kitu ambacho Mungu alikuwa anataka ufanye. Utashangaa umekaa kazini miaka mingi na mpaka unastaafu lakini huna amani moyoni na ukistaafu basi jina linaishia hapo pia. Halafu ile sauti ndo itarudi sasa. How sad.

Unasoma Chuo kwa ajili CV ionekane ina neno "University" au ili ukue-kue kidogo kabla hujaolewa...au unasoma sababu una kitu kinakwambia moyoni kuwa unapaswa kusoma hicho kitu. Au ulichagua kozi kwa kuwa ni nyepesi au kwa sababu "ina AJIRA" au sababu rafiki au anko alisema engineering ndo kozi ya "vichwa" kama wewe. Sasa kichwa gani unaambiwa pa kwenda.

Point ya msingi hapa ni kuwa mahali popote ulipo jitahidi sana kusikiliza sauti ya ndani yako. Siyo maneno ya mzazi tu au mume au mke sijui auntie ambao sauti ya ndani yako hawajui inafananaje. Za ndani kwao zenyewe hawajazisikiliza wataelewaje kuwa huwa kuna sauti ndani ya mtu!? So BE YOU. It's YOUR life. Life is really more than money and fame.

Dunia huyapa heshima kubwa majina ya wale waliofanya vitu vilivyotokana na MSUKUMO fulani ndani yao na siyo waliofanya tu sababu ya fashion au kutaka kujulikana na certainly haiwapi heshima wale waliodharau sauti iliyowaambia ACHA HIKI KAFANYE KILE.

Ni ngumu  kuacha kitu ambacho ni popular machoni pa wengi ili ukafanye kitu ambacho unasukumwa moyoni kufanya hata kama hakieleweki kwa wengine. Lakini ukiweza hilo basi jina lako litakumbukwa miaka mingi hata ukiwa umeondoka.

Ngoja nikupe mifano michache tu ya majina yanayotajwa na kukumbukwa sana na dunia.


1. WILLIAM BOEING

Ilikuwa jioni majira ya saa moja kasoro hivi. Mwangaza wa jua la mwezi wa July uling'arisha anga la magharibi kwa rangi nzuri iliyotulia na jua likaanza kudondoka na kuruhusu giza kuufunika uso wa nchi. Nikiwa futi 30,000 kutoka usawa wa bahari ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kushuhudia jua likizama nikiwa angani mbali kiasi hicho. Kuzama kwa jua (sunset) ni mojawapo ya mambo ninayopendelea sana kuyatazama.

Masikioni mwangu kulikuwa na headphones nikisikiliza muziki wa kusindikizia safari yangu ya kwanza ndani ya ndege aina ya BOEING 737.. Baada ya kutazama jua likiwa limeishia kabisa juu ya mawingu akili ikanirudisha kwenye dirisha la ndege kushoto kwangu lilivyokuwa zuri na lilivyotengenezwa kwa ustadi mkubwa. Na kisha akili yangu ikanileta kwenye ndege yenyewe - BOEING 737.

Muda kidogo baadaye jina la mwanzilishi wa kampuni kubwa ya Boeing likaja kichwani. Huyu ni bwana William Boeing. Nikaanza kutafakari kidogo kuhusu alipoanzia, alichoamua kufanya, ALICHOSUKUMWA kufanya, na dunia inamkumbuka kwa lipi katika hayo.

Akiwa amezaliwa familia "bora" baba yake akiwa mhandisi wa mambo ya madini William alisomeshwa shule za maana mno kwanza Uswizi kisha kwao Marekani kwenye Chuo Kikuu maarufu cha YALE UNIVERSITY. Kama hujui kuhusu Chuo hiki Google tu kidogo uone kusomesha mtu hapo inakuwaje.

Lakini William akakatisha masomo yake YALE UNIVERSITY na AKAAMUA kwenda kufanya biashara ya MBAO!! Dah!.  Kuna watu wana maamuzi magumu. Huwa nasema ni rahisi kuacha VETA ili ukafanye mambo yako. Lakini kuacha YALE UNIVERSITY ukauze MBAO? Hiyo ni level nyingine ya maamuzi. Trust me.

Lakini akafanikiwa sana katika hiyo biashara na kupata fedha nyingi mno. Akajulikana kama muuza mbao maarufu.

 Lakini katika safari zake kibiashara siku moja akatembelea maonyesho ya kibiashara huko Seattle na kuona watu wametengeneza mashine fulani ambayo waliirusha angani IKIWA NA MTU.  Moyo wake ukapiga PAAP! Akapata MSUKUMO mpya kabisa wa kuunda NDEGE yake. Na akaacha kila kitu na hela zake akazielekeza kwenye hilo jambo lililompa msukumo mpya.

Alipitia mengi lakini akafanikiwa. Na leo hii dunia inamkumbuka kwa jambo hilo. Ukitazama leo ndege aina ya BOEING zilivyo leo ni mwendelezo tu wa alichokianzisha. Dunia haikumbuki mbao ngapi aliuza. Ukitaja jina/neno Boeing watu hawalihusishi na mbao bali na kampuni kubwa ambayo imegusa maisha ya watu wengi mno. Na hakuna siku inayoenda leo ambapo hagusi maisha ya watu dunia hii. Na hayupo.

What about you? Think about your end. Forget the comfort. Work on your legacy. Utakumbukwa kwa kipi? Kwamba ulikuwa polisi au mhasibu afu basi? Kuna mapolisi au wahasibu wangapi dunia hii hadi ukumbuke ukumbuke wewe? Gusa maisha ya watu hasa wasikokujua kabisa.


2. FRANCIS SCOTT KEY

Huenda hili likawa jina geni kwako. Huyu alikuwa mwanasheria maarufu tu huko Marekani zamani za kale. Alifanya kazi kubwa mno kama mwanasheria hadi akafikia kuwa DISTRICT ATTORNEY hiki ni cheo cha heshima mno katika kila jimbo la Marekani. Kumbuka Marekani kila jimbo ni nchi. Yeye alikuwa District of Columbia. Yani "jikoni". Hivi Mungu akupe nini?

Lakini kuna jambo lilitokea kati ya mwaka1812 hadi 1815. Nalo ni vita kati ya Marekani na Uingereza. Kuna wamarekani wakakamatwa na Jeshi la Uingereza. Yeye kama mwanasheria akawa amepelekwa kwenda kuNEGOTIATE hao watu waachiliwe. Bahati mbaya naye akashikiliwa. Akakaa kwenye kambi ya adui kwa muda mrefu mno huku akishuhudia nchi yake ikidondoshewa mabomu na hana cha kufanya. Lakini siku moja alfajiri mapema mno mapambazuko yakianza na usiku kucha eneo la Marekani lililokuwa karibu na ile kambi likiwa limeshushiwa "mvua" ya mabomu usiku kucha huyu bwana Francis Scott Key huku akitazama kwa masikitiko eneo la nchi yake lililopigwa mabomu usiku kucha akashangaa kuona bendera ya Marekani ikiwa ipo kwenye mlingoti ikipepea. Kitu hicho kilimpa MSUKUMO wa ajabu mno moyoni. Akapata faraja kubwa kuwa licha ya mabomu yote yale lakini bendera ya nchi yake ilikuwa bado ikipepea vizuri kabisa. Akapata MSUKUMO wa kuandika SHAIRI kuhusu hilo tukio. Kichwa cha hilo shairi ni: THE STAR-SPANGLED BANNER (banner=flag)

Miaka kadhaa baadaye Bunge la Marekani (Congress) likapitisha resolution ya shairi hilo kuwa WIMBO WA TAIFA WA MAREKANI!

Leo hii Francis Scott Key hakumbukwi kwa kesi nyingi alizosimamia kwa kazi aliyosomea bali kwa kitu alichoandika bila kusomea. Popote pale wimbo wa TAIFA wa Marekani unapoimbwa  kila siku anagusa maisha ya watu wengi mno wa nchi yake na nje ya nchi yake wanaoguswa na shairi lake.

Usikute wewe unaweza kuchora picha moja tu au kutunga kitabu kimoja tu na dunia ikakukumbuka kwa hilo ila unang'ang'ana uwe maarufu kama Tundu Lissu.
Think about that.


3. NELSON MANDELA

Mwanamasumbwi na mwanasheria pia msomi kutoka Chuo Kikuu cha FORT HARE na kile cha WITWATERSRAND. Na akiisha kupikwa huko katika vyuo AKAAMUA kufanya kazi kama mwanasheria jijini JOHANNESBURG.

Lakini serikali ya watu wazungu ilipopitisha sheria ya ubaguzi wa rangi Mandela akapata  MSUKUMO mpya ndani yake siyo wa kuwa hakimu au jaji no. Ulikuwa ni msukumo wa kupigania USAWA na kupinga sera za kibaguzi kwa moyo wake wote. Msukumo wa kuwa mwanaharakati.

Alipitia magumu mengi, ndoa yake ya kwanza na bi Evelyn Mase ikafa.
Akaanza kufatiliwa na serikali na kukamatwa mara kwa mara. Mwisho akapewa kesi nzito na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela ambacho alikitumikia katika magereza matatu tofauti ikiwemo la Robben Island.

Miaka 27 baada ya kufungwa akaachiwa. Dunia haikumbuki gloves zake au kesi alizosimamia bali UANAHARAKATI WAKE na KUPIGANIA KWAKE USAWA. Pia dunia inamkumbuka Mandela kama mtu aliyekuwa hana kinyongo na mtu. Mfano licha ya yeye kuachana na mke wake wa kwanza kwa sababu za Evelyn kumtuhumu Mandela kutokuwa mwaminifu na Evelyn kubadili dini na kuolewa na mtu mwingine na nk lakini Evelyn alipokufa Mandela na familia walihudhuria msiba vizuri kwa hisia zote. Lakini pia alipotolewa gerezani alimsamehe mtu aliyeidhinisha Mandela afungwe maisha!!
Dunia inakumbuka hilo.

What about you?


4. ABRAHAM LINCOLN

Mwanasheria mwingine huyu. Tena huyu alikuwa mwanasheria kwa KUJIFUNDISHA mwenyewe na kisha kwenda kufanya BAR EXAM (wanasheria wanajua hii kitu..siku hizi kuna LAW SCHOOL)

So huyu ni kichwa sana acha wewe ambaye umefundishwa na maprofessa wazuri na maktaba unayo na computer na internet na hao waliokufundisha wanakupa mtihani na bado unafeli afu unasema eti profesa kanifelisha! Ungejifundisha mwenyewe nyumbani kama Lincoln afu ndo ukapewe mtihani ungeelewa hata swali linahusu nini kweli? Nataka uone tofauti yako na Abbe! Alikuwa kichwa si mchezo.

Alisimamia kesi kadha wa kadha na kupata ushindi mnono hasa kwa kutumia kipawa chake cha kuongea vizuri.

Hata hivyo dunia leo haimkumbuki kama mwanasheria nguli na kichwa bali kama mojawapo ya maraisi bora kabisa wa Marekani na hasa kwa kuzuia umiliki wa watumwa huko Marekani na kuzuia nchi kusambaratika ilipoingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mgogoro wa umiliki wa watumwa ambao ulizalisha chama cha Republicans mwaka1854. Baada ya Congress kupitisha sheria ya KANSAS-NEBRASKA ACT ambayo ilitaka kila jimbo liamue lenyewe endapo litaruhusu watu wake wamiliki watumwa au la. Majimbo kadhaa yakapinga hiyo sheria yakitaka sheria isiwepo suala la kuchagua kumiliki au kutomiliki. Ndipo Republican Party ilipoanzia hapo na LINCOLN akapata MSUKUMO mkubwa wa kuachana na sheria na kuingia kwenye siasa za uongozi wa juu rasmi akijiunga na chama cha Republican mwaka 1856 na kuwa raisi miaka minne tu baadaye!

Wajasiriamali na watafuta mafanikio wanamkumbuka Lincoln kwa jinsi alivyopambana bila kuchoka kutoka level za chini hadi kufikia kuwa raisi wa Marekani. Sheria ilikuwa tu mahali alipoanzia lakini uongozi wa nchi ukawa ni msukumo wa ndani. Msukumo mkali mno wa ndani uliomvusha kwenye changamoto za vipindi vigumu vya kushindwa uchaguzi kupoteza mke kupata nervous breakdown nk hadi akaja kuwa raisi.

Usidharau msukumo wa ndani. Lincoln angeweza kubaki mahakamani lakini jina    lake lingeishia siku yake ya kufa kama maelfu ya wanasheria wenzake huko ambao hakuna anayewajua wala kuwakumbuka.


5. TAIKICHIRO MORI

Kila mtu anamjua Bill Gates hasa kwa kuwa ni tajiri namba moja duniani. Lakini ni vizuri kupitia historia na kujifunza kwa waliowahi kumtangulia katika nafasi hii.
Taikichiro Mori ni mmoja wapo na alikuwa tajiri namba moja duniani mwaka 1992 utajiri wake ukiwa net worth $13 billion.

Na dunia inamkumbuka hivyo yani licha ya kuwa alikuwa academician mzuri huko Japan na mwenye mafanikio katika eneo hilo.

Alipata mafanikio mazuri katika masomo yake hadi kufikia kuwa mwalimu wa Chuo Kikuu.  Na huko katika kufundisha akafanikiwa hadi kufikia level ya DEAN wa KITIVO CHA BIASHARA katika Chuo kiitwacho YOKOHAMA CITY UNIVERSITY. Ukiwa dean wewe ni mtu mkubwa. Alidumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi alipostaafu mwaka 1959.

Ni baada ya kustaafu ndo alipopata MSUKUMO mpya wa kufanya biashara ya REAL ESTATE. Nadhani hela zake mafao hizo. Lol. Alifanya hiyo biashara kwa miaka mingi na akafanikiwa mno ndo hadi kufikia 1992 akawa tajiri wa kwanza duniani. Dunia inajua alipoanzia lakini inakumbuka na kuheshimu ilichomsukuma kufanya.

Sasa kustaafu ualimu au uhandisi au unesi au chochote siyo mwisho wa maisha. Kama kuna sauti ndani inakwambia kagombee udiwani au kafungue mgahawa tii sauti usifanye mgumu moyo wako. Usiseme miye mzee. Kuna mstaafu mwenzako mzee alitajirika uzeeni. Huyu si mwingine bali.....


6. HARLAND SANDERS (a.k.a Colonel Sanders)Huyu naye alikuwa mwanasheria lakini sheria ikagoma "kumtoa" baada ya miaka mingi. Akaona afanye vingine kama kuuza insurance covers nayo ikagoma. Akaamua kuuza taa tu sasa. Taa nazo zikampa headache tu. Mpaka anastaafu anapata mafao anayaangalia hivi anaona ujinga kabisa bora akajiue tu.

Lakini kabla ya kujiua akiwa mahali anapanga mipango ya kujiua akapata msukumo mdogo tu ndani kwamba kabla hajajiua aandike kwenye karatasi vitu vyote ambavyo hajawahi kufanya. Akiwa anaandika akakumbuka kuwa yeye alikuwa ni bonge la mpishi. Na kwamba alikuwa ametengeneza formula  (recipe) ya kupika kuku kwa kumchanganya na viungo zaidi ya 10 tofauti tofauti ambavyo ni yeye tu alikuwa anavijua na kuku alikuwa mtamu asikwambie mtu. Khaaa. Akaahirisha kujiua akaenda kuanza kupika kuku ili sasa badala ya kula mwenyewe akawauzie wengine. Lol. Akaanza kuuza kwenye sehemu watu wanakojaza mafuta kwenye gari. Anawaambia huyu kuku ukimla lazima utampenda maana nimeweka recipe ya viungo vingi vizuri vya asili. Kama mchezo akaanza kuingiza vijisenti. Akiwa na umri wa miaka 62 akapata MSUKUMO mwingine wa kuisajili biashara yake kama franchise business akiwa anaiita KENTUCKY FRIED CHICKEN. Kuku wa kukaanga kutoka jimbo la  KENTUCKY. Hiyo ilikuwa mwaka 1952.

Miaka 12 tu baadaye mwaka 1964 biashara ilikuwa imechanganyia akaiuza kwa $2 million. Bilioni kama nne za kitanzania leo. Fikiria mtu mwenye hela aina hiyo mwaka 64!!! Akiwa mzee wa miaka 74.

Kwa hiyo kama umepigika huoni mbele unataka ufe tu mwambie shetani hivi: NAAHIRISHA KUJIUA SITAKUFA BALI NITAISHI NA NITAFANYA KITU HAKIJAWAHI KUTOKEA HATA KAMA NI KUKAANGA DAGAA UPYA.

Ilimradi usikilize sauti ya ndani yako kwa utulivu. Tulia sikiliza. Mungu akiongea utajua tu I tell you. Utashangaa hakuna atakayekufundisha cha kufanya utahangaika huku na kule wewe mwenyewe utajishangaa hutakuwa na muda na critics na wanaokucheka wala hutatafuta kuonewa huruma tena. Utashangaa mifupa yako ina nguvu akili yako imeamka. Huo nao ni kama ubatizo mpya kabisa nakwambia. Na dunia haitataka kujua sijui ulisoma wapi au ulifanya kazi wapi. Dunia itataka kutangaza jina lako kupitia mambo uliyoyafanya kupitia MSUKUMO NDANI YAKO. Kitabu kinasema UTII NI BORA ZAIDI... Ndo maana Sprite wanasema TII KIU YAKO. Sasa mi nasema TII SAUTI YA NDANI YAKO na utashangaa toka hapo hutajitaji alarm ikuamshe utaamka mwenyewe tu.  Kwani jogoo huwa anaamshwa na alarm? Yeye ndo alarm clock. Sasa ukitii sauti ya ndani utashangaa wewe ndo unakuwa ALARM CLOCK.

Usifanye kitu kwa kuogopa watu watakuonaje kama hutafanya. Kuna watu wakiona RANGE ROVER inapita huwa wanasema: DAH MUNGU ALIUMBA VICHWA AISEE. Utukufu unaenda kwa Mungu. Kuna watu wakila KFC huwa wanamtukuza Mungu. Kuna watu wa wakipanda ndege au wakiimba wimbo wa TAIFA au wakilala hoteli nzuri nzuri au wakinunua iPhone huwa wanajisemea dah Mungu aliumba vichwa. Hayo yote na mengine ni zao la watu WALIOTII SAUTI YA NDANI MWAO. Kuna watu wanapaswa waogeee au kusafishia nyumba sabuni yako halafu ile harufu tu mtu anaisikilizia anamtukuza Mungu. Lakini wewe unataka kukata tamaa. Eti huwezi kuuza sabuni.

Kuna mtu mwingine.. Robin Sharma.. aliacha sheria pia baada ya sheria kumpa stress za kutosha akapata MSUKUMO  kuandika kitabu kinaitwa MEGA LIVING ili kusaidia watu jinsi ya kumanage stress. Kisha akaandika THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI

na THE LEADER WHO HAD NO TITLE na akagusa maisha ya mamilioni ya watu na baadaye kukodiwa na mpaka makampuni makubwa duniani kama NIKE, MICROSOFT, PwC, HP ili afundishe viongozi wa hayo makampuni na wafanyakazi wao. Unakuta analipwa hadi dola laki tano kwa saa na anafundisha masaa matano.  So siku hiyo moja anakuwa ameingiza dola milioni moja na nusu.  Yani bilioni tatu za kitanzania kwa siku moja. Hiyo ndo THAMANI anayopewa mtu aliyetii sauti ya muumba wake kutoka ndani.

Ndege huimba kwa msukumo ulio ndani yao. Siyo kwa kuwa ndege wenzake watamwonaje asipoimba. Wewe unafanya vitu ili watu wakuelewe? Yesu hawakumwelewa watakuelewa wewe? Mimi huwa naandika tu sijali atakayeshindwa kuelewa nachosema. Naangalia msukumo ulio ndani ukiniambia andika kuhusu hiki naandika. Hata ikiwa saa saba za usiku.

Ukitazama watu wangapi wanaafiki ndo ufanye kitu wakati moyoni mwako tayari kuna mwafaka ujue hiyo ni dalili ya WOGA na kutotii.  Kumbuka kitabu kinasema UTII NI BORA.
TII SAUTI YA NDANI YAKO


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.
WhatsApp #o788367511
All Calls and SMS #o752367511
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni