Alhamisi, 13 Oktoba 2016

JAMBO LA TATU (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA TATU
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)


#TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 3.


3. JAMBO LA TATU:
AJIRA NI AINA MPYA YA UFUGAJI (EMPLOYMENT IS JUST A FORM OF DOMESTICATION)

Duniani hapa kuna watu wanafuga vitu vingi sana. Kuna watu wanafuga nywele, kuna watu wanafuga kucha, kuna watu wanafuga wanyama, nk. Na kuna watu wanafuga WATU.

Sasa katika kundi hili la watu wanaofuga watu si ulishasikia kuwa kuna watu wanafuga sijui majambazi, sijui wanafuga magaidi, sijui wanafuga nini. Point yangu hapa ni kuwa kumbe mtu anaweza kufugwa. Tena kwa RIDHAA yake. Na kwa yeye mwenyewe kutuma maombi ya kufugwa. Na akikubaliwa maombi yake anaweza kutoa hadi sadaka ya shukrani. Sasa kwa nini naeleza mambo haya ni kwa sababu naongelea vitu nilivyoobserve na kujifunza kwa muda mrefu vinavyosababisha watu walioajiriwa hata wakiwa na potential kubwa kiasi gani kichwani lakini anaishia katika maisha duni sana hasa uzeeni. Hawezi kamwe kupata uhuru wa kipato. Shida ni nini licha ya bidii kubwa na kujituma kwingi na elimu ndefu... Anhaa nikajifunza kuwa shida nyingine hapa ni hii ya kutojua kuwa na yeye ni MFUGO. Anafugwa. So wewe unadhani ni kipi kizuri kufuga: kuku au mtu? Anyway. Tuendelee.

Sasa ili ufuge kitu na kifugike lazima ukipe incentive. Kwa kuwa naongelea mifugo nitalazimika kutaja majina au aina za wanyama wanaofugwa. So naamini wasomaji wangu ni watu wazima wenye uwezo wa kuchambua na kuelewa kuwa hiyo ni mifano tu ili kufikisha ujumbe.

Sasa tuendelee. Yes. Ili ufuge kitu na kifugike lazima ukipe #incentive. Hata kama unafuga kucha lazima uzipe incentive ya kuendelea kubakia. Nywele pia. Lazima uzipeleke saluni, uzilishe vizuri, nk, nk. Kama unafuga wanyama kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku, bata, mbwa au paka lazima uwape incentive ili wawe na amani ya kuendelea kuwepo.

Ndivyo na ilivyo katika kufuga mtu.

Bahati mbaya haya mambo watu wengi hawayatilii maanani sana japokuwa yanagusa DESTINY zao. Future zao. Kesho zao. Ndoto zao. Hatma za maisha yao. Uzee wao. Wanachofurahia tu ni zile incentive za muda wanazopata for the time being. Wanasahau kuwa mfugo ni mfugo tu.

So tragic.

Unajua kuku hata afurahi vipi kupewa ulezi na vyote avipendavyo mwisho wake unajulikana. Ngombe wa maziwa hata aletewe majani mazuri kutoka vile viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au kutoka kokote kule kwenye rutuba zaidi ale ashibe afurahi bado destiny yake (as far as kufugwa kwake is concerned) ni KUPRODUCE MAZIWA kwa mfugajimfugaji

Sasa ni #hatari sana kwa huyu ng'ombe kuridhika na kuletewa majani mazuri na maji na kuoshwa na kusafishiwa banda lake akaridhika. Lakini kwa kuwa ni NG'OMBE hilo hatuna shida nalo.

Lakini sasa vipi ikiwa ni binadamu??

Akaridhika pia kuwekewa banda (office cubicle)
, na kuletewa lunch, na maji ya bure bure kwenye dispenser, na kuwekewa dawati, na computer na kuwekewa umeme, nk..? Na akasahau kuwa anapewa vitu hivyo kama incentive tu kidogo ili AKAMULIWE MAZIWA TENA YA KUTOSHA. Tena not once or twice. Ata-produce hayo MAZIWA mpaka siku yakiisha anaambiwa sasa umri wako umeenda unapaswa ukakae na familia uangalie mambo yako na wewe.
Can you imagine that?

Sasa nikuulize, tofauti ya huyu binadamu na yule ng'ombe ni ipi hasa? I mean, with due respect. Lakini waajiriwa wengi hawajioni hivyo. Wanadhani mwajiri wao ana shida na wao. Kumbe shida yake ni MAZIWA. Hawajui kwa nini siku wasipotoa maziwa ya kutosha kwa nini mwajiri anakuwa mkali. Wengi wao wako so brainwashed kiasi kwamba mwajiri akifoka hata kama sababu siyo za msingi wanakosa amani siku nzima. Hata wangekuwa wameshika dini vipi. Mindset.

Sikia my friend. Mindset yako ikikamatwa sawasawa utabadilishana ardhi yako na mtu anakupa kioo. Wazungu hawakututawala physically kwa sababu walikuwa na miili ya kutisha ila ni kwa sababu walijua kucheza na MINDSET tu. Na hata sasa wanatutawala kiuchumi kwa sababu wanajua sana hii kitu mindset. Wanajua kucheza na ufahamu! Africa is still fast asleep. Ndivyo na waajiri walivyo. Wanajua kucheza na mindset. We angalia kiongozi wa juu wa kampuni au shirika kubwa kabisa hapa kwetu ambalo nibla kimataifa tena awe mzungu labla akija kutoka huko Ulaya kulitembelea hilo shirika na akampongeza mwajiriwa yeyote na kumsifia na labda kumpa zawadi ya labda Tsh milioni moja kwa utendaji mzuri. Tena hiyo milioni yenyewe iwe katika dola. Afu mzungu ndiye aombe kupiga picha ya ukumbusho na huyo mbongo. Weee! Huyo mtu anaweza kufia kwenye hilo shirika au hiyo kampuni. Hata angekuwa na ndoto za kuanzisha biashara yake mwenyewe. Hatoki. Why? MINDSET. Hapo mzungu kacheza tu na mindset. Utatoa MAZIWA mengi mno tena hata bila kukamuliwa sana.

Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa kuna sayansi ya kupata nyama nzuri kutoka kwa ng'ombe wakati wa kumchinja. Nilishangaa. Au kupata MAZIWA bora kabla ya kumkamua. Kumbe SIYO suala tu la kumlisha vizuri. Akasema nchi za huko wanachofanya siku ya kumchinja ng'ombe wanamtreat vizuri hajawahi kuona. Yani wanampet pet na kumpa vitu vizuri mno. Yani mwili wake unakuwa very relaxed.  Ng'ombe mpaka anafika machinjioni haoni hata dalili ya kumtia hofu hata kidogo. Amerelax. Mwili uko vizuri. Na akasema ukimtreat ng'ombe vizuri mwili wake huwa unarelease kemikali fulani za muhimu kuifanya nyama yake iwe bora zaidi ukimchinja wakati huo akiwa katika hali ya kurelax! See?

Sasa akanambia ng'ombe akishakuwa amerelax kuna vitu bado vinampet pet huku anaogeshwa mgongoni "anafurahi" akiwa amewekwa sehemu ambayo hawezi kutikisika (yeye hajui)sababu yupo katika mazingira masafi kweli kweli hasikii harufu yoyote ya damu nk hapo ndo inashuswa the SHARPEST BLADE shingoni kwake. Yani hakuna nukta ya ng'ombe kuona kilichotokea. Unaambiwa hapo unapata the best meat.

Alooo! Nikashangaa. Huku kwetu ng'ombe hadi afike machinjioni ameshapigwa stiki kuliko zile alizolamba yule denti.. teh teh.. Ndo unakuta nyama ya ngombe ya leo leo lakini khaa! Kama ya jana. Anyway point hapo ng'ombe kadanganywa. Akadhani anapendwa sana. Kumbe loooh. Siku ya ng'ombe kupendwa sana ndiyo....malizia.

Sasa mazingira hayo hayo ndo huwazunguka waajiriwa wengi. Wanadhani wanapendwa. No. In a point of fact kinapendwa unachoproduce. Acha kuproduce uone. Utapewa majina mabaya hujapata kuona. Au akipatikana "ng'ombe" anayeweza kuzalisha MAZIWA mengi zaidi yako tena kwa muda mfupi utafanyiwa visa hadi utoke mwenyewe. Unabaki kusema "Namwachia Mungu". Unamwachia Mungu? Wakati unaletewa majani kwenye banda hukujua kuwa anayekupa hayo majani ana kitu anataka kwako?


So kwa ujumla wake mazingira hayo ya kufugwa hayawezi kumpa mwajiriwa yeyote uwezo wa kufikia UHURU WA KIPATO.

Angalia watu wote waliofikia uhuru wa kipato. Wanafugwa na mtu yeyote? Jibu ni hapana. Hayupo tajiri yeyote duniani ambaye KAAJIRIWA. Why not? Ni kwa sababu wanajua kuwa kuajiriwa is tantamount to kufugwa. Ni sawa tu na kufugwa. Yes. Unapewa kila kitu unachohitaji ili kumzalishia mtu mwingine anachohitaji yeye. Sasa nani kati yenu atakuwa na financial freedom siku moja? Think about it.

Ukiwaangalia waajiriwa wengi ambao wamegeuza ajira kuwa ndiyo DESTINY yao unaweza kuona kati yao kuna baadhi (ASHAKUM SI MATUSI) wameanza kubehave kama kuku, au bata, kondoo, mbuzi, ng'ombe nk. Afu mwingine kwa sababu anajiona katika mifugo wenzake yeye ndo mwenye mwili mwili mkubwa kama ng'ombe (ana cheo)
 anahisi yeye hawezi kuwa kama kuku. Anasahau kila mtu ana produce cha kwake. Mwingine mayai, mwingine MAZIWA. Na wote mwisho wao hawaujui kamwe.


Hilo ni jambo la kuzingatia sana kama wewe ni mwajiriwa ama wewe ni mwanafunzi unayesoma ili kupata ajira au ni graduate unalilia ajira. That's the future you're crying for. Nakushauri kaa chini angalia nini Mungu aliweka ndani yako kisha mwombe akusaidie jinsi ya kukitimiza. Vijana wengi wamekuwa so BRAINWASHED kuwa wanasoma ili wakaajiriwe. Na hii inaanza mbali. Nani analeta hii brainwashing kama siyo WAFUGAJI? Mind you ukipenda kufugwa ukafikiri umefika kwa sababu unahisi wewe ni jogoo (cheo) wengine ni kuku wa kawaida. Au kwa kuwa wewe banda lako linawaka taa 24/7 na misosi nje nje
wakati wengine wanalala banda lenye giza na msosi wanatafuta mwenyewe mara waliwe na mwewe mara wajifiche ukasahau kuwa wewe ni kuku tu wa kisasa wao wa kienyeji ila nyinyi nyote ni kuku tu basi kuna shida katika fahamu zako. Kwa kuwa wewe umeajiriwa UN mwingine kaajiriwa gereji unahisi uko vizuri eeh. Sawa.

Anyway..
Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa zote kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya tatu zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA.
Na bado zingine saba!
Endelea kuwa na mimi.


But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 3 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM.
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA NNE.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS and Calls: +255752366511
WhatsApp: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com (ndo hii)

Barikiwa!


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni