Jumatatu, 17 Oktoba 2016

JAMBO LA SABA (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA SABA
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 7.

7. JAMBO LA SABA: ONGEZEKO LA KIPATO CHAKO NI HADI UOMBE AU MWAJIRI APENDE.. (BEING UNDER A MASTER a.k.a. BOSS)

Nianze leo kwa kusema kama umeajiriwa na unasoma hii makala yangu ya leo na huna NDOTO ya kufikia kuwa na uhuru wa kipato nakushauri usitilie maanani sana wala mawazo haya usiyajali sana maana huenda utaona hayaingii akilini. Na kiukweli nakushauri hata usiendelee zaidi kusoma. Lakini kama unatamani kufikia level siku moja uwe huna changamoto ya fedha tena then nakuomba tuendelee pamoja.

So.....

Changamoto nyingine niliyoiona katika kujifunza kwangu inayomkwamisha mwajiriwa yeyote kufikia uhuru wa kipato ni kwamba hana uwezo wa kuongeza kipato chake wakati wowote anaotaka bali hilo jambo linategemea aidha AOMBE kuongezewa kipato (au hata kubembeleza kwa baadhi ya waajiriwa) AMA hata kama hajaomba basi itokee MWAJIRI wake (au bosi) apende au kuamua kukuongezea kipato.

Sasa siko hapa kumsifia mtu aliyejiajiri lakini katika hili mtu aliyejiajiri anaweza kuamua kesho wapate pesa zaidi. Yes. Akaamua tu kuwa kesho ataanza kazi zake SAA 11 alfajiri. Na atakunywa chai tu na atafunga kazi zake saa nne usiku. Huyu yuko likely kuongeza kipato hiyo kesho. Na akiamua keshokutwa pia kiongezeke hilo hasa liko mikononi mwake.
Lakini kwa mtu aliyeajiriwa kuongeza kipato (mshahara) ni MCHAKATO ambao yeye hana control nao kivile. Yes. Maana unaweza kuwa umeajiriwa ukafanya kazi alfajiri hadi usiku afu kumbe bosi wako akahisi unataka uchukue cheo chake. Atakupiga vita hadi basi. Inaweza shida isiwe bosi wewe ukapiga kazi kweli kweli lakini nyinyi kama ofisi in general hamjazalisha kwa kiwango MWAJIRI alichotaka. Na inawezekana mmezalisha alichotaka ila hamuwezi kumlazimisha awapandishe mishahara wakati anawalipa kwa viwango halali vya serikali. Kwa hiyo unaweza kukaa na kipato FLAT (mfano milioni 1 kwa mwezi) kwa miaka miwili mfululizo au hata mitano. Unapiga kazi kubwa lakini kipato kipo FLAT sababu kuongezeka mshahara ni mchakato usio na control nao.

Kuna ambao ajira zao zina vigezo vya kuongezeka mshahara. Mfano ukienda kuongeza elimu ndo kipato kinaongezeka.  So haijalishi sana umefanya kazi vipi bila elimu. Sasa hapo kuna nyakati inategenea pia huyo mwanadamu atakayekuwa anakufundisha huko chuoni ukitofautiana naye unaweza uka"DISCO" na hilo ongezeko la mshahara likaota mbawa. Na ndo maana waajiriwa wengi wanaosoma sijui kufanya hizo Masters za kupandisha mishahara hata hawasomi kuongeza weledi bali lengo ni mshahara upande. Unakuwa mtumwa wa elimu. Sasa unataka kuongeza kipato kwa wrong formula. Formula sahihi ya kuongeza kipato ni either kuongeza significance ya huduma unayotoa au kuongeza idadi ya matatizo unayotatua. That's why kuna watu hawajasoma kivile na wanaongezeka kipato kila wakati. Lakini sasa kwa sababu mfumo uliopo ni AJIRA basi the right formula doesn't necessarily apply. Ukiwa BANK TELLER ukaongeza ubora wa huduma unayoitoa utaishia kuwa EMPLOYEE OF THE MONTH (which is encouraging by the way) lakini huwezi kuongezeka kipato kwa sababu umepiga kazi kama punda kwa mwezi mzima. No. Mshahara wako kama ni laki tano ndiyo utaikuta kwenye ATM hapo nje. Si ndo ulisaini mwenyewe kwenye contract.

Which brings us to another issue. Kwamba thamani yako kifedha kama MWAJIRIWA (your monetary value as an employee) haiko kwenye ubora wa kazi zako bali kwenye what you NEGOTIATED from the start. Sasa shida ni kuwa kwa waajiriwa wengi unapoomba kazi hauko katika position strong ya negotiation. Unakuta mtu anataka tu kazi. Haangalii WORTH yake. Anaogopa akiikosa hiyo atakaa nyumbani mpaka lini. Watu wengi wanapenda kuishi kwa KUPIGA SHIDA SINDANO YA GANZI. Immediate relief. Short-term comfort. Not long term financial growth. Haangalii kama kuna possibility ya kipato chake anachoanza nacho kukua baadaye.
Worse, haangalii kama endapo kitakua kitakua kwa kuzingatia thamani halisi ya contribution yake kama individual. Ganzi ikiisha inakuwa shida mara mbili. Hilo limekuwa kaburi la kuchimba mwenyewe kwa waajiriwa walio wengi.
Sasa anakaa hapo. Anashangaa sukari inapanda hana njia zaidi ya kulalamika mpaka ishuke. Why? Kwa sababu kipato chake hakipandi kutokana na mfumuko wa bei. Lakini mfanyabiashara wa mahindi au magari mafuta yakipanda anaongeza bei ya mahindi. Anayekuja kulalamika ni mwajiriwa ambaye hana uwezo wa kuongeza kipato kesho yake hata afanyeje kazi. Na bado anataka kufanikiwa kiuchumi. Wanashangaa siku zinaenda. Mwisho anamaliza miaka 20 kwenye mfumo wa ajira. Ana Ph.D ya kuajiriwa unadhani utamshauri kuanza biashara akuelewe. Anaogopa. Ukizingatia wiki iliyopita nilisema anakuwa na LIMITED EXPERIENCE. Akichungulia upande wa wafanyabiashara wanaoanza anaona wengi WANASTRUGGLE. Anaogopa kugive up laki nane ya kila mwezi afu aje kustruggle kuanzisha sijui mradi sijui biashara. Anaona wengine wameanza biashara wakafeli wakapoteza mitaji wameanza moja tena. Anataka akija kuanza hela yake isipotee! Anafanya ANALYSIS kwanza. Miaka inaenda. Utumwa unaendelea kumtumikia mtu aliyemwajiri. Mwisho anakuwa sugu wa shida za kimaisha. Inakuwa sehemu ya maisha.
End of the story.

Kwa kuwa naongelea route ya kufikia FINANCIAL FREEDOM kiujumla hili jambo  la mwajiriwa kutokuwa na maamuzi kuhusu lini kipato chake kipande na kwa kiwango gani linafanya kazi kumzuia mwajiriwa kufikia uhuru wa kipato. Na hata kikipanda hakiko REAL-WORTH-BASED. Hivi kama unalipwa mshahara wa milioni 2 per month do you really think thats your worth? Mpaka mtu akupe milioni mbiki ujue unachozalisha ni maybe 10 times. Kwa hiyo basi huwezi kufikia uhuru wa kipato endapo ili kuongeza kipato chako lazima uwe in good terms na MWAJIRI au mwalimu wa Masters ili usije kukosa Masters. Waajiri wengi wametumia hiyo power waliyonayo ya kudetermine nani apate ongezeko la kipato na wakati gani, kuwanyonya na kuwakamua waajiriwa kadri iwezekanavyo na wengine hata kufikia hatua mbaya ya kuomba rushwa ya ngono ili kuboresha maslahi ya mwajiriwa husika. What a tragedy!! Usione hayakukuti kuna watu wanasimulia mambo.

Sometimes utafanya wewe kazi halafu atapanda cheo na kipato BOSI wako. Ndo wakubwa wanamwona yeye. Your worth watajifanya hawaioni. Au utaambiwa fungu hakuna. Subiri bajeti ijayo ipite. Subiri kwanza tuone hii hali. Unaambiwa ngoja tuone huyu Magufuli (Rais JPM) tuone kwanza mwelekeo. Mwelekeo gani mnanyonya tu waajiriwa!!?

Haya mambo hunitatiza sana. Sijui wewe mwajiriwa.

Kama wewe unasoma hapa na una uwezo wa kusema mwezi ujao nataka mshahara wangu uwe mara mbili ya huu wa mwezi huu na hilo likawezekana basi hongera sana. Lakini naamini unasoma makala yangu hii ukiwa Sayari ya #Jupiter.
Siyo duniani..

Kwa kuwa muda leo umenitupa mkono na nilikuahidi kuwa nitaandika kitu leo naomba niishie hapa. Ni karibu SAA 12 na nusa sasa jioni. Naamini utapata kitu hata katika haya machache.

Na kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoandika kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 7 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado zingine 3 tu.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 7 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 8.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis People,

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni