Alhamisi, 24 Novemba 2016

TAKING ACTION: THE BIGGEST SIGN THAT YOU WILL BECOME SUCCESSFUL KUCHUKUA HATUA: DALILI KUU YA KUWA UTAKUWA MTU WA MAFANIKIO


Wakati wa mwanzo kabisa wa huduma (ministry) ya Yesu Kristo hapa duniani kuna watu walikuwa wa kwanza kwanza kufanikiwa kujua (ku-taste) ukuu wake kwa namna ya pekee sana. 

Lakini wote hao mpaka kufikia kuexperience jambo hilo walichukua HATUA fulani ya mwanzo ya kumfata. Ambayo huenda ingeonekana ndogo mno wakati wanaichukua KUMBE ndo ikawa hatua muhimu kupita kiasi!

Kila mmoja kati yao alienda kwa Yesu kwa style tofauti. Kuna aliowaita mwenyewe. Na kuna waliomfata wenyewe. Na katika hao wote kuna waliomfuata au kumjia wakiwa bado hawajui vizuri wanachotaka kwake. 
Kuna waliomfata kwa sababu wamealikwa tu na watu waliowaamini. 
Na kuna waliomfata wakiwa na mashaka wanataka labda tu wakathibitishe mashaka yao.

Lakini point yangu hapa ni kwamba WALICHUKUA HATUA!

Ngoja nitoe mifano kidogo:


Mfano wa Kwanza:

Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji.

Kuna wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walikuwa na mwalimu wao one day yani huyo Mbatizaji. Wakasikia anamwongelea Yesu kuwa ndo "dili lenyewe yani". Yani kwamba ndo kitu TRENDING. Maana alianza kusema siku moja: "TAZAMA MWANA-KONDOO WA MUNGU, AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU...." Wanafunzi wake waka-note. Lakini hawakuchukua hatua yoyote. Ndivyo ilivyo sometimes. 
Kesho yake tena akiwa yuko na wawili kati ya wanafunzi wake Yesu akapita zake Yohana alipomwona akarudia tena "TAZAMA, MWANA-KONDOO WA MUNGU!" So hao wawili wakam-UNFOLLOW Yohana Mbatizaji rasmi wakamfata Yesu. Na Yesu akawaona akawauliza wanataka nini kwake jamaa nao wakamuuliza tu "UNAKAA WAPI?". Hahaaaa...Kama bongo hapa ukiuliza swali unajibiwa na swali. Hii kumbe imeanza zamani. Akawaambia tu "COME AND SEE". Note this... Hao wawili walienda na kukaa na Yesu kwa masaa machache tu and it changed their lives completely.
Lakini yote ilianzia na wao kuchukua hatua.
Kumbuka kuna wanafunzi walibaki kwa Yohana maisha yao yote mpaka anakatwa kichwa!
They never took action kumfata Yesu kamwe.
Only TWO did.

Sikia ndugu yangu, mafanikio siyo suala la 'wenzako' wanasemaje bali WEWE unaonaje. Usipoangalia utabaki na watu ambao wanakoenda ni dead-end. Yes dead-end kwa sababu mission ya Yohana Mbatizaji iliisha Yesu alipoanza kazi but hata Yohana Mbatizaji hakutambua bado aliendelea na kazi akiwa na matarajio mengine. Maana kuna siku akawatuma tena hao wanafunzi wake. Hebu kamuulizeni hivi ndo yeye mwanakondoo kweli au tusubiri mwingine? Funny. Wakapewa nao majibu mazuri na Yesu wakayaleta kwa Yohana Mbatizaji. Na ajabu wanafunzi wale wale waliendelea kumfata Yohana huyo huyo badala ya kumfata Yesu. Licha ya kuona mambo amazing aliyofanya Yesu na licha ya kuwa Yesu alishatambulishwa kwao na Yohana Mbatizaji siku nyingi!

Nazidi kukuonyesha kuwa usifate watu tu kwa kuwa ni wengi. No. Think for yourself. Ni wanafunzi wawili tu kati ya wanafunzi wa Yohana ambao walimfata Yesu!
Only two.
Tena hawakuwa na hakika kivile. Lakini walipomfata Yesu. Kwa maana ya kuwa "FOLLOWERS" kabisa basi masaa machache tu ya kukaa naye yalitosha sana kuthibitisha kuwa walifanya the decision of their lifetime!

Mafanikio ni ya wachache.
Na ni personal issue. 
Avoid group thinking. 


Mfano wa Pili: 

Hapa tunauona kwa  SIMONI (PETRO). 
Sasa kati ya wanafunzi wale wawili wa Yohana waliomfata Yesu mmoja alikuwa ni ndugu ya Simoni. Anaitwa Andrea. Alipotoka tu kwa Yesu stop ya kwanza ilikuwa kwa ndugu yake. Akamwambia Broooo! "TUMEMWONA MASIHI (KRISTO)". So kitendo bila kuchelewa akampeleka Simoni kwa Yesu. Kumbe Simoni kuchukua ile action ya kwenda kwa Yesu ilikuwa very muhimu. Maana ile kafika tu kwa Yesu akakutana na surprise ya kupewa jina jipya linaloendana na destiny yake. Bonge la surprise. Well, surprise hasa siyo kupewa jina jipya per se. Surprise ni kuwa Simoni alikuwa ameishi miaka yote duniani bila mafanikio kumbe moja ya limiting factor kwake kufikia mafanikio ilikuwa JINA. Yesu akamwambia from now utaitwa KEFA (au tafsiri yake tuliyozoea sisi, PETRO, yani Jiwe)!! Duh. 
Mafanikio makubwa ya Petro yalianzia kwenye kubadilishwa jina.
Lakini KWANZA alichukua hatua kwenda kwa huyo Yesu mwenyewe!
Action.
Ni neno dogo sana. Lakini limefanya wengi kubaki duni na kutoishi destiny zao sababu kuna mahali hawakuchukua hatua stahiki.

Unaweza kuwa unatafuta mafanikio and your purpose in life bila kujua kipi kinakulimit, mpaka siku uchukue hatua fulani ndogo tu. 
Labda kwenda mahali. 
Labda kusoma kitabu fulani. 
Labda kuhudhuria semina au mafunzo fulani. 
Labda kukutana na mtu fulani. 
Labda kwenda mji fulani, etc. na huo ukawa mwanzo wa safari yako ya mafanikio.

Petro angekataa kwenda kwa huyo Yesu ingekuwaje? Huenda angevua samaki mpaka siku anakufa na asingefikia mafanikio. Maana destiny yake ilikuwa imefichwa katika kazi ya kuhubiri na kusimama imara katika kanisa la kwanza nk. Siyo kuanzisha soko kubwa la samaki wakavu na dagaa mchele.

A very small, even sometimes seemingly insignificant action, inaweza kubadili maisha yako completely.
Muulize Petro.


Mfano wa Tatu:

Mwingine ni NATHANAELI. 
Huyu jamaa alikuwa mtu mmoja mwenye roho nzuri mno. Ana pure intentions katika mambo yake yote. Mtu safi. Siku moja akakutana na mtu fulani wanafahamiana. Anaitwa Filipo! Ebana Nathanaeli mambo vipi? Poa. Afu huyu Filipo anamwambia Nathanaeli... Ebanaee sikia "TUMEMWONA YEYE ALIYEANDIKIWA NA MUSA KATIKA TORATI, NA (aliyeandikiwa pia na) MANABII, YESU, MWANA WA YUSUFU, MTU WA NAZARETI". Nathanaeli akasema We Filipo, acha hizo, toka lini Nazareti kukatoka jambo jema lolote. Let alone unaongelea jambo kubwa kama hili?

Ndo maisha yalivyo. Ukimpa mtu habari yoyote unayoona nzuri kwake usishangae akawa wa kwanza kukujaza wewe tena DOUBTS. Unaweza kuta unadeal na mtu ambaye ndivyo mindset yake ilivyo. Labda umetoka Sumbawanga juzi juzi na umeona huko fursa moja muhimu mno na umeamua kumshirikisha pia. Usishangae akaanza kukuhubiri wewe na kukuuliza: "Toka lini Sumbawanga kukatoka......? We unapajua Sumbawanga vizuri? Usikute hicho ulichoona kiini macho tu? Sumbawanga si mchezo?" See? Usipokuwa makini wewe mwenyewe unapotezea kabisa. Hahaaa poor you. Umesahau ndivyo watu walivyo. So usitetereke. Filipo hakutetereka. Watu wako hivyo always. Umemshirikisha kuna jambo zuri Tanga atakwambia: Toka lini Tanga kukawa na..... Hayo ndo maswali ya wanadamu: Toka lini wazaramo wakapata.....? Toka lini? Chaweza kitu chema kutokea Mkuranga??
Zoea tu hayo maswali.

Ni kawaida ya watu kuuliza. Hata kama wana moyo mzuri ama nia njema kama Nathanaeli. Mashaka ni sehemu ya ubinadamu. Na nilichojifunza mpaka sasa ni kuwa mashaka ni sehemu ya fursa ya kumfunza mtu. So usikasirike mtu akikuonea shaka. Ni opportunity tu ya wewe kumwondoa shaka. Ndicho Yesu alichofanya.

So Nathanaeli akawa na shaka na ujumbe wa Filipo. "LAWEZA NENO JEMA KUTOKA NAZARETI?" Filipo akamwambia Nathanaeli "NJOO UONE". Powerful.

Nathanaeli alipokuja akakutana pia na surprise.

Kwamba kumbe Yesu alikuwa anajua everything kuhusu maisha yake. Maana alipokaribia tu Jesus was like, waooh, now huyu ndo muisraeli pure asiye na ila ndani yake. Which was true. But kumbe mafanikio ya Nathanaeli pia yalitegemea mno yeye aanze kuishi BILA MASHAKA MASHAKA. And moja wapo ya vitu muhimu nilivyojifunza kwa Yesu ni His INCREDIBLE ABILITY TO ELIMINATE DOUBT! Coz Nathanaeli akashangaa. Huyu mtu ndo tunaonana kwa mara ya kwanza amenijuaje? So ikabidi aulize. Aisee " UMEPATAJE KUNITAMBUA (kwamba ninaishi bila ila in my life?". Yesu akatoa jibu lililozidisha BELIEF ya Nathanaeli. Akasema like, usishangae nimejuaje kuwa unaishi bila ila, najua vingi tu, mfano mimi nilikuona kabla hata hujakutana na Filipo kuna wakati ulikuwa umekaa chini ya mti fulani hivi (Yesu aliutaja jina kabisa mti wenyewe: fig tree. Mtini). Daaah! Nathanaeli alikuja na doubts lakini mwisho akaondokewa na mindset iliyojaa doubts. Na ukawa mwanzo mpya kuelekea destiny yake.


But what if angekataa kutake action kwenda na Filipo? You see my point? Angeweza kuishi vizuri bila ila, bila kusema uongo wala kumfanyia mtu jambo baya na mwisho asingefanikiwa kuishi destiny yake kwa kuwa mafanikio kufikia destiny yake yalikuwa yamefichwa kwenye yeye kuishi pasipo mashaka mashaka maishani mwake. Alikuwa vizuri kimaadili nk lakini mind yake imejaa doubts. It means hakuna na imani. Biblia inasema bila ya imani HAIWEZEKANI kumpendeza Mungu. Can you imagine. Kuishi na mashaka mashaka ni binge moja la limiting factor kwa wengi. That's why ni muhimu kufind out the truth. Kweli tu ndo itakuweka HURU. Kumbe kuishi na mashaka kuhusu vitu ni UTUMWA.

Nathanaeli alipotake action tu kila kitu kikabadilika!

Action..
Unamkumbuka yule kijana tajiri? Yesu alimwambia KAUZE KILA KITU KISHA UJE.

Action ikawa ngumu.
Action.

Siyo rahisi. But ndo kila kitu. 

Ndiyo maana watu wanatangaza semina za dini, makongamano, mikesha, mikutano ya biashara na ujasiriamali, umuhimu wa kujisomea vitabu. Everyday! Lakini wewe unaignore tu. You don't take ANY action. Unascroll tu. Na kwa kuwa msiochukua hatua mko wengi unajifariji. Unadhani ili kitu kiwe dili lazima kila mtu akifate. Unasahau wanafunzi wengi zaidi wa Yohana walishindwa kutake action mpaka wakafika DEAD-END!
Be careful my friend. 
Be careful.

Sisi tutaendelea kusema tu maana tunajua kwa nini tunasema soma vitabu. Tumesoma na tumeona namna vimetusaidia. Tunajua why tunakwambia hudhuria seminars. Kajifunze ujasiriamali using'ang'ane na ajira. But you're not taking ANY action. Wewe endelea kujifariji kwa kuwa mko wengi. Ukifika DEAD-END utakumbuka. Sisi hatutaacha hata kama hakuna anayeamini tusemacho. Yesu mwenywe yaliwahi kumkuta na akamwambia Nikodemo: SISI TUNASEMA TUNALOLIJUA NA TUNASHUHUDIA TULILOLIONA LAKINI NYINYI HAMKUBALI..!! (Yohana 3:11)

Na hata Isaya, nabii yule wa kale, aliwahi kuuliza: UNADHANI KUNA MTU AMESADIKI HABARI TULIYOILETA? 
(Isaya 53:1)

So my friend habari niliyoileta Leo ndo hii:

LEARN TO TAKE ACTION.


Usiangalie wenzako.  Usiangalie bosi wako.
Sometimes hata mzazi huangalii kama atakuwa kikwazo kufikia destiny yako. Aliumbwa kukuongoza siyo kuzuia destiny yako na kukupangia ya kwake yeye. 

Usije ukashindwa kufikia mafanikio ukakosa mafanikio kumbe kisa kuna kitabu kimoja tu hukusoma ndani yake kulikuwa na chapter ina ujumbe wako!
Au kwa sababu kuna mtu mmoja tu hukukutana naye angeongea na wewe dakika 10 na maisha yako yangebadilika!
Au kuna clip fupi au audio au message kama hii uliona NDEFU wakati ingekuwa inaongelea Wema Sepetu ungeona mbona story umekuwa fupi?? Hahaaaa. Poor you. 
Be careful.

Learn the science and art of TAKING ACTION.
Waliofanikiwa wote walijifunza kwanza umuhimu wa KUTAKE ACTION.


Have a great day.

Kwa mawasiliano zaidi
WhatsApp Only: #o788366511
Sms+Calls        : #o752366511
Instagram         :@andremuhozya

Kujifunza zaidi nenda:
www.andreamuhozya.blogspot.com


Love you lots!


Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam Tanzania
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni