Ijumaa, 14 Oktoba 2016

JAMBO LA NNE (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA NNE
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)


TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 4.


4. JAMBO LA NNE:
MSHAHARA NI PATO LENYE MAKATO MENGI NA KODI KULIKO MAPATO MENGINE YOYOTE (A SALARY IS THE MOST TAXABLE INCOME)


So, how's Nyerere Day my peoplezzz???

I hope iko vizuri. Basi kwangu pia iko vizuri. Hii picha inanikumbusha utotoni. Ilikuwa sebuleni enzi hizo hata sijui Mwalimu Nyerere ndo nani.
Anyway tuachane na picha.


Ila leo nina swali kidogo?
Hivi ni nani aliyebuni mifumo hii ya kodi tuliyo nayo leo?

Aah basi ngoja tu niende straight.

Ni hivi. Ni vigumu kwa mwajiriwa kufikia uhuru wa kipato kwa sababu kitu kinachoitwa mshahara kinaliwa na midomo mingi mno. Mshahara unaliwa na midomo lukuki kabla "mabaki" hayajakufikia wewe. Sijui unanielewa? Unachokipata ni MABAKI ya kitu unachozalisha. Yani kama unazalisha 100% basi ukipata saaaanaaaaaa ni 20%. Otherwise utapata 15% au in most cases 10% ya kitu unachozalisha. Sasa kama unafurahia 10% ya kitu unachozalisha na una elimu ndefu ya kusoma digrii na KUFANYA masters basi kuna shida fulani mahali fulani. Hii ndiyo sababu nyingine kwa nini mwajiriwa yeyote amebanwa. Ulishawahi kuishi "uswazi"? Hahaaa yani uswazi ukimfata mtu ukafikiri hiyo anayopita ni njia inaendelea mbele unashangaa inaishia nyumbani kwake. Khaa! Au chooni kwa mtu. Huamini? We wa kishua ee? Haya ngoja nikupe mfano wa kishuashua basi. We si unajua barabarani kuna alama za barabarani. Kuna njia zingine ukienda unakutana na kibao kinasema: HAKUNA NJIA! Umenielewa sasa? Ndo hivyo na kwa mwajiriwa. Njia ya kuelekea mtaa unaoitwa "UHURU WA KIPATO" ukitokea mtaa wa KUAJIRIWA unakutana na alama ya NO ENTRY. Hapo unageuza tu njia unarudi ulikotoka.
Sijui unanielewa??

Nimetafakari kwa muda na kujifunza mambo haya kwa kina. Ni kwamba watu walio design TAX SYSTEM yani mifumo ya kodi duniani hawakuwa maskini bali "wenye nazo". Sasa unadhani walidesign mfumo wa kodi umnufaishe nani kati ya maskini na tajiri?
Kati ya mwajiriwa na mwajiri?

Ngoja nikupe mfano:
Mwaka jana ulifanyika utafiti nchini Marekani wa jinsi matajiri na maskini wanavyolipa kodi. Ilidhihirika kwamba 20% ya Wamarekani (ambao hawa ni watu wa kipato cha chini) hulipa kodi  10.9% ya mapato yao.
Halafu kundi la watu wa kipato cha kati (yaani Middle Class People) wanalipa 9.4% ya kipato chao kama kodi.
Lakini the top 1% ya Wamarekani (hawa ni matajiri) wanalipa only 5.4% ya mapato yao kama kodi.


Sasa hii iko duniani kote generally. Kwamba mfumo wa kodi uko UPSIDE-DOWN. Aliyetakiwa kulipa kodi kidogo ndo analipa sana. Anayetakiwa kulipa nyingi analipa kidogo. Na hii in a way unakuta ina mantic yake. Yani kwamba asilimia 5.4 ya kodi ya mapato ya Bill Gates ni kiasi gani? Nyingi si ndiyo. Kwa hiyo ili usimvunje moyo wa kuongeza ajira nk bora ukubali hiyo halafu kodi nyingine utawakata wafanyakazi wake kidogo kidogo. Ila hiyo kidogo kidogo ni nyingi mno kwa huyo mwajiriwa. Lakini sasa ufanyeje. Ndo waajiriwa hawana pa kutokea.

Na bahati mbaya kuna misamaha ya kodi kisheria kabisa kwa matajiri na wawekezaji. Hujawahi kusikia? Of course umewahi! Lakini kwa waajiriwa HAINAGA USHEMEJI WANAKATAGA. Nani akusamehe kodi? Thubutu!!

Sasa usipokuwa na maarifa ya hivi vitu utaendelea kudai mshahara uongezeke kumbe hakuna cha maana unachodai. Unaoperate katika mfumo ulio kinyume chako already. Afu unafunga na kuomba Mungu akusaidie uongezwe mshahara. Yani ni sawa na mtoto wa shule kulilia kuwa class monitor au monitress. Hiyo haikufanyi ufaulu mitihani zaidi ya wenzako. Mfumo wa kufaulu ni ule ule. Mama Ndalichako hajuagi huyu alikuwa head boy au head girl. Anachoangalia ni maksi tu. Sasa kulilia kupanda cheo mara ukafanye mastaz ya watu unaisumbua tu kisa unataka kupanda cheo kumbe unajilisha upepo tu.

Tazama mfano huu:

Tarehe 1 mwezi Mei (Mei Mosi) ambayo siku hizi imegeuka na kuwa siku ya WAAJIRIWA badala ya siku ya WAFANYAKAZI. Waajiriwa wameiteka. Hahaaaa. Undava undava.

Anyway. Tarehe 1.5.2016 (mwaka huu) Rais wetu mpendwa Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli alitangaza kuwa MAKATO yanayojulikana kama PAY AS YOU EARN (PAYE) yatashushwa kutoka 11% hadi 9%. Basi ukipenda katafute clip jinsi wafanyakazi, I mean sorry, WAAJIRIWA jinsi walivyoshangilia. Utafikiri sasa unafuu wa maisha umewadia. Yani kama yale maisha bora ya Mhe. JK sasa yamewasili. Lakini je ni kweli?

Tazama hapa kidogo:
Kwa kawaida kwa sasa mshahara chini ya TZS 170,000/- hauna makato. And you can tell why? Sasa huyo si kwamba serikali haitaki kumkata. No. Inataka ila sasa ifanyeje huyu mtu naye aishi. Angalau nauli na hela ya kula asikose.

Lakini kiuhalisia ukichunguza kiundani kwa jicho fulani hivi la mbali utagundua kama makato yake atayabeba mtu mwingine. Sijajuaga ni nani ila huwa nahisi hivyo eti.

Anyway. Tuendelee. Mshahara wa kuanzia TZS 170,000/- hadi 360,000/- ambao ndo ulikuwa ukikatwa PAYE ya 11% ndo Mhe Rais alitangaza kuwa itapungua hadi 9%.

Narudia si kwamba serikali haitaki pesa. Inataka. Lakini kuna mahali kwingine inakuwa inakata kureplace hicho ilichoki-relinguish! Think my friend. It's still LEGAL to think.

Haya mshahara wa kuanzia TZS 360,000/- hadi 540,000/- utakatwa PAYE hiyo mpya lakini hapa kuna Excess Charge ya 20%!!!!! Mayooooooo!
Na mshahara wa TZS 540,000/- na kuendelea una hiyo PAYE na Excess Charge ya 25%!!!!!!

Sijui unaelewa? Sasa umepunguziwa 11% to 9% ya PAYE but mshahara wako una Excess Charge of that magnitude. 
Tuendelee kidogo. Ukiachilia hayo but pia kwa kuwa "huwezi kujitunza uzeeni wewe mwenyewe" basi unalazimishwa kutunziwa pesa zako kama SOCIAL SECURUTY FUNDS.
Makato mengine hayo.
Ulisoma Chuo? Mkopo wa watu umelipa?
Makato mengine hayo.
Makato lukukiii..
Ndo maana siku zile wakabaki wameshika mabango SHEMEJI UNATUACHAJE? Heee! Sasa sijui huyu wa sasa akitoka wataulizaje? Sikia rafiki.. Mfumo wa ajira haunaga USHEMEJI ndugu. 


Kumbuka hakuna maduka ya waajiriwa na wafanyabiashara. Au unadhani siku ukistaafu utakuwa unanunua sukari duka tofauti. Duka la wastaafu.

Sasa ukizingatia makato hayo yote hapo juu na ukija kufikiria kuwa wewe ndo unayezalisha pesa ya umeme, maji, kodi ya jengo ili mwajiri wako amudu vyote hivyo. Na wewe ndo unazalisha FAIDA ya shareholders kama upo kwenye corporate setup. Utaelewa kwa nini wewe ni kama punda fulani hivi ambaye watu husema bora punda afe mzigo ufanyeje.....?
Watu wana maneno!

Sasa Mungu akufanyeje? Akubebe! Jifunze kutumia mfumo mwingine ili ufike mtaa wa  uhuru wa kipato! It's that simple.
Even if it's not easy.

Nadhani unanielewa. Ndiyo maana leo NYERERE DAY 2016 nikakumbuka kumbe wakati Mwalimu anaaga dunia nilikuwa nina mwaka mmoja toka kuja jijini hili la "Darisalama" (kwa sauti ya Paul Makonda). Ni wakuja mimi mwenzenu.. hahaaa. Nikawaza kuwa kumbe wakati Mwalimu anaaga dunia kuna watu walikuwa ndo wamepata ajira zao za kwanza walitoka kibaruani siku ile tukakimbia nao kuelekea Msasani wakati huo mi hata msasani sijui ni wapi wakuja miye. Natiririka tu. Anyway.Ukipiga mahesabu mpaka sasa ni 17 years right? Lakini kumbe kuna watu wakati Mwalimu anaaga dunia walikuwa kwenye ajira kwa miaka 8 tayari au zaidi. Means mpaka hivi leo wana "kajubilei" fulani hivi ka kudumu kwenye mfumo wa AJIRA kwa miaka 25!!! Watu hao ambao wamedumu kwenye ajira tofauti tofauti wakiishi kwa kutegemea ajira kama MAIN SOURCE ya kipato chao mpaka sasa ukiwatizama HAWANA dalili yoyote ya kuwa wanaelekea kufikia ule mtaa wa UHURU wa kipato.

Kama wewe ni mwajiriwa jiulize uko mbali kiasi gani kufikia "kajubilei kako" ka miaka 25 ya ajira. Na ukifika huko utakuwa umesogea kiasi gani kufikia financial freedom. Wengi husema  aah mimi siwezi kuajiriwa miaka 25 wewe. Kuna mtu anasema: Mimi siyo "bw*ge" mimi. Mi ntaajiriwa miaka hii???" Hapo anaonyesha vile vidole vya Chadema. I tell you kuna watu nakutana nao wanasema hivyo. Utashangaa anakata miaka minne, mitano, sita, anahamia kampuni X anakata mwaka mmoja huko ukikutana naye anakwambia "Saivi NAFANYA Masters!" Afu hivi masters huwa "INAFANYWAJE" hata sijui. Akirudi na Masters yake mshahara unapanda kidooogo labda imeongezeka laki mbili hapo juu. Anakutana na EXCESS CHARGE.

Na akitaka kuacha kazi anaambiwa SOCIAL SECURITY FUNDS unaweza ukapata ukifika miaka 55. Anakuwa "MPOULEY".


Anyway.. Leo nisikuchoshe na maneno mengi. Usije kuchelewa kwenda kula batazzzzz...

But bottomline is...
Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa zote kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 4 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Don't read them in isolation.

Na bado zingine 6.
Endelea kuwa na mimi.


But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 4 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA TANO.


Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!


Semper Fidelis,


Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni