Jumamosi, 12 Novemba 2016

KUANZIA LEO HUTAKOSA MTAJI WA KUANZA BIASHARA


Kila siku watu wananitafuta wanataka kujifunza biashara. Lakini wengi wao wanasema shida ni kukosa ➡ ➡

Mimi huwa nawaaambia kuwa mtaji (pesa) siyo shida kabisa. Tatizo ni kukosa WAZO SAHIHI la biashara. So tafuta wazo sahihi la biashara.

Why?

Well kwa sababu ukipata WAZO SAHIHI la biashara pesa zina kawaida ya kuwa na "KIHEREHERE" cha kufata WAZO SAHIHI lilipo. Ndo maana watu wote waliofanikiwa walianza bila pesa! Hata Donald Trump alianza bila pesa ila akakopa kwa baba yake.
Jeff Bezos alianza bila pesa.
Facebook walianza bila pesa.
Google walianzia gereji tena kwenye gereji (parking) ya mama mwenye nyumba wao, hawakuwa na hela ila walikuwa na WAZO SAHIHI.
Bill Gates alianza na WAZO SAHIHI kuuza software.

Wewe una WAZO gani sasa? Unawaza kufungua saluni au kuuza CD za muziki? Kuuza mbao? Kuuza nyumba? Kuuza magari? Vyakula? Kufanya Network Marketing? Kubuni software au Application fulani fulani? Haina shida. Whatever utaamua kufanya kuna kitu muhimu kuangalia. Je hiloni wazo sahihi la biashara KWAKO?

Likishakuwa sahihi kwako hela itakuja tu.

Hii ni kwa sababu WAZO likiwa sahihi unaweza kwenda kwa mtu ambaye hujawahi kutarajia kumfata kumwambia akupe mtaji na atakupa! Na hata akawa hajaelewa kila kitu still akakupa! Kwa hiyo kuanzia Leo usihangaike na mtaji. Mimi ni shahidi wa jambo hili katika safari yangu ya biashara na ujasiriamali.

So... Hangaika kwanza kujua unachotaka kukufanya ni SAHIHI KWAKO?

KANUNI NI HII (THE AGM's PRINCIPLE OF START-UP CAPITAL ATTRACTION):

"WAZO LIKIWA SAHIHI KWAKO INA MAANA KUNA SULUHISHO FULANI UNALETA KWA WANADAMU WA MAHALI FULANI KWA WAKATI HUO. PESA ZITATOKA ZITOKAKO KUKUFATA WEWE ILI KUKUWEZESHA KUTIMIZA KUSUDI HILO LA KUTATUA HIYO SHIDA YA WATU"

The whole universe will conspire to bring the money you NEED to get started. That's very important.


SWALI MUHIMU NI HILI:

Sasa utajuaje kuwa WAZO fulani la Biashara ni sahihi KWAKO? Hapa nakupa kanuni yangu nyingine.
(Hii nimeiita THE AGM's PRINCIPLE OF DETERMINING THE RIGHT BUSINESS IDEA). This one ni threefold. Ina vitu vitatu: THINKING, TALKING  and STARTING. Tunaanza kimoja kimoja. Ili ujue kuwa ulichonacho ni THE RIGHT BUSINESS IDEA vitu vitatu vitatokea kwako. Visipotokea ujue hiyo business idea siyo yako! Ni sahihi kwa mtu mwingine. Au siyo sahihi kwako kwa sasa.

Je, ni vitu gani hivyo?

1. YOU CAN'T STOP THINKING ABOUT IT.


Yaani hilo wazo la biashara ukishakutana nalo litakujaa kwenye fikra (mind/heart) kwa namna ya tofauti sana kiasi kwamba utakuwa consumed na hilo wazo kila uendako. Hii ni muhimu sana kujichunguza. Huwezi kuwa na wazo sahihi la biashara halafu eti likawa halipo kichwani kwako siku nzima unaendelea na mambo yako siku nzima huiwazi kabisa hadi baadaye. Au mpaka mtu akuulize eti. Aisee. Ukiwa na wazo sahihi litakuwa kichwani all the time.

Katika kufundisha kwangu biashara niliwahi kwenye Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na katika kuongea na wanafunzi nikajikuta ninaongea na kijana mmoja ambaye incidentally alikuwa ndo raisi wa wanafunzi. Na katika kubadilishana naye mawazo one of the things alichoniambia ni kuwa yeye huwa anatest rafiki zake kama akiwapa idea fulani kuhusu mambo ya wanafunzi labda mfano kuanzisha mradi wa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu nk anasema akikupa hiyo idea wewe mwanafunzi mwenzake halafu usipomtafuta ndani ya wiki nzima basi hilo jambo alilokwambia halijaingia akilini mwako sawa sawa. Hiyo ndo test yake. Na hapo hatakuuliza tena. Wow!

Brilliant young man! Now anamiliki App maarufu inaitwa SOMA APP. Google hiyo kitu umwone alipofika.

Ndo hivyo hivyo sasa. Ukiona umepata wazo fulani la biashara halafu halizunguki kichwani mwako mchana na usiku ni dalili kuwa si la kwako.
Na si kwamba ni wazo baya. Ah-ah! Ni zuri ila tu siyo sahihi kwako tu. Hiyo ni test ya kwanza.
Jipime.


2. YOU CAN'T STOP TALKING ABOUT IT.

You just can't!


Mentor wangu amekuwa akinikumbusha kitu kwamba Biblia inasema kimtokacho mtu ni kile kiujazacho moyo wake( Out of a heart's OVERFLOW the mouth speaketh). So kitu kinachomtoka mtu iwe ni lugha (kiswahili, kiingereza au kimarangu) or aina ya lugha yake (ya kistaarabu, matusi, nk) vinaonyesha tu huyu mtu mind/spirit yake imejaa nini?

Sasa hata katika hili la mtaji. Kanuni ama test ya pili ni kwamba kwa kuwa wazo litakuwa litakuwa limejaa in your mind/heart/spirit kiasi cha kwamba ndo hicho hicho unafikiria kila wakati. Yani WAZO hilo la biashara limejaa mawazoni mwako kiasi kwamba ukinywa maji unaliona kwenye glass!!! Basi kitakachofuata ni kuwa kila ukiongea utataka uliongelee. Na utaanza kushangaa unataka tu kuwa karibu na watu wanaoweza kukufeed taarifa sahihi kuhusu hilo wazo. Hutataka kukaa karibu na watu wasioweza kukupanua zaidi kuhusu wazo lako. Hutakaa tena karibu na watu wanaoweza kukucheka au kukukatisha tamaa. Maana utakuwa huivi nao tena. Hata kama ni WAZAZI au ndugu. Utashangaa unataka kampani ya watu wanaongelea biashara biashara zaidi kuliko kuongelea Trump kashinda kweli au bado wanahesabu kura. Sijui utabiri ulikuwa wa uongo au wa ukweli. Utajikuta hizo habari hazikuvutii tena. I'm telling you, ukishapata WAZO SAHIHI la biashara likakukaa sawa sawa kichwani basi lugha yako itachange AUTOMATICALLY.

Are you hearing what I'm telling you?

Na kuna watu utawaboa mno. Maana kimtokacho mtu ni kile kiujazacho moyo wake. Na wewe na wao sasa mioyo/mind zenu zimejawa na kuwa consumed na vitu tofauti! You can't stop talking about your business idea. Hilo la pili.
Twende la tatu.

3. YOU CAN'T WAIT TO GET STARTED

Hili ni muhimu zaidi.

Utafika mahali huoni haja ya kuishi bila kulifanya hilo WAZO kuwa halisi. Yani utahangaika kama mama mjamzito akikaribia kujifungua. Coz you are PREGNANT. Na ujauzito wako wa hiyo idea yako haufichiki tena kila anayekujua anafahamu. Na sasa utafikia hatua una UTUNGU wa kuzaa.

Siyo wewe. Ni idea inataka kuja. Utakosa amani moyoni bila kuona hiyo idea ikiwa halisi. Wa kukuita kichaa watakuita kichaa. Wa kukucheka ndo muda wao huu maana unahangaika kama kuku anayeanza kutaga kwa mara ya kwanza yani hata kwenye bustani atataga. Ndo hapa nimekwambia Google walianzia garage. Facebook walianzia bwenini. Si unasikia Bakhressa alianzaje? Wa kukukatisha tamaa wataongeza juhudi utadhani wako muda wa majeruhi. Hiki ni kipindi huwezi kutulia. Na hapa sasa imani inakuwa KALI sana kama vile umekuwa kichaa. Yani ndo hapa ukiambiwa shuka kwenye boti utembee juu ya maji unashuka fasta! Utawaza baadaye. Imani kali! Hapa ndo watu huwa wanapata mitaji wa njia ambazo hakuwahi kuzifikiria kuwa atakuja kufanya siku moja. Hapa mimi binafsi napafahamu sana. Yani ni unakuwa na CONVICTION kiasi kwamba hata ukimfata mtu kumwomba mtaji anaweza kukusikiliza moyo ukamchoma tu bila sababu hata hajakuelewa vizuri akakupa.
Are following me?


HAPA ndipo watu wengi wanalia eti ooh "sina mtaji". Nani kakwambia mtaji ni shida my friend? Shida ni WEWE!! Huna conviction moyoni. So hata ukiongea na mtu kuhusu IDEA ya biashara unayotaka kuifanya mtu haoni kabisa kama unachotaka kufanya kinatoka moyoni mwako. Unaongea EMPTY words! Mdomo tu unaongea. Moyo haupo. Na hili limewakosesha watu wengi fedha za kuanzia kwa kutokuwa na conviction.

Sikia ndugu mpendwa.. Watu wenye uwezo wa kukupa mtaji huwa hawasikilizi mdomo wanasikiliza SPIRIT yako inasemaje? Wanajua mdomo ukiwa unaongea na MOYO ukiwa unaongea. Kuna tofauti. Kama maneno unayotamka kuhusu why unamwomba hela yakiwa empty atajua tu. Na yakiwa yanakuja na CONVICTION pia atajua.


*Case Studies:*
Jifunze kwa wawili hawa

(i) Joe Kusaga alipotaka kuanzisha Clouds FM alienda kuomba hati ya nyumba ya baba yake ili akakope pesa benki. Na wakampa hati bila kujua huko mbele itakuwaje. Why? Kwa sababu ya CONVICTION aliyokuwa nayo moyoni. Jaribu wewe sasa uone hao wazazi kama hawajakuitia Dr Chris Mauki aje akupe ushauri wa KISAIKOLOJIA!

(ii.) Jeff Bezos wa AMAZON DOT COM.

Huyu alipotaka kuanzisha mtandao wa kuuza vitabu kwa njia ya internet hakuwa na hela akawaomba wazazi wake wampe pensheni yao aanzishie biashara. Can you imagine? Hivi wewe ukiwafata wazazi wako leo ukawaomba pesheni yao hapo ndo wamestaafu eti wakupe wewe huyo ukaanzishe biashara.. Hivi wataona empty words au wataona moyo wako wote uko consumed na hilo WAZO SAHIHI la biashara? Jeff wazazi walimuuliza umesema unataka pensheni yetu sisi, ukaanzishe biashara kwenye internet? Internet ndo nini? Enzi hizo hata wazazi wake hawajui internet ni nini. Ni kama wewe tu bibi yako au hata mzazi kijijini hajui internet sijui blog sijui tovuti afu leo umwambie"Baba hizo hela ulizouza korosho mi naomba ninataka kufungua TOVUTI!!!" Hahaaaa. Imagine! Sasa Jeff wazazi  hawakumwelewa lakini walimpa PENSHENI. Why? Because ALIKUWA NA WAZO SAHIHI, na likawa limejaa kwenye MIND yake and akawa hawezi kuacha kuwaza wala kuliongelea na alipoongea na wazazi wake moyo wake wooote ulikuwa juu ya MANENO yake. Walimpa aisee. Bila kumwelewa.


Sasa huwa nakutana na watu hasa vijana wanalialia tu. Anasema "nimeongea na ba mkubwa anipe mtaji nikafungue saluni hata hajanielewa!" Kweli? Are you sure uliongea kutoka moyoni halafu hakuelewa?

Mwingine anasema: "Nimepata WAZO la biashara nimemwambia mama mdogo anipe mtaji hata hajanielewa". Sasa ndugu yangu unaomba mtaji huku unang'ata kucha utadhani unaongea na boyfriend kweli huyo mama mdogo atakuelewa?

Mwingine anasema Oh "nimeongea na mume wangu anipe tafu kidogo kuhusu mtaji wala hata hanielewi". No my friend. Wewe ndo hujajielewa upo wapi katika utayari wao mumeo siyo shida. Huna conviction.. Unaongea na mtu kuhusu mtaji as if unaongea naye kuhusu nauli ya bajaji. Huna passion. Kwani ukiomba nauli au ada kwa mzazi unahitaji PASSION yoyote? No. Lakini kama ukidhani ukiongea naye hivyo hivyo kuhusu mtaji atakupa utashangaa ada ya milioni tatu alilipa ila mtaji wa laki tano au saba hakupi!!! Why? Huna CONVICTION. Maneno yako hayana uzito unaoweza kumchoma mtu  moyoni. And that is YOUR problem. Mtu anayekupa mtaji kipimo chake pekee ni HOW SERIOUS ARE YOU. Akiona hauko setious anakujibu tu "sina hela" au "ngoja baadaye". Ukioma unaambiwa NGOJA na wewe unaridhika ujue ni kweli ulistahili kunyimwa mtaji. Huwezi kuwa na ujauzito wa kujifungua afu mtu akwambie ngoa usijifungue leo ngoja kesho.
So how come wazo lako limefikia muda wake halafu mtuwingine ambaye wazo hilo si lake akwambie SUBIRI na wewe usubiri kweli?

Nakupa elimu ADIMU hapa. Izingatie sana. Ni elimu nyeti sana..

So usiseme "sina mtaji". No my friend. Mtaji si kazi yako. Ni kazi ya watu wengine. Mtaji unaweza kutoka kwenye mshahara, au kukopa kwa mtu au kuuza kitu cha thamani ulichonacho. Wanunuzi watapatikana bila wewe kuelewa imekuwaje. Yes ukiwa consumed na idea yako utauza anything even everything. Yani hata simu unaweza kuuza ili ukusanye pesa upate pa kuanzia zingine utaomba huko mbele kwa mbele.

But problem nya watu wengi sana sana ni kuwa hawana PASSION na wazo la biashara alilonalo. Nikiongelea kuuza simu hapo unajisemea aah broh we nipe idea nyingine tu ya kupata mtaji. Kuna mtu alinijibu hivyo ati. See?

Inawezekana inanibidi nikukumbushe mfano wa yule jamaa kwenye Biblia. Aliona hazina mahali kwenye shamba la mtu. (That's a business idea). Au unaionaje wewe? Hiyo kitu ilimconsume mpaka alienda kuuza kila alichokuwa nacho akaenda kununua lile shamba.
Bila kuchelewa. Huenda wakati anauza mkewe aligombana naye. Lakini baadaye akawa very wealthy.

Kwa hiyo mimi huwa nawaambia watu hasa vijana kwamba ukiona unashidwa kupata MTAJI dunia ya Leo ujue either:

1. HUNA WAZO SAHIHI LA BIASHARA

na kama unalo basi ni kuwa

2.  HALIJAKUJAA SAWASAWA KIFIKRA

Likijaa sawasawa utamfata hata Dewji na appointment utapata na atakupa huo mtaji hata ungekuwa milioni 40 anakupa. Lakini sasa akikusikiliza je ataona maneno ya mtu ambaye yuko consumed na idea yake kutoka moyoni au ataona maneno tu ya mtu anaomba pesa kinyonge kinyonge?

Money is not a problem. YOU are the problem. Watu wa kukupa mtaji unataka au kununua vitu vyako unavyouza ili upate mtaji wapo lukuki!


Ila wanachohitaji ni CONFIDENCE wakati unaomba hiyo hela. Siyo UNYONGE na kuonewa huruma.

Ukifuata ushauri wangu huo hutokaa ukose mtaji wa kuanzia biashara.


Kwa maoni, ushauri, critique, au Appointment.



Thank you and God bless,

Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania
East Africa.
WhatsApp only: +255 788 366 511
SMS/Calls:  +255 752 366 511

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni