Jumatano, 26 Oktoba 2016

USIENDELEZE TATIZO KUWA SEHEMU YA SULUHISHO.

Habari za wakati huu..

Watu #wengi mno wamekulia katika maisha duni ya #kimaskini.  Wamezaliwa familia duni, kusomeshwa kwa tabu au kushindwa kwenda shule au kuishia "njiani". Kukosa mavazi, kukosa malazi, kukosa chakula, kifupi kukosa basic needs. Bill Gates anasema kama wewe pia umezaliwa katika familia maskini hilo siyo kosa lako. Ila ukifa maskini hilo ni kosa lako. Unasikia maneno hayo? So shida siyo utokako rafiki. Shida ni uendako. Where are you going?

Shida ni maamuzi yako hapo ulipo. Je, umechukua uamuzi wa kuendeleza mlolongo wa umaskini ama umedhamiria kukata huo mzizi wa umaskini na uanzishe mkondo wa mafanikio kuanzia kwako kwenda kwenye uzao wako ujao mbele yako? That's the issue.

Tatizo haliko kwa wazazi wako diwani wako au mbunge wako au Naibu Spika au Meya wa Manispaa tatizo lipo kwenye fikra zako na maamuzi yako.  Umeamua nini? Kulalamika au kuchukua hatua. Kusoma message kama hizi za kukupa tumaini jipya na mawazo mbadala au kushabikia comments za watu wanaotukanana na kudhalilishana kila siku mitandaoni? Yote hayo ni maamuzi.

Umeamua kujiendeleza kwa kujisomea vitabu vya namna ya kufanikiwa kama kina #Shigongo walivyofanya au umeamua kusoma link za blog za umbea na vitu vinavyoua uwezo wako wa kuwaza vema? Umeamua kusikiliza clip za kina Jim Rohn au Darren Hardy huko YouTube au wewe ni nyimbo za Justin Bieber au za Ali Kiba na Diamond? Yote ni maamuzi.

Umeamua kuandika malengo yako ya mwaka huu na ya miaka mitano ijayo kwenye notebook yako ili uwe na ramani binafsi ya maisha yako au wewe unajiendea tu kulingana na matukio ya kila siku kwenye mitandao. Yaani ukiamka tu hata huna malengo unaanzia Facebook kuona kuna habari gani mpya, kisha uende WhatsApp kujua kuna video gani imetumwa ya kuchekesha. Bila kujua kidogo kidogo umri unaenda kidogo kidogo unaendelea kuulea na kuukomaza umaskini ulioukuta katika familia.

Magroup ya WhatsApp yamegeuka kuwa source ya taarifa kichwani mwako badala ya kupata taarifa kwenye vitabu vya kukusaidia kujikwamua katika maisha na hata kuikwamua familia yako au badala ya kuangalia videos za watu wanaokuonyesha njia ya kupitia wewe unataka video za watu wanaokata viuno tu au clip za bungeni basi. Halafu ukimaliza kupoteza muda wa masaa sita mtandaoni kesho unalaumu serikali kwa kutokukukwamua kiuchumi. Are you serious?? Muda unaoutumia kusoma vitu visivyokuwa na tija na kufatilia mijadala mireefu iliyokupeleka mbele kimafanikio muda huo ungeutumia kujifunza vitu muhimu ungeweza kupiga hatua haraka na kuwa msaada kwa wenzako wengi ambao hawana mwelekeo bado. Lakini kwa kuwa umeshailevya akili yako na vitu visivyokupeleka popote nayo inakukumbusha kila siku kuendelea kuilisha vitu hivyo hivyo.

Uko addicted na vitu vya kuchekesha chekesha tu eti unajifariji kuwa unacheka uongeze siku. Nani alikudanganya siku zinaongezwa kwa kucheka? Unazidi kujaza kichwa chako vitu ambavyo siyo serious wakati tatizo ulilonalo la kuuondoa umaskini ni tatizo serious.  Yaani adui yuko serious kajipanga kukumaliza afu  wewe unamwendea kwa kuchekacheka. Muda unayoyoma na wewe unazidi kuendeleza gurudumu la umaskini ulioukuta nyumbani kwenu.. Kutunza muda wako kwa WIVU ndiyo uamuzi wa kwanza mkubwa unaopaswa kuuchukua ili upige hatua kuelekea mafanikio.

Watu wengi ni #wabobezi wa kupoteza muda.  🕣🕣Mungu aliumba 24hours tu kwa kila mtu. Jinsi unavyopoteza muda wako ndivyo unavyopoteza fursa muhimu mno.  Mfano. Kuna wakati utafika hutakuwa na nguvu ulizonazo leo za kufanya kazi nk. Utajutia sana muda wako wa sasa. Usiambatane na mtu anayepoteza muda wake kwani kama wake anaupoteza hataona shida kupoteza wa kwako. Muda unaenda sana rafiki.

Hushangai mtu anafikia kupata mtoto halafu hana pampers.🚼🚼 Yaani utadhani mtoto kashtukiza kuja. Ama utadhani wamekuja wote mzazi na mtoto duniani siku moja. Huoni ajabu? Hiyo ni kwa sababu hakujua kuwa pampers zilitakiwa kuandaliwa zamani.  Wakati alipokuwa anaupoteza muda. Linda muda wako.  Utajitenga na umaskini taratibu taratibu. Umaskini hauna kawaida ya kuwapata watu wanaotumia muda wao vema kwa manufaa. Nzi hufuata uchafu si vinginevyo. Umaskini vile vile hufuata watu wasiojua thamani ya muda. Umaskini ni kama ugonjwa wa kipindupindu. Ili uwe maskini lazima kuna kanuni za mafanikio uzivunje. Kipindupindu pia ni kanuni za afya tu umevunja. Usikubali kuendeleza umaskini kuutoa kwa wazazi na kuwarithisha watoto wako huo ugonjwa.  Hebu chukia. Kama unavyochukia kipindupindu (kama unakichukia that is, maana watu wengine hata hawajielewi kabisa). Umaskini si kitu cha kukumbatia. Ni ugonjwa unaochangia kuharibu misingi mingi ya kiroho, kifamilia na taifa kwa ujumla. Amua kuutimua maishani mwako. Na ndo nasema njia ya kwanza ni kujifunza kutumia muda wako vizuri. Tembelea www.andreamuhozya.blogspot.com kujifunza zaidi.

Njia nyingine ni kujifunza kuangalia fursa mbali mbali zinazokuzunguka. Unajua linapokuja suala la fursa watu wengi wanahitaji kufundishwa jinsi ya kujua kitu fulani ni fursa na kitu fulani ni fursa ya sasa na kingine ni fursa ya miaka ijayo. Si kila mtu anajua. Usipoangalia fursa zilizopo na zijazo utalaumu serikali mpaka siku unakufa. Ili kuuzimisha moto wa umaskini unaotafuna jamii yako na familia yako inabidi ujifunze kutambua na kutumia fursa zilizopo mbele yako na uzifanyie kazi.

Umaskini hauna kawaida ya kuogopa mshahara wako. Utapata mishahara kila mwezi kwa miaka 20 - 40 hadi ustaafu na umaskini utakuwa bado ni sehemu ya maisha yako.  Why? Kwa sababu mshahara ni ujira kidogo tu wa kumwezesha mfanyakazi asije kazini uchi wala asije kwa miguu wala asije kazini akiwa na njaa. Basi.  Mshahara si njia ya kuuondoa umaskini. Ndiyo maana watu wengi walioajiriwa bado ni maskini. Umaskini hauogopi mshahara
. Ni ugonjwa mbaya na mgumu dozi ya mshahara haisaidii.  Ni sawa na kutaka kumaliza malaria sugu kwa panadol. Lazima utafute FURSA za kukusaidia kujikwamua hapo ulipo.  Fursa zipo nyingi mno. Ni lazima ujue pia fursa ipi inafaa katika mazingira yako. Usije ukawa kama mimi kabla sijajua vema mambo haya nilikuwa nauza vitu mahali ambapo hakuna wateja wa vitu vya aina ile. Usicheke.  Sikuwa na maarifa. Now ninayo ndo nakumegea na wewe. So ni hivi:

~ Tumia muda wako kutafuta fursa zilizopo.

~ Tumia muda wako kuzielewa hizo fursa vizuri.

~ Tumia muda wako vizuri kuzitofautisha hizo fursa.

~ Na tumia muda wako kufanyia kazi fursa uliyoamua kuituma kuutokomeza umaskini kutoka kwenye familia yako.

Kwa matumizi hayo ya muda sioni kama utahitaji Bunge liwe LIVE kwanza au sioni kama utakuwa na muda wa kulalamikia serikali kuhusu umaskini wako na familia yako. Ifike mahali ukubali kuwa jukumu la kujikwamua kutoka katika umaskini ni LA KWAKO mwenyewe.  Siku ukijivika hilo jukumu ndo siku utakayokuwa umeanza kuwa mtu mzima kiukweli ukweli. Mtu yeyote ambaye anataka au kutamani kukwamuliwa kutoka umaskini bado hajakuwa vizuri.  Simaanishi kuwa usiombe msaada.  La hasha. Kila mtu huhitaji msaada. ILA kuna watu wanataka mtu mwingine aje awasaidie kuishi maisha yao hapa duniani afu wajikute wamefanikiwa.  That's never going to happen. Wake up! Tumia muda tafuta fursa.  Ziko nyingi. Nenda semina mbali mbali ujifunze.

Kama unawaza kujikwamua kimaisha ila hujui wapi uanzie au unatatanishwa na fursa unazoziona au una hofu ya kujaribu basi wasiliana nasi kwa WhatsApp #o788366511 #o752366511 tushauriane.  Usikubali kurithi umaskini na kuwarithisha watoto wako.


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni