Jumapili, 21 Mei 2017

IN EVERY SITUATION LEARN TO TELL YOURSELF: "OKAY... SO WHAT NEXT?" KATIKA KILA HALI JIFUNZE KUJIAMBIA MANENO HAYA: "NI SAWA... KWA HIYO NINI KINACHOFUATA?"*******
Asante nyingi kwa Mungu kutupa nafasi hii kujifunza pamoja.
*******


Mara nyingi mno tukikosa vitu tunavyotarajia kupata huwa mioyo yetu inasinyaa.

Hivi ulishawahi kusinyaa moyo? Dah.

Yani mtu unakosa raha. Unajiona hufai na kuona bora wenzako wana bahati. Hii haijalishi kama mtu amekataliwa na boyfriend au girlfriend. Au mwingine hata amekataliwa tu friend request Facebook.  Hahaaaa. Au wamemBLOCK.

Yaani mtu akikublock halafu ukajua kuwa ame-kublock halafu ulikuwa unaona ni mtu muhimu kwako unajisikiaje? Rejected right? Halafu unafanyaje unalia?

Hali huwa ni mbaya zaidi linapofikia suala la mtu amekosa dili. Mfano sisi wajasiriamali yani dili nzuri ghafla ikayeyuka. Aisee. Ukimuuliza Andrea vipi anakujibu "We acha tu"

Au kwa wenzetu "wanaotafuta kazi" pale akikosa AJIRA. Au ameachishwa KAZI. Yaani "hali ya hewa" huwa inakuwa kama imevurugika vibaya sana. Vijana waliokosa AJIRA huwa wengine wanakata tamaa. Mabinti wadogo vishawishi vinakuwa na mvuto zaidi ili aanze kuishi kama "wenzake". Watu wazima kidogo anaweza kukosa mwelekeo na hata kuzorota afya.

Wengi wetu huwa hatuna kawaida ya kutulia na kusahau yaliyopita na kuganga yaliyopo na yajayo! Yani mtu akikosa ajira anakuwa kama kila kitu kimestop!

Kwa wewe uliye kundi hilo naomba niseme na wewe kidogo kabla sijaendelea. BRIAN ACTON na JAN KOUM walianzisha mtandao wa WhatsApp BAADA ya kukosa AJIRA. Mmoja kakosa ajira Facebook mwingine kakosa Twitter.

Lakini walikuja kuuuza huo mtandao wa WhatsApp kwa $22 billion. Yani trilioni 45 za kitanzania. (Mwanzo ilikuwa waiuze kwa $19 bilioni lakini dau likaongezeka) ukisoma hii link utaona hilo http://www.dailymail.co.uk/sciencetech/article-2782370/Facebook-completes-19-billion-acquisition-WhatsApp-European-regulators-green-light.html

Sijui unaelewa kukaa tu na computer na kichwa chako na kuwaza vizuri halafu miaka kadhaa tu baadaye wakawa na utajiri huo?

Na mimi kinachonifurahisha zaidi katika hawa jamaa ni kuwa walimuuzia mtu aliyemnyima mmoja wao kazi. Facebook!

Muhimu ni kuwa hawajalalamikia mtu wala kutaka kujiua.  Walikaa wakaendelea na MENGINE.

Hii tabia ya kuendelea na mengine ni jambo muhimu mno maishani. Ukiwa mtu wa kuangalia PAST tu nini kilipaswa kiweje na kwa nini hakijawa.. na kuanza kusema WHY ME? Utashangaa unakufa kabla hujaishi. Serious. Unafikiri Mungu mjinga? We fanya mengine. Mi siku hizi nina usemi wangu : THE PAST 1 MINUTE IS GONE AND I'M NOT INTERESTED IN IT.
So kama kuna kitu nimefanya au sikufanya basi. Nataka kujua zaidi kuhusu NOW. Kesho nayo mwenye nayo hajanipa bado so NOW ndo pa kuishi. Not the past 1 minute or day or month or year. It's gone. And sitaki kuiwazawaza.

Ndivyo walivyoishi hawa jamaa wa WhatsApp. Yani iko hivi... nakuja kwako kuomba kazi unasema HAKUNA NAFASI. Afu mi na smile najibu tu "OKAY". Then naenda kuanzisha kitu kingine na baadaye wewe uliyesema HAKUNA NAFASI unaanza kunibembeleza nikuuzie nilichobuni halafu mimi nasema kama unakitaka basi utakinunua lakini lazima tufanye wote kazi. Na unakubali. Problem solved. Sasa ukilia na kusubiri watumbuliwe wengine ili wewe uajiriwe na wewe ni jipu.

Ukikosa ULICHOTAKA fanya mengine. Sasa mwingine hapa anauliza "mengine yapi?". SASA si ndo maana juu ya shingo yako kuna kichwa. Au kiliwekwa cha nini.  Kina macho. Pua. Kinywa. Masikio. Nywele. Sasa macho ulipewa ya nini? Ya kutolea machozi? Na kichwa ndani yake kuna UBONGO. Uliwekewa wa nini sasa? Si ungepewa kichwa cha kuku basi.

My point is ukikosa chochote usianze kuwaza milele na milele.

Kwenye kitabu changu nimeandika kuhusu  Steve Jobs jinsi alivyoanzisha kampuni ya Apple. Halafu baadaye corporate politics zikaingia akapigwa chini kutoka kwenye kampuni aliyoanzisha mwenyewe. Inauma mno.

But what did he do? Huyu mimi nikimkumbukaga huwa najifunza sana. Yeye hakulialia milele na milele kama wengi wetu. Alienda kuanzisha kampuni NYINGINE.
Halafu jina la hiyo Kampuni nyingine akaiita "NeXT". Na hapa ndo nimepata title ya makala hii.

Yes. NEXT. So kuna NEXT nyingi mno maishani mwetu. What's your NEXT opportunity? Usililie mlango uliofunga. Kitu kikishatokea songa mbele. Steve Jobs aliifanya hiyo NeXT ikawa nzuri na bora mno kiasi kwamba APPLE waliomtema wakalazimika KUMNUNUA tena. Na sharti lake likawa anawauzia lakini lazima awepo kwenye uongozi wa Apple. Na wakakubali. Ndo kisa cha Jobs kurudi Apple na leo iPhone ni brand kubwa na aghali mno sababu yake.

Sasa kama wewe ni msanii wa muziki umeenda studio wamekukataa usilielie. Kaimbe hata kwenye birthday za watu huko bure. Watu watakuona huko huko. Kwani mwenye studio kabaki na sauti yako na miguu yako? Hapana. Basi angalia your NEXT OPPORTUNITY.

Umeanzisha biashara kila unayemjua ANAAHIDI TU kuwa atakuungisha halafu hawakuungishi wala nini. Unaacha eti. Eti unasema hakuna wateja. Kweli? Nchi hii  ina mamilioni ya watu. Waliokataa kukuungisha hata 50 hawafiki unakataje tamaa? We jiulize tu nani my NEXT customer. Wengine watakuungisha mbeleni. Mi nina mteja wangu mmoja hakununua kwangu miaka mitatu mfululizo lakini kuna siku akaja na sikutumia hata nguvu kumwambia chochote. Leo ni mteja mzuri mno. Three years! Ningeacha baada ya mwaka je? So cha muhimu ni kujiuliza WHAT'S YOUR NEXT.. next opportunity, next relationship, next deal, next student,  next coach or manager, next client, next team, next radio show, next job, next business. Kuna mpaka next husband au wife. Sembuse AJIRA?

Your future iko kwenye "NEXT" zako. Siyo kwenye "LAST". Juzi nikawa naongea na binti mmoja kwenye simu anahitaji ushauri fulani. Lakini kila nikiongea naye huwa anapenda kusema I DID THIS I WAS LIKE THIS nk. Nikamwambia tu I'm not interested in your past coz I'm not going to the past and neither are you. Nikamwambia maneno "DID.. WAS" nk hayaletagi melody nzuri masikioni mwangu so asiwe ananiambia. Aseme zaidi kuhusu SASA. NOW.

Najaribu kuupunguzia ubongo wangu mzigo wa kuwaza kinyumenyume!
Nadhani na wewe unatakiwa usiwaze hivyo.  Fikiria WHAT NEXT. Kisha anza kufanyia kazi.

Maisha lazima yakupe LADHA ZOTE ndugu. Nzuri na ambazo si nzuri. Tamu na zisizo tamu. The key is to take each and move on.

Kuna siku nikiwa mwanafunzi Makongo. Nimetoka shule na njaa balaaa. Nimefika home mchana saa tisane hivi nikakuta maziwa yamebakia kidogo kikombe kimoja tu so nikachemsha halafu nikaweka vijiko vya kutosha vya sukari yani nimekoroga hadi raha angalau ule utamu utasaidia kudanganyishia njaa.. Sasa ile kunywa tu khaaaa! Kumbe nilidhani niliweka sukari kumbe chumvi!! Tena ya kutosha. Aisee yani nilicheka kweli.. njaa ikapata bonge la surprise.
Ndo hivyo. Sometimes unataka sukari life inakupa chumvi...tena ya kutosha. Move on.. Find your NeXT.

Ndivyo maisha yalivyo.

Watu wengi wanaishi kwa mazoea. Kuna mtu aliuza nyumba ili agombee ubunge mwaka juzi 2015. Ukisikia KUJILIPUA ndo kama hivi yani. Akapata hela zake akaingia kwenye mchakato wa uchaguzi. Biashara ikawa "kichaa". Kidogo naye awe kichaa. Maana ubunge hana, nyumba hana, hela nazo hana na marafiki nao hana. Hapo ndo utaelewa kukoroga kitu kwenye maziwa bila kuonja kwanza kama ni sukari kweli. Alipata frustrations za kutosha. Lakini hakujiua. Alianza moja akachechemea taratibu naamini anaendelea na maisha baada ya uchaguzi. Amepata NeXT yake. Ndivyo inavyotakiwa ufanye. Move on. Ukibaki na WHY tu utapata madonda tumboni na mvi za ghafla bila kutarajia na bado utakuwa hujabadilisha kilichotokea! Don't be small minded. Move on.

Awamu hii ya JPM kuna watu wametumbuliwa hadharani. Kuna watu wametuhumiwa na madawa. Kuna watu wamezodolewa na kukashifiwa hadharani. Na katika hao wote kuna makundi mawili. Kuna ambao hawakufunua kinywa chao kabisa. Hata mara moja. Hawa ni Big Minded people.  Na kuna waliowaza "KWA NINI WAMENITAJA". Hawa ni small minded people. Maana watu wameanza kutajwa toka shule ya msingi majina ya wapiga kelele. Au Swahili Speakers. Wakala stiki na zilishapoa. Wengine walitajwa kuwa wamebadili dini ili wawe raisi wa nchi. Hawakupiga mayowe. Sasa wewe wa kwanza kutajwa dunia hii? Yesu alionyesha watakaombetray wawili: Yuda  (atamuuza) na Petro (atamkana). Mmoja alijiua mwingine akalia na kutubu na kukomaa kiutu uzima. Wewe ni Petro au Yuda in that regard? Think for yourself.

Ndo kipindi hiki cha JPM mwingine ana kutu moyoni eti "Kwa nini wamemtumbua baba yangu"? Small minded people. Mwingine ana kutu moyoni eti "Hivi kwa nini girlfriend hajajibu message yangu siku ya tatu leo na naona tiki za blue?" Move on. Don't live in the past.

Wana wa Israeli walikuwa wanawaza kinyumenyume tu. Matango na viungo vya chakula walivyoexperience utumwani. Wakatamani hadi kuzikwa kwenye makaburi kuliko kufa jangwani wakasahau wako huru. Wanachotaka hawakioni wakawa watu wa kupiga "mayowe" tu na kulalamika kila wakati. Nadhani unajua kilichowakuta. So wewe pia kama  ULICHOTAKA hakijawa basi find your "NeXT". Hiyo ndo positive thinking iliyomrudisha Steve Jobs Apple na kuwafanya hao waanzilishi wa WhatsApp kuwa matajiri mno.
Kama hukubali ni sawa pia.

Lakini maisha mazuri na ya utulivu (good and tranquil life) kwa wengi yamekuwa ndoto kwa sababu ya kuwa na WHY zisizoisha. Anabaki anajiuliza hivyo tu. Usibaki na WHY. Swali sahihi ni *WHY NOT?* Yaani: why not nisikose mimi kazi. Nilitaka akose nani ili mi nipate. Kwa nini usitajwe wewe? Kwa nini nisisemwe mimi vyeti vyangu. Nataka nani ndo asemwe. Yes, sometimes WHY is a selfish question. Unajiwazia wewe zaidi. Unaunyima ubongo wako fursa ya kuwa CREATIVE. Unabaki na KUTU moyoni kisa boyfriend kakuacha huli wala hunywi na kujiua unataka. Kisa tu hukujiuliza swali sahihi: Why Not. Kwa nini usiachwe. Kwani wewe umekuwa Mungu? Mungu mwenyewe kuna malaika walimwacha. Sembuse wewe? Kuna watu wametelekezwa na wazazi sembuse boyfriend. Eti anasema inauma wewe hujui tu. No move on. Find your NeXT. Unajuaje labda anayefuata ndo ulikuwa umeumbiwa. Trump alililia wake zake walioondoka? Alifind NeXT. Kumbe huyo ndo First Lady. Ujue kama hujaoa First Lady ikulu huipati hata uweje. Sasa wenye ndoto za kuwa maraisi sijasema umpige chini mkeo unahisi ndo siyo sahihi. Lol. Trump huyo hapo. Ana mind hii ya MOVING ON. Democrats mpaka leo hawaamini walipoteza uchaguzi. Kuna watu wanaamini walishinda uchaguzi. Bado wako na WHY. Why siko IKULU. Move on kwanza.

Ukijifunza kuishi kwenye NEXT utapiga hatua kubwa na kuwashangaza wengi.  FIND YOUR NEXT.
Serengeti Boys yetu imetolewa kwenye michuano. What's NeXT? Au tupo tu hatujui nini tufanye. Watakaa tu au watapewa hata zawadi kuwatia moyo. What NeXT.

Umeomba mkopo benki wamekunyima. What NeXT. Move on. Labda wamekunyima kunde tu.......! Shukuru tu Mungu and tafuta what NeXT.
NeXT ndo kila kitu.


****
By the way ile siku niliyokoroga chumvi ya kutosha kwenye maziwa hadi njaa ikapata surprise  niliangalia mfukoni nikakuta nina sh mia tatu. Enzi hizo. Nikaenda kwa Mangi. Sasa unadhani njaa ilipata dawa au hapana?

Find your NeXT my friend.

Mungu akubariki sana!Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
Blog: www.andreamuhozya.blogspot.com
WhatsApp #o788366511

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni