Jumapili, 16 Oktoba 2016

JAMBO LA SITA (KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

JAMBO LA SITA
(KATIKA MAMBO 10 YANAYOMNYIMA MWAJIRIWA YEYOTE UWEZO WA KUFIKIA UHURU WA KIPATO)

TUNAENDELEA:

Kwa neema ya Mungu naendelea ku-share mambo 10 (yani jambo moja kwa siku) yanayomnyima mwajiriwa uwezo wa kufikia UHURU wa kipato. Kwa maana nyingine ataendelea kuwa mtumwa wa kipato).

Na leo naendelea na sababu ya 6.

6. JAMBO LA SITA: KUWA CHINI YA  "BWANA"... (BEING UNDER A MASTER a.k.a. BOSS)

Miaka mingi iliyopita kulikuwa na mfumo rasmi na halali kisheria wa uchumi (uzalishaji mali) ulioitwa UTUMWA (SLAVERY). Mfumo huo uliruhusu MTU kumiliki watu ambao waliitwa watumwa. Na yeye kuitwa " bwana" au kwa kiingereza SLAVE MASTER. Kwa hiyo neno master ni neno zito kuliko wengi tunavyoweza kulichukulia.

Miaka mingi baada ya mfumo huo kukawa na mfumo wa UKABAILA (FEUDALISM) ambapo watumwa waligeuzwa kuwa watumishi hasa mashambani kwa ajili ya kusustain mfumo huo mpya wa uchumi. Na biashara ya watumwa (SLAVE TRADE) ikashamiri ili wamiliki wa mashamba makubwa Ulaya na Marekani wapate nguvu kazi rahisi (cheap labour) ya kutumika kuzalisha mali mashambani na kutumika majumbani nk.

Baada ya muda kwa sababu ya mafanikio katika sayansi na teknolojia basi zikaja zama za viwanda. Na hapa ndo ikatokea changamoto kati ya watu waliokuwa wakimiliki watumwa na wale waliokuwa wakimiliki viwanda. Wamiliki wa viwanda pia walihitaji watu. Lakini siyo watu tu. No walihitaji watu ambao wako "HURU". Sasa ni hiyo concept ya "uhuru" ambayo nitaiongelea hapa leo. Kwa hiyo wenye viwanda wakaingia vita na wamiliki wa watumwa. Kampeni za kuzuia biashara ya watumwa zikaanzishwa. Si kwa sababu watumwa walikuwa wanapendwa sana no. Ni kwa sababu kulikuwa na mfumo mpya unaowahitaji. Mpaka kina Sultan Seyyid Said nk wakajikuta katika hiyo vita. Huko nchini Marekani kukatokea vita kati ya wanazi wa Democrats ambao ndo walikuwa wakimiliki watumwa na wale wa Republicans ambao walikuwa hasa na viwanda sasa. Miaka minne iliyompa ABRAHAM LINCOLN jina lisilosahaulika Marekani kwa kushinda hiyo vita na kukomesha utumwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa ujumla viwanda duniani vilihitaji labourers. Na wakapatikana. Wakaanza kwenda wenyewe kuajiriwa viwandani. Na mahali kwingine. Leo hii mfumo ume evolve watu hawafanyi kazi viwandani tu bali sekta mbali mbali. Mashuleni, mashambani, mahospitalini, huduma za usafiri, huduma za ushauri (consultations, mfano sheria, kodi, mahesabu, nk), mahotelini, etc. Watu leo wameajiriwa kila eneo la uzalishaji mali.

Katika uhusiano wa zamani wa utumwa mtumwa alikuwa chini ya "BWANA" yaani Master. Katika kutafuta njia ya kuleta mahusiano mapya kati ya wafanyakazi waliotoka utumwani na waajiri wao wapya likabuniwa neno jipya linaitwa BOSS ili watu wasiendelee kujifeel kama bado wapo chini ya MASTER. Kimsingi neno "boss" limetolewa katika neno la kidachi (Dutch) linaloitwa BAAS ambalo cha ajabu linamaanisha MASTER/BWANA. Kwa hiyo neno boss ni neno MASTER tu ila limepakwa rangi rangi mpaka uzikwangue rangi ndo utajua.

Kimsingi basi mahusiano yaliyopo kati ya mwajiriwa na mwajiri au mwakilishi wa mwajiri ni yale yale tu kati ya mtumwa na bwana wake. Kilichobadilika ni uhusiano umepakwa rangi.

Juzi nilisema kuwa kuna kitu kinaitwa MINDSET. Na nikasema MINDSET yako ikikamatwa utabadikishana ardhi yako na mtu afu yeye anakupa kioo. Mindset.

Kilichofanyika ni kucheza na mindset tu ya mtumwa yule yule. Yani kumuuliza: kati ya kuwa mtumwa na kulala kwenye mabanda na kushinda mashambani unavuna pamba kwa mijeledi huna haki hata ya kuzaana.. Kati ya hayo maisha na kuishi huru ukilipwa vijisenti kutokana na nguvu zako na vikakusaidia kununua chakula UNACHOTAKA, na kununua vijinguo unavyotaka na kulala unakotaka na hata kijiuhuru cha kwenda mahali mahali kula bata jioni na wenzako mkijipongeza kumaliza siku na kupeana michapo ya hapa na pale NI YAPI WEWE UNACHAGUA???

Unadhani mtumwa angechagua nini? Yani hapo hata iweje anachagua "B". Kabla hata hujamaliza kumuuliza. Na ni kweli. It's good. But that's the problem with most of us. We just settle for anything good. Basi. Kumbe huyo anayekuuliza amecreate tu mazingira ya win-WIN situation. Hapo nimeandika win ya herufi ndogo na WIN ya hefuri kubwa. Kumbe unakuwa una illusion ya kuwa uko huru lakini ni utumwa ule ule tu ile umekuwa upgraded. Ukitaka mtu asiache kutumia simu unafanyaje. Upgrade it. Kila siku simu zinavitu vipya. Na vina mafufaa. Lakini ndo win WIN.

Na kwa kuwa topic yangu ni kuhusu kwa nini MWAJIRIWA hawezi kufikia uhuru wa kipato ndo maana hii win WIN situation naiongelea. Kwamba mwajiriwa ni a modern day slave. Bado ana MASTER. Ambaye anamwambia what to do.

I. Unapoajiriwa unapewa Job Description.. Kazi yako ni kuvuna pamba kila siku asubuhi mpaka jioni ujira wako ni huu. Unakubali unakataa?
Wachache hukataa. Mtumwa hakuwa na choice. Waajiriwa pia HAWANA choice. Yani mfano ukichoka si unaweza kupumzika. Mwajiriwa hata akichoka kupumzika siyo choice kazi lazima ziishe. Bora punda afanyeje...........? Unakumbuka?

II. Waajiriwa wamefungwa pingu pia.
Wajiriwa wamekuwa watumwa wa kipato in the sense kwamba hawezi kuacha kwenda hata kama hajisikii vizuri. Kazi zake anafanya nani? Pamba yake atavuna nani? Hela itakuwaje asipoenda? So anahisi yuko huru kwa sababu anaenda mwenyewe kumbe hajui kuwa kuna INVICIBLE CHAINS tu. Au somewhat loose chains. Hazionekani kwa macho tu lakini zipo. Kwani nchi zetu sisi hizi ziko huru? Si ni bendera tu. Bado uchumi wa nchi zetu uko mikononi mwa wengine. Mpaka leo nchi za Africa Magaribi zinalipa kodi kwa ufaransa kwa miundombinu ambayo ufaransa ilijenga wakati wa ukoloni. Colonial tax.
Kataa kulipa uone.
Hahaaaa
Ndo hivyo. Invincible chains.
Tragic.
Waajiriwa wengi wamekuwa watumwa kiasi kwamba akihisi kesho kazi hana anaweza kuugua ghafla. Kama umeajiriwa jiulize kama kesho ukifika ofisini ukaambiwa hakuna kazi tena.. From nowhere. Utapiga kamluzi kuzuri au utapiga "yeleuwiiii" moja ya hatari au kupigwa bumbuwazi hapo. Enchained.
That's how it is.
Bosi yupo kuhakikisha hutambui uwepo wa hiyo minyororo.

III. Your MASTER (boss) is a-l-w-a-y-s righhhht!!!!!
Waajiriwa wengi wanajua hii situation. Hutakiwi kutofautiana na boss wako sana. Au Mara kwa Mara. Atamwaga ugali na mboga na kuzima jiko.
So kama vipi kama unaona mawazo ya bosi siyo sawa we potezea tu maisha yasonge. Usawa wenyewe huu wa kusomeshana namba. We tulia mwache "anajua anachokifanya."
Waajiriwa wengi wako hivyo. Mawazo yao mazuri hawathubutu kuyaweka wazi kama yanakinzana na mtazamo wa MASTER! or Mistress! Hii imeua creativity ya waajiriwa wengi na wameamua kufia ajirani bila kujua wanainyima dunia mambo mazuri mno. Ackton na Koum wangeajiriwaga Facebook kama walivyotaka huenda Leo hii kusingekuwa na WhatsApp. Sometimes losing your job usiichukulie negative. Ukaamua kutafuta nyingine. Think. Why kuna shida katika ajira yako. Why ideas zako watu wanasema nzuri na wewe unajua fika but bosi wako hazikubali. Think. Unaweza kuwa unainyima dunia jambo kubwa mno kwa kung'ang'ana tu kubaki ajirani. Boss tu ndo yuko sahihi.
Umekuwa mtumwa wa fikra zake yeye.
Za kwako ziko kichwani kwa ajili ya nini sasa. Mapambo au?
Simaanishi umchukie bosi ila ndo ujue.

IV. Watumwa walikuwa wakipewa adhabu zinazoshabihiana na za waajiriwa. Reprimand. Kufokewa. Kupunguziwa "share" (kukatwa mshahara), nk. Katika ulimwengu wa Biashara hakuna mtu wa kukupa adhabu. Huhitaji adhabu. Adhabu ni kwa watoto. Ukiacha penal system. Mtu mzima unahitaji ushauri not reprimand ambayo ipo zaidi kudiscourage makosa wakati makosa ni sehemu ya kujifunza. Unadhani Dewji hakosei? Kwani Bhakressa akivunja printer bahati mbaya anakatwa mshahara? Vunja wewe sasa utasikia Mara gross negligence Mara sijui nini. Utadhani umevunja glass ya bi mkubwa enzi za utoto. Ndo utaelewa maana ya kuwa na boss.
Ukizidisha makosa utakatwa "mguu" kama #KuntaKinte wa ile movie ya #ROOTS. Kipato kikatike.

V. Watumwa walikuwa wakipewa incentives mbali mbali kuwahamasisha kuzalisha zaidi. Chakula zaidi. Sherehe mbili tatu. Siku yao maalumu kupumzika. Nk.  Ndivyo ilivyo kwa waajiriwa pia. Mei Mosi. Family Day. Nk. Afu waajiriwa wanependa sikukuu kweli. Labda ili kuescape kidogo kutumwatumwa. Wapumzike kidogo watembee waone hata bichi.
Sijawahi kusikia siku ya WAWEKEZAJI.
Anyway..
Bosi wako yupo kusimamia vitu kama hivyo viwepo na kumonitor effectiveness yake.

VI. Lengo halisi la slave masters lilikuwa kumsqueeze mtumwa mpaka jasho lake la mwisho kwa "malipo" kiduchu. Lengo la WAAJIRI wa leo ni lile lile. Kazi ya bosi ni kuhakikisha hilo linatimia kikamilifu.

Kuna researcher mmoja wa Harvard Business School aliandika makala kwenye mtandao wa FORBES inaitwa: "The Messy Link Between Slave Owners And Modern Management". Kaisome, google hiyo title utapata.

Sasa katika #mazingira hayo ya uwepo wa MASTER-SLAVE relationship uhuru wa kipato hauwezi kupatikana. Nimesema huu ni essentially mfumo ule ule tu ila umepakwa rangi. Kama magari ya baadhi ya yadi za kitaa. Unakuta gari lina mvuto kwa nje kumbe. Nunua tu baada ya muda utaanza kuelewa kwa nini walikubali kukupunguzia bei...

Again, bottomline is Uhuru wa kipato kwa mfumo wa ajira ni myth. Ndo maana wastaafu wengi wana suffer. Hawakujua walikuwa wakitumika katika win-WIN situation.

Kama ulisoma makala zangu hizi toka mwanzo utaanza kuona kuwa sababu zote nilizoandika kuanzia ile ya kwanza hadi hii ya 6 zinafanya kazi kinyume cha MWAJIRIWA. Ziunganishe utaelewa vizuri. Again..Don't read them in isolation.

Bado zingine 4.
Endelea kuwa na mimi.

But kwa leo hicho ndiyo kikwazo cha 6 cha kumzuia mwajiriwa asifikie kamwe FINANCIAL FREEDOM. Ule MTAA WA UHURU (WA KIPATO).
Leo naishia hapa. Kesho kwa neema ya Mungu nitaendelea na LIMITING FACTOR YA 7.

Kwa maswali. Maoni. Critique. Ushauri. Au kujifunza zaidi nk.
SMS, WhatsApp and Calls: +255752366511
WhatsApp Only: +255788366511
Blog: andreamuhozya.blogspot.com

Barikiwa Sana!

Semper Fidelis my People,

Semper Fi,

Andrea G. Muhozya
Dar es Salaam, Tanzania,
East Africa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni