Jumatano, 12 Oktoba 2016

JAMBO LA PILI (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA UWEZO MWAJIRIWA YEYOTE KUTOWEZA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA PILI
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA UWEZO MWAJIRIWA YEYOTE KUTOWEZA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)


TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato). Naamini u mzima na kwenye afya bora.

Ambatana nami tena kidogo hapa...


2. JAMBO LA PILI:
AJIRA HUMPA MTU UZOEFU FINYU (LIMITED EXPERIENCE)

Nimekuwa nikizungumza na waajiriwa wengi (hasa wale ambao ninawaona kuwa wana potential kubwa sana ya kufanya mambo makubwa hapa duniani) na nimekuwa nikiwa-challenge kuhusu kuchukua hatua na kuanza kutendea kazi ndoto zao. Wengi wao huniambia tu "Of course mi nimeajiriwa kupata tu experience (uzoefu) kisha nitaenda kufanya mambo yangu". Na hata wanafunzi wa vyuo ambao nimekuwa nikiongea nao kuhusu kutotegemea ajira tu wamekuwa wakiniambia wanataka kuajiriwa kwanza wapate uzoefu na mtaji (hapa huwa najichekea kimoyomoyo) kisha waende wakafanye mambo yao.

Sasa ukitazama watu wote waliofikia kuwa na UHURU WA KIPATO yani uwezo wa kufanya chochote anachotaka kinachohitaji pesa, wote wana kitu kingine in common. Wana EXPERIENCE ya mambo mengi sana na ukibahatika kukaa nao unaweza kushangaa sana na ndo utafahamu kumbe hawajafanikiwa kwa bahati mbaya.
Lakini mtu ukiwa mwajiriwa hilo ni jambo gumu kuwa nalo (kupata uzoefu mpana). Labda nitoe mifano kidogo.

Ukikaa na mtu aliyefanikiwa sana kifedha unaweza kuanza kujiukiza amejuaje kuhusu mambo ya kitaalamu kama haya huyu mtu? We elewa tu. Imemchukua miaka mingi ya kujaribu vitu tofauti tofauti na kupata huo uzoefu. Tofauti na mtu aliyeajiriwa.

Mfano:
Mtu umeajiriwa MAPOKEZI.
Uzoefu wa kazi ya mapokezi ni pamoja na:
kupokea simu,
kupokea wageni,
kuwaongoza wageni pa kuelekea,
kuwaitia wageni wenyeji wao,
kuchora mistari kwenye daftari la wageni ili waweze kusaini,
kuwapa watu funguo kwenda vyumbani kama ni hotelini,
kupokea barua za field au za watu wanaokuja kuomba kazi kama ni mapokezi kampuni,
na vitu vya aina hiyo.

Now that is a very limited experience kwa mtu anayetaka kufikia uhuru wa kipato. Uhuru wa kipato hauji kwa mtu ambaye kitu ambacho ana uzoefu nacho ni kupokea wageni tu vitu na vya aina hiyo. Yani hajui chochote kuhusu:

~ kutafuta masoko (wateja). Maana yake huyu hajui pesa inakujaje?
~ kutunza fedha na mahesabu
~ kubuni bidhaa mpya au huduma mpya za kuwapa wateja siku zijazo
~  Utatuzi wa migogoro ya wafanyakazi unafanyikaje hajui
~ Hajui IT wanafanyaga nini huko nyuma hana idea angalau kidogo tu ya kawaida ikamsaidie kujua siku akitaka kufanya "mambo yake mwenyewe"
~ Nk.

Kama ni mhasibu wa kampuni au mwanasheria wa kampuni hajui chochote zaidi ya kutunza fedha au kusimamia kesi. See? Very limited.

Sasa basi kwa kuwa kipato chake kinatokana na uzoefu huo finyu ndo maana siyo rahisi kwake kukua zaidi kifedha. Ili kukua kifedha inabidi uwe na ufahamu na UZOEFU MPANA wa mambo yanayohusiana na fedha ikiwemo kupokea wageni kutangaza bidhaa au huduma zako, kutatua migogoro, kutafuta wateja, kutunza fedha, nk, nk.

Sasa simaanishi kuwa wewe ndo uvifanye hivyo vitu kila siku hapana. Namaanisha uwe na uzoefu navyo hata kama uliwahi kufanya kwa mwezi mmoja ukaacha au kwa wiki moja kujifunza tu au kwa mwaka, nk. Kama kweli unataka kufikia uhuru wa kipato badaye kama sasa hivi wewe ni mwajiriwa basi amua hata kujitolea BURE kwa muda wako wa ziada kufanya kazi kwa mtu hata for free ambayo ni tofauti na ile unayoifanyia kule ulikoajiriwa. Fanya tu. This is an INVALUABLE advice I'm giving you right here. Trust me. Utajifunza vitu vingi kudeal na watu wapya katika eneo ambalo siyo COMFORT ZONE yako kazini. Mfano wewe ni IT personnel kazini kwako. Omba kwa mtu binafsi uwe unasaidiana na reception wake kupokea wageni, nk. Ni kama kitu cha kijinga we. But do it. Mwambie just one month. Or one week. Kinachotafutwa ni wewe kupata uzoefu angalau kidogo lakini wa mambo mengi. Of course ukiweza kupata uzoefu huo tofauti kwa muda mrefu zaidi utajua mambo mengi.

Sasa siku ukija kuanzisha biashara yako unakuwa una idea kuhusu wageni, una idea kuhusu fedha, masoko, IT. Hufanyi wewe, umeajiri watu na wala hujui terminologies za Marketing kama wao lakini YOU HAVE AN IDEA WHAT THEY ARE SUPPOSED TO DO. Hakuna tajiri mbumbumbu kwa taarifa yako. Hata kama hajaenda shule. Usifikiri shule ndo kipimo cha ufahamu. Kuna watu wana Masters ya Biashara na wanachokijua ni terminologies tu na Theories lakini kuna mtu anauza mahindi Iringa hata mlango wa darasa la saba hakubahatika kuusogelea ila anafahamu kuhusu mbegu bora, msimu bora, wateja wakoje na jinsi ya kudeal nao, usafirishaji upoje, serikali ikibana hela ufanyeje, pombe za kienyeji zinazotumia mahindi zina effect gani kwenye bei ya mahindi, ufanyeje ili upate masoko ya mbali, ufanyeje mteja anapokuja unampokeaje, unamkaribishaje, ufanyeje ukipeleka hela benki hata kama hujui kuandika wala kuweka sahihi unachoweza ni dole gumba tu ila una milioni 100. See? Sasa wewe kafanye hiyo biashara na Masters yako wakati unachokijua kwa uzoefu wa ajira ni kuandika ripoti yenye terminologies nzuri nzuri na kiingereza chako cha Babbrojohasen sijui ile babra nini. Utashangaa utajikuta unaangukia pua na unalazimika kuanza moja kabisa licha ya elimu uliyonayo kwa kuwa una LIMITED EXPERIENCE. Na ndo maana waajiriwa wengi wanashangaa mtu akiwa anafanya biashara na bado hajawa milionea toka ameanza. Wanamcheka. Hawajui yupo kwenye mchakato wa kupata huo uzoefu. Wao wanataka wakianza biashara iwe level sawa na pale kazini alipoajiriwa. Thubutu. Muulize mwajiri wako. You must gain vast experience first..

Sasa UZOEFU huwa unakuja kidogo kidogo kwa muda mrefu. Ndo maana matajiri wengi utasikia kaanza "ZAMANI". Alianza anauza sijui mihogo. Uzoefu. Alianza anauza maandazi. Uzoefu. Mwingine utasikia alianza anasafirisha mizigo ya watu kwa baiskeli. Uzoefu. Kuna huyu jamaa mmiliki wa Peacock Hotel ambaye anasema alianza kwa kuuza karanga. Uzoefu.!! Joseph Kusaga wakati ameanza si alikuwa anapigisha muziki tu kwenye kumbi za Starehe? Leo hii Clouds Media ni media house ya maana. Na tena wakati anaenda kusajili jina la redio yake watu wakawa wanacheka eti MAWINGU (CLOUDS) FM. Yaani mawingu. Wanamwona wa ajabu.  Uzoefu. Ana uzoefu wa kuchekwa pia.  Waajiriwa wengi wanataka utajiri uje tu ghafla. Anadhani kwa kuwa amefanya kazi benki miaka mingi na yeye ataanzisha benki tu ghafla. Anasahau kuwa hapo malipo sasa ameajiriwa kuhesabu pesa za watu tu na kugonga mihuri. Limited experience. Hajui hizo pesa zinakujaje? Hajui zinapelekwaga wapi? Hata mihuri hajui inatokaga wapi na ni sh ngapi na kwa nini? Anachojua kunyanyua muhuri na kukandamiza kwenye karatasi. Hajui kwa nini wateja wanakuwa wengi au siku zingine wachache. Anafurahi kupewa tips za elfu 20 au hata dola 100 na mapedeshee wanaokuja kuleta hela. Anasahau hana experience kama wao. Anabaki kusema wanauza unga. Yani kila MTU mwenyewe hela nyingi ni Unga au Freemason.. Akili za kichawi kichawi tu kichwani. Na mawazo finyu.

Waajiriwa wengi ni watu VEEERY POTENTIAL kubadilisha hata Uchumi wa nchi au dunia. Lakini shida wamekubali kuishi kwa LIMITED EXPERIENCE.  Na wanamwamini Mungu kuwa IPO siku na wao watakuwa na uhuru wa kipato. Sikia my friend. Biblia inasema hata shetani anaamini Mungu na kutetemeka. But Mungu ni Mungu wa KANUNI. Mtafute MTU anaitwa MGISA MTEBE anaweza kukufafanulia zaidi hili la Mungu wa kanuni ndo utajua kwa nini wapagani wanafanikiwa na kwenye dini zao na Mungu wao wapo macho kodo!


Anyway..
Kama ulisoma makala yangu ya jana iliyoelezea kuwa limiting factor ya kwanza kwa nini mwajiriwa hawezi akafikia Uhuru wa kipato ni kwamba kupata pesa you must show up. Then unganisha ni hii ya pili kuwa you will show up but you end up with limited experience. Utaanza kuona kuwa zote mbili zinafanya kazi against you.
Na bado zingine nane!
Endelea kuwa na mimi.


But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha pili cha kumzuia Mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM.
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA TATU.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS and Calls: +255752366511
WhatsApp: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com (ndo hii)

Barikiwa!


Semper Fi,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni