Alhamisi, 8 Desemba 2016

THE THREE KINDS OF PEOPLE YOU WILL ASSOCIATE WITH AND THE RESULTS THEREOF .. AINA TATU ZA WATU UTAKAOHUSIANA NAO NA MATOKEO UNAYOPASWA KUTARAJIAWakati niko High School mwalimu wangu wa somo la Historia alipenda kusema kuwa dalili mojawapo ya kutoelekea mafanikio yako ni kuwa na mahusiano ya kila siku (day-to-day) na watu kwa kuwa mambo unayoongea wanayaona ni point kweli kweli. Au kwa kuwa unawazidi pesa au level ya maisha.. Au kuwa na ukaribu na watu sababu tu mnafanya kazi pamoja au mnafanya vitu vya kufanana bila kujali kama kuna value yoyote wanaongeza katika maisha yako. Au kuwa na ukaribu na watu kwa kuwa tu wote mmetokea sehemu moja  - bila ya kujali wanakoelekea na wewe unakoelekea.  Katika hili alipenda sana kutoa mfano wa wakati yeye akiwa Chuo Kikuu jinsi alivyokataa kuwa katika "UMOJA" wa watu wa kabila lake, kwa sababu alikuwa akisema "IT'S NOT ABOUT WHERE YOU COME FROM BUT WHERE YOU'RE GOING". Yaani muhimu siyo wapi unatoka bali wapi unaenda.
Wise man.

Ukichunguza maisha ya watu wengi utagundua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya level ya maisha yao na watu wanaoji-associate nao.  Hata wewe unaweza kuona hilo. Wataalamu wanaita hii kitu LAW OF ASSOCIATION. Ambayo wanasema kuwa "Wewe ni WASTANI wa watu watano ulio na ukaribu nao zaidi"

Yaani ufahamu wako, pesa zako, mali zako, na hata ndoto zako, huwa zinakuwa ni WASTANI wa vile vya watu wako watano unaoji-associate nao kwa ukaribu. Kwa hiyo ukitaka kubadili level ya maisha yako basi badili tu gia. Gia yenyewe ni nini? Gia ni aina ya marafiki zako watano wa karibu.


Kimsingi kuna MAKUNDI matatu makuu ambayo unatakiwa kuyajua linapokuja suala la watu ulio na ukaribu nao. Or rather, watu walio na ukaribu na wewe.


I. WATU UNAOWAZIDI UWEZO

Hili ni kundi la kwanza. Na hili ni kundi litakalokufanya ushindwe kufikia mafanikio yako. Sasa inawezekana umelelewa katika mazingira ambayo hukuwa ukitambulika kwenu. Na Mungu si Athumani sasa umepiga hatua fulani kiufahamu. Ama kifedha. Ama kiroho. Na hivyo kuna watu wanatamani kuwa tu karibu na wewe. Sasa usiingie mtego wa kuwafanya kuwa your ASSOCIATES. Utarudi nyuma sana. Maana hawa hawana cha maana cha kuadd maishani mwako. Bali they are the takers. They'll take everything you have and give you nothing in return.  Hawa ni watu ambao sometimes wanaona wako entitled kupokea kutoka kwako na siyo kutoa. Usipowasaidia au kuwashauri au kuwainua watakuona mbaya. Be wary of them. My auntie aliwahi niambia usiwasaidie watu mpaka wakaona hakuna haja ya kuomba wala kumtegemea Mungu. Utakuwa wewe umekuwa Mungu wao and God will punish you.

So kundi hili hawana cha kukupa cha maana. They're at the bottom. Ukiwaweka hawa karibu utaishia kulose hata zile gifts ambazo Mungu alikupa. Hawa ni walalamishi. Negative thinking. They have the victim's mentality. Hawatakufikisha popote.
Pause now and think. Je katika watu ulio na ukaribu nao sana kuna watu wa aina hiyo? Cut off the relationship mapema. Anza tu kupunguza u karibu. It's for your own good. And eventually theirs too. Kama una watu ambao kwa mfano una ukaribu nao mwaka mzima huu January till now December but hujapata any value in any way from them ondoka. Wanasema if you are the smartest in the group then leave that group.

Jiangalie je are you the smartest and more knowledgeable and more successful katika kundi ulilopo la marafiki zako au watu wako wa karibu?

Leave!
Or you'll never grow.


II. WATU MNAOLINGANA AU KUFANANA UWEZO/MAISHA/MTAZAMO

Birds of a feather......! Walijisemea waingereza. And rightly so!

Hapa kuna shida zaidi. Hawa ni watu ambao mpo level sawa kimaisha. Kiufahamu. Etc. Hapa tunaita YOUR COMFORT ZONE. Hapa ni pagumu kutoka kuliko kundi la kwanza. Maana kundi la kwanza ni watu unaweza kusema tu "banae hawa wananitumia tu ngoja niondoke". Lakini kundi hili la watu unaolingana nao,, wote mna "ELIMU YA JUU", okay, wote mna "maisha flani hivi". Sijui unanielewa. Kama ni wanafunzi wote mnategemea mkopo in one way or another. Kama ni wajasiriamali wote mko mnafananafanana hata kama mnafanya vitu tofauti. Kwa kifupi you "speak the same language". Yani unafeel at home ukiwa around nao. Uko nyumbani. Hujisikii kama "intruder". Yani wewe jiangalie hapo ulipo ni watu gani ambao ni "washkaji zako" au "mashosti" wa toka long time. You kind of palled up with them long ago and you kind of don't see yourself moving ahead without them. Hao yani. Watu ambao wakikwambia "Aisee weekend wapi?" Majibu unayo? Watu ambao mnaiva siyo kwa sababu mnasaidiana kugrow ila kwa sababu mko level moja ya maisha. Hao watu ndiyo kitanzi cha wewe kutofikia KILELE CHA MAFANIKIO YAKO. I'm telling you. Huwezi tu kuamua kuwa busy na kucompromise muda wa wewe na wao. Mmekunywa wote bia toka enzi Merryland inavuma hapo ITV kisha mkahamia Break Point baadaye mkaenda Rose Garden nk. Mmetoka "mbali". Hao watu ambao uko nao comfortable  ni kikwazo cha wewe kukua. Sababu kiwango cha muda wako wanachotumia bila kuadd value yoyote ya maana ni kikubwa sana. Hawa watu kitu muhimu duniani kama APPOINTMENT mkipanga kisha ukachelewa hawawezi kukukaripia au "kukusema" ili uone umefanya mistake kubwa. No. Watakuuliza tu maswali ya kijinga "Umepita kwa mchepuko nini??" Coz hata appointment ikiwa ni ya jambo nyeti kabisa but aina ya watu hao ni watu wasio na character ya kukupush kuchukulia mambo serious. Kama unahisi hapo ulipo umepiga hatua basi jaribu kujitenga kidogo na comfort zone yako utashangaa utakavyokwenda mbali zaidi. Watu wengi huishia hapa katika maisha. Wako juu lakini wako kwenye kitu tunaita PLATEAU OF SUCCESS. Kweli kabisa anaonekana amefanikiwa lakini yuko kwenye plateaut. Kuna tofauti ya kupanda ili milima na nyanda za juu kusini na kupanda hadi Kibo ya Kilimanjaro. Ni Kibo tu ambayo dunia nzima itaona umepanda juu kweli kweli. Being the highest point kwa hapa Africa! See? Plateau Success itakufaa kwa sasa lakini siku ukija kugundua badala ya kwenda Nyanda za Juu Kusini ulitakiwa ujikakamue uende kwa Wachaga ukafike Kibo pia utagundua umepoteza muda mwingi sana wa thamani. I'm not trying to tell you kuishi bila marafiki. No I'm trying to tell you marafiki zako *WA KARIBU* wasiwe unaowazidi au mnaolingana tu. Jaribu kupunguza marafiki wa aina mbili katika circle yako ya watu wa karibu uanze kuongeza aina ya tatu ya marafiki.


III. WATU WANAOKUZIDI KWA VITU VINGI AU VYOTE

Kuingiza watu wa aina hii katika circle ya watu wako wa karibu inahitaji UJIKANE NAFSI kwanza. Na hili ndo humu. Kuwa na watu unaowazidi ndo wakawa your CONFIDANTS haihitaji kujikana inahitaji "ujinga" flani  hivi kichwani. Maana kama mipango yako ya ndani na siri zako nk unawashirikisha zaidi watu unaowazidi ambao hawana uwezo wa kucontribute chochote kufikia malengo yako kivile inahitaji uwe umejivika ujinga flani kwanza. Kuwafanya your comfort zone kuwa your CONFIDANTS pia haihitaji kujikana ni kama wajibu maana kila mtu tuko comfortable na mwenzake na hawa ndo huwa wanachomeana kwa wakubwa nk. But kuwa na u karibu na watu MNAOLINGANA haihitaji kujikana. Ila ukitaka katika watu wako wa karibu awemo Dewji unaonaje? Inabidi uifanyie kazi hiyo nafasi siyo? Why? Sababu watu waliofanikiwa huwa wako busy zaidi na mambo yaliyowafanya wafanikiwe. Kiukweli hawana sana muda na vitu kama matokeo ya mpira labda kama anataka kununua timu au ana timu tayari. Hawana muda sana kujua Lema anatoka lini ameonewa au la. Hicho  katika list ya vitu vilivyompa utajiri. Mtoto wa Diamond atapewa jina gani. Hilo halipiti kichwani mwake. Nadhani unaona tofauti sasa?

Ili huyu mtu awe kiongozi mwa watu wako wa karibu basi atakutest kwa vitu vidogo vidogo na kisha vikubwa nk. Anataka kujua unaweza kuaminiwa na information nyeti au uko fragile. Atakupa kitu umwekee umtunzie kisha atakwambia anakihitaji siku 10 baadaye then three days later atakwambia samahani Nina emergency kile kitu naomba umpelekee mtu fulani mahali fulani. Anatest je jibu lako litakuwa na "lakini"? Je utadeliver results au utampa excuses?
Imagine alipewa pesa Fulani ndogo tu labda laki akakuomba umwekee hadi siku 10 ndo ataihitaji na akakwambia sababu kwa nini hataki kukaa na hiyo pesa hapo anajua una shida ya pesa vibaya mno. Maskini unaenda kuitumia ukijua siku kumi kwanza mshahara utakuwa ushatoka afu anakupigia kesho yake tu kuwa inahitaji ka. Tena anakutumia SMS tu. Inahitajika mahali kuna mtu wa karibu nami ana shida muhimu. Akihisi tu response yako inaonyesha uliitumia basi mmeishana.

Mtu aliyefanikiwa atakupima kujua motive yako ya kutaka u karibu na yeye ni ipi? What's your "why"? And the WHY behind that "why"? Atajua tu. Nadhani unaona kwa nini matajiri na waliofanikiwa wanakuwa na marafiki wachache mno. Akiona una deserve attention yake atakuwa na ukaribu na wewe hata kama ni kwa mipaka lakini anajua wewe una DNA ya mafanikio na ya greatness. Ukuu. So utaongeza kitu kwake pia in the long run. Otherwise baki huko huko chini usijenivuta kurudi chini kuliko kwa thinking yako. Negative mind yako. Poverty mindset yako. Watu waliofanikiwa wanajali muda. So ukitaka kuwa na ukaribu naye jijengee tabia ya kukeep time na appointments bila VIJISABABU.

Kundi hili ukifanikiwa kuwa na mmoja tu akawa mtu wako wa karibu. Yani kuna vitu akipata a nakupigia simu tu from nowhere kukwambia "Aisee ulinambia unataka kufanya hivi na vile nimefikiria nikasema kwa nini usifanye hivi na hivi kwanza?" Hivi kama mtu aliyefanikiwa anaweza kuacha mambo yake akakupigia simu yeye mwenyewe kukupa mawazo yake unadhani ni bure? Si keshaona wewe ni "mwenzake" japo upo chini bado.

Hili kundi limewashinda wengi kuwa nalo karibu. But ndo kundi lenye majibu ya maswali yako mengi kama unataka kuifikia KIBO ya mafanikio yako pia!

Lakini kama umeridhika na level ya nyanda za juu kusini sawa endelea na mashosti na washkati. Eti my colleagues. Wasomi wana maneno! Haya bana.

Rafiki yangu Josiah Otege alionge akiiongelea juzi anaita LAW OF ASSOCIATION. Alifafanua vema sana umuhimu wa kuassociate na the right people.a kuna Dada mmoja anaitwa June Uronu  juzi juzitatehe 1 December mida ya saa moja na nusu usiku aliandika maneno yafuatayo kwenye ukuta wake wa Facebook: "NGUVU ZA MATAJIRI WOTE HAZIPO BENKI KWENYE ACCOUNT ZAO, ZIPO KWA WATU WALIOMO KWENYE MAISHA YAO YA KILA SIKU"

Akamalizia kusema: "UKIKUBALI KUZUNGUKWA NA WATU WAVIVU, WAZEMBE, WAMBEA NA WALEVI WA STAREHE WEWE UTAKUWA MASKINI HADI UZIKWE"

Powerful message!
Ndo maana nakumbuka mpaka siku na muda! Nilitamani kila mtu aisome ndo maana nimeireproduce hapa. Mdogo wangu mwingine anaitwa Elizabeth C Luzutta naye akasema "BE CAREFUL THE FRIENDS YOU CHOOSE, YOU WILL END UP LIKE THEM"

Hawa watu watatu wote niliowataja wameandika ujumbe unaoshabihiana kwq nyakati tofauti katika mazingira tofauti. Na Mimi nimeshare hayo makundi ili upate nyongeza ya vile wengine wlivyotangulia kusema. Hope itakusaidia kuangalia watu ulioruhusu kwenye circle yako ya urafiki. Nimejifunza kuwa lazima u-cut off baadhi ya mahusiano ili uende mbali. Imeleta shida kwangu lakini kwa sababu najua ninakokwenda kuna watu wala hawaelekei huko so why nikae nao tunajadili kuhusu kwenda wapi sasa wakati wenzangu wamefika? Nimefanya makosa mengi lakini KOSA kubwa nililolifanya muda mrefu ni AINA YA WATU niliokubali kuwa na u karibu nao.. Maana walinishepu nikawa kama wao. But not anymore!  I have set a new standard for ME. Na mimi natafuta marafiki wapya watakaoni challenge kukua na kufikia KIBO ya mafanikio aliyoniwekea Mungu mbele yangu. It's sad to lose some "friends" but kwenye kutimiza kusudi la kuumbwa kwako usiangalie sana feelings au inconvenience. Kofi Anan aliwahi kusema:/WHAT MATTERS IS NOT THE INCONVENIENCE, WHAT MATTERS IS DOING THE RIGHT THING".

Huwezi kwenda Mtwara halafu unaambatana na watu wanaenda Ukerewe! #InahitajiUjingaFlani hiyo au siyo.

Mwaka huu unapoisha angalia watu wako wa karibu ni wapi. Je unataka kuendeleza u rafiki wa karibu na watu gani?

UNAOWAZIDI?
Kwa sababu hawawezi kukuchallenge?
#InahitajiUjingaFlaniHivi

MNAOLINGANA?
Kwa sababu unajisikia nyumbani?
#InahitajiKuridhikaFlaniHivi

WANAOKUZIDI?
Kwa sababu watakuchallenge na kukufanya ujichunguze wewe binafsi na mienendo yako?
#InahitajiKujikanaFulaniHivi

So who are your friends?


Mwaka huu 2016 BILL GATES na WARREN BUFFET walisherehekea miaka 25 ya URAFIKI wakati wewe unasherehekea miaka mitano ya urafiki wa Facebook na huyo rafiki yako. Kuna siku mtakuwa mmekuwa marafiki kwa miaka 25 pia!  Swali ni je, Urafiki wenu utakuwa umekufanya ufikie ndoto zako au upoteze ndoto zako na maono yako na destiny yako? Siyo mpenzi sana wa mpira siku hizi kama miaka 8 iliyopita lakini nikimwangalia Cristiano Ronaldo ana aina fulani tu ya marafiki kwenye team yake. Wengine ni wafanyakazi wenzake tu. Lakini friends wa karibu very few. Na wote wanaperform vizuri..siyo wa Team B. Why? Coz birds of a feather...!
Role models wake ni high performers na confidants wake pia.
What about you?

20 years toka sasa utakuwa mtu mzima tu wa kutosha. Urafiki utachangia sana utakuwa mtu wa aina gani. Kataa friend request nyingine Facebook. Siyo sifa kufika limit ya watu 5000 Facebook afu kati yao una watu wasiozidi 10 tu ambao ndo wanakusaidia angalau kujitambua na kuwa bora zaidi ya jana. Why on earth have the 5000? Kama Yesu angeanza na watu 5000 na kisha akafika mwisho na kugundua kumbe alitakiwa aanze na 12 tu angekuwa ameDISCO. Lakini alijua.

Alikuwa na 12 tu na kati ya hao akawa na 3 tu wa karibu (Petro, Yakobo na Yohana) and kati ya hao akawa na 1 (Yohana) tu wa karibu zaidi.

Watu waliofanikiwa ndivyo walivyo..wanajua vizuri kuwa lazima kuwa na circle ndogo ya watu wa karibu. Ndo maana ukitaka wakuweke kwenye hiyo circle you've got to prove yourself worth!

Huwezi kuwa "mjanja" kuliko Yesu. Unataka uwe na urafiki na kila mtu. Aliyewaumba mwenyewe wengine hawataki urafiki naye. Wewe ndo utawaweza? My friend be careful. And good luck as you brace for 2017!


With lots of love,


Semper Fi,


Andrea G Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

WhatsApp Only:  +255788366511
Calls & SMS :       +255752366511
Blog:                      www.andreamuhozya.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni