Jumapili, 23 Oktoba 2016

AKILI YAKO ISIPOKAA SAWA MAFANIKIO HUTAYAONA


Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikichunguza maisha ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa. Lengo langu hasa ni kufikia mafanikio makubwa na kuwasaidia wengine wanaotaka kufanikiwa pia.

Nimejifunza vitu vingi kutoka kwa watu waliofanikiwa ambao niliweza kuonana nao ana kwa ana. Na hata wale ambao bado sijaweza kupata fursa ya kuwaona nimekwisha jifunza tayari mambo muhimu kutoka kwao.

Leo nataka niongee kitu ambacho watu wengi wanaotaka kufanikiwa hawajakijua bado. Na hivyo wanakwama kupiga hatua kimafanikio na mwisho wanajikuta wanakata tamaa ya kutafuta mafanikio tena.

Hiki kitu kinaitwa MINDSET. Yaani MTAZAMO. Yani ni kweli sikatai kabisa kuwa kufanikiwa kunahitaji vitu kadhaa muhimu. Najua na wewe unavijua na hata nikisema tuvitaje kwa pamoja unajua.
Vitu kama:

~ kufanya kazi kwa bidii sana (kujituma),
~ kuishi kwa kuweka malengo,
~ kuwa na hamasa yani kitu kinachokuhamasisha  au kukusukuma kufanya kazi malengo yako (motivation),
~ pia kuwa na coach, na mentor na role model wako ni muhimu sana kwa ajili ya inspiration
~ na vitu vya aina hiyo

Lakini nimekuja kufahamu kuwa kuna jambo la msingi sana ambalo ndo nataka nikushirikishe hapa ambalo usipolijua utahangaika sana kufikia mafanikio. Jambo hilo ni kwamba ili vitu vyote tulivyotaja hapo juu ili vizae matunda sahihi na kukuletea mafanikio inabidi uwe na kitu kimoja kwanza: AKILI ILIYOKAA SAWA au unaweza kuita MTAZAMO SAHIHI (THE RIGHT MINDSET)

Mazingira ambayo tumezaliwa na kutokea au kukulia yana nafasi kubwa sana ya kutujenga kimtazamo. Yani MTAZAMO wako kuhusu mafanikio jinsi ulivyo unachangiwa sana na mahali ulipokulia, watu waliokulea (wazazi, shule, kabisa/msikiti etc) toka ukiwa mdogo. Pia jamii iliyokuwa inakuzunguka ukiwa mdogo.
Halafu na watu wanaokuzunguka sasa.
Hao woote wanachangia sana kukufanya kujenga MTAZAMO ulionao kuhusu maisha na kuhusu mafanikio.

Kuna watu kutokana na mazingira niliyoyaeleza hapo juu wamejenga mtazamo kuwa hawawezi kufanikiwa kimaisha mpaka uwe mjini au uwe na degree au utoke familia bora au uende Ulaya au Marekani hata akizama baharini.
Hata kama ni kwenda kuosha vyombo. Yani bora akaoshe vyombo Dubai kuliko kuuza mitumba au kuanzisha mradi mdogo Tanzania. Wengine wameshajiona kama wanyama vichwani mwao bila kujua. Mwingine anajiona mbwa. Yani wewe unaongea naye unamwona ni binadamu kumbe mwenzio MTAZAMO wake anajiona kama mbwa. Hujawahi sikia mtu anasema "bora ningezaliwa MBWA Marekani?" Huyo mtazamo wake ni kuwa mbwa walioko Marekani wana mafanikio kuliko yeye. Kama na wewe huo ni mtazamo wako unapaswa kutubu mbele za Mungu haraka mno yani usijisumbue kutafuta mafanikio wakati ushamfanya Mungu ni mjinga kwa kukuumba binadamu. Tubu kwanza. Unaweza ukawa na bidii na ndoto kubwa na malengo lakini mtazamo wa kwamba mpaka uende Marekani ndo ufanikiwe siyo mtazamo sahihi kukufikisha katika mafanikio.

Kuna ambao mtazamo wao ni kuwa akioa binti aliyesoma au kama ni binti ana mtazamo akiolewa na mtu mwenye uwezo mzuri kifedha hapo yeye pia atafanikiwa. Hawa wa hivi hata umfundishe biashara vipi. Hata umhamasishe vipi kuwa anaweza bado yeye ànawaza kupata mjamaa mwenye nazo. Na hawa baadhi yao wanajikuta wanachezewa tu na kushushwa thamani wakidhani wamepata mtu sahihi kumbe wamekosea mno sababu ya kuwa na mtazamo huo. Anaweza akawa na bidii ya kazi lakini mtazamo huo siyo mtazamo sahihi ili ufikie mafanikio.

Kuna wenye mtazamo kuwa kwa kuwa UKAWA haikuchukua dola hawawezi kufanikiwa. Na kuna wanaodhani kwa kuwa CCM imekamata dola ndo watafanikiwa. Sikia kufanikiwa ni suala binafsi. Kuna watu wamefanikiwa Tanzania na kuna watu Marekani ni hohe hahe. Kuna watu wanaipenda UKAWA/CCM ambao hata siyo wanasiasa kabisa wamefanikiwa na kuna wanaoiopenda UKAWA/CCM ambao ni hohehahe. Tofauti siyo chama kipi anapenda. Tofauti ni kichwani kwako kuna mtazamo UPI kuhusu mafanikio. Hufanikiwi kwa sababu ya chama unachoshabikiaunachoshabikia

Kuna watu wana mtazamo kuwa ili ufanikiwe labda uwe na sapoti ya watu wa karibu. Utasikia mtu anasema "Sisi wabongo hatupendani ndo maana hatufanikiwi" kashajenga hiyo. Kuwa hawezi kufanikiwa kwa kuwa hawapendani. Au "yani mi nina ndugu wana uwezo ila hata kukupa sapoti yani utadhani hawanijui". Anadhani ndugu wakimpa sapoti ndo atafanikiwa. Ni kweli wote waliofanikiwa wanapendwa, au walipewa sapoti na ndugu? Ukijua story za waliofanikiwa utashangaa mno. Huo siyo mtazamo sahihi.

Wengine wanafikiri kufanikiwa ni bahati. Hawa ndo wanawaza kuvaa pete za bahati. Au kuangalia nyota zinasemaje kwenye gazeti. Kuna watu wamesoma nyota toka darasa la saba mpaka sasa wana miaka 40 maisha yameshaanza rasmi na bado mafanikio hayasomeki. Huo siyo mtazamo sahihi. Watu hawafanikiwi kwa sababu birthday yako mvua imenyesha na jua likawaka. Huo ni ushirikina. Na hata ukifanikiwa mafanikio yako yatakutesa mpaka either uyakatae ufe maskini au uteseke na kuishi na majoka ndani ya nyumba sijui kulala na majini makaburini sijui kuua wazazi au watoto na kuishi kwa moyo ulio na majuto mno na uchungu usiosemeka maisha yako yote hata kama kwa nje unatoa tabasamu na kuwaambia vijana wasikate tamaa watatoka kumbe wewe una joka chumbani.
Huo siyo mtazamo sahihi.

Kuna mitazamo mingi mno ambayo si sahihi. Na nimeanza kusaidia kutoa elimu kidogo kidogo kwa vijana wenzangu kupitia kwenye blog yangu www.andreamuhozya.blogspot.com kuhusu mambo mbali mbali lakini pia kwa njia ya WhatsApp.

Kama wewe pia unataka kufanikiwa na umefanya vitu mbali mbali kwa bidii lakini bado hujaona mwelekeo njoo tuongee kuhusu mambo ya mtazamo. Ni muhimu kuliko unavyoweza kufikiria. Usije ukapoteza muda mwingi mno kufanya kitu ambacho ungeweza kuwa umeshafanikiwa ila kuna mahali una mindset isiyo sahihi. Au usijepoteza muda kufanya kitu kisicho na faida bila kujua kwa sababu ya kufata mkumbo tu. Afu mwisho unajikuta mtu mzima na majukumu makubwa mengi hela huna unaanza kupata pressure miaka 40 tu. Njoo tushauriane mambo muhimu.

Usiijaze mind yako na picha chafu za kwenye mitandao na vitu vya kuchekeshachekesha tu huko WhatsApp. Mafanikio yanahitaji akili iliyo SAFI. Lazima uwe na the RIGHT MIND. Ilishe akili yako vitu muhimu vya kuifanya itafakari siyo ilale tu na kukaa bila kukua. Mfano makundi mengi ya WhatsApp yamekuwa na vitu vya kitoto kitoto tu. Na watu ndo wanafurahi. Picha za ajabu ajabu na habari za umbea na entertainment tu haziifanyi akili yako ndo ikue. Unahitaji vitu tofauti. Unahitaji MTAZAMO mpya. Kama kweli upo serious na mafanikio yako. Muda haukusubiri. October inayoyoma. Mwaka unaisha.. Umefanikiwa malengo mangapi so far? Be yourself. Kuwa wewe. Angalia maisha yako!

Karibu tuzungumze WhatsApp #o788-366511 au #o752366511


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni